445 Mfanano wa Wale Wanaotumiwa na Mungu

1 Vigezo vya Mungu kuwatumia watu ni kama ifuatavyo: Mioyo yao inamgeukia Mungu, wanasumbuliwa na maneno ya Mungu, wanakuwa na mioyo ya kutamani, na wako na azimio la kutafuta ukweli. Ni watu wa aina hii tu ndio wanaoweza kupata kazi ya Roho Mtakatifu na mara kwa mara wapate nuru na mwangaza. Watu ambao Mungu huwatumia huonekana kwa nje kama watu wasio na akili na kama wasio na uhusiano wa kawaida na wengine, ingawa wao huzungumza na adabu, hawazungumzi kiholela, na wanaweza daima kuwa na moyo uliotulia mbele ya Mungu. Na hana upendo wa kuelekea nje au matendo ya juu juu, lakini anapokuwa akieleza mambo ya kiroho anaweza kufungua roho yake na kwa kujinyima awatolee wengine mwangaza na nuru ambayo amepata kutoka kwa uzoefu wake wa hakika mbele za Mungu. Hivi ndivyo anavyodhihirisha upendo wake kwa Mungu na kuridhisha mapenzi ya Mungu.

2 Wengine wote wanapokuwa wanamkashifu na kumdhihaki, ana uwezo wa kutoelekezwa na watu wa nje, matukio, au vitu, na bado anaweza kutulia mbele za Mungu. Mtu wa aina hii inavyooneka yuko na utambuzi wake mwenyewe wa pekee. Bila kujali wengine, moyo wake kamwe haumwachi Mungu. Wengine wanapokuwa wakizungumza kwa furaha na kwa vichekesho, moyo wake bado unasalia mbele za Mungu, kutafakari neno la Mungu au kusali kwa kimya kwa Mungu aliye moyoni mwake, akitafuta makusudi ya Mungu. Kamwe hawatilii maanani udumishaji wa uhusiano wa kawaida na wengine. Mtu wa aina hii inavyoonekana hana falsafa ya maisha. Kwa nje, mtu huyu ni mchangamfu, anayependwa, asiye na hatia, lakini pia anamiliki hisia ya utulivu. Huu ni mfano wa mtu ambaye Mungu anamtumia.

Umetoholewa kutoka katika “Ni Muhimu Sana Kuanzisha Uhusiano wa Kawaida na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 444 Una Uhusiano wa Kawaida na Mungu?

Inayofuata: 446 Kuwa na Uhusiano wa Kawaida na Mungu ili Ukamilishwe

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp