315 Kuweka Fikira Kuhusu Kristo ni Kumwasi Mungu
1 Ndani ya akili zenu, Mungu aliye mbinguni ni mnyoofu sana, mwenye haki, na mkubwa, anayestahili ibada na upendezewaji, lakini Mungu huyu aliye duniani ni mbadala tu na chombo cha Mungu aliye mbinguni. Mnaamini Mungu huyu hawezi kuwa sawa na Mungu wa mbinguni, na hata zaidi hawezi kutajwa kwa pumzi moja na Yeye. Ifikapo kwa ukubwa na heshima ya Mungu, ni mali ya utukufu wa Mungu aliye mbinguni, lakini ifikapo kwa tabia na upotovu wa mwanadamu, vinahusishwa na Mungu aliye duniani.
2 Mungu aliye mbinguni daima ni mkuu, ilhali Mungu wa duniani daima ni asiye na maana, mdhaifu na asiyejimudu. Mungu aliye mbinguni haathiriwi na hisia, kwa haki tu, ilhali Mungu aliye duniani ana motisha za kibinafsi tu na Hana haki na mantiki yoyote. Mungu aliye mbinguni hana udanganyifu hata kidogo na daima ni mwaminifu, ilhali Mungu wa duniani daima ana upande mdanganyifu. Mungu aliye mbinguni anampenda sana mwanadamu, ilhali Mungu wa duniani anamjali mwanadamu isivyotosha, hata kumpuuza kabisa. Ufahamu huu usio sahihi umewekwa kwa muda mrefu kwa mioyo yenu na unaweza pia kuendelezwa mbele katika siku za usoni.
3 Mnachukulia matendo yote ya Kristo kwa msimamo wa wadhalimu na kuhukumu kazi Yake yote na utambulisho Wake na kiini Chake kwa mtazamo wa waovu. Mmefanya kosa kubwa sana na kufanya kile ambacho hakijawahi kufanywa na wale kabla yenu. Yaani, mnamtumikia tu Mungu mkuu aliye mbinguni na taji juu ya kichwa Chake na hammshughulikii kamwe Mungu mnayemchukulia kuwa asiye na maana kabisa kiasi cha kutoonekana kwenu. Hii siyo dhambi yenu? Huu sio mfano halisi wa kosa lenu dhidi ya tabia ya Mungu?
Umetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani” katika Neno Laonekana katika Mwili