82 Njia ya Pekee kwa Binadamu Kuingia katika Mapumziko

1 Wanaoweza kusimama imara wakati wa kazi ya Mungu ya hukumu na kuadibu siku za mwisho—yaani, wakati wa kazi ya mwisho ya utakaso—watakuwa wale watakaoingia katika raha ya mwisho na Mungu; kwa hivyo, wanaoingia rahani wote watakuwa wametoka katika ushawishi wa shetani na kupokewa na Mungu baada tu ya kupitia kazi Yake ya mwisho ya utakaso. Hawa watu ambao hatimaye wamepokewa na Mungu wataingia katika raha ya mwisho.

2 Kiini cha kazi ya Mungu ya kuadibu na hukumu ni kutakasa binadamu, na ni ya siku ya raha ya mwisho. Vinginevyo, binadamu wote hawataweza kufuata aina yao ama kuingia katika raha. Hii kazi ni njia ya pekee ya binadamu kuingia rahani. Kazi ya Mungu ya utakaso pekee ndiyo itatakasa udhalimu wa binadamu, na kazi Yake ya kuadibu na hukumu pekee ndiyo itadhihirisha hayo mambo yasiyotii miongoni mwa binadamu, hivyo kutenga wanaoweza kuokolewa kutoka wale wasioweza, na wale watakaobaki kutoka wale ambao hawatabaki.

3 Kazi Yake ya mwisho ya kuadhibu waovu na kuwatuza wazuri inafanywa kabisa ili kutakasa kabisa binadamu wote, ili Aweze kuleta binadamu watakatifu mno katika pumziko la milele. Hatua hii ya kazi Yake ni kazi Yake muhimu zaidi. Ni hatua ya mwisho ya kazi Yake yote ya usimamizi. Kama Mungu hangewaangamiza waovu lakini badala yake kuwaacha wabakie, basi binadamu wote bado hawangeweza kuingia rahani, na Mungu hangeweza kuleta binadamu katika ulimwengu bora. Kazi ya aina hii haingekuwa imekamilika kabisa. Atakapomaliza kazi Yake, binadamu wote watakuwa watakatifu kabisa. Mungu anaweza kuishi kwa amani rahani kwa namna hii pekee.

Umetoholewa kutoka katika “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 81 Hukumu ya Siku za Mwisho Ndiyo Kazi ya Kukamilisha Enzi

Inayofuata: 83 Maelezo ya Ndani ya Maneno ya Mungu Katika Siku za Mwisho

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp