374 Bado Hujapata Mengi Kutoka kwa Mungu?

1 Ingawa Ayubu alipitia majaribu kutoka kwa Yehova, alikuwa tu mtu mwenye haki aliyemwabudu Yehova, na hata alipokuwa akipitia majaribu hayo hakulalamika kumhusu Yeye, lakini alithamini sana kukutana kwake na Yehova. Watu wa leo hawathamini tu uwepo wa Yehova, bali humkataa, humchukia sana, hulalamika kumhusu, na hudhihaki uwepo Wake. Je, hamjapata zaidi ya kidogo? Je, mateso yenu kweli hayajakuwa makubwa sana? Je, baraka zenu hazijakuwa nyingi kuliko zile za Maria na Yakobo? Je, upinzani wenu haujakuwa hafifu? Inawezekana kuwa yale Nimehitaji kwenu, yale Nimeuliza kutoka kwenu yamekuwa makuu mno na mengi sana?

2 Ghadhabu Yangu iliachiliwa huru tu juu ya wale Waisraeli walionipinga Mimi, si moja kwa moja juu yenu, lakini kile ambacho mmepata kimekuwa tu hukumu Yangu isiyo na huruma na mafichuzi pamoja na utakaso mkali usio na huruma. Licha ya haya watu bado wananipinga na kunikana Mimi bila hata chembe ya utii. Na hata kuna baadhi ya watu ambao hujitenga na Mimi na kunikataa; aina hiyo ya mtu si bora zaidi kuliko bendi ya Kora na Dathani wakimpinga Musa. Mioyo ya watu imekuwa migumu sana, na asili zao ni kaidi sana. Kamwe hawatabadili mienendo yao ya zamani. Je, watu na aina hii ya tabia wanawezaje kujua kwamba wamefurahia baraka zaidi ya mara mia kuliko zile za Ayubu?

3 Wanawezaje kugundua kwamba kile wanachokifurahia ni baraka ambazo zimeonekana katika enzi zote kwa nadra sana, ambazo hakuna mtu aliyewahi kuzifurahia awali? Dhamiri za watu zinawezaje kuhisi aina hii ya baraka ambayo hubeba adhabu? Kusema ukweli, chote Ninachohitaji kwenu ni ili muweze kuwa mifano kwa kazi Yangu na kuwa mashahidi kwa ajili ya tabia Yangu yote na matendo Yangu yote, na ili muweze kuwekwa huru kutokana na mateso ya Shetani. Lakini wanadamu daima huchukizwa na kazi Yangu na wanakuwa na uhasama kwake kimakusudi. Aina hiyo ya mtu anawezaje kutonichochea Mimi kurejesha sheria za Israeli na kuleta juu yake ghadhabu Yangu kwa ajili ya Israeli?

Umetoholewa kutoka katika “Ufahamu wako wa Baraka ni Upi?” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 373 Kwa Nini watu Hawampendi Mungu kwa Kweli?

Inayofuata: 375 Unastahili Kweli Kuwa Mmoja wa Watu wa Mungu?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp