284 Uchungu wa Binadamu Unaibukaje?
1 Kwa sababu watu hawatambui mipango ya Mungu, na ukuu wa Mungu, siku zote wanakabiliana na hatima hiyo kwa kuasi, kwa mtazamo wa kuasi, na siku zote wanataka kutupilia mbali mamlaka na ukuu wa Mungu, na mambo yale ambayo hatima imewahifadhia, wakitumai kwamba watabadilisha hali zao za sasa na kubadilisha hatima yao. Lakini hawawezi kufaulu; wanazuiliwa kwa kila sehemu ya mabadiliko katika maisha. Mvutano huu, unaoendelea ndani ya nafsi ya mtu, ni wa maumivu; maumivu haya hayasahauliki; na wakati wote huu mtu anapoteza maisha yake mwenyewe.
2 Sababu ya maumivu haya ni nini? Ni kwa sababu ya njia ambazo watu huchukua, njia ambazo watu huchagua kuishi katika maisha yao. Baadhi ya watu huenda wasitambue mambo haya. Lakini unapojua kwa kweli, unapotambua kwa kweli kwamba Mungu anao ukuu juu ya hatima ya binadamu, unapoelewa kwa kweli kwamba kila kitu ambacho Mungu amekupangilia na kukuamulia ni chenye manufaa makubwa, na ni ulinzi mkubwa, basi unahisi maumivu yako yakipungua kwa utaratibu, na uzima wako wote unaanza kutulia, kuwa huru na kukombolewa.
3 Huzuni ya binadamu, si kwamba binadamu anatafuta maisha mazuri, si kwamba anatafuta umaarufu na utajiri au anang’ang’ana dhidi ya hatima yake mwenyewe kupitia kwenye ukungu, lakini kwamba baada ya yeye kuona uwepo wa Muumba, baada ya yeye kujifunza hoja kwamba Muumba anao ukuu juu ya hatima ya binadamu, bado hawezi kurekebisha njia zake, hawezi kuvuta miguu yake kutoka kwenye mtego, lakini anaufanya moyo wake kuwa mgumu na anasisitizia makosa yake. Afadhali aendelee kutapatapa kwenye matope, akiapa kwa ukaidi dhidi ya ukuu wa Muumba, akiupinga mpaka mwisho wake mchungu, bila ya hata chembechembe kidogo ya majuto, na mpaka pale anapolazwa akiwa amevunjika na anavuja damu ndipo anapoamua hatimaye kusalimu amri na kugeuka na kubadilisha mwenendo. Kwa kweli huu ni huzuni kwa binadamu. Kwa hivyo Ninasema, wale wanaochagua kunyenyekea ni werevu na wale waliochagua kutoroka ni vichwa vigumu.
Umetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III” katika Neno Laonekana katika Mwili