240 Kutoenda Mbali na Maneno ya Mungu

1 Natafakari maneno ya Mungu na najitafakari mwenyewe kwa dhati. Mungu ameniinua nitekeleze wajibu ili Anifundishe. Lakini nimetumia fursa hii kujionyesha. Kazi yangu izaapo matunda kidogo, mimi hubadilisha hata ninavyotembea na ninavyoongea. Natangaza kumpa Mungu utukufu wote lakini nahesabu michango yangu mwenyewe. Naamini daima katika vipaji vyangu lakini simwombi Mungu kwa dhati. Kwa kutotafuta ukweli katika mambo yote, nagonga mwamba baada ya mwamba. Ni baada tu ya kuingia gizani ndipo nimeona nilivyo mwovu na fukara. Ee Mungu! Mwishowe najua siwezi kufanya chochote bila Wewe.

2 Sikujua kamwe umuhimu wa kanuni katika kushughulikia mambo. Daima nilihisi kuwa kila kitu kingefanywa kupitia vipaji. Sasa nimetambua kuwa mbali na maneno ya Mungu, siendi popote. Kutegemea vipaji kazini bila kutafuta ukweli hakika hakutafaulu. Bila utii na upendo kwa Mungu, kutekeleza wajibu wangu ni bure. Bila aibu nilikwenda kinyume na dhamiri yangu na kuiba utukufu kutoka kwa Mungu, hata nilijionyesha na kujigamba. Huo utachukuliwaje kama moyo wa uchaji kwa Mungu? Kutofuatilia ukweli, nikisisitiza juu ya njia yangu, ningekosaje kujikwaa? Ee Mungu! Hukumu Yako imeniruhusu nijue tabia yako ya haki.

3 Mimi ni mwasi sana, lakini bado Mungu ananipa nuru na kuniongoza. Nionapo upendo na huruma ya Mungu nahisi majuto na mdeni zaidi. Mimi ni mdogo na duni mno, chembe ya vumbi tu. Napaswa kumlipa Mungu ninapoweza kutekeleza wajibu wa kiumbe aliyeumbwa. Nachukia kwamba zamani nilitimiza wajibu wangu bila kutafuta ukweli. Kupoteza nafasi nyingi za kukamilishwa kuliuumiza moyo wa Mungu kweli. Ni baada tu ya kuchivywa katika uchungu ndipo nilijua ukweli ni wa thamani kweli. Ni baada ya kupogolewa na kushughulikiwa na Mungu tu ndipo nilijua nilivyopotoka sana. Niko tayari kufanya kila niwezalo kufuatilia ukweli, kukubali hukumu ya Mungu, na kutakaswa. Nitajitolea mwenyewe kabisa kutekeleza wajibu wangu kuufariji moyo wa Mungu.

Iliyotangulia: 239 Niliona Upendo wa Mungu katika Kuadibu na Hukumu

Inayofuata: 241 Mwishowe Naishi Kwa Kudhihirisha Mfano wa Bibinadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

84 Umuhumi wa Maombi

1 Maombi ni njia moja ya mwanadamu kishirikiana na Mungu, kuita Roho Wake na kuguswa na Mungu. Kadiri unavyoomba zaidi, ndivyo...

115 Nimeuona Upendo wa Mungu

1 Mwenyezi Mungu, ni Wewe unayenipenda. Katika ulimwengu mchafu Umenichagua mimi! Hivyo nimekuja mbele Yako, naam, nimekuja mbele Yako,...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki