306 Binadamu Wapotovu Hawastahili Kumwona Kristo

1 Kila mara mnataka kumwona Kristo, lakini Nawasihi msijipandishe hadhi hivyo; kila mtu anaweza kumwona Kristo, lakini Nasema hakuna ambaye ni wa kufaa kumwona Kristo. Kwa sababu asili ya binadamu imejazwa na uovu, kiburi, na uasi, wakati unapomwona Kristo, asili yako itakuharibu na itakuhukumu hadi kufa. Wakati wowote, fikira zako zinaweza kukita mizizi, kiburi chako kianze kuchipuka, na uasi wako kuzaa mitini. Unawezaje kufaa kushiriki na Kristo na ubinadamu kama huo?

2 Je, kweli unaweza kumchukua Yeye kama Mungu kila wakati wa kila siku? Je, kweli utakuwa na hali halisi ya utiifu kwa Mungu? Mnamuabudu Mungu mkubwa ndani ya mioyo yenu kama Yehova wakati mnamchukua Kristo anayeonekana kama mwanadamu. Hisia zenu ni duni mno na ubinadamu wenu ni wa hali ya chini! Hamwezi kumfikiria Kristo kama Mungu milele; ni mara chache tu, mnapotaka, ndio mnamshika na kumwabudu kama Mungu. Hii ndiyo sababu Ninasema nyinyi si waumini wa Mungu, ila kikundi cha washirika ambao wanaopigana dhidi ya Kristo.

3 Iwapo utaenda kumwona Mungu kabla ya kupogolewa au kupitia hukumu, basi bila shaka utakuwa mpinzani wa Mungu na utakuwa katika njia ya kuangamizwa. Asili ya mwanadamu kwa kawaida ina uhasama kwa Mungu, kwa kuwa watu wote wamepotoshwa kabisa na shetani. Hakuna kizuri kinachoweza kupatikana kwa mtu kujaribu kushirikiana na Mungu kutokana na upotovu wake. vitendo na maneno yake kwa hakika vitafichua upotovu wake kila wakati; na katika kushirikiana na Mungu, uasi wake utafichuka katika vipengele vyote. Binadamu, kwa kutojua anakuja anampinga Kristo, kumdanganya Kristo, na kumtelekeza Kristo; hili litakapofanyika, mwanadamu atakuwa katika hali ya hatari zaidi na, hili likiendelea, atapata adhabu.

Umetoholewa kutoka katika “Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 305 Hustahili Kuwasiliana na Mungu kwa Mantiki kama Hiyo

Inayofuata: 307 Hii Ndiyo Imani Yako?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp