599 Kuishi kwa ajili ya Kutimiza Wajibu Wako Kuna Maana

Mungu hukuruhusu uishi na ikiwa unaweza kuishi kwa ajili ya Mungu na kuishi ili kutekeleza wajibu wa kiumbe, basi unaishi maisha yenye maana.

1 Ni hawa wanaokubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho ambao ni wenye akili zaidi. Baada ya kupitia hukumu na kuadibiwa kwa miaka kadhaa, wanakuja kuelewa bila kujua kusudi la usimamizi wa Mungu wa wanadamu na pia siri ya usimamizi Wake na wokovu wa wanadamu. Wanakuja kuelewa mapenzi ya Mungu na kujua ukuu Wake. Wanahisi kuwa wanaishi maisha yenye utajiri, amani, na maana. Mungu hukuruhusu uishi na ikiwa unaweza kuishi kwa ajili ya Mungu na kuishi ili kutekeleza wajibu wa kiumbe, basi unaishi maisha yenye maana. Ikiwa unaishi maisha ya maiti anayetembea, asiye na roho, kutokubali ukweli, unaishi kwa ajili ya mwili tu, basi huishi maisha yenye maana, kwani maisha yako hayana thamani.

2 Kati ya binadamu wote, ninyi ndinyi mliojaaliwa na kuteuliwa; mlizaliwa katika enzi hii, katika nchi ya joka kubwa jekundu, na Yeye huwaruhusu mtekeleze wajibu wenu wa sasa. Mmependwa na Mungu; mmechaguliwa na Yeye. Hii ni baraka. Mungu anawapenda na anawaruhusu mjitumie kwa ajili Yake, mtekeleze wajibu wenu katika familia ya Mungu, mtekeleza wajibu wa kiumbe, na kutoa sehemu ya bidii yenu. Hii sio baraka? Sasa mnaweza kuishi kila siku mkimshuhudia Mungu na kueneza injili ya ufalme wa Mungu; jambo hilo limeidhinishwa na Mungu.

3 Mungu anakupa fursa hii uishi kwa njia hii na kujitumia kwa ajili Yake —hili ni jambo la maana. Mnapaswa kuthamini fursa hii, na kuhisi fahari na heshima. Kuweza kutekeleza wajibu huu katika enzi hii, katika mazingira haya, na katika hali hizi ni fursa adimu sana! Mungu huchagua kwa uangalifu kutoka miongoni mwa binadamu, na amewachagua. Hii ni fursa yenu. Hii ni baraka yenu kubwa. Baraka hii ni kubwa zaidi kuliko baraka za watakatifu katika enzi zote na vizazi vyote!

Umetoholewa kutoka kwa ushirika wa Mungu

Iliyotangulia: 598 Unapaswa Kukubali Uchunguzi wa Mungu Katika Kila Kitu

Inayofuata: 600 Kufanikiwa ama Kushindwa Kunategemea Njia Atembeayo Mwanadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp