491 Maarifa Si Mbadala wa Uhalisi

1 Kwa nini watu wengi zaidi wametumia jitihada nyingi kusoma maneno ya Mungu lakini wana maarifa tu na hawawezi kusema kitu chochote kuhusu njia halisi baada ya hapo? Unadhani kwamba kuwa na maarifa ni sawa na kuwa na ukweli? Unaweza kuzungumza maarifa mengi kama mchanga ulivyo ufuoni, lakini hakuna yaliyo na njia ya kweli. Je, wewe hujaribu kuwapumbaza watu kwa kufanya hivi? Kadiri nadharia inavyokuwa ya juu, ndivyo inavyokosa uhalisi zaidi, na ndivyo inavyokosa zaidi uwezo wa kuwapeleka watu katika uhalisi; kadiri nadharia inavyokuwa ya juu, ndivyo inavyokufanya umuasi na kumpinga Mungu. Usizichukulie nadharia za kiwango cha juu kama hazina ya thamani; zina madhara, na hazina kazi yoyote! Pengine baadhi ya watu wanaweza kuzungumza juu ya nadharia za juu sana—lakini nadharia hizo hazina kitu chochote cha uhalisi, maana watu hawajazipitia wao binafsi, na kwa hiyo hawana njia ya kutenda. Watu kama hao hawawezi kuwaongoza wengine katika njia sahihi, na watawapotosha.

2 Angalau kabisa, unapaswa kuweza kutatua shida za sasa za watu na kuwaruhusu kupata kuingia; hii tu ndiyo inachukuliwa kama ibada, na baada ya hapo ndipo utakuwa na sifa za kufaa kumfanyia Mungu kazi. Siku zote usizungumze maneno ya kifahari, ya ajabu, na usiwalazimishe watu kukutii wewe pamoja na vitendo vyako visivyofaa. Kufanya hivyo hakutaleta matokeo, na kunaweza kuongeza tu mkanganyiko wa watu. Kuendelea kwa namna hii kutazalisha mafundisho mengi, ambazo zitawafanya watu wakuchukie. Hivyo ndivyo ulivyo udhaifu wa mwanadamu, na kwa kweli unadhalilisha. Kwa hivyo, zungumza zaidi juu ya matatizo ambayo yapo kwa kweli. Usiyachukulie matukio ya watu wengine kama mali yako binafsi na kuyaonyesha waziwazi ili wengine wastahi; unapaswa kutafuta suluhisho lako binafsi mwenyewe. Hiki ndicho ambacho kila mtu anapaswa kuweka katika vitendo.

Umetoholewa kutoka katika “Sisitiza Uhalisi Zaidi” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 490 Fanya Jitihada Katika Kutenda Kwako Neno la Mungu

Inayofuata: 492 Ushauri wa Mungu kwa Mwanadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp