101 Nisingekuwa Nimeokolewa na Mungu

Nisingekuwa nimeokolewa na Mungu, ningekuwa bado naelea duniani,

nikipambana kwa uchungu katika dhambi, nikiishi bila tumaini lolote.

Nisingekuwa nimeokolewa na Mungu, ningekuwa bado nimekanyagwa na ibilisi,

nikifurahia raha za dhambi, bila kujua palipo njia ya maisha ya binadamu.

Mwenyezi Mungu ni mwenye rehema kwangu, maneno Yake yananiita.

Naisikia sauti ya Mungu na nimeinuliwa mbele ya kiti Chake cha enzi.

Kila siku nala na kunywa maneno ya Mungu, naelewa ukweli mwingi.

Naona upotovu wa binadamu ni wa kina kirefu, kweli tunahitaji wokovu wa Mungu.

Ukweli wa Mungu unanitakasa na kuniokoa.

Nimehukumiwa na kusafishwa mara kwa mara, na tabia yangu ya maisha inabadilishwa kwa namna fulani.

Kwa kupitia haki na utakatifu wa Mungu, nakuja kuelewa uzuri Wake.

Naweza kumcha Mungu na kuepuka uovu, na kuishi kwa kudhihirisha mfano wa binadamu.

Nimemwona Mungu uso kwa uso, nimeonja upendo Wake wa kweli.

Kupitia hukumu na kuadibu kwa Mungu, napokea wokovu Wake wa siku za mwisho.

Kwa kutimiza wajibu wangu kwa uaminifu, moyo wangu una furaha na wenye amani.

Kwa kupendana tunaishi mbele ya Mungu kwa uongozi na baraka za Mungu.

Natenda ukweli, kumtii Mungu na kuishi kwa kudhihirisha maisha ya kweli.

Kazi ya Mungu ni halisi na hai, Mungu ni wa kuheshimiwa na wa kupendeza.

Kwa kuona upendo Wake na uzuri wake nataka kutoa maisha yangu Kwake.

Nitafuatilia ukweli na kumpenda milele, nitatimiza wajibu wangu kulipiza upendo Wake.

Iliyotangulia: 100 Upendo Hukesha

Inayofuata: 102 Mungu na Aguse Roho Zetu Mara Nyingine Tena

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp