160 Jinsi ya Kumjua Mungu wa Vitendo

1 Je, unapaswa kujua nini kuhusu Mungu wa vitendo? Mungu wa vitendo Mwenyewe anajumuisha Roho, Nafsi, na Neno, na hii ndiyo maana ya kweli ya Mungu wa utendaji Mwenyewe. Ufahamu wa Mungu wa vitendo unajumuisha kujua na kuyapitia maneno Yake, na kuelewa sheria na kanuni za kazi ya Roho Mtakatifu, na jinsi Roho wa Mungu anavyofanya kazi katika mwili. Kwa hivyo, pia, inajumuisha kujua kwamba kila tendo la Mungu katika mwili linaongozwa na Roho, na kwamba maneno Anenayo ni maonyesho ya moja kwa moja ya Roho. Hivyo, ukitaka kumjua Mungu wa vitendo, lazima kimsingi ujue jinsi ambavyo Mungu hufanya kazi katika ubinadamu na katika uungu; hili, wakati ule ule, linahusu maonyesho ya Roho, ambayo watu wote hujihusisha nayo.

2 Ni nini kilichomo katika maonyesho ya Roho? Wakati mwingine Mungu hufanya kazi miongoni mwa ubinadamu, na wakati mwingine katika uungu—lakini kwa jumla, Roho anatawala katika pande zote mbili. Roho anafanya kazi kawaida, lakini kuna pande mbili za uelekezaji Wake kwa Roho: Upande mmoja ni kazi Yake kwa ubinadamu, na upande mwingine ni kupitia uungu. Unafaa kujua haya wazi wazi. Kazi ya Roho hubadilika kulingana na matukio: Wakati kazi Yake ya binadamu inahitajika, Roho anaielekeza kazi hii ya binadamu, na wakati kazi ya uungu inahitajika, uungu hujitokeza moja kwa moja kuifanya. Kwa sababu Mungu hufanya kazi katika mwili na kujionyesha katika mwili, Anafanya kazi katika ubinadamu na katika uungu.

3 Kuonekana kwa Mungu katika mwili kunamaanisha kuwa kazi yote na maneno ya Roho wa Mungu yanafanywa katika ubinadamu wake wa kawaida, na kupitia mwili Wake uliopatikana. Kwa maneno mengine, Roho wa Mungu huelekeza kazi Yake ya ubinadamu na hutekeleza kazi Yake ya uungu katika mwili, na katika Mungu kupata mwili unaweza kuona kazi ya Mungu katika ubinadamu na kazi kamili ya uungu; huu ndio umuhimu wa utendaji hata zaidi wa kuonekana kwa Mungu wa vitendo katika mwili. Maana ya Mungu wa vitendo ni kuwa kazi Yake ya ubinadamu na kazi Yake ya uungu, kama inavyoelekezwa na Roho, inaonyeshwa kupitia mwili Wake, ili watu waone kuwa Yeye ni wazi na mwenye kufanana na kiumbe chenye uhai, na ni halisi na wa hakika.

Umetoholewa kutoka katika “Unapaswa Kujua kuwa Mungu wa Vitendo Ni Mungu Mwenyewe” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 159 Ubinadamu wa Kristo Waelekezwa na Uungu wa Mungu

Inayofuata: 161 Chanzo cha Mwanadamu Kumpinga na Kutomtii Kristo

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp