283 Maisha ya Mwanadamu Yako Chini ya Ukuu wa Mungu Kabisa

1 Kama mtu anasadiki tu katika hatima—hata anahisi kwa kina kuihusu—lakini papo hapo hawezi kujua, kutambua, kunyenyekea, na kukubali ukuu wa Muumba kuhusu ile hatima ya binadamu basi maisha yake yatakuwa kwa kweli msiba mkuu, maisha yaliyopita kwa masikitiko, utupu; yeye atakuwa hawezi kutii utawala wa Muumba, kuwa binadamu aliyeumbwa katika hali ya kweli zaidi ya kauli hiyo, na kufurahia idhini ya Muumba. Mtu anayejua na kupitia kwa kweli ukuu wa Muumba anafaa kuwa katika hali amilifu, isiyo baridi au ya kutoweza kusaidika. Huku wakati uo huo akikubali kwamba mambo yote yanategemea hatima ya maisha, yeye anafaa kumiliki ufafanuzi sahihi wa maisha na hatima: kwamba kila maisha yanategemea ukuu wa Muumba.

2 Wakati mtu anapoangalia nyuma kwenye barabara aliyotembelea, wakati mtu anapokusanya tena kila awamu ya safari ya maisha yake, mtu anaona kila hatua, haijalishi kama barabara ya mtu inakuwa mbaya au nzuri, Mungu alikuwa akiongoza njia ya mtu, akipanga kila kitu. Ilikuwa ni mipangilio ya umakinifu ya Mungu, upangiliaji Wake makinifu ulioongoza mtu, bila kujua, hadi kufikia leo. Ili kuweza kukubali ukuu wa Muumba, ili kupokea wokovu Wake—utajiri mwingi kweli! Kama mtazamo wa mtu katika ukuu wa Mungu juu ya hatima ya binadamu ni amilifu, basi mtu anapotazama nyuma katika safari yake, wakati mtu anapong’amua kwa kweli ukuu wa Mungu, mtu huyo ataweza kutamani kwa dhati kunyenyekea kila kitu ambacho Mungu amepangilia, atakuwa na jitihada zaidi na ujasiri wa kumwacha Mungu kuunda hatima yake, ili kuacha kuasi dhidi ya Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 282 Mungu Aliamua Majaliwa ya Mwanadamu Kitambo

Inayofuata: 284 Uchungu wa Binadamu Unaibukaje?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp