Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

1 Wimbo wa Ufalme (I) Ufalme Unashuka Duniani

Umati unamshangilia Mungu,

umati unamsifu Mungu, unamsifu Mungu;

watu wote wanamtaja Mungu mmoja wa kweli,

Mungu mmoja wa kweli, Mungu mmoja wa kweli.

Ufalme unashuka duniani mwa wanadamu.

1

Umati unamshangilia Mungu, umati unamsifu Mungu;

watu wote wanamtaja Mungu mmoja wa kweli,

watu wote wanamtaja Mungu mmoja wa kweli,

watu wote wanayainua macho yao kuviangalia vitendo vya Mungu.

Ufalme unashuka duniani mwa wanadamu, nafsi ya Mungu ni ya fahari na yenye neema.

Nani asingesherehekea kwa ajili ya hili? Ni nani asingecheza kwa furaha?

Ee, Sayuni! Ee, Sayuni! Ee, Sayuni!

Inua bendera yako ya ushindi umsherehekee Mungu!

Imba wimbo wako wa ushindi ili ulieneze jina takatifu la Mungu!

2

Viumbe wote duniani kote! Harakisheni kujitakasa ili muweze kufanywa kuwa sadaka kwa Mungu!

Ee, nyota juu mbinguni!

Rudini kwenye maeneo yenu kwa haraka ili muonyeshe nguvu kuu ya Mungu angani!

Mungu anazisikiliza sauti za watu duniani,

wanaomimina upendo na uchaji wao mwingi kwa ajili Yake katika wimbo!

Ha, ha, ha, ha.

Ha, ha, ha, ha.

Ha, ha.

Katika siku hii, huku viumbe wote wakirudishiwa uhai, Mungu anashuka katika dunia ya wanadamu.

Katika wakati huu, mambo yalivyo,

maua yote yanachanua kwa wingi, ndege wote wanaimba kwa sauti moja, vitu vyote vinajawa na furaha!

Kwa sauti ya saluti ya ufalme, ufalme wa Shetani unaanguka.

Katika siku hii, huku viumbe wote wakirudishiwa uhai, Mungu anashuka katika dunia ya wanadamu.

Katika wakati huu, mambo yalivyo, maua yote yanachanua kwa wingi, ndege wote wanaimba kwa sauti moja, vitu vyote vinajawa na furaha!

Kwa sauti ya saluti ya ufalme, ufalme wa Shetani unaanguka,

ukiangamizwa katika mngurumo wa wimbo wa ufalme, usiinuke tena!

3

Nani duniani anathubutu kuinuka na kupinga?

Mungu anaposhuka duniani, Mungu anaposhuka duniani, 

Analeta kuchoma, Analeta ghadhabu,

Analeta maafa ya aina yote.

Falme za dunia sasa ni ufalme wa Mungu!

Juu angani, mawingu yanagaagaa na kujongea kama mawimbi;

chini ya anga, maziwa na mito

yanatapakaa na kutoa muziki wa kusonga kwa furaha.

Wanyama wanaopumzika wanaibuka kutoka kwenye matundu yao,

na watu wote ambao wamelala wanaamshwa na Mungu.

Siku ambayo watu wote wameingojea hatimaye imefika!

Siku ambayo watu wote wameingojea hatimaye imefika!

Wanamwimbia Mungu nyimbo nzuri sana!

Mwimbia Mungu!

Mwimbia Mungu!

Mwimbia Mungu!

Mwimbia Mungu!

Wanamwimbia Mungu nyimbo nzuri sana!

Umetoholewa kutoka katika “Wimbo wa Ufalme” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia:Dibaji

Inayofuata:Wimbo Wa Ufalme (II) Mungu Amekuja, Mungu Ni Mfalme

Maudhui Yanayohusiana