185 Jinsi Mungu Awaonavyo Binadamu

1 Kwa hivyo baada ya Bwana Yesu kupitia na kushuhudia maisha ya binadamu katika dhambi, kulikuwa na tamanio kuu lililojionyesha katika moyo Wake—kuwaruhusu wanadamu kujiondoa kutoka katika maisha yao ya kupambana na dhambi. Tamanio hili lilimfanya kuhisi zaidi na zaidi kwamba lazima Aende katika msalaba na kuzichukua dhambi za binadamu haraka iwezekanavyo, kwa dharura. Hizi ndizo zilizokuwa fikira za Bwana Yesu wakati huo, baada ya Yeye kuishi na watu na kuwaona, kuwasikia, na kuhisi umaskini wa maisha yao ndani ya dhambi.

2 Kwamba Mungu mwenye mwili Angekuwa na nia ya aina hii kwa mwanadamu, kwamba Angeweza kueleza na kufichua tabia ya aina hii—je, hili ni jambo ambalo mtu wa kawaida angekuwa nalo? Ingawa kuonekana kwa Mungu mwenye mwili ni kama mwanadamu, Anajifunza maarifa ya mwanadamu na kuongea lugha ya mwanadamu, na wakati mwingine Anaonyesha hata mawazo Yake kwa jinsi na hisia za mwanadamu, namna Anavyowaona wanadamu, kiini cha vitu, na namna ambavyo watu waliopotoka wanavyomwona mwanadamu na kiini cha vitu kwa hakika si sawa kabisa. Mtazamo Wake na kimo Anachosimamia ni jambo ambalo halifikiwi na mtu aliyepotoka.

3 Hii ni kwa sababu Mungu ni ukweli, mwili Anaouvalia unamiliki pia kiini cha Mungu, na fikira Zake na kile ambacho kinadhihirishwa na ubinadamu Wake pia ni ukweli. Bila kujali ni vipi ambavyo mwili wa Mungu mwenye mwili ulivyo wa kawaida, ulivyo kama wengine, ulivyo wa chini, au hata namna ambavyo watu wanamdharau Yeye, fikira Zake na mwelekeo Wake kwa wanadamu ni mambo ambayo hakuna binadamu angeweza kufuatisha na wala hakuna binadamu angeweza kuiga. Siku zote Atawaangalia wanadamu kutoka kwa mtazamo wa uungu, kutoka katika kimo cha madaraka Yake kama Muumba. Siku zote Atawaona wanadamu kupitia katika kiini na akili ya Mungu. Hawezi kabisa kuwaona wanadamu kutoka katika kimo cha mtu wa kawaida na kutoka kwa mtazamo wa mtu aliyepotoka.

Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 184 Mungu Alikuwa Mwili ili Kumshinda Shetani na Kumwokoa Mwanadamu

Inayofuata: 186 Mwanadamu Aweza Kumwelewa Mungu Bora Kupitia Mungu Mwenye Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp