109 Mfano wa Mtu Ampendaye Mungu

Kiitikio

Wale wampendao Mungu hutekeleza wajibu wao kwa uaminifu na ndio waliobarikiwa zaidi na Mungu.

Wale wampendao Mungu ni watu waaminifu ambao Mungu anawapenda.

Wale wampendao Mungu humtii na kufuata mapenzi Yake.

Ni wale tu wampendao Mungu ndio wanaostahili kukamilishwa kupitia hukumu na kuadibu.

1

Wale wampendao Mungu ni wanyoofu, mioyo yao ni miaminifu na safi.

Wanamfuata Kristo kwa moyo wote bila mashaka au kusita.

Wale wampendao Mungu kweli wana njaa na kiu ya haki.

Wanapenda ukweli na hutegemea maneno ya Mungu kuishi; hawawezi kumwacha Mungu.

2

Wale wampendao Mungu humtii, ni wema na wenye huruma kutoka ndani ya mioyo yao.

Sio wazembe kamwe katika majukumu yao, wayajali mapenzi ya Mungu katika mambo yote.

Wale wampendao Mungu kweli wanashiriki fikira na mahangaiko ya Mungu.

Wanajitumia kwa uaminifu na huvumilia ugumu bila malalamiko, hawataji thawabu yoyote kamwe.

3

Wale wampendao Mungu humwogopa Mungu, hutenda ukweli mara tu wanapouelewa.

Wao hukubali ukaguzi wa Mungu katika kila kitu, wako wazi kabisa, wanaishi katika nuru.

Wale wampendao Mungu kweli hutafuta mapenzi Yake katika mambo yote.

Ni wenye maadili katika usemi na vitendo, na wanaishi kwa kudhihirisha uhalisi wa ukweli.

4

Wale wampendao Mungu wamejitolea Kwake, wanashuhudia katika majaribu.

Afadhali wapoteze maisha yao kuliko kumsaliti Mungu.

Wale wampendao Mungu kweli hulenga kutafuta kumjua Mungu.

Wanatii mipangilio ya Mungu bila malalamiko, mioyo yao yenye upendo kwa Mungu haibadiliki kamwe.

Iliyotangulia: 108 Wale Wanaompenda Mungu kwa Dhati Wote ni Watu Waaminifu

Inayofuata: 110 Mpende Mungu Uishi Katika Nuru

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

83 Upendo wa Kweli

1 Namrudia Mungu na kuuona uso Wake upendezao, nikiwa huru kutokana na udhibiti wa kaida za dini. Neno Lake linanijaza na raha na furaha...

115 Nimeuona Upendo wa Mungu

1 Mwenyezi Mungu, ni Wewe unayenipenda. Katika ulimwengu mchafu Umenichagua mimi! Hivyo nimekuja mbele Yako, naam, nimekuja mbele Yako,...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki