449 Udhihirisho wa Kazi ya Roho Mtakatifu

1 Roho Mtakatifu anapofanya kazi ili kuwapa watu nuru, kwa ujumla Yeye huwapa ufahamu wa kazi ya Mungu, na ufahamu wa kuingia kwao kwa kweli na hali yao ya kweli. Yeye pia huwasababisha waelewe nia za dharura za Mungu na madai Yake kwa mwanadamu leo, ili wawe na azimio la kudhabihu kila kitu ili wamridhishe Mungu, wampende Mungu hata wakikumbana na mateso na dhiki, na kuwa shahidi kwa Mungu hata ikimaanisha kumwaga damu yao au kutoa maisha yao, na kufanya hivyo bila majuto. Ukiwa na azimio la aina hii, inamaanisha unayo misisimko na kazi ya Roho Mtakatifu—lakini jua kwamba huna misismko ya aina hii kila wakati.

2 Wakati mwingine katika mikutano unapoomba na kula na kunywa maneno ya Mungu, unaweza kuhisi kuguswa na kupata msukumo mno. Linaonekana jambo la kuburudisha kabisa wakati watu wengine wanashiriki baadhi ya uzoefu na ufahamu wao wa maneno ya Mungu, na moyo wako uko wazi na mchangamfu kabisa. Hii yote ni kazi ya Roho Mtakatifu. Kama wewe ni kiongozi na Roho Mtakatifu anakupa nuru na mwangaza usio wa kawaida unapoenda kanisani kufanya kazi, Anakupa umaizi wa shida ambazo zipo katika kanisa, Anakuwezesha kujua jinsi ya kushiriki kuhusu ukweli ili kuzitatua, Anakufanya uwe mwenye bidii ya ajabu sana, mwenye kuwajibika na uliye makini katika kazi yako, hii yote ni kazi ya Roho Mtakatifu.

Umetoholewa kutoka katika “Utendaji (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 448 Hali ya Kawaida Huleta Ukuaji wa Haraka Maishani

Inayofuata: 450 Umeingia Katika Njia Sahihi ya Kumwamini Mungu?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp