284 Kutembea kwenye Njia ya Kumpenda Mungu

1

Sijali jinsi njia ya imani katika Mungu ilivyo ngumu,

natekeleza tu mapenzi ya Mungu kama wito wangu;

sembuse kujali ikiwa nitapokea baraka au kuteseka katika siku zijazo.

Sasa kwa kuwa nimeamua kumpenda Mungu, nitakuwa mwaminifu hadi mwisho.

Bila kujali ni hatari au dhiki gani zinazojificha nyuma yangu,

bila kujali mwisho wangu utakuwa upi,

ili kukaribisha siku ya Mungu ya utukufu,

nafuata kwa makini nyayo za Mungu na kujitahidi kuendelea mbele.

2

Nauona moyo wa Mungu una wasiwasi sana.

Napaswa kufanyaje wajibu wangu ili kushiriki mzigo wa Mungu?

Njia ya kueneza injili ya ufalme ni ndefu na yenye miinuko mikali.

Ikiwa nampenda Mungu, basi napaswa kuteseka ili kushuhudia Kwake.

Kwa kuwa nimechagua kumpenda Mungu, nafaa kujitolea Kwake.

Niko tayari kupitia chochote ili kuufariji moyo wa Mungu.

Mungu huvumilia fedheha kubwa sana ili awaokoe wanadamu.

Ikiwa tunampenda Mungu, tunapaswa kufikiria mapenzi Yake.

Mungu anatujaribu ili kuona iwapo tunampenda kwa kweli au la.

Ikiwa tunaelewa ukweli, basi tunapaswa kujitahidi kuwa na ushuhida kwa Mungu.

Bila kujali mateso, majaribio na dhiki ni kubwa kiasi gani,

kumpenda Mungu na kutekeleza mapenzi Yake daima kutakuwa kipaumbele,

na hakika tutapata sifa Zake.

Iliyotangulia: 283 Mwishowe Naweza Kumpenda Mungu

Inayofuata: 285 Wimbo wa Kumpenda Mungu Bila Majuto

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp