316 Mna Udhalimu Pekee Mioyoni Mwenu

1 Nyote mnaamini kwamba mko tayari kulipa gharama ya ukweli, lakini ni wangapi walioteseka kweli kwa ajili ya ukweli? Yote yaliyo ndani ya mioyo yenu ni uovu, na hivyo mnaamini kwamba yeyote, bila kujali ni nani, ni mjanja na asiye mwaminifu. Hata mnaamini kwamba Mungu mwenye mwili angekuwa bila moyo wa ukarimu na upendo wema kama tu binadamu wa kawaida. Zaidi ya hayo, mnaamini kwamba tabia ya adabu na asili yenye huruma na ukarimu ziko kwa Mungu wa mbinguni pekee. Na mnaamini kwamba mtakatifu kama huyu hayuko, na kwamba giza na uovu tu ndio unaotawala duniani, ilhali Mungu ni kitu ambacho mwanadamu huwekea matumaini yake ya mazuri na mema, na mtu maarufu aliyebuniwa na mwanadamu.

2 Mnamwabudu sana Mungu aliye mbinguni. Mnapenda sana sura zilizo kuu na kuheshimu wanaojulikana kwa ajili ya umbuji wao. Mnaamrishwa kwa furaha na Mungu Anayejaza mikono yenu na utajiri, na mnatamani sana Mungu Anayeweza kutimiza tamaa zenu zote. Yule tu msiyemwabudu ni Mungu huyu asiye mkuu; Chombo chenu tu cha chuki ni ushirikiano na huyu Mungu ambaye hakuna mwanadamu anayeweza kumchukulia kuwa mkuu. Kitu pekee ambacho hamko tayari kufanya ni kumtumikia huyu Mungu ambaye hajawahi kuwapa senti hata moja, na Yule tu msiyemtamani ni huyu Mungu asiyependeza. Mungu kama huyu hawezi kuwawezesha kupanua upeo wenu wa macho, kuhisi kana kwamba mmepata hazina, sembuse kutimiza mnachotaka. Mbona, basi, mnamfuata? Je, mmefikiria kuhusu maswali kama haya?

Umetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 315 Kuweka Fikira Kuhusu Kristo ni Kumwasi Mungu

Inayofuata: 317 Mungu Achunguza Maneno na Matendo ya Mwanadamu kwa Siri

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp