245 Naomba tu Nimpende Mungu Maisha Yangu Yote

1 Nilimwamini Bwana kwa miaka mingi sana lakini nilijua tu jinsi ya kufurahia neema Yake. Kamwe sikumpenda Mungu kweli. Nilifanya kazi na kuteseka tu, nikitaka kubadilisha hili na baraka za ufalme wa mbinguni. Sasa, ni kwa kupitia hukumu mbele ya kiti cha Kristo tu ndipo nimeujua ukweli: Mungu humwokoa mwanadamu kwa kuonyesha ukweli ili Ausafishe upotovu wake, Amfanye aelewe ukweli na kutenda ukweli ili aweze kuishi mbele ya Mungu. Lakini nilipotoshwa sana na Shetani na nikapoteza dhamiri na mantiki yangu. Nilitamani tu neema ya Mungu lakini sikuyatenda maneno Yake kabisa. Nilitaka tu kubadilisha mateso na kazi yangu na baraka za ufalme wa mbinguni na uzima wa milele, lakini kamwe sikuyajali mapenzi ya Mungu na sikuishi kwa kudhihirisha ukweli wa maneno ya Mungu. Kwa kumwamini Mungu lakini nikijadiliana na Mungu, kwa kweli nilikuwa nikijaribu kumdanganya na kumwasi.

2 Hukumu na ufunuo wa maneno ya Mungu pekee ndivyo vilivyoniruhusu kuona wazi ukweli wa upotovu wangu mwenyewe. Mimi ni mwenye kiburi, mwenye majivuno, mwovu, mdanganyifu, mbinafsi na mwenye kustahili dharau, nisiye na sura ya binadamu. Nikiwa mpotovu sana, nisingepitia hukumu ya Mungu, basi ningemjuaje Mungu au kumtii Mungu? Bila kumjua Mungu na bila kumcha, ningewezaje kustahili kuishi mbele Yake? Kupitia hukumu, majaribu na usafishaji, nimeona kuwa upendo wa Mungu ni halisi sana. Ingawa nimepitia maumivu makali, hatimaye tabia yangu potovu inapata utakaso. Kwa kujua haki na utakatifu wa Mungu, moyo umchao Mungu wainuka ndani yangu. Ni kwa kutenda ukweli tu, na kumpenda na kumtii Mungu, ndipo ninaishi kwa kudhihirisha kiasi kidogo cha mfano wa binadamu. Hukumu ya Mungu imeniwezesha kuupata ukweli, na kwa kumjua Mungu naweza kuishi tena. Nimepata wokovu mkubwa wa Mungu, na naomba tu kutafuta kumpenda Mungu maisha yangu yote.

Iliyotangulia: 244 Wokovu wa Mungu kwa Mwanadamu Ni Halisi Sana

Inayofuata: 246 Kufuatilia Ukweli Tu Ndiko Kunaweza Kuleta Uzima

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp