L. Kuhusu Jinsi ya Kumtumikia Mungu na Kumshuhudia

469. Tangu mwanzo wa kazi Yake katika ulimwengu mzima, Mungu amewaamulia kabla watu wengi kumhudumia, wakiwemo watu kutoka kila tabaka la maisha. Kusudio Lake ni kutimiza mapenzi Yake mwenyewe na kuhakikisha kwamba kazi Yake hapa ulimwenguni inatimia kwa urahisi. Hili ndilo kusudio la Mungu katika kuwachagua watu wa kumhudumia. Kila mtu anayemhudumia Mungu lazima aelewe mapenzi haya ya Mungu. Kupitia kazi hii Yake, watu wanaweza kuona vizuri zaidi hekima ya Mungu na kudura ya Mungu, na kuona kanuni za kazi Yake hapa ulimwenguni. Mungu kwa kweli anakuja ulimwenguni kufanya kazi Yake, kuwasiliana na watu, ili nao waweze kuona vizuri zaidi matendo Yake. Leo, kundi hili la watu lina bahati kubwa kwa kundi hili lenu kumhudumia Mungu wa utendaji. Hii ni baraka isiyopimika kwenu. Kwa kweli ni Mungu anayewainua. Katika kumteua mtu ili amhudumie, Mungu siku zote huwa na kanuni Zake binafsi. Kumhudumia Mungu hakika, kama vile watu wanavyofikiria, si suala tu la kuwa na shauku. Leo mnaona kwamba mtu yeyote anayeweza kumhudumia Mungu akiwa mbele Yake anafanya hivyo kwa sababu wana mwongozo wa Mungu na kazi ya Roho Mtakatifu, na kwa sababu wao ni watu wanaofuata ukweli. Haya ndiyo mahitaji ya kiwango cha chini zaidi ambayo wote wanaomhudumia Mungu wanapaswa kuwa nayo.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Njia ya Huduma ya Kidini lazima Ipigwe Marufuku

470. Wanaomhudumia Mungu wanapaswa kuwa marafiki wema wa Mungu, wanapaswa kumfurahisha Mungu, na kuwa na uaminifu wa hali ya juu kwa Mungu. Bila kujali iwapo unatenda bila kuonekana na watu, au mbele ya watu, unaweza kupata furaha ya Mungu mbele za Mungu, unaweza kusimama imara mbele za Mungu, na bila kujali jinsi watu wengine wanavyokutendea, wewe huifuata njia yako mwenyewe kila mara, na kuushughulikia kwa makini mzigo wa Mungu. Mtu wa aina hii pekee ndiye rafiki mwema wa Mungu. Marafiki wema wa Mungu wanaweza kumhudumia Yeye moja kwa moja kwa sababu wamepewa agizo kuu la Mungu, na mzigo wa Mungu, wao wanaweza kuuchukulia moyo wa Mungu kama moyo wao wenyewe, na mzigo wa Mungu kama mzigo wao wenyewe, na hawazingatii iwapo watafaidi au watapoteza matarajio: Hata wasipokuwa na matarajio, na hawatafaidi chochote, watamwamini Mungu daima kwa moyo wa upendo. Kwa hivyo, mtu wa aina hii ni rafiki mwema wa Mungu. Marafiki wema wa Mungu ni wasiri Wake pia; ni wasiri wa Mungu pekee ndio wanaoweza kushiriki katika kutotulia Kwake, matamanio Yake, na ingawa mwili wao una uchungu na ni mdhaifu, wanaweza kuvumilia uchungu na kuacha kile wanachokipenda ili kumridhisha Mungu. Mungu huwapa watu wa aina hii mizigo mingi, na kile ambacho Mungu anataka kufanya kinathibitishwa katika ushuhuda wa watu kama hawa. Yaani, watu hawa wanapendwa na Mungu, wao ni watumishi wa Mungu wanaoupendeza moyo Wake, na ni watu wa aina hii pekee ndio wanaoweza kutawala pamoja na Mungu. Ukishakuwa rafiki mwema wa Mungu ndipo utakapoweza kabisa kutawala pamoja na Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu

471. Mtu anayemhudumia Mungu kwa ukweli ni Yule anayeitafuta roho ya Mungu na anayefaa kutumiwa na Mungu na anayeweza kuacha dhana zake za kidini. Ikiwa unataka kunywa na kula kwako kwa maneno ya Mungu kuzaa matunda, basi ni sharti uache dhana zako za kidini. Ikiwa unataka kumhudumia Mungu, basi ni muhimu zaidi kuacha dhana zako za kidini na kutii maneno ya Mungu kwa kila unachokifanya. Hizi ni sifa za lazima kwa yeyote anayemhudumia Mungu. Ukikosa ufahamu huu, punde tu unapohudumu utasababisha hitilafu na usumbufu, na ukiendelea kushikilia dhana zako, basi bila shaka utagongwa chini na Mungu, usinyanyuke daima. Chukulia wakati wa sasa kama mfano. Mengi ya matamshi na kazi za leo hazilingani na Biblia pamoja na kazi zilizofanywa na Mungu hapo awali, na kama huna nia ya kutii, basi unaweza kuanguka wakati wowote. Ikiwa unataka kuhudumu kulingana na mapenzi ya Mungu, basi unapaswa kuziacha kwanza dhana zako za kidini na urekebishe mitazamo yako. Mengi ya yale yatakayosemwa katika siku za usoni hayatalingana na yaliyosemwa zamani na ikiwa sasa unakosa nia ya kutii, hutaweza kuipita njia iliyo mbele yako. Ikiwa njia moja ya Mungu ya kufanya kazi imechipuka ndani yako na huachii dhana zako, basi njia hii itakuwa dhana zako za kidini. Ikiwa kile Mungu Alicho kimekita mizizi ndani yako, basi umepata ukweli, na ikiwa maneno na ukweli wa Mungu unaweza kuwa maisha yako, kamwe hutakuwa na dhana kuhusu Mungu. Walio na ufahamu wa kweli kuhusu Mungu hawatakuwa na dhana na hawatatii mafundisho ya kidini.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Wale tu Wanaoijua Kazi ya Mungu Leo Ndio Wanaoweza Kumhudumia Mungu

472. Kumtumikia Mungu si kazi rahisi. Wale ambao tabia yao potovu haibadiliki hawawezi kamwe kumhudumia Mungu. Kama tabia yako haijahukumiwa na kuadibiwa na neno la Mungu, basi tabia yako bado inamwakilisha Shetani. Hii inatosha kuthibitisha kwamba huduma yako kwa Mungu ni kutokana na nia yako nzuri wewe binafsi. Ni huduma inayotokana na asili yako ya kishetani. Unamhudumia Mungu na hulka yako ya kiasili, na kulingana na mapendeleo yako ya kibinafsi; na zaidi, unaendelea kufikiria kwamba Mungu anapenda chochote kile unachopenda kufanya, na kwamba Mungu anachukia chochote kile ambacho hupendi kufanya, na unaongozwa kabisa na mapendeleo yako binafsi katika kazi yako. Je, huku kunaweza kuitwa kumhudumia Mungu? Hatimaye tabia yako ya maisha haitabadilishwa hata chembe; badala yake, utakuwa msumbufu hata zaidi kwa sababu umekuwa ukimhudumia Mungu, na hii itafanya tabia yako potovu kukita mizizi zaidi. Kwa njia hii, utaendeleza kwa ndani sheria kuhusu huduma kwa Mungu zitokanazo kimsingi na hulka yako binafsi, na uzoefu unaotokana na kuhudumu kwako kulingana na tabia yako binafsi. Hili ni funzo kutokana na uzoefu wa kibinadamu. Ni falsafa ya binadamu ya kuishi katika dunia. Watu kama hawa ni wa Mafarisayo na wale wajumbe wa kidini. Kama hawatawahi kuzinduka na kutubu, basi hakika watageuka na kuwa wale Makristo wa uwongo na wapinga Kristo watakaowadanganya watu katika siku za mwisho. Makristo wa uwongo na wapinga Kristo waliozungumziwa watainuka kutoka miongoni mwa watu kama hawa. Kama wale wanaomhudumia Mungu watafuata hulka yao na kutenda kulingana na mapenzi yao binafsi, basi wamo katika hatari ya kutupwa nje wakati wowote. Wale wanaotumia miaka yao mingi ya uzoefu kwa kumhudumia Mungu ili kutega mioyo ya watu, kuwasomea na kuwadhibiti, kujiinua wao wenyewe—na wale katu hawatubu, katu hawakiri dhambi zao, katu hawakatai manufaa ya cheo—watu hawa wataanguka mbele ya Mungu. Hawa ni watu walio kama Paulo, waliojaa majivuno ya vyeo vyao na wanaoonyesha ukubwa wao. Mungu hatawakamilisha watu kama hawa. Aina hii ya huduma huzuia kazi ya Mungu. Watu wanapenda kushikilia vitu vya kale. Wanashikilia fikira za kale, wanashikilia vitu vya kale. Hiki ni kizuizi kikuu katika huduma yao. Kama huwezi kuvitupa vitu hivi, vitu hivyo vitayakaba maisha yako yote. Mungu hatakupongeza, hata kidogo, hata kama utaivunja miguu yako au mgongo wako ukitia bidii, au hata ukifa katika “huduma” ya Mungu. Kinyume cha mambo ni kwamba: Atasema kwamba wewe ni mtenda maovu.

Kufikia leo, Mungu atawakamilisha kirasmi wale wasiokuwa na fikira za kidini, ambao wako tayari kuweka pembeni nafsi zao za kale, na ambao wanamtii tu Mungu kwa moyo wa kawaida, na kuwafanya kuwa watimilifu wale wanaotamani neno la Mungu. Watu hawa wanafaa kusimama na kumhudumia Mungu. Kwake Mungu kunayo hekima nyingi na isiyoisha. Kazi Yake ya kustaajabisha na matamshi Yake yenye thamani vinasubiri hata idadi kubwa ya watu waweze kuvifurahia. Kama ilivyo sasa, wale walio na fikira za kidini, wanaochukua hali ya ukubwa, na wale ambao hawawezi kujiweka pembeni wanaona vigumu sana kukubali vitu hivi vipya. Hakuna fursa ya Roho Mtakatifu kuwakamilisha watu hawa. Kama mtu hajaamua kutii, na hana kiu ya neno la Mungu, basi mtu huyo hataweza kupokea mambo mapya. Wataendelea tu kuwa waasi zaidi na zaidi, kuwa wajanja zaidi na zaidi, na hatimaye kujipata kwenye njia mbaya. Katika kufanya kazi Yake sasa, Mungu atawainua watu zaidi wanaompenda kwa kweli na wanaoweza kukubali mwangaza mpya. Na Atakatiza kabisa maafisa wa kidini wanaoonyesha ukubwa wao. Wale wanaokataa mabadiliko kwa ukaidi: Hataki hata mmoja wao. Je, unataka kuwa mmoja wa watu hao? Je, unatekeleza huduma yako kulingana na mapendeleo yako, au unafanya kile Mungu anachotaka? Hili ni jambo ambalo lazima ujijulie mwenyewe. Je, wewe ni mmojawapo wa maafisa wa kidini, au wewe ni mtoto mchanga anayefanywa kuwa mtimilifu na Mungu? Je, ni kiwango kipi cha huduma yako ambacho kinapongezwa na Roho Mtakatifu? Ni kiwango kipi ambacho Mungu hatasumbuka kukumbuka? Baada ya miaka mingi ya huduma, maisha yako yamebadilika kiasi kipi? Je, uko wazi kuhusu mambo haya yote? Kama unayo imani ya kweli, basi utaweka pembeni fikira zako za kale za kidini na utamhudumia Mungu kwa njia bora zaidi na kwa njia mpya. Hujachelewa sana kusimama sasa. Fikira za kale za kidini zitayakaba maisha ya mtu. Uzoefu ambao mtu anapata utamwongoza mbali na Mungu, kufanya mambo kwa njia yake mwenyewe. Usipoviweka vitu hivi chini, vitakuwa kikwazo katika kukua kwa maisha yako. Mungu siku zote amewakamilisha wote wanaomhudumia. Hawatupilii mbali kwa urahisi tu. Kama tu utakubali kwa kweli hukumu na kuadibu kwa neno la Mungu, kama unaweza kuweka pembeni matendo yako na sheria za kidini za kale, na kukoma kutumia fikira za kale za kidini kama kipimo cha neno la Mungu hii leo, ni hapo tu ndipo kutakuwa na mustakabali kwako. Lakini kama utashikilia vitu vya kale, kama bado unavithamini, basi huwezi kupata wokovu. Mungu hawatambui watu kama hao. Kama kweli unataka kukamilishwa, basi lazima uamue kutupilia mbali kabisa kila kitu cha kale. Hata kama kile kilichokuwa kimefanywa awali kilikuwa sahihi, hata kama ilikuwa ni kazi ya Mungu, ni lazima bado uweze kuiweka pembeni na uache kuishikilia. Hata kama ilikuwa kazi ya Roho Mtakatifu iliyo wazi, iliyofanywa moja kwa moja na Roho Mtakatifu, leo lazima uiweke pembeni. Hufai kuishikilia. Hili ndilo Mungu anahitaji. Kila kitu lazima kifanywe upya. Katika kazi ya Mungu na neno la Mungu, Harejelei vitu vya kale ambavyo vilishapita, na vilevile Hafukui historia ya kale. Mungu siku zote ni mpya na kamwe si mzee. Hashikilii hata maneno Yake mwenyewe ya kitambo inayoonyesha kwamba Mungu hafuati mafundisho ya dini yoyote. Katika hali hii, kama mwanadamu, kama siku zote unashikilia kabisa vitu vya kale, ukikataa kuviachilia na kuvitumia kwa njia ya fomyula, huku naye Mungu hafanyi kazi tena katika njia Alizokuwa akifanya awali, basi maneno yako na matendo yako siyo ya kukatiza? Je, hujawa adui wa Mungu? Je, uko radhi kuyaacha maisha yako yote yaharibike kwa sababu ya mambo haya ya kale? Mambo haya ya kale yatakufanya kuwa mtu anayezuia kazi ya Mungu. Je, mtu kama huyo ndiye wewe unataka kuwa? Kama kweli hutaki kuwa hivyo, basi acha mara moja kile unachofanya na ubadilike; anza tena upya. Mungu hakumbuki huduma yako ya kale.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Njia ya Huduma ya Kidini lazima Ipigwe Marufuku

473. Kila mtu ambaye ameamua anaweza kumhudumia Mungu—lakini ni lazima iwe kwamba wale tu ambao wanayashughulikia kwa makini mapenzi ya Mungu na kuyafahamu mapenzi ya Mungu ndio wanaohitimu na walio na haki ya kumhudumia Mungu. Nimegundua hili kati yenu: Watu wengi wanaamini ya kuwa bora tu wanaeneza injili kwa bidii kwa ajili ya Mungu, waende barabarani kwa ajili ya Mungu, wajitumie na kuacha vitu kwa ajili ya Mungu, na kadhalika, basi huku ni kumhudumia Mungu; hata zaidi, watu wa kidini huamini kwamba kumhudumia Mungu kuna maana ya kukimbia hapa na pale wakiwa na Biblia mikononi mwao, wakieneza injili ya ufalme wa mbinguni na kuwaokoa watu kwa kuwafanya watubu na kuungama; kuna wakuu wengi wa kidini wanaofikiri kwamba kumhudumia Mungu ni kuhubiri makanisani baada ya kusoma na kufunzwa katika chuo cha seminari, kuwafunza watu kwa kusoma sura za Biblia; pia kuna watu katika maeneo ya umaskini wanaoamini kwamba kumhudumia Mungu kuna maana ya kupokea uponyaji na kufukuza mapepo, au kuwaombea ndugu, au kuwahudumia; miongoni mwenu, kunao wengi wanaoamini kwamba kumhudumia Mungu kuna maana ya kula na kunywa maneno ya Mungu, kumwomba Mungu kila siku, na pia kutembelea na kufanya kazi katika makanisa kila mahali; kunao ndugu wengine wanaoamini kwamba kumhudumia Mungu kunamaanisha kutoolewa wala kulea familia kamwe, na kutoa nafsi zao zote kwa Mungu. Ilhali watu wachache wanajua maana ya kweli ya kumhudumia Mungu. Ingawa kunao wengi wanaomhudumia Mungu kama nyota angani, idadi ya wale wanaoweza kuhudumu moja kwa moja, na wanaoweza kutumikia kulingana na mapenzi ya Mungu, ni hafifu—ndogo isiyo na maana. Kwa nini Ninasema hivi? Ninasema hivi kwa sababu wewe hufahamu kiini cha fungu la maneno “huduma kwa Mungu,” na unafahamu machache sana kuhusu jinsi ya kutumikia kulingana na mapenzi ya Mungu. Kuna hitaji la haraka kwa watu kuelewa hasa ni aina gani ya huduma kwa Mungu ndiyo inayoweza kulingana na mapenzi Yake.

Ikiwa ungependa kutumikia kulingana na mapenzi ya Mungu, ni lazima kwanza ufahamu ni watu wa aina gani wanamfurahisha Mungu, ni watu wa aina gani wanachukiwa na Mungu, ni watu wa aina gani wanafanywa kuwa kamili na Mungu, na ni watu wa aina gani wana sifa zinazostahili kumhudumia Mungu. Hiki ni kiasi kidogo zaidi unachopaswa kujiandaa nacho. Isitoshe, unapaswa kujua malengo ya kazi ya Mungu, na kazi ambayo Mungu Ataitenda hapa na wakati huu. Baada ya kufahamu haya, na kupitia kwa mwongozo wa maneno ya Mungu, kwanza unafaa kuingia, na kupokea agizo la Mungu kwanza. Unapopata uzoefu wa kweli kwa msingi wa maneno ya Mungu, na unapojua kweli kazi ya Mungu, utakuwa umehitimu kumhudumia Mungu. Na unapomhudumia ndipo Mungu hufungua macho yako ya kiroho, na kukuruhusu kuwa na ufahamu mkubwa zaidi wa kazi Yake na kuiona dhahiri zaidi. Ukiingia katika ukweli huu, uzoefu wako utakuwa wa kina zaidi na wa kweli, na wale wote ambao wamepata uzoefu wa aina hiyo wataweza kutembea miongoni mwa makanisa mengi na kuwatolea ndugu zako, ili muweze kutumia nguvu za kila mmoja kufidia upungufu wako na kupata maarifa mengi zaidi ndani ya roho zenu. Ni baada tu ya kutimiza matokeo haya ndipo utakapoweza kutumikia kulingana na mapenzi ya Mungu na kufanywa mkamilifu na Mungu wakati wa kufanya huduma yako.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu

474. Wale wanaoweza kuyaongoza makanisa, kuwaruzuku watu maisha, na kuwa mtume kwa watu, wanapaswa kuwa na uzoefu halisi, ufahamu sahihi wa masuala ya kiroho, kuelewa vyema na kuwa na uzoefu wa ukweli. Watu wa namna hiyo tu ndio wanaostahili kuwa watenda kazi au mitume wanaoyaongoza makanisa. Vinginevyo, wanaweza kutufuata tu kidogo na hawawezi kuongoza, sembuse kuwa mtume mwenye uwezo wa kuwapatia watu uhai. Hii ni kwa sababu kazi ya mitume siyo kukimbia au kupigana; ni kufanya kazi ya kutoa huduma ya maisha na kuwaongoza wengine katika kubadili tabia zao. Wale wanaofanya kazi hii wanaagizwa kubeba mzigo mkubwa, ambao si kitu ambacho kila mtu anaweza kufanya. Kazi ya aina hii inaweza tu kufanywa na wale ambao wana maisha ya uwepo, yaani, wale ambao wana uzoefu wa ukweli. Haiwezi kufanywa na kila mtu ambaye anaweza kukata tamaa, anaweza kukimbia au yupo tayari kutumia pesa; watu ambao hawana uzoefu wa ukweli, wale ambao hawajapogolewa au kuhukumiwa, hawawezi kufanya kazi ya aina hii. Watu ambao hawana uzoefu, yaani, watu wasio na ukweli, hawawezi kuona ukweli kwa uwazi kwa kuwa wao wenyewe hawako katika hali hii. Hivyo, mtu wa aina hii si kwamba hawezi tu kufanya kazi ya kuongoza bali atakuwa mlengwa wa kuondolewa ikiwa hatakuwa na ukweli kwa muda mrefu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu

475. Kazi inapozungumziwa, mwanadamu anaamini kwamba kazi ni kusafiri kwenda huku na huko kwa ajili ya Mungu, akihubiri kila sehemu, na kugharimia rasilmali kwa ajili ya Mungu. Ingawa imani hii ni sahihi, ni ya kuegemea upande mmoja sana; kile ambacho Mungu anamwomba mwanadamu si kusafiri kwenda huku na huko kwa ajili ya Mungu; ni huduma zaidi na kujitoa ndani ya roho. Ndugu wengi hawajawahi kufikiria juu ya kumfanyia Mungu kazi hata baada ya miaka mingi sana ya uzoefu, maana kazi kama mwanadamu anavyoielewa haipatani na ile ambayo Mungu anaitaka. Kwa hiyo, mwanadamu havutiwi kwa namna yoyote ile na kazi ya Mungu, na hii ndiyo sababu kuingia kwa mwanadamu ni kwa kuegemea upande mmoja kabisa. Nyinyi nyote mnapaswa kuingia kwa kumfanyia Mungu kazi, ili muweze kupata uzoefu wa vipengele vyake vyote. Hiki ndicho mnapaswa kuingia ndani. Kazi haimaanishi kutembea huku na huko kwa ajili ya Mungu; maana yake ni iwapo maisha ya mwanadamu na kile ambacho mwanadamu anaishi kwa kudhihirisha ni kwa ajili ya Mungu kufurahia. Kazi inamaanisha mwanadamu kutumia uaminifu alio nao kwa Mungu na maarifa aliyo nayo juu ya Mungu ili kumshuhudia Mungu na kumhudumia mwanadamu. Huu ndio wajibu wa mwanadamu, na yote ambayo mwanadamu anapaswa kutambua. Kwa maneno mengine, kuingia kwenu ni kazi yenu; mnatafuta kuingia wakati wa kazi yenu kwa ajili ya Mungu. Kupitia kazi ya Mungu hakumaanishi tu kwamba unajua jinsi ya kula na kunywa neno Lake; na muhimu zaidi, mnapaswa kuweza kumshuhudia Mungu, kumtumikia Mungu, na kumhudumia na kumkimu mwanadamu. Hii ni kazi, na pia kuingia kwenu; hiki ndicho kila mwanadamu anapaswa kukitimiza. Kuna watu wengi ambao wanatilia mkazo tu katika kusafiri huku na huko kwa ajili ya Mungu, na kuhubiri kila sehemu, lakini hawazingatii uzoefu wao binafsi na kupuuza kuingia kwao katika maisha ya kiroho. Hiki ndicho kinasababisha wale wanaomtumikia Mungu kuwa watu wanaompinga Mungu. …

Mtu anafanya kazi ili kutimiza mapenzi ya Mungu, kuwaleta wale wote wanaoutafuta moyo wa Mungu mbele Yake, kumleta mwanadamu kwa Mungu, na kuitambulisha kazi ya Roho Mtakatifu na uongozi wa Mungu kwa mwanadamu, kwa kufanya hivyo atakuwa anayakamilisha matunda ya kazi ya Mungu. Kwa sababu hii, ni muhimu kuelewa kiini cha kufanya kazi. Kama mtu anayetumiwa na Mungu, watu wote wanafaa kumfanyia kazi Mungu, yaani, wote wana fursa ya kutumiwa na Roho Mtakatifu. Hata hivyo kuna hoja moja mnayopaswa kuielewa: Mwanadamu anapofanya kazi iliyoagizwa na Mungu, mwanadamu anakuwa amepewa fursa ya kutumiwa na Mungu, lakini kile kinachosemwa na kujulikana na mwanadamu sio kimo cha mwanadamu kabisa. Mnaweza tu kujua vizuri kasoro zako katika kazi yenu, na kupokea nuru kubwa kutoka kwa Roho Mtakatifu, kwa kufanya hivyo mtakuwa mnaweza kupata kuingia kuzuri katika kazi yenu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (2)

476. Huduma ambayo imetenganishwa na matamshi ya sasa ya Roho Mtakatifu ni huduma ambayo ni ya mwili, na ya dhana, na haiwezi kuwa kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu. Kama watu huishi miongoni mwa dhana za kidini, basi hawawezi kufanya lolote lenye kustahili kwa mapenzi ya Mungu, na hata ingawa wao humhudumia Mungu, wao huhudumu katikati ya mawazo na dhana zao, na hawawezi kabisa kuhudumu kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu. Wale ambao hawawezi kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu hawaelewi mapenzi ya Mungu, na wale ambao hawaelewi mapenzi ya Mungu hawawezi kumhudumia Mungu. Mungu hutaka huduma inayoupendeza moyo Wake mwenyewe; Hataki huduma ambayo ni ya dhana na mwili. Kama watu hawawezi kuzifuata hatua za kazi ya Roho Mtakatifu, basi wao huishi katikati ya dhana. Huduma ya watu hao hukatiza na huvuruga, na huduma ya aina hii huenda kinyume na Mungu. Hivyo wale ambao hawawezi kuzifuata nyayo za Mungu hawawezi kumhudumia Mungu; wale ambao hawawezi kuzifuata nyayo za Mungu humpinga Mungu bila shaka, na ni wasioweza kulingana na Mungu. “Kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu” kuna maana ya kufahamu mapenzi ya Mungu leo, kuweza kutenda kwa mujibu wa masharti ya sasa ya Mungu, kuweza kutii na kumfuata Mungu wa leo, na kuingia kwa mujibu wa matamshi mapya zaidi ya Mungu. Huyu pekee ndiye mtu ambaye hufuata kazi ya Roho Mtakatifu na yuko ndani ya mkondo wa Roho Mtakatifu. Watu hao hawawezi tu kupokea sifa za Mungu na kumwona Mungu, lakini wanaweza pia kujua tabia ya Mungu kutoka kwa kazi ya karibuni zaidi ya Mungu, na wanaweza kujua dhana na ukaidi wa mwanadamu, na asili na kiini cha mwanadamu, kutoka kwa kazi Yake ya karibuni zaidi; pia, wanaweza kutimiza polepole mabadiliko katika tabia yao wakati wa huduma yao. Ni watu kama hawa pekee ndio wanaoweza kumpata Mungu, na ambao wamepata kwa halisi njia ya kweli.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Ufuate Nyayo Zake

477. Unapomhudumia Mungu wa leo, ikiwa unashikilia vitu vilivyoangaziwa nuru na Roho Mtakatifu hapo zamani, basi huduma yako itasababisha hitilafu na vitendo vyako vitakuwa vimepitwa na wakati na havitakuwa tofauti na ibada ya kidini. Ikiwa unaamini kuwa wanaomhudumia Mungu wanafaa kuwa wanyenyekevu na wavumilivu…, na ukiweka ufahamu wa aina hii katika vitendo leo hii, basi vitendo kama hivi ni dhana ya kidini, na vitendo kama hivyo ni maigizo ya kinafiki. “Dhana za kidini” inarejelea vitu vilivyopitwa na wakati (kutia ndani ukubalifu wa maneno yaliyonenwa na Mungu zamani na kufichuliwa na Roho Mtakatifu), na vikiwekwa katika vitendo leo, basi vitahitilafiana na kazi ya Mungu na havitamfaidi mwanadamu. Iwapo mwanadamu hawezi kuyatakasa dhana za kidini yaliyomo ndani yake, basi yatakuwa kizuizi kizito katika kumuhudumia Mungu. Walio na dhana za kidini hawana njia ya kuendelea sawia na hatua za kazi ya Roho Mtakatifu, watakuwa nyuma hatua moja, halafu mbili—kwani hizi dhana za kidini humfanya mwanadamu kuwa mtu wa kujitukuza na mwenye kiburi. Mungu hahisi kumbukumbu kwa ajili ya Alichokinena na kukifanya hapo zamani; kama kimepitwa na wakati, basi Anakiondoa. Hakika unaweza kuziacha dhana zako? Ukiyakatalia maneno aliyoyanena Mungu hapo zamani, je hili linadhihirisha kuwa unaijua kazi ya Mungu? Kama huwezi kukubali mwangaza wa Roho Mtakatifu leo na badala yake unashikilia mwangaza wa zamani, hili laweza kuthibitisha kuwa unafuata nyayo za Mungu? Je, bado huwezi kuziacha dhana za kidini? Ikiwa ndivyo ilivyo, basi utakuwa mpinga Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Wale tu Wanaoijua Kazi ya Mungu Leo Ndio Wanaoweza Kumhudumia Mungu

478. Wengi humhudumia Mungu kwa misingi ya hisia kali, na hawajui katu amri za utawala za Mungu, sembuse kuelewa athari za neno Lake. Na kwa hivyo, na nia zao nzuri, mara nyingi wanaishia kufanya vitu vinavyokatiza usimamizi wa Mungu. Kwa hali za uzito sana, wanatupwa nje na kunyang’anywa fursa yoyote zaidi ya kumfuata, na wanatupwa kuzimu bila ya kuwa na uhusiano wowote mwingine na nyumba ya Mungu unakoma. Watu hawa hufanya kazi katika nyumba ya Mungu wakiwa na nia nzuri zisizojua na wanaishia kuikasirisha tabia ya Mungu. Watu huleta njia zao za kuwahudumia wakuu na mabwana katika nyumba ya Mungu na kujaribu kufanya yatumike, wakidhania kwa kiburi kwamba njia kama hizo zinaweza kutumika hapa bila jitihada. Hawakuwahi kufikiria kwamba Mungu hana ile tabia ya mwanakondoo bali ile ya simba. Kwa hiyo, wanaojihusisha na Mungu kwa mara ya kwanza wanashindwa kuwasiliana na Yeye, kwani moyo wa Mungu ni tofauti na ule wa binadamu. Ni baada tu ya kuelewa ukweli mwingi ndipo unapoweza kujua siku zote kumhusu Mungu. Maarifa haya si mafungu wala mafundisho, lakini yanaweza kutumika kama hazina ya kuingia katika matumaini ya karibu na Mungu, na ithibati kwamba Anafurahishwa na wewe. Kama unakosa uhalisi wa maarifa na hujajiandaa ukweli, basi huduma yako ya shauku itakuletea tu hali ya chuki ya kupindukia na kuchukizwa sana kwa Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maonyo Matatu

479. Katika ulimwengu wa dini, watu wengi huteseka pakubwa maishani mwao mwote, kwa kuihini miili yao au kuubeba msalaba wao, au hata kuteseka na kustahimili hadi pumzi zao za mwisho! Wengine huwa wanafunga hadi siku ya kifo chao. Katika maisha yao yote wanajinyima chakula kizuri na mavazi mazuri, wakisisitiza mateso tu. Wanaweza kuihini miili yao na kuinyima miili yao. Uwezo wao wa kustahimili mateso unastahili sifa. Ila fikira zao, mawazo yao, mielekeo yao ya kiakili, na kwa hakika asili yao ya kale, havijashughulikiwa hata kidogo. Hawana ufahamu wowote wa kweli kujihusu. Picha ya Mungu akilini mwao ni ile ya kijadi na ya kidhahania, Mungu asiye yakini. Uamuzi wao wa kuteseka kwa ajili ya Mungu unaletwa na azma na asili yao chanya. Hata ikiwa wanamwamini Mungu, hawamfahamu Mungu wala kuyafahamu mapenzi Yake. Wanamfanyia Mungu kazi na kumtesekea Mungu kama vipofu. Hawawekei utambuzi thamani yoyote na hawajishughulishi na jinsi ambayo huduma yao inatimiza mapenzi ya Mungu kwa kweli. Aidha hawajui jinsi ya kutimiza ufahamu kuhusu Mungu. Mungu wanayemhudumia si Mungu katika sura Yake ya asili, ila ni Mungu waliyejifikiria, Mungu waliyemsikia, au Mungu wa kihadithi wanayemsoma katika maandiko. Kisha wanatumia mawazo yao dhahiri na mioyo yao ya kiungu kumtesekea Mungu na kuifanya kazi ambayo Mungu anapaswa kufanya. Huduma yao haiko sahihi, kiasi kwamba hakuna yeyote kati yao anayeweza kuhudumu kulingana na mapenzi ya Mungu. Haijalishi wako radhi kiasi gani kuteseka, mitazamo yao asilia ya huduma na picha ya Mungu akilini mwao havibadiliki kwani hawajapitia hukumu ya Mungu na kuadibu na usafishaji Wake na ukamilifu, na kwa sababu hakuna yeyote aliyewaongoza na ukweli. Japo wanasadiki kwa Yesu Mwokozi, hamna kati yao aliyewahi kumwona Mwokozi. Wamemsikia tu kwa hadithi na uvumi. Hivyo huduma yao ni sawa na kuhudumu mara mojamoja macho yao yakiwa yamefungwa kama kipofu anayemhudumia baba yake. Ni nini kinaweza kupatikana kutokana na huduma kama hiyo? Na ni nani anaweza kuikubali? Huduma yao haibadiliki kamwe toka mwanzo hadi mwisho. Wanapokea mafunzo ya kibinadamu na kukita huduma yao katika uasili wao na kile wanachokipenda wao. Hili laweza kuzalisha faida gani? Hata Petro, aliyemwona Yesu, hakujua jinsi ya kumhudumia Mungu kwa njia inayotimiza mapenzi ya Mungu. Ni katika uzee wake ndipo alipopata ufahamu. Hili linaonyesha nini kuhusu wanadamu vipofu ambao hawajapitia ushughulikiaji na hawana upogoaji na ambao hawajawahi kupata yeyote wa kuwaongoza? Je, si huduma ya wengi miongoni mwenu leo ni kama ile ya vipofu? Wale wote ambao hawajapokea hukumu, hawajapokea upogoaji na ushughulikiaji, na hawana mabadiliko—je, wao si waliokosa kushindwa kabisa? Wana manufaa gani watu kama hao? Ikiwa fikira zako, ufahamu wako wa maisha, na ufahamu wako wa Mungu hauonyeshi mabadiliko mapya na hautoi faida hata kidogo, hutatimiza chochote kizuri katika huduma yako.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (3)

480. Yesu aliweza kukamilisha agizo la Mungu—kazi ya ukombozi wa wanadamu wote—kwa sababu alikabidhi kila tatizo kwa mapenzi ya Mungu, bila kufuata mipango na fikira Zake binafsi. Basi pia, Yeye Alikuwa rafiki mwema wa Mungu—Mungu Mwenyewe, jambo ambalo nyote mnalielewa vizuri sana. (Kwa kweli, alikuwa Mungu Mwenyewe aliyetolewa ushahidi na Mungu; Ninataja jambo hili hapa kwa kuutumia ukweli wa Yesu ili kuonyesha mfano wa suala hili.) Aliweza kuuweka mpango wa usimamizi wa Mungu katika kiini cha mambo yote, na kila mara alimwomba Baba wa mbinguni na kuyatafuta mapenzi ya Baba wa mbinguni. Aliomba, na kusema: “Mungu Baba! Timiza kile ambacho ni mapenzi Yako, na usitende kulingana na nia Zangu; ingekuwa heri ukitenda kulingana na mpango Wako. Mwanadamu anaweza kuwa dhaifu, lakini kwa nini unapaswa kumshughulikia? Ni vipi ambavyo mwanadamu anaweza kustahili kukuhangaisha, mwanadamu ambaye ni kama chungu mkononi Mwako? Ndani ya moyo Wangu, Ninatamani tu kutimiza mapenzi Yako, na Ninatamani Utende Unachotaka kutenda ndani Yangu kulingana na makusudio Yako mwenyewe.” Alipokuwa njiani kuelekea Yerusalemu, Yesu alihisi maumivu makali, kama kwamba kisu kilikuwa kimedungwa ndani ya moyo Wake, ilhali hakuwa na nia yoyote ya kwenda kinyume cha Neno lake; kila mara kulikuwa na nguvu zenye uwezo mkuu zilizomvutia Yeye kuelekea mahali ambapo Angesulubiwa. Mwishowe, alipigiliwa misumari juu ya msalaba na akawa mfano wa mwili wenye dhambi, akiikamilisha kazi hiyo ya ukombozi wa wanadamu, na kufufuka kutoka kwa pingu za kifo na Kuzimu. Mbele Yake, kifo, jehanamu, na Kuzimu vilipoteza nguvu zao, na vilishindwa Naye. Aliishi miaka thelathini na tatu, na katika miaka hiyo yote daima Alifanya kila Alichoweza kutimiza mapenzi ya Mungu kulingana na kazi ya Mungu wakati huo, bila kuzingatia atakachofaidi au kupoteza Yeye binafsi, na kila mara akiwaza kuhusu mapenzi ya Mungu Baba. Hivyo, baada ya Yeye kubatizwa, Mungu alisema: “Huyu ni Mwana wangu Mpendwa, ambaye Ninapendezwa naye.” Kwa sababu ya huduma Yake mbele ya Mungu, iliyokuwa na upatanifu na mapenzi ya Mungu, Mungu aliuweka mzigo mzito wa kuwakomboa wanadamu wote juu ya mabega yake na akamfanya ajitolee kuutimiza, na Alikuwa na ujuzi na ustahiki wa kuikamilisha kazi hii muhimu. Katika maisha Yake yote, alivumilia mateso yasiyokuwa na kipimo kwa ajili ya Mungu, na alijaribiwa na Shetani mara nyingi, lakini hakufa moyo. Mungu alimpa kazi ya aina hiyo kwa sababu Alimwamini Yeye, na kumpenda Yeye, na hivyo basi Mungu mwenyewe alisema: “Huyu ni Mwana wangu Mpendwa, ambaye Ninapendezwa naye.” Wakati huo, ni Yesu pekee ambaye angeweza kutimiza agizo hili, na hii ilikuwa sehemu moja ya Mungu kutimiza kazi Yake ya kuwakomboa wanadamu wote katika Enzi ya Neema.

Ikiwa, kama Yesu, unaweza kuushughulikia kwa makini mzigo wa Mungu, na kuyakataa mambo ya mwili wako, Mungu atakuaminia kazi Zake muhimu, ili uweze kufikia masharti ya kumhudumia Mungu. Ni katika hali hizo pekee ndipo utakapothubutu kusema kwamba unafanya mapenzi ya Mungu na kukamilisha agizo Lake, hapo ndipo utakapothubutu kusema unamhudumia Mungu kweli. Ukilinganishwa na mfano wa Yesu, unaweza kuthubutu kusema kwamba wewe ni mwandani wa Mungu? Je, unaweza kuthubutu kusema kwamba unafanya mapenzi ya Mungu? Je, unaweza kuthubutu kusema kwamba kweli unamhudumia Mungu? Leo, hufahamu aina hii ya huduma kwa Mungu, unaweza kuthubutu kusema kwamba wewe ni rafiki mwema wa Mungu? Ukisema kwamba unamhudumia Mungu, humkufuru Yeye? Fikiria kuhusu hilo: Je, unamhudumia Mungu, au unajihudumia wewe mwenyewe? Unamhudumia Shetani, ilhali kwa ukaidi unasema kwamba unamhudumia Mungu—katika jambo hili humkufuru Mungu? Watu wengi walio nyuma Yangu wanatamani baraka ya cheo, wana ulafi wa chakula, wanapenda kulala na kuushughulikia mwili kwa makini, kila mara wakiogopa kwamba hakuna njia ya kuondoka ndani ya mwili. Hawaifanyi kazi yao ya kawaida kanisani, lakini wanalitumia kanisa vibaya, au wanawaonya ndugu zao kwa maneno Yangu, wanasimama juu na kuwatawala wengine. Watu hawa huendelea kusema kwamba wanafanya mapenzi ya Mungu, wao husema kila mara kwamba ni marafiki wema wa Mungu—huu si upuuzi? Ikiwa una motisha iliyo sahihi, lakini huwezi kutumikia kulingana na mapenzi ya Mungu, basi wewe unakuwa mpumbavu; lakini ikiwa motisha yako si sahihi, na bado unasema kwamba unamhudumia Mungu, basi wewe ni mtu anayempinga Mungu, na unastahili kuadhibiwa na Mungu! Sina huruma kwa watu wa aina hiyo! Wao ni doezi katika nyumba ya Mungu, na kila mara wao hutamani raha za mwili, na hawazingatii mambo ambayo Mungu anayapenda; kila mara wao hutafuta mambo yaliyo mazuri kwao, wala hawatilii maanani mapenzi ya Mungu, mambo yote wanayoyafanya hayaongozwi na Roho wa Mungu, kila mara wao hufanya hila dhidi ya ndugu zao na kuwadanganya, na kuwa ndumakuwili, kama mbweha ndani ya shamba la mizabibu, akiiba mizabibu kila mara na kulikanyaga na kuliharibu shamba la mizabibu. Je, watu wa aina hiyo wanaweza kuwa marafiki wema wa Mungu? Je, unastahili kupokea baraka za Mungu? Wewe huwajibiki kuhusu maisha yako na kanisa, unastahili kupokea agizo la Mungu? Ni nani anayeweza kuthubutu kumwamini mtu kama wewe? Unapohudumu kwa njia hii, je, Mungu anaweza kuthubutu kukuaminia kazi kubwa zaidi? Je, si wewe unachelewesha mambo?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu

481. Kile ambacho umepitia na kuona kinazidi kile ambacho watakatifu na manabii wengine wa awali walivyoshuhudia, lakini je unaweza kutoa ushuhuda mkubwa zaidi kuliko maneno ya hawa watakatifu na manabii waliotangulia? Kile Ninachokupa wewe sasa kinazidi kile Nilichompa Musa na ni kikubwa zaidi kuliko kile nilichompa Daudi, kwa hivyo vilevile Ninakuomba ushuhuda wako uzidi ule wa Musa na kwamba maneno yako yawe makubwa zaidi kuliko yale ya Daudi. Ninakupa vyote hivi mara mia moja, kwa hivyo vilevile ninakuomba nawe unilipe tena vivyo hivyo. Lazima ujue kwamba Mimi Ndimi ninayempa maisha mwanadamu, na kwamba wewe ndiwe unayepokea maisha kutoka Kwangu na lazima unitolee ushuhuda Mimi. Huu ndio wajibu wako, ambao Ninashusha kwako na ambao unastahili kunifanyia Mimi. Nimekupa utukufu Wangu wote, na kukupatia maisha ambayo watu wateule, Waisraeli, hawakuwahi kupokea. Bila kukosea, unastahili kunitolea ushuhuda, na kuutoa ujana wako kwa ajili Yangu na kuyatoa maisha yako. Yeyote yule ninayempa Mimi utukufu Wangu ataweza kunitolea Mimi ushuhuda na kunipatia maisha yake. Haya yote yametabiriwa mapema. Ni utajiri wako wewe ambao Ninawekea utukufu Wangu kwako wewe na wajibu wako ni kuutolea ushuhuda utukufu Wangu. Kama unaniamini tu Mimi ili kupata utajiri, basi kazi Yangu haitakuwa yenye umuhimu, na hutakuwa unatimiza wajibu wako. Waisraeli waliona tu huruma Yangu, upendo Wangu na ukubwa Wangu nao Wayahudi walitoa tu ushuhuda wa subira Yangu na ukombozi Wangu. Waliona kazi kidogo sana ya Roho Yangu; huenda ikawa kwamba kiwango chao cha uelewa kilikuwa sehemu ndogo sana ya ile ambayo wewe umesikia na kuona. Kile ulichoona kinazidi hata kile ambacho makuhani wakuu waliona miongoni mwao. Siku hii, ukweli ambao umeelewa umezidi wao; kile ambacho umeona siku hii kinazidi kile kilichoonwa kwenye Enzi ya Sheria pamoja na Enzi ya Neema na kile ambacho umepitia kinazidi hata kile ambacho Musa na Eliya walipitia. Kile ambacho Waisraeli walielewa kilikuwa tu sheria ya Yehova na kile ambacho waliona kilikuwa tu ni mgongo wake Yehova; kile ambacho Wayahudi walielewa kilikuwa tu ukombozi wa Yesu, kile walichopokea kilikuwa neema waliyowekewa na Yesu, na kile walichoona kilikuwa ni taswira ya Yesu ndani ya nyumba ya Wayahudi. Kile utakachoona siku hii ni utukufu wa Yehova, ukombozi wa Yesu na matendo Yangu yote ya siku hii. Umesikia pia maneno ya Roho Yangu, hekima Yangu teule, na ukaja kujua kuhusu maajabu Yangu, na umeweza kujifunza kuhusu tabia Yangu. Nimeweza pia kukuambia kuhusu mpango Wangu wa usimamizi. Kile ambacho umeona si tu Mungu mwenye upendo na huruma, lakini yule aliyejawa na haki. Umeiona kazi Yangu ya maajabu na kujua kwamba Nimejawa na hasira na adhama. Aidha, umejua kwamba Niliwahi kuzishusha hasira Zangu katika nyumba ya Israeli, na kwamba leo hii, umeshushiwa wewe. Umeelewa zaidi kuhusu mafumbo Yangu kule mbinguni kuliko vile alivyoelewa Isaya pamoja na Yohana; unajua zaidi kuhusu uzuri Wangu na kustahiwa Kwangu kuliko watakatifu wote wa vizazi vilivyotangulia. Kile ulichopokea si ukweli Wangu tu, njia Yangu, maisha Yangu, lakini maono na ufunuo ambavyo ni vikubwa zaidi kuliko vile vya Yohana. Umeelewa mafumbo mengine mengi zaidi na pia umeona sura Yangu kamili; umekubali mengi kuhusu hukumu Yangu na tabia Yangu ya haki. Kwa hivyo, ingawaje ulizaliwa kwenye siku za mwisho, uelewa wako ni ule wa siku za awali na za kale; umeweza pia kupitia ni nini kilichomo kwenye siku hii, na kile kilichotimizwa na mkono Wangu. Kile Ninachokuomba kinawezekana, kwani kile Nilichokupa ni kingi mno na ni mengi ambayo umeona Kwangu mimi. Kwa hivyo, Ninakuomba kunishuhudia Mimi kama vile watakatifu wa awali walivyofanya na hili ndilo tamanio tu la moyo Wangu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unajua Nini Kuhusu Imani?

482. Kile Ninachotafuta ni uaminifu na utiifu wako sasa, upendo wako na ushuhuda wako sasa. Hata kama hujui kwa wakati huu kile ambacho ushuhuda unamaanisha au kile ambacho upendo unamaanisha, unafaa kuniletea kila kitu, na kunikabidhi mimi hazina za pekee ulizonazo: uaminifu na utiifu wako. Unafaa kujua, agano la kushinda Kwangu Shetani limo ndani ya uaminifu na utiifu wa binadamu, sawa tu na vile ilivyo katika agano la kumshinda kabisa binadamu. Wajibu wa imani Yako Kwangu mimi ni kunishuhudia Mimi, kuwa mwaminifu Kwangu mimi na si mwingine yeyote, na kuwa mtiifu hadi mwisho. Kabla Sijaanza hatua inayofuata ya kazi Yangu, utawezaje kunishuhudia Mimi? Utawezaje kuwa mwaminifu na mtiifu Kwangu mimi? Je, unajitolea uaminifu wako wote katika utendakazi au utakata tamaa tu? Au afadhali unyenyekee katika kila mpangilio Wangu (uwe wa kifo au wa kuangamiza) au kutoroka hapo katikati ili kuepuka kuadibiwa? Ninakuadibu ili uweze kunishuhudia Mimi, na kuwa mwaminifu na mtiifu Kwangu mimi. Pia, kuadibu huku kwa sasa kunalenga katika kufichua hatua inayofuata ya kazi Yangu na kuruhusu kazi hiyo kuendelea bila kutatizwa. Hivyo basi Nakushawishi wewe kuwa mwenye hekima na kutochukulia maisha yako au umuhimu wa kuwepo kwako kuwa ule ambao hauna manufaa kamwe. Unaweza kujua haswa kazi Yangu ijayo itakuwa ipi? Je, unajua namna Nitakavyofanya kazi katika siku zijazo na namna ambavyo kazi Yangu itakavyobadilika? Unafaa kujua umuhimu wa kile ambacho umepitia katika kazi Yangu, na zaidi, umuhimu wa imani yako Kwangu mimi. Nimefanya mengi kweli; iweje Nikate tamaa Nikiwa katikati kama unavyofikiria? Nimefanya kazi kubwa kweli; ninawezaje kuiharibu? Kwa hakika, Nimekuja kuhitimisha enzi hii. Hii ni kweli, lakini zaidi, lazima ujue kwamba Ninafaa kuanzisha enzi mpya, kuanzisha kazi mpya, na, zaidi ya yote, kueneza injili ya ufalme. Kwa hivyo unafaa kujua kwamba kazi ya sasa inalenga katika kuanzisha tu enzi mpya, na kuweka msingi wa kueneza injili katika wakati ujao na kuihitimisha enzi ya sasa katika wakati ujao. Kazi Yangu si rahisi sana kama unavyofikiria, wala si kwamba haina manufaa au maana kama unavyoweza kutaka kuamini. Kwa hivyo, lazima bado Nikuambie: Unastahili kujitolea maisha Yako katika kazi Yangu, na zaidi, unastahili kujitolea wewe mwenyewe katika utukufu Wangu. Aidha, wewe kunishuhudia ndicho kile kitu ambacho Nimetamani kwa muda mrefu, na kingine ambacho Nimetamani hata zaidi ni wewe kueneza injili Yangu. Unastahili kuelewa kile kilichomo ndani ya moyo Wangu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unajua Nini Kuhusu Imani?

483. Je, unaweza kuwasilisha tabia inayoonyeshwa na Mungu katika kila enzi kwa njia thabiti, kwa lugha inayowasilisha umuhimu wa enzi hiyo kwa njia inayofaa? Je, wewe unayepitia kazi ya Mungu ya siku za mwisho unaweza kueleza tabia ya Mungu yenye haki kwa utondoti? Je, unaweza kushuhudia kuhusu tabia ya Mungu kwa uwazi na usahihi? Utawezaje kupitisha kile ambacho umeona na kupitia kupitia kwa maskini hawa wa kuhurumiwa, na waumini wa kidini wa kumcha Mungu waliojitolea na waliojawa na njaa na kiu ya haki na wanaongoja uwe mchungaji wao? Ni watu wa aina gani ndio wanangoja uwe mchungaji wao? Unaweza kuwaza kweli? Je, unajua mzigo ulio begani mwako, kazi yako na majukumu yako? Hisia yako ya kihistoria ya mwito iko wapi? Utahudumu vipi kama kiongozi mzuri wa wakati unaofuata? Je, unao hisia nzuri ya uongozi? Utaeleza mkuu wa kila kitu kama nini? Je, ni mkuu wa kila kitu kilicho hai na viumbe vyote duniani? Una mipango ipi ya kuendelea kwa hatua inayofuata ya kazi? Ni watu wangapi ndio wanangoja uwe mchungaji wao? Je, jukumu lako ni nzito? Wao ni masikini, wa kuhurumiwa, vipofu na waliopotea na wanalia gizani, “Njia iko wapi?” Jinsi gani wanatamani mwangaza, kama nyota iangukayo kutoka angani, ianguke ghafla na kutawanya nguvu za giza zilizowakandamiza wanadamu kwa miaka mingi. Ni nani anayeweza kujua jinsi wanavyotumaini kwa hamu, na wanavyotamani hili usiku na mchana? Wanadamu hawa wanaoteseka mno wamebaki wafungwa katika jela za giza, bila tumaini la kuwachiliwa huru, hata ile siku ambayo mwanga utaonekana; ni lini hawatalia kwa uchungu tena? Roho hizi dhaifu ambao kamwe hazijapewa pumziko kwa hakika zinateseka na bahati hii mbaya. Kwa muda mrefu wamefungiwa nje na kamba zisizo na huruma na historia iliyokwama katika wakati. Ni nani amewahi kusikia sauti ya vilio vyao? Ni nani amewahi kuona nyuso zao zenye taabu? Umewahi kufikiria jinsi moyo wa Mungu ulivyosononeka na ulivyo na wasiwasi? Anawezaje kustahimili kuona mwanadamu asiye na hatia, Aliyemuumba kwa mikono Yake Mwenyewe akiteswa na makali? Mwishowe, wanadamu ndio wasio na bahati na waliopewa sumu. Hata ingawa wamenusurika mpaka siku hii, ni nani angefikiri kuwa wamepewa sumu na yule mwovu kwa muda mrefu? Je, umesahau kuwa wewe ni mmoja wa waathiriwa? Kwa ajili ya upendo wako kwa Mungu, una nia ya kufanya kila uwezalo kuwaokoa walionusurika? Je, huna nia, ya kutumia nguvu zako zote kulipiza Mungu anayempenda binadamu kama nyama na damu Yake Mwenyewe? Unaitafsiri vipi hali ya kutumiwa na Mungu kuishi maisha yako yasiyo ya kawaida? Je, unao kweli uamuzi na matumaini ya kuishi kwa kudhihirisha maisha ya maana ya mtu mcha Mungu anayemtumikia Mungu?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kushughulikiaje Wito Wako wa Baadaye?

484. Kumshuhudia Mungu hasa ni suala la kuzungumza kuhusu maarifa yako ya kazi ya Mungu, kuhusu jinsi Mungu huwashinda watu, kuhusu jinsi Yeye huwaokoa watu, kuhusu jinsi Yeye huwabadili watu; ni suala la kuzungumza kuhusu jinsi Yeye huwaongoza watu kuingia katika uhalisi wa ukweli, Akiwawezesha washindwe, wakamilishwe na kuokolewa na Yeye. Kushuhudia kunamaanisha kuzungumza kuhusu kazi Yake na yote ambayo umepitia. Ni kazi Yake pekee inayoweza kumwakilisha, na ni kazi Yake pekee inayoweza kumfichua kwa umma, kwa ukamilifu Wake; kazi Yake inamshuhudia. Kazi na matamshi Yake vinamwakilisha Roho moja kwa moja; kazi Anayofanya inatekelezwa na Roho, na maneno Anayonena yanazungumzwa na Roho. Vitu hivi vinaonyeshwa tu kupitia mwili wa Mungu, lakini kwa kweli, ni maonyesho ya Roho. Kazi yote Anayofanya na maneno yote Anayozungumza yanawakilisha kiini Chake. Ikiwa Mungu hangezungumza ama kufanya kazi baada ya kujivika mwili na kuja miongoni mwa wanadamu, na kisha Awatake mjue uhalisi Wake, ukawaida Wake na kudura Yake, je, ungeweza? Je, ungeweza kujua kiini cha Roho? Je, ungeweza kujua sifa za kiasili za mwili Wake ni zipi? Ni kwa sababu tu mmepitia kila hatua ya kazi Yake ndiyo Anawataka mumshuhudie. Ikiwa hamngekuwa na uzoefu kama huu, basi Hangesisitiza kwamba mumshuhudie. Kwa hivyo, unapomshuhudia Mungu, hushuhudii tu kuhusu sura Yake ya nje ya ubinadamu wa kawaida, lakini pia kazi Anayofanya na njia Anayoongoza; unapaswa kushuhudia kuhusu jinsi ulivyoshindwa na Yeye na umekamilishwa katika vipengele vipi. Unapaswa kuwa na ushuhuda wa aina hii. … Umepitia kuadibiwa, hukumu, usafishaji, majaribu, vipingamizi na majaribio hatua kwa hatua, na umeshindwa; umeweka kando matarajio ya mwili, nia zako binafsi, na maslahi ya ndani ya mwili. Yaani, maneno ya Mungu yameushinda moyo wako kabisa. Ingawa hujakua katika maisha yako kwa kiwango Anachotaka, unayajua mambo haya yote na unashawishika kabisa na kile Anachofanya. Kwa hivyo, hili linaweza kuitwa ushuhuda, ushuhuda ambao ni halisi na wa kweli. Kazi ambayo Mungu amekuja kufanya, kazi ya hukumu na kuadibu, inakusudiwa kumshinda mwanadamu, lakini pia Anahitimisha kazi Yake, akimaliza enzi na kutekeleza kazi ya hitimisho. Anakamilisha enzi nzima, Akiwaokoa wanadamu wote, Akiwakomboa wanadamu kutoka katika dhambi kabisa; Anawapata wanadamu Aliowaomba kikamilifu. Unapaswa kushuhudia haya yote. Umepitia kazi nyingi sana ya Mungu, umeiona kwa macho yako mwenyewe na kuipitia wewe binafsi; wakati umefika mwisho kabisa, ni lazima uweze kutenda kazi inayokupasa uifanye. Litakuwa jambo la kusikitisha kweli usipoweza! Katika siku zijazo, wakati injili inaenezwa, unapaswa kuweza kuzungumzia maarifa yako mwenyewe, ushuhudie yote uliyoyapata moyoni mwako na utumie jitihada yote. Kiumbe aliyeumbwa anapaswa kufanikisha hili. Umuhimu wa kweli wa hatua hii ya kazi ya Mungu ni upi? Athari yake ni ipi? Na ni kiwango chake kipi kinatekelezwa ndani ya mwanadamu? Watu wanapaswa kufanya nini? Unapoweza kuzungumza kwa uwazi kuhusu kazi yote ambayo Mungu mwenye mwili amefanya tangu aje duniani, basi ushuhuda wako utakuwa kamili. Unapoweza kuzungumza kwa uwazi kuhusu vitu hivi vitano: umuhimu wa kazi Yake; maudhui yake; kiini chake; tabia inayowakilisha; na kanuni zake, basi hili litathibitisha kwamba unaweza kumshuhudia Mungu, kwamba kweli una maarifa. Mahitaji yangu kwenu si ya juu sana, na yanaweza kutimizwa na wale wote wanaofuatilia kwa kweli. Ikiwa umeazimia kuwa mmoja wa mashahidi wa Mungu, ni lazima uelewe kile Mungu anachochukia sana na kile Mungu Anachopenda. Umepitia kazi Yake nyingi; kupitia kazi hii, ni lazima upate kujua tabia Yake, uelewe mapenzi Yake na mahitaji Yake kwa wanadamu, na utumie maarifa haya kumshuhudia na kutenda wajibu wako.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Utendaji (7)

485. Mnapokuwa na ushuhuda wa, mnapaswa kuzungumza hasa kuhusu jinsi Mungu anavyowahukumu na kuwaadibu watu, ni majaribio yapi anayoyatumia kuwasafisha wanadamu na kubadilisha tabia zao. Mnapaswa pia kuzungumza kuhusu kiwango cha upotovu ambacho kimefichuliwa katika uzoefu wenu, kiasi ambacho mmestahimili na jinsi ambavyo hatimaye mlishindwa na Mungu; kiasi cha maarifa ya kweli ya kazi ya Mungu mlicho nacho, na jinsi mnavyopaswa kumshuhudia Mungu na kumlipiza kwa ajili ya upendo Wake. Mnapaswa kuweka umuhimu katika lugha ya aina hii, huku mkiisema kwa njia rahisi. Msizungumze juu ya nadharia tupu. Zungumzeni mambo halisi zaidi, zungumzeni kwa dhati. Hivi ndivyo jinsi mnavyopaswa kupitia. Msijiandae kwa nadharia zinazoonekana kuu, zilizo tupu katika juhudi la kujionyesha; kufanya hivyo kunawafanya muonekane wenye majivuno sana na msio na maana. Mnapaswa kuzungumza zaidi kuhusu mambo ya kweli na halisi kutoka kwa uzoefu wenu ambayo ni ya kweli na ya dhati; hili ndilo la manufaa zaidi kwa wengine, na ndilo linalowafaa zaidi kuona. Ninyi mlikuwa watu waliompinga Mungu zaidi na ambao waliegemea kumtii Yeye kwa kiasi kidogo zaidi, lakini sasa mmeshindwa—msisahau hilo kamwe. Mnapaswa kutenga tafakari na fikira nyingi kwa masuala haya kwa bidii. Baada ya kugundua hili, mtajua jinsi ya kushuhudia; vinginevyo mnaweza kufanya vitendo vya aibu na vya kipumbavu.

Kimetoholewa kutoka katika “Ni Kwa Kufuatilia Ukweli Tu Ndiyo Unaweza Kupata Mabadiliko Katika Tabia Yako” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

486. Ili kushuhudia kazi ya Mungu, lazima utegemee uzoefu na maarifa yako, na gharama ambayo umelipa. Unaweza kuyaridhisha mapenzi Yake kwa njia hii pekee. Je, wewe ni mtu ambaye hushuhudia kazi ya Mungu? Je, una matamanio haya? Kama unaweza kulishuhudia jina Lake, na hata zaidi, kazi Yake, na kama unaweza kuishi kwa kudhihirisha sura ambayo Yeye anataka kutoka kwa watu Wake, basi wewe ni shahidi wa Mungu. Je, unashuhudia kwa ajili ya Mungu vipi kwa hakika? Unafanya hivyo kwa kutafuta na kuwa na hamu sana ya kuishi kwa kulidhihirisha neno la Mungu na, kwa kuwa na shahidi kwa maneno yako, kuwaruhusu watu wajue kazi Yake na kuona matendo Yake. Kama kweli unatafuta yote haya, basi Mungu atakukamilisha. Ikiwa yote unayotafuta ni kukamilishwa na Mungu na kubarikiwa mwishoni kabisa, basi mtazamo wa imani yako katika Mungu si safi. Unapaswa kuwa ukifuatilia jinsi ya kuona matendo ya Mungu katika maisha ya kweli, jinsi ya kumridhisha Yeye Anapokufichulia mapenzi Yake, na kutafuta jinsi unavyopaswa kushuhudia maajabu na hekima Yake, na jinsi ya kushuhudia jinsi Anavyokufundisha nidhamu na kukushughulikia. Haya yote ni mambo unayopaswa kuwa ukiyatafakari sasa. Kama upendo wako kwa Mungu ni ili tu uweze kushiriki katika utukufu wa Mungu baada ya Yeye kukukamilisha, basi bado hautoshi na hauwezi kukidhi mahitaji ya Mungu. Unahitaji kuwa na uwezo wa kushuhudia kazi ya Mungu, kutosheleza mahitaji Yake, na kuwa na uzoefu wa kazi ambayo Amefanya kwa watu kwa njia ya utendaji. Iwe ni uchungu, majonzi, au huzuni, lazima upitie vitu hivi vyote katika kutenda kwako. Vitu hivi vinanuiwa kukukamilisha kama Yule anayemshuhudia Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaopaswa Kukamilishwa Lazima Wapitie Usafishaji

487. Ijapokuwa imani yenu ni ya kweli kabisa, hakuna kati yenu anayeweza kueleza kunihusu kabisa, na hakuna kati yenu anayeweza kushuhudia uhalisi mnaouona. Tafakari kuhusu jambo hili. Sasa hivi wengi wenu hamyatimizi wajibu wenu, mkifuata vitu vya mwili, mkishibisha mwili na kuburudika kwa mwili. Mnamiliki ukweli mdogo. Mnawezaje basi kushuhudia yote ambayo mmeyaona? Mna uhakika kuwa mtakuwa mashahidi Wangu? Iwapo siku moja utashindwa kushuhudia yote ambayo umeyaona leo, basi utakuwa umepoteza jukumu la kiumbe aliyeumbwa. Hakutakuwa na maana kabisa ya kuwepo kwako. Utakuwa hustahili kuwa binadamu. Mtu anaweza hata kusema kuwa wewe si binadamu! Nimefanya kazi isiyo na kifani kwako. Lakini kwa sababu kwa sasa hujifunzi chochote, hujui chochote, na kufanya kazi bure, Nikitaka kuipanua kazi Yangu utatazama bila kuelewa, bila kusema chochote na kuwa asiye na umuhimu wowote. Hiyo haitakufanya mtenda dhambi mkubwa zaidi? Wakati huo utakapofika, je, hutakuwa na majuto makuu? Hutazama katika huzuni kubwa? Sifanyi kazi hii yote sasa kwa sababu ya kukosa la kufanya na uchoshi, bali kuweka msingi kwa kazi Yangu ya baadaye. Sio kwamba Niko katika njia isiyopitika na Nahitajika kubuni kitu kipya. Unafaa kuelewa kazi ambayo Nafanya; si kitu kinachofanywa na mtoto anayecheza mtaani, bali ni kwa uwakilishi wa Baba Yangu. Unafaa kujua kuwa si Mimi tu Ninayefanya haya yote pekee Yangu bali Namwakilisha Baba Yangu. Wakati uo huo, jukumu lako ni kufuata, kuheshimu, kubadilika, na kushuhudia kwa makini. Unachofaa kuelewa ni kwa nini unafaa kuniamini. Hili ndilo swali muhimu kwa kila mmoja wenu kuelewa. Baba Yangu, kwa ajili ya utukufu Wake, ndiye Aliyewachagua ninyi kwa ajili Yangu kutoka wakati Alipoumba dunia. Haikuwa kwa ajili ya kitu kingine ila kwa ajili ya kazi Yangu na kwa ajili ya utukufu Wake, ndio maana Aliweka hatima yenu awali. Ni kwa sababu ya Baba Yangu ndio unaniamini; ni kwa sababu ya Baba Yangu kukuamua kabla ndio maana unanifuata Mimi. Hakuna kati ya haya ambayo ulichagua kwa hiari yako mwenyewe. La muhimu zaidi ni kwamba muelewe kuwa ninyi ni wale ambao Baba Yangu alinitawazia kwa ajili ya kushuhudia kwa niaba Yangu. Kwa sababu Aliwatawaza Kwangu, mnafaa kuzifuata njia ambazo Natawaza kwenu na njia na maneno ambayo Ninawafunza, kwani ni jukumu lenu kuzifuata njia Zangu. Hili ndilo kusudi la asili la imani yenu Kwangu. Kwa hivyo Nawaambieni, ninyi ni watu tu ambao Baba Yangu Alitawaza Kwangu ili mfuate njia Zangu. Hata hivyo, mnaamini tu Kwangu; ninyi si wa Kwangu kwa sababu ninyi si wa familia ya Wayahudi bali ni wa joka la zama. Kile Ninachowasihi ni muwe washahidi Wangu, lakini leo lazima mtembee kwa njia Zangu. Haya yote ni kwa ajili ya ushuhuda wa baadaye. Mkihudumu tu kama watu ambao wanasikiliza njia Zangu pekee, basi hamtakuwa na thamani yoyote na umuhimu wa Baba Yangu kuwatawaza Kwangu utapotea. Ninachosisitiza kuwaambia ni hiki: Mnapaswa kutembea katika njia Zangu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufahamu Wako Kumhusu Mungu Ni Upi?

Iliyotangulia: K. Kuhusu Jinsi ya Kupata Kumjua Mungu

Inayofuata: M. Kuhusu Jinsi ya Kutupilia Mbali Ushawishi wa Shetani na Kupata Wokovu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp