789 Unapaswa Kumjua Mungu Kupitia Kazi Yake

1 Aligeuka na kuwa mtu—mtu wa kawaida aliyetekeleza kazi na agizo la Mungu. Hii ilimaanisha kwamba lazima angefanya kazi ambayo mtu wa kawaida asingeweza kufanya, huku akivumilia mateso ambayo binadamu wa kawaida hawezi kuvumilia. Mateso haya yanawakilisha nini? Yanawakilisha Mapenzi ya Mungu kwa wanadamu. Yanasimamia udhalilishaji Alioteseka na gharama Aliyolipia kwa sababu ya wokovu wa binadamu, kukomboa dhambi zake, na kukamilisha awamu hii ya kazi Yake. Yanamaanisha binadamu angekombolewa kutoka katika msalaba na Mungu. Hii ndiyo gharama iliyolipwa kwa damu, kwa maisha, gharama ambayo viumbe walioumbwa hawawezi kumudu. Ni kwa sababu Anacho kiini cha Mungu na Amejihami na kile Mungu anacho na alicho, ndiyo maana Anaweza kuvumilia aina hii ya mateso na aina hii ya kazi. Hili ni jambo ambalo hakuna kiumbe aliyeumbwa anaweza kufanya badala Yake. Hii ni kazi ya Mungu katika Enzi ya Neema na ufunuo wa tabia Yake.

2 Katika Enzi ya Ufalme, Mungu akawa mwili tena, kwa njia sawa na ile Aliyotumia mara ya kwanza. Katika kipindi hiki cha kazi, Mungu angali anaonyesha bila kusita neno Lake, anafanya kazi anayofaa kufanya na kuonyesha kile Anacho na alicho. Wakati huohuo, Anaendelea kuvumilia na kustahili na kutotii na kutojua kwa binadamu. Je, Mungu hafichui kila wakati tabia Yake na kuonyesha mapenzi yake katika kipindi hiki cha kazi pia? Hivyo basi, kuanzia uumbaji wa binadamu hadi sasa, tabia ya Mungu, nafsi Yake na miliki Zake, na mapenzi Yake, siku zote yamekuwa wazi kwa kila mmoja. Mungu hajawahi kuficha kimakusudi kiini Chake, tabia Yake au mapenzi Yake. Ni vile tu mwanadamu hajali kuhusu kile ambacho Mungu anafanya, mapenzi Yake ni yapi—ndio maana uelewa wa binadamu kumhusu Mungu ni finyu mno.

Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 788 Wanadamu Hawana Ufahamu wa Mapenzi ya Mungu

Inayofuata: 790 Mapenzi Ya Mungu Yamekuwa Wazi kwa Kila Mtu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp