254 Utakaribishaje Kurudi kwa Kristo?

1 Bila shaka, Mungu Anapopata mwili mara hii, kazi Yake ni kuonyesha tabia Yake, kimsingi kupitia kuadibu na hukumu. Akitumia haya kama msingi, Analeta ukweli zaidi kwa mwanadamu, kuonyesha njia zaidi za matendo, na hivyo Hufikia lengo Lake la kumshinda mwanadamu na kumwokoa mwanadamu kutokana na tabia yake potovu. Hili ndilo liko katika kazi ya Mungu katika Enzi ya Ufalme. Watu wakibaki katika Enzi ya Neema, basi hawatawahi kujiweka huru kutokana na tabia zao za upotovu, sembuse kujua tabia ya asili ya Mungu. Wanadamu wakiishi daima katika wingi wa neema ila hawana njia ya maisha inayowaruhusu kumjua Mungu na kumridhisha Mungu, basi kamwe hawataweza kumpata Mungu kwa kweli hata ingawa wanaamini Kwake. Hiyo ni aina ya imani ya kutia huruma.

2 Wakati umemaliza kusoma kitabu hiki, wakati umepitia matukio yote ya kazi ya Mungu mwenye mwili katika Enzi ya Ufalme, utahisi kwamba matumaini ya miaka mingi hatimaye yametimika. Utahisi kwamba ni sasa tu ndipo umemwona Mungu uso kwa uso; ni sasa tu ndipo umeutazama uso wa Mungu, umesikia matamshi ya Mungu Mwenyewe, umeifahamu hekima ya kazi ya Mungu, na kuhisi kwa kweli jinsi Mungu ni wa kweli na mwenye nguvu. Utafahamu kuwa umepata vitu vingi ambavyo watu wa nyakati zilizopita hawajawahi kuviona wala kuwa navyo. Wakati huu, utajua kwa uhakika ni nini hasa kuamini katika Mungu, na ni nini kupendeza nafsi ya Mungu.

3 Bila shaka, ukikwamilia maoni ya kitambo, na ukatae au ukane ukweli wa kupata mwili kwa Mungu mara ya pili, basi utabaki mkono mtupu na hutapata chochote, na mwishowe utakuwa na hatia ya kumpinga Mungu. Wale wanaotii ukweli na kunyenyekea kwa kazi ya Mungu watakuja chini ya jina la Mungu mwenye mwili wa pili—Mwenyezi. Wataweza kukubali uelekezi binafsi wa Mungu, na watapata ukweli zaidi na wa juu zaidi na watapokea maisha ya kweli ya mwanadamu. Je, unatamani kujiondolea tabia yako potovu? Je, unatamani kupata ukweli wa juu? Je unatamani kuishi maisha yaliyo na thamani? Je, unatamani kufanywa mkamilifu na Mungu? Basi, je, utakaribisha vipi kurudi kwa Yesu?

Umetoholewa kutoka katika Dibaji ya Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 253 Mungu Ndiye Bwana wa Viumbe Vyote

Inayofuata: 255 Anayeshikilia Ukuu Juu ya Kila Kitu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp