321 Mungu Atawezaje Kuwasamehe Wale Wanaotelekeza Maneno Yake?

1 Wakati Nilieneza mbingu na kuumba vitu vyote, Sikuruhusu kiumbe yeyote kushiriki atakavyo, sembuse kuruhusu jambo lolote kuvuruga kazi Yangu na usimamizi Wangu, vile linavyopenda. Sikuvumilia mtu au kitu chochote; Ningewezaje kuwaacha walio wakatili na wa kinyama Kwangu? Ningewezaje kuwasamehe wale ambao wanaasi dhidi ya maneno Yangu? Ningewezaje kuwaacha wanaoniasi? Kama ungekuwa mwaminifu Kwangu, Yehova, je, ungeweza kujichukulia sadaka kutoka katika madhabahu Yangu? Je, ungeweza kutumia ulimi wako wa sumu kukufuru jina Langu takatifu? Ungeweza kuliasi neno Langu kwa njia hii? Je, ungeweza kuuchukua utukufu Wangu na jina langu takatifu kama chombo ambacho kwalo unamtumikia Shetani, yule mwovu?

2 Maisha Yangu yametolewa kwa ajili ya furaha ya watakatifu. Ningewezaje kukuruhusu ucheze na maisha Yangu jinsi utakavyo, na kuyatumia kama chombo kwa ajili ya migogoro kati yenu? Mngewezaje kuwa wakatili sana, na watovu sana katika njia ya wenye wema, katika jinsi mlivyo Kwangu? Je, hamjui kwamba tayari Nimeandika matendo yenu maovu katika neno hili la maisha? Jinsi gani mngeweza kuepuka siku ya ghadhabu Ninapoadibu Misri? Ningewezaje kuwaruhusu kunipinga na kuniasi kwa njia hii, mara kwa mara? Uvumilivu Wangu ulitayarishwa kwa ajili ya matendo yenu maovu, na upo kwa ajili ya kuadibu kwenu siku hiyo. Je, ninyi si wale mtakaopata hukumu ya ghadhabu Yangu punde Nifikapo mwisho wa uvumilivu Wangu?

3 Si mambo yote yapo mikononi Mwangu, Mwenyezi? Ningewezaje kuwaruhusu mniasi hivyo, chini ya mbingu? Maisha yenu yatakuwa magumu sana kwa kuwa mmekutana na Masiha, ambaye ilisemekana Angekuja, lakini ambaye kamwe Hakuja. Je, si nyinyi ni maadui Wake? Yesu amekuwa rafiki wenu, lakini bado mu maadui wa Masiha. Je, hamjui kwamba ingawa nyinyi ni marafiki wa Yesu, matendo yenu maovu yamejaza vyombo vya wale ambao ni wa karaha? Ingawa nyinyi mu karibu sana na Yehova, je, hamjui kwamba maneno yenu mabaya yamefikia masikio ya Yehova na kuchochea ghadhabu Yake? Ingekuwaje awe karibu nawe, na jinsi gani Yeye asingevichoma hivyo vyombo vyako, ambavyo vimejaa matendo mabaya? Ingekuwaje Asiwe adui wako?

Umetoholewa kutoka katika “Hakuna Aliye wa Mwili Anayeweza Kuepuka Siku ya Ghadhabu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 320 Usemi na Matendo Yako ni Machafu Machoni pa Mungu

Inayofuata: 322 Mungu Apata Nini Kutoka kwa Mwanadamu?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp