579 Jinsi Unavyopaswa Kufanya Wajibu Wako

1 Ikiwa mwanadamu haonyeshi anachopaswa kuonyesha wakati wa kutoa huduma au kutimiza kile kilicho katika uwezo wake kiasili, na badala yake huzembea na kufanya tu bila ari yoyote, atakuwa amepoteza majukumu yake ambayo kiumbe anapaswa kuwa nayo. Mwanadamu kama huyu anachukuliwa kuwa mtu hafifu na duni apotezaye nafasi; itakuaje kwamba mtu kama huyu aitwe kiumbe? Je, hao si ni vyombo vya upotovu ving’aavyo kwa nje ila vimeoza kwa ndani? Kama mwanadamu ameshindwa kutekeleza wajibu wake, anafaa kujihisi mwenye hatia na mdeni; anapaswa kuudharau udhaifu wake na kukosa umuhimu, uasi na uharibifu wake, na zaidi ya hayo, anafaa kujitolea maisha na damu sadaka kwa ajili ya Mungu. Hapo tu ndipo atakapokuwa kiumbe ampendaye Mungu kwa kweli, na ni mwanadamu kama huyu tu anayestahili baraka na ahadi za Mungu, na kukamilishwa na Yeye.

2 Na wengi wenu je? Mnamtendeaje Mungu aishiye miongoni mwenu? Mmefanyaje wajibu wenu mbele Zake? Je, mmefanya yote mliyoitwa kufanya, hata kwa gharama ya maisha yenu? Mmetoa sadaka gani? Je, hamjapokea mengi kutoka Kwangu? Mnaweza kuonyesha tofauti? Mna uaminifu kiasi gani Kwangu? Mmenitolea huduma vipi? Na kuhusu yote Niliyowapa na kuwafanyia je? Je, mmeyazingatia yote? Je, mmeyahukumu na kuyalinganisha haya yote kwa dhamiri yoyote ndogo mliyo nayo? Maneno na matendo yenu yanawezaje kuwa ya kustahili? Je, yawezekana hizo sadaka zenu kidogo zinalingana na yote Niliyowapa?

3 Sina chaguo jingine na Nimejitolea kwenu kwa moyo wote, na bado mna nia zenye uovu kunihusu na hamnipendi kwa dhati. Huo ndio upeo wa wajibu wenu, jukumu lenu la pekee. Au sivyo? Hamjui kwamba hamjatimiza wajibu wa kiumbe aliyeumbwa hata kidogo? Mnawezaje kuchukuliwa kama kiumbe aliyeumbwa? Je, hamjui wazi mnachopaswa kuonyesha nakuishi kwa kudhihirisha katika maisha yenu? Mmeshindwa kutimiza wajibu wenu, ila mnataka mpate huruma na neema tele za Mungu. Neema hiyo haijaandaliwa kwa wasio na thamani na wa hali duni kama nyinyi, bali kwa wale ambao hawaombi kitu ila wanatoa kwa moyo wa dhati.

Umetoholewa kutoka katika “Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu Mwenye Mwili na Wajibu wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 578 Jinsi ya Kuchukulia Agizo la Mungu

Inayofuata: 580 Kutenda Maneno ya Mungu na Kumridhisha Mungu Huja Kwanza

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp