K. Kuhusu Jinsi ya Kupata Kumjua Mungu
453. Hatua tatu za kazi ya Mungu ndizo ukamilifu wa kazi ya Mungu ya kumwokoa mwanadamu. Mwanadamu lazima ajue kazi ya Mungu, tabia ya Mungu katika kazi ya wokovu, na bila ukweli huu, maarifa yako kumhusu Mungu yatakuwa tu maneno matupu, ni mahubiri ya starehe tu. Maarifa kama haya hayawezi kumshawishi au kumshinda mtu, maarifa kama haya yako nje ya uhalisi, na si ukweli. Yanaweza kuwa mengi, na mazuri masikioni, lakini kama hayaambatani na tabia ya asili ya Mungu, basi Mungu hatakusamehe. Sio tu kwamba Hatayasifu maarifa yako, bali pia Atakuadhibu kwa kuwa wewe ni mtenda dhambi ambaye umemkufuru. Maneno ya kumjua Mungu hayazungumzwi kwa mzaha. Ingawa unaweza kuwa na ulimi laini wenye maneno matamu, na ingawa maneno yako ni yenye busara kiasi kwamba unaweza kubishana kitu kisichowezekana, bado huna elimu ya kuzungumza kuhusu maarifa ya Mungu. Mungu si mtu ambaye unaweza kumhukumu kwa pupa, ama kumsifu bila mpangilio, ama kumdharau bila kujali. Unamsifu mtu yeyote na kila mmoja, lakini unatatizika kupata maneno sahihi ya kuelezea neema kuu ya Mungu—hili ndilo ambalo kila aliyeshindwa anajifunza. Ingawa kuna wataalam wengi wa lugha wanaoweza kumwelezea Mungu, usahihi wa kile wanachoelezea ni asilimia moja tu ya ukweli unaozungumzwa na watu wa Mungu, watu ambao wana misamiati michache tu, lakini wana uzoefu mwingi wa kurejelea. Hivyo inaweza kuonekana kwamba maarifa ya Mungu yapo katika usahihi na vitendo, na wala si katika utumiaji mzuri wa maneno au misamiati mingi, na kwamba maarifa ya mwanadamu na maarifa ya Mungu hayahusiani kabisa. Somo la kumjua Mungu liko juu zaidi kuliko sayansi yoyote ya asili ya wanadamu. Ni somo linaloweza kufikiwa tu na idadi ndogo sana ya watu wanaotafuta kumjua Mungu, na haliwezi kufikiwa na mtu yeyote tu mwenye kipaji. Kwa hivyo hampaswi kuona kumjua Mungu na kufuatilia ukweli kana kwamba ni vitu ambavyo vinaweza kufikiwa hata na mtoto mdogo tu. Pengine umefanikiwa kikamilifu katika maisha yako ya kifamilia, ama kazi yako, ama katika ndoa yako, lakini inapofika kwenye ukweli, na somo la kumjua Mungu, huna lolote la kujivunia, hujatimiza malengo yoyote. Kuweka ukweli katika vitendo, inaweza kusemwa, ni jambo gumu kwenu, na kumjua Mungu ni tatizo kubwa hata zaidi. Hili ni tatizo lenu, na pia ni tatizo linalokabiliwa na wanadamu wote. Kati ya wale wenye mafanikio katika kumjua Mungu, karibu wote hawajafikia kiwango. Mwanadamu hajui maana ya kumjua Mungu, ama kwa nini ni muhimu kumjua Mungu, ama ni kiwango gani ambacho ni lazima mtu afikie ili aweze kumjua Mungu. Hiki ndicho kinachowachanganya sana wanadamu, na ni kitendawili kikubwa zaidi kinachokabiliwa na wanadamu—na hakuna anayeweza kujibu swali hili, wala aliye tayari kujibu swali hili, kwa sababu, hadi leo, hakuna kati ya wanadamu aliyefanikiwa katika kusomea kazi hii. Pengine, kitendawili cha hatua tatu za kazi kitakapofanywa kijulikane kwa wanadamu, kutatokea kwa mfululizo kundi la watu wenye vipaji wanaomjua Mungu. Bila shaka, Natumaini kuwa hivyo ndivyo ilivyo, na, hata zaidi, Niko katika harakati za kutekeleza kazi hii, na Ninatumaini kuona kujitokeza kwa vipaji zaidi kama hivi katika siku za hivi karibuni. Watakuja kuwa wale wanaoshuhudia ukweli wa hatua hizi tatu za kazi, na, bila shaka, watakuwa pia wa kwanza kushuhudia hizi hatua tatu za kazi. Lakini hakuna kitu ambacho kingekuwa cha kuhuzunisha na kusikitisha zaidi ikiwa watu kama hao wenye talanta hawatatokea siku ambayo kazi ya Mungu itafika mwisho, au ikiwa kuna mtu mmoja au wawili tu kama hao ambao wamekubali kibinafsi kufanywa wakamilifu na Mungu mwenye mwili. Ingawa, hii pekee ndio hali mbaya zaidi. Kwa vyovyote vile, Ninatumai kuwa wale wote wanaotafuta kwa kweli wanaweza kupata baraka hii. Tangu mwanzo wa wakati, hakujawahi kuwa na kazi kama hii, kazi kama hiyo haijawahi kutokea katika historia ya maendeleo ya mwanadamu. Kama kweli unaweza kuwa mmoja wa wale wa kwanza wanaomjua Mungu, je, si hii itakuwa heshima ya juu kuliko viumbe vyote vilivyoumbwa? Je, kuna kiumbe mwingine kati ya wanadamu anayeweza kusifiwa na Mungu zaidi? Kazi kama hii ni ngumu kutekeleza, lakini mwishowe bado itatoa matokeo. Bila kujali jinsia au utaifa wao, wale wote wenye uwezo wa kufikia maarifa ya Mungu, mwishowe, watapokea heshima kuu ya Mungu, na watakuwa tu wenye kumiliki mamlaka ya Mungu. Hii ndiyo kazi ya leo, na pia ndiyo kazi ya siku za usoni; ni kazi ya mwisho na ya juu zaidi kukamilishwa katika miaka 6,000 ya kazi, na ni njia ya kufanya kazi ambayo inafichua kila aina ya mwanadamu. Kupitia kazi ya kumfanya wanadamu amjue Mungu, madaraja tofauti ya mwanadamu yanadhihirishwa: Wale wanaomjua Mungu wamehitimu kupokea baraka za Mungu na kupokea ahadi zake, wakati wale wasiomjua Mungu hawajahitimu kupokea baraka za Mungu wala kupokea ahadi zake. Wale wanaomjua Mungu ni wandani wa Mungu, na wale wasiomjua Mungu hawawezi kuitwa wandani wa Mungu; wandani wa Mungu wanaweza kupokea baraka zozote za Mungu, lakini wale wasio wandani wa Mungu hawastahili kazi Yake yoyote. Iwe ni dhiki, usafishaji, au hukumu, mambo haya yote ni kwa ajili ya kumruhusu mwanadamu mwishowe aweze kufikia maarifa ya Mungu, na ili mwanadamu aweze kumtii Mungu. Hii ndiyo athari pekee ambayo hatimaye itapatikana.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu
454. Kile Mungu alicho nacho na uwepo wa Mungu, kiini cha Mungu, tabia ya Mungu—yote yamewekwa wazi katika maneno Yake kwa binadamu. Anapopitia maneno ya Mungu, katika mchakato wa kuyaweka katika vitendo mwanadamu atapata kuelewa kusudi la maneno Anayonena Mungu, na kuelewa chanzo na usuli wa maneno ya Mungu, na kuelewa na kufahamu maneno ya Mungu. Kwa binadamu, haya ni mambo yote ambayo mwanadamu lazima ayapitie, ayatambue, na kuyafikia ili kuufikia ukweli na uzima, kutambua nia za Mungu, kubadilishwa katika tabia yake, na kuweza kutii ukuu na mipango ya Mungu. Katika wakati huo ambao mwanadamu anapitia, anafahamu, na kuvifikia vitu hivi, atakuwa kupata kumwelewa Mungu polepole, na kwa wakati huu pia atakuwa amepata viwango tofauti vya maarifa kumhusu Yeye. Ufahamu huu na maarifa haya hayatoki katika kitu ambacho mwanadamu amefikiria au kutunga, ila kutoka kwa kile ambacho anafahamu, anapitia, anahisi, na anashuhudia ndani yake mwenyewe. Ni baada tu ya kufahamu, kupitia, kuhisi, na kushuhudia vitu hivi ndipo ufahamu wa mwanadamu kumhusu Mungu utapata ujazo, ni maarifa haya tu anayoyapata kwa wakati huu ndio yaliyo halisi, ya kweli na sahihi, na mchakato huu—wa kupata kuelewa kwa kweli na ufahamu wa Mungu kwa kuelewa, kupitia, kuhisi, na kushuhudia maneno Yake—sio kingine ila ushirika wa kweli kati ya mwanadamu na Mungu. Katikati ya aina hii ya ushirika, mwanadamu anakuja kuelewa kwa kweli na kufahamu nia za Mungu, anakuja kuelewa kwa kweli na kujua kile Mungu alicho na uwepo wa Mungu, anakuja kuelewa kujua kwa kweli kiini cha Mungu, anakuja kuelewa na kujua tabia ya Mungu polepole, anafikia uhalisi wa kweli, na ufafanuzi sahihi, kuhusu ukweli wa utawala wa Mungu juu ya vitu vyote vilivyoumbwa, na kupata mambo ya muhimu na ufahamu wa utambulisho wa Mungu na nafasi Yake. Katika ushirika kama huo, mwanadamu anabadilika, hatua kwa hatua, mawazo yake kuhusu Mungu hayamfikirii Yeye kwa mawazo yaliyoundwa, ama kutawaliwa na wasiwasi wake mwenyewe kumhusu Yeye, ama kutomwelewa, ama kumshutumu, ama kutoa hukumu Kwake, ama kuwa na mashaka Naye. Kwa sababu hii, mwanadamu atakuwa na kiwango kidogo cha kutomwelewa Mungu, atakuwa na vipingamizi vichache kwa Mungu, na kutakuwa na matukio machache ambayo mwanadamu atamwasi Mungu. Kwa upande mwingine, kujali na utiifu wa mwanadamu kwa Mungu, utaongezeka kwa kiasi kikubwa, na uchaji wake kwa Mungu utakuwa wa kweli zaidi na pia wa kina zaidi. Katikati ya ushirika kama huo, sio tu kwamba mwanadamu atapata kuruzukiwa ukweli na ubatizo wa maisha, bali pia kwa wakati huo huo atapata maarifa ya kweli ya Mungu. Katika aina hii ya ushirika, sio tu kwamba mwanadamu atapata kubadilishwa tabia yake na kupata wokovu, bali pia kwa wakati huo atafikia uchaji na ibada ya kweli ya kiumbe aliyeumbwa kwa Mungu. Baada ya kuwa na aina hii ya ushirika, imani ya mwanadamu katika Mungu haitakuwa tena ukurasa tupu wa karatasi, ama ahadi ya maneno matupu, ama aina ya kufuata kwa upofu na kuabudu sanamu; ni; katika aina hii ya ushirika pekee ndio maisha ya mwanadamu yatakua kuelekea ukomavu siku baada ya siku, na ni wakati huu ndio tabia yake itabadilika polepole, na imani yake kwa Mungu, hatua kwa hatua, itatoka kwenye imani isiyo dhahiri na imani isiyo na uhakika mpaka kufikia utiifu wa kweli na kujali, na kuwa na uchaji wa kweli, na mwanadamu pia, katika mchakato wa kumfuata Mungu, ataendelea polepole kutoka kwenye mtazamo baridi mpaka kufikia mtazamo wa kiutendaji, kutoka kuwa yule aliye hasi mpaka kuwa chanya; ni kwa aina hii ya ushirika pekee ndipo mwanadamu atafikia kuelewa kwa kweli na ufahamu wa Mungu, kufikia maarifa ya kweli ya Mungu.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Dibaji
455. Maarifa ya mamlaka ya Mungu, nguvu za Mungu, utambulisho wa Mungu mwenyewe, na kiini cha Mungu hayawezi kupatikana kwa kutegemea fikira zako. Kwa kuwa huwezi kutegemea fikira ili kutambua mamlaka ya Mungu, basi ni kwa njia gani unaweza kupata maarifa ya kweli ya mamlaka ya Mungu? Kwa kula na kunywa maneno ya Mungu, kupitia ushirika, na kupitia kwa uzoefu wa maneno ya Mungu, utaweza kuwa na uzoefu na uthibitisho wa mamlaka ya Mungu hatua kwa hatua, na hivyo basi utapata kuelewa kwa utaratibu na kuongeza maarifa kuyahusu. Hii ndiyo njia pekee ya kupata maarifa ya mamlaka ya Mungu; hakuna njia za mkato. Kukuambia kwamba usifikirie sio sawa na kukufanya ukae kimya ukisubiria uharibifu, au kukuzuia usifanye lolote. Kutotumia ubongo wako kuwaza na kufikiria kunamaanisha kutotumia mantiki kukisia, kutotumia maarifa kuchanganua, kutotumia sayansi kama msingi, lakini badala yake kufahamu, kuhakikisha, na kuthibitisha kuwa Mungu unayemsadiki anayo mamlaka, kuthibitisha kwamba Yeye anashikilia ukuu juu ya hatima yako, na kwamba nguvu Zake nyakati zote zinathibitisha kuwa Yeye ndiye Mungu Mwenyewe wa kweli, kupitia kwa matamshi ya Mungu, kupitia ukweli, kupitia kwa kila kitu unachokabiliana nacho maishani. Hii ndiyo njia pekee ambayo mtu yeyote anaweza kutimiza ufahamu wa Mungu. Baadhi ya watu husema kwamba wangependa kupata njia rahisi ya kutimiza lengo hili, lakini, je, unaweza kufikiria kuhusu njia kama hiyo? Ninakwambia, hakuna haja ya kufikiria: Hakuna njia nyingine! Njia ya pekee ni kujua na kuthibitisha kwa uangalifu na kwa uthabiti kile ambacho Mungu anacho na alicho kupitia kwa kila neno Analonena na kwa kila kitu Anachofanya. Hii ndiyo njia ya pekee ya kumjua Mungu. Kwani kile ambacho Mungu anacho na alicho, na kila kitu cha Mungu, si kitu kisicho na maana na tupu, bali ni halisi.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I
456. Mungu anafanya kazi ya hukumu na kuadibu ili kwamba mwanadamu amjue, na kwa ajili ya ushuhuda Wake. Bila hukumu Yake juu jya tabia potovu ya mwanadamu, basi mwanadamu hangeweza kujua tabia Yake ya haki isiyoruhusu kosa lolote, na hangeweza kubadili ufahamu Wake wa Mungu kuwa mpya. Kwa ajili ya ushuhuda Wake, na kwa ajili ya usimamizi Wake, Anafanya ukamilifu Wake kuwa wazi kwa kila mtu, hivyo kumwezesha mwanadamu kupata ufahamu wa Mungu, na kubadili tabia yake, na kuwa na ushuhuda mkuu kwa Mungu kupitia kuonekana kwa Mungu hadharani. Mabadiliko ya tabia ya mwanadamu yanafanikishwa kupitia kazi nyingi tofauti za Mungu; bila mabadiliko ya aina hii katika tabia ya mwanadamu, mwanadamu hangeweza kuwa na ushuhuda kwa Mungu, na hangeweza kuambatana na nia za Mungu. Mabadiliko ya tabia ya mwanadamu yanaashiria kwamba mwanadamu amewekwa huru kutoka kwa utumwa wa Shetani na kutoka kwa ushawishi wa giza, na kwa kweli amekuwa mfano na kielelezo cha kazi ya Mungu, shahidi wa Mungu, na mtu ambaye anaambatana na nia za Mungu. Leo hii, Mungu mwenye mwili Amekuja duniani kufanya kazi Yake, na Anahitaji kwamba mwanadamu apate ufahamu kumhusu, apate kumtii Yeye, na awe na ushuhuda Kwake—mwanadamu anapaswa kujua kazi Yake ya vitendo na ya kawaida, anapaswa kutii maneno Yake yote na kazi ambayo haiambatani na mawazo ya mwanadamu, na anapaswa kuwa na ushuhuda kwa kazi Yake yote anayofanya kumwokoa mwanadamu, na vilevile matendo Yake yote ya kumshinda mwanadamu. Wale walio na ushuhuda kwa Mungu lazima wawe na ufahamu wa Mungu; ni ushuhuda wa aina hii tu ndio ulio sahihi, na wa vitendo, na ni ushuhuda wa aina hii tu ndio unaoweza kumwaibisha Shetani. Mungu anawatumia wale ambao wamepata kumjua kupitia hukumu Yake, kuadibu, na upogoaji, kuwa na ushuhuda Kwake. Yeye huwatumia wale waliopotoshwa na Shetani kumtolea Yeye ushuhuda. Yeye huwatumia wale ambao tabia yao imebadilika, na wale ambao wamepokea baraka Zake, kumtolea ushuhuda. Yeye hamhitaji mwanadamu amsifu kwa kinywa chake, wala hana hitaji lolote la sifa na ushuhuda kutoka kwa aina ya Shetani, ambao hawajaokolewa na Yeye. Ni wale tu wanaomjua Mungu ndio wanaostahili kumtolea Mungu ushuhuda, na ni wale tu ambao tabia zao zimebadilika ndio wanastahili kumshuhudia Mungu, na Mungu hatamruhusu mwanadamu aliletee jina Lake aibu kwa makusudi.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu
457. Kupata kujua dutu ya Mungu si jambo dogo. Lazima uelewe tabia Yake. Katika njia hii, polepole na bila kujua, utaanza kujua dutu ya Mungu. Wakati umeingia katika maarifa haya, utajikuta unasonga mbele kwenye hali ya juu na nzuri zaidi. Mwishowe, utakuja kujisikia aibu kwa nafsi yako ya kuchukiza, kiasi kwamba unahisi hakuna mahali pa kujificha. Wakati huo, kutakuwa na machache zaidi na zaidi katika mwenendo wako ya kukosea tabia ya Mungu, moyo wako utakuwa karibu zaidi na zaidi na ule wa Mungu, na polepole upendo wako Kwake utaongezeka ndani ya moyo wako. Hii ni ishara ya wanadamu kuingia katika hali nzuri. Lakini kufikia sasa bado hamjapata hili. Mnaposhughulika huku na kule kwa ajili ya majaaliwa yenu, ni nani anayependa kujaribu kujua dutu ya Mungu? Kama hali hii itaendelea, mtakiuka amri za utawala bila kujua, kwani mnafahamu kidogo sana kuhusu tabia ya Mungu. Kwa hivyo, je, si kile ambacho mnafanya sasa kinaweka msingi wa makosa yenu dhidi ya tabia ya Mungu? Kwamba Ninawaambia muielewe tabia ya Mungu haipingani na kazi Yangu. Kwani mkikosea amri za utawala mara nyingi, basi ni nani kati yenu anayeweza kutoroka adhabu? Je, basi kazi Yangu haingekuwa bure kabisa? Kwa hivyo, Ningali Nawaambia kwamba, pamoja na kuchunguza mienendo yenu binafsi, muwe waangalifu zaidi na hatua mnazochukua. Haya ndiyo yatakuwa mahitaji ya juu zaidi Ninayotoa kwenu, na Ninatumai kwamba nyote mtayafikiria kwa umakini na kuyaona kuwa muhimu kabisa. Endapo siku itafika ambapo matendo yenu yatanichochea Mimi hadi kuwa katika hali iliyojaa hasira, basi matokeo yatakuwa ya kwenu peke yenu kuyafikiria, na hakutakuwa na mwingine yeyote atakayechukua adhabu hiyo kwa niaba yenu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu
458. Kumjua Mungu kunamaanisha nini? Kunamaanisha kuwa na uwezo wa kujua shangwe, hasira, huzuni na furaha Yake; huku ndiko kumjua Mungu. Unadai kwamba umemwona Yeye, ilhali huelewi shangwe, hasira, huzuni, na furaha Yake, na huelewi tabia Yake. Vile vile huelewi haki Yake wala rehema Zake, wala hujui Anachokipenda ama Anachokichukia. Huu si ufahamu wa Mungu. Kwa hivyo, watu wengine wanaweza kumfuata Mungu lakini hawawezi kwa kweli kumwamini: hii ndiyo tofauti. Ikiwa unamjua Mungu, unamwelewa, na unaweza kuelewa mapenzi Yake kiasi, basi unaweza kumwamini kwa kweli, kumtii kwa kweli, kumpenda kwa kweli, na kumwabudu Yeye kwa kweli. Ikiwa huelewi mambo haya, basi wewe ni mfuasi tu ambaye hufuata tukuenda na umati. Hiyo haiwezi kuitwa kutii kwa kweli au ibada ya kweli. Je, ibada ya kweli inafanyika vipi? Bila ubaguzi wale wote ambao kwa kweli wanamjua Mungu humwabudu na kumcha kila wanapomwona; wote hulazimika kusujudu na kumwabudu Yeye. Kwa sasa, wakati Mungu mwenye mwili yuko kazini, ndivyo kadri ufahamu watu walionao wa tabia Yake na kile Alicho nacho na kile Alicho, ndivyo zaidi watakavyovithamini vitu hivi na ndivyo zaidi watamchaa Yeye. Kwa kawaida, kadiri watu walivyo na ufahamu mdogo, ndivyo wanavyokosa kuwa makini zaidi, na hivyo wanamtendea Mungu kama mwanadamu. Ikiwa watu kwa kweli wanngemjua na kumwona Mungu wangetetemeka kwa hofu. “Lakini yule ajaye baada ya mimi ni mwenye nguvu zaidi kuliko mimi, ambaye sistahili kuvichukua viatu vyake.”—kwa nini Yohana alisema haya? Ijapokuwa kwa kina hakuwa na ufahamu mkubwa, alijua kwamba Mungu ni wa kustaajabisha. Ni watu wangapi siku hizi wanaweza kumcha Mungu? Iwapo hawajui tabia Yake, basi wanawezaje kumcha Mungu? Watu hawajui kiini cha Kristo wala kuelewa tabia ya Mungu, sembuse kuwezakumwabudu Mungu. Ikiwa wanaona tu kuonekana kwa nje kwa kawaida kwa Kristo ilihali hawajui asili Yake, basi ni rahisi kwa wao kumchukulia Kristo kama tu mtu wa kawaida. Huenda wakachukua mtazamo usio wa heshima Kwake, na wanaweza kumdanganya, kumkataa, kutomtii, na kutoa hukumu Kwake. Wanaweza kujiona wenye haki na kutochukulia neno Lake kwa makini; wanaweza hata kuibua fikira, shutuma na kumkufuru Mungu. Ili kutatua masuala haya mtu lazima ajue kiini na uungu wa Kristo. Hiki ndicho kipengele kikuu cha kumjua Mungu; ni kile amabacho yeyote anayeamini katika Mungu wa utendaji wanapaswa kuingia na kufanikisha.
Neno, Vol. 3. Mihadhara ya Kristo wa Siku za Mwisho. Sehemu ya Tatu
459. Ni sheria ya Mbinguni na kanuni za duniani kumwamini Mungu na kumjua Mungu, na leo—wakati wa enzi ambapo Mungu mwenye mwili Anafanya kazi Yake mwenyewe—ndio wakati mwafaka hasa wa kumjua Mungu. Kumridhisha Mungu kunaafikiwa kwa msingi wa kufahamu mapenzi ya Mungu, na kuyafahamu mapenzi ya Mungu, ni muhimu kumjua Mungu. Ufahamu huu wa Mungu ni maono ambayo muumini anapaswa kuwa nayo; huu ndio msingi wa imani ya mwanadamu katika Mungu. Iwapo mwanadamu hana ufahamu huu, basi imani yake katika Mungu si dhahiri, na imejengwa juu ya nadharia tupu. Ingawa ni uamuzi wa watu kama hawa kumfuata Mungu, hawafaidi chochote. Wale wote wasiopata chochote kwenye mkondo huu ndio watakaoondolewa—wao wote hawana kazi. … Iwapo mwanadamu hawezi kupokea maono haya, basi hawezi kupata kazi mpya ya Mungu, na iwapo mwanadamu hawezi kutii kazi mpya ya Mungu, basi mwanadamu hana uwezo wa kuyaelewa mapenzi ya Mungu, na hivyo ufahamu wake wa Mungu ni bure. Kabla mwanadamu atimilize maneno ya Mungu, lazima ayajue maneno ya Mungu, hivyo ni kusema, aelewe mapenzi ya Mungu; ni kwa njia hii tu ndiyo maneno ya Mungu yanaweza kutekelezwa kwa usahihi na kulingana na moyo wa Mungu. Hili lazima liwe na kila mmoja anayetafuta ukweli, na ndiyo njia ambayo lazima kila mmoja anayejaribu kumjua Mungu aipitie. Njia ya kuyajua maneno ya Mungu ndiyo njia ya kumjua Mungu, na pia njia ya kuijua kazi ya Mungu. Na hivyo, kujua maono hakuashirii tu kuujua ubinadamu wa Mungu mwenye mwili, lakini pia kunajumuisha kujua maneno na kazi ya Mungu. Kutokana na maneno ya Mungu wanadamu wanapata kuelewa mapenzi ya Mungu, na kutokana na maneno ya Mungu wanapata kuelewa tabia ya Mungu na pia kujua kile Mungu alicho. Imani katika Mungu ndiyo hatua ya kwanza katika kumjua Mungu. Harakati ya kusonga kutoka katika imani ya mwanzo katika Mungu mpaka imani kuu kwa Mungu ndiyo njia ya kumjua Mungu, na harakati ya kuipitia kazi ya Mungu. Ikiwa unaamini tu katika Mungu kwa ajili ya kumwamini Mungu, na si kwa ajili ya kumjua Yeye, basi hakuna uhalisi kwa imani yako, na imani yako haiwezi kuwa safi—kuhusu hili hakuna tashwishi. Iwapo, wakati wa harakati anapopata uzoefu wa kazi ya Mungu mwanadamu anapata kumjua Mungu polepole, basi hatua kwa hatua tabia yake itabadilika pia, na imani yake itaongezeka kuwa ya kweli zaidi. Kwa njia hii, wakati mwanadamu anafaulu katika imani yake kwa Mungu, ataweza kumpata Mungu kwa ukamilifu. Mungu alijitoa pakubwa kuingia katika mwili mara ya pili na kufanya kazi Yake binafsi ili mwanadamu apate kumjua Yeye, na ili mwanadamu aweze kumwona. Kumjua Mungu[a] ndiyo matokeo ya mwisho yanayofikiwa katika mwisho wa kazi ya Mungu; ndilo hitaji la mwisho la Mungu kwa mwanadamu. Anafanya hili kwa ajili ya ushuhuda Wake wa mwisho, na ili kwamba mwanadamu mwishowe na kwa kikamilifu aweze kumgeukia Yeye. Mwanadamu anaweza tu kumpenda Mungu kwa kumjua Mungu, na ili ampende Mungu lazima amjue Mungu. Haijalishi vile anavyotafuta, au kile anachotafuta kupata, lazima aweze kupata ufahamu wa Mungu. Ni kwa njia hii tu ndiyo mwanadamu anaweza kumridhisha Mungu. Ni kwa kumjua Mungu tu ndio mwanadamu anaweza kumwamini Mungu kwa ukweli, na ni kwa kumjua Mungu tu ndio anaweza kumwogopa na kumheshimu Mungu kwa kweli. Wale wasiomjua Mungu hawataweza kumwogopa na kumheshimu Mungu kwa kweli. Kumjua Mungu kunahusisha kujua tabia ya Mungu, kuelewa mapenzi ya Mungu, na kujua kile Mungu alicho. Na haijalishi ni kipengee gani cha kumjua Mungu, kila mojawapo kinamhitaji mwanadamu alipe gharama, na kinahitaji nia ya kutii, ambapo bila hivi hakuna atakayeweza kufuata mpaka mwisho.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu
Tanbihi:
a. Nakala ya kwanza inasema “Kazi ya kumjua Mungu.”
460. Matokeo ya funzo la kumjua Mungu hayawezi kufikiwa kwa siku moja au mbili: Mwanadamu lazima apate uzoefu wa matukio mengi, apitie mateso, na awe na utiifu wa kweli. Kwanza kabisa, anza na kazi na maneno ya Mungu. Lazima uelewe kumjua Mungu kunajumuisha nini, jinsi ya kupata maarifa kuhusu Mungu, na jinsi ya kumwona Mungu katika matukio yako. Hili ndilo kila mtu lazima afanye wakiwa bado hawajamjua Mungu. Hakuna anayeweza kushika kazi na maneno ya Mungu kwa mara moja, na hakuna anayeweza kupata maarifa ya ukamilifu wa Mungu kwa muda mfupi. Kinachohitajika ni harakati mahususi ya matukio, na bila haya hakuna mwanadamu atakayeweza kumjua au kumfuata Mungu kwa kweli. Mungu Anapofanya kazi zaidi, ndivyo mwanadamu anavyozidi kumjua. Zaidi kazi ya Mungu inavyokinzana na mawazo ya mwanadamu, ndivyo ufahamu wa mwanadamu Kwake unavyofanywa upya na wenye kina kirefu. Iwapo kazi ya Mungu ingebaki milele bila kubadilika, basi mwanadamu angekuwa tu na ufahamu mdogo wa Mungu. Kati ya uumbaji na wakati wa sasa, vitu ambavyo Mungu alifanya wakati wa Enzi ya Sheria, Alichofanya wakati wa Enzi ya Neema, na kile Afanyacho wakati wa Enzi ya Ufalme: lazima ujue vizuri sana maono haya. Lazima mjue kazi ya Mungu.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu
461. Katika kipindi hiki akimfuata Yesu, Petro alikuwa na maoni mengi kuhusu Yeye na siku zote Alimhukumu kutokana na mtazamo wake. Ingawa alikuwa na kiwango fulani cha ufahamu wa Roho Mtakatifu, ufahamu huu haukuwa wazi kabisa, na haya yanaonekana katika maneno yake aliposema: “Lazima nimfuate yeye aliyetumwa na Baba wa mbinguni. Lazima nimtambue yule aliyechaguliwa na Roho Mtakatifu.” Hakuelewa mambo yale ambayo Yesu alifanya na hakuwa dhahiri kuyahusu. Baada ya kumfuata kwa muda fulani alivutiwa kwa kile alichofanya Yeye na kusema, na kwa Yesu Mwenyewe. Alikuja kuhisi kwamba Yesu alivutia upendo na heshima; alipenda kujihusisha na Yeye na kuwa kando Yake, na kusikiliza maneno Yake Yesu kulimpa ruzuku na msaada. Katika kipindi kile alichomfuata Yesu, Petro alitazama na kutia moyoni kila kitu kuhusu maisha Yake: Matendo Yake, maneno Yake, mwendo Wake na maonyesho Yake. Alipata ufahamu wa kina kwamba Yesu hakuwa kama binadamu wa kawaida. Ingawa mwonekano Wake wa binadamu ulikuwa wa kawaida kabisa, Alijaa upendo, huruma, na ustahimilivu kwa binadamu. Kila kitu alichokifanya au kusema kilikuwa chenye msaada mkubwa kwa wengine, na akiwa kando Yake, Petro aliona na kujifunza mambo ambayo hakuwahi kuyaona wala kuyasikia awali. Aliona kwamba ingawa Yesu hakuwa na kimo kikubwa wala ubinadamu usio wa kawaida, Alikuwa na hali ya ajabu na isiyo ya kawaida kabisa kumhusu. Ingawa Petro hakuweza kuyafafanua kabisa, aliweza kuona kwamba Yesu alikuwa na mwenendo tofauti na kila mtu mwingine, kwani Aliyafanya mambo yaliyokuwa tofauti kabisa na yale yaliyofanywa na binadamu wa kawaida. Tangu wakati huo akiwa na Yesu, Petro alitambua pia kwamba hulka Yake ilikuwa tofauti na ile ya binadamu wa kawaida. Siku zote alikuwa na mwenendo dhabiti na hakuwahi kuwa na haraka, hakupigia chuku wala kupuuza chochote, na aliyaishi maisha Yake kwa njia iliyofichua hulka iliyokuwa ya kawaida na ya kuvutia. Katika mazungumzo, Yesu alikuwa mwenye madaha na uzuri, mwenye uwazi na mchangamfu ilhali pia mtulivu, na Hakuwahi kupoteza heshima Yake katika utekelezaji wa kazi Yake. Petro aliona kwamba Yesu wakati mwingine alikuwa mnyamavu, ilhali nyakati nyingine alizungumza kwa mfululizo. Wakati mwingine Alikuwa na furaha sana kiasi kwamba alionekana kuwa njiwa anayerukaruka na kuchezacheza, na ilhali nyakati nyingine Alihuzunika sana kiasi cha kwamba hakuzungumza kamwe, ni kana kwamba alikuwa mama aliyechoka sana. Nyakati nyingine Alijawa na hasira, kama askari jasiri anayefyatuka kuwaua adui, na wakati mwingine hata kama simba anayenguruma. Nyakati nyingine Alicheka; nyakati nyingine aliomba na kulia. Haijalishi ni vipi Yesu alivyotenda, Petro alizidi kuwa na upendo na heshima isiyokuwa na mipaka Kwake. Kicheko cha Yesu kilimjaza kwa furaha, huzuni Yake ikamtia simanzi, hasira Yake ikamtetemesha, huku huruma Zake, msamaha na madai makali Aliyotoa kwa watu yalimfanya aje kumpenda Yesu kwa kweli, na akaweza kumcha na kumtamani kwa kweli. Bila shaka, Petro alikuja kutambua haya yote kwa utaratibu baada ya kuishi kando yake Yesu kwa miaka michache.
Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu
462. Ikiwa unataka kumjua Mungu na upate kweli kumjua na kumfahamu Yeye, basi usizuiwe tu katika hatua tatu za kazi ya Mungu, na usizuiwe tu katika hadithi za kazi ambayo Mungu alitekeleza wakati mmoja. Ukijaribu kumjua hivyo, basi unajaribu kumzuilia Mungu kwa mipaka fulani. Wewe unamwona Mungu kama ni kitu kidogo sana Ni jinsi gani kufanya hivyo kungeathiri watu? Hungeweza kujua maajabu na mamlaka ya juu kabisa ya Mungu, na hungeweza kamwe kujua nguvu za Mungu na kudura na eneo la mamlaka Yake. Ufahamu kama huo ungeathiri uwezo wako wa kukubali ukweli kwamba Mungu ni Mtawala wa vitu vyote, na vilevile maarifa yako ya utambulisho wa kweli na hadhi ya Mungu. Kwa maneno mengine, iwapo ufahamu wako kumhusu Mungu umewekewa mipaka katika eneo, unachoweza kupokea pia kimewekewa mipaka. Ndiyo maana ni lazima upanue eneo na kufungua upeo wa macho yako. Iwe ni eneo la kazi ya Mungu, usimamizi wa Mungu, na utawala wa Mungu, au vitu vyote vinavyotawaliwa na kusimamiwa na Mungu, unapaswa kujua yote na kupata kujua matendo ya Mungu yaliyo ndani. Kupitia njia hii ya ufahamu, utahisi bila kujua kwamba Mungu anatawala, anasimamia na kuvipa vitu vyote miongoni mwao. Wakati huo huo, utahisi kweli kwamba wewe ni sehemu ya vitu vyote, na kiungo cha vitu vyote. Mungu anapovipa vitu vyote, wewe pia unakubali utawala na utoaji wa Mungu. Huu ni ukweli usioweza kupingwa na yeyote.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII
463. Namna ambavyo uelewa juu ya Mungu ulivyo mkubwa katika mioyo ya watu, unaamua nafasi kubwa kiasi gani Anachukua katika mioyo yao. Namna ambavyo kiwango cha maarifa ya Mungu kilivyo katika mioyo yao ndivyo kwa kiwango kikubwa Mungu alivyo katika mioyo yao. Ikiwa Mungu unayemfahamu yupo tupu na ni yule asiye yakini, basi yule Mungu unayemwamini pia ni tupu na ni yule asiye yakini. Mungu unayemfahamu anaishia ndani ya mipaka ya upeo wa maisha yako binafsi, na hahusiani na Mungu wa kweli Mwenyewe. Kwa hiyo, kuyajua matendo ya Mungu, kuujua uhalisi wa Mungu na uweza Wake, kuujua utambulisho wa kweli wa Mungu Mwenyewe, kujua kile Anacho na alicho kujua kile Alichokuonyesha miongoni mwa vitu vyote—haya ni muhimu sana kwa kila mtu anayetafuta maarifa ya Mungu. Haya yana uhusiano wa moja kwa moja na iwapo watu wanaweza kuingia kwa uhalisi wa ukweli. Ikiwa unauwekea mipaka uelewa wako juu ya Mungu katika maneno tu, ikiwa unauwekea mipaka uelewa wako mdogo tu, Neema ya Mungu unayoihesabu, au shuhuda zako ndogo kwa Mungu, basi Ninasema kwamba yule Mungu unayemwamini si Mungu Mwenyewe wa kweli kabisa, na inaweza pia kusemwa kuwa Mungu unayemwamini ni Mungu wa fikira tu, si Mungu wa kweli. Hii ni kwa sababu Mungu wa kweli ni Yule ambaye Anatawala kila kitu, ambaye Anatembea miongoni mwa kila kitu, ambaye Anasimamia kila kitu. Yeye ndiye Anashikilia majaliwa ya binadamu wote—ambaye anashikilia majaliwa ya kila kitu. Kazi na matendo ya Mungu ambaye Ninamzungumzia hayaishii kwa sehemu ndogo tu ya watu. Yaani, haiishii tu kwa watu tu ambao sasa wanamfuata. Matendo Yake yameonyeshwa miongoni mwa vitu vyote, katika vitu vyote kuendelea kuishi, na katika sheria za mabadiliko ya vitu vyote. Kama huwezi kuona au kutambua matendo yoyote ya Mungu kati ya vitu vyote, basi huwezi kutoa ushuhuda kwa matendo Yake yoyote. Ikiwa huwezi kuwa na ushuhuda wowote kwa Mungu, ikiwa unaendelea kuzungumza juu ya huyo anayeitwa Mungu mdogo ambaye unamfahamu, Mungu huyo ambaye anaishia kwenye mipaka ya mawazo yako tu, na yupo ndani ya akili yako finyu, ikiwa unaendelea kuzungumza juu ya aina hiyo ya Mungu, basi Mungu hataisifu imani yako. Unapokuwa na ushuhuda kwa ajili ya Mungu, ikiwa unatumia tu jinsi unavyofurahia neema ya Mungu, kukubali adhabu na kurudi Kwake, na kufurahia baraka Zake katika ushuhuda wako Kwake, ambao kwa kiasi kikubwa hautoshi na hauwezi kumridhisha. Ikiwa unataka kuwa na ushuhuda kwa ajili ya Mungu kwa namna ambayo inakubaliana na mapenzi Yake, kuwa na ushuhuda kwa Mungu Mwenyewe wa kweli, basi unapaswa kuona kile Mungu anacho na alicho kutokana na matendo Yake. Unapaswa kuona mamlaka ya Mungu kutoka katika udhibiti Wake wa kila kitu, na kuona ukweli wa jinsi Anavyowakimu binadamu wote. Ikiwa unakiri tu kwamba chakula chako cha kila siku na kinywaji na mahitaji yako katika maisha yanatoka kwa Mungu, lakini huoni ukweli kwamba Mungu anawakimu binadamu wote kwa njia ya vitu vyote, kwamba anawaelekeza wanadamu, basi hutaweza kamwe kuwa na ushuhuda kwa ajili ya Mungu. Lengo Langu la kusema haya yote ni lipi? Iko hivyo ili usiweze kulichukulia hili kirahisi, ili msiamini kwamba mada hizi Nilizozizungumzia hazina uhusiano na kuingia kwenu binafsi katika maisha, na ili msichukue mada hizi kama tu aina ya maarifa au mafundisho. Ikiwa unasikiliza ukiwa na mtazamo kama huo, hutapata kitu hata kimoja. Mtapoteza fursa kubwa hii ya kumjua Mungu.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX
464. Hata mwanadamu akiendelea kuchunguza sayansi na sheria za vitu vyote, ni katika eneo lililowekewa mipaka pekee, ilhali Mungu anadhibiti vitu vyote. Kwa mwanadamu, hiyo ni isiyo na kikomo. Wanadamu wakichunguza kitu fulani kidogo ambacho Mungu alifanya, wangetumia maisha yao yote kukichunguza bila kupata matokeo yoyote ya kweli. Ndiyo maana ukitumia ufahamu na kile ulichojifunza kumsoma Mungu, hutaweza kamwe kumjua au kumwelewa Mungu. Lakini ukitumia njia ya kutafuta ukweli na kumtafuta Mungu, na kumtazama Mungu kutokana na mtazamo wa kuanza kumjua Mungu, basi siku moja utakubali kwamba matendo na hekima ya Mungu viko kila mahali, na utajua pia hasa ni kwa nini Mungu huitwa Bwana wa vitu vyote na chanzo cha uhai kwa vitu vyote. Kadiri unavyokuwa na maarifa kama hayo, ndivyo utakavyoelewa ni kwa nini Mungu huitwa Bwana wa vitu vyote. Vitu vyote na kila kitu, pamoja na wewe, daima vinapokea mtiririko thabiti wa utolewaji wa Mungu. Utaweza pia kuhisi dhahiri kwamba katika ulimwengu huu, na miongoni mwa wanadamu hawa, hakuna yeyote isipokuwa Mungu anayeweza kuwa na nguvu kama hizo na kiini kama hicho kutawala, kusimamia, na kudumisha kuwepo kwa vitu vyote. Ukitimiza ufahamu kama huo, utakubali kwa kweli kwamba Mungu ni Mungu wako. Ukifikia kiwango hiki, umemkubali Mungu kwa kweli na kumruhusu awe Mungu wako na Bwana wako. Ukiwa na ufahamu kama huo na maisha yako yakifikia kiwango kama hicho, Mungu hatakujaribu na kukuhukumu tena, wala Hatakushurutisha ufanye mambo, kwa sababu unamfahamu Mungu, unajua moyo Wake, na umemkubali Mungu kwa kweli ndani ya moyo wako.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII
465. Watu mara nyingi husema kwamba si jambo rahisi kumjua Mungu. Mimi, hata hivyo, nasema kwamba kumjua Mungu si jambo gumu kamwe, kwani Mungu mara kwa mara huruhusu binadamu kushuhudia matendo Yake. Mungu hajawahi kusitisha mazungumzo Yake na mwanadamu; Yeye hajawahi kujificha kutoka kwa binadamu, wala Yeye hajajificha. Fikira Zake, mawazo Yake, maneno Yake na matendo Yake vyote vimefichuliwa kwa mwanadamu. Kwa hivyo, mradi tu mwanadamu angependa kumjua Mungu, anaweza kumwelewa hatimaye na kumjua Yeye kupitia aina zote za mambo na mbinu. Sababu inayomfanya binadamu kufikiria kwa kutojua kwamba Mungu amemwepuka kimakusudi, kwamba Mungu amejificha kimakusudi kutoka kwa binadamu, kwamba Mungu hana nia yoyote ya kumruhusu mwanadamu kumwelewa na kumjua Yeye, ni kwa sababu hamjui Mungu ni nani, na wala hataki kumuelewa Mungu; na hata zaidi, hajali kuhusu fikira, matamshi au matendo ya Muumba…. Kusema kweli, kama mtu atatumia tu muda wake wa ziada vizuri katika kuzingatia na kuelewa matamshi au matendo ya Muumba na kuuweka umakinifu mchache kwa fikira za Muumba na sauti ya moyo Wake, haitakuwa vigumu kwa wao kutambua ya kwamba fikira, maneno na matendo ya Muumba, vyote vinaonekana na viko wazi. Vilevile, itachukua jitihada kidogo kutambua kwamba Muumba yuko miongoni mwa binadamu wakati wote, kwamba siku zote Anazungumza na binadamu na vitu vyote, na kwamba Anatekeleza matendo mapya kila siku. Kiini Chake na tabia Yake vimeonyeshwa katika mazungumzo Yake na binadamu; fikira na mawazo Yake vyote vinafunuliwa kabisa katika matendo Yake; Anaandamana na mwanadamu na kumtazama wakati wote. Yeye anatumia maneno Yake asiyotamka kuwaambia wanadamu na vitu vyote kwa utulivu: “Mimi niko mbinguni, na Mimi nimo miongoni mwa vitu vyote. Ninaangalia, Ninasubiri; Niko kando yako….” Mikono Yake ni yenye joto na nguvu; nyayo Zake ni nyepesi; sauti Yake ni laini na yenye neema, umbo Lake hupita na kugeuka, likiwakumbatia wanadamu wote; uso Wake ni mzuri na mpole. Hajawahi kuondoka, hajawahi kutoweka. Usiku na mchana, Yeye yuko na mwanadamu siku zote, Asiyeondoka upande wao kamwe.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II
466. Wakati watu hawamwelewi Mungu na hawajui tabia Yake, mioyo yao haiwezi kamwe kumfungukia Yeye kwa kweli. Mara tu wanapomwelewa Mungu, wataanza kuthamini na kufurahia kile kilicho moyoni Mwake kwa shauku na imani. Unapothamini na kufurahia kile kilichomo ndani ya moyo wa Mungu, moyo wako utaanza kwa utaratibu, kidogokidogo, kuwa wazi Kwake. Wakati moyo wako unakuwa wazi Kwake, utahisi jinsi ambavyo mabadilishano yako na Mungu yalivyokuwa ya aibu na dharau, madai yako kwa Mungu, na tamaa zako mwenyewe za kupita kiasi. Moyo wako unapofunguka kwa kweli kwa Mungu, utaona kwamba moyo Wake ni ulimwengu usio na mwisho, na utaingia katika ulimwengu ambao hujawahi kuupitia awali. Katika ulimwengu huu hakuna usaliti, hakuna udanganyifu, hakuna giza, hakuna maovu. Kunao ukweli wa dhati na uaminifu; kuna nuru na uadilifu tu; kuna haki na huruma. Kumejaa upendo na utunzaji, kumejaa rehema na uvumilivu, na kupitia katika ulimwengu huu utahisi shangwe na furaha ya kuwa hai. Mambo haya ndiyo ambayo Atakufichulia utakapoufungua moyo wako kwa Mungu. Ulimwengu huu usio na mwisho umejaa hekima za Mungu, na umejawa na nguvu Zake; umejaa pia upendo Wake na mamlaka Yake. Hapa unaweza kuona kila kipengele cha kile ambacho Mungu Anacho na Alicho, kile kinachomletea Yeye furaha, kwa nini Anakuwa na wasiwasi na kwa nini Anakuwa na huzuni, kwa nini Anakuwa na hasira…. Haya ndiyo ambayo kila mmoja anayeufungua moyo wake na kumruhusu Mungu kuingia ndani anaweza kuona. Mungu anaweza tu kuingia katika moyo wako ikiwa utaufungua kwa ajili Yake. Unaweza kuona tu kile Mungu Anacho na Alicho, na unaweza kuona tu mapenzi Yake kwako, kama Ameingia katika moyo wako. Wakati huo, utagundua kwamba kila kitu kuhusu Mungu ni chenye thamani, kwamba kile ambacho Anacho na Alicho kinastahili kuthaminiwa sana. Ukilinganisha na hayo, watu wanaokuzunguka, vitu na matukio katika maisha yako, hata wapendwa wako, mwandani wako, na mambo unayopenda, si muhimu sana. Ni madogo mno, na ni ya kiwango cha chini; utahisi kwamba hakuna kitu chochote cha nje kitakachoweza kukuvuta tena, au kwamba kitu chochote cha nje kitakachowahi tena kuweza kukushawishi ukilipie gharama yoyote ile. Katika kunyenyekea kwa Mungu utaona ukuu Wake na mamlaka Yake ya juu; aidha, katika jambo Alilofanya ambalo hapo awali uliliamini kuwa ni dogo mno, utaweza kuiona hekima Yake na uvumilivu Wake usio na mwisho, na utaiona subira Yake, uvumilivu Wake na ufahamu Wake kwako. Hili litazaa ndani yako upendo Kwake. Siku hiyo, utahisi kwamba mwanadamu anaishi katika ulimwengu mchafu sana, kwamba watu walio upande wako na mambo yanayokutokea katika maisha yako, na hata wale unaowapenda, upendo wao kwako, na ulinzi wao kama ulivyojulikana au kujali kwao kwako havistahili hata kutajwa—Mungu tu ndiye mpendwa wako na ni Mungu tu ndiye unayethamini zaidi. Siku hiyo itakapowadia, Naamini kwamba kutakuwa na baadhi ya watu watakaosema: Upendo wa Mungu ni mkuu sana na kiini Chake ni kitakatifu mno—ndani ya Mungu hakuna udanganyifu, hakuna uovu, hakuna wivu, na hakuna mabishano, lakini ni haki tu na uhalisi, na kila kitu ambacho Mungu Anacho na Alicho vyote vinafaa kutamaniwa na binadamu. Binadamu wanafaa kujitahidi na kuwa na hamu ya kuvipata. Ni kwa msingi gani ndipo uwezo wa mwanadamu wa kutimiza haya umejengwa? Unajengwa kwa msingi wa ufahamu wa binadamu wa tabia ya Mungu, na ufahamu wao kuhusu kiini cha Mungu. Hivyo basi kuelewa tabia ya Mungu na kile ambacho Anacho na Alicho, ni funzo la maisha yote kwa kila mtu na ni lengo la maisha yote linalofuatiliwa na kila mtu anayelenga kubadilisha tabia yake, na kutamani kumjua Mungu.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III
467. Mungu Mwenyewe ni Mungu Mwenyewe. Hatawahi kuwa sehemu ya uumbaji, na hata kama Atakuwa mwanachama miongoni mwa viumbe vilivyoumbwa, tabia Yake ya asili na kiini Chake havitabadilika. Hivyo basi, kumjua Mungu si sawa na kujua kitu; kumjua Mungu si kuchunguza kitu, na wala si sawa na kumwelewa mtu. Kama mwanadamu atatumia dhana au mbinu yake ya kujua kifaa au kumwelewa mtu ili kumjua Mungu, basi hutawahi kuweza kutimiza maarifa ya Mungu. Kumjua Mungu hakutegemei uzoefu au kufikiria kwako, na hivyo basi hufai kulazimisha uzoefu wako au kufikiria kwako kwa Mungu. Haijalishi uzoefu au kufikiria kwako ni kwa kipekee namna gani, huko kote bado ni finyu; na hata zaidi, kufikiria kwako hakulingani na hoja, isitoshe hakulingani na ukweli, na pia hakulingani na tabia na kiini cha kweli cha Mungu. Hutawahi kamwe kufanikiwa kama utategemea mawazo yako ili kuelewa kiini cha Mungu. Njia ya pekee ni hii: kukubali yote yanayotoka kwa Mungu, kisha kwa utaratibu uweze kuyapitia na kuyaelewa. Kutakuwa na siku ambayo Mungu atakupa nuru ili uweze kuelewa kwa kweli na kumjua Yeye kwa sababu ya ushirikiano wako na kwa sababu ya njaa na kiu yako ya kupenda ukweli.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II
468. “Kumcha Mungu na kujiepusha na maovu” na kumjua Mungu ni uhusiano usiogawanyishwa na uliounganishwa kwa nyuzi zisizohesabika, na uhusiano kati yao ni dhahiri. Iwapo mtu anataka kupata uwezo wa kujiepusha na maovu, lazima kwanza amche Mungu kwa kweli; iwapo mtu anataka kupata uwezo wa kumcha Mungu kwa kweli, lazima awe na maarifa ya kweli kuhusu Mungu; Iwapo mtu anataka kupata maarifa ya Mungu, lazima kwanza apate uzoefu wa maneno ya Mungu, aingie katika uhalisi wa maneno ya Mungu, apitie kuadibu na nidhamu ya Mungu, kuadibu na hukumu Yake; ikiwa mtu anataka kupata uzoefu maneno ya Mungu, lazima aje ana kwa ana na maneno ya Mungu, aje ana kwa ana na Mungu, na kumwomba Mungu Ampe fursa ya kupitia maneno ya Mungu katika kila aina ya mazingira yanayowahusisha watu, matukio na vitu; iwapo mtu anataka kuja ana kwa ana na Mungu na maneno ya Mungu, lazima kwanza awe na moyo wa kweli na wenye uaminifu, awe tayari kuukubali ukweli, kukubali kupitia mateso, awe na azimio na ujasiri wa kujiepusha uovu, na azimio la kuwa kiumbe halisi…. Kwa njia hii, ukiendelea mbele hatua kwa hatua, utamkaribia Mungu zaidi, moyo wako utakuwa safi zaidi, na maisha yako na thamani ya kuwa hai, pamoja na maarifa yako kumhusu Mungu, yatakuwa ya maana zaidi na yatakuwa hata yenye kung’aa zaidi. Mpaka siku moja, utahisi kuwa Muumba sio fumbo tena, kwamba Muumba hajawahi kufichwa kutoka kwako, kwamba Muumba hajawahi kuificha sura Yake kutoka kwako, kwamba Muumba hayuko mbali na wewe hata kidogo, kwamba Muumba siye Yule tena ambaye unamtamani kila mara katika mawazo yako lakini kwamba huwezi kumfikia kwa hisia zako, kwamba Anasimama kwa kweli kama mlinzi kulia na kushoto kwako, Akiruzuku maisha yako, na kudhibiti majaliwa yako. Hayuko katika upeo wa mbali, wala Hajajificha juu mawinguni. Yuko kando yako, akiwa na mamlaka juu ya kila kitu chako, Yeye ndiye kila kitu ulicho nacho, na Yeye ni kitu pekee ulicho nacho. Mungu kama huyo Anakuruhusu umpende kutoka moyoni, umshikilie, umweke karibu, umtamani, uhofu kumpoteza, na kutokuwa tayari kumkana tena, kumwasi tena, ama kumwepuka tena ama kumweka mbali. Kile unachotaka ni kumjali tu, kumtii, kulipia kila kitu Anachokupa, na kujisalimisha katika utawala Wake. Haukatai tena kuongozwa, kuruzukiwa, kutazamwa, na kutunzwa na Yeye, haukatai tena kile Anachoamuru na kupangilia kwa ajili yako. Unachotaka tu ni kumfuata, kutembea kando Yake iwe ni kushoto ama kulia Kwake, kile unachotaka ni kumkubali kama uzima wako wa pekee, kumkubali kama Bwana wako wa pekee, Mungu wako wa pekee.
Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Dibaji