105 Nina Furaha Sana Kuishi Mbele za Mungu
1
Ndugu furahieni maneno ya Mungu
na muishi kwa furaha mbele za Mungu.
Kupitia ushirika wa maneno ya Mungu,
ufahamu wetu wa ukweli unakuwa halisi.
Dhana za kidini zinaondolewa,
na twaona kwamba maneno ya Mungu ni ukweli.
Twaweza kuhudhuria karamu ya harusi ya Mwanakondoo,
mioyo yetu ina furaha isiyo na kifani.
Kwa kupitia hukumu ya Mungu,
tunatakaswa na kumjua Mungu wa vitendo.
Tulifuata ibada tu, imani yetu haikuwa dhahiri.
Sasa Kristo wa siku za mwisho Anena maneno Yake;
haya yatukimu, kutuchunga na ni ya kweli.
Tunapojua ukweli, twawekwa huru, twaishi mbele za Mungu.
2
Ndugu, dada furahieni maneno ya Mungu
na muishi kwa furaha mbele za Mungu.
Tunaposhiriki ukweli, tunakuja kujua kiburi chetu, udanganyifu wetu, ukosefu wetu wa ubinadamu.
Twajichukia wenyewe, tukiunyima mwili.
Twaamua kumpendeza Mungu, kutenda ukweli.
Kuwa waaminifu, twalinganisha maneno yetu na vitendo;
mioyo yetu yote yahisi oh, utamu ulioje!
Hakuna njia za Shetani, hakuna uwongo.
Kwa pamoja, tunatii ukweli, twaingia katika maneno ya Mungu.
Tunapendana na kusaidiana, kutenda kulingana na ukweli,
kujizoesha kumpenda Mungu, fanya wajibu vizuri.
Twaishi kwa kudhihirisha mfano wa binadamu
kumtukuza na kumshuhudia.
3
Ndugu furahieni maneno ya Mungu
na muishi kwa furaha mbele za Mungu.
Maneno ya Mungu yatuongoza katika mateso, nyakati ngumu.
Joka kubwa jekundu ni foili[a] ya Mungu.
Kuona uweza na hekima ya Mungu,
daima tutamfuata Mungu kwa imani kamili.
Kupitia majaribu na shida ya kila aina,
sasa twamjua Mungu na tumeokolewa na Yeye.
Ni fadhila ya Mungu kushiriki
mateso ya Kristo, ufalme na uvumilivu.
Kadiri watu wa Mungu wakomaavyo zaidi,
ndivyo joka kuu jekundu liangukavyo.
Maneno ya Mungu yametimia kikamilifu.
Ufalme wa Kristo uko duniani, tunamsifu Mungu daima.
Ndugu, dada furahieni maneno ya Mungu
na muishi kwa furaha mbele za Mungu.
Tanbihi:
a. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.