19 Mfalme wa Ufalme ni Mshindi

1 Wakati umeme unatoka Mashariki—ambao pia ni wakati hasa Naanza kutamka maneno Yangu—umeme unapotoka, mbingu yote inaangazwa, na mabadiliko yanatokea kwenye nyota zote. Wanadamu wote wanakuwa kana kwamba wamepangwa vizuri. Chini ya mng’aro wa mwale huu wa mwangaza kutoka Mashariki, wanadamu wote wanafichuliwa katika maumbo yao ya asili, macho yao yaking’aa, wakikosa uhakika wa kile wanachopsawa kufanya, na sembuse jinsi ya kuficha sifa zao mbaya. Wanadamu wote wako na hofu na wasiwasi, wote wanangoja, wote wanatazama; na ujio wa mwanga Wangu, wote wanasherehekea katika siku waliozaliwa, na vilevile wote wanailaani siku waliyozaliwa. Hisia zinazopingana haziwezi kuelezeka; machozi ya kujiadhibu huunda mito, na yanabebwa mbali juu ya mvo unaofagia, kwenda mara moja yasionekane tena.

2 Kwa mara nyingine, siku Yangu inakaribia jamii ya binadamu, mara nyingine ikiamsha jamii ya binadamu, ikiwapa binadamu hatua ya kutengeneza mwanzo mpya. Moyo Wangu unapiga na, kufuatia mdundo wa mpigo wa moyo Wangu, milima inaruka kwa furaha, maji yanacheza kwa furaha, na mawimbi, kwa wakati ufaao, yanagonga juu ya mawe ya mwamba. Ni vigumu kuonyesha kile kilicho ndani ya moyo Wangu. Nataka vitu vyote visivyo safi vichomeke na kuwa majivu Nikitazama, Nataka wana wote wa kutotii wapotee kutoka mbele ya macho Yangu, wasikawie tena katika uwepo. Sijatengeneza mwanzo mpya katika makao ya joka kubwa jekundu pekee, Nimeanza pia kazi mpya katika ulimwengu. Hivi karibuni falme za dunia zitakuwa ufalme Wangu; hivi karibuni falme za dunia zitakoma kuwepo milele kwa sababu ya ufalme Wangu, kwa sababu Nimetimiza ushindi tayari, kwa sababu Nimerejea kwa ushindi.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 12” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 18 Saluti ya Ufalme Inaposikika

Inayofuata: 20 Uso wa Mfalme wa Ufalme ni Mtukufu Kupindukia

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp