692 Mtazamo Wa Mwanadamu Kwa Majaribu

1 Unapoitembea njia ya leo, ufuatiliaji unaofaa zaidi ni wa aina gani? Katika ufuatiliaji wako, unapaswa kujiona kama mtu wa aina gani? Unafaa kujua jinsi unavyopaswa kukabili yote yanayokukumba leo, yawe majaribu ama taabu, ama kuadibu na laana isiyo ya huruma. Unapaswa kuyazingatia kwa uangalifu katika hali zote. Nasema hili kwa sababu yanayokukumba leo hata hivyo ni majaribu mafupi yanayotokea tena na tena; huenda huyaoni kuwa yanayosumbua sana kiakili, na hivyo unayaacha mambo yaende mrama, na huyachukulii kuwa rasilmali ya thamani katika ufuatiliaji wa maendeleo. Wewe ni asiyejali kweli! Sana kiasi kwamba unaifikiria rasilmali kana kwamba ni wingu linaloelea machoni pako, na huyathamini haya mapigo makali yanayokuja mara kwa mara—mapigo ambayo ni ya muda mfupi na yanayoonekana kuwa dhaifu kwako—ila unayatazama kwa utulivu, usiyafikirie kwa dhati na kuyachukulia tu kama mapigo ya mara moja. Wewe ni mfidhuli sana!

2 Badala ya kutazama nidhamu na mapigo haya yanayorudiwa kama ulinzi bora kabisa, unayaona kuwa uchokozi wa Mbinguni usio na sababu, ama vinginevyo kama adhabu inayokufaa. Wewe ni mpumbavu sana! Unazifungia nyakati nzuri gizani bila huruma; mara kwa mara unaona nidhamu na mapigo mazuri kuwa mashambulio kutoka kwa adui zako. Huwezi kubadilika kulingana na mazingira yako sembuse kutaka kufanya hivyo kwani huna hiari ya kupata chochote kutoka kwa kuadibu huku kunakorudiwa na unakoona kuwa katili. Hufanyi juhudi yoyote kutafuta au kuchunguza, na, unajikabidhi tu kwa yale majaaliwayako, kwenda pahali popote itakapokuelekeza. Yanayoonekana kwako kuwa marudio makali hayajaubadili moyo wako wala hayajatwaa udhibiti wa moyo wako; badala yake, yanakuchoma moyoni. Unaona “kuadibu huku katili” kuwa adui wako katika maisha haya tu na hujapata chochote. Wewe unajidai sana!

3 Ni mara chache ambapo unaamini kwamba unapitia majaribu kama haya kwa sababu wewe ni duni sana; badala yake, unajiona aliye na bahati mbaya sana, na kusema kwamba Mimi daima hutafuta makosa kwako. Kufikia leo, kwa kweli una kiasi kipi cha maarifa ya kile Ninachosema na kufanya? Usifikiri kwamba una kipaji cha asili, uliye chini kidogo ya mbingu lakini juu sana ya dunia. Wewe si mwerevu zaidi kuliko mtu mwingine yeyote—na hata inaweza kusemwa kwamba wewe ni mpumbavu zaidi kuliko watu wowote duniani walio na mantiki, kwani unajiona sana kuwa bora, na hujawahi kujiona kuwa mtu wa chini; inaonekana kwamba unayachunguza matendo Yangu kwa utondoti kabisa. Kwa kweli, wewe ni mtu ambaye kimsingi hana mantiki, kwa kuwa hufahamu kabisa Nitakachofanya sembuse kutambua Ninachofanya sasa. Kwa hivyo Nasema kwamba wewe hata hulingani na mkulima mzee anayefanya kazi kwa bidii shambani, mkulima ambaye hafahamu maisha ya binadamu hata kidogo na bado anategemeabaraka za Mbinguni wakati anapolima shamba. Huyafikirii maisha yako hata kidogo, hujui chochote chenye sifa sembuse kujijua. Wewe “una hadhi ya juu” sana!

Umetoholewa kutoka katika “Wale Wasiojifunza na Wanaosalia Wajinga: Je, Wao Sio Wanyama?” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 691 Kuja kwa Magonjwa ni Upendo wa Mungu

Inayofuata: 693 Mungu Hatimaye Huwapata wale Walio na Ukweli

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp