297 Binadamu Wamekoma Kuwa Kile Atakacho Mungu

1 Mwanadamu ameendelea kwa makumi ya maelfu ya miaka ya historia mpaka kufikia alipo leo. Hata hivyo, mwanadamu wa uumbaji Wangu wa asili kwa muda mrefu uliopita amezama katika upotovu. Tayari amecha kuwa kile Ninachotaka, kwa hivyo wanadamu, Ninavyowaona, hawastahili tena jina la uanadamu. Badala yake wao ni uchafu wa wanadamu, ambao Shetani amewateka nyara, maiti zilizooza zinazotembea ambamo Shetani huishi na huvalia.

2 Watu hawaamini hata kidogo kuwepo Kwangu, wala hawakaribishi kuja Kwangu. Mwanadamu kwa shingo upande tu huyajibu maombi Yangu, na kwa muda anakubaliana nayo, na hashiriki kwa kweli katika furaha na huzuni za maisha pamoja na Mimi. Kwa vile wanadamu huniona Mimi kama Asiyeeleweka, bila ya kutaka wao hujifanya wanatabasamu Kwangu, kuleta namna ya kujidekeza kwa yule aliye na madaraka. Hii ni kwa sababu watu hawana ufahamu wa kazi Yangu, sembuse mapenzi Yangu kwa wakati wa sasa.

3 Nitakuwa wazi na nyinyi nyote: Siku itakapofika, mateso ya mwanadamu yeyote ambaye huniabudu yatakuwa rahisi kubeba kuliko yenu. Kiwango cha imani yenu Kwangu hakiwezi, kwa hakika, kuzidi kile cha Ayubu—hata imani ya Mafarisayo Wayahudi inaishinda yenu—na hivyo, siku ya moto ikifika, kuteseka kwenu kutakuwa kali zaidi kuliko kule kwa Mafarisayo walipokemewa na Yesu, kuliko kule kwa wale viongozi 250 waliompinga Musa, na kuliko kule kwa Sodoma chini ya moto mkali wa uharibifu wake.

Umetoholewa kutoka katika “Maana ya Kuwa Mtu Halisi” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 296 Huzuni ya Binadamu Aliyepotoka

Inayofuata: 298 Ukweli wa Matokeo ya Kupotoshwa kwa Mwanadamu na Shetani

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp