408 Kweli Umeyatoa Maisha Yako Katika Imani Yako?

1 Na kuhusu imani yako katika Mungu, je? Umeyatoa maisha yako kwa kweli? Mngepitia majaribu sawa na yale ya Ayubu, hakuna hata mmoja miongoni mwenu anayemfuata Mungu leo hii angeweza kusimama imara, nyote mngeanguka chini. Na kunayo, kawaida kabisa, tofauti kubwa kati ya ninyi na Ayubu. Leo, kama nusu ya mali yenu ingetwaliwa mngethubutu kukana kuwepo kwa Mungu; kama mtoto wenu wa kiume au wa kike angechukuliwa kutoka kwenu, mngekimbia barabarani mkilalamika vikali; kama njia yako ya pekee kupata riziki ingegonga mwamba, ungejaribu kuanza kujadiliana mada hiyo na Mungu; ungeuliza kwa nini Nilisema maneno mengi sana hapo mwanzo kukutisha wewe. Hakuna kitu chochote ambacho hamngethubutu kufanya katika nyakati kama hizi.

2 Hili linaonyesha kwamba hamjapata umaizi wowote wa kweli, na hamna kimo cha kweli. Hivyo, majaribu yaliyo ndani yenu ni makubwa mno, kwani ninyi mnajua mengi sana, lakini kile mnachoelewa kweli si hata sehemu moja kwa elfu ya kile mnachofahamu. Msikome tu kwa ufahamu na maarifa pekee; mngeona vyema kiasi gani mnachoweza kutia katika vitendo kwa kweli, kiasi gani cha nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu kilipatikana kupitia katika jasho la bidii yenu wenyewe, na katika matendo mangapi yenu mmetambua azimio lenu wenyewe. Unapaswa kuchukua kimo chako na kutenda kwa uzito. Katika imani yako kwa Mungu, hupaswi tu kujaribu kufanya mambo kwa namna isiyo ya dhati kwa ajili ya yeyote—kama unaweza hatimaye kupata ukweli na uzima au la hutegemea ufuatiliaji wako mwenyewe.

Umetoholewa kutoka katika “Utendaji (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 407 Umepata Chochote Kutoka Miaka ya Imani?

Inayofuata: 409 Watu Hawamwamini Mungu kwa Kweli

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp