368 Chuki ya Enzi Imesahaulika?

1 Katika jamii hii ya giza anapatwa na ajali baada ya ajali, lakini hajawahi kufahamu hili. Ni lini atakapoachana na wema wake wa kibinafsi na tabia ya mawazo ya kiutumwa? Kwa nini hajali moyo wa Mungu kiasi hicho? Je, anajifanya haoni ukandamizaji na shida hii? Je, hatamani kuwe na siku ambayo atabadilisha giza kuwa nuru? Je, hatamani zaidi kuponya uonevu dhidi ya haki na ukweli? Je, yupo tayari kutazama tu bila kufanya chochote watu wakitupilia mbali ukweli na kupindua ukweli? Je, anafurahia kuendelea kuvumilia matendo haya mabaya? Je, yupo radhi kuwa mtumwa? Je, yupo tayari kuangamia mkononi mwa Mungu pamoja na watumwa wa taifa hili lililoanguka? Azma yako ipo wapi? Malengo yako yapo wapi? Heshima yako ipo wapi? Maadili yako yapo wapi? Uhuru wako upo wapi? Je, uko tayari kutoa maisha yako yote kwa ajili ya joka kuu jekundu, mfalme wa pepo? Je, unafurahi kumwacha akutese hadi kufa?

2 Kina chake ni vurugu na giza, ilhali mtu wa kawaida, anayeteseka na mateso kama hayo, analalamika bila kupumzika. Ni lini mwanadamu ataweza kunyanyua kichwa chake juu? Mwanadamu amekuwa kimbaumbau na amekonda, anawezaje kuridhika na ibilisi huyu katili na dikteta? Kwa nini asiyatoe maisha yake kwa Mungu mapema awezavyo? Kwa nini bado anayumbayumba? Anaweza kumaliza kazi ya Mungu lini? Hivyo anaonewa na kunyanyaswa bila sababu yoyote, maisha yake yote hatimaye yatakuwa bure; kwa nini ana haraka hivyo ya kufika, na haraka hiyo ya kuondoka? Kwa nini hahifadhi kitu kizuri cha kumpa Mungu? Je, amesahau milenia ya chuki? Azma yako ipo wapi? Malengo yako yapo wapi? Heshima yako ipo wapi? Maadili yako yapo wapi? Kwa nini hahifadhi kitu kizuri cha kumpa Mungu? Je, amesahau milenia ya chuki?

Umetoholewa kutoka katika “Kazi na Kuingia (8)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 367 Mungu Huwaokoa Watu Kutoka katika Maisha ya Mateso Duniani

Inayofuata: 369 Walio Gizani Wanapaswa Kuinuka

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp