85 Hukumu kwa Neno Inawakilisha Mamlaka ya Mungu Bora Zaidi

1 Katika kazi ya siku za mwisho, neno ni kubwa zaidi ya udhihirisho wa ishara na maajabu, na mamlaka ya neno yanashinda yale ya ishara na maajabu. Neno linaweka wazi tabia zote potovu katika moyo wa mwanadamu. Huwezi kutambua binafsi wewe mwenyewe. Yatakapofunuliwa kwako kupitia kwa neno, utakuja kujua mwenyewe; hutaweza kuyakataa, na utashawishika kikamilifu. Je haya si mamlaka ya neno? Haya ndiyo matokeo yanayopatikana kwa kazi ya wakati huu ya neno. Kupitia kazi hii ya kuadibu na hukumu, mwanadamu atakuja kujua hali yake kamili ya uchafu na upotovu ndani Yake, na ataweza kubadilika kabisa na kuwa msafi. Ni hivi tu ndivyo mwanadamu ataweza kustahili kurudi katika kiti cha enzi cha Mungu.

2 Mwanadamu anatwaliwa na Mungu kupitia hukumu na kuadibu na neno; kwa kutumia neno kusafisha, hukumu na kufichua, uchafu wote, fikira, nia, na matumaini ya mtu mwenyewe katika moyo wa mwanadamu zinafuliwa. Kwa hiyo, kile ambacho mmepitia wakati wa sasa ni matokeo ambayo hutimizwa kupitia kwa neno, hata makuu zaidi ya yale ambayo hutimizwa kupitia kwa Yesu kufanya ishara na maajabu. Utukufu wa Mungu na mamlaka ya Mungu Mwenyewe ambayo ninyi huona hayaonekani tu kupitia kwa usulubishaji, uponyaji wa magonjwa na ufukuzaji wa pepo, lakini zaidi kupitia kwa hukumu ya neno Lake. Hili hukuonyesha wewe kwamba sio tu ufanyaji wa ishara, uponyaji wa magonjwa na ufukuzaji wa pepo ndiyo mamlaka na nguvu za Mungu, bali kwamba hukumu ya neno la Mungu inaweza kuwakilisha vyema zaidi mamlaka ya Mungu na kufichua uweza Wake.

Umetoholewa kutoka katika “Fumbo la Kupata Mwili (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 84 Mungu Amhukumu na Kumkamilisha Mwanadamu kwa Maneno Yake Katika Siku za Mwisho

Inayofuata: 86 Mungu Anafanikisha Vyote Katika Siku za Mwisho Hasa Kwa Maneno

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp