803 Ni kwa Kumjua Mungu tu Ndiyo Unaweza Kumwabudu kwa Kweli
1 Bila ubaguzi wale wote ambao kwa kweli wanamjua Mungu humwabudu na kumcha kila wanapomwona; wote hulazimika kusujudu na kumwabudu Yeye. Kwa sasa, wakati Mungu mwenye mwili yuko kazini, ndivyo kadri ufahamu watu walionao wa tabia Yake na kile Alicho nacho na kile Alicho, ndivyo zaidi watakavyovithamini vitu hivi na ndivyo zaidi watamchaa Yeye. Kwa kawaida, kadiri watu walivyo na ufahamu mdogo, ndivyo wanavyokosa kuwa makini zaidi, na hivyo wanamtendea Mungu kama mwanadamu. Ikiwa watu kwa kweli wanngemjua na kumwona Mungu wangetetemeka kwa hofu. “Lakini yule ajaye baada ya mimi ni mwenye nguvu zaidi kuliko mimi, ambaye sistahili kuvichukua viatu vyake.”—kwa nini Yohana alisema haya? Ijapokuwa kwa kina hakuwa na ufahamu mkubwa, alijua kwamba Mungu ni wa kustaajabisha.
2 Watu hawajui kiini cha Kristo wala kuelewa tabia ya Mungu, sembuse kuwezakumwabudu Mungu. Ikiwa wanaona tu kuonekana kwa nje kwa kawaida kwa Kristo ilihali hawajui asili Yake, basi ni rahisi kwa wao kumchukulia Kristo kama tu mtu wa kawaida. Huenda wakachukua mtazamo usio wa heshima Kwake, na wanaweza kumdanganya, kumkataa, kutomtii, na kutoa hukumu Kwake. Wanaweza kujiona wenye haki na kutochukulia neno Lake kwa makini; wanaweza hata kuibua fikira, shutuma na kumkufuru Mungu. Ili kutatua masuala haya mtu lazima ajue kiini na uungu wa Kristo. Hiki ndicho kipengele kikuu cha kumjua Mungu; ni kile amabacho yeyote anayeamini katika Mungu wa utendaji wanapaswa kuingia na kufanikisha.
Umetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kumjua Mungu Mwenye Mwili” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo