Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II

Katika mkutano wetu wa mwisho tuliweza kuzungumzia mada muhimu sana. Je, mnakumbuka mada hiyo ilikuwa kuhusu nini? Hebu Niirudie. Mada ya ushirika wetu wa mwisho ilikuwa: Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe. Je, mada hii ni muhimu kwenu? Ni sehemu gani katika mada hii ni muhimu kwenu? Kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, au Mungu Mwenyewe? Ni sehemu ipi inawavutia zaidi? Ni sehemu ipi mnayotaka kusikiliza kuhusu zaidi? Najua ni vigumu kwenu ninyi kulijibu swali hilo, kwa sababu tabia ya Mungu inaweza kuonekana katika kila kipengele cha kazi Yake, na tabia Yake inafichuliwa katika kazi Yake siku zote na pahali pote, na, kutokana na hayo, inamwakilisha Mungu Mwenyewe; katika mpango wote wa usimamizi wa Mungu, kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe vyote hivi haviwezi kutenganishwa.

Maudhui ya ushirika wetu wa mwisho kuhusu kazi ya Mungu yaliweza kuangazia mambo yaliyofanyika kitambo kwenye Biblia. Maudhui hayo yote yalikuwa hadithi kuhusu binadamu na Mungu, na yalimfanyikia binadamu na wakati huohuo yakahusisha kushiriki na maonyesho ya Mungu, hivyo basi hadithi hizi zinashikilia thamani na umuhimu mkubwa katika kumjua Mungu. Baada tu ya kuwaumba wanadamu, Mungu Alianza kujihusisha na binadamu na kuzungumza na binadamu, na tabia yake ikaanza kuonyeshwa kwa binadamu. Kwa maneno mengine, tangu Mungu alipojihusisha kwanza na wanadamu, Alianza kuweka wazi kwa mwanadamu, bila kukatizwa, kiini Chake halisi na kile Anacho na alicho. Licha ya kama watu wa awali au watu wa leo wanaweza kuona au kuelewa kiini hicho, kwa ufupi Mungu huzungumza na mwanadamu na kufanya kazi miongoni mwa binadamu, Akifichua tabia Yake na Akionyesha kiini Chake—jambo ambalo ni ukweli, na lisilopingika na mtu yeyote. Hii inamaanisha pia kwamba tabia ya Mungu, kiini cha Mungu, na kile Anacho na alicho vyote daima vinatolewa na kufichuliwa Anapofanya kazi na kushirikiana na mwanadamu. Hajawahi kusetiri au kuficha chochote kutoka kwa mwanadamu, lakini badala yake anaweka hadharani na kuachilia tabia Yake Mwenyewe bila ya kuficha chochote. Hivyo basi, Mungu anatumai kwamba binadamu anaweza kumjua Yeye na kuielewa tabia na kiini Chake. Hapendi binadamu kuchukulia tabia Yake na kiini Chake kuwa mafumbo ya milele, wala Hataki wanadamu wamchukulie Mungu kama fumbo lisiloweza kutatuliwa. ni mpaka tu pale ambapo wanadamu watakapomjua Mungu ndipo binadamu atakapojua njia ya kufuata na kuweza kuukubali mwongozo wa Mungu, na wanadamu tu kama hawa ndio wanaoweza kuishi kwa kweli katika utawala wa Mungu, na kuishi katika mwangaza, na kuishi katikati ya baraka za Mungu.

Maneno na tabia iliyowasilishwa na kufichuliwa na Mungu inawakilisha mapenzi Yake, na pia inawakilisha kiini Chake halisi. Wakati Mungu anapojihusisha na binadamu, haijalishi ni nini Anachosema au kufanya, au tabia gani Anayofichua, na haijalishi ni nini binadamu anaona kuhusu kiini cha Mungu na kile Anacho na alicho, vyote vinawasilisha mapenzi ya Mungu kwa binadamu. Licha ya kiwango ambacho binadamu anaweza kutambua, kufahamu, au kuelewa, vyote hivi vinawakilisha mapenzi ya Mungu—mapenzi ya Mungu kwa binadamu. Hili halina shaka! Mapenzi ya Mungu kwa wanadamu ni jinsi Anavyohitaji watu wawe, kile Anachohitaji wafanye, jinsi Anavyowahitaji waishi, na jinsi Anavyowahitaji wawe na uwezo wa kutosheleza mapenzi ya Mungu. Je, mambo haya hayawezi kutenganishwa na kiini cha Mungu? Kwa maneno mengine, Mungu huwasilisha tabia Yake na yote ambayo Anayo na aliyo kwa wakati uleule Anapofanya madai kwa mwanadamu. Hakuna uongo, hakuna kujifanya, hakuna kuficha, na hakuna kutia chumvi. Lakini ni kwa nini mwanadamu hana uwezo wa kujua, na kwa nini mwanadamu hajawahi kutambua kwa uwazi tabia ya Mungu? Kwa nini mwanadamu hajawahi kutambua nia za Mungu? Kile ambacho kimefichuliwa na kutolewa na Mungu ni kile ambacho Mungu Mwenyewe Anacho na alicho; na ni kila sehemu na kipengele cha tabia Yake ya kweli—kwa hivyo kwa nini mwanadamu hawezi kuiona? Kwa nini binadamu hana uwezo wa kuwa na maarifa ya kina? Kunayo sababu muhimu ya haya. Na sababu yenyewe ni ipi? Tangu wakati wa uumbaji, binadamu hajawahi kumchukulia Mungu kama Mungu. Hapo awali, haijalishi ni nini Mungu alifanya kuhusu mwanadamu—mwanadamu ambaye alikuwa ametoka kuumbwa tu—mwanadamu alimchukulia Mungu kama mwandani wake tu na wala si zaidi ya hapo, kama mtu wa kutegemewa, na hakuwa na maarifa yoyote wala uelewa wa Mungu. Hivi ni kusema, mwanadamu hakujua kwamba kile kilichotolewa na Kiumbe huyu—Kiumbe huyu ambaye yeye alimtegemea na kumwona kama mwandani wake—Alidhihirisha kiini cha Mungu, wala hakujua kwamba Kiumbe huyu ndiye ambaye Anatawala juu ya vitu vyote. Kwa ufupi, watu wa wakati huo hawakumtambua Mungu hata kidogo. Hawakujua kwamba mbingu na nchi na vitu vyote viliumbwa na Yeye na wala hawakujua ni wapi Alipotokea, na, zaidi hawakujua Yeye Alikuwa nani. Bila shaka, wakati huo Mungu hakumhitaji binadamu kumjua Yeye au kumfahamu Yeye au kuelewa kila kitu Alichofanya, au kufahamishwa kuhusu mapenzi Yake, kwani hizi zilikuwa nyakati za mapema zaidi baada ya uumbwaji wa mwanadamu. Wakati Mungu alipoanza matayarisho ya kazi ya Enzi ya Sheria, Mungu alifanya mambo fulani kwa binadamu na pia Akaanza kumtolea binadamu madai fulani, Akimwambia namna ya kutolea Mungu sadaka na namna ya kumwabudu. Ni wakati huo ndipo binadamu alipopata mawazo machache yaliyo rahisi kuhusu Mungu, ni hapo tu ndipo alipojua tofauti kati ya binadamu na Mungu na kwamba Mungu ndiye Aliyewaumba wanadamu. Wakati binadamu alipojua kwamba Mungu alikuwa Mungu na binadamu alikuwa binadamu kukawa na umbali fulani kati yake na Mungu, lakini Mungu hakuhitaji kwamba binadamu awe na maarifa makuu au uelewa wa kina kumhusu Yeye. Hivyo basi, Mungu anayatoa mahitaji tofauti kwa binadamu kutokana na hatua na hali za kazi Yake. Mnaona nini katika haya? Je, ni kipengele gani cha tabia ya Mungu unachokiona? Je, Mungu ni wa kweli? Je, matakwa ya Mungu kwa wanadamu yanawafaa? Katika nyakati za awali kabisa kufuatia uumbaji wa Mungu wa wanadamu, wakati Mungu alikuwa bado Hajafanya kazi ya ushindi na ukamilifu kwa wanadamu, na Hakuwa amezungumza nao maneno mengi sana, Aliweka mahitaji kidogo sana kwa wanadamu. Bila kujali kile ambacho binadamu alifanya na namna alivyotenda—hata kama alifanya mambo fulani yaliyomkosea Mungu—Mungu alimsamehe hayo yote, na akayapuuza. Hii ni kwa sababu Mungu Alijua kile Alichokuwa Amempa binadamu na kile kilichokuwa ndani ya binadamu, na basi Alijua kiwango cha mahitaji ambayo anafaa kudai kutoka kwa binadamu. Ingawa kiwango cha mahitaji Yake kilikuwa cha chini sana wakati huo, hii haimaanishi kwamba tabia Yake haikuwa kuu, au kwamba hekima na uweza Wake yalikuwa si chochote bali maneno matupu. Kwa binadamu, kunayo njia moja tu ya kujua tabia ya Mungu na Mungu Mwenyewe: kwa kufuata hatua za kazi ya usimamizi ya Mungu na wokovu wa wanadamu, na kuyakubali maneno ambayo Mungu huzungumzaakiyaelekeza kwa wanadamu. Baada ya mwanadamu kujua kile ambacho Mungu anacho na alicho, na kujua tabia ya Mungu, je, bado mwanadamu angemwomba Mungu amuonyeshe nafsi Yake halisi? Hapana, mwanadamu hangemwomba, na hata asingethubutu kufanya hivyo, kwa kuwa baada ya kuielewa tabia ya Mungu na kile Anacho na alicho, tayari binadamu atakuwa amemwona Mungu Mwenyewe wa kweli, na atakuwa tayari ameona nafsi Yake halisi. Haya ndiyo matokeo yasiyoepukika.

Kadiri kazi na mpango wa Mungu ulivyokuwa ukiendelea bila kukoma na baada ya Mungu kuanzisha agano la upinde wa mvua na binadamu kama ishara kwamba Hangewahi tena kuuangamiza ulimwengu kwa kutumia gharika, Mungu alikuwa na tamanio kubwa la kuwapata wale ambao wangeweza kuwa na mawazo sawa na Yeye. Vivyo hivyo, pia, Alikuwa na tamanio la haraka zaidi la kuwapata wale waliokuwa na uwezo wa kufanya mapenzi Yake duniani, na, isitoshe, kupata kundi la watu ambao wangeweza kuwa huru dhidi ya nguvu za giza, na kutoweza kuwa watumwa wa Shetani, na kuweza kuwa na ushuhuda kwake Yeye duniani. Kupata kundi la watu kama hawa kulikuwa ni tamanio la Mungu kwa muda mrefu, ndicho Alichokuwa akisubiria tangu wakati wa uumbaji. Hivyo basi, licha ya matumizi ya Mungu yagharik Mungu ili kuuangamiza ulimwengu, au agano Lake na binadamu, mapenzi ya Mungu, hali yake ya akili, mpango, na matumaini yote yalibakia vile vile. Kile Alichotaka kufanya, ambacho Alikuwa ametamani kwa muda mrefu kabla ya uumbaji, kilikuwa kupata wale walio miongoni mwa wanadamu ambao Alitamani kuwapata—Kupata watu wa kundi hili ambao wangeweza kufahamu na kujua tabia Yake, na kuyaelewa mapenzi Yake, kundi ambalo lingeweza kumwabudu Yeye. Kundi kama hilo la watu kwa kweli lingeweza kutoa ushuhuda Kwake, na inaweza kusemwa kwamba wangekuwa, wasiri Wake.

Leo, hebu tuendelee kuzifuata nyayo za Mungu na kufuata nyayo za kazi Yake, ili tuweze kufichua fikira na mawazo ya Mungu, na vipengele vyote mbali mbali vinayomhusu Mungu, vyote ambavyo “vimefungwa kabisa” kwa muda mrefu sana. Kupitia mambo haya tutajua hatimaye tabia ya Mungu, kuelewa kiini cha Mungu, tutamruhusu Mungu kuingia kwenye mioyo yetu, na kila mmoja wetu ataweza kumkaribia Mungu polepole, na kupunguza umbali wetu na Mungu.

Sehemu ya kile tulichozungumzia wakati wa mwisho ilihusiana na kwa nini Mungu alianzisha agano na binadamu. Wakati huu, tutakuwa na ushirika kuhusu vifungu vya maandiko vilivyo hapa chini. Hebu tuanze kwa kuyasoma maandiko.

A. Ibrahimu

1. Mungu Amwahidi Ibrahimu Mwana

Mwa 17:15-17 Naye Mungu akasema kwake Ibrahimu, na kuhusu Sarai mke wako, hutamwita kwa jina lake la Sarai, kwa maana Sara ndilo litakuwa jina lake. Na mimi nitambariki yeye, na pia nitakupa mwana kutoka kwake: ndiyo, nitambariki yeye, na yeye atakuwa mama yao mataifa; wafalme wa watu watatoka kwa yeye. Kisha Ibrahimu akaanguka chini kifudifudi, na kucheka, na akasema moyoni, Je, mtoto atazaliwa kwa mtu mwenye umri wa miaka mia moja? naye Sara, aliye na umri wa miaka tisini, atazaa?

Mwa 17:21-22 Lakini nitaliimarisha agano Langu na Isaka, ambaye Sara atakuzalia wewe wakati kama huu mwaka ujao. Naye Akakoma kuzungumza na yeye, na Mungu akapanda juu kutoka kwa Ibrahimu.

Hakuna Awezaye Kuzuia Kazi Ambayo Mungu Ameamua Kufanya

Hivyo, muda mfupi uliopita nyote mmesikia hadithi ya Ibrahimu. Alichaguliwa na Mungu baada ya gharika kuuharibu ulimwengu, jina lake lilikuwa Ibrahimu, na alipokuwa na umri wa miaka mia moja, na mke wake Sara akiwa na umri wa miaka tisini, ahadi ya Mungu ilimjia. Mungu alimwahidi nini? Mungu alimwahidi kile ambacho kinarejelewa katika Maandiko: “Na mimi nitambariki yeye, na pia nitakupa mwana kutoka kwake.” Ni maelezo yapi yaliyofuatia baada ya ahadi ya Mungu ya kumpa mtoto? Maandiko yanaelezea yafuatayo: “Kisha Ibrahimu akaanguka chini kifudifudi, na kucheka, na akasema moyoni, Je, mtoto atazaliwa kwa mtu mwenye umri wa miaka mia moja? naye Sara, aliye na umri wa miaka tisini, atazaa?” Kwa maneno mengine wanandoa hawa wazee walikuwa na umri ulioendasana wa kupata watoto. Naye Ibrahimu alifanya nini baada ya Mungu kutoa ahadi Yake kwake? Alicheka sana na kujiambia, “Je, mtoto atazaliwa kwa mtu mwenye umri wa miaka mia moja?” Ibrahimu aliamini kwamba haikuwezekana—hio ilimaanisha kwamba aliamini kuwa ahadi ya Mungu kwake haikuwa chochote ila mzaha. Kwa mtazamo wa kibinadamu, hili ni jambi lisiloweza kutimizwa na mwanadamu, na vile vile kutimizwa na Mungu na ilikuwa haiwezekani kwa Mungu. Pengine, kwa Ibrahimu, ahadi hii ilikuwa ya kuchekesha. Mungu alimuumba binadamu, lakini yaonekana kwamba hajui kwamba mtu aliyezeeka sana hawezi kupata watoto; Anafikiria kwamba Anaweza kuniruhusu kupata mtoto, Anasema kwamba atanipa mtoto—kwa kweli hilo haliwezekani! Na hivyo, Ibrahimu akaanguka kifudifudi na kucheka, akijiwazia yeye mwenyewe: "Haiwezekani—Mungu anafanya mzaha na mimi, hili haliwezi kuwa kweli." Hakutilia maanani maneno ya Mungu. Hivyo, machoni pa Mungu, Ibrahimu alikuwa binadamu wa aina gani? (Mwenye haki.) Ni wapi ulipojifunza kwamba alikuwa mwenye haki? Ninyi mnafikiria kwamba wale wote ambao Mungu anawaita ni wenye haki na wakamilifu, kwamba wote ni watu wanaotembea na Mungu. Wewe unashikilia mafundisho ya dini! Lazima uone waziwazi kwamba wakati Mungu anapomfasili mtu, Hafanyi hivyo kiholela. Hapa, Mungu hakusema kwamba Ibrahimu alikuwa mwenye haki. Katika moyo Wake, Mungu anavyo viwango vya kumpima kila mtu. Ingawa Mungu hakusema ni mtu wa aina gani ambaye Ibrahimu alikuwa, kwa mujibu wa mwenendo wake, Ibrahimu alikuwa na imani ya aina gani kwake Mungu? Ilikuwa ya kidhahania kidogo? Au alikuwa mwenye imani kubwa? Hapana, hakuwa nayo! Kicheko chake na mawazo yake yalionyesha yeye alikuwa ni nani, kwa hivyo imani yenu kwamba alikuwa mwenye haki ni hadithi tu ya mawazo yenu, ni matumizi yasiyo na mwelekeo wa mafundisho ya kidini, na ni tathmini isiyofaa. Je, Mungu alikiona kicheko cha Ibrahimu na maonyesho yake madogo, Je, Alijua kuyahusu? Mungu alijua. Lakini, je, Mungu angebadili kile Alichokuwa ameamua kufanya? La! Wakati Mungu alipopangilia na kuamua kwamba Angemchagua binadamu huyu, suala hilo lilikuwa tayari limekamilishwa. Si fikira za binadamu wala mwenendo wake ungemshawishi au kuhitilafiana na Mungu hata kidogo; Mungu Asingebadilisha kiholela mpango Wake, wala Asingebadilisha au kuharibu mpango Wake kwa sababu ya mwenendo wa binadamu, hali ambayo ingekuwa ujinga. Ni nini, basi, kimeandikwa katika Mwanzo 17:21-22? “Lakini nitaliimarisha agano langu na Isaka, ambaye Sara atakuzalia wewe wakati kama huu mwaka ujao. Naye akakoma kuzungumza na yeye, na Mungu akapanda juu kutoka kwa Ibrahimu.” Mungu hakutilia maanani hata kidogo kile Ibrahimu alichofikiria au kusema. Na sababu ya kutotilia maanani Kwake ni ipi? Ilikuwa ni kwa sababu kutotilia maanani kwake, kwa wakati huo Mungu hakuhitaji kwamba mwanadamu awe mwenye imani kuu au kwamba aweze kuwa na maarifa makuu kuhusu Mungu, au, hata, aweze kuelewa kile kilichofanywa na kusemwa na Mungu. Hivyo, hakuhitaji kwamba binadamu aelewe kabisa kile Alichoamua kufanya, au watu Alioamua kuwachagua, au kanuni za matendo Yake, kwa maana kimo cha mwanadamu kilikuwa hakitoshi. kwa wakati huo, Mungu alichukulia kile ambacho Ibrahimu alifanya na vyovyote alivyojiendesha yeye mwenyewe kuwa ni kawaida. Hakushutumu, au kukemea, lakini alisema tu: “Sara atakuzalia Isaka majira kama hayamwaka ujao.” Kwa Mungu, baada ya Yeye kutangaza maneno haya, jambo hili lilitimia hatua kwa hatua; machoni pa Mungu, kile ambacho kilikuwa kikamilishwe kwa mpango Wake kilikuwa tayari kimetimizwa. Baada ya kukamilisha mipango katika hili, Mungu aliondoka. Kile binadamu hufanya au kufikiria, kile binadamu huelewa, mipango ya binadamu—hakuna chochote kati ya haya chenye uhusiano wowote na Mungu. Kila kitu hufanyika kulingana na mpango wa Mungu, kulingana na nyakati na hatua zilizowekwa na Mungu. Hiyo ndiyo kanuni ya kazi ya Mungu. Mungu haingilii kati chochote kile ambacho binadamu anafikiria au kujua, ilhali Haachi mpango Wake, wala kuacha kazi Yake kwa sababu binadamu hasadiki wala kuelewa. Mambo ya hakika yanatimizwa kulingana na mpango na fikira za Mungu. Hivi ndivyo hasa tunavyoona kwenye Biblia: Mungu Alisababisha Isaka kuzaliwa wakati ule Aliokuwa amepanga. Je, kweli zinathibitisha kwamba tabia na mwenendo wa binadamu vilizuia kazi ya Mungu? Havikuzuia kazi ya Mungu! Je, imani ndogo ya binadamu kwa Mungu, na dhana zake na fikira kumhusu Mungu viliweza kuathiri kazi ya Mungu? La, havikuathiri! Hata kidogo! Mpango wa usimamizi wa Mungu hauathiriwi na binadamu, suala, au mazingira yoyote. Kila kitu Anachoamua kufanya kitakamilika na kukamilishwa kwa wakati na kulingana na mpango Wake, na kazi Yake haiwezi kutatizwa na binadamu yeyote. Mungu hupuuza vipengele fulani vya ujinga na kutojua kwa binadamu, na hata upinzani na dhana fulani za binadamu Kwake, Akifanya kazi ambayo lazima Afanye bila ya kujali. Hii ni tabia ya Mungu na ni onyesho la uweza Wake.

2. Ibrahimu Amtoa Isaka

Mwa 22:2-3 Naye Akasema, Umchukue mwana wako sasa, mwana wako wa pekee Isaka, unayempenda, na uende hadi nchi ya Moria; na huko umtoe kwa sadaka ya kuteketezwa juu ya mojawapo ya milima ambayo nitakuambia. Naye Ibrahimu akaamka asubuhi mapema, na kuweka tandiko kwa punda wake, akawachukua vijana wake wawili pamoja naye, naye Isaka mwana wake, na akapasua kuni kwa sababu ya hiyo sadaka ya kuteketezwa, na akaondoka, na kuenda pahali ambapo alikuwa ameambiwa na Mungu.

Mwa 22:9-10 Na wakafika pahali hapo ambapo Mungu alikuwa amemwambia; naye Ibrahimu akajenga madhabahu hapo, na kuziweka kuni tayari, na kumfunga Isaka mwana wake, naye akamlaza juu ya madhabahu kwa zile kuni. Na Ibrahimu akanyosha mbele mkono wake, na kukichukua kisu ili amchinje mwana wake.

Kazi ya Usimamizi wa Mungu na Wokovu wa Wanadamu Yaanza na Ibrahimu Kumtoa Isaka

Baada ya kumpa Ibrahimu mwana, maneno ambayo Mungu alikuwa ametamka kwa Ibrahimu yakawa yametimizwa. Hii haimaanishi kwamba mpango wa Mungu uliishia hapa; kinyume cha mambo ni kwamba, mpango adhimuwa Mungu wa usimamizi na wokovu wa wanadamu ndio ulikuwa tu umeanza, na baraka Yake ya mwana kwa Ibrahimu ilikuwa tu ni utangulizi wa mpango wa usimamizi Wake kwa ujumla. Wakati huo, ni nani aliyejua kwamba vita vya Mungu na Shetani vilikuwa vimeanza kimya kimya wakati Ibrahimu alipomtoa Isaka?

Mungu Hajali Kama Binadamu Ni Mjinga—Anahitaji Tu Binadamu Awe Mkweli

Kisha, hebu tuangalie kile Mungu alimfanyia Ibrahimu. Ukiangalia Mwanzo 22:2, Mungu alimtolea Ibrahimu amri ifuatayo: “Umchukue mwana wako sasa, mwana wako wa pekee Isaka, unayempenda, na uende hadi nchi ya Moria; na huko umtoe kwa sadaka ya kuteketezwa juu ya mojawapo ya milima ambayo nitakuambia.” Maana ya Mungu ilikuwa wazi: Alikuwa akimwambia Ibrahimu amtoe mtoto wake wa pekee Isaka, ambaye alimpenda, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa. Tukiiangalia amri ya Mungu leo, je ingali inakinzana na dhana za binadamu? Ndiyo! Kile alichokifanya Mungu wakati huo ni kinyume sana na dhana za binadamu na hakieleweki kwa binadamu. Katika dhana zao, watu husadiki yafuatayo: Wakati binadamu hakusadiki, na akafikiria ni jambo lisilowezekana, Mungu Alimpa mwana, na baada ya kumpata mwana, Mungu alimhitaji amtoe mwana wake sadaka—jambo la ajabu kweli! Mungu kwa hakika alinuia kufanya nini? Kusudio la kweli la Mungu lilikuwa ni nini? Alimpa Ibrahimu mtoto bila masharti yoyote, ilhali pia Alimwomba Ibrahimu aweze kutoa bila masharti. Maji yalikuwa yamezidi unga? Kwa mtazamo wa mtu wa pembeni, hapa maji hayakuwa tu yamezidi unga lakini pia ilikuwa kwa kiasi fulani hali ya “kuunda tatizo pasipo na tatizo.” Lakini Ibrahimu mwenyewe hakusadiki kwamba Mungu alikuwa akihitaji kupita kiasi. Ingawa alikuwa na wasiwasi fulani, na alimshuku kidogo Mungu, alikuwa tayari bado kumtoa mtoto wake. Wakati huu, ni nini unachoona ambacho kinathibitisha kuwa Ibrahimu alikuwa radhi kumtoa mtoto wake? Ni nini kinazungumzwa kwenye sentensi hizi? Maandishi asilia yanaelezea yafuatayo: “Naye Ibrahimu akaamka asubuhi mapema, na kuweka tandiko kwa punda wake, akawachukua vijana wake wawili pamoja naye, naye Isaka mwana wake, na akapasua kuni kwa sababu ya hiyo sadaka ya kuteketezwa, na akaondoka, na kuenda pahali ambapo alikuwa ameambiwa na Mungu” (Mwa 22:3). “Na wakafika pahali hapo ambapo Mungu alikuwa amemwambia; naye Ibrahimu akajenga madhabahu hapo, na kuziweka kuni kwa mpango, na kumfunga Isaka mwana wake, naye akamlaza juu ya madhabahu kwa zile kuni. Na Ibrahimu akanyosha mbele mkono wake, na kukichukua kisu ili amchinje mwana wake” (Mwa 22:9-10). Wakati Ibrahimu alipounyosha mkono wake na kukichukua kisu ili amchinje mwanawe, je, Mungu aliviona vitendo vyake? Naam aliviona. Mchakato wote—kuanzia mwanzo, wakati Mungu alipomwomba Ibrahimu kumtoa Isaka, hadi pale ambapo Ibrahimu alikiinua kisu chake ili amchinje mtoto wake—hilo lilimwonyesha Mungu moyo wa Ibrahimu, na haijalishi kuhusu ujinga wake wa awali, kutojua kwake, na kutomwelewa Mungu kwake, wakati huo moyo wa Ibrahimu kwa Mungu ulikuwa wa kweli, na wenye uaminifu, na kwa kweli alikuwa akienda kumrudisha Isaka, mtoto aliyepewa yeye na Mungu, ili arudi kwa Mungu. Ndani yake, Mungu aliuona utiifu, utiifu uleule ambao Yeye alitamani.

Kwa binadamu, Mungu hufanya mengi yasiyoeleweka na yaliyo ya ajabu. Wakati Mungu anapotaka kumpangia mtu, mpango huu mara nyingi unakinzana na dhana za binadamu, na huwa haueleweki kwa binadamu huyo, ilhali ni kutokuelewana na kutokueleweka huku ndiko majaribio ya Mungu na mtihani Wake kwa binadamu. Ibrahimu, huku haya yakiendelea, aliweza kuonyesha utiifu kwa Mungu uliokuwa ndani yake, jambo ambalo ndilo lililokuwa sharti muhimu zaidi la yeye kuweza kutosheleza mahitaji ya Mungu. Ni wakati huo tu Ibrahimu alipoweza kutii mahitaji ya Mungu, alipomtoa Isaka ndipo Mungu Alipohisi kwa kweli utulivu na kukubaliwa na wanadamu—na Ibrahimu, ambaye Alikuwa amemchagua. Hapo tu ndipo Mungu alipokuwa na uhakika kwamba mtu huyu Aliyekuwa amemchagua Yeye alikuwa kiongozi muhimu ambaye angetekeleza ahadi Yake na mpango Wake wa usimamizi wa baadaye. Ingawa lilikuwa tu jaribio na mtihani, Mungu alihisi kuridhika, Alihisi upendo wa mwanadamu Kwake Yeye, na Alihisi akiwa ametulizwa na binadamu kwa mara ya kwanza. Wakati Ibrahimu alipokiinua kisu chake ili amchinje Isaka, Mungu alimzuia? Mungu hakumruhusu Ibrahimu amtoe Isaka sadaka, kwani Mungu hakuwa na nia yoyote ya kumtoa uhai Isaka. Hivyo, Mungu alimsimamisha Ibrahimu kwa wakati mwafaka. Kwake Mungu, utiifu wa Ibrahimu ulikuwa tayari umepita mtihani, kile alichofanya kilitosha, naye Mungu tayari alikuwa ameona matokeo ya kile Alichokuwa amenuia kufanya. Je, matokeo haya yalimtosheleza Mungu? Inaweza kusemwa kwamba matokeo haya yalikuwa ya kuridhisha kwa Mungu, na kwamba ndiyo ambayo Mungu aliyataka, na ndiyo ambayo Mungu alikuwa ametamani kuyaona. Je, hili ni kweli? Ingawa, katika mazingira tofauti, Mungu hutumia njia tofauti za kumjaribu kila mtu. Kwa Ibrahimu Mungu aliona kile Alichotaka, Aliona kwamba moyo wa Ibrahimu ulikuwa wa kweli, na kwamba utiifu wake haukuwa na masharti na ilikuwa hali hii hasa ya “kutokuwa na masharti” ambayo Mungu alitamani. Watu mara nyingi husema, tayari nimetoa hii, tayari nimeacha kile—kwa nini bado Mungu hajatosheka na mimi? Kwa nini Anaendelea kuniweka katika majaribio? Kwa nini Anaendelea kunijaribu? Hii inadhihirisha ukweli mmoja: Mungu bado hajauona moyo wako, na bado Hajaupata moyo wako. Hivi ni kusema, Hajauona uaminifu kama wa wakati ule ambao Ibrahimu aliweza kukiinua kisu chake ili kumchinja mtoto wake kwa mkono wake mwenyewe na kumtoa kwa Mungu. Bado Hajauona utiifu wako usio na masharti, na hajatulizwa na wewe. Basi, ni kawaida, kwamba Mungu anaendelea kukujaribu. Je, haya si kweli? Tutaachia hapa kwa mada hii. Halafu, tutasoma “Ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu.”

3. Ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu

Mwa 22:16-18 Mimi nimeapa kujipitia, akasema Yehova, kwa maana umefanya jambo hili, na hujamzuilia mwana wako, mwana wako wa pekee: Kuwa katika kubariki nitakupa baraka, na katika kuzidisha uzao wako nitazidisha mithili ya nyota za mbinguni, na mithili ya mchanga uliopo kwenye ukanda wa pwani; na uzao wako utakuwa na mlango wa maadui zao; Na kupitia uzao wako kila taifa la dunia litabarikiwa; kwa sababu umeitii sauti Yangu.

Huu ni ukamilifu wa maelezo ya baraka za Mungu kwa Ibrahimu. Ingawaje ni fupi, maudhui yake ni mengi: Yanajumuisha sababu ya, na usuli wa, zawadi ya Mungu kwa Ibrahimu, na kile ambacho Alimpa Ibrahimu. Pia imejaa mhemko wa furaha na msisimko Aliotumia Mungu kutamka maneno haya, pamoja na haraka ya tamanio Lake la kuwapata wale wanaoweza kusikiliza maneno Yake. Katika haya, tunaona upendo wa Mungu, na wema Wake kwa, wale wanaotii maneno Yake na kufuata amri Zake. Hivyo, pia, tunaiona gharama Anayolipia ili kupata watu, na utunzaji na fikira Anazotumia kuweza kuwapata. Zaidi ya hayo, kifungu hicho, kilicho na maneno “Mimi nimeapa kujipitia,” kinatupa hisia yenye nguvu ya uchungu na maumivu Aliyoyapitia Mungu na Mungu peke yake nyuma ya pazia la kazi hii ya mpango Wake wa usimamizi. Ni kifungu chenye kuchochea fikira, na ambacho kilishikilia umuhimu maalum, na kuwa na athari kubwa kwa wale waliofuata baadaye.

Binadamu Anapata Baraka za Mungu kwa Sababu ya Uaminifu na Utii Wake

Je, baraka aliyopewa Ibrahimu na Mungu tuliyoisoma hapa ni kubwa? Ilikuwa kubwa kiasi gani? Kunayo sentensi moja muhimu hapa: “Na kupitia uzao wako mataifa yote ya dunia yatabarikiwa,” ambayo inaonyesha kwamba Ibrahimu alizipokea baraka ambazo hazikuwahi kutolewa kwa yeyote aliyekuwepo kabla au baada. Wakati, alipoulizwa na Mungu, Ibrahimu alimrejesha mwana wake wa pekee—mtoto wake pekee wa kiume na mpendwa Isaka—kwa Mungu (hapa hatuwezi kutumia neno “alimtoa sadaka”; tunafaa kusema alimrejesha mtoto wake kwa Mungu), sio tu kwamba Mungu hakumruhusu Ibrahimu amtoe Isaka, lakini pia Alimbariki. Ni kwa ahadi gani Alimbariki Ibrahimu? Ahadi ya kuzidisha uzao wake. Na walizidishwa mara ngapi? Maandiko yanatuelezea rekodi hii: “... mithili ya nyota za mbinguni, na mithili ya mchanga uliopo kwenye ukanda wa pwani; na uzao wako utakuwa na mlango wa maadui zao; Na kupitia uzao wako kila taifa la dunia litabarikiwa.” Mungu Aliyatamka maneno haya katika muktadha upi? Hivi ni kusema, ni vipi ambavyo Ibrahimu alizipokea baraka za Mungu? Alizipokea kama vile tu Mungu anavyosema kwenye maandiko: “kwa sababu umeitii sauti Yangu.” Yaani, kwa sababu Ibrahimu alikuwa amefuata amri ya Mungu, kwa sababu alikuwa amefanya kila kitu ambacho Mungu alikuwa amesema, Alichohitaji na kuamuru bila ya malalamiko hata kidogo, hivyo Mungu akatoa ahadi hiyo kwake. Kuna sentensi moja muhimu katika ahadi hii ambayo inagusia fikira za Mungu wakati huo. Je, mmeiona? Huenda hamkutilia maanani sana maneno ya Mungu kwamba “Mimi nimeapa kujipitia.” Yale yanamaanisha ni kwamba, wakati Mungu alipoyatamka maneno haya, Alikuwa anajiapisha Mwenyewe. Watu huapa kupitia niniwakati wanapokula kiapo? Wanaapa kwa Mbingu, hivi ni kusema, wanakula kiapo kwa Mungu na kuapa kwa Mungu. Huenda watu wasiwe na uelewa mwingi wa hali hiyo ambayo Mungu Alijiapisha mwenyewe, lakini mtaweza kuelewa Nitakapowapatia maelezo sahihi. Alipokabiliana na mtu ambaye aliweza tu kuyasikia maneno Yake lakini hakuuelewa moyo Wake kwa mara nyingine kulimfanya Mungu kujihisi mpweke na mwenye upungufu. Katika hali ya kukata tamaa—na, yaweza kusemwa, bila kujijua—Mungu alifanya jambo la kawaida sana: Mungu aliweka mkono Wake juu ya moyo Wake na kujisemea Mwenyewe wakati alipokuwa Akimpa Ibrahimu ahadi hii, na kutokana na haya binadamu akamsikia Mungu akisema “Mimi nimeapa kujipitia.” Kupitia vitendo vya Mungu, unaweza kujifikiria wewe mwenyewe. Unapoweka mkono wako juu ya moyo wako, na kujizungumzia, je, una wazo la wazi kwa kile unachokisema? Je, mtazamo wako ni wenye uaminifu? Je, unazungumza kwa uwazi, kutoka kwenye moyo wako? Kwa hivyo, tunaona hapa kwamba Mungu alipozungumza na Ibrahimu, Alikuwa mkweli na mwaminifu. Wakati huohuo alipokuwa Akizungumza na Ibrahimu na kumbariki, Mungu alikuwa pia Akijizungumzia Mwenyewe. Alikuwa Akijiambia: Nitambariki Ibrahimu na kuuzidisha uzao wake kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani, kwa sababu alitii maneno Yangu na ndiye Niliyemchagua. Wakati Mungu aliposema “Mimi nimeapa kujipitia,” Mungu Aliamua kwamba ndani ya Ibrahimu Angetoa wateule wa Israeli, na baadaye Angewaongoza watu hawa kusonga mbele sambamba na kazi Yake. Yaani, Mungu angekifanya kizazi cha Ibrahimu kubeba kazi ya usimamizi wa Mungu, na kazi ya Mungu na ile iliyoonyeshwa na Mungu ingeanza na Ibrahimu, na kuendelea katika vizazi vya Ibrahimu, na hivyo kutambua nia ya Mungu ya kumwokoa mwanadamu. Mnasemaje, hiki si kitu kilichobarikiwa? Kwa binadamu, hakuna baraka kubwa zaidi kuliko hii; hii, inaweza kusemwa, ndiyo baraka kubwa zaidi. Baraka aliyopata Ibrahimu haikuwa kuzidishwa kwa uzao wake, lakini ilikuwa Mungu kutimiza usimamizi Wake, agizo Lake na kazi Yake kwa vizazi vya Ibrahimu. Hii inamaanisha kwamba baraka alizopata Ibrahimu hazikuwa za muda mfupi, lakini ziliendelea kwa kadri mpango wa usimamizi wa Mungu ulivyoendelea. Wakati Mungu alipoongea, wakati Mungu alipoapa kwa nafsi Yake Mwenyewe, tayari Alikuwa ameamua. Je, mchakato wa uamuzi huu ulikuwa wa kweli? Ulikuwa halisi? Mungu aliamua kwamba, kuanzia wakati huo na kuendelea, jitihada Zake, gharama Aliyolipia, kile Anacho na alicho, kila kitu Chake, na hata maisha Yake yangekabidhiwa kwaIbrahimu na vizazi vya Ibrahimu. Na ndivyo pia Mungu alivyoamua kwamba, kuanzia kwenye kundi hili la watu, Angedhihirisha matendo Yake, na kumruhusu binadamu kuiona hekima, mamlaka na nguvu Yake.

Kuwapata Wale Wanaomjua Mungu na Wanaoweza Kumshuhudia Ndilo Tamanio la Mungu Lisilobadilika

Wakati huohuo Alipokuwa akijizungumzia Mwenyewe, Mungu alizungumza pia na Ibrahimu, lakini mbali na kusikiliza baraka ambazo Mungu alimpa, je, Ibrahimu aliweza kuelewa nia ya kweli ya Mungu katika maneno Yake yote wakati huo? Hakuweza! Na hivyo, kwa wakati huo, Mungu alipoapa kwa nafsi Yake Mwenyewe, moyo Wake ulikuwa bado mpweke na wenye huzuni. Hakukuwepo hata na mtu mmoja wa kuweza kuelewa au kufahamu kile Alichonuia na Alichopangilia. Wakati huo, hakuna—akiwemo Ibrahimu—aliyeweza kuongea na Yeye kwa ujasiri, isitoshe hakuna yule aliyeweza kushirikiana na Yeye katika kufanya kazi ambayo lazima Angefanya. Kwa juu juu, Mungu alikuwa Amempata Ibrahimu na Alipata mtu ambaye angetii maneno Yake. Lakini kwa hakika, maarifa ya mtu huyu kuhusu Mungu yalikuwa kidogo mno. Hata ingawa Mungu alikuwa amembariki Ibrahimu, moyo wa Mungu ulikuwa bado hujatosheka. Je, inamaanisha nini kwamba Mungu hakuwa ametosheka? Inamaanisha kwamba usimamizi Wake ulikuwa tu umeanza, inamaanisha kwamba watu Aliotaka kuwapata, watu Aliotamani kuwaona, watu Aliowapenda, walikuwa bado mbali na Yeye; Alihitaji muda, Alihitaji kusubiri, Alihitaji kuwa na subira. Kwani kwa wakati huo, mbali na Mungu Mwenyewe, hakuna yeyote yule aliyejua kile Alichohitaji au kile Alichotaka kupata, au kile Alichotamani. Na hivyo basi, Kwa wakati huo huo aliokuwa akihisi sana furaha Mungu pia alihisi kuwa mwenye uzito wa moyo. Hata hivyi, Hakusitisha hatua Zake, na Aliendelea kupanga hatua inayofuata ya kile ambacho lazima Afanye.

Mnaona nini katika ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu? Mungu alimpa baraka kuu Ibrahimu kwa sababu tu alitii maneno ya Mungu. Ingawa, kwa juu juu, hili linaonekana kuwa jambo la kawaida na bila shaka, ndani yake tunauona moyo wa Mungu: Mungu hasa anathamini utiifu wa mwanadamu Kwake, na anathamini uelewa wa mwanadamu Kwake na uaminifu wake Kwake. Je, Mungu anathamini kwa kiasi gani uaminifu huu? Huenda msielewe ni kiasi kipi ambacho Yeye Anauthamini, na huenda hata kusiwe na yeyote anayeutambua. Mungu alimpa Ibrahimu mwana, na wakati mwana huyo alipokua, Mungu alimhitajiIbrahimu amtoe mwanaweKwake. Ibrahimu alifuata amri ya Mungu kwa umakinifu, alitii neno la Mungu na uaminifu wake ulimpendeza Mungu na ukathaminiwa sana na Mungu. Mungu aliuthamini kwa kiasi gani? Na kwa nini Akauthamini sana? Kwa wakati ambao hakuna aliyefahamu maneno ya Mungu au kuuelewa moyo Wake, Ibrahimu alifanya kitu kilichotikisa mbingu na kutetemesha ardhi, na kikafanya Mungu kuhisi hali fulani ya kutosheka kwa mara ya kwanza, kikamletea Mungu furaha ya kumpata mtu ambaye aliweza kutii maneno Yake. Kutosheka na furaha hii ilitoka kwa kiumbe aliyeumbwa kwa mikono ya Mungu, na ndiyo iliyokuwa “sadaka” ya kwanza ambayo binadamu aliwahi kumpa Mungu na ambayo ilithaminiwa sana na Mungu, tangu binadamu kuumbwa. Mungu alikuwa na wakati mgumu kuisubiria sadaka hii, na Aliichukulia kama zawadi ya kwanza muhimu zaidi kutoka kwa binadamu, ambaye Alikuwa amemuumba. Hii ilimwonyesha Mungu tunda la kwanza la jitihada Zake, na gharama ambayo Alikuwa amelipia na ikamruhusu Yeye kuliona tumaini kwa wanadamu. Baadaye, Mungu alikuwa na hata tamanio kubwa zaidi la kundi la watu kama hao wa kuwa karibu na Yeye, wakimtendea Yeye kwa uaminifu, wakimjali Yeye kwa uaminifu. Mungu alitamani hata kwamba Ibrahimu angeendelea kuishi, kwani Alipenda kuwa na moyo kama huo wa Ibrahimu ukiandamana na Yeye na kuwa na Yeye Alipoendelea na usimamizi Wake. Haijalishi ni nini alichotaka Mungu, ilikuwa ni tamanio tu, wazo tu—kwani Ibrahimu alikuwa tu binadamu aliyeweza kumtii Yeye, na wala hakuwa na uelewa au maarifa hata madogo zaidi kuhusu Mungu. Ibrahimu alikuwa mtu ambaye alipungukiwa sana na viwango vya mahitaji ya Mungu kwa mwanadamu, ambavyo ni: kumjua Mungu, kuwa na uwezo wa kumshuhudia Mungu, na kuwa na nia moja na Mungu. Na hivyo, hangeweza kutembea na Mungu. Katika sadaka ya Ibrahimu ya Isaka, Mungu aliuona uaminifu na utiifu huu wa Ibrahimu, na Akaona kwamba alikuwa amestahimili mtihani wa Mungu kwake. Hata ingawa Mungu aliukubali uaminifu na utiifu wake, bado hakustahili kuwa mwandani wa Mungu, kuwa mtu ambaye alimjua na kumwelewa Mungu, na mtu ambaye alifahamishwa kuhusu tabia ya Mungu; alikuwa mbali sana na kuwa na akili sawa na Mungu na vilevile kuweza kufanya mapenzi ya Mungu. Hivyo basi, katika moyo Wake, Mungu alikuwa bado mpweke na mwenye wasiwasi. Kadiri Mungu alivyokuwa mpweke na mwenye wasiwasi zaidi, ndivyo Alivyohitaji zaidi kuendelea na usimamizi Wake haraka iwezekanavyo, na kuweza kuchagua na kulipata kundi la watu wa kukamilisha mpango Wake wa usimamizi na kutimiza mapenzi Yake haraka iwezekanavyo. Hili ndilo lilikuwa tamanio alilolitaka Mungu ambalo halijabadilika tangu mwanzo hadi sasa. Tangu Alipomuumba binadamu hapo mwanzo, Mungu ametamani kuwa na kundi la washindi, kundi ambalo litatembea na Yeye na linaweza kuelewa, kujua na kufahamu tabia Yake. Nia hii ya Mungu haijawahi kubadilika. Haijalishi ni kwa muda gani bado Atasubiria, haijalishi njia iliyo mbele ni ngumu kiasi gani, hata malengo Anayoyatamani yawe mbali kiasi kipi, Mungu hajawahi kubadilisha au kukata tamaa katika matarajio Yake kuhusu binadamu. Sasa kwa kuwa nimeyasema haya, je, mnatambua chochote kuhusu mapenzi ya Mungu? Pengine kile ulichotambua si cha kina sana—lakini kitajitokeza polepole!

Katika kipindi kile kile Ibrahimu akiwepo, Mungu pia aliliangamiza jiji. Jiji hili liliitwa Sodoma. Bila shaka, watu wengi wanaijua hadithi ya Sodoma, lakini hakuna yeyote aliyejua fikira za Mungu zilizokuwa nyuma ya kuangamiza Kwake jiji hili.

Na hivyo leo, kupitia mazungumzo ya Mungu na Ibrahimu hapa chini, tutajifunza fikira Zake wakati huo, huku pia tukijifunza kuhusu tabia Yake. Kinachofuata, hebu tusome vifungu vya maandiko.

B. Mungu Lazima Aangamize Sodoma

Mwa 18:26 Na Yehova akasema, Nikipata katika Sodoma watu hamsini wenye haki ndani ya mji huo, basi nitapaacha pahali pote kwa sababu yao.

Mwa 18:29 Na akanena tena na Yeye, na kusema, Huenda watu arobaini wakapatikana humo. Naye Akasema, Sitafanya hivyo kwa sababu yao.

Mwa 18:30 Na akamwambia, Huenda watapatikana huko watu thelathini. Naye Akasema, Sitafanya hivyo kwa sababu yao.

Mwa 18:31 Na akasema, Huenda watapatikana huko watu ishirini. Naye Akasema, Sitauharibu kwa sababu yao.

Mwa 18:32 Na akasema, Huenda watapatikana huko watu kumi. Naye Akasema, Sitauharibu kwa sababu yao.

Hizi ni dondoo chache Nilizochagua kutoka kwenye Biblia. Dondoo hizi hazijakamilika kwa matoleo ya awali. Kama mngependa kuziona hizo, mnaweza kuzitafuta kwenye Biblia nyinyi wenyewe; ili kuokoa muda, Nimeondo sehemu ya maudhui kutoka kwenye maudhui halisi. Hapa Nimechagua tu vifungu na sentensi mbalimbali zenye umuhimu, huku nikiziacha sentensi mbalimbali ambazo hazina umuhimu katika ushirika wetu wa leo. Katika vifungu na maudhui yote tunayotumia katika ushirika, zingatio letu haliyaendei maelezo ya hadithi na mwenendo wa binadamu katika hadithi hizi; badala yake, tunazungumzia tu fikira za Mungu na mawazo Yake yalikuwa ni yapi kwa wakati huo. Katika fikira na mawazo ya Mungu, tutaiona tabia ya Mungu, na kutoka katika kila kitu alichofanya Mungu, tutaweza kumuona Mungu Mwenyewe wa kweli—na katika haya tutaweza kutimiza malengo yetu.

Mungu Anawajali tu Wale Wanaoweza Kutii Maneno Yake Na Kufuata Amri Zake

Vifungu hivi vilivyotajwa hapo juu vina maneno kadhaa muhimu: hizo nambari. Kwanza kabisa, Yehova alisema kwamba kama Angewapata wenye haki hamsini ndani ya Jiji, basi Angepanusurisha mahali hapo, hii ni kusema, Asingeangamiza jiji hilo. Hivyo walikuwepo, kwa hakika, wenye haki hamsini ndani ya Sodoma? Hawakuwemo. Muda mfupi baadaye, Ibrahimu alimwambia nini Mungu? Alisema, huenda watakuwepo arubaini waliopatikana humo? Naye Mungu akasema, Sitafanya hivyo. Kisha, Ibrahimu akasema huenda wakawepo thelathini watakaopatikana huko? Naye Mungu akasema, Sitafanya hivyo. Na labda ishirini? Sitafanya hivyo. Kumi, je? Sitafanya hivyo. je, kulikuwa kweli, na watu kumi wenye haki nani ya jiji hilo? Hapakuwa kumi—lakini kulikuwemo na mmoja. Na huyu mmoja alikuwa nani? Alikuwa Lutu. Wakati huo, kulikuwepo tu na mwenye haki mmoja huko Sodoma, lakini je, Mungu alikuwa amemakinika sana au kuwa na mahitaji makubwa kuhusiana na nambari hii? La, hakuwa hivyo! Na wakati binadamu aliendelea kuuliza, “Je, wakiwemo arubaini?” “Je wakiwemo thelathini?” mpaka alipofikia “Je, wakiwemo kumi?” Mungu alisema, “Hata kama wangalikuwemo kumi tu, Nisingeangamiza jiji hilo; Ningelinusurisha, na kuwasamehe wale watu wengine mbali na wale kumi.” Idadi ya watu kumi ingekuwa ya kuhurumiwa vya kutosha, lakini ilitokea kwamba, kwa hakika, hakukuwemo na hata ile idadi inayohitajika ya watu wenye haki kule Sodoma. Unaona, basi, kwamba katika macho ya Mungu dhambi na maovu ya watu wa jiji hilo yalikuwa kwa kiasi kwamba Mungu hakuwa na chaguo lolote ila kuwaangamiza. Je, Mungu alimaanisha nini Aliposema kwamba Asingeliharibu jiji kama kungekuwemo na wenye haki hamsini? Nambari hizi hazikuwa muhimu kwa Mungu. Kile kilichokuwa muhimu kilikuwa kama jiji lilikuwa na wenye haki ambao Yeye aliwataka. Ikiwa jiji hilo lingekuwa na mtu mmoja tu mwenye haki, Mungu asingeruhusu madhara yampate kutokana na Yeye kuangamiza jiji hilo. Kile ambacho haya yote yanamaanisha ni kwamba, haijalishi kama Mungu angeliangamiza jiji au la, na haijalishi idadi ya wenye haki waliokuwa ndani ya jiji hilo, kwake Mungu jiji hili lenye dhambi lilikuwa limelaaniwa na lilikuwa limejaa maovu, na hivyo lilifaa kuangamizwa, na kutoweka kwenye macho ya Mungu huku nao wenye haki wakisali. Haijalishi ni enzi gani, haikujalishi ni hatua gani ya maendeleo ya wanadamu, mtazamo wa Mungu haubadiliki: Anachukia maovu, na Anawajali wenye haki mbele ya macho Yake. Mtazamo huu wa wazi wa Mungu ndiyo pia ufunuo wa kweli wa kiini cha Mungu. Kwa sababu hakukuwepo na mwenye haki yeyote isipokuwa mmoja ndani ya jiji, Mungu hakusita tena. Matokeo yake ni kwamba Sodoma isingeepuka kuangamizwa bila kusita. Mnaona nini katika haya? Katika enzi hiyo, Mungu asingeangamiza jiji kama wamo wenye haki hamsini ndani yake, wala kama kulikuwemo kumi, kumaanisha kwamba Mungu angeamua kuwasamehe na kuwavumilia wanadamu, au Angefanya kazi ya kuwaongoza, kwa sababu ya watu wachache ambao waliweza kumstahi na kumwabudu Yeye. Mungu hutilia maanani matendo yahaki ya binadamu, Hutilia maanani sana kwa wale wanaoweza kumwabudu Yeye, na Anatilia maanani sana wale wanaoweza kufanya matendo mema mbele yake.

Tangu nyakati za awali hadi leo, je, umewahi kusoma ndani ya Biblia kuhusu Mungu kuuwasilisha ukweli, au kuzungumzia kuhusu njia ya Mungu, kwa mtu yeyote? La, hujawahi. Maneno ya Mungu kwa binadamu tunayoyasoma yaliwaambia watu tu cha kufanya. Baadhi walienda na wakayafanya, baadhi hawakuyafanya; baadhi waliyaamini, na baadhi hawakuyaamini, na baadhi hawakusadiki. Hivyo ndivyo ilivyokuwa tu. Hivyo, wenye haki wa enzi hiyo—wale waliokuwa wenye haki machoni pa Mungu—walikuwa wale tu ambao wangeweza kuyasikia maneno ya Mungu na kufuata amri za Mungu. Walikuwa watumishi waliotekeleza maneno ya Mungu miongoni mwa binadamu. Je, watu kama hao wangeweza kuitwa wale wanaomjua Mungu? Je, wangeweza kuitwa watu waliofanywa wakamilifu na Mungu? La, wasingeweza kuitwa hivyo. Na hivyo, licha ya idadi yao, machoni pa Mungu watu hawa wenye haki walistahili kuitwa wandani wa Mungu? Wangeweza kuitwa mashahidi wa Mungu? Hakika sivyo! Kwa hakika hawakustahili kuitwa wandani na mashahidi wa Mungu. Kwa hivyo, Mungu aliwaitaje watu kama hao? Katika Agano la Kale la Biblia, kuna matukio mengi ya Mungu kuwaita “mtumishi Wangu.” Hivyo ni kusema, kwa wakati huo, machoni pa Mungu watu hawa wenye haki walikuwa watumishi wa Mungu, walikuwa watu waliomhudumia Yeye duniani. Na ni kwa jinsi gani Mungu alifikiria kuhusu jina hilo? Kwa nini Akawaita hivyo? Je, Mungu anavyo viwango ambavyo Anatumia katika Kuwaita watu ndani ya moyo Wake? Bila shaka Anavyo. Mungu anavyo viwango, haijalishi kama Anawaita watu wenye haki, wakamilifu, wanyofu, au watumishi. Anapomwita mtu mtumishi Wake, Anayo imani thabiti kwamba mtu huyu anaweza kuwapokea wajumbe Wake, na anaweza kufuata amri Zake, na anaweza kutekeleza kile ambacho ameamrishwa kufanya na wale wajumbe. Na mtu huyu anatekeleza nini? Anatekeleza kile ambacho Mungu anamwamuru binadamu kufanya na kutekeleza duniani. Kwa wakati huo, je, kile ambacho Mungu alimhitaji mwanadamu afanye na kutekeleza duniani kingeweza kuitwa njia ya Mungu? La, kisingeweza. Kwani kwa wakati huo, Mungu alihitaji tu kwamba mwanadamu kufanya mambo machache rahisi; Alitamka amri chache rahisi, Akimwambia binadamu afanye hiki au kile, na si zaidi ya hayo. Mungu alikuwa akifanya kazi kulingana na mpango Wake. Kwa sababu, kwa wakati huo, masharti mengi hayakuwepo, muda ulikuwa haujatimia, na ilikuwa vigumu kwake wanadamu kuvumilia njia ya Mungu, hivyo basi njia ya Mungu ilikuwa bado haijaanza kuwasilishwa mbele kutoka kwenye moyo wa Mungu. Katika haya, tunaona kwamba haijalishi kama walikuwa thelathini au ishirini kati ya wale wenye haki aliowazungumzia Mungu, mchoni Pake wote walikuwa watumishi Wake. Wakati wajumbe wa Mungu walipowajia watumishi hawa, wangeweza kuwapokea, na kufuata amri zao, na kutenda kulingana na maneno yao. Haya ndiyo hasa yaliyofaa kufanywa, na kutimizwa, na wale waliokuwa watumishi machoni Pake Mungu. Mungu ni mwenye busara katika majina Yake kwa watu. Hakuwaita watumishi Wake kwa sababu walikuwa kama mlivyo sasa —kwa sababu walikuwa wamesikia mahubiri mengi, walijua kile ambacho Mungu alifaa kufanya, walielewa mengi kuhusu mapenzi ya Mungu na walifahamu mpango Wake wa usimamizi—lakini na kwa sababu walikuwa waaminifu katika ubinadamu wao na waliweza kutii maneno ya Mungu; wakati Mungu alipowaamuru, waliweza kuweka pembeni kile walichokuwa wakifanya na kutekeleza kile ambacho Mungu aliwaamuru kufanya. Kwa hivyo, kwa Mungu, maana nyingine katika kuita mtumishi ni kwamba walishirikiana na kazi Yake duniani na ingawaje hawakuwa wajumbe wa Mungu, hao ndio waliokuwa watekelezaji na wafuatiliaji wa maneno ya Mungu duniani. Unaona, basi, watumishi hawa au wenye haki hawa walikuwa na umuhimu mkubwa katika moyo wa Mungu. Kazi ile ambayo Mungu alifaa kuishughulikia duniani isingeweza kufanyika bila ya watu wa kushirikiana na Yeye, na wajibu uliotekelezwa na watumishi wa Mungu usingeweza kufanywa na wajumbe wa Mungu. Kila kazi ambayo Mungu alitoa amri kwa watumishi hawa ilikuwa yenye umuhimu mkubwa Kwake, na hivyo basi Asingeweza kuwapoteza. Bila ya ushirikiano wa watumishi hawa na Mungu, kazi Yake miongoni mwa wanadamu ingefikia kikomo, na matokeo yake ni kwamba mpango wa usimamizi wa Mungu na matumaini ya Mungu vyote visingewezekana.

Mungu ni Mwenye Wingi wa Rehema Kwa Wale Anaowajali, na Mwenye Ghadhabu kwa Wale Anaowachukia na Kuwakataa

Katika simulizi za Biblia, je, kulikuwepo na watumishi kumi wa Mungu huko Sodoma? Hapana, hakukuwepo! Je, jiji hilo lilistahili kuhurumiwana Mungu? Ni mtu mmoja tu katika jiji hilo—Lutu—ndiye aliye wapokea wajumbe wa Mungu. Maana ya jambo hili ni kwamba kulikuwa na mtumishi mmoja tu wa Mungu katika jiji hilo, na hivyo basi Mungu hakuwa na chaguo ila kumwokoa Lutu na kuliangamiza jiji la Sodoma. Mazungumzo haya kati ya Ibrahimu na Mungu yanaweza kuonekana kuwa rahisi tu, lakini yanaonyesha ni jambo la kina sana: Kuna kanuni za vitendo vya Mungu, na kabla ya kufanya uamuzi Atachukua muda mrefu akiangalia na kutafakari; kwa hakika Hatafanya maamuzi yoyote au kufikia hitimisho lolote kabla ya wakati muafaka. Mazungumzo kati ya Ibrahimu na Mungu yanatuonyesha kwamba uamuzi wa Mungu wa kuangamiza Sodoma haukuwa mbaya hata kidogo, kwani Mungu alijua tayari kwamba kwenye jiji hakukuwa na watu arubaini wenye haki, na wala thelathini wenye haki, wala ishirini. Hawakuwepo hata kumi. Mtu mwenye haki pekee kwenye jiji alikuwa Lutu. Yote yaliyofanyika ndani ya Sodoma na hali zake ziliangaliwa na Mungu, na yalifahamika kwa Mungu kama sehemu ya nyuma ya mkono Wake. Hivyo, uamuzi Wake usingekosa kuwa sahihi. Kinyume na haya, tukilinganisha uweza wa Mungu, binadamu hajali katu, ni mpumbavu na mjinga sana, asiyejua mambo mengi, asiyeona mbali katu. Haya ndiyo tunayoona katika mazungumzo kati ya Ibrahimu na Mungu. Mungu amekuwa akiwasilisha tabia Yake kuanzia mwanzo hadi leo. Hapa, vilevile, kuna tabia ya Mungu pia tunayofaa kuona. Nambari ni rahisi, na hazionyeshi chochote, lakini hapa kuna maonyesho muhimu sana ya tabia ya Mungu. Mungu asingeangamiza jiji kwa sababu ya watu hamsini wenye haki. Je, hii ni kwa sababu ya huruma za Mungu? Ni kwa sababu ya upendo na uvumilivu Wake? Je mmeuona upande huu wa tabia ya Mungu? Hata kama kungekuwa na wenye haki kumi pekee, Mungu asingeangamiza jiji hili kwa sababu ya watu hawa kumi wenye haki. Je, haya yanaonyesha uvumilivu na upendo wa Mungu au la? Kwa sababu ya rehema, uvumilivu, na kujali kwa Mungu kwa wale watu wenye haki, Asingeliangamiza jiji hilo. Huu ndio uvumilivu wa Mungu. Na hatimaye, ni matokeo gani tunayoyaona? Wakati Ibrahimu aliposema, “Huenda watapatikana huko watu kumi,” Mungu akasema, “Sitauharibu kwa sababu yao.” Baada ya hapo, Ibrahimu hakusema tena—kwani ndani ya Sodoma hakukuwa na wenye haki kumi aliowarejelea, na hakuwa na la kusema zaidi, na kwa wakati huo alielewa ni kwa nini Mungu alikuwa ameamua kuangamiza Sodoma. Katika haya, ni tabia gani ya Mungu unayoiona? Je, Mungu alifanya azimio la aina gani? Yaani, kama jiji hili lisingekuwa na wenye haki kumi, Mungu asingeruhusu uwepo wake, na bila shaka Angeliangamiza. Je hii si hasira ya Mungu? Je, hasira hii inawakilisha tabia ya Mungu? Je, hii tabia ni ufunuo wa kiini cha haki cha Mungu? Je, huu ni ufunuo wa kiini cha haki cha Mungu, ambacho binadamu hafai kuikosea? Baada ya kuthibitisha kwamba hakukuwa na wenye haki kumi kule Sodoma, Mungu alikuwa na uhakika wa kuliangamiza jiji, na angewaadhibu vikali watu walio ndani ya hilo jiji, kwani walimpinga Mungu, na kwa sababu walikuwa wachafu na waliopotoka.

Kwa nini tumechambua vifungu hivi kwa njia hii? Kwa sababu sentensi hizi chache rahisi zinatupa maonyesho kamili ya tabia ya Mungu ya huruma nyingi na ghadhabu kuu. Kwa wakati uleule wa kuwathamini sana wale wenye haki na kuwa na huruma juu yao, kuwavumilia, na kuwajali, ndani ya moyo wa Mungu kulikuwa na chuki kubwa kwa wale waliokuwa ndani ya Sodoma ambao walikuwa wamepotoshwa. Je, hii ilikuwa, au haikuwa huruma nyingi na ghadhabu kubwa? Ni kwanjia gani ambayo Mungu aliuangamiza mji? Kwa moto. Na kwa nini Aliuangamiza kwa kutumia moto? Unapoona kitu kikiungua kwa moto, au wakati uko karibu kuchoma kitu, ni nini hisia zako juu ya kitu hicho? Kwa nini unataka kukichoma? Unahisi kwamba hukihitaji tena, kwamba hutaki tena kukiangalia? Je, unataka kuachana nacho? Matumizi ya Mungu ya moto yanamaanisha kuikataa, na kuichukia, na kwamba hakutaka tena kuiona Sodoma. Hii ilikuwa ni hisia iliyomfanya Mungu kuiteketeza Sodoma kwa moto. Matumizi ya moto yanawakilisha namna ambavyo Mungu alikuwa amekasirika. Rehema na uvumilivu wa Mungu kwa kweli vipo, lakini utakatifu na haki ya Mungu Anapoachilia hasira Yake pia inamwonyesha mwanadamu upande wa Mungu usiovumilia kosa lolote. Wakati binadamu anaweza kabisa kutii amri za Mungu na kutenda kulingana na mahitaji ya Mungu, Mungu ni mwingi wa huruma Zake kwa mwanadamu; wakati mwanadamu amejawa na upotovu, chuki na uadui kwake Yeye, Mungu anakuwa mwenye ghadhabu nyingi. Je, ni kwa kiwango gani Anakuwa amekasirika sana? Hasira yake itaendelea kuwepo mpaka pale ambapo Mungu hataona tena upinzani wa binadamu na matendo maovu, mpaka pale yatakapokuwa hayapo tena mbele ya macho Yake. Hapo tu ndipo ghadhabu ya Mungu itakapotoweka. Kwa maneno mengine, haijalishi mtu huyo ni nani, kama moyo wake umekuwa mbali na Mungu, na yeye amemkataa Mungu, asirudi tena, basi haijalishi ni vipi, kwa mwonekano wote au kuhusiana na matamanio yao binafsi, wanataka kumwabudu na kumfuata na kujinyenyekeza kwa Mungu katika miili yao au katika fikira zao, mara tu mioyo yao inapomwacha Mungu, ghadhabu ya Mungu itaachiliwa bila kikomo. Itakuwa kwamba wakati Mungu anapoiachilia kabisa ghadhabu Yake, akiwa amempa binadamu fursa za kutosha, mara tu inapoachiliwa hakutakuwepo na njia yoyote ya kuirudisha, na hatawahi tena kuwa mwenye huruma na mvumilivu kwa mtu kama huyo. Huu ni upande mmoja wa tabia ya Mungu isiyovumilia kosa. Hapa, inaonekana kawaida kwa watu kwamba Mungu angeliangamiza jiji, kwa kuwa, machoni pa Mungu, jiji lililojaa dhambi lisingeweza kuwepo na kuendelea kubakia pale, na lilikuwa jambo la busara kwamba jiji hilo liangamizwe na Mungu. Lakini katika kile kilichofanyika kabla na kufuatia kuangamiza Kwake Sodoma, tunaiona tabia nzima ya Mungu. Yeye ni mvumilivu na mwenye huruma kwa vitu vilivyo vyema, na vizuri na vya kupendeza; kwa vitu viovu, na vyenye dhambi, na vilivyojaa maovu, Yeye anayo hasira kali, kiasi cha kwamba Haachi kuendeleza hasira Yake. Hivi ndivyo vipengele viwili vikuu na vinavyojitokeza zaidi kuhusu tabia ya Mungu, na, zaidi, vimefichuliwa na Mungu kutoka mwanzo hadi mwisho: huruma nyingi na ghadhabu kuu. Wengi wenu mmepitia huruma ya Mungu, lakini wachache sana wameweza kutambua hasira ya Mungu. Huruma na fadhili za Mungu zinawezakuonekana kwa kila mmoja; yaani, Mungu Amekuwa mwingi wa huruma kwa kila mmoja. Ilhali ni nadra sana—au, inaweza kusemwa, Mungu hajawahi kuwa na ghadhabu kuu kwa mtu yeyote au sehemu yoyote ya watu miongoni mwenu. Tulia! Hivi karibuni au baadaye, hasira ya Mungu itaonekana na kupitiwa na kila mmoja, lakini kwa sasa bado muda haujawadia. Na kwa nini hivi? Kwa sababu wakati Mungu anakuwa na ghadhabu kila mara kwa mtu, yaani, wakati Anapoiachilia hasira Yake kuu kwao, inamaanisha kwamba Amekuwa akichukia na Akikataa kwa muda mrefu mtu huyu, kwamba Anadharau kuwepo kwao, na kwamba Hawezi kuvumilia kuwepo kwao; mara tu hasira Yake itakapokuja juu yao, watatoweka. Leo, kazi ya Mungu bado haijafikia hatua hiyo. Hakuna yeyote kati yenu ambaye ataweza kuivumilia pindi tu Mungu anapoghadhabika kupindukia. Mnaona, basi, kwamba kwa wakati huu Mungu anayo huruma nyingi tu kwenu ninyi nyote, na bado hamjaona hasira Yake kuu. Kama wapo wale wanaobakia wakiwa hawajashawishika, mnaweza kuuliza kuwa hasira ya Mungu ije kwenu, ili mweze kuipitia na kujua kama ghadhabu ya Mungu na tabia Yake isiyokosewa kwa binadamu ipo kwa kweli au la. Mtathubutu kufanya hivyo?

Watu Wa Siku Za Mwisho Wanaiona tu Hasira Ya Mungu Katika Maneno Yake, na Hawaipitii kwa Kweli Hasira Ya Mungu

Je, pande mbili za tabia ya Mungu zinazoonekana kwenye vifungu hivi vya maandiko zinastahili ushirika? Baada ya kuisikia hadithi hii, je, mnao uelewa mpya kuhusu Mungu? Ni uelewa wa aina gani ulio nao? Inaweza kusemwa kwamba kuanzia wakati wa uumbaji mpaka leo, hakuna kikundi ambacho kimefurahia neema au huruma nyingi za Mungu pamoja na fadhili zenye upendo kama kikundi hiki cha mwisho. Ingawa, katika hatua hii ya mwisho, Mungu amefanya kazi Yake ya hukumu na kuadibu, na Amefanya kazi Yake kwa uadhama na hasira, wakati mwingi Mungu anatumia tu maneno kukamilisha kazi Yake; Anatumia maneno ili kufunza, kunyunyiza na kutosheleza, na kulisha. Hasira ya Mungu, wakati haya yakiendelea, siku zote imefichwa, na mbali na kuipitia tabia ya Mungu yenye hasira kwa maneno Yake, watu wachache sana wamepitia ghadhabu Yake ana kwa ana. Hivi ni kusema kwamba, wakati wa kazi ya hukumu na kuadibu kwa Mungu, ingawa hasira iliyofichuliwa katika maneno ya Mungu inawaruhusu watu kupitia uadhama na kutovumilia kosa kwa Mungu, hasira hii haizidi maneno Yake. Kwa maneno mengine, Mungu hutumia maneno ili kumkemea binadamu, kumfichua binadamu, kumhukumu binadamu, kumwadhibu binadamu na hata kumshutumu binadamu—lakini Mungu angali hajawa mwingi wa ghadhabu kwa binadamu, na hata hajaachilia hasira Yake kwa binadamu nje ya maneno yake. Hivyo, rehema na upendo wa Mungu unaompata mwanadamu katika enzi hii ni ufunuo wa tabia ya kweli ya Mungu, ilhali ghadhabu ya Mungu inayopitiwa na mwanadamu ni athari ya sauti na hisia za matamshi Yake. Watu wengi wanachukulia athari hii kimakosa na kuiona kuwa njia ya kweli ya kupitia na maarifa ya kweli ya hasira ya Mungu. Hivyo basi, watu wengi wanasadiki kwamba wameiona huruma ya Mungu na upendo Wake ndani ya maneno Yake, kwamba wameweza pia kushuhudia kutovumilia Kwake kwa kosa la binadamu, na wengi wao wamekuja hata kutambua huruma na uvumilivu wa Mungu kwa mwanadamu. Lakini haijalishi tabia ya mwanadamu ni mbaya kiasi gani, au jinsi tabia yake ilivyo potovu, Mungu daima amekua akivumilia. Katika kuvumilia, nia Yake ni kusubiria maneno Aliyokuwa Ametamka, jitihada Alizofanya na gharama Aliyolipia ili kufikia athari kwa wale Anaotaka kuwapata. Kusubiria matokeo kama haya kunachukua muda, na kunahitaji kuundwa kwa mazingira tofauti kwa mwanadamu, kama vile tu ambavyo watu hawawi watu wazima pindi tu wanapozaliwa; huchukua miaka kumi na minane au kumi na tisa, na baadhi ya watu hata huhitaji miaka ishirini au thelathini kabla hawajakomaa na kuwa mtu mzima halisi. Mungu husubiria kukamilika kwa mchakato huu, Yeye husubiria kuwadia kwa wakati kama huo, na Anangojea kuwasili kwa matokeo haya. Na kwa wakati wote Anaongojea, Mungu ni mwingi wa huruma. Katika kipindi cha kazi ya Mungu, hata hivyo, ni idadi ndogo sana ya watu wanaoangamizwa, na baadhi wanaadhibiwa kwa sababu ya upinzani wao mkubwa kwa Mungu. Mifano kama hiyo ni uthibitisho mkubwa zaidi wa tabia ya Mungu ambayo haivumilii kosa la binadamu, na inathibitisha kabisa uwepo wa kweli wa uvumilivu na ustahimilivu wa Mungu kwa wale wateule. Bila shaka, katika mifano hii halisi, ufunuo wa sehemu ya tabia ya Mungu kwa watu hawa hauathiri kwa ujumla mpango wa usimamizi wa Mungu. Kwa hakika, katika hatua hii ya mwisho ya kazi ya Mungu, Mungu amevumilia kwenye kipindi hiki chote ambacho Amekuwa akisubiria na Amebadilisha uvumilivu Wake na maisha Yake kwa wokovu wa wale wanaomfuata Yeye. Je, mnayaona haya yote? Mungu havurugi mpango Wake bila sababu. Anaweza kuiachilia hasira Yake na Anaweza pia kuwa mwenye huruma; huu ndio ufunuo wa sehemu mbili kuu za tabia ya Mungu. Je, hii iko au haiko wazi kabisa? Kwa maneno mengine, tunapokuja kwa Mungu, sahihi na isiyokuwa sahihi, yenye haki na dhalimu, nzuri na mbaya—hivi vyote vimeonyeshwa waziwazi kwa binadamu. Kile Atakachofanya, kile Anachopenda, kile Anachochukia—yote haya yanaweza kuonyeshwa moja kwa moja katika tabia Yake. Mambo kama hayo yanaweza pia kuwa ya wazi sana na ya kuonekana katika kazi ya Mungu na hayako kijuujuu au kwa ujumla; badala yake, yanawaruhusu watu wote kuitazama tabia ya Mungu na kile Anacho na Alicho hasa kwa njia thabiti, ya kweli na ya kivitendo. Huyu ndiye Mungu Mwenyewe wa kweli.

Tabia ya Mungu Haijawahi Kufichwa Kutoka Kwa Binadamu—Moyo wa Binadamu Umepotoka Kutoka kwa Mungu

Nisingeshiriki kuhusu mambo haya, hakuna yeyote kati yenu ambaye angeweza kutazama tabia ya kweli ya Mungu katika hadithi za Biblia. Hii ni ukweli. Hiyo ni kwa sababu, ingawa hadithi hizi za kibiblia zilirekodi baadhi ya mambo ambayo Mungu alifanya, Mungu alizungumza maneno machache tu na hakuitambulisha tabia Yake kwa njia ya moja kwa moja au kuwasilisha kwa uwazi mapenzi Yake kwa binadamu. Vizazi vya baadaye vimechukulia rekodi hizi kuwa si chochote zaidi ya hadithi, na hivyo inaonekana kwa watu kwamba Mungu anajificha kutoka kwa mwanadamu na kwamba si nafsi ya Mungu ambayo imefichwa kutoka kwa binadamu, lakini tabia na mapenzi Yake. Baada ya ushirika wangu leo, bado mnahisi kwamba Mungu amefichwa kabisa kutoka kwa binadamu? Je, bado mnasadiki kwamba tabia ya Mungu imefichwa kutoka kwa binadamu?

Tangu wakati wa uumbaji, tabia ya Mungu imekuwa sambamba na kazi Yake. Haijawahi kufichwa kutoka kwa binadamu, lakini imewasilishwa kikamilifu na kwa dhahiri kabisa kwa binadamu. Ilhali, kwa kadri muda unavyopita, moyo wa binadamu umekua hata mbali zaidi na Mungu, na kwa kuwa upotovu wa mwanadamu umekuwa wa kina zaidi, binadamu na Mungu wamekuwa wakitengana zaidi na zaidi. Kwa utaratibu lakini kwa uhakika, mwanadamu ametoweka mchoni pa Mungu. Mwanadamu amekuwa hawezi “kumwona”Mungu, jambo ambalo limemwacha yeye bila “habari” zozote kuhusu Mungu; hivyo, hajui kama Mungu yupo, na hata anaenda mbali mno kiasi cha kukataa kabisa kuwepo kwa Mungu. Kwa hivyo, kutofahamu kwa binadamu kuhusu tabia ya Mungu, na kile Anacho na alicho, si kwa sababu Mungu amefichwa kutoka kwa mwanadamu, lakini ni kwa sababu moyo wake umemwacha Mungu. Ingawa mwanadamu anamwamini Mungu, moyo wa mwanadamu haupo na Mungu, na hajui chochote kuhusu namna ya kumpenda Mungu, wala hataki kumpenda Mungu, kwani moyo wake haujawahi kumkaribia Mungu na siku zote anamuepuka Mungu. Kutokana na haya, moyo wa binadamu umekuwa mbali sana na Mungu. Kwa hivyo, moyo wake uko wapi? Kwa hakika, moyo wa binadamu haujaenda popote: Badala ya kuutoa kwa Mungu au kuufunua kwa Mungu ili Aweze kuuona, yeye ameuweka kwa ajili yake mwenyewe. Hii ni pamoja na ukweli kwamba baadhi ya watu mara nyingi wanamwomba Mungu na kusema, “Ee Bwana, utazame moyo wangu—unajua yote ninayofikiria,” na baadhi hata huapa kumruhusu Mungu awaangalie, ili kwamba waweze kuadhibiwa kama watavunja kiapo chao. Ingawa mwanadamu anamruhusu Mungu atazame ndani ya moyo wake, hii haimanishi kwamba anaweza kutii mipango na mipangilio ya Mungu, wala kwamba ameacha hatima na matarajio yake na mambo yake yote chini ya udhibiti wa Mungu. Hivyo, licha ya viapo unavyotoa kwa Mungu au kile unachotamka Kwake, machoni pa Mungu moyo wako bado umefungwa Kwake, kwani unamruhusu Mungu tu kuangalia kwenye moyo wako lakini humruhusu Yeye kuudhibiti. Kwa maneno mengine, hujampa Mungu moyo wako hata kidogo, na unazungumza tu maneno yanayosikika kuwa matamu ili Mungu asikie; wakati huo huo, unaficha nia zako mbalimbali za udanganyifu kutoka kwa Mungu, pamoja na hila, njama, na mipango yako, na unashikilia matarajio na hatima yako mikononi mwako, ukiwa na hofu kubwa kwamba huenda yakachukuliwa na Mungu. Hivyo, Mungu kamwe hauoni uaminifu wa mwanadamu Kwake. Ingawa Mungu anaangalia kina cha moyo wa binadamu, na Anaweza kuona kile ambacho binadamu anafikiria na anataka kufanya moyoni mwake, na Anaweza kuona ni mambo yapi yamewekwa ndani ya moyo wake, moyo wa binadamu haumilikiwi na Mungu, hajautoa ili udhibitiwe na Mungu. Hivi ni kusema, Mungu anayo haki ya kuangalia, lakini Hana haki ya kuudhibiti moyo huo. Katika ufahamu binafsi wa mwanadamu, mwanadamu hataki au hanuii kumwacha Mungu ampangie. Sio tu kwamba mwanadamu amejifungia kutoka kwa Mungu, bali kunao hata watu wanaofikiria njia za kusetiri mioyo yao, kwa kutumia mazungumzo matamu na sifa za kinafiki ili kuunda hali ya uongo na kupata uaminifu wa Mungu, na kuficha uso wao wa kweli usionekane na Mungu. Nia yao ya kutomruhusu Mungu kuona ni kutoruhusu Mungu kuelewa namna walivyo kwa kweli. Hawataki kuitoa mioyo yao kwa Mungu lakini wanajihifadhia wao wenyewe. Muktadha wa jambo hili ni kwamba kile ambacho binadamu anafanya na kile ambacho anataka kimepangiliwa chote, kikapigiwa hesabu, na kuamuliwa na binadamu mwenyewe; haihitaji kushiriki au kuingilia kati kwa Mungu, na isitoshe hahitaji mipango na mipangilio ya Mungu. Kwa hivyo, iwapo ni kuhusiana na amri za Mungu, agizo Lake, au mahitaji ambayo Mungu anamwekea binadamu, uamuzi wa binadamu unatokana na nia na maslahi yake mwenyewe, katika mazingira na hali yake mwenyewe ya wakati huo. Siku zote binadamu anatumia maarifa na utambuzi anaoufahamu, na akili yake mwenyewe, ili kuamua na kuchagua njia anayopaswa kuchukua, na haruhusu kuingiliwa au kudhibitiwa na Mungu. Huu ndio moyo wa mwanadamu ambao Mungu anauona.

Tangu mwanzo hadi leo, ni binadamu tu ambaye ameweza kuzungumza na Mungu. Yaani, miongoni mwa viumbe vyote vilivyo hai na viumbe vya Mungu, hakuna yeyote isipokuwa mwanadamu ambaye ameweza kuzungumza na Mungu. Mwanadamu ana masikio yanayomwezesha kusikia, na macho yanayomwezesha kuona; anayo lugha na fikira zake binafsi, na pia anao uhuru wa kuamua chochote. Anamiliki kila kitu kinachohitajika ili kumsikia Mungu akizungumza, na kuelewa mapenzi ya Mungu, na kukubali agizo la Mungu, na hivyo basi Mungu sawa na Yeye na ambaye anaweza kutembea na Yeye. Tangu Alipoanza kusimamia, Mungu amekuwa akisubiria mwanadamu toe moyo wake Kwake, akimwacha Mungu ausafishe na kuutayarisha ipaswavyo, kumfanya yeye kumtosheleza Mungu na kupendwa na Mungu, kumfanya amche Mungu na kujiepusha na maovu. Mungu hukabidhi matakwa Yake yote kwa mwanadamu, akitaka kumfanya mwanadamu kuwa mwandani Wake ambaye ana nia moja kabla ya enzi hii? Leo, hebu tuendelee kusoma simulizi za Biblia na kuangalia kama kile kilichofanywa na mtu huyu—Ayubu—kina uhusiano wowote na mada ya “kumpa Mungu moyo wako” ambayo tunazungumzia kuhusu leo. Hebu tuone kama Ayubu alimtosheleza Mungu na kupendwa na Mungu.

Maoni yenu ni yapi kuhusu Ayubu? Wakinukuu maandiko halisi, baadhi ya watu husema kwamba Ayubu “alimcha Mungu na kujiepusha na maovu.” “Alimcha Mungu na kujiepusha na maovu”: hayo ndiyo maoni ya Mungu kwa Ayubu yaliyorekodiwa katika Biblia. Kama mkiyatumia maneno yenu binafsi, mnawezaje kumzungumzia Ayubu? Baadhi ya watu wanasema kwamba Ayubu alikuwa mtu mzuri namwenye busara, baadhi wanasema kwamba alikuwa na imani ya kweli kwa Mungu; baadhi wanasema kwamba Ayubu alikuwa damtu mwenye haki na mwenye utu. Mmeiona imani ya Ayubu, hivi ni kusema, katika mioyo yenu mnaona umuhimu mkubwa na mnaionea wivu imani ya Ayubu. Leo, basi, hebu tuzungumzie kile kilichomilikiwa na Ayubu ambacho kinamfanya Mungu apendezwe naye sana. Kisha, hebu tusome maandiko yaliyo hapa chini.

C. Ayubu

1. Tathmini ya Mungu kwa Ayubu na katika Biblia

Ayubu 1:1 Palikuwa na mtu katika nchi ya Uzi, ambaye aliitwa Ayubu; na huyo mtu alikuwa mtimilifu na mwaminifu, na ambaye alimcha Mungu, na kuepuka maovu.

Ayubu 1:5 Na ilikuwa hivyo, wakati hizo siku zao za karamu ziliisha, Ayubu aliwatuma na kuwatakasa, na akaamka asubuhi mapema, na kutoa sadaka za kuteketezwa kulingana na hesabu yao wote; kwa sababu Ayubu alisema, Inaweza kuwa kwamba wana wangu wametenda dhambi, na kumlaani Mungu mioyoni mwao. Hivyo ndivyo Ayubu alivyofanya kila siku.

Ayubu 1:8 Naye Yehova akasema kwa Shetani, je, umemfikiria mtumishi Wangu Ayubu, kwamba hakuna hata mtu kama yeye duniani, mtu mtimilifu na mwaminifu, ambaye anamcha Mungu, na kuepuka maovu?

Ni nini hoja kuu unayoiona kwenye vifungu hivi? Vifungu hivi vitatu vifupi vya maandiko vyote vinahusiana na Ayubu. Ingawa ni vifupi, vinaelezea waziwazi alikuwa ni mtu wa aina gani. Kupitia kwa ufafanuzi wake kuhusu tabia ya kila siku ya Ayubu na mwenendo wake, vinaelezea kila mmoja kwamba, badala ya kukosa msingi, ukadiriaji wa Mungu ya Ayubu ulikuwa na msingi wake na ulikuwa umekita mizizi. Vinatuambia kwamba, iwapo ni utathmini wa binadamu kuhusu Ayubu (Ayubu 1:1), au tathmini ya Mungu kwake (Ayubu 1:8), yote ni matokeo ya matendo ya Ayubu mbele za Mungu na mwanadamu (Ayubu 1:5).

Kwanza, hebu tukisome kifungu cha kwanza: “Palikuwa na mtu katika nchi ya Usi, jina lake akiitwa Ayubu; na mtu huyo alikuwa mkamilifu na muadilifu, ni mmoja ambae alimcha Mungu, na kuepukana na uovu.” Hii ni tathmini ya kwanza ya Ayubu katika Biblia, na sentensi hii ni tathmini ya mwandishi kuhusu Ayubu. Kwa kawaida, pia inawakilisha tathmini ya mwanadamu kuhusu Ayubu, ambayo ni “kwamba mwanadamu huyo alikuwa mkamilifu na muadilifu, na aliyemcha Mungu, na kuepuka uovu.” Kisha, na tusome tathmini ya Mungu kumhusu Ayubu: “Hakuna aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na muadilifu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu.” Kati ya tathmini hizi mbili, moja ilitoka kwa binadamu, na nyingine ikatoka kwa Mungu; ni tathmini mbili zenye maudhui sawa. Inaweza kuonekana, basi, kwamba tabia na mwenendo wa Ayubu ulijulikana kwa binadamu, na pia ulisifiwa na Mungu. Kwa maneno mengine, mwenendo wa Ayubu mbele ya binadamu na mwenendo wake mbele za Mungu ulikuwa sawa; aliweka tabia yake na motisha yake mbele za Mungu siku zote, ili hivi viwili viweze kuangaliwa na Mungu, na yeye alikuwa alimcha Mungu na kujiepusha na maovu. Hivyo, katika machoni Mungu, kati ya watu duniani, ni Ayubu tu ambaye alikuwa mkamilifu na mnyofu, ndiye aliyemcha Mungu na kujiepusha na maovu.

Maonyesho Mahususi ya Kumcha Mungu kwa Ayubu na Kujiepusha na Maovu katika Maisha Yake ya Kila siku

Kisha, hebu tuangalie maonyesho mahususi ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu kwa Ayubu. Mbali na vifungu vinavyoitangulia na kuifuata, hebu pia tusome Ayubu 1:5, ambayo ni mojawapo ya maonyesho mahususi ya kumcha Mungu na kujiepusha kwa maovu kwa Ayubu. Inahusu namna ambavyo alimcha Mungu na kujiepusha na maovu katika maisha yake ya kila siku; lililo muhimu zaidi, hakufanya tu kile alichostahili kufanya kwa ajili ya uchaji wake kwa Mungu na kujiepusha na maovu, lakini pia mara kwa mara alitoa sadaka za kuteketezwa mbele za Mungu kwa niaba ya wanae. Alikuwa na hofu kwamba walikuwa mara nyingi “wametenda dhambi, na kumkufuru Mungu mioyoni mwao” walipokuwa katika karamu. Na hofu hii inadhihirishwa vipi ndani ya Ayubu? Maandiko halisi yanatupa maelezo yafuatayo: “Basi ilikuwa, hapo hizo siku za karamu zao zilipokuwa zimetimia, Ayubu hutuma kwao akawatakasa, kisha akaamka asubuhi na mapema, na kutoa sadaka za kuteketezwa kulingana na hesabu yao wote ilivyokuwa.” Mwenendo wa Ayubu unatuonyesha kwamba, badala ya kuonyeshwa katika tabia yake ya nje, kumcha Mungu kwake kulitokea ndani ya moyo wake, na kwamba kumcha Mungu kwake kungepatikana katika kila kipengele cha maisha yake ya kila siku, wakati wote, kwani hakujiepusha na maovu tu yeye mwenyewe, lakini pia alitoa sadaka za kuteketezwa kwa niaba ya wanawe. Kwa maneno mengine, Ayubu hakuwa tu mwenye hofu ya kutenda dhambi dhidi ya Mungu na kumkana Mungu katika moyo wake mwenyewe, bali pia alikuwa na wasiwasi kwamba wanawe wangemtenda Mungu dhambi na kumkana Yeye katika mioyo yao. Kutokana na haya inaweza kuonekana kwamba ukweli wa kumcha Mungu kwa Ayubu unapita uchunguzi, na upo nje ya mashaka ya mwandamu yeyote. Je, alifanya hivi mara chache tu, au mara nyingi? Sentensi ya mwisho ya maandiko ni “Hivyo ndivyo Ayubu alivyofanya siku zote.” Maana ya maneno haya ni kwamba Ayubu hakuenda na kuwaangalia watoto wake mara chache tu, au wakati alipopenda kufanya hivyo, wala hakutubu kwa Mungu kupitia kwa maombi. Badala yake, aliwatuma mara kwa mara na kuwatakasa watoto wake, na kutoa sadaka za kuteketezwa kwa ajili yao. Neno “siku zote” hapa haimaanishi alifanya hivyo kwa siku moja au mbili, au kwa muda mfupi tu. Inasema kwamba maonyesho ya kumcha Mungu kwa Ayubu hayakuwa ya muda tu, na hayakuishia kwenye maarifa aliyokuwa nayo au kwa maneno aliyotamka; badala yake, njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu iliongoza moyo wake, iliamuru tabia yake, na ilikuwa, ndani ya moyo wake chanzo cha kuwepo kwake. Kwamba alifanya hivyo daima inaonyesha kwamba, katika moyo wake, mara nyingi alikuwa na hofu kwamba yeye mwenyewe angetenda dhambi dhidi ya Mungu na alikuwa na wasiwasi pia kwamba watoto wake wa kiume na binti zake wangetenda dhambi dhidi ya Mungu. Inawakilisha namna tu ambavyo uzito wa njia ambayo alimcha Mungu na kujiepusha na maovu ulibebwa ndani ya moyo wake. Alifanya hivyomara kwa mara kwa sababu, ndani ya moyo wake, alikuwa na hofu na wasiwasi—wasiwasi kwamba alikuwa ametenda maovu na kutenda dhambi dhidi ya Mungu, na kwamba alikuwa amepotoka kutoka kwenye njia ya Mungu, na hivyo hakuweza kumridhisha Mungu. Wakati huohuo, alikuwa pia na wasiwasi kuhusu watoto wake wa kiume na binti zake, akiogopa kwamba walikuwa wamemkosea Mungu. Hivyo ndivyo ulivyokuwa mwenendo wa kawaida wa Ayubu katika maisha yake ya kila siku. Ni mwenendo huu wa kawaida ambao unathibitisha kwamba kumcha Mungu na kujiepusha kwa maovu kwa Ayubu si maneno matupu tu, kwamba Ayubu aliishi kwa kudhihirisha kwa kweli ukweli kama huo. “Hivyo ndivyo Ayubu alivyofanya siku zote”: Maneno haya yanatuambia kuhusu matendo ya kila siku ya Ayubu mbele za Mungu. Alipofanya hivyo kila mara, je tabia yake na moyo wake vilifika mbele za Mungu? Kwa maneno mengine, Mungu mara nyingi alipendezwa na moyo wake na tabia yake? Basi, ni katika hali gani na katika muktadha gani Ayubu alifanya hivyo daima? Baadhi ya watu wanasema kwamba ilikuwa ni kwa sababu Mungu alijitokeza kwa Ayubu mara kwa mara na ndiyo maana alitenda hivyo.” baadhi wanasema kwamba: “Alifanya hivyo sikuzote kwa sababu alikuwa na nia ya kujiepusha na maovu” na wengine wanasema: “Labda alifikiri kwamba utajiri wake ulikua haujamjia kwa urahisi, na alijua kwamba alikuwa amepewa na Mungu, na hivyo alikuwa anaogopa sana kupoteza mali zake kwa sababu ya kutenda dhambi au kumchukiza Mungu. Je, kuna maelezo yoyote kati ya haya yaliyo sahihi? Bila shaka, hakuna. Kwa maana, machoni pa Mungu, kile ambacho Mungu alikubali na kuthamini zaidi kuhusu Ayubu haikuwa tu kwamba alifanya hivyo daima; zaidi ya hayo, ulikuwa ni mwenendo wake mbele za Mungu, mwanadamu, na Shetani wakati alipokabidhiwa kwa Shetani na kujaribiwa. Sehemu zilizo hapa chini zinatupa ushahidi wa kushawishi zaidi, ushahidi unaotuonyesha ukweli wa tathmini ya Mungu kwa Ayubu. Kinachofuata, hebu tusome maandiko kwenye vifungu vifuatavyo.

2. Shetani Anamjaribu Ayubu kwa Mara ya Kwanza (Mifugo Yake Yaibiwa na Janga Lawapata Watoto Wake)

a. Maneno Yaliyotamkwa na Mungu

Ayubu 1:8 Naye Yehova akamwambia Shetani, je, umemfikiria mtumishi Wangu Ayubu, kwamba hakuna hata mtu kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mnyoofu, ambaye anamcha Mungu, na kuepuka maovu?

Ayubu 1:12 Naye Yehova akamwambia Shetani, Tazama, vyote alivyo navyo vimo uwezoni mwako; lakini usimguse yeye mwenyewe. Hivyo basi Shetani akaondoka mbele za uwepo wa Yehova.

b. Jibu la Shetani

Ayubu 1:9-11 Kisha Shetani akamjibu Yehova, na kusema, je, Ayubu anamcha Mungu bure? Wewe hukumzingira kila upande na ukingo, na kila upande wa nyumba yake, na kila upande wa yote aliyo nayo? Umeibariki kazi ya mikono yake, nayo mali yake imeongezeka katika nchi. Lakini nyosha mkono wako sasa, uyaguse hayo yote aliyo nayo, naye atakukufuru mbele za uso Wako.

Mungu Amruhusu Shetani Kumjaribu Ayubu ili Imani ya Ayubu iweze Kufanywa Kuwa Kamili

Ayubu 1:8 ndiyo rekodi ya kwanza tunayoiona kwenye Biblia kuhusu mazungumzo kati ya Yehova Mungu na Shetani. Na ni nini alichosema Mungu? Maandiko halisi yanatupatia simulizi ifuatayo: “Kisha Yehova akamwuliza Shetani, je, umemwangalia huyo mtumishi Wangu Ayubu, kwa kuwa hakuna mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mnyoofu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu?” Hii ilikuwa tathmini ya Mungu kuhusu Ayubu kwa Shetani; Mungu alisema kwamba alikuwa mtu mkamilifu na mnyofu, yule aliyemcha Mungu na kujiepusha na maovu. Kabla ya maneno haya kati ya Mungu na Shetani, Mungu alikuwa ameamua kwamba Angemtumia Shetani kumjaribu Ayubu—kwamba Angemkabidhi Ayubu kwa Shetani. Kwa namna moja, hii ingethibitisha kwamba uchunguzi na tathmini ya Mungu kwa Ayubu ulikuwa sahihi na usio na makosa, na ingesababisha Shetani kuaibishwa kupitia ushuhuda wa Ayubu; katika namna nyingine, ingekamilisha imani ya Ayubu kwa Mungu na uchaji wake kwa Mungu. Hivyo, Shetani alipokuja mbele za Mungu, Mungu hakutatiza maneno. Alienda moja kwa moja kwenye hoja na kumuuliza Shetani: “Je, umemfikiria mtumishi Wangu Ayubu, kwa kuwa hakuna mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mnyoofu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu?” Katika swali la Mungu kuna maana ifuatayo: Mungu alijua kwamba Shetani alizunguka kila pahali, na mara nyingi alikuwa amemnyemelea Ayubu, aliyekuwa mtumishi wa Mungu. Alikuwa mara nyingi amemjaribu na kumshambulia, akijaribu kupata njia ya kumwangamiza Ayubu ili kuthibitisha kwamba imani ya Ayubu katika Mungu na kumcha Mungu kwake kusingeweza kusimama imara. Shetani pia alitafuta kwa haraka sana fursa za kumhangaisha Ayubu, ili Ayubu aweze kumkataa Mungu, na kwamba aweze kumpokonya kutoka katika mikono ya Mungu. Lakini Mungu aliuangalia moyo wa Ayubu na kuona kwamba alikuwa mkamilifu na mnyofu, na kwamba alimcha Mungu na kujiepusha na maovu. Mungu alitumia swali moja kumwambia Shetani kwamba Ayubu alikuwa binadamu mkamilifu na mnyofu aliyemcha Mungu na kujiepusha na maovu, kwamba Ayubu asingeweza kumwacha Mungu na kumfuata Shetani. Baada ya kusikia tathmini ya Mungu kuhusu Ayubu, ndani ya Shetani kukatokea hasira kali iliyotokana na udhalilishaji, na akawa mwenye hasira zaidi, na aliyekosa subira ya kumpokonya Ayubu kutoka kwa Mungu, kwani Shetani alikuwa hajawahi kusadiki kwamba mtu angeweza kuwa mkamilifu na mnyofu, au kwamba angeweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Wakati huohuo, Shetani pia alichukizwa na ukamilifu na unyofu ulio ndani ya mwanadamu, na aliwachukia watu ambao wangeweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Na hivyo imeandikwa katika Ayubu 1:9-11 kwamba “Kisha Shetani akamjibu Yehova, na kusema, je, Ayubu anamcha Mungu bure? Wewe hukumzingira kwa ukingo kila upande, na kila upande wa nyumba yake, na kila upande wa yote aliyo nayo? Umeibariki kazi ya mikono yake, nayo mali yake imeongezeka katika nchi. Lakini nyosha mkono wako sasa, uyaguse hayo yote aliyo nayo, naye atakukufuru mbele za uso Wako.” Mungu aliifahamu sana asili ya Shetani, na Alijua vizuri kabisa kwamba Shetani alikuwa na mpango wa muda mrefu wa kumwangamiza Ayubu, na hivyo kwa haya Mungu alitaka, kwa kumwambia Shetani kwa mara nyingine kwamba Ayubu alikuwa mkamilifu na mnyoofu na kwamba alimcha Mungu na kujiepusha na maovu, kumrudisha Shetani pale anapofaa, kumfanya Shetani kufichua uso wake wa kweli na kumshambulia na kumjaribu Ayubu. Kwa maneno mengine, Mungu alisisitiza kimakusudi kwamba Ayubu alikuwa mkamilifu na mnyofu na kwamba alimcha Mungu na kujiepusha na maovu, na kwa njia hii Alimfanya Shetani amshambulie Ayubu kwa sababu ya chuki na hasira za Shetani kutokana na vile ambavyo Ayubu alikuwa binadamu mkamilifu na mnyofu, yule aliyemcha Mungu na kujiepusha na maovu. Kutokana na haya, Mungu angemletea Shetani aibu kupitia kwa ukweli kwamba Ayubu alikuwa binadamu mkamilifu na mnyoofu, yule aliyemcha Mungu na kujiepusha na maovu, na Shetani angeachwa akiwa amedhalilishwa kabisa na kushindwa. Baada ya hapo, Shetani asingekuwa tena na shaka au asingetoa mashtaka kuhusu ukamilifu, unyofu, ucha Mungu au hali ya kujiepusha na maovu ya Ayubu. Kwa njia hii, majaribio ya Mungu na yale ya Shetani yalikuwa yasiyoepukika. Yule tu aliye na uwezo wa kustahimili majaribio ya Mungu na majaribu ya Shetani alikuwa ni Ayubu. Kufuatia mazungumzo haya, Shetani alipewa ruhusa ya kumjaribu Ayubu. Na hivyo awamu ya kwanza ya mashambulizi ya Shetani ilianza. Lengo la mashambulizi haya lilikuwa mali za Ayubu, kwani Shetani alikuwa ametoa mashtaka yafuatayo dhidi ya Ayubu: “Je, Ayubu anamcha Mungu bure? … Umeibariki kazi ya mikono yake, nayo mali yake imeongezeka katika nchi.” Kutokana na haya, Mungu alimruhusu Shetani kuchukua kila kitu ambacho Ayubu alikuwa nacho— hii ndiyo ilikuwa sababu hasa iliyomfanya Mungu azungumze na Shetani. Hata hivyo, Mungu alitoa sharti moja kwa Shetani: “Yote aliyo nayo yamo katika uwezo wako; lakini usimguse yeye mwenyewe” (Ayubu 1:12). Hili ndilo sharti ambalo Mungu alilitoa baada ya kumruhusu Shetani kumjaribu Ayubu na akamweka Ayubu kwenye mikono ya Shetani, na hiyo ndiyo ilikuwa mipaka aliyomwekea Shetani: Alimwamuru Shetani asimdhuru Ayubu. Kwa sababu Mungu alijua kwamba Ayubu alikuwa mkamilifu na mnyofu, na Alikuwa na imani kwamba ukamilifu na unyofu wa Ayubu mbele Zake ulikuwa usio na shaka, na kwamba angeweza kustahimili kujaribiwa; hivyo, Mungu alimruhusu Shetani kumjaribu Ayubu, lakini akaweka kizuizi kwa Shetani: Shetani aliruhusiwa kuchukua mali yote ya Ayubu, lakini asimguse hata kwa kidole. Hii inamaanisha nini? Inamaanisha kwamba Mungu hakumkabidhi Ayubu kabisa kwa Shetani wakati huo. Shetani angeweza kumjaribu Ayubu kwa mbinu zozote zile ambazo alitaka, lakini hakuweza kumdhuru Ayubu mwenyewe, hata unywele mmoja juu ya kichwa chake—kwa sababu kila kitu cha mwanadamu kinadhibitiwa na Mungu, iwapo binadamu anaishi ama anakufa inaamuliwa na Mungu na Shetani hana kibali chochote cha kudhibiti haya. Baada ya Mungu kumwambia Shetani maneno haya, Shetani hakuweza kusubiri kuanza. Alitumia kila mbinu kumjaribu Ayubu, na baada ya muda mfupi tu Ayubu alipoteza kundi kubwa la kondoo na ng’ombe na mali zote alizokuwa amepewa na Mungu…. Na hivyo majaribu ya Mungu yakawa yamemjia.

Ingawa Biblia inatuambia chanzo cha jaribu la Ayubu, je, Ayubu mwenyewe, ambaye alipatwa na majaribu hayo, alijua kuhusu kile kilichokuwa kikiendelea? Ayubu alikuwa tu binadamu wa kawaida; bila shaka hakujua chochote kuhusu hadithi ile iliyokuwa ikiendelea nyuma yake. Hata hivyo, uchaji wake kwa Mungu na ukamilifu pamoja na unyofu wake, ulimfanya kutambua kwamba majaribio ya Mungu yalikuwa yamemjia. Hakujua ni nini kilichokuwa kimefanyika kwenye ufalme wa kiroho, wala nia alizokuwa nazo Mungu katika majaribio hayo. Lakini alijua kwamba haijalishi ni nini ambacho kilikua kimemtokea, alipaswa kushikilia kwa uaminifu ukamilifu wake na unyofu wake, na kwamba alipaswa kudumu katika njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Mtazamo na mwitikio wa Ayubu katika masuala haya uliweza kutazamwa waziwazi na Mungu. Je, Mungu aliona nini? Aliuona moyo wa Ayubu uliyomcha Mungu, kwa sababu kutoka mwanzo hadi wakati ambapo Ayubu alijaribiwa, moyo wa Ayubu ulibakia wazi kwa Mungu, uliwekwa mbele za Mungu, na Ayubu hakuacha ukamilifu wake au unyofu wake, wala hakuutupilia mbali au kugeuka kutoka katika njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu—na hakuna jambo lililokuwa la kumfurahisha Mungu zaidi ya hili. Kisha, tutaangalia ni majaribu gani ambayo Ayubu aliyapitia, na jinsi alivyokabiliana na majaribu hayo. Hebu tusome kutoka kwenye maandiko.

c. Mwitikio wa Ayubu

Ayubu 1:20-21 Kisha Ayubu akainuka, na akalipasua joho lake, na akanyoa kichwa chake, na akaanguka chini, na kuabudu, Naye akasema, Nilitoka kwa tumbo la mama yangu nikiwa uchi, na mimi nitarudi huko nikiwa uchi; Yehova alinipa, na Yehova amechukua; jina la Yehova libarikiwe.

Kwamba Ayubu Alikuwa Tayari Kurudisha Vitu Vyote Alivyomiliki Kulitokana na Kumcha Kwake Mungu

Baada ya Mungu kumwambia Shetani, “Yote aliyo nayo yamo katika uwezo wako; lakini usiunyoshe mkono wako juu yake mwenyewe.” Shetani aliondoka, muda mfupi baadaye Ayubu alipata mashambulizi ya ghafla na makali: Kwanza, ng’ombe na punda wake waliporwa na baadhi ya watumishi wake wakauawa; baadaye, kondoo wake na watumishi wengine zaidi waliteketezwa kwa moto; baada ya hapo, ngamia wake walichukuliwa na hata watumishi wake wengi zaidi wakauawa; hatimaye, maisha ya watoto wake wa kiume na wakike yaliondolewa. Mfululizo huu wa mashambulizi ulikuwa ni mateso aliyoyapata Ayubu wakati wa jaribu la kwanza. Kama alivyoamriwa na Mungu, wakati wa mashambulizi haya Shetani alilenga tu mali zaAyubu na watoto wake, na hakumdhuru Ayubu mwenyewe. Hata hivyo, Ayubu alibadilishwa papo hapo kutoka kuwa mtu tajiri aliyemiliki utajiri mwingi hadi kuwa mtu asiye na chochote. Hakuna yeyote ambaye angeweza kustahimili pigo hili la kushtua sana au kukabiliana nalo kwa usahihi, hata hivyo Ayubu alionyesha upande wake usio wa kawaida. Maandiko yanaelezea yafuatayo: “Ndipo Ayubu akainuka, akaliraruajoho lake, na akanyoa kichwa chake, na akaanguka chini, na kuabudu.” Huu ndio uliokuwa mwitikio wa kwanza wa Ayubu baada ya kusikia kwamba amepoteza watoto wake na mali zake zote. Zaidi ya yote, hakuonekana kuwa ameshangazwa, au kuingiwa na hofu, isitoshe hakuonyesha hasira au chuki. Unaona, basi, kwamba moyoni mwake alikuwa tayari ametambua kuwa majanga haya hayakuwa ajali, au kwamba yalitokana na mkono wa mwanadamu, na wala haikuwa kulipizwa kisasi au kuadhibiwa. Badala yake, majaribio ya Yehova yalikuwa yamemjia yeye; alikuwa ni Yehova ambaye alitaka kuchukua mali na watoto wake. Wakati huo Ayubu alikuwa mtulivu na mwenye kuelewa kwa haraka. Ubinadamu wake mkamilifu na mnyoofu ulimwezesha kwa mantiki na kwa kawaida kuwa na maoni na maamuzi sahihi kuhusiana na maafa yaliyokuwa yamempata, na kwa sababu hiyo, alitenda kwa utulivu wa hali ya juu: “Ndipo Ayubu akainuka, akaliraruajoho lake, na akanyoa kichwa chake, na akaanguka chini, na kuabudu.” “Akalipasua joho lake” inamaanisha kwamba alikuwa uchi, na hakuwa chochote; “akanyoa kichwa chake” inamaanisha kwamba alikuwa amerudi mbele za Mungu kama mtoto mchanga aliyezaliwa; “akaanguka chini, na kuabudu” inamaanisha kwamba alikuwa amekuja ulimwenguni akiwa uchi, na bado hakuwa na chochote leo, alirudishwa kwa Mungu kama mtoto mchanga aliyezaliwa. Mtazamo wa Ayubu kwa yote yaliyompata haungeweza kufikiwa na kiumbe yeyote wa Mungu. Imani yake kwa Yehova ilizidi mipaka ya imani; huku kulikuwa ni kumcha Mungu kwake, kuwa mtiifu kwa Mungu, na hakuweza tu kutoa shukrani kwa Mungu kwa kumpa yeye, lakini pia kwa kuchukua kutoka kwake. Na zaidi ya hayo, aliweza kuwa tayari kurudisha yale yote aliyomiliki, akijumuisha na maisha yake.

Kumcha Mungu na utiifu wa Ayubu kwa Mungu ni mfano kwa wanadamu, na ukamilifu na unyofu wake ulikuwa ndio kilele cha ubinadamu unaofaa kumilikiwa na binadamu. Ingawa hakumwona Mungu, alitambua kwamba Mungu kwa kweli alikuwepo, na kwa sababu ya utambuzi huu alimcha Mungu, na kutokana na uchaji wake kwa Mungu, aliweza kumtii Mungu. Alimpa Mungu uhuru wa kuchukua chochote alichokuwa nacho, hata hivyo hakuwa na manung’uniko, na akaanguka chini mbele za Mungu na kumwambia kwamba, kwa wakati huu, hata kama Mungu angeuchukua mwili wake, angemruhusu yeye kufanya hivyo kwa furaha, bila malalamiko. Mwenendo wake wote ulitokana na ubinadamu wake mkamilifu na mnyofu. Hivi ni kusema, kutokana na kutokuwa na hatia kwake, uaminifu, na wema wake, Ayubu alikuwa thabiti katika kutambua na kuhisi uwepo wa Mungu, na juu ya msingi huu aliweza kujiwekea mahitaji yake mwenyewe na kudhibiti mawazo yake, tabia, mwenendo, na kanuni za kutenda mbele za Mungu kulingana na mwongozo wa Mungu kwake na matendo ya Mungu ambayo alikuwa ameyaona kati ya vitu vyote. Baada ya muda, uzoefu wake ulimsababisha yeye kuwa na hali halisi na ya kweli ya kumcha Mungu na kumfanya pia kujiepusha na maovu. Hiki ndicho kilikuwa chanzo cha uadilifu ambao Ayubu alishikilia kwa uthabiti. Ayubu alikuwa na ubinadamu wenye uaminifu, unyofu, na mwema, na alikuwa na uzoefu halisi wa kumcha Mungu, kumtii Mungu na kujiepusha na maovu, pamoja na maarifa kwamba “Yehova alinipa, na Yehova amechukua.” Ni kwa sababu tu ya mambo haya ndiyo aliweza kusimama imara na kutoa ushuhuda katikati ya mashambulizi hayo makali ya Shetani, na ni kwa sababu tu ya hayo ndiyo aliweza kutomkasirisha Mungu na kutoa jibu la kumridhisha Mungu wakati majaribio ya Mungu yalipomjia. Ingawa mwenendo wa Ayubu katika jaribu la kwanza ulikuwa wa unyofu, vizazi vya baadaye havikuwa na uhakika wa kutimiza hali hiyo ya unyofu hata baada ya kutia bidii maisha yao yote, wala hawangekuwa kwa vyovyote vile na mwenendo wa Ayubu uliofafanuliwa hapo juu. Leo, wakikabiliwa na mwenendo wa unyofu wa Ayubu, na katika kuulinganisha na vilio na azimio la “utiifu kamili na uaminifu hadi kifo” ulioonyeshwa kwa Mungu na wale wanaodai kumwamini na kumfuata Mungu, je mnahisi aibu sana au la?

Wakati unasoma maandiko kuhusu yale mateso yote aliyopitia Ayubu na familia yake, mwitikio wako ni upi? je, unakuwa umepotea katika mawazo yako? je, unashangazwa? Je, majaribio haya yaliyomsibu Ayubu yanaweza kufafanuliwa kama ya “kutisha”? Kwa maneno mengine, inatisha sana kuyasoma majaribu ya Ayubu kama yalivyoelezwa katika maandiko, bila kusema chochote kuhusu vile yangekuwa katika uhalisia. Unaona, basi, kwamba kile kilichompata Ayubu hakikuwa “mazoezi,” bali “vita,” halisi, vilivyo na “bunduki” na “risasi” halisi. Lakini, je, ni nani aliyesababisha apitie majaribu haya? Yaliweza, bila shaka, kutekelezwa na Shetani, yalitekelezwa na Shetani mwenyewe—lakini yaliidhinishwa na Mungu. Je, Mungu alimwambia Shetani amjaribu Ayubu kwa njia gani? Hakumwambia. Mungu alimpa Shetani sharti moja tu, na baadaye jaribu likamjia Ayubu. Wakati jaribu lilipomjia Ayubu, liliwapa watu hisia ya uovu na ubaya wa Shetani, ya nia zake mbaya na chuki yake kwa mwanadamu, na uadui wake kwa Mungu. Katika haya tunaona kwamba maneno yasingeweza kufafanua namna tu ambavyo jaribu hili lilikuwa la kikatili. Inaweza kusemwa kwamba asili yenye nia mbaya ambayo Shetani alimnyanyasa nayo mwanadamu, na uso wake mbaya, vyote vilifichuliwa kabisa kwa wakati huu. Shetani alitumia fursa hii, fursa iliyotolewa kupitia kwa ruhusa ya Mungu, kumnyanyasa Ayubu kwa njia mbaya na ya kikatili, mbinu na kiwango cha ukatili ambao haufikiriki na hauvumiliki kabisa na watu wa leo. Badala ya kusema kwamba Ayubu alijaribiwa na Shetani, na kwamba alisimama imara katika ushuhuda wake wakati wa jaribu hili, ni bora zaidi kusema kwamba katika majaribio hayo yaliyokuwa mbele yake kutoka kwa Mungu, Ayubu alianza kuwa katika mapambano na Shetani ili kuulinda ukamilifu na unyoofu wake, kulinda njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Katika mapambano haya, Ayubu alipoteza kundi kubwa sana la kondoo na ng’ombe, alipoteza mali yake yote na watoto wake wa kike na kiume. Hata hivyo, hakuacha ukamilifu, unyofu, au hali yake ya kumcha Mungu. Kwa maneno mengine, katika pambano hili na Shetani alipendelea kunyang’anywa mali na watoto kuliko kupoteza ukamilifu, unyofu na hali yake ya kumcha Mungu. Alipendelea kushikilia msingi wa maana ya kuwa binadamu. Maandiko yanatoa maelezo mafupi na sahihi ya mchakato mzima ambao Ayubu alipoteza mali zake, na pia yanaandika mwenendo na mtazamo wa Ayubu. Maelezo haya mafupi, na ya wazi yanatoa maana ya kwamba Ayubu alikuwa na utulivu katika kukabiliana na jaribu hili, lakini ikiwa kile kilichotokea kingeundwa upya—na kuongezea pia asili yenye nia mbaya ya Shetani—basi mambo yasingekuwa rahisi au mepesi kama yalivyofafanuliwa kwenye sentensi hizi. Uhalisia ulikuwa wenye ukatili zaidi. Hicho ndicho kiwango cha uharibifu na chuki ambayo Shetani huwashughulikia wanadamu na wale wote wanaoidhinishwa na Mungu. Kama Mungu asingekuwa Amemwambia Shetani asimdhuru Ayubu, bila shaka Shetani angemuua bila sababu yoyote. Shetani hataki mtu yeyote amwabudu Mungu, wala hawataki wale wenye haki machoni pa Mungu na wale walio wakamilifu na wanyoofu waweze kuendelea kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Kwa watu kumcha Mungu na kujiepusha maovu kunamaanisha kwamba wanajiepusha na kumwacha Shetani, na hivyo Shetani alitumia fursa ya ruhusa ya Mungu kukusanya hasira yake na chuki yake yote juu yake Ayubu bila huruma. Unaona, basi, jinsi mateso aliyoyapitia Ayubu yalivyokuwa makubwa, kuanzia akilini hadi mwilini, kutoka nje hadi ndani. Leo, hatuoni jinsi ilivyokuwa kwa wakati huo, na tunaweza tu kupata, kutoka kwenye maelezo ya Biblia, muhtasari kwa ufupi wa hisia za Ayubu alipokuwa akipitia yale mateso kwa wakati huo.

Uadilifu Thabiti wa Ayubu Unamletea Aibu Shetani na Kusababisha Shetani Akimbie kwa Hofu

Kwa hivyo, ni nini ambacho Mungu alifanya wakati Ayubu alipokuwa anapitia mateso hayo? Mungu aliangalia, na kutazama, na Akasubiri matokeo. Mungu Alipokuwa akiangalia na kutazama, je, Alijihisi vipi? Alijihisi kuwa mwenye huzuni, bila shaka. Lakini, kutokana na huzuni Yake, je, Aliweza kujutia ruhusa Yake kwa Shetani ya kumjaribu Ayubu? Jibu ni, Hapana, Asingeweza kujutia. Kwani Yeye aliamini kwa uhakika kwamba Ayubu alikuwa mkamilifu na mnyofu, kwamba alimcha Mungu na kujiepusha na maovu. Mungu alikuwa amempa Shetani nafasi ya kuthibitisha uhaki wa Ayubu mbele ya Mungu, na kufichua uovu wake na kudharauliwa kwake. Zaidi ya hayo, ilikuwa ni fursa kwa Ayubu kushuhudia uhaki wake na kumcha Mungu kwake na kujiepusha na maovu mbele ya watu wa ulimwengu, Shetani, na hata wale wanaomfuata Mungu. Je, matokeo ya mwisho yalithibitisha kwamba tathmini ya Mungu kumhusu Ayubu ilikuwa sahihi na isiyo na makosa? Je, Ayubu alimshinda Shetani kweli? Hapa tunasoma maneno halisi yaliyonenwa na Ayubu, maneno ambayo ni uthibitisho kwamba alikuwa amemshinda Shetani. Alisema: “Nilitoka kwa tumbo la mama yangu nikiwa uchi, na mimi nitarudi huko nikiwa uchi.” Huu ndio mtazamo wa Ayubu wa utiifu kwa Mungu. Kisha, akasema: “Yehova alinipa, na Yehova amechukua; jina la Yehova libarikiwe.” Maneno haya yaliyozungumzwa na Ayubu yanathibitisha kwamba Mungu anaangalia katika kina cha moyo wa mwanadamu, kwamba Anaweza kuona kwenye akili ya mwandamu, na yanathibitisha kwamba kumuidhinisha Kwake Ayubu hakukuwa na kosa, kwamba mwanadamu huyu aliyeidhinishwa na Mungu alikuwa mwenye haki. “Yehova alinipa, na Yehova amechukua; jina la Yehova libarikiwe.” Maneno haya ni ushuhuda wa Ayubu kwa Mungu. Yalikuwa ni maneno haya ya kawaida yaliyomfanya Shetani ashituke, ambayo yalimletea aibu na kumsababisha akimbie kwa hofu kubwa, na, vilevile, ndio, yaliyomfunga pingu Shetani na kumuacha bila rasilimali zozote. Hivyo, pia, ndivyo maneno haya yalivyomfanya Shetani kuhisi matendo ya kustaajabisha na yenye nguvu ya Yehova Mungu, na kumruhusu kutambua haiba isiyo ya kawaida ya mtu ambaye moyo wake ulitawaliwa na njia ya Mungu. Zaidi ya hayo, yalimwonyesha Shetani nguvu za kipekee zilizoonyeshwa na mtu mdogo asiyekuwa na umuhimu wowote katika kushikamana na njia ya kumcha Mungu na kuepukana na uovu. Hivyo, Shetani alishindwa katika pambano la kwanza. Licha ya kuwa “amejifunza kutokana na hili,” Shetani hakuwa na nia ya kumwachilia Ayubu, wala hakukuwa na badiliko lolote katika asili yake yenye nia mbaya. Shetani alijaribu kuendelea kumshambulia Ayubu, na kwa mara nyingine tena akamjia Mungu …

Kisha, hebu tuyasome maandiko kuhusu mara ya pili ambapo Ayubu alijaribiwa.

3. Shetani Amjaribu Ayubu kwa Mara Nyingine Tena (Majipu Mabaya Yaupiga Mwili wa Ayubu)

a. Maneno Yaliyotamkwa na Mungu

Ayubu 2:3 Naye Yehova akamwuliza Shetani, je, umemfikiria mtumishi Wangu Ayubu, kwamba hakuna hata mtu kama yeye duniani, mtu mtimilifu na mwaminifu, ambaye anamcha Mungu, na kuepuka maovu? Na bado anashikilia ukamilifu wake, ingawa ulinichochea dhidi yake, ili mimi nimwangamize bila sababu.

Ayubu 2:6 Naye Yehova akamwambia Shetani, Tazama, yeye yuko katika mkono wako; lakini uuhifadhi uhai wake.

b. Maneno Yaliyotamkwa na Shetani

Ayubu 2:4-5 Naye Shetani akamjibu Yehova, na akasema, Ngozi kwa ngozi, ndiyo, yote ambayo mtu anayo atayatoa kwa sababu ya uhai wake. Lakini nyosha mbele mkono Wako sasa, na uguse mfupa wake na nyama yake, na yeye atakulaani mbele ya uso Wako.

c. Jinsi Ayubu Anavyokabiliana Majaribio

Ayubu 2:9-10 Kisha mkewe akasema kwake, Je, Wewe bado unabaki na ukamilifu wako? mlaani Mungu, ufe. Lakini yeye akasema kwake, Wewe unazungumza mithili ya mmoja wa wanawake walio wapumbavu wanavyozungumza. Ati? tupokee mema kutoka mkononi mwa Mungu, nasi tusipokee mabaya? Katika yote haya Ayubu hakutenda dhambi kwa midomo yake.

Ayubu 3:3-4 Itokomee mbali hiyo siku ambayo nilizaliwa, na huo usiku ambapo ulisemwa, Kuna mtoto mume ameingia katika mimba. Siku ile iwe na kiza; Mungu na asiitazame kutoka juu, wala nuru iiangazie.

Upendo wa Ayubu wa Njia ya Mungu Unazidi Kitu Kingine Chochote

Maandiko yanarekodi maneno haya yaliyozungumzwa kati ya Mungu na Shetani: “Naye Yehova akasema kwa Shetani, je, umemfikiria mtumishi Wangu Ayubu, kwamba hakuna hata mtu kama yeye duniani, mtu mtimilifu na mwaminifu, ambaye anamcha Mungu, na kuepuka maovu? Na bado anashikilia ukamilifu wake, ingawa ulinichochea dhidi yake, ili mimi nimwangamize bila sababu” (Ayubu 2:3). Katika mazungumzo haya, Mungu anarudia swali lile lile kwa Shetani. Ni swali linalotuonyesha tathmini ya uthibitisho wa Yehova Mungu kwa yale ambayo Ayubu alidhihirisha na kuyaishi wakati wa jaribio la kwanza, na swali ambalo si tofauti na tathmini ya Mungu juu ya Ayubu kabla hajajaribiwa na Shetani. Hivyo ni kusema, kabla ya majaribu kumjia, machoni pa Mungu Ayubu alikuwa mkamilifu, na hivyo Mungu alimlinda yeye na familia yake, na Akambariki; alistahili kubarikiwa machoni pa Mungu. Baada ya jaribu hilo, Ayubu hakutenda dhambi kwa midomo yake kwa sababu alikuwa amepoteza mali yake na watoto wake, lakini aliendelea kulisifu jina la Yehova. Mwenendo wake halisi ulimfanya Mungu ampongeze, na kumpa alama zote. Kwa maana machoni pa Ayubu, uzao wake au mali zake hazikutosha kumfanya amkane Mungu. Nafasi ya Mungu katika moyo wake, kwa maneno mengine, haikuweza kubadilishwa na watoto wake au sehemu yoyote ya mali. Wakati wa jaribu la kwanza la Ayubu, alimwonyesha Mungu kwamba upendo wake Kwake na upendo wake wa njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu ulizidi kila kitu kingine. Ni kwamba tu jaribio hili lilimpa Ayubu uzoefu wa kupokea thawabu kutoka kwa Yehova Mungu na kufanya mali yake na watoto wake kuchukuliwa na Yeye.

Kwa Ayubu, huu ulikuwa uzoefu wa kweli na ambao uliisafisha nafsi yake ikawa safi; ulikuwa ni ubatizo wa maisha uliotimiza kuwepo kwake, na, isitoshe, ilikuwa ni karamu yenye thamani iliyojaribu utiifu wake, na uchaji wake kwa Mungu. Jaribu hilo lilibadilisha hadhi ya Ayubu kutoka kuwa mtu tajiri hadi kuwa mtu ambaye hakuwa na chochote, na pia lilimwezesha kuona jinsi Shetani anavyowanyanyasa wanadamu. Ufukara wake haukumfanya amchukie Shetani; badala yake, katika matendo maovu ya Shetani aliona ubaya na kudharauliwa kwa Shetani, pamoja na uadui na uasi wa Shetani kwa Mungu, na hilo lilimtia moyo zaidi kushikilia daima njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Aliapa kwamba asingewahi kumwacha Mungu na kuigeuka njia ya Mungu kwa sababu ya mambo ya nje kama vile mali, watoto au jamaa zake, wala hangewahi kuwa mtumwa wa Shetani, mali, au mtu yeyote; mbali na Yehova Mungu, hakuna mtu ambaye angekuwa Bwana wake, au Mungu wake. Hayo ndiyo yaliyokuwa maazimio ya Ayubu. Kwa upande mwingine wa majaribu, Ayubu pia alipata kitu: Ayubu alipata mengi sana kutokana na majaribio hayo aliyoyapitia kutoka kwa Mungu.

Wakati wa maisha yake katika miongo kadhaa iliyopita, Ayubu aliyaona matendo ya Yehova na kupata baraka za Yehova Mungu kwake. Zilikuwa ni baraka zilizomwacha akihisi wasiwasi mkubwa na mwenye wingi wa shukrani, kwani aliamini kwamba alikuwa hajamfanyia chochote Mungu, ilhali alikuwa amepata baraka nyingi na akawa anafurahia neema nyingi. Kwa sababu hii, mara nyingi aliomba moyoni mwake, akitumaini kwamba angeweza kumlipa Mungu, akitumaini kwamba angekuwa na fursa ya kutoa ushuhuda wa matendo na ukuu wa Mungu, na akitumaini kwamba Mungu angeweza kuujaribu utiifu wake, na, zaidi, kwamba imani yake ingetakaswa, mpaka pale ambapo utiifu wake na imani yake vingepata idhini ya Mungu. Na wakati Ayubu alipojaribiwa, alisadiki kwamba Mungu alikuwa amesikia maombi yake. Ayubu alifurahia sana fursa hii zaidi ya kitu kingine chochote, na hivyo basi hakuthubutu kuchukulia jambo hili kirahisi, kwani tamanio kubwa zaidi la maisha yake lingeweza kutimizwa. Kufika kwa fursa hii kulimaanisha kwamba utiifu na uchaji wake kwa Mungu ungeweza kujaribiwa, na kutakaswa. Zaidi, ilimaanisha kwamba Ayubu alikuwa na fursa ya kupata idhini ya Mungu, hivyo kumleta karibu zaidi na Mungu. Wakati wa jaribio, imani na ufuatiliaji kama huo ulimruhusu kuwa mtimilifu zaidi, na kupata uelewa mkubwa zaidi wa mapenzi ya Mungu. Ayubu pia alikuwa mwenye shukrani zaidi kwa baraka na neema za Mungu, katika moyo wake alimimina sifa nyingi zaidi kwa matendo ya Mungu, na alizidi kumcha Mungu na kumstahi, na kutamani hata zaidi upendo, ukuu, na utakatifu wa Mungu. Kwa wakati huu, ingawa Ayubu alikuwa bado ni mtu ambaye alimcha Mungu na kujiepusha na maovu machoni pa Mungu, kuhusiana na yale aliyoyapitia, imani na maarifa ya Ayubu yalikuwa yameongezeka kwa haraka sana: imani yake ilikuwa imeongezeka, utiifu wake ulikuwa umepata msingi, na uchaji wake kwa Mungu ulikuwa umeongezeka zaidi. Ingawa jaribio hili lilibadilisha roho na maisha ya Ayubu, mabadiliko kama hayo hayakumtosheleza Ayubu, wala hayakumcheleweshea maendeleo yake. Wakati huo huo, alipokuwa akifikiria yale aliyokuwa ameyapata kutokana na jaribio hilo, na akizingatia mapungufu yake mwenyewe, aliomba kimyakimya, akingojea jaribio linalofuata limjie, kwa sababu alitamani sana imani yake, utiifu, na uchaji wake kwa Mungu viweze kuimarishwa kwenye jaribio linalofuata la Mungu.

Mungu Anaziangalia fikira za ndani zaidi za binadamu na yale yote ambayo binadamu anasema na kufanya. Fikira za Ayubu zilifikia masikio ya Yehova Mungu, na Mungu alisikiliza maombi yake na kwa njia hii jaribio la Mungu kwa Ayubu lililofuata liliwasili kama lilivyotarajiwa.

Katikati ya Mateso makuu, Ayubu Anatambua kwa Kweli Utunzaji wa Mungu kwa Wanadamu

Kufuatia maswali ya Yehova Mungu kwa Shetani, Shetani alifurahi kisirisiri. Kwa sababu Shetani alijua kwamba angeweza kwa mara nyingine kuruhusiwa kumshambulia mtu aliyekuwa mkamilifu machoni pa Mungu—jambo ambalo kwa Shetani lilikuwa fursa ya nadra sana. Shetani alitaka kutumia fursa hii ili kudhoofisha kabisa msimamo wa Ayubu ili kumfanya apoteze imani yake kwa Mungu na hivyo basi asimche Mungu tena au kulibariki jina la Yehova. Hali hii ingempa Shetani fursa: Haijalishi ni wapi au ni muda gani, angeweza kumfanya Ayubu kuwa kikaragosi cha kufuata amri zake. Shetani alificha njama zake za maovu bila kuacha alama, lakini hakuweza kudhibiti asili yake ya maovu. Ukweli huu unadokezwa katika majibu yake kwa maneno ya Yehova Mungu, kama yalivyorekodiwa kwenye maandiko. “Naye Shetani akamjibu Yehova, na akasema, Ngozi kwa ngozi, ndiyo, yote ambayo mtu anayo atayatoa kwa sababu ya uhai wake. Lakini nyosha mbele mkono Wako sasa, na uguse mfupa wake na nyama yake, na yeye atakulaani mbele ya uso Wako” (Ayubu 2:4-5). Haiwezekani kutopata maarifa muhimu na hisia yenye nia mbaya ya Shetani kutokana na mazungumzo haya kati ya Mungu na Shetani. Baada ya kusikia uongo huu wa Shetani, wale wote wanaoupenda ukweli na kuchukia uovu bila shaka watakuwa na chuki kubwa zaidi kwa ujinga na kutokuwa na aibu kwa Shetani, watahisi kushangazwa na kuchukizwa na udanganyifu wa Shetani, na, wakati huohuo, watatoa maombi yao ya kina na heri zao za dhati kwa Ayubu, wakiomba kwamba binadamu huyu mwenye unyofu aweze kufikia ukamilifu wake, wakitamani kwamba binadamu huyu anayemcha Mungu na kujiepusha na maovu aweze kushinda daima majaribu ya Shetani, na kuishi kwa mwangaza, na kuishi katikati ya mwongozo na baraka za Mungu, hivyo, pia ndivyo watakavyotamani matendo ya haki ya Ayubu yaweze daima kuenea na kuwahimiza wale wanaofuatilia njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Ingawa shauku yenye nia mbaya ya Shetani inaweza kuonekana kupitia kwa tangazo hili, Mungu alikubali kwa urahisi “ombi” la Shetani—lakini alikuwa pia na sharti moja: “Yeye yuko katika mkono wako; lakini uuhifadhi uhai wake” (Ayubu 2:6). Kwa sababu, kwa wakati huu, Shetani aliomba aunyooshe mkono wake ili adhuru mwili na mifupa ya Ayubu, Mungu Alisema, “lakini okoa maisha yake.” Maana ya maneno haya ni kwamba Alimpa tu Shetani mwili wa Ayubu, lakini Akabakiza uhai wake. Shetani asingeweza kuuchukua uhai wa Ayubu, lakini tofauti na hilo angeweza kutumia njia au mbinu zozote dhidi ya Ayubu.

Baada ya kupata ruhusa kutoka kwa Mungu, Shetani alimkimbilia Ayubu na kuunyosha mkono wake ili kuiathiri ngozi yake na akamsababishia majipu mabaya yaliyoupiga mwili wake wote, na Ayubu akahisi maumivu kwenye ngozi yake. Ayubu aliyasifu maajabu na utakatifu wa Yehova Mungu, jambo ambalo lilimfanya hata Shetani kuwa wazi zaidi katika ufidhuli wake. Kwa sababu alikuwa amehisi furaha ya kumwumiza binadamu, Shetani aliunyosha mkono wake na akakwaruza nyama ya Ayubu, na kusababisha majipu yake mabaya kutunga usaha. Mara moja Ayubu alihisi maumivu na mateso kwenye mwili wake ambayo hayakuwa na kifani, na asingeweza kujisaidia kwa vyovyote vile isipokuwa kujikanda yeye mwenyewe kutoka kichwani hadi miguuni akitumia mikono yake, ni kana kwamba kufanya hivi kungetuliza pigo lililoipata roho yake kutokana na maumivu haya ya nyama za mwili wake. Alitambua kwamba Mungu Alikuwa kando yake akimwangalia, na akajaribu kwa njia bora zaidi kujituliza. Kwa mara nyingine tena alipiga magoti chini, na kusema: “Unatazama ndani ya moyo wa mwanadamu, unaiona taabu yake; kwa nini udhaifu wake unakuhusu wewe? Jina la Yehova Mungu lisifiwe. Shetani aliyaona yale maumivu yasiyovumilika ya Ayubu, lakini hakumwona Ayubu akiliacha jina la Yehova Mungu. Hivyo aliunyoosha mkono wake kwaharaka ili aidhuru mifupa ya Ayubu, akitamani sana kudhuru kila kiungo cha mwili wake. Papo hapo, Ayubu alihisi mateso yasiyo na kifani; ilikuwa ni kana kwamba nyama yake imepasuliwa kutoka kwenye mifupa, na kana kwamba mifupa yake ilikuwa inavunjwa vipande vipande. Mateso haya ya uchungu yalimfanya afikirie ni bora kufa…. Uwezo wake wa kustahimili maumivu hayo ulikuwa umefikia kikomo…. Alitaka kulia, alitaka kuipasua ngozi ya mwili wake ili ajaribu kupunguza maumivu—lakini alizuia kilio chake, wala hakuirarua ngozi ya mwili wake, kwani hakutaka Shetani auone udhaifu wake. Na hivyo alipiga magoti chini kwa mara nyingine tena, lakini kwa wakati huu hakuhisi uwepo wa Yehova Mungu. Alijua kwamba mara nyingi Alikuwa mbele yake, na nyuma yake, na upande wake. Lakini kwenye maumivu haya, Mungu hakuwahi kuyatazama hata mara moja; Aliufunika uso Wake na Akauficha, kwani sababu ya uumbaji Wake wa mwanadamu haikuwa kuleta mateso juu ya mwanadamu. Kwa wakati huu, Ayubu alikuwa akilia, na akijitahidi kadri awezayo kuvumilia maumivu yake ya kimwili, hata hivyo asingeweza tena kujizuia kutoa shukrani kwa Mungu: “Mwanadamu huanguka kwa pigo la kwanza, yeye ni dhaifu na asiye na nguvu, yeye ni mdogo na asiyejua—kwa nini Ungependa kuwa mwenye kumjali na mwenye huruma kwake ? Unanipiga, ilhali inakuumiza kufanya hivyo. Ni nini cha binadamu kinastahili utunzaji na kujali Kwako? Maombi ya Ayubu yalifikia masikio ya Mungu, na Mungu Alikuwa kimya, Akitazama tu bila kutoa sauti.… Baada ya Shetani kujaribu kila ujanja kwenye kitabu bila mafanikio aliondoka kimyakimya, lakini hilo halikuhitimisha majaribio ya Ayubu kutoka kwa Mungu. Kwa sababu nguvu za Mungu zilizokuwa zimefichuliwa ndani ya Ayubu zilikuwa hazijawekwa wazi, hadithi ya Ayubu haikuishia pale ambapo Shetani alijiondoa. Wahusika wengine walipoingia, matukio ya kuvutia zaidi yalikuwa bado yanakuja.

Udhihirisho 0000Mwingine wa Kumcha Mungu na Kujiepusha na Maovu kwa Ayubu ni Kusifu Kwake Jina la Mungu Katika Mambo Yote

Ayubu alikuwa ameteseka kutokana na uharibifu wa Shetani, lakini bado hakuliacha jina la Yehova Mungu. Mke wake ndiye aliyekuwa wa kwanza kujitokeza na akasimama nafasi ya Shetani katika umbo linaloonekana kwa macho ya kibinadamu, akamshambulia Ayubu. Maandiko halisi yanaeleza hivi: “Kisha mkewe akasema kwake, Je, Wewe bado unabaki na ukamilifu wako? mlaani Mungu, ufe” (Ayubu2:9). Haya yalikuwa maneno yaliyozungumzwa na Shetani katika sura ya mwanadamu. Yalikuwa ni mashambulizi, na mashtaka, na vilevile ni kishawishi, jaribu, na kashfa. Baada ya kushindwa kuushambulia mwili wa Ayubu, Shetani sasa alishambulia moja kwa moja uadilifu wa Ayubu, akitaka kutumia jambo hili kumfanya Ayubu aache uadilifu wake, amkane Mungu, na asiendelee kuishi tena. Hivyo, pia, ndivyo Shetani alivyotaka kuyatumia maneno kama hayo kumjaribu Ayubu: Kama Ayubu angeacha jina la Yehova, kisha asingelazimika kuvumilia mateso kama hayo; yeye angejiondolea mateso ya mwili. Akiwa amekabiliwa na ushauri wa mke wake, Ayubu alimkosoa kwa kusema, “Wewe unazungumza mithili ya mmoja wa wanawake walio wapumbavu wanavyozungumza. Ati? tupokee mema kutoka mkononi mwa Mungu, nasi tusipokee mabaya?” (Ayubu 2:10). Ayubu alikuwa amejua kwa muda mrefu maneno haya, lakini kwa wakati huu ukweli wa maarifa ya Ayubu kuhusu maneno haya ulikuwa umethibitishwa.

Wakati mke wake alimshauri amlaani Mungu na afe, maana yake ilikuwa: “Mungu wako anakutendea hivi, kwa hivyo kwa nini usimlaani Yeye? Kama ungali hai unafanya nini? Mungu wako hakutendei haki sana, lakinibado unasema ‘libarikiwe jina la Yehova’. Angewezaje kuleta msiba juu yako huku unalibariki jina Lake? Harakisha na uliache jina la Mungu, na usimfuate yeye tena. Kisha, matatizo yako yataisha.” Kwa wakati huu, ushuhuda ulitolewa ambao Mungu alitaka kuuona kwa Ayubu. Hakuna mtu yeyote wa kawaida ambaye angeweza kuwa na ushuhuda huu, wala hatuusomi katika hadithi zozote za Biblia—lakini Mungu Alikuwa ameuona kabla hata Ayubu hajaongea maneno haya. Mungu Alitaka tu kutumia fursa hii kumruhusu Ayubu kuthibitisha kwa wote kwamba Mungu alikuwa sahihi. Akiwa amekabiliwa na ushauri wa mke wake, sio tu kwamba Ayubu hakuacha udilifu wake wala hakumkana Mungu, bali pia alimwambia mke wake: “Tupokee mema kutoka mkononi mwa Mungu, nasi tusipokee mabaya?” Je, maneno haya yana uzito mkubwa? Hapa, kuna ukweli mmoja tu unaoweza kuthibitisha uzito wa maneno haya. Uzito wa maneno haya ni kwamba yameidhinishwa na Mungu ndani ya moyo Wake, ndiyo yale yaliyotamaniwa na Mungu, ndiyo yale Mungu Alitaka kuyasikia, na ndiyo matokeo ambayo Mungu Alitamani kuyaona; maneno haya pia ndiyo kiini cha ushuhuda wa Ayubu. Katika hili, ukamilifu, unyofu, kumcha Mungu, kujiepusha na maovu kwa Ayubu kulithibitishwa. Thamani ya Ayubu ilikuwa namna ambavyo, alipojaribiwa, na hata wakati mwili wake mzima ulikuwa umefunikwa na majipu mabaya, alipovumilia mateso ya kiwango cha juu zaidi, na wakati mke wake najamaa zake walipomshauri, bado aliyatamka maneno kama hayo. Kwa kuiweka kwa njia nyingine, ndani ya moyo wake alisadiki kwamba, haijalishi ni majaribu ya aina gani, au ni vipi ambavyo dhiki au mateso yalivyokuwa makali, hata kama kifo kingemjia, hangemkana Mungu au kugeuka na kuacha kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Unaona, basi, kwamba Mungu Alishikilia sehemu muhimu sana ndani ya moyo wake, na kwamba kulikuwa tu na Mungu moyoni mwake. Ni kwa sababu ya haya ndipo tunasoma ufafanuzi kama huo kuhusu yeye katika maandiko kama vile: Katika yote haya Ayubu hakutenda dhambi kwa midomo yake. Hakutenda dhambi kwa kutumia mdomo wake tu, lakini ndani ya moyo wake hakulalamika katu kuhusu Mungu. Hakusema maneno mabaya kuhusu Mungu, wala hakutenda dhambi dhidi ya Mungu. Sio tu kwamba kinywa chake kilibariki jina la Mungu, lakini moyoni mwake pia alilibariki jina la Mungu; kinywa chake na moyo wake vilikuwa kitu kimoja. Huyu ndiye aliyekuwa Ayubu wa kweli aliyeonekana na Mungu, na hii ndiyo iliyokuwa sababu ya kweli kwa nini Mungu alimthamini sana Ayubu.

Kuelewa Visivyo Kwingi Kwa Watu Kuhusu Ayubu

Ugumu aliopitia Ayubu haukuwa kazi ya wajumbe waliotumwa na Mungu, wala haukusababishwa na mkono wa Mungu mwenyewe. Badala yake, ulisababishwa na Shetani mwenyewe, adui wa Mungu. Hivyo basi, kiwango cha ugumu alioupitia Ayubu kilikuwa kikubwa. Ilhali kwa wakati huo Ayubu alionyesha, kwa moyo mkunjufu, maarifa yake ya kila siku kumhusu Mungu ndani ya moyo wake, kanuni za matendo yake ya kila siku, na mtazamo wake kwa Mungu—na huu ndio ukweli. Kama Ayubu hangekuwa amejaribiwa, kama Mungu Asingekuwa Amemletea Ayubu majaribio, wakati Ayubu aliposema, “Yehova alinipa, na Yehova amechukua; jina la Yehova libarikiwe,” ungesema kwamba Ayubu alikuwa mnafiki; Mungu alikuwa amempa mali nyingi sana, kwa hivyo bila shaka alilibariki jina la Yehova. Kama, kabla ya kupitia majaribio, Ayubu angekuwa amesema, “Tupokee mema kutoka mkononi mwa Mungu, nasi tusipokee mabaya?” Ungesema kwamba Ayubu alikuwa akitia chumvi, na kwamba hangeliacha jina la Mungu kwa sababu mara nyingi alibarikiwa kwa mkono wa Mungu. Kama Mungu Angekuwa Amemletea janga, basi kwa kweli angeliacha jina la Mungu. Lakini wakati Ayubu alipojikuta katika hali hizi ambazo hakuna mtu yeyote ambaye angezitamani au kutaka kuona, au kutaka zimpate, ambazo watu wangeogopa kupata, hali ambazo hata Mungu mwenyewe Hakuweza kuvumilia kuzitazama, bado Ayubu aliweza kushikilia uadilifu wake: “Yehova alinipa, na Yehova amechukua; jina la Yehova libarikiwe” na “tupokee mema kutoka mkononi mwa Mungu, nasi tusipokee mabaya?” Kama wangekumbwa na mwenendo wa Ayubu kwa wakati huu, wale wanaopenda kuzungumza maneno ya kuvutia, na wale wanaopenda kuongea barua na mafundisho ya kidini, wote wanaachwa bila usemi. Wale wanaotukuza jina la Mungu kwa matamshi pekee, ilhali hawajawahi kukubali majaribio ya Mungu, wanashutumiwa na uadilifu ambao Ayubu alishikilia kwa dhati, na wale ambao hawajawahi kusadiki kwamba binadamu anaweza kushikilia kwa dhati njia ya Mungu wanahukumiwa na ushuhuda wa Ayubu. Wakiwa wamekabiliwa na mwenendo wa Ayubu wakati wa majaribio haya na maneno aliyoyaongea, baadhi ya watu watahisi wamechanganyikiwa, baadhi watamwonea wivu, baadhi wtaahisi mashaka, baadhi wataonekana hata wasio na haja ya kufuatilia mambo haya, huku wakiukataa ushuhuda wa Ayubu kwa sababu sio tu kwamba hawayaoni mateso yaliyompata Ayubu wakati wa majaribio, na kusoma maneno yaliyozungumzwa na Ayubu, bali wanaona tu ule “udhaifu” wa kibinadamu ulioonyeshwa na Ayubu wakati majaribio yalipomjia. “Udhaifu” huu wanaamini kuwa ni kutokukamilika kwa ukamilifu wa Ayubu, ni doa kwa mwanadamu ambaye machoni pa Mungu alikuwa mkamilifu. Hivi ni kusema kwamba, inaaminika kuwa wale ambao ni wakamilifu hawana dosari, hawana doa au uchafu, kwamba hawana udhaifu, hawajui chochote kuhusu maumivu, kwamba hawajawahi kuhisi huzuni au kuvunjika moyo, na hawana chuki au tabia yoyote ya nje isiyofaa; kutokana na haya, watu wengi sana hawaamini kwamba Ayubu alikuwa mkamilifu kweli. Watu hawaidhinishi mambo mengi kuhusu tabia yake wakati wa majaribio yake. Kwa mfano, wakati Ayubu alipopoteza mali zake na watoto wake, hakuweza, kuanza kulia, kama vile watu wanavyofikiria. “Utovu wake wa nidhamu” unawafanya watu kufikiria kwamba hakuwa na hisia, kwa kuwa hakutokwa na machozi au kuwa na hisia za kujali kwa familia yake. Hii ndiyo picha mbaya ya kwanza ambayo watu wanayo kuhusu Ayubu. Wanafikiri tabia yake baada ya hapo kuwa ya kutatanisha zaidi: “akalipasua joho lake” ni kauli iliyotafsiriwa na watu kuonyesha ukosefu wake wa heshima kwa Mungu, na “kunyoa kichwa chake” inaaminika visivyo kuwa inamaanisha kukufuru kwa Ayubu na upinzani wake kwa Mungu. Mbali na maneno ya Ayubu kwamba “Yehova alinipa, na Yehova amechukua; jina la Yehova libarikiwe,” watu hawatambui uhaki wowote ndani ya Ayubu ambao ulisifiwa na Mungu, na hivyo tathmini kuhusu Ayubu iliyofanywa na wengi wao kati yao si chochote zaidi ya kutofahamu, kutokuelewa, mashaka, shutuma, na idhinisho katika nadharia tu. Hakuna kati yao anayeweza kuelewa na kufahamu kwa kweli maneno ya Yehova Mungu kwamba Ayubu alikuwa binadamu mkamilifu na mnyofu, yule aliyemcha Mungu na kujiepusha na maovu.

Kulingana na maoni yao kuhusu Ayubu hapo juu, watu wana mashaka zaidi kuhusiana na uhaki wake, kwani matendo ya Ayubu na mwenendo wake uliorekodiwa katika maandiko haukuwa wenye mguso wa kina kama vile ambavyo watu wangefikiria. Sio tu kwamba hakufanya jambo lolote kubwa, bali pia alichukua kigae ili ajikwangue akiwa amekaa katikati ya majivu. Kitendo hiki pia kinawashangaza watu na kuwafanya wautilie mashaka—na hata kuukataa—uhaki wa Ayubu, kwani wakati akijikwangua Ayubu hakumwomba Mungu, au kutoa ahadi kwa Mungu; wala, zaidi ya hayo, hakuonekana akilia machozi ya uchungu. Wakati huu, watu wanaona tu udhaifu wa Ayubu na si kitu kingine chochote, na hivyo hata wanapomsikia Ayubu akisema “Tupokee mema kutoka mkononi mwa Mungu, nasi tusipokee mabaya?” hawaguswi kamwe, au vinginevyo hawaonekani kuamua chochote, na bado hawawezi kutambua uhaki wa Ayubu kutoka kwa maneno haya. Picha ya msingi ambayo Ayubu anapatia watu wakati wa mateso ya majaribio yake ni kwamba hakuwa mwenye wasiwasi wala mwenye kiburi. Watu hawaioni hadithi inayotokana na tabia yake iliyojitokeza katika kina cha moyo wake, wala hawaioni ile hali yake ya kumcha Mungu ndani ya moyo wake au kushikamana kwake kanuni ya njia ya kujiepusha na maovu. Utulivu wake unawafanya watu kufikiria kuwa ukamilifu na unyofu wake vyote vilikuwa ni maneno matupu tu, kwamba kumcha kwake Mungu kulikuwa ni uvumi tu; ule “udhaifu” alioufichua kwa nje, wakati huo, unawaachia picha ya kina, ukiwapatia “mtazamo mpya” na hata “uelewa mpya” kuhusu binadamu yule ambaye Mungu anamfafanua kuwa mkamilifu na mnyofu. “Mtazamo mpya” na “uelewa mpya” kama huo vyote vinathibitishwa wakati Ayubu alipofungua kichwa chake na kulaani siku aliyozaliwa.

Ingawa kiwango cha mateso aliyoyapitia hakifikiriki wala kufahamika kwa binadamu yeyote, hakuzungumza maneno yoyote ya uzushi, lakini alipunguza tu maumivu ya mwili wake kwa njia zake mwenyewe. Kama ilivyorekodiwa kwenye maandiko, alisema: “Itokomee mbali hiyo siku ambayo nilizaliwa, na huo usiku ambapo ulisemwa, Kuna mtoto mume ameingia katika mimba” (Ayubu 3:3). Pengine, hakuna yeyote aliyewahi kuyazingatia maneno haya na kuona kwamba ni muhimu, na pengine kunao watu ambao wameyazingatia. Kwa maoni yenu, je,, yanamaanisha kwamba Ayubu alimpinga Mungu? Je, ni malalamiko dhidi ya Mungu? Najua kwamba wengi wenu mna mawazo fulani kuhusu maneno haya yaliyozungumzwa na Ayubu na mnasadiki kwamba kama Ayubu alikuwa mkamilifu na mnyofu, hakupaswa kuonyesha udhaifu wowote au huzuni yoyote, na badala yake alifaa kukabiliana vilivyo na shambulizi lolote kutoka kwa Shetani kwa njia nzuri, na hata kutabasamu wakati alikumbwa na majaribu ya Shetani. Hakupaswa kuwa na mwitikio hata mdogo kuhusiana na mateso aliyoyapata kwenye mwili wake kutokana na Shetani, wala hakupswa kuonyesha hisia zozote ndani ya moyo wake. Alipaswa hata kumwomba Mungu Ayafanye majaribio haya kuwa mabaya zaidi. Haya ndiyo yanayofaa kudhihirishwa na kumilikiwa na mtu ambaye ni thabiti na ambaye anamcha Mungu kwa kweli na kujiepusha na maovu. Katikati ya mateso hayo makali, Ayubu hakufanya chochote ila kuiaani siku aliyozaliwa. Hakulalamika kuhusu Mungu, hakuwa na nia yoyote ya kumpinga Mungu. Hili ni rahisi zaidi kusema kuliko kutenda, kwani tangu enzi za zamani hadi kufikia leo, hakuna yeyote ambaye amewahi kupitia majaribiu kama hayo au kuteseka kama vile Ayubu alivyoteseka. Na kwa nini hakuna yeyote ambaye amepitia aina hiyo ya majaribi kama ya Ayubu? Ni kwa sababu, jinsi Mungu Anavyoona, hakuna yeyote anayeweza kuvumilia wajibu au agizo kama hilo, hakuna anayeweza kufanya kama Ayubu alivyofanya, na, zaidi ya hayo, hakuna mtu ambaye angeweza bado, mbali na kuilaani siku ya kuzaliwa kwake, asiachilie jina la Mungu na kuendelea kubariki jina la Yehova Mungu, kama vile Ayubu alivyofanya wakati mateso kama hayo yalipompata. Je, kuna mtu yeyote anayeweza kufanya hivi? Tunaposema haya kuhusu Ayubu, je, tunaipongeza tabia yake? Alikuwa binadamu mwenye haki, na aliyeweza kuwa na ushuhuda kama huo kwa Mungu, aliyeweza kumfanya Shetani akimbie akiwa na kichwa chake mikononi mwake, ili kwamba asiwahi tena kuja mbele za Mungu akimshitaki—kwa hivyo kuna ubaya wa kumpongeza? Je, yawezekana kwamba mna viwango vya juu zaidi kuliko Mungu? Je, inaweza kuwa kwamba ungetenda vyema zaidi kuliko Ayubu wakati majaribu yanapokuja juu yako? Ayubu alisifiwa na Mungu—unaweza kuwa na vipingamizi gani?

Ayubu Anailaani Siku Ya Kuzaliwa Kwake Kwa Sababu Hataki Mungu Apate Maumivu Kwa Sababu Yake

Mara nyingi Ninasema kwamba Mungu hutazama ndani ya mioyo ya watu, na watu hutazama jinsi watu walivyo kwa nje. Kwa sababu Mungu anaangalia ndani ya mioyo ya watu, Anaelewa kiini chao, huku nao watu wanafafanua viini vya watu wengine kutokana na wanavyoonekana kwa nje. Wakati Ayubu alipofungua kinywa chake na kuilaani siku ya kuzaliwa kwake, kitendo hiki kiliwashangaza watu wote wa kiroho, wakiwemo wale marafiki watatu wa Ayubu. Mwanadamu alitoka kwa Mungu, na anapaswa kushukuru kwa uhai na mwili, na vile vile siku ya kuzaliwa kwake, aliyopewa na Mungu, na hapaswi kuilaani. Hili ni jambo ambalo watu wa kawaida wanaweza kuelewa na kufikiria. Kwa yeyote yule anayemfuata Mungu, ufahamu huu ni mtakatifu na hauwezi kukiukwa, na ni ukweli ambao kamwe hauwezi kubadilika. Ayubu, kwa upande mwingine, alizivunja sheria: Aliilaani siku ya kuzaliwa kwake. Hiki ni kitendo ambacho watu wa kawaida huchukulia kuwa kinajumuisha kuvuka hadi kwenye eneo lililokatazwa. Sio tu kwamba Ayubu hastahili uelewa na huruma ya watu, lakini pia hastahili msamaha wa Mungu. Wakati huohuo, hata watu wengi zaidi wanatilia mashaka uhaki wa Ayubu, kwa kuwa inaonekana ni kana kwamba kibali cha Mungu kwake kilimfanya Ayubu ajiachie, kilimfanya kuwa jasiri sana na asiyejali kiasi cha kwamba sio tu hakuweza kumshukuru Mungu kwa kumbariki na kumtunza kipindi cha maisha yake, lakini pia aliilaani siku ya kuzaliwa kwake na kuomba kwamba ingefutiliwa mbali. Je, hii ni nini, kama sio kumpinga Mungu? Mambo hayo ya kijuujuu yanawapa watu uthibitisho wa kushutumu kitendo hiki cha Ayubu, lakini je, ni nani anayejua kile ambacho Ayubu alikuwa akifikiria kwa kweli kwa wakati huo? Na je, ni nani anayeweza kujua sababu ya Ayubu kufanya hivyo? Ni Mungu pekee na Ayubu mwenyewe ndio wanaojua hadithi ya ndani na sababu husika hapa.

Shetani alipounyosha mkono wake ili aidhuru mifupa ya Ayubu, Ayubu alianguka katika mashiko yake, bila kuwa na mbinu za kutoroka au nguvu za kumpinga. Mwili wake na nafsi yake vilipitia maumivu makali sana, na maumivu haya yalimfanya atambue kwa undani kutokuwa na umuhimu, udhaifu, na kutokuwa na nguvu kwa mwanadamu anayeishi katika mwili. Wakati huohuo, alipata ufahamu na uelewa mkubwa wa kwa nini Mungu anazingatia kuwajali na kuwatunza wanadamu. Akiwa ameanguka katika makucha ya Shetani, Ayubu alitambua kwamba binadamu, aliye katika mwili na damu, kwa hakika hana nguvu na ni mdhaifu. Wakati aliposujudu na kumwomba Mungu, alihisi ni kana kwamba Mungu Alikuwa akiufunika uso Wake na kujificha, kwani Mungu Alikuwa Amemweka kabisa katika mikono ya Shetani. Wakati huohuo, Mungu pia Alilia kwa ajili yake, na, zaidi ya hayo, Alihuzunika kwa ajili yake; Mungu Aliumizwa na maumivu yake na Aliumia kwa kudhurika kwake.… Ayubu alihisi maumivu ya Mungu, pamoja na namna ambavyo haikuweza kuvumilika kwa Mungu.… Ayubu hakutaka kuleta huzuni zaidi kwa Mungu, wala hakutaka Mungu alie kwa ajili yake, isitoshe hakutaka kumwona Mungu akiwa katika maumivu kwa sababu yake. Kwa wakati huu, Ayubu alitaka tu ajiondoe mwenyewe kwenye mwili wake, ili asivumilie tena maumivu yaliyoletewa kwake kupitia kwa mwili wake, kwani kwa kufanya hivo kungesitisha Mungu kuteseka kwa maumivu yake—lakini hakuweza kufanya hivyo, na sio tu kwamba ilimbidi avumilie maumivu ya mwili, bali pia mateso ya kutotaka kumfanya Mungu kuwa na wasiwasi. Maumivu haya mawili—moja kutoka kwenye mwili, na mengine kutoka rohoni—yalimletea maumivu makali ya moyoni, na mateso makali kwa Ayubu, na kumfanya ahisi jinsi ambavyo mapungufu ya mwanadamu ambaye ni wa mwili na damu yanavyoweza kumfanya mtu ajihisi kuchanganyikiwa na kukosa msaada. Katika hali hizi, shauku yake kwa Mungu ilizidi kuongezeka sana, na chuki yake kwa Shetani ikazidi kuwa nyingi. Kwa wakati huu, Ayubu angependelea kuwa asigewahi kuzaliwa katika ulimwengu huu wa binadamu, ingekua ni afadhali asingekuwepo, kuliko kumuona Mungu Akilia au Akihisi maumivu kwa sababu yake. Alianza kuuchukia sana mwili wake, kujichukia yeye mwenyewe, kwa siku yake ya kuzaliwa, na hata kwa yote ambayo yalikuwa yanahusiana naye. Hakutaka tena kuwepo na kutajwa kokote zaidi kwa siku yake ya kuzaliwa au chochote kilichohusu siku hiyo, na hivyo alifungua kinywa chake na kuilaani siku yake ya kuzaliwa: “Itokomee mbali hiyo siku ambayo nilizaliwa, na huo usiku ambapo ulisemwa, Kuna mtoto mume ameingia katika mimba. Siku ile iwe na kiza; Mungu na asiitazame kutoka juu, wala nuru iiangazie” (Ayubu 3:3-4). Maneno ya Ayubu yanaonyesha kjiuchukia kwake mwenyewe, “Itokomee mbali hiyo siku ambayo nilizaliwa, na huo usiku ambapo ulisemwa, Kuna mtoto mume ameingia katika mimba,” pamoja na kujilaumu kwake mwenyewe na kuwa na hisia ya hatia kwa kumsababishia Mungu maumivu, “Siku hiyo na iwe giza; Mungu na asiitazame kutoka juu, wala nuru isiiangazie.” Vifungu hivi viwili ni maonyesho ya namna ambavyo Ayubu alijihisi kwa wakati huo, na vinaonyesha kikamilifu ukamilifu, “Siku ile iwe na kiza; Mungu na asiitazame kutoka juu, wala nuru iiangazie.” Vifungu hivi viwili ni maonyesho ya namna ambavyo Ayubu alijihisi kwa wakati huo, na vinaonyesha kikamilifu ukamilifu wake na unyofu wake kwa wote. Wakati huohuo, kama vile tu Ayubu alivyokuwa ametaka, imani na utiifu wake kwa Mungu, pamoja na kumcha Mungu kwake, vyote viliinuliwa kwa kweli. Bila shaka, kuinuliwa huku kwa hakika ni athari ambayo Mungu Alikuwa Ametarajia.

Ayubu Anamshinda Shetani na Kuwa Binadamu Wa Kweli Machoni pa Mungu

Wakati Ayubu alipopitia majaribio yake kwa mara ya kwanza, alinyang’anywa mali zake zote na watoto wake wote, lakini hakuanguka chini na kusema chochote ambacho kilikuwa dhambi dhidi ya Mungu kutokana na hayo. Alikuwa ameshinda majaribu ya Shetani, na alikuwa ameshinda mali zake za kimwili, uzao wake na jaribu la kupoteza mali zake zote za kidunia, ambayo ni kusema kwamba aliweza kumtii Mungu achukue kutoka kwake na akatoa shukrani na sifa kwa Mungu kwa sababu ya hayo. Hivyo ndivyo ulivyokuwa mwenendo wa Ayubu wakati wa jaribiu la kwanza la Shetani, na huo ndio uliokuwa ushuhuda wa Ayubu wakati wa jaribio la kwanza la Mungu. Katika jaribio la pili, Shetani aliunyosha mkono wake ili amdhuru Ayubu, na ingawaje Ayubu aliyapitia maumivu yaliyokuwa makali zaidi kuliko yale aliyokuwa ameyapitia awali, bado ushuhuda wake ulikuwa wa kutosha kuwaacha watu wakiwa wameshangazwa. Alitumia ujasiri wake, imani yake, na utiifu kwa Mungu, pamoja na kumcha Mungu kwake, kwa mara nyingine tena kumshinda Shetani, na mwenendo wake na ushuhuda wake viliweza kwa mara nyingine tena kuidhinishwa na kupata kibali cha Mungu. Wakati wa jaribu hili, Ayubu alitumia mwenendo wake halisi kumtangazia Shetani kwamba maumivu ya mwili wake yasingebadilisha imani yake na utiifu wake kwa Mungu au kuchukua ule upendo wake kwa Mungu na kumcha Mungu; asingemkana Mungu au kuacha ukamilifu wake mwenyewe na unyoofu wake kwa sababu alikuwa amekabiliwa na kifo. Azimio la Ayubu lilimfanya Shetani kuwa mwoga, imani yake ilimwacha Shetani akiwa na hofu na kutetemeka, mvutano wa vita vya maisha yake na kifo chake dhidi ya Shetani vilileta chuki kubwa na hasira ndani ya Shetani; ukamilifu na unyofu wake ulimuacha Shetani akiwa hana chochote zaidi cha kumfanya kiasi cha kwamba Shetani aliyaacha mashambulizi yake kwake na kukata tamaa na mashtaka yake dhidi ya Ayubu mbele za Yehova Mungu. Hii ilimaanisha kwamba Ayubu alikuwa ameushinda ulimwengu, alikuwa ameushinda mwili wake, alikuwa amemshinda Shetani, na alikuwa ameshinda kifo; alikuwa kwa kweli na kwa hakika binadamu aliyemilikiwa na Mungu. Wakati wa majaribio haya mawili, Ayubu alisimama imara katika ushuhuda wake, na kwa hakika aliishi kwa kudhihirisha ukamilifu na unyofu wake, na wigo wa kanuni zake za kuishi za kumcha Mungu na kujiepusha na maovu zikapanuka. Baada ya Ayubu kupitia majaribio haya mawili, maisha yake yalikuwa na uzoefu mwingi, na uzoefu huu ulimfanya yeye kuwa mwenye kimo na uzoefu zaidi, ilimfanya kuwa mwenye nguvu zaidi, na imani kubwa zaidi, na ilimfanya yeye kuwa na ujasiri zaidi kuhusu haki na ustahili wa uadilifu ambao yeye alishikilia kwa dhati. Majaribio ya Yehova Mungu kwa Ayubu yalimwezesha kupitia kwa undani sana na kuhisi utunzaji wa Mungu kwa mwanadamu, na kumruhusu kuhisi thamani ya upendo wa Mungu, ambapo baada ya hapo uchaji wake Mungu ulionekana na kupendwa na Mungu. Majaribio ya Yehova Mungu hayakumpeleka tu Ayubu mbali na Yeye, lakini yaliuleta moyo wa Ayubu karibu na Mungu. Wakati maumivu yale ya mwili yaliyovumiliwa na Ayubu yalifikia kilele, wasiwasi aliouhisi kutoka kwa Yehova Mungu ulimfanya asiwe na budi ila kuilaani siku yake ya kuzaliwa. Mwenendo kama huo haukuwa umepangiliwa mapema lakini ulikuwa ni ufunuo wa asili wa kutilia maanani na upendo wa dhati kwa Mungu kutoka ndani ya moyo wake; ulikuwa ni ufunuo wa kiasili uliotoka kwenye kutilia maanani na upendo wa dhati kwa Mungu. Yaani ni kusema, kwa sababu alijichukia, na hakuwa na radhi na hakuweza kuvumilia kuona Mungu kumwumiza, hivyo kutilia maanani na upendo wake wa dhati vilifika hali ya kujinyima. Wakati huu, Ayubu aliimarisha kuabudu kwake kwa muda mrefu na shauku yake kwa Mungu na upendo wake kwa Mungu hadi kufikia kiwango cha kujali na kupenda. Kwa wakati huohuo, aliweza kupandisha imani na utiifu wake kwa Mungu na kumcha Mungu kwake hadi katika kiwango cha kujali na kupenda. Hakujiruhusu kufanya chochote ambacho kingesababisha madhara kwa Mungu, hakujiruhusu kutenda mwenendo wowote ambao ungemuumiza Mungu, na hakujiruhusu kuleta masikitiko, huzuni au hata kutokuwa na furaha kokote kwake Mungu kwa sababu zake mwenyewe. Machoni pa Mungu, ingawa Ayubu alikuwa bado Ayubu wa hapo awali, imani, utiifu na kumcha Mungu kwake kulikuwa kumemletea Mungu utoshelevu na furaha kamili. Kwa wakati huu, Ayubu alikuwa amefikia ukamilifu ambao Mungu alimtarajia aupate; alikuwa amefikia kuwa mtu anayestahili kabisa kuitwa “mkamilifu na mnyoofu” machoni pa Mungu. Matendo yake ya haki yalimruhusu kumshinda Shetani na kusimama imara katika ushuhuda wake kwa Mungu. Hivyo, pia, matendo yake ya haki yalimfanya kuwa mkamilifu, na kuruhusu thamani ya maisha yake kuinuliwa na kuzidishwa zaidi ya hapo awali, na pia yalimfanya kuwa mtu wa kwanza kutoweza kushambuliwa tena au kujaribiwa zaidi na Shetani. Kwa sababu Ayubu alikuwa mwenye haki, alishtakiwa na kujaribiwa na Shetani; kwa sababu Ayubu alikuwa mwenye haki, alikabidhiwa kwa Shetani; na kwa sababu Ayubu alikuwa mwenye haki, alimdhoofisha na kumshinda Shetani, na kuweza kusimama imara katika ushuhuda wake. Kuanzia hapo, Ayubu akawa mtu wa kwanza ambaye hangewahi kukabidhiwa tena kwa Shetani, alikuwa amekuja kwa kweli mbele za kiti cha enzi cha Mungu na kuishi katika nuru, chini ya baraka za Mungu bila ya upelelezi au uharibifu wa Shetani…. Alikuwa amekuwa mtu wa kweli machoni pa Mungu; alikuwa ameachiliwa huru. …

Kuhusu Ayubu

Baada ya kujua jinsi Ayubu alivyopitia majaribio, kunao uwezekano kwamba wengi wenu watataka kujua maelezo zaidi kuhusu Ayubu mwenyewe, hasa kuhusiana na siri iliyomfanya akapata sifa za Mungu. Hivyo basi leo, hebu tuzungumzie kuhusu Ayubu!

Katika Maisha ya Kila Siku ya Ayubu Tunaona Ukamilifu, Unyofu, Kumcha Mungu, na Kujiepusha na Maovu Kwake

Ikiwa tutamzungumzia Ayubu, basi lazima tuanze na namna ambavyo alitathminiwa kwa mujibu wa matamshi kutoka kwa kinywa cha Mungu mwenyewe: “Hakuna hata mtu kama yeye duniani, mtu mtimilifu na mwaminifu, ambaye anamcha Mungu, na kuepuka maovu.”

Hebu kwanza tujifunze kuhusu ukamilifu na unyofu wa Ayubu.

Je, unaelewa vipi maneno haya “ukamilifu” na “unyofu”? Je, unaamini kwamba Ayubu hakuwa na ukosolewaji wowote, kwamba alikuwa mwenye kuheshimiwa? Bila shaka, hii ingekuwa tafsiri halisi na uelewa wa maneno “ukamilifu” na “unyofu.” Lakini muktadha wa maisha halisi ni muhimu kwa ufahamu wa kweli wa Ayubu—maneno, vitabu, na nadharia pekee hazitaweza kutupa majibu yoyote. Tutaanza na kuyaangalia maisha ya Ayubu ya nyumbani, kuangalia namna mwenendo wake wa kawaida ulivyokuwa maishani mwake. Kufanya hivi kutatwambia kuhusu kanuni na malengo yake maishani, pamoja na hulka yake na mambo yale aliyoyafuatilia. Sasa, hebu tuyasome maneno ya mwisho katika Ayubu 1:3: “Mtu huyo alikuwa mkubwa zaidi kuwaliko watu wengine wote wa mashariki.” Kile ambacho maneno haya yanasema ni kwamba hadhi na heshima ya Ayubu ilikuwa ya juu sana, na ingawaje hatuambiwi kama alikuwa ndiye mkuu zaidi kati ya wanaume wote wa upande wa mashariki kwa sababu ya wingi wa mali zake au kwa sababu alikuwa mkamilifu na mnyofu, na kwamba alimcha Mungu na kujiepusha na maovu, kwa ujumla tunajua kwamba hadhi na heshima ya Ayubu vyote vilithaminiwa sana. Kama ilivyorekodiwa kwenye Biblia, maoni ya kwanza ya watu kuhusu Ayubu yalikuwa kwamba Ayubu alikuwa mkamilifu , kwamba alimcha Mungu na kujiepusha na maovu na kwamba alikuwa na mali nyingi na alikuwa na hadhi ya kuheshimika. Kwa mtu wa kawaida anayeishi katika mazingira kama haya na hali kama hizo, mlo wa Ayubu, ubora wa maisha, na nyanja mbalimbali za maisha yake binafsi yote yangekuwa ni mambo ambayo yangezingatiwa na watu wengi; hivyo ni lazima tuendelee kuyasoma maandiko: “Nao wana wake walienda na kufurahia karamu katika nyumba zao, kila kwa siku yake; na wao wakatuma na kuwaita ndugu zao wa kike watatu ili wakule na kunywa pamoja na wao. Na ilikuwa hivyo, wakati hizo siku zao za karamu ziliisha, Ayubu aliwatuma na kuwatakasa, na akaamka asubuhi mapema, na kutoa sadaka za kuteketezwa kulingana na hesabu yao wote; kwa sababu Ayubu alisema, Inaweza kuwa kwamba wana wangu wametenda dhambi, na kumlaani Mungu mioyoni mwao. Hivyo ndivyo Ayubu alivyofanya kila siku” (Ayubu 1:4-5). Kifungu hiki kinatuambia mambo mawili: Jambo la kwanza ni kwamba watoto wa kiume na wa kike wa Ayubu walifanya karamu mara kwa mara, wakila na kunywa sana; pili ni kwamba Ayubu mara kwa mara alitoa sadaka za kuteketezwa kwa sababu alikuwa na wasiwasi kwa ajili ya wanawe, akiogopa kwamba walikuwa wakitenda dhambi, kwamba katika mioyo yao walikuwa wakimkufuru Mungu. Katika maandiko haya maisha ya watu wa aina mbili tofauti yanafafanuliwa. Maisha ya kwanza, watoto wa kiume na wa kike wa Ayubu, mara nyingi walifanya karamu kwa sababu ya utajiri wao, wakiishi kwa ubadhirifu, wakila na kunywa hadi mioyo yao iridhike, wakifurahia maisha ya kiwango cha juu yaliyotokana na utajiri wa mali. Wakiishi maisha kama haya, ilikuwa lazima kwamba mara kwa mara wangetenda dhambi na kumkosea Mungu—ilihali hawakujitakasa wala kutoa sadaka za kuteketezwa kutokana na hayo yote. Unaona, basi, kwamba Mungu hakuwa na nafasi katika mioyo yao, kwamba hawakufikiria kuhusu neema za Mungu, wala kuogopa kumkosea Mungu, isitoshe hawakuogopa kumuacha Mungu katika mioyo yao. Bila shaka zingatio letu si watoto wa Ayubu, lakini ni kwa kile ambacho Ayubu alifanya alipokabiliwa na mambo kama haya; hili ndilo suala jingine lililofafanuliwa katika kifungu, na ambalo linahusisha maisha ya kila siku ya Ayubu na kiini cha ubinadamu wake. Wakati Biblia inapofafanua kushiriki kwa watoto wake wa kike na kiume katika karamu mbalimbali hakuna mahali ambapo Ayubu anatajwa; inasemekana tu kwamba ni watoto wake wa kiume na wa kike walio kula na kunywa pamoja. Kwa maneno mengine, hakuandaa karamu, wala hakujiunga na watoto wake wa kiume na wa kike katika kula kwa kupita kiasi. Ingawa alikuwa tajiri na mwenye mali nyingi na watumishi wengi, maisha ya Ayubu hayakuwa ya anasa. Hakudanganywa na mazingira yake ya juu kabisa aliyoyaishi na wala hakujawa na ulafi wa anasa za mwili au kusahau kutoa sadaka za kuteketezwa kwa sababu ya utajiri wake, isitoshe pia haya yote hayakumsababisha kuanza kujiepusha na Mungu ndani ya moyo wake kwa utaratibu. Kwa hivyo, ni wazi kwamba, Ayubu alikuwa na nidhamu katika maisha yake, hakuwa na tamaa au kupenda anasa kutokana na baraka za Mungu kwake, na hakuzingatia juu ya ubora wa maisha. Badala yake, alinyenyekea na akawa asiye na majivuno, hakuwa mwenye kujidai na alikuwa mtulivu na mwangalifu mbele za Mungu. Mara nyingi alifikiria kuhusu neema na baraka za Mungu, na siku zote alimcha Mungu. Katika maisha yake ya kila siku, Ayubu mara nyingi aliamka mapema ili kutoa sadaka za kuteketezwa kwa ajili ya wana na binti zake. Kwa maneno mengine, Ayubu mwenyewe alimcha Mungu na pia alitumaini kwamba watoto wake wangeweza vilevile kumcha Mungu na kutotenda dhambi dhidi ya Mungu. Utajiri wa mali za Ayubu haukuwa na nafasi yoyote ndani ya moyo wake, wala haukuchukua ile nafasi iliyoshikiliwa na Mungu; haijalishi kama ilikuwa ni kwa ajili yake mwenyewe au watoto wake, vitendo vyote vya kila siku vya Ayubu viliunganishwa katika kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Uchaji wake kwa Yehova Mungu hakukuishia kinywani mwake, lakini ulitiwa katika vitendo, na ukajionyesha katika kila sehemu ya maisha yake. Mwenendo huu halisi wa Ayubu unatuonyesha kwamba alikuwa mwaminifu, na alimiliki kiini kilichopenda haki na mambo yaliyokuwa mazuri. Kwamba Ayubu mara nyingi alituma sadaka ya kuteketezwa kwa niaba ya watoto wake wa kiume na wa kike na kuwatakasa kunamaanisha kwamba hakuruhusu wala kuidhinisha tabia ya watoto wake; badala yake katika moyo wake alichukizwa na tabia yao, na akawashutumu vikali. Alikuwa amethibitisha kwamba mwenendo wa watoto wake wa kike na wa kiume haukumpendeza Yehova Mungu na hivyo basi mara nyingi aliwaita kwenda mbele za Yehova Mungu na kutubu dhambi zao. Vitendo vya Ayubu vinatuonyesha upande mwingine wa ubinadamu wake: ule ambao unaonyesha kwamba hakuwahi kutembea na wale ambao mara nyingi walitenda dhambi na kumkosea Mungu, lakini badala yake alijiepusha na kutotaka kuwa nao. Hata ingawa watu hawa walikuwa ni watoto wake wa kike na wa kiume, hakuziacha kanuni zake binafsi kwa sababu walikuwa ni jamaa zake mwenyewe, wala hakujihusisha katika dhambi zao kwa sababu ya hisia zake mwenyewe. Badala yake aliwasihi kutubu na kupata ustahimilivu wa Yehova Mungu na akawaonya kutomwacha Mungu kwa ajili ya kujifurahisha kwao kwa tamaa. Kanuni za namna ambavyo Ayubu aliwashughulikia wengine haziwezi kutenganishwa na zile kanuni za kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Alipenda kile kilichokubalika na Mungu na kuchukia kile kiĺichomchukiza Mungu; na aliwapenda wale waliomcha Mungu mioyoni mwao, na kuwachukia wale waliotenda maovu au kutenda dhambi dhidi ya Mungu. Upendo na chuki kama hiyo zilionyeshwa katika maisha yake ya kila siku, na ndio uliokuwa unyofu wenyewe wa Ayubu ulioonekana machoni pa Mungu. Kwa kawaida, haya pia ndiyo maonyesho na kuishi kulingana na ubinadamu wa kweli wa Ayubu katika mahusiano yake na wengine katika maisha yake ya kila siku, ambayo ni lazima tujifunze kuyahusu.

Maonyesho ya Ubinadamu wa Ayubu Wakati wa Majaribio Yake (Kuelewa Ukamilifu, Unyofu, Kumcha Mungu na Kujiepusha na Maovu kwa Ayubu Wakati wa Majaribio Yake)

Kile tulichozungumzia hapo juu ni vipengele mbalimbali vya ubinadamu wa Ayubu vilivyoonyeshwa katika maisha yake ya kila siku kabla ya majaribio yake. Bila shaka, maonyesho haya mbalimbali yanatupa ufahamu wa awali pamoja na uelewa wa unyofu wa Ayubu, kumcha Mungu na kujiepusha na maovu kwake, na unatupa uthibitisho wa awali. Sababu inayonifanya kusema “awali” ni kwa kuwa watu wengi bado hawana uelewa wa kweli wa hulka ya Ayubu na kiwango ambacho alifuatilia njia ya kutii na kumcha Mungu. Hivi ni kusema, ufahamu wa watu wengi kumhusu Ayubu hauendi mbali zaidi ya yale maoni fulani ambayo yanamfaa yeye kama ilivyoelezewa katika vifungu viwili kwenye Biblia vilivyo na maneno yake “Yehova alitoa, na Yehova ametwaa; jina la Yehova na libarikiwe” na “je, tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya?” Hivyo, kuna haja kubwa yetu sisi kuelewa namna ambavyo Ayubu aliishi kwa kudhihirisha ubinadamu wake alipokuwa akipokea majaribu ya Mungu; kwa njia hii, ubinadamu wote wa kweli wa Ayubu utaweza kuonyeshwa kwa ukamilifu wake.

Wakati Ayubu aliposikia kwamba mali zake zilikuwa zimeibiwa, kwamba wana na binti zake walikuwa wamepoteza maisha yao, na kwamba watumishi wake walikuwa wameuawa, alitenda hivi: “Ndipo Ayubu akainuka, akalirarua joho lake, na akanyoa kichwa chake, na akaanguka chini, na kuabudu” (Ayubu 1:20). Maneno haya yanatuambia ukweli mmoja: Baada ya kuzisikiza habari hizi, Ayubu hakushikwa na wasiwasi, hakulia au kuwalaumu wale watumishi ambao walikuwa wamempa habari hizo, isitoshe hakukagua eneo la uhalifu ili kuchunguza na kuthibitisha taarifa na kutaka kujua ni nini haswa kilichotokea. Hakuonyesha maumivu au majuto yoyote kutokana na kupoteza mali zake, wala hakuangua kilio kutokana na kuwapoteza watoto wake, wapendwa wake. Kinyume chake ni kwamba, alirarua joho lake, kisha akanyoa kichwa chake, na kuanguka chini, na kuabudu. Vitendo vya Ayubu ni tofauti sana na vile vya binadamu wa kawaida. Vinawachanganya watu wengi, na kuwaruhusu kumkosoa Ayubu ndani ya mioyo yao kwa “kukosa huruma.” Kwa kupoteza ghafla mali zao, watu wa kawaida wangeonekana kuwa wamevunjika moyo, au wamekata tamaa—au kama ilivyo kwa baadhi ya watu, wanaweza hata kupatwa na mfadhaiko mkubwa. Hii ni kwa sababu, katika mioyo yao, mali za watu zinawakilisha jitihada za maisha yao yote—ndiyo ambayo maisha yao yanategemea, ndilo tumaini linalowafanya kuishi; kupoteza mali zao kunamaanisha jitihada zao zimeambulia patupu na kwamba hawana tumaini tena na kwamba pia hawana siku za usoni. Huu ndio mtazamo wa mtu yeyote wa kawaida kuhusiana na mali zake na uhusiano wa karibu walio nao na mali hizo, na huu pia ndio umuhimu wa mali katika macho ya watu. Hivyo, idadi kubwa ya watu wanahisi wakiwa wamechanganyikiwa na mtazamo mtulivu wa Ayubu kuhusiana na kupoteza mali zake. Leo, tutauondoa mkanganyiko ambao watu wote walihisi kwa kuelezea kile kilichokuwa kikiendelea moyoni mwa Ayubu.

Akili za kawaida zinasema kwamba, kwa kuwa alikuwa amepewa mali nyingi kama hizo na Mungu, Ayubu angepaswa kuona aibu mbele za Mungu kwa sababu ya kupoteza mali hizi, kwani hakuwa ameziangalia au kuzitunza; hakuwa ameshikilia mali alizopewa na Mungu. Hivyo, aliposikia kwamba mali zake zilikuwa zimeibiwa, mwitikio wake wa kwanza ulifaa kuwa kuenda kwenye eneo la uhalifu na kuchukua hesabu ya kila kitu kilichokuwa kimepotea na kisha kutubu kwa Mungu ili aweze kwa mara nyingine kupokea baraka za Mungu. Ayubu, hata hivyo hakufanya hivi, na kwa kawaida alikuwa na sababu zake mwenyewe za kutofanya hivyo. Ndani ya Moyo wake, Ayubu aliamini sana kwamba kila kitu alichomiliki alikuwa amepewa na Mungu na hakikuwa kimetokana na jitihada zake yeye mwenyewe. Hivyo, hakuziona baraka hizo kama jambo la kutilia maanani, lakini alishikilia ile njia aliyopaswa kuichukua kwa bidii sana kama kanuni zake za kuishi. Alizithamini baraka za Mungu, na akatoa shukrani kutokana nazo, lakini hakutamanishwa nazo wala hakutafuta baraka zaidi. Huo ndio uliokuwa mtazamo wake kuhusu mali. Hakufanya chochote kwa minajili ya kupata baraka, wala kuwa na wasiwasi au kuhuzunishwa kutokana na ukosefu au kupoteza baraka za Mungu; hakufurahi kupindukia, na kwa njia isiyo na mipaka kwa sababu ya baraka za Mungu na wala hakupuuza njia ya Mungu wala kusahau neema ya Mungu kwa sababu ya zile baraka ambazo alifurahia mara kwa mara. Mtazamo wa Ayubu kwa mali zake unafichua kwa watu ubinadamu wake wa kweli: Kwanza, Ayubu hakuwa binadamu mwenye tamaa, na hakuwa na madai katika maisha yake ya kimwili. Pili, Ayubu hakuwahi kuwa na wasiwasi au kuogopa kwamba Mungu angechukua kila kitu alichokuwa nacho, na ndio uliokuwa mtazamo wake wa utiifu kwa Mungu ndani ya moyo wake; yaani, hakuwa na madai au malalamiko kuhusu ni lini au kama Mungu angechukua kutoka kwake, na wala hakuuliza sababu, lakini alilenga tu kutii mipango ya Mungu. Tatu, hakuwahi kusadiki kwamba mali zake zilitokana na jitihada zake, lakini kwamba alipewa na Mungu. Hii ilikuwa imani ya Ayubu kwa Mungu, na onyesho la imani yake. Je, ubinadamu wa Ayubu na ufuatiliaji wake wa kweli wa kila siku umefanywa kuwa wazi katika muhtasari huu wa hoja tatu kumhusu yeye? Ubinadamu na ufuatiliaji wa Ayubu ni vitu vilivyokuwa muhimu katika mwenendo wake mtulivu alipokabiliwa na hali ya kupoteza mali zake. Ilikuwa hasa kwa sababu ya ufuatiliaji wake wa kila siku ndipo Ayubu akawa na kimo na imani ya kusema, “Yehova alinipa, na Yehova amechukua; jina la Yehova libarikiwe,” wakati wa majaribio ya Mungu. Maneno haya hayakupatwa kwa usiku mmoja, na wala hayakujitokeza tu kwa ghafla katika kichwa cha Ayubu. Yalikuwa yale ambayo alikuwa ameyaona na kuyapata kwa miaka mingi ya kupitia safari ya maisha. Akilinganishwa na wale wote wanaotafuta tu baraka za Mungu na wanaoogopa kwamba Mungu atachukua kutoka kwao, nao wanachukia hali hio na wanalalamikia kuhusu hali hiyo, je utiifu wa Ayubu ni wa kweli haswa? Ikilinganishwa na wale wote wanaoamini kwamba kuna Mungu, lakini ambao hawajawahi kuamini kwamba Mungu anatawala juu ya vitu vyote, je, Ayubu hana uaminifu na unyofu mkubwa?

Urazini wa Ayubu

Uzoefu halisi wa Ayubu na ubinadamu wake wenye unyofu na uaminifu ulimaanisha kwamba alifanya uamuzi na uchaguzi wenye urazini zaidi alipozipoteza mali zake na watoto wake. Chaguzi hizo za busara zisingeweza kutenganishwa na yale aliyoyafuatilia kila siku na matendo ya Mungu ambayo alikuwa ameyajua katika maisha yake ya siku baada ya siku. Uaminifu wa Ayubu ulimfanya aweze kuamini kwamba mkono wa Yehova unatawala juu ya vitu vyote; imani yake ilimruhusu kujua ukweli wa ukuu wa Yehova Mungu juu ya vitu vyote; maarifa yake yalimfanya kuwa tayari na kuwa na uwezo wa kutii ukuu na mipangilio ya Yehova Mungu juu ya vitu vyote; utiifu wake ulimwezesha kuwa mkweli na mkweli zaidi katika uchaji wake kwa Yehova Mungu; uchaji wake ulimfanya kuwa halisi zaidi na zaidi katika kujiepusha kwake na maovu; hatimaye, Ayubu akawa mkamilifu kwa sababu alimcha Mungu na kujiepusha na maovu; na ukamilifu wake ulimfanya kuwa na hekima zaidi na kukampa urazini wa kipekee.

Je, tunapaswa kuelewa vipi neno hili, “urazini”? Tafsiri halisi ni kwamba inamaanisha kuwa mwenye akili nzuri, kuwa mwenye mantiki na wa kueleweka katika kufikiria kwako, kuwa na maneno ya kueleweka, matendo na maamuzi yenye kueleweka, na kuwa na viwango vya maadili vilivyo sawa na vya kawaida. Lakini urazini wa Ayubu hauelezewi sana kwa urahisi. Inaposemwa hapa kwamba Ayubu alikuwa na urazini wa kipekee, inahusiana na ubinadamu wake na mwenendo wake mbele zaMungu. Kwa sababu Ayubu alikuwa mwaminifu, aliweza kuamini na kuutii ukuu wa Mungu, uliompa maarifa ambayo yasingeweza kupatikana na wengine na maarifa haya yalimfanya kuweza kutambua, kuamua, na kufafanua kwa usahihi zaidi yale yaliyompata, na yaliyomwezesha kwa usahihi na kwa uwazi zaidi kuchagua ni nini cha kufanya na ni nini cha kushikilia kwa uthabiti. Hivi ni kusema kwamba maneno, tabia, na kanuni zake zilizofuatana na matendo yake, na kwa utaratibu ambao alitenda, ulikuwa wa kila siku, ulio dhahiri, na mahususi, na haukukosa mwelekeo, haukuwa na mihemko ya ghafla au ya kihisia. Alijua namna ya kushughulikia chochote kile kilichompata, alijua jinsi ya kusawazisha na kukabiliana na uhusiano kati ya matukio mbalimbali magumu, pia alijua jinsi ya kushikilia njia ambayo anapaswa kuishikilia, na, vilevile, alijua namna ya kuchukulia ule utoaji na uchukuaji wa Yehova Mungu. Huu ndio uliokuwa urazini wenyewe wa Ayubu. Ilikuwa hasa ni kwa sababu Ayubu alikuwa na urazini kama huu ndio maana akasema, “Yehova alinipa, na Yehova amechukua; jina la Yehova libarikiwe,” alipozipoteza mali zake na watoto wake wa kiume na wa kike.

Wakati Ayubu alipokabiliwa na maumivu makali ya mwili, na malalamiko ya jamaa zake na marafiki zake, na wakati alipokabiliwa na kifo, mwenendo wake halisi kwa mara nyingine tena ulionyesha kimo chake kwa mambo yote.

Asili Halisi ya Ayubu: Mkweli, Aliye safi, na Asiye na Uongo

Hebu tusome Ayubu 2:7-8: “Hivyo Shetani akatoka mbele za uwepo wa Yehova, na akamgonga Ayubu kwa majipu ya kuuma kutoka kwenye wayo wa mguu wake hadi utosini mwa kichwa chake. Na akachukua kigae kwa ajili ya kujikuna nacho; naye akakaa chini kwenye majivu.” Huu ni ufafanuzi wa mwenendo wa Ayubu wakati ambapo majipu mabaya yalipojitokeza kwenye mwili wake. Wakati huu, Ayubu aliketi kwenye majivu huku akiyavumilia. Hakuna aliyemtibu yeye, na hakuna aliyemsaidia kupunguza maumivu kwenye mwili wake; badala yake, alitumia kigaye kujikwangua sehemu ya juu ya majipu yake yenye maumivu. Kwa juujuu, hii ilikuwa awamu tu ya mateso ya Ayubu na haina uhusiano wowote na ubinadamu wake na kumcha Mungu kwake, kwani Ayubu hakuongea maneno yoyote kuonyesha hali na maoni yake kwa wakati huo. Lakini bado matendo ya Ayubu na mwenendo wake ulikuwa ni onyesho la kweli la ubinadamu wake. Kwenye rekodi ya sura iliyopita tunasoma kwamba Ayubu alikuwa ndiye mkuu zaidi kati ya wanaume wote wa mashariki. Kifungu hiki cha sura ya pili, nacho, kinatuonyesha kwamba binadamu huyu aliyekuwa mkuu kwa upande wa mashariki hakika alichukua kigae ili kujikwangua nacho huku akiwa ameketi kwenye majivu. Je, hakuna utofauti wowote wa wazi kati ya fafanuzi hizi mbili? Ni utofauti unaotuonyesha nafsi ya kweli ya Ayubu: Licha ya nafasi na hadhi yake ya kifahari, hakuwahi kuzipenda wala kuzpa umakini wowote; hakujali namna wengine walivyoangalia nafasi yake, wala hakujali kama hatua au mwenendo wake ungekuwa na athari mbaya kwa nafasi yake; hakujihusisha katika manufaa ya hadhi, wala hakufurahia ufahari uliokuja pamoja na hadhi na nafasi yake katika jamii. Alijali tu kuhusu thamani yake na umuhimu wa kuishi kwake machoni pa Yehova Mungu. Nafsi ya kweli ya Ayubu ilikuwa kiini chake: Hakupenda umaarufu na utajiri, na wala hakuishi kwa ajili ya umaarufu na utajiri; alikuwa mkweli, na aliye safi, na asye na unafiki wowote.

Utenganisho wa Ayubu kati ya Upendo na Chuki

Upande mwingine wa ubinadamu wa Ayubu unaonyeshwa katika mazungumzo yake na mke wake: “Kisha mkewe akasema kwake, Je, Wewe bado unabaki na ukamilifu wako? mlaani Mungu, ufe. Lakini yeye akasema kwake, Wewe unazungumza mithili ya mmoja wa wanawake walio wapumbavu wanavyozungumza. Ati? tupokee mema kutoka mkononi mwa Mungu, nasi tusipokee mabaya?” (Ayubu 2:9-10). Kwa kuona mateso aliyokuwa akipitia, mke wa Ayubu alijaribu kumshauri Ayubu ili amsaidie kuepuka mateso yake—lakini zile “nia nzuri” hazikupata idhini ya Ayubu; badala yake, ziliamsha hasira ndani yake, kwa sababu aliikataa imani yake na utiifu wake kwa Yehova Mungu, na pia alikataa uwepo wa Yehova Mungu. Hali hii isingeweza kuvumilika kwa Ayubu, kwani hakuwahi kujiruhusu kufanya chochote ambacho kingempinga au kumuumiza Mungu, sembuse kwa watu. Angewezaje kubakia vilevile bila kujali chochote wakati alipowaona wengine wakiongea maneno yaliyomkufuru na kumtukana Mungu? Hivyo basi alimwita mke wake “mwanamke mpumbavu.” Mtazamo wa Ayubu kwa mke wake ulikuwa ule wa hasira na chuki, pamoja na ule wa kushutumu na kukemea. Haya ndiyo yaliyokuwa maonyesho ya asili ya ubinadamu wa Ayubu ambayo yalitofautisha kati ya upendo na chuki na yalikuwa uwakilishi wa kweli wa ubinadamu wake uliokuwa na unyofu. Ayubu alikuwa na hisia ya haki—ambayo ilimfanya achukie mielekeo mibaya, na ilimfanya achukie, ashutumu, na kukataa uzushi wa kipuuzi, mabishano ya kijinga, na madai yasiyokuwa na msingi, na ikamruhusu kushikilia kwa uthabiti kanuni zake na msimamo wake wakati alipokuwa amekataliwa na wengi na kuachwa na wale walio kuwa karibu na yeye.

Ukarimu na Uaminifu wa Ayubu

Kwa sababu, kutoka katika mwenendo wa Ayubu, tunaweza kuona maonyesho ya vipengele mbalimbali vya ubinadamu wake, je, tunaona nini kuhusu ubinadamu wa Ayubu wakati alipofungua kinywa chake kuilaani siku yake ya kuzaliwa? Hii ndiyo mada tutakayozungumzia hapa chini.

Hapo juu, Nimezungumzia chimbuko la laana ya Ayubu ya siku ya kuzaliwa kwake. Mnaona nini katika haya? Kama Ayubu asingekuwa mkarimu na asiye na upendo, kama angekuwa asiyejali na asiye na hisia, na asiye na ubinadamu, je, angejali kuhusu tamanio la moyo wa Mungu? Na je, angeweza kuidharau siku ya kuzaliwa kwake mwenyewe kwa sababu aliujali moyo wa Mungu? Kwa maneno mengine kama Ayubu alikuwa hana ukarimu na aliyepungukiwa na ubinadamu, je, angeweza kuhuzunishwa na maumivu ya Mungu? Je, angeweza kuilaani siku ya kuzaliwa kwake kwa sababu Mungu alikuwa amehuzunika kwa sababu yake? Bila shaka, jibu ni hapana! Kwa sababu alikuwa mkarimu, Ayubu aliutunza moyo wa Mungu; kwa sababu aliutunza moyo wa Mungu, Ayubu alihisi maumivu ya Mungu; kwa sababu alikuwa mkarimu, alipata maumivu makali zaidi kutokana na kuyahisi maumivu ya Mungu; kwa sababu aliyahisi maumivu ya Mungu, alianza kuichukia siku ya kuzaliwa kwake, na hivyo akailaani siku yake ya kuzaliwa. Kwa watu wa nje, mwenendo wote wa Ayubu wakati wa majaribio yake ni mfano wa kuigwa. Kulaani kwake tu siku yake ya kuzaliwa ndiko kunakoweka picha ya kiulizo juu ya ukamilifu na unyofu wake, au kutoa tathmini tofauti. Kwa hakika, haya ndiyo yaliyokuwa maonyesho ya kweli zaidi ya kiini cha ubinadamu wa Ayubu. Kiini cha ubinadamu wake hakikufichwa au kufungwa, au kubadilishwa na mtu mwingine. Alipoilaani siku yake ya kuzaliwa, alionyesha ukarimu na uaminifu uliokuwa ndani ya moyo wake; alikuwa kama chemichemi ya maji ambayo maji yake yalikuwa safi sana na angavu kiasi cha kufichua sehemu ya chini kabisa ya chemichemi hio.

Baada ya kujifunza haya yote kuhusu Ayubu, watu wengi zaidi bila shaka watakuwa na tathmini sahihi na isiyo na ubaguzi kuhusu kiini cha ubinadamu wa Ayubu. Wanapaswa pia kuwa na ufahamu wa kina, wa kivitendo, na uliopevuka zaidi wa utimilifu na unyofu wa Ayubu kama ulivyozungumzwa na Mungu. Ni matumaini Yangu kwamba, uelewa na ufahamu huu utawasaidia watu kuanza kuingia katika njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu.

Uhusiano Kati ya Mungu kumkabidhi Ayubu kwa Shetani na Malengo ya Kazi ya Mungu

Ingawa watu wengi sasa wanatambua kwamba Ayubu alikuwa mkamilifu na mnyofu na kwamba alimcha Mungu na kujiepusha na maovu, utambuzi huu hauwapi uelewa mkubwa zaidi wa nia za Mungu. Kwa wakati huohuo wakiwa wanonea wivu ubinadamu na ufatiliaji wa Ayubu, wanamuuliza Mungu swali lifuatalo: Ayubu alikuwa mkamilifu na mnyofu sana, watu walimpenda sana, kwa hivyo kwa nini Mungu akamkabidhi kwa Shetani na kumtia katika maumivu haya makali? Maswali kama hayo yanatarajiwa kuwepo katika mioyo ya watu wengi—au tuseme, shaka hili hasa ndilo swali katika mioyo ya watu wengi. Kwa sababu imewachanganya watu wengi sana, ni, lazima tuliwasilishe swali hili waziwazi na kulielezea kikamilifu.

Kila kitu ambacho Mungu anafanya ni muhimu, na kina umuhimu wa kipekee, kwani kila kitu anachofanya ndani ya binadamu kinahusu usimamizi wake na wokovu wa wanadamu. Kwa kawaida, kazi ambayo Mungu aliifanya ndani ya Ayubu si tofauti, ijapokuwa Ayubu alikuwa mkamilifu na mnyofu machoni pa Mungu. Kwa maneno mengine, licha ya kile ambacho Mungu anafanya au mbinu ambazo Anatumia kuifanya, licha ya gharama, au lengo Lake, dhumuni la matendo Yake halibadiliki. Kusudi Lake ni kufanya kazi ya maneno ya Mungu ndani ya mwanadamu, pamoja na mahitaji ya Mungu na mapenzi ya Mungu kwa mwanadamu; kwa maneno mengine, ni kufanya kazi ndani ya mwanadamu kwa yale yote ambayo Mungu anayaamini kuwa ni chanya kulingana na hatua Zake, ili kumwezesha binadamu kuuelewa moyo wa Mungu na kufahamu kiini cha Mungu, na kumruhusu aweze kutii ukuu na mipangilio ya Mungu, na hivyo basi kumruhusu binadamu kuweza kufikia kiwango cha kumcha Mungu na kujiepusha na maovu—yote haya ni kipengele kimoja cha kusudi la Mungu katika kila kitu Anachofanya. Kipengele kingine ni kwamba, kwa sababu Shetani ndiye foili na chombo cha huduma katika kazi ya Mungu, mara nyingi binadamu hukabidhiwa kwa Shetani; hizi ndizo mbinu ambazo Mungu hutumia ili kuwaruhusu watu kuweza kuona maovu, ubaya, nakudharaulika kwa Shetani katikati ya majaribu na mashambulizi ya Shetani na hivyo basi kuwasababisha watu kumchukia Shetani na kuweza kutambua kile ambacho ni kibaya. Mchakato huu unawaruhusu kwa utaratibu kuanza kuwa huru dhidi ya udhibiti wa Shetani, na dhidi ya mashtaka, uingiliaji kati, na mashambulizi ya Shetani—hadi, kwa sababu ya maneno ya Mungu, maarifa yao na utiifu wao kwa Mungu, na imani yao kwa Mungu na kuweza kwao kumcha Mungu, wanashinda dhidi ya mashambulizi ya Shetani na kushinda dhidi ya mashtaka ya Shetani; hapo tu ndipo watakapokuwa wamekombolewa kabisa dhidi ya utawala wa Shetani. Ukombozi wa watu unamaanisha kwamba Shetani ameshindwa, unamaanisha kwamba wao si chakula tena katika kinywa cha Shetani—kwamba badala ya kuwameza wao, Shetani amewaachilia. Hii ni kwa sababu watu kama hao ni wanyofu, kwa sababu wanayo imani, utiifu na wanamcha Mungu, na kwa sababu wako huru kabisa dhidi ya Shetani. Wamemletea Shetani aibu, wamemfanya Shetani kuwa mwoga, na wamemshinda kabisa Shetani. Imani yao katika kumfuata Mungu, na utiifu na kumcha Mungu kunamshinda Shetani, na kumfanya Shetani kukata tamaa kabisa na wao. Watu kama hawa ndio ambao Mungu amewapata kwa kweli, na hili ndilo lengo kuu la Mungu katika kumwokoa binadamu. Kama wangependa kuokolewa, na wangependa Mungu awapate kabisa, basi wale wote wanaomfuata Mungu lazima wakabiliane na majaribu na mashambulizi yakiwa makubwa na hata madogo kutoka kwa Shetani. Wale wanaotoka katika majaribu na mashambulizi haya na wanaweza kumshinda kabisa Shetani ni wale waliookolewa na Mungu. Hivi ni kusema kwamba wale waliookolewa na Mungu ni wale ambao wamepitia majaribio ya Mungu, na ambao wamejaribiwa na kushambuliwa na Shetani mara nyingi sana. Wale waliookolewa na Mungu wanayaelewa mapenzi na mahitaji ya Mungu, na wanaweza kuukubali ukuu na mipangilio ya Mungu na hawaachi njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu katikati ya majaribu ya Shetani. Wale waliookolewa na Mungu wanamiliki uaminifu, wao ni wakarimu, na wanaweza kutofautisha kati ya upendo na chuki, wanayo hisia ya haki na urazini, na wanaweza kumjali Mungu na kuthamini sana kila kitu ambacho ni cha Mungu. Watu kama hao hawafungwi, kufanyiwa upelelezi, kushtakiwa au kudhulumiwa na Shetani; wako huru kabisa, wamekombolewa na kuachiliwa kabisa. Ayubu alikuwa mtu kama huyo mwenye uhuru na huu ndio umuhimu hasa wa kwa nini Mungu alikuwa amemkabidhi kwa Shetani.

Ayubu alidhulumiwa na Shetani, lakini pia aliweza kupata uhuru na ukombozi wa milele, na kupata haki ya kutowahi kukabidhiwa tena kwa upotovu, unyanyasaji, na mashtaka ya Shetani, na badala yake kuishi katika nuru ya uso wa Mungu kwa uhuru na bila vizuizi na kuishi katikati ya baraka alizopewa na Mungu. Hakuna ambaye angechukua au kuangamiza, au kupata haki hii. Ilitolewa kwa Ayubu kutokana na imani yake, azimio lake, na utiifu na uchaji wake Mungu; Ayubu alilipia gharama ya maisha yake ili kuweza kupata shangwe na furaha duniani, ili kufanikiwa kupata haki na kuweza kustahili, kama ilivyoamriwa mbinguni na kutambuliwa na dunia, ili kumwabudu Muumba bila kusumbuliwa kama kiumbe wa kweli wa Mungu duniani. Hayo pia ndiyo yaliyokuwa matokeo makubwa zaidi ya majaribu yaliyovumiliwa na Ayubu.

Wakati watu bado hawajaokolewa, maisha yao mara nyingi yanaingiliwa na hata kudhibitiwa na, Shetani. Kwa maneno mengine, watu ambao hawajaokolewa ni wafungwa wa Shetani, hawana uhuru, hawajaachiliwa na Shetani, hawana sifa au haki ya kumwabudu Mungu, na wanafuatiliwa kwa karibu na kushambuliwa vikali na Shetani. Watu kama hawa hawana furaha ya kuzungumzia, hawana haki ya uwepo wa kawaida wa kuzungumzia, na zaidi hawana heshima ya kuzungumzia. Ni pale tu unaposimama imara na kupigana na Shetani, kwa kutumia imani yako katika Mungu na utiifu Kwake, pamoja na kumcha Mungu kama silaha ambazo utatumia kupigana vita vya kufa na kupona dhidi ya Shetani, kiasi cha kwamba utamshinda kabisa Shetani na kumsababisha akate tamaa na kuwa mwoga kila anapokuona wewe, ili aache kabisa mashambulizi na mashtaka yake dhidi yako—hapo tu ndipo utakapookolewa na kuwa huru. Kama umeamua kutengana kabisa na Shetani, lakini huna silaha zitakazokusaidia kupigana na Shetani, basi bado utakuwa katika hatari; kwa kadri muda unavyosonga, baada ya wewe kuteswa na Shetani kiasi cha kwamba huna hata nguvu kidogo iliyobakia ndani yako, na bado hujaweza kuwa na ushuhuda, bado hujajifungua kabisa kuwa huru dhidi ya mashtaka na mashambulizi ya Shetani dhidi yako, basi utakuwa na tumaini dogo la wokovu. Mwishowe, wakati hitimisho la kazi ya Mungu litakapotangazwa, bado utakuwa katika mashiko ya Shetani, usiweze kujiachilia kuwa huru, na hivyo hutawahi kuwa na fursa au tumaini. Matokeo yake, hivyo basi, ni kwamba watu kama hao watakuwa katika utumwa wa Shetani kabisa.

Kubali Majaribio ya Mungu, Shinda Majaribu ya Shetani, na Umruhusu Mungu Aipate Nafsi Yako Yote

Wakati wa kazi ya utoaji Wake wa kudumu na msaada kwa binadamu, Mungu anawaambia binadamu kuhusu mapenzi Yake na mahitaji Yake yote, na Anaonyesha matendo Yake, tabia Yake, na kile Anacho na alicho kwa binadamu. Lengo ni kuweza kumtayarisha binadamu ili awe na kimo, na kumruhusu binadamu kupata kweli mbalimbali kutoka kwa Mungu wakati anaendelea kumfuata Yeye—ukweli ambao ni silaha anazopewa mwanadamu na Mungu ambazo atatumia kupigana na Shetani. Hivyo akiwa na silaha hizo, binadamu lazima akabiliane na majaribio ya Mungu. Mungu anazo mbinu na njia nyingi za kumjaribu binadamu, lakini kila mojawapo inahitaji “ushirikiano” wa adui wa Mungu: Shetani. Hivi ni kusema, baada ya kumpa binadamu silaha ambazo atatumia kupigana na Shetani, Mungu anamkabidhi binadamu kwa Shetani na kumruhusu Shetani “kujaribu” kimo cha mwanadamu. Kama mwanadamu anaweza kufanikiwa kutoka kwenye vita vilivyoundwa na Shetani, kama anaweza kuepuka kuzingirwa na Shetani na bado akaishi, basi mwanadamu atakuwa ameushinda mtihani. Lakini kama binadamu atashindwa kuepuka vita vilivyoundwa na Shetani, na akajisalimisha kwa Shetani, basi hatakuwa amelishinda jaribio. Haijalishi ni kipengele kipi cha binadamu ambacho Mungu anakichunguza, kigezo cha uchunguzi Wake ni kama binadamu atasimama imara katika ushuhuda wake atakaposhambuliwa na Shetani au la, na kujua kama amemuacha Mungu au la na akajisalimisha na akajinyenyekeza kwa Shetani baada ya kunaswa na Shetani. Inaweza kusemwa kwamba, iwapo binadamu anaweza kuokolewa au la yote haya yanategemea kama anaweza kumzidi na kumshinda Shetani, na kama ataweza kupata uhuru au la inategemea kama anaweza kuinua, yeye binafsi, silaha alizopewa na Mungu ili kushinda utumwa wa Shetani, na kumfanya Shetani akose kabisa tumaini na kumwacha peke yake. Kama Shetani atakosa tumaini na kumwachilia mtu, hii inamaanisha kwamba Shetani hatawahi tena kujaribu kumchukua mtu huyu kutoka kwa Mungu, hatawahi tena kumshtaki na kumsumbua mtu huyu, hatawahi tena kutaka kumtesa au kumshambulia; mtu kama huyu tu ndiye atakuwa kwa kweli amepatwa na Mungu. Huu ndio mchakato mzima ambao Mungu anawapata watu.

Onyo na Nuru Iliyotolewa kwa Vizazi vya Baadaye Na Ushuhuda wa Ayubu

Huku wakielewa mchakato ambao Mungu anampata kabisa mtu, watu wataweza pia kuelewa nia na umuhimu wa Mungu kumkabidhi Ayubu kwa Shetani. Watu hawasumbuliwi tena na maumivu makali ya Ayubu, na wanatambua kwa upya umuhimu wake. Hawana wasiwasi tena ikiwa wao wenyewe watapitia majaribu sawa na yale ya Ayubu, na hawapingi au kukataa tena ujio wa majaribio ya Mungu. Imani ya Ayubu, utiifu, na ushuhuda wake wa kumshindaShetani, vyote hivi vimekuwa ni chanzo cha msaada mkubwa na faraja kwa watu. Kwa Ayubu, wanaona tumaini la wokovu wao wenyewe, na wanaona kwamba kupitia imani, na utiifu na kumcha Mungu, inawezekana kabisa kumshinda Shetani, na kutawala juu ya Shetani. Wanaona kwamba mradi tu wakubali ukuu na mipangilio ya Mungu, na kuwa na azimio na imani ya kutomwacha Mungu baada ya kupoteza kila kitu, basi wanaweza kuleta aibu na kushindwa kwa Shetani, na kwamba wanahitaji tu kuwa na azimio na ustahimilivu wa kusimama imara katika ushuhuda wao—hata kama itamaanisha kupoteza maisha yao—ili Shetani aweze kuaibika na kurudi nyuma kwa haraka. Ushuhuda wa Ayubu ni onyo kwa vizazi vya baadaye, na onyo hili linawaambia kwamba kama hawatamshinda Shetani, basi hawatawahi kuweza kujiondolea mashtaka na usumbufu wa Shetani, na wala hawatawahi kuweza kutoroka dhulma na mashambulizi ya Shetani. Ushuhuda wa Ayubu uliwapatia nuru vizazi vya baadaye. Mwangaza huu unawafundisha watu kwamba ni pale tu watapokuwa wakamilifu na wanyofu ndipo watakapoweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu; unawafunza kwamba ni pale tu wanapomcha Mungu na kujiepusha na maovu ndipo watakapoweza kuwa na ushuhuda wenye nguvu na wenye ushindi mkubwa sana kwa Mungu; na pale tu watakapokuwa na ushuhuda wenye nguvu na wenye ushindi mkubwa sana kwa Mungu ndipo hawatawahi kudhibitiwa na Shetani, na wataishi katika mwongozo na ulinzi wa Mungu—na hapo tu ndipo watakapokuwa wameokolewa kwa kweli. Hulka ya Ayubu na ufuatiliaji wake wa maisha unafaa kuigwa na kila mmoja anayefuata wokovu. Kile alichoishi kwa kudhihirisha katika maisha yake yote na mwenendo wake wakati wa majaribio yake ni hazina yenye thamani kwa watu wote wanaotaka kufuata njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu.

Ushuhuda wa Ayubu Wamafariji Mungu

Kama Nikiwaambia sasa kwamba Ayubu ni mtu mzuri, huenda msiweze kutambua maana iliyopo katika maneno haya, na huenda msiweze kung’amua mawazo yaliyofanya Nizungumze maneno haya yote; lakini subirini mpaka siku ile mtakapokuwa mmepitia majaribu sawa na au yale yanayofanana na yale ambayo Ayubu aliyapitia, wakati mtakapokuwa mmepitia magumu, wakati mtakapokuwa mmepitia majaribio yaliyopangiliwa kwa ajili yenu na Mungu mwenyewe, wakati utakapojitolea kila kitu ulicho nacho, na kuvumilia udhalilishaji na ugumu ili uweze kumshinda Shetani na kuwa na ushuhuda kwa Mungu katikati ya vishawishi hivi vyote—basi utaweza kutambua maana ya maneno haya Ninayoyaongea. Wakati huo, utahisi kwamba wewe ni duni kuliko Ayubu, utahisi namna Ayubu alivyo mzuri na kwamba anastahili kuigwa; wakati huo utakapowadia, utatambua namna ambavyo maneno yale yaliyo bora yaliyozungumzwa na Ayubu yalivyo muhimu kwa yule aliyepotoka na anayeishi katika nyakati hizi, na utatambua namna ilivyo vigumu kwa watu wa leo kuweza kutimiza kile ambacho Ayubu alitimiza. Unapohisi kuwa ni vigumu, utatambua jinsi moyo wa Mungu ulivyo na wasiwasi na mashaka, utatambua namna gharama aliyolipa Mungu kuwapata watu kama hao ilivyo ya juu, na jinsi kile ambacho Mungu hufanya na kutoa kwa ajili ya mwanadamu kilivyo cha thamani. Kwa sababu sasa mmeyasikia maneno haya, je, mnao ufahamu sahihi na tathmini sahihi kuhusu Ayubu? Machoni penu, je, Ayubu alikuwa kweli mtu mkamilifu na mnyofu aliyemcha Mungu na kujiepusha na maovu? Nasadiki kwamba watu wengi bila shaka watasema ndiyo. Kwani ukweli kuhusu kile ambacho Ayubu alitenda na kufichua hakiwezi kupingwa na binadamu yeyote au Shetani. Hilo ndilo thibitisho la nguvu zaidi kuhusu ushindi wa Ayubu dhidi ya Shetani. Thibitisho hili lilitolewa katika Ayubu, na ndio ushuhuda wa kwanza uliopokelewa na Mungu. Hivyo, Ayubu aliposhinda majaribu ya Shetani na kuwa na ushuhuda kwa Mungu, Mungu aliona tumaini kwa Ayubu, na moyo Wake ulifarijiwa na Ayubu. Tangu wakati wa uumbaji mpaka wakati wa Ayubu, huu ndio ulikuwa wakati wa kwanza ambao Mungu kwa kweli alipitia na kujua faraja ilikuwa ni nini, na ilimaanisha nini kufarijiwa na mwanadamu. Huo ndio ulikuwa wakati wa kwanza ambao Alikuwa ameona, na kupata ushuhuda wa kweli ambao ulitolewa kwa ajili Yake.

Ninaamini kwamba, baada ya kuusikia ushuhuda wa Ayubu na maelezo ya vipengele mbalimbali vya Ayubu, watu wengi watakuwa na mipangokwa ajili ya njia iliyopo mbele yao. Hivyo, pia, Ninaamini kwamba watu wengi zaidi walio na wasiwasi na woga wataanza kwa utaratibu kuwa watulivu katika mwili na akili zao, na wataanza kuhisi utulivu, kidogo kidogo …

Vifungu vilivyo hapa chini ni maelezo pia kumhusu Ayubu. Acha tuendelee kusoma.

4. Ayubu Asikia Kuhusu Mungu Kupitia Kusikia kwa Sikio

Ayubu 9:11 Ona, Anapita karibu na mimi, na Simwoni: Anapita kwenda mbele pia, lakini siwezi kumwona.

Ayubu 23:8-9 Tazama, nasonga mbele, lakini hayuko huko; na nyuma, lakini siwezi kumwona: Kwa mkono wa kushoto, ambapo Yeye hufanya kazi, lakini siwezi kumwona: Yeye hujificha Mwenyewe katika mkono wa kulia, kiasi kwamba siwezi kumwona.

Ayubu 42:2-6 Najua ya kwamba Wewe unaweza kufanya kila kitu, na ya kwamba hakuna wazo linaloweza kuzuilika kutoka Kwako. Ni nani yeye anayeficha ushauri bila maarifa? hivyo, nimesema neno nisilolifahamu; vitu vilivyo vya ajabu sana kwangu, ambavyo nisivyovijua. Sikiza, nakusihi, nami nitazungumza: Nitauliza kutoka Kwako, Nawe useme kwangu. Nimesikia kukuhusu kwa kusikia na masikio: lakini sasa jicho langu lakuona. Ndiyo sababu najichukia, na kutubu kwenye mavumbi na majivu.

Ingawa Mungu Hajajidhihirisha kwa Ayubu, Ayubu Anaamini katika Ukuu wa Mungu

Je, maneno haya yana msukumo gani? Je, kuna yeyote kati yenualiyetambua kwamba kunao ukweli hapa? Kwanza, Ayubu alijuaje kwamba Mungu yupo? Kisha, alijuaje kwamba mbingu na dunia na vitu vyote vinatawaliwa na Mungu? Kunacho kifungu kinachojibu maswali haya mawili: “Nimesikia habari Zako, kwa kusikia kwa masikio; bali sasa jicho langu linakuona. Kwa sababu hiyo najichukia mwenyewe, na kutubu katika mavumbi na majivu.” Kutokana na maneno haya tunajifunza kwamba, badala ya kumwona Mungu kwa macho yake mwenyewe, Ayubu alikuwa amejifunza kuhusu Mungu kutoka kwenye hekaya. Ni katika hali hizi ndipo alipoanza kuitembea njia ya kumfuata Mungu, na baadaye akathibitisha uwepo wa Mungu katika Maisha yake, na katika vitu vyote. Kuna ukweli usiopingika hapa—ukweli huo ni upi? Licha ya kuweza kufuata njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, Ayubu alikuwa hajawahi kumwona Mungu. Je, katika hili, hakuwa sawa na watu wa leo? Ayubu alikuwa hajawahi kumwona Mungu, maana yake ni kwamba ingawa alikuwa amewahi kumsikia Mungu, hakujua ni wapi Mungu alikuwa, au Mungu ni wa namna ganiifanana, au ni nini ambacho Mungu alikuwa akifanya. Haya yote ni mambo yanayojitegemea; kusema ukweli, ingawa alimfuata Mungu, Mungu alikuwa hajawahi kumtokea au kuzungumza na yeye. Je, huu si ukweli? Ingawa Mungu alikuwa hajaongea na Ayubu au kumpa amri zozote, Ayubu alikuwa ameuona uwepo wa Mungu na kuuona ukuu Wake katika vitu vyote, na katika hekaya ambazo kwazo Ayubu alikuwa amesikia kuhusu Mungu kwa kusikia kwa masikio, alikuja kuanza maisha ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Hiyo ndiyo iliyokuwa asili na mchakato ambao Ayubu alimfuata Mungu. Lakini haikujalisha ni vipi alivyomcha Mungu na kujiepusha na maovu, ni vipi ambavyo alishikilia uadilifu wake, bado Mungu alikuwa hajawahi kujitokeza kwake. Hebu tukisome kifungu hiki. Alisema, “Ona, Anapita karibu na mimi, na simwoni: Anapita kwenda mbele pia, lakini siwezi kumwona” (Ayubu 9:11). Yale ambayo maneno haya yanasema ni kwamba Ayubu huenda alimhisi Mungu karibu na yeye au pengine hakumhisi—lakini alikuwa hajawahi kuweza kumwona Mungu. Kuna nyakati ambazo alikuwa akimfikiria Mungu akiwa anapita mbele yake au akitenda, au akimwongoza binadamu, lakini alikuwa hajawahi kujua. Mungu humjia binadamu wakati ambapo hatarajii; binadamu hajui ni lini Mungu atamjia, au ni wapi Anatakapomjia yeye, kwa sababu binadamu hawezi kumwona Mungu, kwa hivyo, kwa binadamu Mungu amejificha kutoka kwake.

Imani ya Ayubu Katika Mungu Haitikisiki Kwa Sababu ya Ukweli Kwamba Mungu Amejificha Kutoka Kwake

Katika kifungu kifuatacho cha maandiko, Ayubu anasema, “Tazama, nasonga mbele, lakini Hayuko huko; na nyuma, lakini siwezi kumwona: Kwa mkono wa kushoto, ambapo Yeye hufanya kazi, lakini siwezi kumwona: Yeye hujificha katika mkono wa kulia, kiasi kwamba siwezi kumwona” (Ayubu 23:8-9). Katika maelezo haya, tunajifunza kwamba katika hali alizopitia Ayubu, Mungu alikuwa Amejificha kutoka kwake wakati wote huo; Mungu alikuwa hajajitokeza waziwazi kwake, na alikuwa hajamzungumzia waziwazi maneno yoyote, lakini moyoni mwake, Ayubu alikuwa ana uhakika wa kuwepo kwa Mungu. Alikuwa siku zote ameamini kwamba Mungu huenda anatembea na yeye au huenda Anatenda akiwa kando yake, na kwamba ingawa hakuweza kumwona Mungu, Mungu alikuwa kando yake Akitawala mambo yote kumhusu yeye. Ayubu alikuwa hajawahi kumwona Mungu, lakini aliweza kubaki kuwa mwaminifu katika imani yake, jambo ambalo hakuna mtu mwingine aliyeweza kulifanya. Je, ni kwa nini watu wengine hawakuweza kufanya hivyo? Ni kwa sababu Mungu hakuzungumza na Ayubu au kumtokea, na kama asingekuwa ameamini kwa kweli, asingeweza kuendelea, wala asingeweza kushikilia njia hiyo ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Je, huu si ukweli? Je, unajisikiaje unaposoma kuhusu Ayubu akiyasema maneno haya? Je, unahisi kwamba ukamilifu na unyoofu wa Ayubu, na haki yake mbele za Mungu, ni vya kweli, na wala si kutia chumvi kwa upande wa Mungu? Ingawa Mungu alimtendea Ayubu kwa njia sawa na watu wengine, na hakujitokeza wala kuongea na yeye, Ayubu bado alishikilia uadilifu wake, bado aliamini katika ukuu wa Mungu, na, isitoshe, mara kwa mara alitoa sadaka za kuteketezwa na kuomba mbele za Mungu kutokana na hofu yake ya kumkosea Mungu. Katika uwezo wa Ayubu wa kumcha Mungu bila ya kuwahi kumwona Mungu, tunaona jinsi alivyopenda mambo chanya, na jinsi imani yake ilivyokuwa thabiti na ya kweli. Hakukana kuwepo kwa Mungu kwa sababu Mungu alikuwa amejificha kutoka kwake, wala hakupoteza imani yake na kumkataa Mungu kwa sababu hakuwahi kumwona Yeye. Badala yake, katikati ya kazi iliyofichwa ya Mungu ya kutawala vitu vyote, alikuwa ametambua kuwepo kwa Mungu na akahisi ukuu wa Mungu na nguvu za Mungu. Hakukata tamaa katika kuwa mnyofu kwa sababu Mungu alikuwa amejificha, wala hakuiacha njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu kwa sababu Mungu alikuwa hajawahi kumwonekania. Ayubu alikuwa hajawahi kuuliza kwamba Mungu aonekane waziwazi kwake ili Athibitishe kuwepo Kwake, kwa kuwa tayari alikuwa ameona ukuu wa Mungu katika vitu vyote na aliamini kwamba alikuwa amepata baraka na neema ambazo wengine hawakuwa wamepata. Ingawa Mungu alibaki kuwa amejificha kutoka kwake, imani ya Ayubu kwa Mungu haikuwahi kutikisika. Hivyo, alivuna kile ambacho hakuna yeyote aliyewahi kuvuna: Kibali cha Mungu na baraka za Mungu.

Ayubu Alibariki Jina la Mungu na Hafikirii Kuhusu Baraka au Janga

Kuna ukweli ambao haujawahi kurejelewa katika hadithi za maandiko kuhusu Ayubu, na ukweli huu ndio utakaokuwa lengo letu leo. Ingawa Ayubu alikuwa hajawahi kumwona Mungu au kusikia maneno ya Mungu kwa masikio yake mwenyewe, Mungu alikuwa na nafasi katika moyo wa Ayubu. Je, mtazamo wa Ayubu kwa Mungu ulikuwa ni upi? Ulikuwa, kama ulivyorejelewa awali, “jina la Yehova libarikiwe.” Kubariki kwake jina la Mungu hakukuwa na masharti, hakukujalisha muktadha, na hakukuzuiliwa na sababu yoyote ile. Tunaona kwamba Ayubu alikuwa ameukabidhi moyo wake kwa Mungu, akiuruhusu utawaliwena Mungu; kila kitu alichofikiria, kila kitu alichoamua, na kila kitu alichopanga katika moyo wake kilikuwa wazi kwa Mungu na wala moyo wake haukuwa umefungwa kwa Mungu. Moyo wake haukumpinga Mungu, na hakuwahi kumwomba Mungu amfanyie chochote au kumpa chochote, na hakuwa na matamanio ya kupita kiasi kwamba angepata chochote kutokana na yeye kumwabudu Mungu. Ayubu hakuzungumzia mabadilishano na Mungu, na wala hakutoa ombi lolote au madai yoyote kwa Mungu. Kulisifu kwake jina la Mungu kulikuwa ni kwa sababu ya nguvu kuu na mamlaka ya Mungu katika kutawala vitu vyote, na haikutegemea ikiwa alipata baraka au alipatwa na janga. Aliamini kwamba haijalishi kama Mungu anawabariki watu au kuleta maafa juu yao, nguvu na mamlaka ya Mungu hayatabadilika, na hivyo, bila kujali hali za mtu, jina la Mungu linapaswa kusifiwa. Kwamba binadamu amebarikiwa na Mungu ni kwa sababu ya ukuu wa Mungu, na janga linapompata mwanadamu, vivyo hivyo, pia ni kwa sababu ya ukuu wa Mungu. Nguvu na mamlaka ya Mungu vyote vinatawala na kupangilia kila kitu kumhusu mwanadamu; mabadiliko yasiyo ya kawaida kuhusu utajiri wa binadamu ni maonyesho ya nguvu na mamlaka ya Mungu, na licha ya maoni ya mtu, jina la Mungu linapaswa kusifiwa. Haya ndiyo ambayo Ayubu aliyapitia na kuishia kujua katika miaka ya maisha yake. Fikira na matendo yote ya Ayubu yalifikia masikio ya Mungu na kufika mbele za Mungu, na yalionekana na Mungu kuwa ya muhimu. Mungu aliyapenda sana maarifa haya ya Ayubu na akamthamini sana Ayubu kwa kuwa na moyo kama huo. Moyo huu ulisubiria amri ya Mungu siku zote, na kila mahali, na haikujalisha ni kwa muda gani au mahali gani, uliweza kukaribisha chochote kile kilichompata. Ayubu hakutoa mahitaji yoyote kwa Mungu. Kile alichohitaji kutoka kwake mwenyewekilikuwa kusubiria, kukubali, kukabiliana na kutii mipangilio yote iliyotoka kwa Mungu; Ayubu aliamini hili kuwa wajibu wake, na ndicho hasa kile ambacho Mungu Alitaka. Ayubu alikuwa hajawahi kumwona Mungu, wala kumsikia Akismea maneno yoyote, Akitoa amri zozote, Akiyatoa mafundisho yoyote, au kumwelekeza kuhusu chochote. Kwa maneno ya leo, kwa yeye kuweza kuwa na mtazamo kama huo kwa Mungu, wakati Mungu alikuwa hajampa nuru, mwongozo, au uandalizi kuhusiana na ukweli—hili lilikuwa lenye thamani sana, na kwa yeye kuonyesha mambo kama hayo kulitosha kwa Mungu, na ushuhuda wake ulipongezwa na Mungu, na kutathminiwa na Mungu. Ayubu alikuwa hajawahi kumwona Mungu au kumsikia Mungu binafsi akitamka mafundisho yoyote kwake, lakini kwa Mungu moyo wake na yeye mwenyewe vyote vilikuwa vyenye thamani zaidi kuliko wale watu ambao, mbele za Mungu waliweza tu kuongea kuhusiana na nadharia za kina, ambao waliweza tu kujigamba na kuongea kuhusu kutoa sadaka lakini walikuwa hawajawahi kuwa na maarifa ya kweli ya Mungu na walikuwa hawajawahi kumcha Mungu kwa kweli. Kwa kuwa moyo wa Ayubu ulikuwa safi, na haukufichwa kuonekana na Mungu, na ubinadamu wake ulikuwa wenye uaminifu na ukarimu, na alipenda haki na kile kilichokuwa kizuri. Ni mtu kama huyu tu ambaye alikuwa na moyo na ubinadamu kama huo ndiye aliyeweza kufuata njia ya Mungu, na kuwa na uwezo wa kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Mtu kama huyo aliweza kuuona ukuu wa Mungu, aliweza kuona mamlaka na nguvu Zake, na aliweza kufikia utiifu kwa ukuu Wake na mipangilio Yake. Ni mtu kama huyu tu ndiye aliyeweza kulisifu jina la Mungu kwa kweli. Hii ni kwa sababu hakuangalia kama Mungu angembariki au Angemletea janga, kwa sababu alijua kwamba kila kitu kinadhibitiwa na mkono wa Mungu, na kwamba binadamu kuwa na wasiwasi ni ishara ya upumbavu, ujinga, na kutoweza kufikiria vyema, pamoja na ishara kuwa na shaka kuhusu ukweli wa ukuu wa Mungu juu ya juu ya vitu vyote, na kutomcha Mungu. Maarifa ya Ayubu hasa ndiyo ambayo Mungu alitaka. Hivyo basi, je, Ayubu alikuwa na maarifa makubwa ya kinadharia kumhusu Mungu kuliko ninyi? Kwa sababu kazi na matamko ya Mungu wakati huo yalikuwa machache, halikuwa jambo rahisi kutimiza maarifa ya Mungu. Mafanikio kama hayo ya Ayubu hayakuwa jambo dogo. Alikuwa hajapitia kazi ya Mungu wala kuwahi kumsikia Mungu akiongea, au kuuona uso wa Mungu. Kwamba aliweza kuwa na mtazamo kama huo kwa Mungu yalikuwa hasa matokeo ya ubinadamu wake na ufuatiliaji wake binafsi, ubinadamu na ufuatiliaji ambao watu hawana leo. Hivyo, katika enzi hiyo, Mungu alisema, “Hakuna mtu ambaye yuko kama yeye ulimwenguni, mtu aliye mkamilifu na mwaminifu.” Katika enzi hiyo, Mungu alikuwa tayari amefanya tathmini kama hiyo kumhusu Ayubu, na Alikuwa amefikia hitimisho kama hilo. Je, ingekuwa kweli zaidi kwa kiasi gani leo hii?

Ingawa Mungu Amejificha Kutoka kwa Mwanadamu, Matendo Yake Miongoni mwa Vitu Vyote Yanamtosha Mwanadamu Kumjua Yeye

Ayubu alikuwa hajauona uso wa Mungu, wala kusikia matamshi yaliyonenwa na Mungu, na sembuse yeye binafsi alipitia kazi ya Mungu, lakini kumcha kwake Mungu na ushuhuda aliokuwa nao wakati wa majaribu unashuhudiwa na kila mmoja, na unapendwa, unafurahiwa, na kupongezwa na Mungu, na watu wanayaonea wivu na kuvutiwa nayo, na hata zaidi ya hayo, wanaimba sifa zao. Hakukuwa na chochote kikubwa au kisicho cha kawaida kuhusu maisha yake: Kama tu mtu yeyote wa kawaida, aliishi maisha yasiyo ya kina, akienda kufanya kazi wakati wa macheo na akirudi nyumbani kupumzika wakati wa magharibi. Tofauti ni kwamba wakati wa miongo kadhaa ya kawaida ya maisha yake, alipata utambuzi katika njia ya Mungu, na akatambua na kuelewa nguvu kuu na ukuu wa Mungu kuliko mtu mwingine yeyote aliyewahi kuwa nao. Hakuwa mwerevu zaidi kuliko mtu yeyote wa kawaida, maisha yake hayakuwa yenye ushupavu sana, wala, aidha, hakuwa na ustadi maalum usioonekana. Hata hivyo, kile alichokuwa nacho, kilikuwa ni hulka iliyokuwa na uaminifu, ukarimu na unyofu, na hulka iliyopenda kutopendelea, haki, na iliyopenda mambo chanya—hakuna kati ya mambo haya yanayomilikiwa na watu wengi wa kawaida. Alitofautisha kati ya upendo na chuki, alikuwa na hisia ya haki, hakukubali kushindwa na alikuwa hakati tamaa, na alikuwa mwangalifu sana katika kufikiria kwake. Hivyo, kwawakati wake wa kawaida duniani aliyaona mambo yote yasiyo ya kawaida ambayo Mungu alikuwa amefanya, na aliuona ukuu, utakatifu, na haki ya Mungu, aliona kujali kwa Mungu, neema Yake, na ulinzi Wake kwa binadamu, na aliuona utukufu na mamlaka ya Mungu mkuu zaidi. Sababu ya kwanza iliyomfanya Ayubu aweze kupata mambo haya yaliyokuwa zaidi ya mtu yeyote wa kawaida ilikuwa kwamba alikuwa na moyo safi, na moyo wake ulimilikiwa na Mungu na kuongozwa na Muumba. Sababu ya pili ilikuwa ni ufuatiliaji wake: ufuatiliaji wake wa kuwa mtu asiye na kasoro na mkamilifu, na wa kuwa mtu aliyekubaliana na mapenzi ya Mbinguni, aliyependwa na Mungu, na aliyejiepusha na uovu. Ayubu alimiliki na kufuatilia mambo haya huku akiwa hawezi kumwona Mungu au kusikia maneno ya Mungu; ingawa alikuwa hajawahi kumwona Mungu, alikuwa amejua mbinu ambazo kwazo Mungu hutawala juu ya vitu vyote, na kuelewa hekima ambayo Mungu anatumia ili kufanya hivyo. Ingawa alikuwa hajawahi kusikia maneno ambayo yalikuwa yametamkwa na Mungu, Ayubu alijua kwamba matendo ya kumthawabisha binadamu na kuchukua kutoka kwa binadamu yote yalitoka kwa Mungu. Ingawa miaka ya maisha yake haikuwa tofauti na ile ya mtu wa kawaida, hakuruhusu kutokuwa wa ajabu kwa maisha yake kuathiri maarifa yake ya ukuu wa Mungu juu ya vitu vyote, au kuathiri kufuata kwake kwa njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Machoni pake, sheria za mambo yote zilijaa matendo ya Mungu, na ukuu wa Mungu ungeweza kuonekana katika sehemu yoyote ya maisha ya mtu. Hakuwa amemwona Mungu lakini aliweza kutambua kwamba matendo ya Mungu yako kila mahali, na katika wakati wake wa kawaida duniani, kwa kila upande wa maisha yake aliweza kuona na kutambua matendo ya kipekee na ya ajabu ya Mungu, na aliweza kuona mipangilio ya ajabu ya Mungu. Hali ya kujificha na ukimya wa Mungu haukuzuia utambuzi wa Ayubu wa matendo ya Mungu, wala haukuathiri maarifa yake kuhusu ukuu wa Mungu juu ya vitu vyote. Maisha yake ya kila siku, yalikuwa na utambuzi, wa ukuu na mipangilio ya Mungu, ambaye Amejificha miongoni mwa vitu vyote. Katika maisha yake ya kila siku alisikia pia na kuelewa sauti ya moyo wa Mungu na maneno ya Mungu, ambaye yuko kimya miongoni mwa vitu vyote ilhali Anaeleza sauti ya moyo Wake na maneno Yake kwa kutawala sheria za vitu vyote. Unaona, basi, kwamba ikiwa watu wana ubinadamu na ufuatiliaji kama wa Ayubu, basi wanaweza kupata utambuzi na maarifa kama ya Ayubu, na kupata ule ufahamu na maarifa sawa kuhusu ukuu wa Mungu juu ya vitu vyote kama Ayubu. Mungu hakuwa Amemtokea Ayubu au kuongea na yeye, lakini Ayubu aliweza kuwa mkamilifu na mnyofu, na pia aliweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Kwa maneno mengine, bila ya Mungu kumtokea au kuzungumza na mwanadamu, matendo ya Mungu katika vitu vyote na ukuu Wake juu ya vitu vyote yanatosha kwa mwanadamu ili kuweza kuwa na ufahamu wa uwepo, nguvu na mamlaka ya Mungu, nguvu na mamlaka ya Mungu yanatosha kumfanya mwanadamu afuate njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Kwa sababu mwanadamu wa kawaida kama vile Ayubu aliweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, basi kila mtu wa kawaida anayemfuata Mungu anapaswa pia kuweza kufanya hivyo. Ingawa maneno haya yanaweza kusikika kana kwamba ni hitimisho la kimantiki, hili halikiuki sheria za mambo. Bado ukweli haujalingana na matarajio: Kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, kunaweza kuonekana, ni kwa ajili ya Ayubu na Ayubu pekee. Kwa kutaja “kumcha Mungu na kujiepusha na maovu,” watu hufikiri kwamba hii inafaa tu kufanywa na Ayubu, ni kana kwamba njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu ilikuwa imebandikwa jina la Ayubu na haikuhusiana na watu wengine. Sababu ya hili ni wazi: Kwa sababu Ayubu tu ndiye aliyemiliki hulka iliyokuwa na uaminifu, ukarimu, na unyofu, na iliyopenda kutopendelea na haki na mambo yaliyokuwa mazuri, hivyo ni Ayubu tu ambaye angeweza kufuata njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Mnaweza kuwa ninyi nyote mmeelewa maana hapa—kwamba kwa sababu hakuna mtu aliye na ubinadamu ulio na uaminifu, ukarimu, na unyofu, na ule ambao unapenda kutopendelea na haki na ule ambao ni mzuri, basi hakuna mtu anayeweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, na hivyo watu hawawezi kamwe kupata furaha ya Mungu au kusimama imara katikati ya majaribio. Hii pia ina maana kwamba, isipokuwa Ayubu, watu wote wangali wamefungwa na kunaswa na Shetani; wote wanashtakiwa, wanashambuliwa, na kudhulumiwa na yeye. Wao ndio wale ambao Shetani anajaribu kuwameza, na wote hawana uhuru, ni wafungwa ambao wametekwa nyara na Shetani.

Kama Moyo wa Mwanadamu Una Uadui na Mungu, Mwanadamu Anawezaje Kumcha Mungu na Kujiepusha na Maovu?

Kwa sababu watu wa leo hawamiliki ubinadamu sawa na Ayubu, vipi kuhusu kiini cha asili yao, na mtazamo wao kwa Mungu? Je, wanamcha Mungu? Je, wanajiepusha na maovu? Wale wasiomcha Mungu na kujiepusha na maovu wanaweza tu kujumlishwa kwa maneno matatu: “maadui wa Mungu.” Mara nyingi ninyi husema maneno haya matatu, lakini hamjawahi kujua maana yake halisi. Maneno “maadui wa Mungu” yanayo kiini ndani yake: Hayasemi kwamba Mungu anamuona mwanadamu kama adui, lakini kwamba binadamu anamuona Mungu kama adui. Kwanza, watu wanapoanza kumwamini Mungu, ni yupi kati yao asiyekuwa na malengo yake mwenyewe, motisha, na matamanio? Hata ingawa upande wao mmoja unaamini katika uwepo wa Mungu, na kuuona uwepo wa Mungu, bado imani yao katika Mungu ina hizo motisha, na malengo yao makubwa katika kumwamini Mungu ni kupokea baraka Zake na vitu wanavyotaka. Katika uzoefu wa maisha ya watu, mara nyingi wao hufikiria wenyewe: “Nimeacha familia yangu na kazi yangu kwa ajili ya Mungu, na Yeye amenipa nini? Ni lazima niijumuishe, na kuithibitisha—je, nimepokea baraka zozote hivi karibuni? Nimetoa mengi sana kwa wakati huu, nimekimbia na kukimbia, na nimeteseka sana—je, Mungu amenipa ahadi zozote kama malipo? Je, Ameyakumbuka matendo yangu mema? Je, mwisho wangu utakuwaje? Je, ninaweza kupokea baraka za Mungu? …” Kila mtu mara kwa mara hufanya hesabu kama hizi ndani ya moyo wake, na kutoa madai yao kwa Mungu yanayoendana na motisha zao, malengo yao na mawazo yao ya mabadilishano. Hivi ni kusema, ndani ya moyo wake, mwanadamu siku zote anamjaribu Mungu, siku zote anapanga mipango kuhusu Mungu, kila mara anabishana na Mungu kuhusu mwisho wake mwenyewe, na kujaribu kumfanya Mungu atoe kauli, ili, aweze kuona kama Mungu anaweza kumpa kile anachotaka au la. Wakati huohuo akimfuata Mungu, binadamu hamchukulii Mungu kama Mungu. Siku zote mwanadamu amejaribu kufanya mipango na Mungu, akitoa madai Kwake bila kukoma, na hata anamkandamiza Yeye katika kila hatua, akijaribu kupiga hatua ya maili moja licha ya kupewa inchi moja. Wakati huohuo akijaribu kufanya mabadilishano na Mungu, binadamu pia anabishana na Yeye, na wapo hata watu ambao, wakati majaribio yanapowapata au wanapojipata katika hali fulani, mara nyingi huwa wanakuwa dhaifu, hasi na walegevu katika kazi zao, na wanajaa malalamiko kumhusu Mungu. Tangu wakati ambapo mwanadamu alianza kumwamini Mungu, amemchukulia Mungu kama pembe inayotoa neema nyingi, kama kifaa chenye manufaa, na amejichukulia yeye mwenyewe kuwa mdai mkubwa zaidi wa Mungu, na ni kana kwamba kujaribu kupata baraka na ahadi kutoka kwa Mungu ni haki na jukumu la mwanadamu la asili, huku jukumu la Mungu likiwa ni kumlinda na kumtunza mwananadamu na kumruzuku. Huu ndio ufahamu wa kimsingi wa “imani katika Mungu” wa wale wote wanaomwamini Mungu, na ufahamu wao wa kina zaidi wa dhana ya imani katika Mungu. Kutoka katika kiini cha asili ya mwanadamu hadi katika ufuatiliaji wake wa kibinafsi, hakuna kitu chochote kinachohusiana na kumcha Mungu. Nia ya mwanadamu katika kumwamini Mungu huenda isiwe na uhusiano wowote na kumwabudu Mungu. Hivi ni kusema kwamba, mwanadamu hajawahi kufikiria wala kuelewa kwamba imani katika Mungu inahitaji kumcha Mungu, na kumwabudu Mungu. Kwa mujibu wa haya yote, kiini cha mwanadamu kiko wazi. Kiini hiki ni kipi? Ni kwamba moyo wa mwanadamu una nia mbaya, unaficha usaliti na udanganyifu, haupendi kutenda bila upendeleo na kwa haki, na kwa kile ambacho ni chanya, na ni wenye kustahili dharau na wenye tamaa sana. Moyo wa mwanadamu sio kwamba unaweza kufungwa zaidi kwa Mungu; bali mwanadamu, hajampa Mungu moyo wake kabisa. Mungu hajawahi kuona moyo wa kweli wa mwanadamu, wala hajawahi kuabudiwa na mwanadamu. Haijalishi jinsi gharama ambayo Mungu amelipia ilivyo kubwa, au ni kiasi gani cha kazi Anayofanya, au ni kwa kiwango gani Anampatia mwanadamu, mwanadamu anabakia yule asiyeona hayo yote, na hajali kuyahusu. Mwanadamu hajawahi kumpa Mungu moyo wake, anataka tu kuujali moyo wake yeye mwenyewe, kufanya uamuzi wake mwenyewe—sababu ikiwa kwamba mwanadamu hataki kufuata njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, au kutii ukuu na mipangilio ya Mungu, wala hataki kumwabudu Mungu kama Mungu. Hivyo ndivyo hali ya mwanadamu ilivyo leo. Sasa hebu tumwangalie tena Ayubu. Kwanza kabisa, je, alifanya mpango na Mungu? Je, alikuwa na motisha zisizo sahihi katika kushikilia imara njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu? Kwa wakati huo, je, Mungu alikuwa ameongea na yeyote kuhusu mwisho unaokuja? Wakati huo, Mungu alikuwa hajatoa ahadi zozote kwa yeyote kuhusu mwisho, na ilikuwa katika hali hii ndipo Ayubu aliweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Je, watu wa leo wanaweza kulinganishwa na Ayubu? Kuna tofauti nyingi sana; wamo katika makundi tofauti. Ingawa Ayubu hakuwa na maarifa mengi ya Mungu, alikuwa amempa Mungu moyo wake na ulimilikiwa na Mungu. Hakuwahi kufanya mabadilishano na Mungu, na hakuwa na matamanio yoyote ya kupita kiasi au madai kwa Mungu; badala yake, aliamini kwamba “Yehova alitoa, na Yehova amechukua.” Hili ndilo alilokuwa ameliona na kupata kutokana na kushikilia njia ya kumcha Mungu kwa uaminifu na kujiepusha na maovu katika miaka mingi ya maisha. Vivyo hivyo, alikuwa pia amepata matokeo yanayowakilishwa katika maneno: “Je, tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya?” Sentensi hizi mbili ndizo ambazo alikuwa ameona na akaja kujua kutokana na mtazamo wake wa utiifu kwa Mungu katika uzoefu wa maisha yake, na ndizo pia zilikuwa silaha zake zenye nguvu zaidi ambazo alizitumia kushinda wakati wa majaribu ya Shetani, na ndizo zilikuwa msingi wa kusimama kwake imara katika ushuhuda kwa Mungu. Wakati huu, je, bado mnamwona Ayubu kama mtu mzuri? Je, mnatumaini kuwa mtu kama huyo? Je, mnaogopa kukabili majaribu yai vya Shetani? Je, mnaazimiakumwomba Mungu ili aweze kuwapitisha katika majaribu kama haya ya Ayubu? Bila shaka watu wengi wasingethubutu kuomba kwa ajili ya mambo kama hayo. Ni wazi, basi, kwamba imani yenu ni ndogo kiasi cha kusikitisha; ikilinganishwa na ile ya Ayubu, imani yenu haistahili kutajwa. Nyinyi ndio adui wa Mungu, hamumchi Mungu, hamwezi kusimama imara katika ushuhuda wenu kwa Mungu, na hamwezi kuyashinda mashambulizi, mashtaka, na vishawishi vya Shetani. Ni nini kinachowafanya mstahili kupokea ahadi za Mungu? Baada ya kusikia hadithi ya Ayubu na kuelewa nia ya Mungu katika kumwokoa mwanadamu na maana ya wokovu wa mwanadamu, je, sasa mna imani ya kukubali majaribu sawa na ya Ayubu? Je, hampaswi kuwa na azimio dogo la kujiruhusu kufuata njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu?

Msiwe na Wasiwasi Wowote Kuhusu Majaribio ya Mungu

Baada ya kupata ushuhuda kutoka kwa Ayubu kufuatia mwisho wa majaribio yake, Mungu aliamua kwamba angepata kundi au zaidi ya kundi—la watu kama Ayubu, ilhali Aliamua kutowahi tena kumruhusu Shetani kumshambulia na kumnyanyasa mtu mwingine yeyote kwa kutumia mbinu ambazo kwazo alimjaribu, kumshambulia na kumnyanyasa Ayubu, kwa kuwekekana dau na Mungu; Mungu hakumruhusu Shetani tena kufanya mambo kama hayo kwa binadamu ambaye ni mdhaifu, mpumbavu, na mjinga—ilikuwa inatosha kwamba Shetani alikuwa amemjaribu Ayubu! Kutomruhusu Shetani kuwanyanyasa watu jinsi anavyotaka ni rehema za Mungu. Kwa Mungu, ilitosha kwamba Ayubu alikuwa ameteseka kwa majaribu na unyanyasaji wa Shetani. Mungu hakumruhusu Shetani tena kufanya mambo kama hayo, kwani maisha na kila kitu cha watu wanaomfuata Mungu yanatawaliwa na kupangiliwa na Mungu, na Shetani hana haki ya kuwatawala waliochaguliwa na Mungu apendavyo—mnapaswa kuwa wazi kuhusu hoja hii! Mungu anajali kuhusu udhaifu wa mwanadamu, na anaelewa upumbavu na ujinga wake. Ingawa, ili kwamba mwanadamu aweze kuokolewa kikamilifu, ni, lazima Mungu amkabidhi kwa Shetani, Mungu hayuko radhi kumwona tena binadamu akiwahi kuchezewa kama mpumbavu na kunyanyaswa na Shetani, na hataki tena kumwona binadamu akiteseka siku zote. Binadamu aliumbwa na Mungu, na inaeleweka kikamilifu kwamba Mungu anatawala na anapangilia kila kitu cha binadamu; hili ni jukumu la Mungu na mamlaka ambayo Mungu anatawala vitu vyote! Mungu hamruhusu Shetani amnyanyase na kumtumia vibaya binadamu apendavyo, Hamruhusu Shetani kutumia mbinu mbalimbali za kumpotosha binadamu, na vilevile, Hamruhusu Shetani kuingilia kati ukuu wa Mungu kwa binadamu, wala Hamruhusu Shetani akanyage na kuangamiza Sheria ambazo kwazo Mungu hutawala vitu vyote, sembuse kuhusu kazi kubwa ya Mungu ya kuwasimamia na kuwaokoa wanadamu! Wale ambao Mungu anataka kuwaokoa na wale ambao wanaweza kuwa na ushuhuda kwa Mungu, wao ndio kiini na udihirisho wa kazi ya Mungu ya mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita, pamoja na gharama ya jitihada Zake katika kazi Yake ya miaka elfu sita. Mungu anawezaje kuwakabidhi watu hawa kwa Shetani hivihivi.

Watu mara nyingi wanakuwa na wasiwasi na wana uoga wa majaribio ya Mungu, ilhali siku zote wanaishi katika mtego wa Shetani, na kuishi katika maeneo hatari ambapo wanashambuliwa na kunyanyaswa na Shetani—lakini hawaogopi na hawashangazwi. Ni nini kinaendelea? Imani ya binadamu katika Mungu ina mipaka tu kwa vitu anavyoweza kuona. Hana ufahamu hata kidogo kuhusu upendo na kujali kwa Mungu kwa binadamu, au huruma Zake na kumzingatia Kwake mwanadamu. Lakini kwa hofu na wasiwasi kidogo kuhusu majaribio, hukumu na kuadibu kwa Mungu, na adhama na hasira Yake, binadamu hana ufahamu hata kidogo wa nia nzuri za Mungu. Wakati majaribu yanapotajwa, watu wanahisi ni kana kwamba Mungu ana nia zilizofichwa na hata wengine wanaamini kwamba Mungu ana mipango miovu, wasijue hata kile ambacho Mungu atawafanyia; hivyo, kwa wakati huohuo wanaotaka kuwa watiifu kabisa kwa ukuu na mipangilio ya Mungu, wanafanya kila wawezalo kuzuia na kupinga ukuu wa Mungu juu ya binadamu na mipangilio Yake kwa binadamu, kwani wanasadiki kwamba kama hawatakuwa makini watapotoshwa na Mungu, na kwamba ikiwa hawataendelea kushikilia hatima zao wenyewe, basi kila kitu walicho nacho kinaweza kuchukuliwa na Mungu, na maisha yao huenda hata yakaisha. Binadamu yumo katika kambi la Shetani, lakini hawi na wasiwasi kamwe kuhusu kunyanyaswa na Shetani, na ananyanyaswa na Shetani lakini haogopi kamwe kuchukuliwa mateka na Shetani. Siku zote anasema kwamba anaukubali wokovu wa Mungu, ilhali hajawahi kumwamini Mungu au kuamini kwamba Mungu atamwokoa kwa kweli kutoka kwenye makucha ya Shetani. Kama, sawa na Ayubu, binadamu anaweza kunyenyekea kwa mipango na mipangilio ya Mungu na anaweza kuitoa nafsi yake yote mikononi mwa Mungu, basi, je, hatima ya binadamu haitakuwa sawa na ile ya Ayubu—kupokea baraka za Mungu? Kama binadamu anaweza kukubali na kunyenyekea katika utawala wa Mungu, ni, nini kipo cha kupoteza? Na hivyo Napendekeza kwamba uwe mwangalifu katika matendo yako, na uwe mwangalifu kwa kila kitu kitakachokuja juu yako. Usiwe na pupa au kutenda bila kufikiria, na usimtendee Mungu na watu, mambo, na vitu ambavyo Amekupangia kwa kutegemea mihemko au asili yako, au kulingana na mawazo yako na dhana zako; lazima uwe makini katika vitendo vyako, na lazima uombe na utafute zaidi, ili kuepuka kuichochea hasira ya Mungu. Kumbuka hili!

Kisha, tutaangalia jinsi Ayubu alivyokuwa baada ya majaribio yake.

5. Ayubu Baada ya Majaribio Yake

Ayubu 42:7-9 Na basi ikawa, kwamba baada ya Yehova kusema maneno haya kwa Ayubu, Yehova akasema kwa Elifazi Mtemani, Ghadhabu yangu inawaka dhidi yako, na dhidi ya hao marafiki zako wawili: kwa sababu nyinyi hamjasema kunihusu kile kilicho sawa, jinsi alivyofanya mtumishi Wangu Ayubu. Kwa hivyo sasa, jichukulieni ng’ombe wa kiume saba, na kondoo wa kiume saba, na muende kwake mtumishi Wangu Ayubu, na mjitolee sadaka ya kuteketezwa; na mtumishi Wangu Ayubu atawaombea: kwa kuwa yeye nitamkubali: Nisije nikawatendea kulingana na makosa yenu, hivi kwamba nyinyi hamkusema kunihusu kile kilicho sawa, kama alivyofanya mtumishi Wangu Ayubu. Hivyo Elifazi Mtemani, na Bildadi Mshuhi, na Sofari Mnaamathi, wakaenda, na kufanya vile Yehova alivyowaamrisha: Yehova pia akamkubali Ayubu.

Ayubu 42:10 Naye Yehova akaubadilisha uteka wa Ayubu, wakati alipowaombea marafiki zake: Yehova pia akampa Ayubu kiasi kilichozidishwa mara mbili kuliko yale aliyokuwa nayo awali.

Ayubu 42:12 Kwa hivyo Yehova akabariki Ayubu zaidi baadaye maishani kuliko mwanzo wake: kwa sababu alikuwa na kondoo elfu kumi na nne, na ngamia elfu sita, na elfu moja ya jozi za ng’ombe, na elfu moja ya punda wa kike.

Ayubu 42:17 Kwa hivyo Ayubu akafariki, akiwa mzee na aliyejawa na siku.

Wale Wanaomcha Mungu na Kujiepusha Na Maovu Wanatazamwa kwa Upendo na Mungu, Huku Wale Walio Wapumbavu Wanaonekana kuwa Duni na Mungu

Katika Ayubu 42:7-9, Mungu Anasema kwamba Ayubu ni mtumishi Wake. Matumizi Yake ya neno “mtumishi” kumrejelea Ayubu yanaonyesha umuhimu wa Ayubu katika moyo Wake; ingawa Mungu hakumwita Ayubu kitu chenye heshima zaidi, jina hili halikuwa na uhusiano wowote na umuhimu wa Ayubu ndani ya moyo wa Mungu. “Mtumishi” hapa ni jina la lakabu la Mungu kwa Ayubu. Marejeleo mengi ya Mungu kwa “mtumishi Wangu Ayubu” yanaonyesha jinsi ambavyo Alipendezwa na Ayubu, ingawa Mungu hakusema kuhusu maana iliyopo katika neno “mtumishi,” ufafanuzi wa Mungu wa neno “mtumishi” unaweza kuonekana kupitia kwa maneno Yake katika kifungu hiki cha maandiko. Kwanza Mungu alimwambia Elifazi Mtemani: “ghadhabu Yangu inawaka juu yako, na juu ya hao marafiki zako wawili; kwa kuwa ninyi hamkunena yaliyo sawa katika habari Zangu, kama jinsi alivyonena mtumishi Wangu Ayubu.” Maneno haya ndiyo mara ya kwanza kwa Mungu kuwaambia watu waziwazi kwamba alikuwa Ameyakubali yale yote yaliyokuwa yamesemwa na kufanywa na Ayubu baada ya majaribio ya Mungu kwake, na ndio kwa mara ya kwanza Alikuwa amethibitisha waziwazi ukweli na usahihi wa yale yote Ayubu aliyokuwa ameyafanya na kuyasema. Mungu alikuwa na ghadhabu kwa Elifazi na wengine kwa sababu ya mazungumzo yao yasiyokuwa sahihi na ya kipumbavu, kwa sababu, kama Ayubu hawakuweza kuuona uso wa Mungu au kuyasikia maneno Aliyosema maishani mwao, lakini Ayubu alikuwa na maarifa sahihi ya Mungu, huku wao waliweza tu kukisia bila kuelewa kuhusu Mungu, wakienda kinyume na mapenzi ya Mungu katika yote waliyoyafanya na wakamfanya Ajisikie kuwachukia. Kwa hivyo, kwa wakati huo huo Akikubali yale yote yaliyokuwa yamefanywa na kusemwa na Ayubu, Mungu alizidi kuongeza hasira Zake kwa wale wengine, kwani sio tu kwamba ndani yao Hakuweza kuona uhalisia wowote wa kumcha Mungu, bali pia hawakuwa na chochote cha kumcha Mungu kwa yale waliyoyasema. Na hivyo kilichofuata Mungu alitoa mahitaji yafuatayo kwao. “Kwa hivyo sasa, jichukulieni ng’ombe wa kiume saba, na kondoo wa kiume saba, na muende kwake mtumishi wangu Ayubu, na mjitolee sadaka ya kuteketezwa; na mtumishi wangu Ayubu atawaombea: kwa kuwa yeye nitamkubali: nisije nikawatendea kulingana na makosa yenu.” Katika kifungu hiki Mungu anamwambia Elifazi na wengine kufanya jambo ambalo litakomboa dhambi zao, kwani upumbavu wao ulikuwa ni dhambi dhidi ya Yehova Mungu, na hivyo wangelazimika kutoa sadaka za kuteketezwa ili kusahihisha makosa yao. Sadaka za kuteketezwa mara nyingi hutolewa kwa Mungu, lakini jambo lisilo la kawaida kuhusu sadaka hizi za kuteketezwa ni kwamba zilitolewa kwa Ayubu. Ayubu alikubaliwa na Mungu kwa sababu alitoa ushuhuda kwa Mungu wakati wa majaribio yake. Marafiki hawa wa Ayubu, wakati huo huo, walifichuliwa wakati wa majaribio yake, kwa sababu ya upumbavu wao, walishutumiwa na Mungu na wakachochea hasira ya Mungu, na wanapaswa kuadhibiwa na Mungu—kuadhibiwa kwa kutoa sadaka za kuteketezwa mbele ya Ayubu—na baadaye Ayubu aliwaombea ili kuiondoa ile adhabu na hasira ya Mungu kwao. Nia ya Mungu ilikuwa ni kuwaaibisha wao, kwani hawakuwa watu waliomcha Mungu na kujiepusha na maovu, na walikuwa wameshutumu uadilifu wa Ayubu. Kwa upande mmoja, Mungu alikuwa akiwaambia kwamba Hakukubali matendo yao, bali Alimkubali sana na kumfurahia Ayubu; kwa upande mwingine, Mungu alikuwa akiwaambia kwamba kukubaliwa na Mungu kunamwinua mwanadamu mbele ya Mungu, kwamba binadamu anachukiwa na Mungu kwa sababu ya upumbavu wake, na anamkosea Mungu kwa sababu hiyo, na ni duni na mchafu machoni pa Mungu. Huu ndio ufafanuzi uliotolewa na Mungu kuhusu watu wa aina mbili, ni mitazamo ya Mungu kwa watu hawa wa aina mbili, na ni ufafanuzi wa Mungu kuhusu thamani na hadhi ya watu wa aina hizi mbili. Ingawa Mungu alimwita Ayubu mtumishi Wake, machoni pa Mungu huyu “mtumishi” alikuwa mpendwa Wake, na alipewa mamlaka ya kuwaombea wengine na kuwasamehe makosa yao. “Mtumishi huyu” aliweza kuzungumza moja kwa moja na Mungu na kuja moja kwa moja mbele za Mungu, na hadhi yake ilikuwa ya juu na yenye kuheshimika zaidi kuliko ya wale wengine. Hii ndiyo maana halisi ya neno “mtumishi” kama ilivyonenwa na Mungu. Ayubu alipewa heshima hii ya pekee kwa sababu ya uchaji wake kwa Mungu na kujiepusha na maovu, na sababu iliyofanya wengine wasiitwe watumishi na Mungu ni kwa sababu hawakumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Mitazamo hii miwili tofauti ya Mungu ni mitazamoeo yake kwa watu wa aina mbili: Wale wanaomcha Mungu na kujiepusha na maovu wanakubaliwa na Mungu, na wanaonekana wenye thamani machoni Pake, huku wale ambao ni wapumbavu hawamchi Mungu na hawawezi kujiepusha na maovu, na hawawezi kupokea kibali cha Mungu, mara nyingi wanachukiwa na kushutumiwa na Mungu, na ni wa hali ya chini machoni pa Mungu.

Mungu Anampa Ayubu Mamlaka

Ayubu aliwaombea marafiki zake, na baadaye, kwa sababu ya maombi ya Ayubu, Mungu hakuwatendea kama walivyostahili juu ya upumbavu wao—Hakuwaadhibu au kuchukua adhabu yoyote dhidi yao. Na kwa nini ilikuwa hivyo? Ilikuwa ni kwa sababu maombi yaliyotolewa kwa ajili yao na mtumishi wa Mungu, Ayubu, yalikuwa yamefikia masikio Yake; Mungu aliwasamehe kwa sababu Aliyakubali maombi ya Ayubu. Na tunaona nini katika haya? Mungu anapombariki mtu, Anampa thawabu nyingi, na si za kimwili tu: Mungu anawapa pia mamlaka, na Kuwapa haki ya kuwaombea wengine, na Mungu husahau na kusamehe makosa ya watu hao kwa sababu Anayasikia maombi haya. Haya ndiyo mamlaka yenyewe ambayo Mungu alimpa Ayubu. Kupitia kwa maombi ya Ayubu ya kusitisha kushutumiwa kwao, Yehova Mungu aliwaletea aibu wale watu wapumbavu—ambayo, bila shaka, ndiyo iliyokuwa adhabu Yake maalum kwa Elifazi na wale wengine.

Ayubu Anabarikiwa kwa Mara Nyingine Tena na Mungu, na Hashtakiwi Tena na Shetani

Miongoni mwa matamko ya Yehova Mungu kuna maneno kwamba “nyinyi hamkusema maneno yaliyo sawa katika habari Zangu, kama alivyonena mtumishi Wangu Ayubu.” Ni nini kile ambacho Ayubu alikuwa amesema? Ni kile tulichozungumzia hapo awali, pamoja na kile ambacho kurasa nyingi za maneno katika kitabu cha Ayubu ambacho Ayubu amerekodiwa kuwa aliyasema. Katika kurasa hizi nyingi za maneno, Ayubu hajawahi hata mara moja kuwa na malalamiko au mashaka yoyote kumhusu Mungu. Yeye anasubiria tu matokeo. Ni kusubiri huku ambako ndiko mtazamo wake wa utiifu, ulipatikana, na kutokana na maneno aliyomwambia Mungu, Ayubu alikubaliwa na Mungu. Alipovumilia majaribio na kuteseka, Mungu alikuwa kando yake, na ingawa mateso yake hayakupunguzwa na uwepo wa Mungu, Mungu aliona kile Alichotaka kuona na kusikia kile Alichotaka kusikia. Kila mojawapo ya matendo na maneno ya Ayubu yaliweza kufikia macho na masikio ya Mungu; Mungu alisikia na Akaona—na huu ni ukweli. Maarifa ya Ayubu kumhusu Mungu na fikira zake kumhusu Mungu katika moyo wake wakati huo, katika kipindi hicho, hayakuwa dhahiri sana kama kama ya watu wa leo, lakini katika muktadha wa wakati huo, Mungu aliweza kutambua bado kila kitu alichokuwa amesema, kwa sababu tabia yake na fikira zake ndani ya moyo wake, na kile alichokuwa ameeleza na kufichua, yalitosha kwa mahitaji Yake. Kwa ule wakati ambao Ayubu alipitia majaribio, yale ambayo alifikiria katika moyo wake na kuamua kuyafanya yaliweza kumwonyesha Mungu matokeo, ambayo yalimtosheleza Mungu, na baadaye Mungu akayaondoa majaribio ya Ayubu, Ayubu alitoka katika taabu zake, na majaribio yake yakawa yameondoka yasiwahi kumpata tena. Kwa sababu Ayubu alikuwa tayari amepitia majaribio, na akawa amesimama imara katika majaribio haya, na akamshinda kabisa Shetani, Mungu alimpatia baraka ambazo kwa kweli alistahili. Kama ilivyorekodiwa katika Ayubu 42:10, 12, Ayubu alibarikiwa kwa mara nyingine tena, na akabarikiwa hata zaidi ya mara ya kwanza. Wakati huu Shetani alikuwa amejiondoa, na hakusema tena au kufanya chochote, na kuanzia hapo na kuendelea Ayubu hakusumbuliwa au kushambuliwa tena na Shetani, na Shetani hakutoa mashtaka tena dhidi ya baraka za Mungu kwa Ayubu.

Ayubu Aishi Nusu ya Mwisho ya Maisha Yake Katikati ya Baraka za Mungu

Ingawa baraka Zake wakati huo zilikuwa tu zinajumuisha kondoo, ng’ombe, ngamia, mali, na kadhalika, baraka ambazo Mungu alitaka kumpa Ayubu katika moyo Wake zilikuwa nyingi zaidi ya hizi. Kwa wakati huo, je, kulirekodiwa, ni aina gani za ahadi za milele ambazo Mungu alipenda kumpa Ayubu? Katika baraka Zake kwa Ayubu, Mungu hakugusia au kutaja kuhusu mwisho wake, na haijalishi umuhimu au nafasi ambayo Ayubu alikuwa nayo ndani ya moyo wa Mungu, kwa ujumla Mungu alikuwa mwangalifu sana katika baraka Zake. Mungu hakutangaza mwisho wa Ayubu. Hii inamaanisha nini? Kwaawkati huo, ambao mpango wa Mungu ulikuwa bado haujafikia sehemu ya kutangaza mwisho wa binadamu, mpango huo ulikuwa bado haujaingia katika hatua ya mwisho ya kazi yake, Mungu hakutaja chochote kuhusu mwisho, alitoa tu baraka za kimwili kwa mwanadamu. Maana ya hii ni kwamba nusu ya mwisho ya maisha ya Ayubu ilipita katikati ya baraka za Mungu na hii ndiyo iliyomfanya kuwa tofauti na wale watu wengine—lakini kama wao alizeeka, na kama mtu yeyote yule wa kawaida siku ilifika ambapo aliuambia ulimwengu kwaheri. Na hivyo imerekodiwa kwamba “Kwa hivyo Ayubu akafa, akiwa mzee na aliyejawa na siku” (Ayubu 42:17). Ni nini maana ya “akafa akiwa amejawa na siku” hapa? Katika enzi ambayo Mungu alikuwa bado Hajatangaza mwisho wa watu, Mungu aliweka muda wa kuishi kwa Ayubu, na wakati umri huo ulipofika Alimruhusu Ayubu kuondoka kwa kawaida kutoka kwenye ulimwengu huu. Kuanzia kwenye baraka ya pili ya Ayubu hadi kifo chake, Mungu hakuongeza ugumu wowote zaidi. Kwa Mungu, kifo cha Ayubu kilikuwa cha kawaida, na pia cha lazima; kilikuwa kitu cha kawaida sana na wala si hukumu au shutuma. Alipokuwa hai, Ayubu alimwabudu na kumcha Mungu; kuhusiana na aina ya mwisho aliokuwa nao baada ya kifo chake, Mungu hakusema chochote, wala kutoa maoni yoyote kuhusu hilo. Mungu ni mwenye utaratibu sana katika kile Anachosema na kufanya, na maudhui na kanuni za maneno na matendo Yake yanaendana na hatua ya kazi Yake na kipindi ambacho Anafanya kazi. Ni mwisho wa aina gani ambao mtu kama Ayubu alikuwa nao katika moyo wa Mungu? Je, Mungu alikuwa amefikia uamuzi wa aina yoyote katika moyo Wake? Bila shaka Alikuwa! Ni vile tu hili lilikuwa halijulikani kwa binadamu; Mungu hakutaka kumwambia binadamu wala Hakuwa na nia yoyote ya kumwambia binadamu. Na hivyo, kwa kuongea kwa juujuu tu, Ayubu alikufa akiwa amejawa na siku, na hivyo ndivyo maisha ya Ayubu yalivyokuwa.

Thamani ya Maisha Aliyoishi kwa kudhirisha Ayubu Wakati wa Maisha Yake

Je, Ayubu aliishi maisha yenye thamani? Thamani yake ilikuwa wapi? Ni kwa nini inasemwa kwamba aliishi maisha yenye thamani? Kwa binadamu, thamani yake ilikuwa gani? Kutoka katika mtazamo wa binadamu, aliwawakilisha wanadamu ambao Mungu anataka kuwaokoa, kwa kuwa na ushuhuda wa kipekee kwa Mungu mbele ya Shetani na watu wa ulimwengu. Alitimiza wajibu ambao ulistahili kutimizwa na kiumbe wa Mungu, na kuweka mfano halisi wa kuigwa, na kutenda kama kielelezo, kwa wale wote ambao Mungu angependa kuwaokoa, akiwaruhusu watu kuona kwamba inawezekana kabisa kumshinda Shetani kwa kumtegemea Mungu. Thamani yake kwa Mungu ilikuwa ni ipi? Kwa Mungu, thamani ya maisha ya Ayubu ilikuwa ndani ya uwezo wake wa kumcha Mungu, kumwabudu Mungu, kushuhudia matendo ya Mungu, na kusifu matendo ya Mungu, kumletea Mungu faraja na kitu cha kufurahia; kwa Mungu, thamani ya maisha ya Ayubu ilikuwa pia kwa namna ambavyo, kabla ya kifo chake, Ayubu alipitia majaribio na kumshinda Shetani, na akawa na ushuhuda wa kipekee kwa Mungu mbele ya Shetani na watu wa ulimwengu, ili kwamba Mungu apate utukufu miongoni mwa wanadamu, akiutuliza moyo wa Mungu na kuuruhusu moyo wa Mungu wenye shauku uyaone matokeo, na kuliona tumaini. Ushuhuda wake uliweka kielelezo cha uwezo wa kusimama imara katika ushuhuda wa mtu kwa Mungu, na kuweza kumwaibisha Shetani kwa niaba ya Mungu, katika kazi ya Mungu ya kuwasimamia wanadamu. Je, hii si thamani ya maisha ya Ayubu? Ayubu alileta tulizo kwa moyo wa Mungu, alimpa Mungu kionjo cha furaha ya kutukuzwa, na akaanzisha mwanzo mzuri kwa mpango wa usimamizi wa Mungu. Na kuanzia wakati huo na kuendelea, jina la Ayubu likawa ishara ya kutukuzwa kwa Mungu, na ishara ya ushindi wa wanadamu dhidi ya Shetani. Kile Ayubu aliishi kwa kudhihirisha wakati wa maisha yake na ushindi wake wa kipekee dhidi ya Shetani milele utabakia ukifurahiwa mno na Mungu, na ukamilifu wake, unyoofu, na uchaji wake kwa Mungu utaheshimiwa na kuigwa na vizazi vitakavyokuja. Atathaminiwa milele na Mungu kama lulu inayong'aa, isiyo na dosari, na hivyo pia anastahili kuthaminiwa na mwanadamu!

Kisha, hebu tuangalie kazi ya Mungu wakati wa Enzi ya Sheria.

D. Taratibu za Enzi ya Sheria

Amri Kumi

Kanuni za Kujenga Madhabahu

Taratibu za Kuwatendea Watumishi

Taratibu za Wizi na Fidia

Kushika Mwaka wa Sabato na Sikukuu Tatu

Taratibu za Siku ya Sabato

Taratibu za Kutoa Sadaka

Sadaka za kuteketezwa

Sadaka za Nafaka

Sadaka za Amani

Sadaka za Dhambi

Sadaka za Hatia

Taratibu za Sadaka za Kuhani (Haruni na Watoto Wake wa Kiume Waamrishwa Kutii)

Sadaka za Kuteketezwa na Kuhani

Sadaka za Nafaka na Kuhani

Sadaka za Dhambi na Kuhani

Sadaka za Hatia na Kuhani

Sadaka za Amani na Kuhani

Taratibu za Ulaji wa Sadaka na Kuhani

Wanyama Walio Halali na Wale Walio Haramu (Wale Wanaoweza na Wasioweza Kuliwa)

Taratibu za Utakasaji wa Wanawake Baada ya Kujifungua

Viwango vya Uchunguzi wa Ukoma

Taratibu kwa Wale Ambao Wameponywa Ukoma

Taratibu za Kuzitakasa Nyumba Zilizoambukizwa

Taratibu za Wale Wanaosumbuliwa na Kutokwa na Uchafu Usio wa Kawaida

Siku ya Upatanisho Wa Mungu na Binadamu Ambayo Lazima Iadhimishwe Mara Moja Kwa Mwaka

Sheria za Kuchinja Ng’ombe na Mbuzi

Katazo kwa Kufuata Matendo ya Kuchukiza ya Watu wa Mataifa (Kutokuoana Ndugu kwa Ndugu, na Kadhalika)

Taratibu Ambazo Lazima Zifuatwe na Watu (“Mtakuwa watakatifu: kwani Mimi Yehova Mungu wenu ni mtakatifu” (Walawi 19:2))

Kunyongwa kwa Wale Wanaotoa Watoto Wao Kafara kwa Moleki

Taratibu za Adhabu ya Uhalifu wa Uasherati

Sheria Zinazopaswa Kuzingatiwa na Makuhani (Sheria za Tabia Yao ya Kila Siku, Sheria za Matumizi ya Vitu Vitakatifu, Sheria za Kutoa Sadaka na Kadhalika)

Sikukuu Zinazopaswa Kuadhimishwa (Siku ya Sabato, Pasaka, Pentekoste, Siku ya Upatanisho, na Kadhalika)

Taratibu Nyinginezo (Kuwashwa kwa Taa, Mwaka wa Jubilii, Ukombozi wa Ardhi, Ulaji wa Viapo, Utoaji wa Zaka, na Kadhalika)

Taratibu za Enzi ya Sheria ni Thibitisho la Kweli la Mwongongozo wa Mungu kwa Wanadamu Wote

Hivyo, mmezisoma taratibu na kanuni hizi za Enzi ya Sheria, sivyo? Je, taratibu hizi zinajumuisha mawanda mapana? Kwanza, zinajumuisha Amri Kumi, na baada ya hizo kuna taratibu za namna ya kujenga madhabahu, na kadhalika. Hizo zinafuatwa na taratibu za kushika Sabato na kuadhimisha sikukuu tatu, na baada ya hizo kuna taratibu za kutoa sadaka. Je, mnaona kuna aina ngapi za sadaka ambazo zipo? Kuna sadaka za kuteketezwa, sadaka za nafaka, sadaka za amani, sadaka za dhambi, na kadhalika. Zinafuatwa na taratibu za sadaka za kuhani, zikiwemo sadaka za kuteketezwa na sadaka za nafaka zilizotolewa na Kuhani, na aina nyingine za sadaka. Taratibu za nane ni za ulaji wa sadaka na Kuhani. Na kisha kuna taratibu zinazopaswa kudumishwa wakati wa maisha ya watu. Kuna masharti ya vipengele vingi vya maisha ya watu, kama vile taratibu za kile wanachoweza au wasichoweza kula, za utakasaji wa wanawake baada ya wao kujifungua, na kwa wale ambao wameponywa ugonjwa wa ukoma. Katika taratibu hizi, Mungu Anafikia hadi kiwango cha kuzungumzia kuhusu ugonjwa, na kunazo hata sheria za kuchinja kondoo na ng’ombe, na kadhalika. Kondoo na ng’ombe waliumbwa na Mungu, na hivyo unapaswa kuwachinja jinsi Mungu anavyokuambia; bila shaka, kuna, sababu kwa maneno ya Mungu; na kwa hakika ni sawa kutenda kama ilivyoamriwa na Mungu, na kwa kweli itakuwa ni ya manufaa kwa watu! Pia kuna sikukuu na sheria zinazopaswa kufuatwa, kama vile siku ya Sabato, Pasaka, na nyinginezo—Mungu alizungumzia juu ya haya yote. Hebu tuangalie zile za mwisho: taratibu nyinginezo—kuwasha taa, mwaka wa Jubilii, ukombozi wa ardhi, ulaji wa viapo, utoaji wa zaka, na kadhalika. Je, hizi zinajumuisha mawanda mapana? Kitu cha kwanza cha kuzungumziwa ni suala la sadaka za watu, kisha kuna utaratibu kwa uwizi na fidia, na kushika siku ya Sabato…; kila moja ya maelezo ya maisha yanahusishwa. Hivi ni kusema, wakati Mungu alianza kazi Yake rasmi ya mpango Wake wa usimamizi, Aliweka wazi taratibu nyingi ambazo zilipaswa kufuatwa na binadamu. Taratibu hizi zilikuwa ni ili kumruhusu binadamu kuishi maisha ya kawaida ya binadamu hapa duniani, maisha ya kawaida ya binadamu ambayo hayajatenganishwa na Mungu na uongozi Wake. Mungu alimwambia binadamu kwanza namna ya kujenga madhabahu, namna ya kupangilia madhabahu. Baada ya hapo, Alimwambia binadamu namna ya kutoa sadaka, na kubainisha jinsi ambavyo mwanadamu alipaswa kuishi—kile alichopaswa kuzingatia katika maisha, kile alichopaswa kutii, na kile alichopaswa na ambacho hakupaswa kufanya. Kile ambacho Mungu aliweka wazi kwa binadamu kilikuwa kinajumuisha yote, na kwa hizi desturi, taratibu, na kanuni Alidhibiti tabia za watu, Aliyaongoza maisha yao, Aliongoza kuanza kwao kuingia katika sheria za Mungu, Aliwaongoza kuja mbele ya madhabahu ya Mungu, Aliwaongoza katika kuishi maisha miongoni mwa vitu vyote ambavyo Mungu alikuwa amemuumbia mwandamu ambavyo vilikuwa na utaratibu, ukawaida, na kiasi. Kwanza Mungu alitumia taratibu na kanuni hizi rahisi ili kuweka mipaka kwa binadamu, ili kwamba hapa duniani mwandamu aweze kuwa na maisha ya kawaida ya kumwabudu Mungu, aweze kuwa na maisha ya kawaida ya mwanadamu; hivi ndivyo yalivyo maudhui mahususi ya mwanzo wa mpango Wake wa usimamizi wa miaka elfu sita. Taratibu na sheria zinajumuisha maudhui mapana mno, yote ni maelezo ya mwongozo wa Mungukwa mwanadamu wakati wa Enzi ya Sheria, ilikuwa ni lazima yakubaliwe na kuheshimiwa na watu waliokuwa katika Enzi ya Sheria, ni rekodi ya kazi iliyofanywa na Mungu katika Enzi ya Sheria, na ni uthibitisho wa kweli wa uongozi na mwongozo wa Mungu kwa wanadamu wote.

Wanadamu DaimaHawatenganishwi na Mafundisho na Ruzuku ya Mungu

Katika taratibu hizi tunaona kwamba mtazamo wa Mungu katika kazi Yake, katika usimamizi Wake, na kwa wanadamu ni wa umakinifu zaidi, wa uangalifu, wa kina, na wa kuwajibika. Anaifanya kazi ambayo lazima Afanye miongoni mwa wanadamu kulingana na hatua Zake, bila ya hitilafu hata kidogo, Akiongea maneno ambayo nilazima Ayaongee kwa wanadamu bila ya kosa au upungufu hata kidogo, Akimruhusu binadamu kuona kwamba hawezi kutenganishwa na uongozi wa Mungu, na Akimwonyesha namna ambavyo yale yote ambayo Mungu anayafanya na kuyasema yana umuhimu kwa wanadamu. Bila kujali jinsi mwanadamu alivyo katika enzi iliyofuata, kwa ufupi, mwanzoni kabisa—wakati wa Enzi ya Sheria—Mungu aliyafanya mambo haya rahisi. Kwa Mungu, dhana za watu kumhusu Mungu, ulimwengu na mwanadamu katika enzi hiyo zilikuwa za kidhahania na zisizoeleweka, na ingawaje walikuwa na fikra na nia zenye utambuzi, zote zilikuwa hazina uwazi na si sahihi, na hivyo wanadamu walikuwa hawawezi kutenganishwa kutoka kwa mafundisho na utoaji wa Mungu kwao. Wanadamu wa hapo awali hawakujua chochote, na hivyo Mungu alilazimika kuanza kumfunza binadamu kuanzia kwenye kanuni za juujuu na za kimsingi zaidi kwa minajili ya kuishi na taratibu zinazohitajika za kuishi, Akiingiza mambo haya katika moyo wa binadamu kidogo kidogo, na kumpa binadamu uelewa wa Mungu kwa utaratibu, kutambua na kuelewa uongozi wa Mungu kwa utaratibu, na dhana ya kimsingi ya uhusiano kati ya binadamu na Mungu, kupitia kwa taratibu hizi na kupitia kwa sheria hizi, ambazo zilikuwa za maneno. Baada ya kufikia matokeo haya, ndipo Mungu alipoweza tu, kidogo kidogo, kufanya kazi ambayo Angeweza kufanya baadaye, na hivyo taratibu hizi na kazi iliyofanywa na Mungu katika Enzi ya Sheria zikawa ndiyo msingi wa kazi Yake ya kuwaokoa wanadamu na hatua ya kwanza ya kazi katika mpango wa usimamizi wa Mungu. Ingawa, kabla ya kazi ya Enzi ya Sheria, Mungu alikuwa amezungumza na Adamu, Hawa, na vizazi vyao, lakini amri na mafundisho hayo hayakuwa na mpangilio au mahususi kiasi cha kutolewa moja baada ya nyingine kwa mwanadamu, na hayakuwa yameandikwa, wala hazikuwa kanuni. Hii ni kwa sababu, kwa wakati huo, mpango wa Mungu haukuwa umeenda mbali kiasi hicho; ni pale tu Mungu alipomwongoza mwanadamu kwenye hatua hii ndipo Alipoanza kuzungumza taratibu hizi za Enzi ya Sheria, na kuanza kumfanya binadamu kuzitekeleza. Ulikuwa ni mchakato unaohitajika, na matokeo yasingeweza kuepukika. Desturi na taratibu hizi rahisi zinamwonyesha binadamu hatua za usimamizi wa kazi ya Mungu na hekima ya Mungu inayofichuliwa katika mpango Wake wa usimamizi. Mungu anajua ni maudhui yapi na ni mbinu zipi za kutumia ili kuanza, ni mbinu zipi za kutumia ili kuendelea, na ni mbinu zipi za kutumia katika kumalizia ili kwamba Aweze kupata kundi la watu wanaotoa ushuhuda Kwake, Aweze kupata kundi la watu wenye mawazo sawa na Yake. Anajua kile kilicho ndani ya mwanadamu, na kujua kile kinachokosekana kwa mwanadamu, Anajua kile Anachopaswa kutoa, na jinsi Anavyopaswa kumwongoza mwanadamu, na vivyo hivyo Anajua kile ambacho mwanadamu anapaswa na asichopaswa kufanya. Mwanadamu ni kama kikaragosi: Hata ingawa hakuwa na uelewa wowote wa mapenzi ya Mungu, alilazimika kuongozwa na kazi ya Mungu ya usimamizi, hatua kwa hatua hadi leo. Hapakuwa na chochote kile kisichojulikana katika moyo wa Mungu kuhusu kile Alichopaswa kufanya; katika moyo wake kulikuwa na mpango ulio wazi na dhahiri sana, na Alitekeleza kazi ambayo Yeye Mwenyewe alitaka kuifanya kulingana na hatua Zake na mpango Wake, Akiendelea mbele kutoka kwa ule wa juujuu hadi wa kina. Hata ingawa Hakuwa ameonyesha kazi ambayo Angeifanya baadaye, kazi Yake iliyofuata bado iliendelea kutekelezwa na kuendelea mbele kulingana kabisa na mpango Wake, ambayo ni maonyesho ya kile Mungu anacho na alicho, na pia ni mamlaka ya Mungu. Haijalishi ni hatua ipi ya mpango Wake wa usimamizi ambao Anafanya kazi, tabia Yake na kiini Chake vinamwakilisha Yeye mwenyewe. Hii ni kweli kabisa. Bila kujali enzi, au hatua ya kazi, kuna mambo ambayo hayatabadilika kamwe: ni watu wa aina gani ambao Mungu anawapenda, ni watu wa aina gani ambao Anawachukia, tabia Yake na yote ambayo Anayo na Aliyo. Ijapokuwa taratibu na kanuni hizi ambazo Mungu alizianzisha katika kazi ya Enzi ya Sheria zinaonekana kuwa ni rahisi na za juujuu kwa watu wa leo, na hata ingawa ni rahisi kueleweka na kutimizwa, ndani ya hizo bado kuna hekima ya Mungu, na bado kuna tabia ya Mungu na kile ambacho Anacho na Alicho. Kwani ndani ya taratibu hizi zinazoonekana rahisi, uwajibikaji na utunzaji wa Mungu kwa wanadamu unaonyeshwa, na kiini kizuri cha fikira zake, hivyo kumruhusu mwanadamu kutambua kwa uhakika ukweli kwamba Mungu anatawala juu ya vitu vyote na vitu vyote vinadhibitiwa na mkono Wake. Haijalishi ni kiwango kipi cha maarifa ambacho wanadamu watajifunza, au ni nadharia ngapi au mafumbo mangapi anayoyaelewa, kwa Mungu hakuna hata moja kati ya hizi inayoweza kuchukua nafasi ya utoaji Wake, na uongozi Wake kwa wanadamu; wanadamu milele hawatatenganishwa na mwongozo wa Mungu na kazi ya kibinafsi ya Mungu. Huu ndio uhusiano usioweza kutenganishwa kati ya mwanadamu na Mungu. Haijalishi kama Mungu anakupa amri, au taratibu, au Anakupa ukweli ili kuyaelewa mapenzi Yake, haijalishi ni nini Anachofanya, nia ya Mungu ni kumwongoza binadamu hadi katika siku nzuri ya kesho. Maneno yaliyotamkwa na Mungu na kazi Anayofanya ni ufunuo wa kipengele kimoja cha kiini Chake, na vilevile ni ufunuo wa kipengele kimoja cha tabia Yake na hekima Yake, zote hizi ni hatua za lazima katika mpango Wake wa usimamizi. Hili halifai kupuuzwa! Mapenzi ya Mungu yamo katika chochote Anachofanya; Mungu haogopi maoni yasiyo sahihi, wala haogopi dhana au fikira zozote za binadamu kuhusu Yeye. Yeye hufanya kazi Yake tu na kuendeleza usimamizi Wake kulingana na mpango Wake wa usimamizi, usiozuiliwa na mtu yeyote, jambo lolote, au kitu chochote.

Vyema. Ni hayo tu kwa leo. Tuonane wakati mwingine!

Novemba 9, 2013

Iliyotangulia: Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I

Inayofuata: Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp