704 Kuijua Asili Yako Mwenyewe ni Muhimu kwa Badiliko Katika Tabia

1 La muhimu katika kufikia badiliko katika tabia ni kujua asili ya mtu mwenyewe, na hili ni lazima lifanyike kulingana na ufunuo kutoka kwa Mungu. Ni katika neno la Mungu tu ambapo mtu anaweza kujua asili yake mbaya, afahamu katika asili yake mwenyewe sumu mbalimbali za Shetani, atambue kuwa yeye ni mjinga na mpumbavu, na atambue dalili dhaifu na hasi katika asili yake. Baada ya haya kujulikana kikamilifu, na unaweza kwa hakika kujichukia na kunyima mwili, daima kutekeleza neno la Mungu, na kuwa na mapenzi ya kujiwasilisha kikamilifu kwa Roho Mtakatifu na kwa neno la Mungu, basi utakuwa umeianza njia ya Petro. Bila neema ya Mungu, na bila nuru na mwongozo kutoka kwa Roho Mtakatifu, ingekuwa vigumu kuitembea njia hii, kwa sababu watu hawamiliki ukweli na hawawezi kujisaliti wenyewe.

2 Kwa hivyo kama ujuzi wa watu juu yao wenyewe ni wa juujuu sana, watapata kuwa haiwezekani kutatua matatizo, na tabia zao za maisha hazitabadilika kabisa. Ni muhimu kujijua mwenyewe kwa kiwango cha kina kabisa, ambayo inamaanisha kuijua asili yako mwenyewe: ni vipengele vipi ambavyo vimejumuishwa katika asili hiyo, jinsi vitu hivi vilivyoanza, na kule vilipotoka. Aidha, unaweza kuchukia mambo haya kweli? Je, umeona nafsi yako mwenyewe mbaya na asili yako mbovu? Ikiwa kwa hakika unaweza kuuona ukweli kujihusu mwenyewe, basi utaanza kujichukia mwenyewe kabisa. Wakati unapojichukia mwenyewe kabisa na kisha unatenda neno la Mungu, utakuwa na uwezo wa kunyima mwili na kuwa na nguvu ya kutekeleza ukweli bila shida.

Umetoholewa kutoka katika “Kujijua Mwenyewe Hasa Ni Kujua Asili ya Binadamu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 703 Kubadili Tabia Yako Kunaanza na Kuelewa Asili Yako

Inayofuata: 705 Mabadiliko ya Tabia Pekee Ndiyo Mabadiliko ya Kweli

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp