439 Mwache Mungu Aingie Moyoni Mwako

Mungu anaweza tu kuingia katika moyo wako kama utaufungua kwa ajili Yake. Unaweza kuona tu kile Mungu Alicho nacho na kile Alicho, na unaweza kuona tu mapenzi Yake kwako, kama Ameingia katika moyo wako.

1 Wakati huo, utagundua kwamba kila kitu kuhusu Mungu ni chenye thamani, kwamba kile Alicho nacho na kile Alicho kina thamani sana ya kuthaminiwa. Ukilinganisha na hayo, watu wanaokuzunguka, vifaa na matukio katika maisha yako, hata wapendwa wako, mwandani wako, na mambo unayopenda, si muhimu sana. Ni madogo mno, na ni ya kiwango cha chini; utahisi kwamba hakuna chombo chochote cha anasa ambacho kitaweza kukuvutia tena, na au kwamba kitu chochote yakinifu kitawahi kukushawishi tena ukilipie gharama yoyote tena. Kwa unyenyekevu wa Mungu utaona ukubwa Wake na mamlaka Yake ya juu; aidha, katika jambo Alilofanya uliloliamini kuwa dogo mno, utaweza kuiona hekima Yake na uvumilivu Wake usio na mwisho, na utaiona subira Yake, uvumilivu Wake na ufahamu Wake kwako. Hili litazaa ndani yako upendo Kwake.

2 Siku hiyo, utahisi kwamba mwanadamu anaishi katika ulimwengu mchafu, kwamba watu walio upande wako na mambo yanayokufanyikia katika maisha yako, na hata kwa wale unaopenda, upendo wao kwako, na ulinzi wao kama ulivyojulikana au kujali kwao kwako havistahili hata kutajwa—Mungu tu ndiye mpendwa wako na ni Mungu tu unayethamini zaidi. Upendo wa Mungu ni mkubwa na kiini Chake ni kitakatifu mno—ndani ya Mungu hakuna udanganyifu, hakuna uovu, hakuna wivu, na hakuna mabishano, lakini ni haki tu na uhalisi, na kila kitu Alicho nacho Mungu na kile Alicho vyote vinafaa kutamaniwa na binadamu. Binadamu wanafaa kujitahidi na kuwa na hamu ya kuvipata.

Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 438 Unapoufungua Moyo Wako kwa Mungu

Inayofuata: 440 Maisha Ya Kiroho Yanayofaa Yanapaswa Kudumishwa Daima

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp