706 Jinsi Mungu Apimavyo Mabadiliko Katika Tabia za Watu
1 Mgeuzo katika tabia haufanyiki ghafla sana, na haimaanishi kwamba unaweza kutia ukweli katika vitendo katika kila mazingira baada ya wewe kuelewa ukweli. Hii inahusisha asili ya mwanadamu. Upande wa nje, inaonekana kana kwamba unatia ukweli katika vitendo, lakini kwa kweli, hali ya matendo yako haionyeshi kwamba unatia ukweli katika vitendo. Kuna watu wengi ambao, punde tu wanayo mienendo fulani ya nje, huamini. “Je, kwani sitimizi wajibu wangu? Je, sikuacha familia na kazi yangu? Je, kwani sitii ukweli katika vitendo kwa kutimiza wajibu wangu?” Lakini Mungu hatambui kwamba unatia ukweli katika vitendo. Wale wote ambao matendo yao yamechafuliwa na nia na malengo ya kibinafsi hawatendi ukweli. Kusema kweli, aina hii ya mwenendo huenda itashutumiwa na Mungu; haitasifiwa au kukumbukwa na Yeye. Kulichangua hili zaidi, unafanya uovu na mwenendo wako unampinga Mungu.
2 Kutoka nje, mambo haya unayoyafanya yanaonekana kuambatana na ukweli: Hukatizi wala kusumbua chochote na hujafanya maharibifu yoyote ya kweli au kukiuka ukweli wowote. Kinaonekana kuwa chenye mantiki na cha maana, ilhali asili ya matendo yako inahusika na kufanya uovu na kumpinga Mungu. Kwa hivyo unapaswa kupambanua kama kumekuwa na mabadiliko katika tabia yako na kama unatia ukweli katika vitendo kwa kutazama nia nyuma ya matendo yako kulingana na maneno ya Mungu. Haiamuliwi na maneno au maoni ya kibinadamu. Badala yake, inategemea Mungu kusema kama unakubali mapenzi Yake au la, kama matendo yako yana uhalisi wa ukweli au la, na kama yanafikia mahitaji Yake na viwango Vyake au la. Kujipima tu dhidi ya matakwa ya Mungu ndiyo sahihi.
Umetoholewa kutoka katika “Unachopaswa Kujua Kuhusu Kuigeuza Tabia Yako” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo