733 Wanadamu Wanakosa Mantiki Sana

1 Watu huwa hawadai mengi kutoka kwao wenyewe, lakini hudai mengi kutoka kwa Mungu. Wanamtaka Awaonyeshe ukarimu wa kipekee na kuwa na subira na uvumilivu kwao, kuwatunza, kuwaruzuku, kuwatabasamia, na kuwatunza kwa njia nyingi. Wanatarajia kwamba Hatakuwa mkali kwao hata kidogo au kufanya chochote ambacho kinaweza kuwakasirisha hata kidogo, na wao huridhika tu Akiwaongelesha maneno matamu kila siku. Wanadamu wamepungukiwa na mantiki sana! Watu hawako wazi juu ya wanakopaswa kusimama, wanachopaswa kufanya, kile wanachopaswa kukamilisha, ni maoni gani wanayopaswa kuwa nayo, ni nafasi gani wanapaswa kusimamia ili kumhudumia Mungu, na ni mahali gani wanafaa kuwa ili kujiweka ndani. Watu wenye nafasi ndogo hujipenda sana, na watu wasiokuwa na nafasi pia hujipenda kweli. Watu huwa hawajielewi kamwe.

2 Kwa sasa mna mahitaji mengi mno na ni mengi kupita kiasi. Nia zako nyingi zinathibitisha kwamba wewe hujasimama katika nafasi ya sawa, nafasi yako iko juu mno, na umejiona kama mheshimiwa kuzidi kiasi kana kwamba wewe huko chini zaidi ya Mungu. Kwa hiyo wewe ni mgumu wa kushughulikiwa, na hii ni asili ya Shetani hasa. Kama mnaweza kuendelea na imani yenu, kutolalamika kamwe, na kutimiza wajibu wako kama kawaida bila kujali ni nini kinachosemwa kwako, jinsi unavyotendewa kwa ukali kwa ukali na jinsi unavyopuuzwa, basi utakuwa mtu mwenye kukomaa na wenye uzoefu, Na kwa kweli utakuwa na hadhi fulani na mantiki ya kawaida. Hutahitaji vitu vya Mungu, hutakuwa na tamaa za ubadhirifu, na hutaomba vitu vya watu wengine au vya Mungu kwa msingi wa vitu unavyovipenda. Hii inaonyesha kuwa unamiliki mfano wa mtu kwa kiwango fulani.

Umetoholewa kutoka katika “Watu Ambao Hufanya Madai Daima kwa Mungu Ndio Wenye Busara Kidogo Zaidi” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 732 Kwa Nini Mwanadamu Humdai Mungu Kila Mara?

Inayofuata: 734 Una Uwezekano wa Kumwasi Mungu Unapokuwa na Madai Kwake

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp