96 Watu Wanamjua Mungu Bora Kupitia Kazi ya Maneno

1 Katika siku za mwisho, Mungu hasa hutumia neno kumfanya mwanadamu kuwa mkamilifu. Hatumii ishara na maajabu kumdhulumu mwanadamu, ama kumshawishi mwanadamu; hii haiweki wazi nguvu za Mungu. Iwapo Mungu angeonyesha tu ishara na maajabu, basi hakungekuwa na uwezo wa kuweka wazi ukweli wa Mungu, na hivyo haingewezekana kumfanya mwanadamu mkamilifu. Mungu hamfanyi mwanadamu mkamilifu kwa kutumia ishara na maajabu, ila Anatumia neno kunyunyizia na kumchunga mwanadamu, na baada ya haya kunapatikana utiifu kamili wa mwanadamu na ufahamu wa mwanadamu kuhusu Mungu. Hili ndilo lengo la kazi Anayofanya na maneno Anenayo. Mungu hatumii mbinu ya kuonyesha ishara na maajabu ili kumfanya mwanadamu kamili—Anatumia maneno, na Anatumia mbinu nyingi za kazi kumfanya mwanadamu kamili. Iwe ni usafishaji, kushughulikia, upogoaji, ama kupewa maneno, Mungu hunena kutoka taswira nyingi tofauti kumfanya mwanadamu kamili, na kumpa mwanadamu maarifa kuu ya kazi, hekima na ajabu ya Mungu.

2 Katika Enzi ya Sheria ya Agano la Kale, Mungu pia Alionyesha ishara na maajabu kadhaa—lakini kazi Anayofanya Mungu leo ni kazi halisi, na kwa uhakika hawezi kuonyesha ishara na maajabu sasa. Kama Angeonyesha ishara na maajabu, kazi Yake halisi ingevurugwa, na hangeweza kufanya kazi nyingine zaidi. Iwapo Mungu angesema neno litumiwe kumfanya mwanadamu kuwa kamili, lakini pia Aonyeshe ishara na maajabu, basi mwanadamu kumwamini ama kutomwamini kweli kungeweza kuwekwa wazi? Hivyo, Mungu hafanyi vitu vya aina hiyo. Kuna udini mwingi sana katika mwanadamu; Mungu amekuja katika nyakati za mwisho ili kutoa dhana zote za kidini na vitu visivyo vya kidunia ndani ya mwanadamu, na kumfanya mwanadamu ajue ukweli wa Mungu. Amekuja kutoa picha ya Mungu ambayo ni ya dhahania na bunifu—picha ya Mungu ambaye, kwa maneno mengine, hayupo hata kidogo. Na hivyo, sasa kitu cha pekee kilicho cha thamani ni wewe kuwa na ufahamu kuhusu hali halisi! Katika imani yake kwa Mungu, kile anachotafuta mwanadamu ni ukweli, anachotafuta ni uzima, na sio ishara na maajabu. Hivi ndivyo linavyopaswa kuwa lengo la wote wanaoamini katika Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 95 Maana Halisi ya Neno Kuonekena katika Mwili

Inayofuata: 97 Mungu Hutumia Maneno Kuushinda Ulimwengu Mzima Katika Siku za Mwisho

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp