406 Imani Yako iko Vipi Hasa?

1 Vinywa vyenu vimejaa maneno ya uongo na uchafu, usaliti na kiburi. Kamwe hamjawahi kunena maneno ya ukweli Kwangu, wala maneno matakatifu, wala maneno ya kunitii baada ya kulipitia neno Langu. Hatimaye, hii imani yenu ni ya aina gani? Nyoyo zenu zimejaa tamaa na mali, mawazo yenu yamejaa mali ya kilimwengu. Kila siku, mnafanya hesabu jinsi mtakavyofaidika kutoka Kwangu, mkihesabu kiasi cha mali na vitu vya kidunia mlivyopata kutoka Kwangu. Kila siku, mnangoja baraka zaidi ziwashukie ili muweze kufurahia, hata zaidi na vyema zaidi, vitu zaidi vya raha.

2 Vile vilivyo katika mawazo yenu kila wakati si Mimi, wala ukweli utokao Kwangu, bali ni mume (mke), mwanao, bintiyo au mlacho na kuvaa, na vile mtakavyoburudika na starehe nzuri zaidi. Hata mlishindilie tumbo lenu kwa vyakula hadi pomoni, je, si nyinyi bado ni zaidi ya maiti tu? Hata wakati ambapo, kwa nje, mnavalia mavazi ya kupendeza sana, si nyinyi bado ni maiti inayotembea isiyo na uhai? Mnafanya kazi kwa bidii kwa ajili ya tumbo lenu mpaka mnapotokwa na mvi, ilhali hakuna aliye tayari kuutoa unywele mmoja kwa ajili ya kazi Yangu. Mnasafiri kila mara, mnafanya kazi na kupiga bongo kwa ajili ya miili yenu, na kwa sababu ya watoto wenu, ilhali hakuna yeyote anayeshughulika wala kufikiria kuhusu mapenzi Yangu. Ni nini ambacho bado mnatarajia kufaidi kutoka Kwangu?

Umetoholewa kutoka katika “Wengi Wanaitwa, Lakini Wachache Wanachaguliwa” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 405 Hii ni Imani ya Kweli Katika Mungu?

Inayofuata: 407 Umepata Chochote Kutoka Miaka ya Imani?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp