Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

182 Ni Bahati Yetu Nzuri Kumhudumia Mungu

1

Tunasikia sauti ya Mungu na kuthibitisha kuonekana na kazi ya Mungu.

Tunahisi msisimko sana kumwona Mungu wa vitendo uso kwa uso.

Tuna bahati sana kukaribisha kurudi kwa Bwana.

Ee! Kwa kuhudhuria sikukuu pamoja na Mungu,

tunainuliwa hadi katika ufalme wa mbinguni!

Kuanzia sasa kuendelea tutakula, kunywa na kufurahia maneno ya Mungu,

tunafurahia sana kuwa na Mungu.

Ee! Tuko tayari kufanya kazi kama wanyama wa mzigo kwa ajili ya Mungu

na kutii mipango na taratibu Zake.

Kwa mioyo yetu yote, tutamhudumia Mungu maisha yetu yote,

na tutasifu tabia ya Mungu yenye haki milele.

2

Tukitaka sana na kutamani kubarikiwa,

tunakutana na ufunuo na hukumu ya maneno ya Mungu.

Mioyo yetu inachomwa na upanga Wake

na tunahisi maumivu na uchungu mwingi.

Sisi ni wapotovu hatustahili kuuona uso wa Mungu.

Kwa kumwamini Mungu ili kubarikiwa

na kuingia katika ufalme wa mbinguni pekee

Miaka mingi sana ya kutamani imepotea yote,

tunadhoofika katika maumivu na mioyo yetu imevunjika.

Maneno ya Mungu yanashinda mioyo yetu, tumeridhika kabisa,

na tunaanguka chini mbele Yake.

3

Ni kupitia hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu

pekee ndiyo tunaona jinsi ambavyo tumepotoshwa sana.

Tukiwa tumejawa nia na tamaa ya kubarikiwa,

tabia zetu potovu hazijatakaswa.

Si tu kwamba hatustahili kuingia katika ufalme wa mbinguni pekee,

kwa neema ya Mungu ndio tunahudumu.

Tuko tayari na ni bahati yetu nzuri.

Huu ndio upendo na baraka kubwa zaidi ya Mungu.

Ee! Tuko tayari kufanya kazi kama wanyama wa mzigo kwa ajili ya Mungu

na kutii mipango na taratibu Zake.

Kwa mioyo yetu yote, tutamhudumia Mungu maisha yetu yote,

na tutasifu tabia ya Mungu yenye haki milele.

Leo, tunaweza kumhudumia Mungu,

na tunahisi kuwa hatustahili kabisa.

Hatujali ikiwa tutabarikiwa au tutakutana na maafa,

wala hatujali hatima yetu itakuwa nini.

Mungu anamshinda Shetani kwa maneno Yake na kutuokoa kutoka gizani.

Iliyotangulia:Ee Mungu, Siwezi Kukuacha

Inayofuata:Moyo wa Mungu Haujaliwazwa Bado

Maudhui Yanayohusiana

 • Nimeuona Upendo wa Mungu

  1 Mwenyezi Mungu, ni Wewe unayenipenda. Katika ulimwengu mchafu Umenichagua mimi! Hivyo nimekuja mbele Yako, naam, nimekuja mbele Yako, nikiishi maish…

 • Nitampenda Mungu Milele

  1 Ee Mungu! Maneno Yako yananiita nirudi Kwako. Nakubali kufundishwa katika ufalme Wako mchana na usiku. Mara nyingi sana nilikuwa dhaifu na hasi, m…

 • Kusudi la Kazi ya Mungu la Usimamizi

  1 Mungu ana mpango wa usimamizi wa miaka 6,000, uliyogawanywa katika hatua tatu, kila moja inaitwa enzi. Kwanza ni Enzi ya Sheria, kisha Enzi ya Neema…

 • Mradi tu Usimwache Mungu

  Upendo na huruma za Mungu hupenyeza katika kila sehemu ya kazi ya usimamizi Wake, na bila kujali kama watu wanaweza kuelewa nia njema za Mungu, bado …