307 Hii Ndiyo Imani Yako?

1 Ni kwa nini humheshimu Mungu ilhali unaamini kuwepo Kwake? Ni kwa nini, basi, haumchi Mungu moyoni mwako iwapo unaamini kuwa Mungu Yupo? Unakubali kuwa Kristo ni kupata mwili kwa Mungu, basi ni kwa nini uwe na dharau Kwake? Kwa nini unatenda bila heshima Kwake? Ni kwa nini unamhukumu wazi wazi? Ni kwa nini siku zote unachunguza Yeye anakoenda? Mbona usijisalimishe katika mipango Yake? Ni kwa nini hutendi kulingana na neno Lake? Ni kwa nini unamhadaa na kumpokonya matoleo Yake? Ni kwa nini unazungumza katika nafasi ya Kristo? Ni kwa nini unatoa hukumu ya kubaini iwapo kazi Yake na neno Lake ni ya kweli? Mbona unathubutu kumkufuru Yeye kisiri? Ni mambo haya na mengine ndiyo yanayounda imani yenu?

2 Kila sehemu ya usemi na tabia zenu hufichua dalili za kutoamini katika Kristo ulizobeba ndani yako. Nia na malengo yenu kwa yale mnayoyafanya yamejaa kutoamini; hata hiyo hisi itokayo kwa macho yenu imetiwa doa na dalili hizi. Kwa maneno mengine, kila mmoja wenu, katika kila dakika ya kila siku, amebeba vipengele vyenu vya kutoamini. Hii ina maana kuwa kila wakati mko katika hatari ya kumsaliti Kristo, kwa maana damu iliyo ndani ya mishipa yenu imechanganyika na kutomwamini Mungu Aliyepata mwili. Kwa hivyo, Ninasema kwamba nyayo mnazoziwacha katika njia ya imani katika Mungu si nyingi. Safari yenu katika njia ya kumwamini Mungu haina msingi mzuri, na badala yake mnafanya kazi bila ya kujali matokeo yake.

Umetoholewa kutoka katika “Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu?” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 306 Binadamu Wapotovu Hawastahili Kumwona Kristo

Inayofuata: 308 Iko Wapi Imani Yako ya Kweli?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp