104 Nataka Kupenda Mungu Zaidi

1

Upendo wa Mungu unayeyusha moyo wangu,

na kusafisha dhana zangu zenye makosa.

Nauelewa moyo Wake, upendo Wake ulio na nguvu.

Kuanzia sasa, nisilalamike tena kamwe;

upendo wote uliopotea sasa umerejeshwa.


Mungu hunipa fadhila nyingi katika upendo;

nataka kumpa maisha yangu.


Nampenda Mungu wangu kwa dhati.

Naapa sitaondoka kutoka Kwake kamwe.

Upendo wa Mungu kwa mwanadamu ni halisi sana, wa kweli mno;

Siustahili hata nikitoa kila kitu changu.

Nataka kumpenda kabisa, kwa kina zaidi, kwa kina zaidi.

2

Upendo wa Mungu hauna mipaka, na ninakubali wangu ni mdogo.

Anakuja katika nchi hii chafu ili kumfanya mwanadamu awe mkamilifu.

Anampa mwanadamu njia ya uzima wa milele.

Anampa mwanadamu moyo Wake wote; upendo Wake ni mkuu sana.


Mungu hunipa fadhila nyingi katika upendo;

nataka kumpa maisha yangu.


Nampenda Mungu wangu kwa dhati.

Naapa sitaondoka kutoka Kwake kamwe.

Upendo wa Mungu kwa mwanadamu ni halisi sana, wa kweli mno;

Siustahili hata nikitoa kila kitu changu.

Nataka kumpenda kabisa, kwa kina zaidi, kwa kina zaidi.

3

Natamani kutimiza wajibu wangu wote kuonyesha upendo kwa Mungu,

na kufuatilia ukweli ili kuufariji moyo Wake.

Nitashikilia ukarimu na upendo wa Mungu;

nitalenga yale ambayo ameniaminia.


Ugumu na majaribu, hayana maana;

katika kila dhoruba bado nitampenda Yeye.

Upendo kwa Mungu hautegemezwi tu kwa dhamiri;

Hakungekuwa na upendo wa kweli bila mateso.


Nampenda Mungu wangu kwa dhati.

Naapa sitaondoka kutoka Kwake kamwe.

Upendo wa Mungu kwa mwanadamu ni halisi sana, wa kweli mno;

Siustahili hata nikitoa kila kitu changu.

Nataka kumpenda kabisa, kwa kina zaidi, kwa kina zaidi.

Iliyotangulia: 103 Sala ya Watu wa Mungu

Inayofuata: 105 Ee Mungu, Wajua Jinsi Ninavyokutamani Sana?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

273 Upendo Safi Bila Dosari

1 Upendo ni hisia safi sana, safi bila dosari. Tumia moyo wako, tumia moyo wako kupenda na kuhisi na kutunza. Upendo hauweki masharti au...

83 Upendo wa Kweli

1 Namrudia Mungu na kuuona uso Wake upendezao, nikiwa huru kutokana na udhibiti wa kaida za dini. Neno Lake linanijaza na raha na furaha...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki