522 Ishi Katika Maneno ya Mungu ili Uwe na Kazi ya Roho Mtakatifu

1 Kama unaweza daima kula na kunywa maneno ya Mungu na pia kuwa makini na mapenzi Yake na kutenda maneno Yake, basi wewe ni wa Mungu, na wewe ni mtu anayeishi ndani ya maneno ya Mungu. Je, uko tayari kuepuka kumilikiwa na Shetani na kuishi katika nuru ya Mungu? Kama unaishi ndani ya maneno ya Mungu, basi Roho Mtakatifu atakuwa na nafasi ya kutenda kazi Yake; kama unaishi chini ya ushawishi wa Shetani, basi Roho Mtakatifu hatakuwa na nafasi ya kutenda kazi yoyote. Kama watu wanaishi ndani ya maneno ya Mungu, basi Roho Mtakatifu atakuwa pamoja nao na kutenda kazi juu yao; kama watu hawaishi ndani ya maneno ya Mungu, basi wanaishi ndani ya utumwa wa Shetani. Watu wanaoishi katika tabia ya kiufisadi hawana uwepo wala kazi ya Roho Mtakatifu.

2 Kama unaishi ndani ya nyanja ya maneno ya Mungu, kama unaishi katika hali inayohitajika na Mungu, basi wewe ni Wake na kazi Yake itatendwa juu yako; kama huishi ndani ya nyanja ya matakwa ya Mungu lakini badala yake unamilikiwa na Shetani, basi hakika wewe unaishi chini ya upotovu wa Shetani. Ni kwa kuishi ndani ya maneno ya Mungu tu na kutoa moyo wako Kwake, ndipo unaweza kukidhi matakwa Yake; lazima ufanye asemavyo Mungu, lazima ufanye maneno ya Mungu msingi wa kuwepo kwako na hali halisi ya maisha yako, na ni hapo tu ndipo utakuwa wa Mungu. Kama kwa dhati unatenda kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu, Atatenda kazi juu yako na kisha utaishi chini ya baraka za Mungu, uishi katika nuru ya uso wa Mungu, kufahamu kazi ambayo Roho Mtakatifu hutenda, na pia kuhisi furaha ya uwepo wa Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Epuka Ushawishi wa Giza na Utapatwa na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 521 Ni Yule Anayefuatilia Ukweli tu Ndiye Anayeza Kufanywa Mkamilifu na Mungu

Inayofuata: 523 Fuata Maneno ya Mungu na Huwezi Kupotea

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp