688 Bila Kujali Afanyayo Mungu, Yote ni kwa Ajili ya Kuwaokoa Binadamu
1 Mungu hufanya kazi ndani ya kila mtu, na bila kujali mbinu Yake ni ipi, ni watu, vitu au masuala ya aina gani ambayo Yeye hutumia kufanya huduma, au maneno Yake yana sauti ya aina gani, Ana lengo moja tu la mwisho: kukuokoa. Kabla ya kukuokoa, Anahitaji kukubadili, hivyo utakosaje kuteseka kidogo? Ni lazima upate kuteseka. Kuteseka huku kunaweza kuhusisha mambo mengi. Wakati mwingine Mungu huwainua watu, mambo, na vitu ambavyo viko karibu nawe ili kwamba uweze kujitambua, vinginevyo unaweza kushughulikiwa moja kwa moja, kukupogolewa, na kufunuliwa. Kama vile tu mtu aliye juu ya meza ya upasuaji–lazima upitie maumivu kiasi kwa ajili ya matokeo mazuri.
2 Kama kila wakati Mungu anapokupogoa na kukushughulikia na kila wakati Anaibua watu, mambo, na vitu, hilo huchochea hisia zako na kukuongezea nguvu, basi kupitia hayo kwa njia hii ni sahihi, na utakuwa na kimo na utaingia katika uhalisi wa ukweli. Ikiwa, kila wakati unapopogolewa na kushughulikiwa, na kila wakati Mungu anapoinua mazingira yako, wewe huhisi maumivu au usumbufu wowote, na huhisi chochote kabisa, na kama huji mbele za Mungu kuelewa mapenzi Yake, wala huombi au kutafuta ukweli, basi wewe kweli ni mtu asiyejali kabisa! Watu ambao hawajali kabisa kamwe si hawatambui kiroho; kwa hiyo, Mungu hana njia ya kufanya kazi kwao.
3 Mungu akipanga mazingira, watu, vitu, na mambo fulani kwa ajili yako, Akikupogoa na kukushughulikia na ukijifunza kutokana na hili, ikiwa umejifunza kuja mbele za Mungu kutafuta ukweli, na, bila kujua, umetiwa nuru na kuangaziwa na kupata ukweli, ikiwa umepitia mabadiliko katika mazingira haya, umepata thawabu, na kupiga hatua, ukianza kuwa na ufahamu mdogo kuhusu mapenzi ya Mungu na kuacha kulalamika, basi yote haya yatamaanisha kuwa umesimama imara katikati ya majaribio ya mazingira haya, na umestahimili jaribio. Kwa hiyo, utakuwa umeshinda majaribu haya.
Umetoholewa kutoka katika “Ili Kupata Ukweli, Lazima Ujifunze Kutoka kwa Watu, Mambo, na Vitu Vinavyokuzunguka” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo