Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III

Vikao hivi kadhaa vya ushirika vimekuwa na athari kubwa kwa kila mmoja wa watu. Kwa sasa, watu wanaweza hatimaye kuhisi uwepo wa kweli wa Mungu na kwamba Mungu kwa hakika yuko karibu sana na wao. Ingawa watu wamemwamini Mungu kwa miaka mingi, hawajawahi kuelewa kwa kweli mawazo na fikira Zake kama wanavyozielewa sasa, wala hawajawahi kupata kwa kweli uzoefu wa matendo Yake halisi kama walio nao kwa sasa. Kama ni maarifa au matendo halisi, watu wengi wamejifunza kitu kipya na kutimiza ufahamu wa juu zaidi, na wametambua kosa lililopo katika ufuatiliaji wao wa kale, wametambua hali yao waliyopitia ya juujuu na kwamba mambo mengi sana hayaambatani na mapenzi ya Mungu, na wametambua kwamba kile ambacho binadamu amepungukiwa nacho zaidi ni maarifa ya tabia ya Mungu. Maarifa haya kwa upande wa watu ni aina ya maarifa ya utambuzi; kufikia kiwango cha maarifa ya kirazini kunahitaji ushughulikiaji wa kina na utiliaji mkazo wa utaratibu kwenye hali yao yote wanayopitia. Kabla ya binadamu kumwelewa Mungu kwa njia ya kweli, kwa dhahania inaweza kusemekana kwamba wanaamini kwa uwepo wa Mungu mioyoni mwao, lakini hawana ufahamu halisi wa maswali mahususi kama vile Yeye ni Mungu wa aina gani kwa hakika, mapenzi Yake ni nini, tabia Yake ni ipi, na mtazamo Wake halisi kwa binadamu ni upi. Hali hii huhusisha pakubwa imani ya watu katika Mungu—imani yao haiwezi kwa ufupi kufikia utakatifu au ukamilifu. Hata kama utakuwa ana kwa ana na neno la Mungu, au kuhisi kwamba umekumbana na Mungu kupitia katika hali zako ulizopitia, bado haiwezi kusemwa kwamba unamwelewa Yeye kabisa. Kwa sababu hujui fikira za Mungu, au kile Anachopenda na kile Anachochukia, kile kinachomfanya kuwa na ghadhabu na kile kinachomletea furaha, huna ufahamu wa kweli kumhusu. Imani yako imejengwa katika msingi wa hali isiyokuwa dhahiri na ile ya fikira, kwa msingi wa matamanio yako ya dhahania. Bado ingali mbali na imani halisi, na wewe bado ungali mbali na kuwa mfuasi wa kweli. Fafanuzi za mifano kutoka kwenye hadithi hizi za Biblia zimemruhusu binadamu kuujua moyo wa Mungu, kujua ni nini Yeye Alichokuwa akifikiria katika kila hatua ya kazi Yake na kwa nini Aliifanya kazi hii, nia Yake ya asili ilikuwa nini na mpango Wake ulikuwa upi Alipofanya kazi ile, namna ambavyo Alifikia fikira Zake na namna Alivyojitayarisha na kuendeleza mpango Wake. Kupitia katika hadithi hizi, tunaweza kupata ufahamu mahususi wenye maelezo ya kina, ya kila nia mahususi ya Mungu na kila wazo halisi wakati wa kazi Yake ya usimamizi ya miaka elfu sita, na mtazamo Wake kwa binadamu katika nyakati tofauti na enzi tofauti. Kuelewa kile ambacho Mungu alikuwa Anafikiria, mtazamo Wake ulikuwa upi na tabia Aliyoifichua alipokuwa Akikumbana na kila hali, kunaweza kumsaidia kila mtu kwa kina zaidi kuweza kutambua kuwepo Kwake kwa hakika, na kuhisi kwa kina zaidi ukweli na uhalisi Wake. Lengo Langu katika kusimulia hadithi hizi si kwamba watu waweze kuelewa historia ya kibiblia, wala si kuwasaidia kupata uzoefu wa vitabu vya Biblia au watu walio ndani yake, na hasa si kuwasaidia watu kuelewa maelezo zaidi kuhusu kile ambacho Mungu alifanya katika Enzi ya Sheria. Ni kuwasaidia watu kuelewa mapenzi ya Mungu, tabia Yake, na kila sehemu ndogo Yake, na kuongeza ufahamu na maarifa ya Mungu yenye uhalisi zaidi na usahihi zaidi. Kwa njia hii, mioyo ya watu inaweza, hatua kwa hatua, kufunguka kwa ajili ya Mungu na kuwa karibu zaidi na Mungu, na wanaweza kumwelewa Yeye zaidi, tabia Yake, kiini Chake, na kumjua vema zaidi Mungu wa kweli Mwenyewe.

Ufahamu wa tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho vinaweza kuwa na athari nzuri kwa binadamu. Vinaweza kuwasaidia kuwa na imani zaidi kwa Mungu, na kuwasaidia kufanikisha utiifu wa kweli na uchaji Kwake. Basi, wao tena si wafuasi wasioona, au wanaomwabudu tu bila mpango. Mungu hataki wajinga au wale wanaofuata umati bila mpango, lakini Anataka kundi la watu ambao wana ufahamu na maarifa wazi katika mioyo yao kuhusu tabia ya Mungu na wanaweza kuchukua nafasi ya mashahidi wa Mungu, watu ambao hawawezi kamwe kumwacha Mungu kwa sababu ya uzuri Wake, kwa sababu ya kile Alicho nacho na kile Alicho, na kwa sababu ya tabia Yake ya haki. Kama mfuasi wa Mungu, endapo katika moyo wako bado kuna ukosefu wa ubayana, au kuna hali tata au mkanganyo kuhusu kuwepo kwa kweli kwa Mungu, tabia Yake, kile Alicho nacho na kile Alicho, na mpango Wake wa kumwokoa binadamu, basi imani yako haiwezi kupata sifa za Mungu. Mungu hataki mtu wa aina hii kumfuata Yeye, na pia Hapendi mtu wa aina hii akija mbele Yake. Kwa sababu mtu wa aina hii hamwelewi Mungu, hawezi kutoa moyo wake kwa Mungu—moyo wake umemfungwa Kwake, hivyo basi imani yake katika Mungu imejaa kasoro mbalimbali. Kumfuata kwake Mungu kunaweza tu kusemwa kuwa ni kwa kipumbavu. Watu wanaweza tu kupata imani ya kweli na kuwa wafuasi wa kweli kama watakuwa na ufahamu na maarifa ya kweli wa Mungu, jambo ambalo linaleta utiifu na uchaji wa kweli Kwake. Ni kwa njia hii tu ndiyo anaweza kuutoa moyo wake kwa Mungu, kuufungua Kwake. Hili ndilo Mungu anataka, kwa sababu kila kitu wanachofanya na kufikiria, kinaweza kustahimili majaribu ya Mungu, na kinaweza kumshuhudia Mungu. Kila kitu Ninachowasiliana nanyi kuhusiana na tabia ya Mungu, au kuhusu kile Alicho nacho na kile Alicho, au mapenzi Yake na fikira Zake katika kila kitu Anachofanya, na kutoka kwenye mtazamo wowote ule, kutoka kwa upande wowote ule Nakizungumzia, yote haya ni kukusaidia kuwa na uhakika zaidi kuhusu uwepo wa kweli wa Mungu, na kuelewa na kushukuru zaidi kwa kweli upendo Wake kwa mwanadamu, na kuelewa na kufahamu vyema zaidi kwa kweli kile anachojali Mungu kuhusu binadamu, na tamanio Lake la dhati la kumsimamia na kumwokoa mwanadamu.

Uchambuzi wa Fikira, Mawazo na Matendo ya Mungu Tangu Auumbe Ulimwengu

Leo kwanza kabisa tutafanya muhtasari wa fikira, mawazo, na kila hatua ya Mungu tangu Alipomuumba binadamu, na kuangalia ni kazi gani Alitekeleza kuanzia uumbaji wa ulimwengu hadi mwanzo rasmi wa Enzi ya Neema. Tunaweza kisha kugundua ni fikira na mawazo yapi ya Mungu ambayo hayajulikani kwa binadamu, na kuanzia hapo tunaweza kuweka wazi mpangilio wa mpango wa usimamizi wa Mungu na kuelewa kwa kina muktadha ambao kwao Mungu alianzisha kazi Yake ya usimamizi, chanzo chake na mchakato wake wa maendeleo, na pia kuelewa kwa undani ni matokeo yapi Anayotaka kutoka katika kazi Yake ya usimamizi—yaani, kiini na kusudio la kazi Yake ya usimamizi. Kuelewa mambo haya tunahitaji kurudi hadi ule wakati wa kitambo, mtulivu na kimya ambapo hakukuwa na binadamu …

Mungu Amuumba Binadamu Aishiye Yeye Mwenyewe

Wakati Mungu aliinuka kutoka kitandani Mwake, fikira ya kwanza Aliyokuwa nayo ilikuwa hii: kumuumba binadamu hai, halisi, binadamu anayeishi—mtu wa kuishi naye na kuwa mwenzake wa kila mara. Mtu huyu angemsikiliza, na Mungu angempa siri Zake na kuongea na yeye. Kisha, kwa mara ya kwanza, Mungu aliuchukua udongo kwenye mkono na kuutumia kumuumba mtu wa kwanza kabisa aliye hai ambaye Alikuwa amemfikiria, na kisha Akakipa kiumbe hiki hai jina—Adamu. Punde Mungu alipompata mtu huyu aliye hai na anayepumua, Alihisi vipi? Kwa mara ya kwanza, Alihisi furaha ya kuwa na mpendwa, na mwandani. Aliweza kuhisi pia kwa mara ya kwanza uwajibikaji wa kuwa baba pamoja na kujali kunakoandamana na hisia hizo. Mtu huyu aliye hai na anayepumua alimletea Mungu furaha na shangwe; Alihisi aliyefarijika kwa mara ya kwanza. Hili lilikuwa jambo la kwanza ambalo Mungu aliwahi kufanya ambalo halikukamilishwa kwa fikira Zake au hata matamshi Yake, lakini lilifanywa kwa mikono Yake miwili. Wakati kiumbe aina hii—mtu aliye hai na anayepumua—aliposimama mbele ya Mungu, aliyeumbwa kwa nyama na damu, aliye na mwili na umbo, na aliyeweza kuongea na Mungu, Alihisi aina ya shangwe ambayo Hakuwa amewahi kuhisi kabla. Kwa kweli alihisi kwamba uwajibikaji Wake na kiumbe huyu hai haukuwa na uhusiano tu katika moyo Wake, lakini kila jambo dogo alilofanya pia lilimgusa na likaupa moyo Wake furaha. Kwa hivyo wakati kiumbe huyu hai aliposimama mbele ya Mungu, ilikuwa ndiyo mara ya kwanza kuwahi kufikiria kuwapata watu wengi zaidi kama hawa. Huu ndio uliokuwa msururu wa matukio ulioanza kwa fikira hii ya kwanza ambayo Mungu alikuwa nayo. Kwa Mungu, matukio haya yote yalikuwa yakifanyika kwa mara ya kwanza, lakini katika matukio haya ya kwanza, haijalishi vile Alivyohisi wakati huo—furaha, uwajibikaji, kujali—hakukuwa na yeyote yule wa kushiriki furaha hii na Yeye. Kuanzia wakati huo, Mungu alihisi kwa kweli upweke na huzuni ambayo Hakuwahi kuwa nao mbeleni. Alihisi kwamba binadamu wasingekubali au kuelewa mapenzi Yake na kujali Kwake, au nia Zake kwa mwanadamu, hivyo basi Alihisi huzuni na maumivu katika moyo Wake. Ingawa Alikuwa amefanya mambo haya kwa binadamu, binadamu hakuwa na habari na hakuelewa. Mbali na furaha, shangwe na hali njema ambayo binadamu alimletea pia viliandamana kwa haraka na hisia Zake za kwanza za huzuni na upweke. Hizi ndizo zilizokuwa fikira na hisia za Mungu wakati huo. Mungu alipokuwa akifanya mambo haya yote, moyoni Mwake Alitoka katika furaha Akaingia katika huzuni na kutoka katika huzuni Akaingia katika maumivu, vyote vikiwa vimechanganyika na wasiwasi. Kile Alichotaka kufanya tu kilikuwa kuharakisha kumruhusu mtu huyu, kizazi hiki cha binadamu kujua ni nini kilichokuwa moyoni Mwake na kuelewa nia Zake haraka iwezekanavyo. Kisha, wangekuwa wafuasi Wake na kupatana na Yeye. Wasingemsikiliza tena Mungu akiongea na kubakia kimya; wasingeendelea kutojua namna ya kujiunga na Mungu katika kazi Yake, na zaidi ya yote, wasingekuwa tena watu wasiojali na kuelewa mahitaji ya Mungu. Mambo haya ya kwanza ambayo Mungu alikamilisha ni yenye maana sana na yanashikilia thamani nyingi kwa minajili ya mpango Wake wa usimamizi na ule wa binadamu leo.

Baada ya kuviumba viumbe vyote na binadamu, Mungu hakupumzika. Asingesubiri kuutekeleza usimamizi Wake wala Asingeweza kusubiri kuwapata watu Aliowapenda mno miongoni mwa wanadamu.

Mungu Afanya Msururu wa Kazi Zisizo na Kifani Katika Wakati wa Enzi ya Sheria

Kisha, si kipindi kirefu baada ya Mungu kuwaumba binadamu, tunaona kutoka katika Biblia ya kwamba kulikuwa na gharika kubwa kote ulimwenguni. Nuhu anatajwa kwenye rekodi ya gharika, na inaweza kusemekana kwamba Nuhu ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kupokea mwito wa Mungu ili afanye kazi na Yeye ili kukamilisha kazi ya Mungu. Bila shaka, wakati huo ndio uliokuwa pia wa kwanza kwa Mungu kumwita mtu ulimwenguni kufanya kitu kulingana na amri Yake. Mara tu Nuhu alipokamilisha kuijenga safina, Mungu alileta gharika katika nchi kwa mara ya kwanza. Mungu alipoiharibu nchi kwa gharika, ndiyo ilikuwa mara ya kwanza tangu kuviumba viumbe ambapo Alihisi kuzidiwa na maudhi kwa binadamu; hili ndilo lililomlazimu Mungu kufanya uamuzi wa uchungu wa kuharibu kizazi hiki cha binadamu kupitia kwa gharika. Baada ya gharika kuiharibu dunia, Mungu alifanya agano Lake la kwanza na binadamu kwamba Hatawahi kufanya hivi tena. Ishara ya agano hili ilikuwa upinde wa mvua. Hili ndilo lililokuwa agano la kwanza la Mungu na binadamu, hivyo basi upinde wa mvua ndio uliokuwa ishara ya kwanza ya agano lililotolewa na Mungu; upinde huu wa mvua ni jambo halisi lililopo. Ni kule kuwepo kabisa kwa upinde huu wa mvua ambako humfanya Mungu mara nyingi ahisi huzuni kutokana na kizazi cha binadamu cha awali ambacho Amepoteza, na huwa ni kumbusho la kila mara Kwake kuhusiana na kile kilichowafanyikia…. Mungu asingepunguza mwendo Wake—Asingesubiri kuchukua hatua ya kufuata katika usimamizi Wake. Hivyo basi, Mungu alimchagua Ibrahimu kama chaguo Lake la kwanza kwa kazi Yake kotekote Israeli. Hii ndiyo iliyokuwa pia mara ya kwanza kwa Mungu kumchagua mteuliwa kama huyo. Mungu aliamua kuanza kutekeleza kazi Yake ya kumwokoa binadamu kupitia kwa mtu huyu, na kuendeleza kazi Yake miongoni mwa vizazi vya mtu huyu. Tunaweza kuona katika Biblia kwamba hivi ndivyo Mungu alivyomfanyia Ibrahimu. Basi Mungu akaifanya Israeli kuwa nchi ya kwanza iliyochaguliwa, na Akaianza kazi Yake ya Enzi ya Sheria kupitia kwa watu Wake waliochaguliwa, Waisraeli. Tena kwa mara ya kwanza, Mungu aliwapa Waisraeli sheria na kanuni za moja kwa moja ambazo mwanadamu anafaa kufuata, na Akazieleza kwa kina. Hii ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Mungu kumpatia binadamu sheria kama hizo mahususi na wastani kuhusu namna wanavyofaa kutoa kafara, namna wanavyofaa kuishi, kile wanachofaa kufanya na kutofanya, ni sherehe na siku gani wanazofaa kutilia maanani, na kanuni za kufuata katika kila kitu walichofanya. Hii ndiyo iliyokuwa mara ya kwanza kwa Mungu kumpa binadamu taratibu na kanuni hizo zenye maelezo na uwastani kwa ajili ya maisha yao.

Ninaposema “mara ya kwanza,” inamaanisha Mungu hakuwa Amewahi kukamilisha kazi kama hiyo tena. Ni kitu ambacho hakikuwepo awali, na hata ingawa Mungu alikuwa Amemuumba binadamu na Alikuwa ameumba aina zote za viumbe na vitu vyenye uhai, Hakuwa amewahi kukamilisha kazi ya aina hiyo. Usimamizi wa Mungu kwa binadamu; yote ilihusu binadamu na wokovu Wake na usimamizi wa binadamu. Baada ya Ibrahimu, Mungu alifanya chaguo tena kwa mara ya kwanza—Alimchagua Ayubu kuwa ndiye chini ya sheria ndiye ambaye angestahimili majaribio ya Shetani huku akiendelea kumcha Mungu na kujiepusha na uovu na kuweza kumtolea Yeye ushuhuda. Hii pia ndiyo iliyokuwa mara ya kwanza kwa Mungu kuruhusu Shetani kumjaribu mtu na mara ya kwanza Alipoweka dau na Shetani. Mwishowe, kwa mara ya kwanza, Mungu alimpata mtu aliyekuwa na uwezo wa kusimama kama shahidi Wake huku akiwa amemkabili Shetani—mtu ambaye angeweza kumshuhudia Yeye na kumwaibisha kabisa Shetani. Tangu Mungu alipomuumba mwanadamu, huyu ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza, aliyempata ambaye aliweza kumshuhudia Yeye. Punde alipokuwa amempata mtu huyu, Mungu alikuwa na hata hamu zaidi ya kuendeleza usimamizi Wake na kuchukua hatua inayofuata katika kazi Yake, Akitayarisha chaguo Lake lifuatalo na mahali Pake pa kazi.

Baada ya kushiriki kuhusu haya yote, je, mnao ufahamu wa kweli wa mapenzi ya Mungu? Mungu anazingatia tukio hili la usimamizi Wake wa binadamu, la wokovu Wake wa binadamu, kama muhimu sana kuliko chochote kingine. Huyafanya mambo haya yote si kwa kutumia akili Zake tu, wala si kwa kutumia maneno Yake tu, na vilevile Yeye hafanyi hivi hususan kwa juujuu tu—Yeye huyafanya mambo haya yote kwa mpango, kwa viwango, na kwa mapenzi Yake. Ni wazi kwamba kazi hii ya kumwokoa binadamu imeshikilia umuhimu mkubwa kwa Mungu na hata binadamu. Haijalishi kazi ilivyo ngumu, haijalishi changamoto ni kubwa jinsi gani, haijalishi binadamu ni wanyonge jinsi gani, au binadamu amekuwa mwasi wa kweli, hakuna chochote kati ya haya ambacho ni kigumu kwa Mungu. Mungu hujibidiisha Mwenyewe, Akitumia jitihada Zake za bidii za kazi na kusimamia kazi ambayo Yeye Mwenyewe Anataka kutekeleza. Yeye pia Anapanga kila kitu na kuwatawala watu wote na kazi ambayo Anataka kukamilisha—hakuna chochote kati ya haya ambacho kimefanywa awali. Ndiyo mara ya kwanza Mungu ametumia mbinu hizi na kulipa gharama kubwa kwa minajili ya mradi huu mkubwa wa kusimamia na kumwokoa mwanadamu. Huku Mungu akiwa Anatekeleza kazi hii, hatua kwa hatua Anawaonyesha na kuachilia kwa wanadamu bila kuficha juhudi Zake nyingi, kile Alicho nacho na kile Alicho, hekima na uweza, na kila dhana ya tabia Yake. Anaachilia na kuonyesha haya yote kwa mwanadamu kidogo kidogo, Akifichua na kuonyesha mambo haya kwa namna ambayo Hajawahi kufanya awali. Kwa hivyo, katika ulimwengu mzima, mbali na watu ambao Mungu analenga kuwasimamia na kuwaokoa, hakujawahi kuwepo na viumbe vyovyote vilivyo karibu na Mungu, ambavyo vinao uhusiano wa karibu sana na Yeye. Katika moyo Wake, yule mwanadamu Anayetaka kumsimamia na kumwokoa ndiye muhimu zaidi, na Anamthamini mwanadamu huyu zaidi ya kitu kingine chochote; hata ingawa Amelipia gharama ya juu na ingawa Anaumizwa na kutosikilizwa bila kukoma na wao, Hakati tamaa na Anaendelea bila kuchoka katika kazi Yake bila ya malalamiko au majuto. Hii ni kwa sababu Anajua kwamba hivi karibuni au baadaye, binadamu siku moja wataitikia mwito Wake na kuguswa na maneno Yake, kutambua kwamba Yeye ndiye Bwana wa uumbaji, na kurudi upande Wake …

Baada ya kusikia haya yote leo, mnaweza kuhisi kwamba kila kitu ambacho Mungu anafanya ni kawaida sana. Yaonekana kwamba binadamu siku zote wamehisi mapenzi fulani ya Mungu kwao kutokana na matamshi Yake na pia kazi Yake, lakini siku zote kuna umbali fulani katikati ya hisia zao au maarifa yao na kile ambacho Mungu anafikiria. Kwa hivyo, Nafikiri ni muhimu kuwasiliana na watu wote kuhusu ni kwa nini Mungu alimuumba mwanadamu, na maelezo zaidi yanayoonyesha tamanio Lake la kuwapata watu aliokuwa Akitumainia. Ni muhimu kushiriki habari hii na kila mmoja, ili kila mmoja aweze kuwa wazi moyoni mwake. Kwa sababu kila fikira na wazo la Mungu, na kila awamu na kila kipindi cha kazi Yake vinafungamana ndani ya, na vyote hivi vimeunganishwa kwa karibu na, usimamizi Wake mzima wa kazi, unapoelewa fikira na mawazo ya Mungu, na mapenzi Yake katika kila hatua ya kazi Yake, ni sawa na ufahamu wa chanzo cha kazi ya mpango Wake wa usimamizi. Ni katika msingi huu ndipo ufahamu wako wa Mungu unapoanza kuwa wa kina. Ingawa kila kitu ambacho Mungu alifanya Alipoumba kwanza ulimwengu ambacho Nilitaja awali ni taarifa fulani tu kwa watu sasa na yaonekana kwamba hayana umuhimu sana katika utafutaji wa ukweli, katika mkondo wa kile ambacho utapitia kutakuwa na siku ambapo hutafikiria kuwa ni jambo rahisi sana kama mkusanyiko tu wa taarifa, wala kwamba ni kitu rahisi sana kama mafumbo fulani. Kwa kadri maisha yako yanavyoendelea na pale ambapo pana msimamo kidogo wa Mungu katika moyo wako, au unapokuja kuelewa waziwazi na kwa kina mapenzi Yake, utaweza kuelewa kwa kweli umuhimu na haja ya kile Ninachozungumzia leo. Haijalishi ni kwa kiwango kipi umeyakubali haya; ni muhimu kwamba uelewe na ujue mambo haya. Wakati Mungu anapofanya jambo, wakati Anapotekeleza kazi Yake, haijalishi kama amefanya na mawazo Yake au kwa mikono Yake, haijalishi kama ni mara ya kwanza ambapo Amelifanya au kama ni mara ya mwisho—mwishowe, Mungu anao mpango, na makusudio Yake na fikira Zake vyote vimo katika kila kitu Anachokifanya. Makusudio na fikira hizi vinawakilisha tabia ya Mungu, na vinaonyesha kile Alicho nacho na kile Alicho. Vitu hivi viwili—tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho—lazima vieleweke na kila mmoja. Punde mtu anapoelewa tabia Yake na kile Alicho nacho na kile Alicho, ataanza kuelewa kwa utaratibu ni kwa nini Mungu anafanya kile Anachofanya na kwa nini Anasema kile Anachosema. Kutokana na hayo, anaweza kuwa na imani zaidi ya kumfuata Mungu, kuufuatilia ukweli, na kufuatilia mabadiliko katika tabia. Hivyo ni kusema, ufahamu wa binadamu kuhusu Mungu na imani yake katika Mungu haviwezi kutenganishwa.

Iwapo kile ambacho watu hupata ufahamu kuhusu au kupata kuelewa ni tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho, basi kile wanachofaidi kitakuwa ni maisha yanayotoka kwa Mungu. Baada ya maisha haya kuhemshwa ndani yako, uchaji wako wa Mungu utakuwa mkubwa zaidi na zaidi, na kuvuna mavuno haya kunafanyika kwa kawaida sana. Kama hutaki kuelewa au kujua kuhusu tabia ya Mungu au kiini Chake, kama hutaki hata kutafakari juu ya mambo haya au kuyazingatia, Naweza kukuambia kwa hakika kwamba hiyo njia unayoifuatilia katika imani yako kwa Mungu haitawahi kukuruhusu kuyaridhisha mapenzi Yake au kupata sifa Zake. Zaidi ya hayo, huwezi kamwe kufikia wokovu—hizi ndizo athari za mwisho. Wakati watu hawamwelewi Mungu na hawajui tabia Yake, mioyo yao haiwezi kamwe kuwa wazi Kwake. Punde wanapomwelewa Mungu, wataanza kuthamini na kufurahia kile kilicho moyoni Mwake kwa kivutio na imani. Unapothamini na kufurahia kile kilichomo ndani ya moyo wa Mungu, moyo wako utaanza kwa utaratibu, kidogokidogo, kuwa wazi Kwake. Wakati moyo wako unakuwa wazi Kwake, utahisi namna ambavyo mabadilishano yako na Mungu yatakavyokuwa ya aibu na duni, madai yako kutoka kwa Mungu na matamanio yako mengi binafsi. Moyo wako unapofunguka kwa kweli kwa Mungu, utaona kwamba moyo Wake ni ulimwengu usio na mwisho, na utaingia katika ulimwengu ambao hujawahi kuupitia awali. Katika ulimwengu huu hakuna kudanganya, hakuna udanganyifu, hakuna giza, hakuna maovu. Kunao ukweli wa dhati na uaminifu; kunayo nuru na uadilifu tu; kunayo haki na huruma. Umejaa upendo na utunzaji, umejaa rehema na uvumilivu, na kupitia katika ulimwengu huu utahisi shangwe na furaha ya kuwa hai. Mambo haya ndiyo ambayo Atakufichulia utakapoufungua moyo wako kwa Mungu. Hii dunia isiyo na kikomo imejaa hekima ya Mungu, na imejaa kudura Yake; umejaa pia upendo Wake na mamlaka Yake. Hapa unaweza kuona kila kipengele cha kile Mungu Alicho nacho na kile Alicho, ni nini kinachomletea Yeye shangwe, kwa nini Anakuwa na wasiwasi na kwa nini Anakuwa na huzuni, kwa nini Anakuwa na hasira…. Haya ndiyo ambayo kila mmoja anayeufungua moyo wake na kumruhusu Mungu kuingia ndani anaweza kuona. Mungu anaweza tu kuingia katika moyo wako kama utaufungua kwa ajili Yake. Unaweza kuona tu kile Mungu Alicho nacho na kile Alicho, na unaweza kuona tu mapenzi Yake kwako, kama Ameingia katika moyo wako. Wakati huo, utagundua kwamba kila kitu kuhusu Mungu ni chenye thamani, kwamba kile Alicho nacho na kile Alicho kina thamani sana ya kuthaminiwa. Ukilinganisha na hayo, watu wanaokuzunguka, vifaa na matukio katika maisha yako, hata wapendwa wako, mwandani wako, na mambo unayopenda, si muhimu sana. Ni madogo mno, na ni ya kiwango cha chini; utahisi kwamba hakuna chombo chochote cha anasa ambacho kitaweza kukuvutia tena, na au kwamba kitu chochote yakinifu kitawahi kukushawishi tena ukilipie gharama yoyote tena. Kwa unyenyekevu wa Mungu utaona ukubwa Wake na mamlaka Yake ya juu; aidha, katika jambo Alilofanya uliloliamini kuwa dogo mno, utaweza kuiona hekima Yake na uvumilivu Wake usio na mwisho, na utaiona subira Yake, uvumilivu Wake na ufahamu Wake kwako. Hili litazaa ndani yako upendo Kwake. Siku hiyo, utahisi kwamba mwanadamu anaishi katika ulimwengu mchafu, kwamba watu walio upande wako na mambo yanayokufanyikia katika maisha yako, na hata kwa wale unaopenda, upendo wao kwako, na ulinzi wao kama ulivyojulikana au kujali kwao kwako havistahili hata kutajwa—Mungu tu ndiye mpendwa wako na ni Mungu tu unayethamini zaidi. Wakati siku hiyo itawadia, Naamini kwamba kutakuwa na baadhi ya watu watakaosema: Upendo wa Mungu ni mkubwa na kiini Chake ni kitakatifu mno—ndani ya Mungu hakuna udanganyifu, hakuna uovu, hakuna wivu, na hakuna mabishano, lakini ni haki tu na uhalisi, na kila kitu Alicho nacho Mungu na kile Alicho vyote vinafaa kutamaniwa na binadamu. Binadamu wanafaa kujitahidi na kuwa na hamu ya kuvipata. Ni kwa msingi gani ndipo uwezo wa mwanadamu wa kutimiza haya umejengwa? Unajengwa kwa msingi wa ufahamu wa binadamu wa tabia ya Mungu, na ufahamu wao kuhusu kiini cha Mungu. Hivyo basi kuelewa tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho, ni funzo la maisha yote kwa kila mtu na ni lengo la maisha yote linalofuatiliwa na kila mtu anayelenga kubadilisha tabia yake, na kutamani kumjua Mungu.

Mara ya Kwanza ya Mungu Kuwa Mwili Ili Afanye Kazi

Tumezungumza tu kuhusu kazi yote ambayo Mungu amekamilisha, misururu ya mambo Aliyoyafanya kwa mara ya kwanza. Kila mojawapo ya mambo haya yanahusiana na mpango wa Mungu wa usimamizi na mapenzi ya Mungu. Yanahusiana pia na tabia binafsi ya Mungu na kiini Chake. Kama tunataka kuelewa zaidi ya kile Alicho nacho Mungu na kile Alicho, sisi hatuwezi kukoma katika Agano la Kale au katika Enzi ya Sheria, lakini tunahitaji kusonga mbele pamoja na hatua ambazo Mungu alichukua katika kazi Yake. Hivyo basi, Mungu alipotamatisha Enzi ya Sheria na kuanza Enzi ya Neema, hatua zetu binafsi zimefika katika Enzi ya Neema—enzi iliyojaa neema na ukombozi. Katika enzi hii, Mungu tena Alifanya kitu cha muhimu sana kwa mara ya kwanza. Kazi katika enzi hii mpya kwa Mungu na hata kwa mwanadamu ilikuwa sehemu mpya ya kuanzia. Sehemu hii mpya ya kuanzia ilikuwa tena kazi mpya ambayo Mungu alifanya kwa mara ya kwanza. Kazi hii mpya ilikuwa kitu ambacho hakikuwahi kutokea awali ambacho Mungu alitekeleza na hakikufikirika na binadamu na viumbe vyote. Ni kitu ambacho kwa sasa kinajulikana kwa watu wote—hii ndiyo iliyokuwa mara ya kwanza Mungu aligeuka kuwa binadamu, mara ya kwanza Alianza kazi mpya kwa umbo la binadamu, Akiwa na utambulisho wa mwanamume. Kazi hii mpya ilionyesha kwamba Mungu alikuwa Amekamilisha kazi Yake katika Enzi ya Sheria, kwamba Asingefanya au kusema tena chochote chini ya sheria. Wala Asingewahi tena kuzungumza au kufanya chochote kwa mfano wa sheria au kulingana na kanuni au masharti ya sheria. Yaani, kazi Yake yote inayotokana na sheria ilisitishwa milele na isingeendelezwa, kwa sababu Mungu alitaka kuanza kazi mpya na kufanya mambo mapya, na mpango Wake kwa mara nyingine tena ulikuwa na sehemu mpya ya kuanzia. Hivyo basi, Mungu lazima Angemwongoza binadamu hadi katika enzi inayofuata.

Kama hii ilikuwa habari ya shangwe au ya kisirani kwa binadamu ilitegemea kiini chao kilikuwa kipi. Inaweza kusemekana kwamba hizi hazikuwa habari za shangwe, lakini zilikuwa habari za kisirani kwa baadhi ya watu, kwa sababu Mungu alipoanza kazi Yake mpya, watu hao ambao walifuata tu sheria na masharti, ambao walifuata tu kanuni lakini hawakumcha Mungu wangeegemea upande wa kutumia kazi nzee ya Mungu ili kuishutumu kazi Yake mpya. Kwa watu hawa, hizi zilikuwa habari za kisirani; lakini kwa kila mtu aliyekuwa hana hatia na aliyekuwa wazi, aliyekuwa mwenye ukweli kwa Mungu na aliyekuwa radhi kupokea ukombozi Wake, Mungu kuwa mwili kwa mara ya kwanza zilikuwa habari zenye shangwe sana. Kwani tangu kuwepo na binadamu, hii ndiyo iliyokuwa mara ya kwanza Mungu kuonekana na kuishi miongoni mwa wanadamu katika umbo ambalo halikuwa Roho; badala yake, Alizaliwa na mwanadamu na kuishi miongoni mwa watu kama Mwana wa Adamu, na kufanya kazi katikati yao. Hii “mara ya kwanza” ilizivunja dhana za watu na pia ilikuwa zaidi ya kufikiria kote. Aidha, wafuasi wote wa Mungu walipata manufaa ya kushikika na kuonekana. Mungu hakuikomesha tu enzi nzee, lakini pia Alikomesha mbinu Zake za kale za kufanya kazi pamoja na mitindo ya kufanya kazi. Hakuruhusu tena wajumbe Wake kuwasilisha mapenzi Yake, na hakufichika tena katika mawingu na hakuonekana tena au kuongea kwa binadamu kupitia kwa ishara za amri kwa radi. Tofauti na chochote kile cha awali, kupitia kwa mbinu ambayo haikufirika kwa binadamu ambayo pia ilikuwa ngumu kwa wao kuelewa na kukubali—kupata mwili—Aligeuka na kuwa Mwana wa Adamu ili kuendeleza kazi ya enzi hiyo. Kitendo hiki cha Mungu kiliwashtua wanadamu; kiliwafanya wawe na aibu, kwa sababu Mungu kwa mara nyingine alikuwa ameanza kazi mpya ambayo Hakuwahi kufanya tena. Leo, tutaangalia ni kazi gani mpya ambayo Mungu alikamilisha katika enzi mpya, na katika haya yote ya kazi mpya, tabia ya Mungu nayo ilikuwa vipi, na nini Alicho nacho na kile Alicho ambayo tunaweza kuelewa?

Yafuatayo ni maneno yaliyorekodiwa katika Agano Jipya la Biblia:

1. Yesu Avunja Masuke ya Mahindi na Kula Siku ya Sabato

Mat 12:1 Wakati huo katika siku ya Sabato Yesu alipitia mashamba ya nafaka; na wanafunzi wake walihisi njaa, nao wakaanza kung’oa masuke ya nafaka na kuyala.

2. Mwana wa Adamu Ndiye Bwana wa Sabato

Mat 12:6-8 Lakini nasema kwenu, Kwamba mahali humu yumo aliye mkubwa kuliliko hekalu. Lakini iwapo mngejua maana ya hili, Naitaka rehema, na siyo sadaka, msingewashutumu wale wasio na hatia. Kwa sababu Mwana wa Adamu ni Bwana hata wa siku ya Sabato.

Hebu kwanza tuangalie dondoo hii: “Wakati huo katika siku ya Sabato Yesu alipitia mashamba ya nafaka; na wanafunzi wake walihisi njaa, nao wakaanza kung’oa masuke ya nafaka na kuyala.”

Kwa nini Nimeichagua dondoo hii? Dondoo hii ina uhusiano upi na tabia ya Mungu? Katika maandiko haya kitu cha kwanza tunachojua ni kwamba ilikuwa ni siku ya Sabato, lakini Bwana Yesu alipita kule nje na kuwaongoza wanafunzi Wake katika mashamba ya nafaka. Lakini kilicho “telezi zaidi” ni kwamba waliweza hata “wakaanza kung’oa masuke ya nafaka na kuyala.” Katika Enzi ya Sheria, sheria za Yehova Mungu ilisema kwamba watu wasingeweza kuenda vivi hivi tu au kushiriki katika shughuli katika siku ya Sabato—kulikuwa na mambo mengi ambayo hayangefanywa siku ya Sabato. Hatua hii ya Bwana Yesu ilikuwa ya kuchanganya hasa kwa wale waliokuwa wameishi chini ya sheria kwa muda mrefu, na iliweza hata kuchochea upinzani mkubwa. Kuhusiana na mchanganyiko wao na namna walivyouzungumzia kile ambacho Yesu alifanya, tutaweka hilo pembeni kwa sasa na kuzungumzia kwanza kwa nini Bwana Yesu alichagua kufanya hivi katika siku ya Sabato, kwa siku zote, na kile Alichotaka kuwasilisha kwa watu waliokuwa wakiishi katika enzi ya kale kupitia katika hatua hii. Huu ndio uhusiano kati ya dondoo hii na tabia ya Mungu ambayo Ningependa kuzungumzia.

Bwana Yesu alipokuja, Alitumia vitendo Vyake vya utendaji kuwambia watu: kwamba Mungu alikuwa ameiondoa Enzi ya Sheria na alikuwa ameanza kazi mpya, na kwmba kazi hii mpya haikuhitaji utilifu maanani wa Sabato. Wakati Mungu kutoka katika mipaka ya siku ya Sabato, hicho kilikuwa tu kionjo cha mapema cha kazi Yake mpya. Bwana Yesu alipoanza kazi Yake, tayari Alikuwa ameacha nyuma zile pingu za Enzi ya Sheria, na alikuwa ametupilia mbali zile taratibu na kanuni zilizokuwa za enzi hiyo. Ndani yake hakuwa na dalili za chochote kuhusiana na sheria; Alikuwa ameitupa nje mzima mzima na hakuifuata tena, na Hakuhitaji tena mwanadamu kuifuata. Kwa hivyo hapa unaona kwamba Bwana Yesu alipita katika mashamba siku ya Sabato; Bwana hakupumzika lakini, alikuwa akipita kule nje akifanya kazi. Hatua hii Yake ilikuwa ya kushtua kwa dhana za watu na iliweza kuwawasilishia ujumbe kwamba Hakuishi tena chini ya sheria na kwamba Alikuwa ameacha ile mipaka ya Sabato na kujitokeza mbele ya mwanadamu na katikati yao katika taswira mpya, huku akiwa na njia mpya ya kufanya kazi. Hatua hii Yake iliwaambia watu kwamba Alikuwa ameleta pamoja naye kazi mpya iliyoanza kwa kwenda nje ya sheria na kwenda nje ya Sabato. Wakati Mungu alitekeleza kazi Yake mpya, Hakushikilia tena ya kale, na Hakujali tena kuhusu taratibu za Enzi ya Sheria. Wala Hakuathirika na kazi Yake mwenyewe katika enzi ya awali, lakini Alifanya kazi kwa kawaida katika siku ya Sabato na wakati wanafunzi Wake waliona njaa, waliweza kuvunja masuke na wakala. Haya yote yalikuwa kawaida sana machoni mwa Mungu. Mungu angeweza kuwa na mwanzo mpya kwa nyingi za kazi Anazotaka kufanya na mambo Anayotaka kusema. Punde Anapokuwa na mwanzo mpya, Hataji kazi Yake ya awali tena wala kuiendeleza. Kwani Mungu anazo kanuni Zake katika kazi Yake. Anapotaka kuanzisha kazi mpya, ndipo Anapotaka kumleta mwanadamu katika awamu mpya ya kazi Yake, na wakati kazi Yake imeingia katika awamu ya juu zaidi. Kama watu wanaendelea kutenda kulingana na misemo au taratibu za kale au kuendelea kushikilia kabisa kwazo, Hatakumbuka au kulisifu jambo hili. Hii ni kwa sababu tayari Ameileta kazi mpya, na ameingia katika awamu mpya ya kazi Yake. Anapoanzisha kazi mpya, Anaonekana kwa mwanadamu akiwa na taswira mpya kabisa, kutoka katika mtazamo mpya kabisa, na kwa njia mpya kabisa ili watu waweze kuona dhana zile tofauti za tabia Yake na kile Alicho nacho na kile Alicho. Hii ni mojawapo ya malengo Yake katika kazi Yake mpya. Mungu hashikilii ya kale au kutumia njia isiyotumika na wengi; Anapofanya kazi na kuongea sio njia ya kutilia mipaka kama vile watu wanavyofikiria. Ndani ya Mungu, vyote ni huru na vimekombolewa, na hakuna hali ya kukinga, hakuna vizuizi—kile Anachomletea mwanadamu vyote ni uhuru na ukombozi. Yeye ni Mungu aliye hai, Mungu ambaye kwa kweli, na kwa hakika yupo. Yeye si kikaragosi au sanamu ya udongo, na Yeye ni tofauti kabisa na sanamu ambazo watu huhifadhi na kuabudu. Yeye yuko hai na mwenye nguvu na kile ambacho maneno Yake na kazi Yake humletea binadamu vyote ni uzima na nuru, uhuru na ukombozi wote, kwa sababu Yeye anashikilia ukweli, uzima, na njia—Yeye hajazuiliwa na chochote katika kazi yoyote Yake. Bila kujali watu wanavyosema na namna wanavyoona au kukadiria kazi Yake mpya, Ataitekeleza kazi Yake bila hofu. Hatakuwa na wasiwasi kuhusu dhana zozote za yeyote au kazi na maneno Yake kuelekezewa vidole, au hata upinzani wao mkubwa katika kazi Yake mpya. Hakuna yeyote miongoni mwa viumbe vyote anayeweza kutumia akili ya binadamu, au kufikiria kwa binadamu, maarifa au maadili ya binadamu kupima au kufasili kile ambacho Mungu anafanya, kutia fedheha, au kutatiza au kukwamiza kazi Yake. Hakuna kizuizi chochote katika kazi Yake na kile Anachokifanya; na haitawekewa kizuizi chochote na binadamu yeyote, tukio, au kitu, wala haitakatizwa na nguvu zozote za kikatili. Kwa mjibu wa kazi Yake mpya kuhusika, Yeye ni Mfalme anayeshinda daima, na nguvu zozote za kikatili na uzushi wote na hoja za uwongo za mwanadamu zimekanyagiwa chini ya kibao Chake cha kuwekea miguu. Haijalishi ni hatua gani mpya ya kazi Yake ambayo Anatekeleza, ni hakika itaendelezwa na ipanuliwe katika mwanadamu, na hakika itatekelezwa bila kuzuiliwa duniani kote mpaka pale ambapo kazi Yake kubwa imekamilika. Huu ndio uweza na hekima ya Mungu, na mamlaka na nguvu Zake. Hivyo basi, Bwana Yesu angeweza kwenda kule nje waziwazi na kufanya kazi katika siku ya Sabato kwa sababu ndani ya moyo Wake hakukuwa na sheria zozote, na hakukuwa na maarifa au kanuni zozote zilizotokana na binadamu. Kile Alichokuwa nacho kilikuwa ni kazi mpya ya Mungu na njia Yake, na kazi Yake ndio iliyokuwa njia ya kumweka huru mwanadamu, kumwachilia, kumruhusu kuwepo katika nuru na kumruhusu kuishi. Na wale wanaoabudu sanamu au miungu ya uwongo wanaishi kila siku wakiwa wamefungwa na Shetani, wakiwa wamezuiliwa na aina zote za sheria na mila—leo kitu kimoja hakiruhusiwi, kesho kingine—hakuna uhuru katika maisha yao. Wao ni sawa na wafungwa katika pingu wasio na shangwe ya kuzungumzia. “Kuzuiliwa” linawakilisha nini? Linawakilisha shurutisho, utumwa na uovu. Punde tu mtu anapoabudu sanamu, anaabudu mungu wa uwongo, akimwabudu roho wa uovu. Kuzuiliwa kunaenda sambamba na hilo. Huwezi kula hiki au kile, leo huwezi kwenda nje, kesho huwezi kuwasha jiko lako, siku inayofuata huwezi kuhamia katika nyumba mpya, siku fulani lazima zichaguliwe kwa minajili ya harusi na mazishi, na hata za wakati wa kujifungua mtoto. Haya yote yanaitwa nini? Haya yanaitwa kuzuiliwa; ni utumwa wa mwanadamu, na ndizo pingu za maisha za Shetani na roho wa maovu wanaowadhibiti, na wanaozuilia mioyo yao na mili yao. Je, kuzuiliwa huku kunapatikana kwa Mungu? Tunapozungumzia utakatifu wa Mungu, unafaa kwanza kufikiria haya: Kwa Mungu hakuna vizuizi. Mungu anazo kanuni katika maneno na kazi Yake, lakini hakuna kuzuiliwa, kwa sababu Mungu Mwenyewe ndiye ukweli, njia na uzima.

Sasa hebu tuangalie dondoo ifuatayo: “Lakini nasema kwenu, Kwamba mahali humu yumo aliye mkubwa kuliliko hekalu. Lakini iwapo mngejua maana ya hili, Naitaka rehema, na siyo sadaka, msingewashutumu wale wasio na hatia. Kwa sababu Mwana wa Adamu ni Bwana hata wa siku ya sabato” (Mat 12:6-8). “Hekalu” hapa linamaanisha nini? Kwa ufupi, “hekalu” linaashiria jengo refu la kupendeza, na katika Enzi ya Sheria, hekalu lilikuwa ni pahali pa makuhani kumwabudu Mungu. Bwana Yesu aliposema “mahali humu yumo aliye mkubwa kuliliko hekalu,” “mmoja” ilikuwa ikirejelea nani? Ni wazi, “mmoja” ni Bwana Yesu katika mwili kwa sababu Yeye tu ndiye aliyekuwa mkuu kuliko hekalu. Na maneno hayo yaliwaambia watu nini? Yaliwaambia watu watoke hekaluni—Mungu alikuwa tayari ameshatoka nje na hakuwa tena akifanyia kazi ndani yake, hivyo basi watu wanafaa kutafuta nyayo za Mungu nje ya hekalu na kufuata nyayo Zake katika kazi Yake mpya. Usuli wa Bwana Yesu kusema haya ilikuwa kwamba chini ya sheria, watu walikuwa wameiona hekalu kama kitu kilichokuwa kikuu zaidi kuliko Mungu Mwenyewe. Yaani, watu waliliabudu hekalu badala ya kumwabudu Mungu, hivyo basi Bwana Yesu akawaonya kutoabudu sanamu, lakini kumwabudu Mungu kwa sababu Yeye ndiye mwenye mamlaka ya juu zaidi. Hivyo basi, alisema: “Naitaka rehema, na siyo sadaka.” Ni wazi kwamba katika macho ya Bwana Yesu, watu wengi sana katika sheria hawakumwabudu tena Yehova, lakini walikuwa tu wakipitia mchakato wa kutoa sadaka na Bwana Yesu aliamua kwamba mchakato huu ulikuwa ibada ya sanamu. Waabudu sanamu hawa waliliona hekalu kama kitu kikuu, cha juu zaidi kuliko Mungu. Ndani ya mioyo yao kulikuwa tu na hekalu, wala si Mungu, na kama wangelipoteza hekalu, wangepoteza mahali pao pa kukaa. Bila ya hekalu hawakuwa na mahali popote pa kuabudu na wasingeweza kutoa sadaka zao. Mahali pao pa kukaa kama palivyojulikana ndipo walipofanyia shughuli zao kwa jina la kumwabudu Yehova Mungu, na hivyo basi wakaruhusiwa kuishi katika hekalu na kutekeleza shughuli zao binafsi. Ule utoaji sadaka wao kama ulivyojulikana ulikuwa tu kutekeleza shughuli zao za kibinafsi za aibu wakisingizia kwamba walikuwa wanaendesha ibada yao katika hekalu. Hii ndiyo iliyokuwa sababu iliyowafanya watu wakati huo kuliona hekalu kuwa kuu kuliko Mungu. Kwa sababu walilitumia hekalu kama maficho, na sadaka kama kisingizio cha kuwadanganya watu na kumdanganya Mungu, Bwana Yesu alisema haya ili kuwaonya watu. Mkitumia maneno haya kwa wakati wa sasa, yangali bado halali na yenye umuhimu sawa. Ingawa watu wa leo wameweza kupitia kazi tofauti za Mungu kuliko watu wa Enzi ya Sheria walivyowahi kupitia, kiini cha asili yao ni kile kile. Katika muktadha wa kazi leo, watu bado watafanya aina sawa ya mambo kama yale ya “hekalu kuwa kuu kuliko Mungu”. Kwa mfano, watu huona kutimiza wajibu wao kama kazi yao; wanaona kutoa ushuhuda kwa Mungu na kupigana na joka kubwa jekundu kama harakati ya kisiasa ya kulinda haki za kibinadamu, kwa ajili ya demokrasia na uhuru; wao hugeuza wajibu wao ili kutumia weledi wao kuwa ajira, lakini wanachukulia kumcha Mungu na kujiepusha na maovu tu kama kipande cha kanuni ya kidini ya kufuatwa; na kadhalika. Je, maonyesho haya kwa upande wa binadamu hasa hayako sawa na “hekalu ni kuu kumliko Mungu”? Isipokuwa tu kwamba miaka elfu mbili iliyopita, watu walikuwa wakiendeleza shughuli zao za kibinafsi katika hekalu linaloshikika, lakini leo, watu wanaendeleza shughuli zao za kibinafsi katika mahekalu yasiyogusika. Wale watu wanaothamini masharti huona masharti kuwa kuu zaidi kuliko Mungu, wale watu wanaopenda hadhi huona hadhi kuu zaidi kuliko Mungu, wale watu wanaopenda ajira zao huziona ajira hizo kuwa kuu zaidi kuliko Mungu na kadhalika—maonyesho yao yote yananifanya Mimi kusema: “Watu humsifu Mungu kuwa ndiye mkuu zaidi kupitia kwa maneno yao, lakini kwa macho yao kila kitu ni kikuu zaidi kuliko Mungu.” Hii ni kwa sababu punde tu watu wanapopata fursa katika njia yao ya kumfuata Mungu ili kuonyesha vipaji vyao, au kuendelea na shughuli zao binafsi za kibiashara au ajira yao binafsi, wanakuwa mbali na Mungu na kufanya kwa bidii ajira wanayoipenda. Kuhusiana na kile ambacho Mungu amewaaminia, na mapenzi Yake, mambo hayo yote yametupiliwa mbali kitambo. Katika hali hii, ni nini tofauti baina ya watu hawa na wale wanaoendesha biashara zao katika hekalu miaka elfu mbili iliyopita?

Kisha, hebu tuangalie sentensi ya mwisho katika dondoo hii ya maandiko: “Kwa sababu Mwana wa Adamu ni Bwana hata wa siku ya Sabato.” Je, kunao upande wa utendaji kwa sentensi hii? Je, unaweza kuona upande wa utendaji kwa sentensi hii? Kila kitu anachosema Mungu kinatoka moyoni Mwake, kwa hivyo kwa nini Alisema hivi? Unaielewa vipi sentensi hii? Unaweza kuelewa maana ya sentensi hii sasa, lakini wakati huo si watu wengi walikuwa wanaielewa kwa sababu binadamu alikuwa tu ametoka katika Enzi ya Sheria. Kwao, kutoka katika Sabato lilikuwa jambo gumu sana kufanya, sembuse kuelewa Sabato ya kweli ilikuwa nini.

Sentensi “Mwana wa Adamu ni Bwana hata wa siku ya Sabato.” inawaambia watu kwamba kila kitu cha Mungu ni visivyo vya mwili, na ingawa Mungu anaweza kukupa mahitaji yako yote ya kimwili, punde tu mahitaji yako yote ya mwili yametimizwa, utoshelevu unaotokana na mambo haya unaweza kuchukua nafasi ya ufuatiliaji wako wa ukweli? Kwa kweli hiyo haiwezekani! Tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho ambayo tumeweza kushiriki pamoja ni kweli. Haiwezi kupimwa kupitia kwa gharama ya juu ya vifaa vya kimwili wala thamani yake kupimwa kwa pesa, kwa sababu si kifaa cha anasa, na kinatoa mahitaji ya moyo wa kila mmoja. Kwa kila mmoja, thamani ya ukweli huu usioshikika inafaa kuwa kubwa zaidi kuliko thamani ya vitu vyovyote vya anasa unavyofikiria kuwa ni vizuri, sivyo? Kauli hii ni kitu mnachohitaji kukiwazia. Hoja kuu ya kile nilichosema ni kwamba kile Alicho nacho Mungu na kile Alicho na kila kitu cha Mungu ndivyo vitu muhimu zaidi kwa kila mtu na haviwezi kubadilishwa na kifaa chochote cha anasa. Nitakupa mfano: Ukiwa na njaa, unahitaji chakula. Chakula hiki kinaweza kuwa kizuri kwa kiasi fulani au kinaweza kuwa kimekosa kitu fulani kwa kiasi fulani, lakini mradi tu umekula ukashiba, hisia ile mbaya ya kuwa na njaa haitakuwepo tena—itakuwa imeondoka. Unaweza kuketi pale kwa amani, na mwili wako utakuwa umepumzika. Njaa ya watu inaweza kutatuliwa kwa chakula, lakini ukiwa unamfuata Mungu na kuhisi kwamba huna ufahamu wowote Wake, unawezaje kutatua utupu huu katika moyo wako? Hali hii inaweza kusuluhishwa kwa chakula? Au unapomfuata Mungu na huelewi mapenzi Yake, ni nini unachoweza kutumia ili kufidia ile njaa katika moyo wako? Katika mchakato wa uzoefu wako wa wokovu kupitia kwa Mungu, wakati ukifuatilia mabadiliko katika tabia yako, kama huelewi mapenzi Yake au hujui ukweli ni nini, kama huelewi tabia ya Mungu, huhisi wasiwasi sana? Huhisi njaa na kiu kuu katika moyo wako? Je, hizi hisia hazikuzuii dhidi ya kuhisi pumziko katika moyo wako? Hivyo basi unaweza kufidia vipi njaa hiyo katika moyo wako—kunayo njia ya kutatua suala hilo? Baadhi ya watu huenda kufanya ununuzi, baadhi hupata rafiki wa kuwaambia yaliyo moyoni, baadhi hulala mpaka watosheke, wengine husoma zaidi maneno ya Mungu, au wakatia bidii zaidi na kutumia jitihada nyingi zaidi kukamilisha wajibu wao. Je, mambo haya yanaweza kutatua ugumu wako halisi? Nyinyi nyote mnaelewa kikamilifu aina hizi za mazoea. Unapohisi kuwa huna nguvu, unapohisi tamanio kubwa la kupata nuru kutoka kwa Mungu ili kukuruhusu kujua uhalisi wa ukweli na mapenzi Yake, ni nini unachohitaji kingi zaidi? Kile unachohitaji si mlo kamili, na wala si maneno machache mema. Zaidi ya hayo, si lile tulizo na kutosheka kwa muda kwa mwili—kile unachohitaji ni Mungu kuweza kukueleza moja kwa moja, kwa wazi kile unachofaa kufanya na namna unavyofaa kukifanya, kuweza kukuonyesha wazi ukweli ni nini. Baada ya kuelewa haya, hata kama ni sehemu ndogo tu, huhisi kuwa umetosheka zaidi katika moyo wako kuliko vile ambavyo ungekuwa umekula mlo mzuri? Wakati moyo wako umetosheka, huo moyo wako, nafsi yako nzima, havipati pumziko la kweli? Kutokana na mfano huu na uchambuzi, je, mnaelewa sasa ni kwa nini Nilitaka kusemezana na nyinyi kuhusu sentensi hii, “Mwana wa Adamu ni Bwana hata wa siku ya Sabato”? Maana yake ni kwamba kile kinachotoka kwa Mungu, kile Alicho nacho na kile Alicho, na kila kitu Chake vyote ni vikuu zaidi kuliko kitu kingine chochote, kikiwemo kile kitu au yule mtu ambaye uliwahi kuamini kuwa unamthamini zaidi. Hivyo ni kusema, kama mtu hawezi kupata maneno kutoka katika kinywa cha Mungu au kama haelewi mapenzi Yake, hawezi kupata pumziko. Katika yale mtakayopitia katika siku zako za usoni, mtaelewa ni kwa nini Nilitaka nyinyi kuona dondoo hii leo—hii ni muhimu sana. Kila kitu ambacho Mungu anafanya ni ukweli na maisha. Ukweli kwa mwanadamu ni kitu ambacho hawawezi kukosa katika maisha yao, kitu ambacho hawawezi kuishi bila; unaweza pia kusema kwamba ndicho kitu kikuu zaidi. Ingawa huwezi kukiangalia au kukigusa, umuhimu wake kwako hauwezi kupuuzwa; ndicho kitu cha pekee kinachoweza kukuletea pumziko moyoni mwako.

Je, ufahamu wenu wa ukweli umefungamana na hali yenu ya kibinafsi? Katika maisha halisi, lazima kwanza ufikirie ukweli upi unahusiana na watu, matukio, na vitu ambavyo umekumbana navyo; ni miongoni mwa ukweli huu ndimo unaweza kupata mapenzi ya Mungu na kuunganisha kile ulichokumbana nacho na mapenzi Yake. Iwapo hujui ni vipengele vipi vya ukweli vinavyohusiana na mambo ambayo umekumbana nayo lakini badala yake unaenda kwa njia ya moja kwa moja kutafuta mapenzi ya Mungu, huu ni mtazamo ambao hauna mwelekeo ambao hauwezi kufanikisha matokeo. Kama unataka kutafuta ukweli na kuelewa mapenzi ya Mungu, kwanza unahitaji kuangalia ni mambo ya aina gani ambayo yametendeka kwako, ni vipengele vipi vya ukweli ambavyo mambo hayo yana uhusiano navyo, na kisha uutafute ukweli maalum katika neno la Mungu ambalo linahusiana na kile ulichopitia. Kisha utafute njia ya matendo ambayo ni sahihi kwako katika ukweli huo; kutokana na njia hii unaweza kupata ufahamu usio wa moja kwa moja kuhusu mapenzi ya Mungu. Kutafuta na kutenda ukweli si kutumia kanuni au kufuata fomyula bila kufikiria. Ukweli si wa kifomyula, wala si sheria. Haujakufa—ni uzima wenyewe, ni kitu ambacho kina uhai, na ni kanuni ambayo lazima kilichoumbwa kifuate katika Maisha na kanuni ambayo lazima mwanadamu awe nayo katika maisha yake. Hiki ni kitu ambacho lazima, kwa vyoyote vile, uelewe kupitia uzoefu. Haijalishi ni katika awamu gani ambayo umeifikia katika uzoefu wako, huwezi kutenganishwa na neno la Mungu au ukweli, na kile unachoelewa kuhusu tabia ya Mungu na kile unachojua kuhusu kile Alicho nacho Mungu na kile Alicho ni vitu ambavyo vimeonyeshwa vyote katika maneno ya Mungu; vimeungana kabisa na ule ukweli. Tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho mwenyewe ni ukweli kwa njia yake; ukweli ni dhihirisho halisi la tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho. Unafanya kile Mungu Alicho nacho kuonyesha waziwazi kile Mungu alisema; unakuonyesha moja kwa moja kile ambacho Mungu hapendi, kile ambacho Hapendi, kile Anachokutaka ufanye na kile ambacho Hakuruhusu ufanye, watu ambao Anawachukia na watu ambao Anawafurahia. Katika ule ukweli ambao Mungu anaonyesha watu wanaweza kuona furaha, hasira, huzuni, na shangwe Yake, pamoja na kiini Chake—huu ndio ufichuzi wa tabia Yake. Mbali na kujua kile Mungu Alicho nacho na kile Alicho, na kuelewa tabia Yake kutoka katika neno Lake, kile kilicho muhimu zaidi ni haja ya kufikia ufahamu huu kupitia kwa uzoefu wa kimatendo. Kama mtu atajiondoa katika maisha halisi ili kumjua Mungu, hataweza kutimiza hayo. Hata kama kuna watu wanaoweza kupata ufahamu fulani kutoka katika neno la Mungu, ufahamu wao umewekewa mipaka ya nadharia na maneno, na kunatokea tofauti na vile ambavyo Mungu alivyo mwenyewe kwa kweli.

Kile tunachozungumzia sasa kimo ndani ya ule upana wa hadithi zilizorekodiwa katika Biblia. Kupitia katika hadithi hizi, na kupitia uchambuzi wa mambo haya yaliyofanyika, watu wanaweza kuelewa tabia Yake na kile Alicho nacho na kile Alicho ambayo Ameonyesha, na kuwaruhusu kujua kila kipengele cha Mungu kwa upana zaidi, kwa kina zaidi, kikamilifu, na kwa undani zaidi. Hivyo basi, njia pekee ya kujua kila kipengele cha Mungu ni kupitia hadithi hizi? La, siyo! Kwani kile Mungu anachosema na kazi Anayofanya katika Enzi ya Ufalme kinaweza kuwasaidia watu kwa njia bora zaidi kujua tabia Yake, na kuijua kikamilifu. Hata hivyo, Nafikiri ni rahisi zaidi kujua tabia ya Mungu na kuelewa kile Alicho nacho na kile Alicho kupitia baadhi ya mifano au hadithi zilizorekodiwa katika Biblia ambazo watu wamezoeana nazo. Nikichukua maneno ya hukumu na kuadibu na ukweli ambao Mungu anaonyesha leo ili kukufanya umjue Yeye neno kwa neno, utahisi kwamba haipendezi sana inachosha mno, na baadhi ya watu hata watahisi kwamba maneno ya Mungu yanaonekana kuwa yanafuata fomyula fulani. Lakini tukichukulia hadithi hizi za Biblia kama mifano ya kuwasaidia watu kujua tabia ya Mungu, basi haitaonekana kuwa ya kuchosha. Unaweza kusema kwamba katika mkondo wa kuonyesha mifano hii, maelezo ya kile kilichokuwa moyoni mwa Mungu wakati huo—hali Yake ya moyo au hisia Zake za moyoni, au fikira na mawazo Yake—vimesimuliwa kwa watu katika lugha za kibinadamu, na lengo la haya yote ni kuwaruhusu kushukuru, kuhisi kile Mungu Alicho nacho na kile Alicho na kujua kwamba si fomula. Si hadithi ya kale, au kitu ambacho watu hawawezi kuona wala kugusa. Ni kitu ambacho kwa kweli kipo ambacho watu wanaweza kuhisi, na kufahamu. Hili ndilo lengo la msingi. Unaweza kusema kwamba watu wanaoishi katika enzi hii wamebarikiwa. Wanaweza kuzitumia hadithi za Biblia kupata ufahamu mpana zaidi wa kazi za awali za Mungu; wanaweza kuiona tabia Yake kupitia katika kazi ambayo Amefanya. Na wanaweza kuelewa mapenzi ya Mungu kwa mwanadamu kupitia kwa tabia hizi ambazo Ameonyesha, kuelewa maonyesho yale thabiti ya utakatifu Wake na utunzaji Wake kwa binadamu ili kuweza kufikia maelezo zaidi na maarifa ya kina zaidi kuhusu tabia ya Mungu. Naamini kwamba nyinyi nyote mnaweza kuhisi haya yote!

Ndani ya upana wa kazi ambayo Bwana Yesu alikamilisha katika Enzi ya Neema, unaweza kuona kipengele kingine cha kile Alicho nacho Mungu na kile Alicho. Kilionyeshwa kupitia kwa mwili Wake, na kikawezeshwa kwa watu kuiona na kufahamu zaidi kupitia kwa ubinadamu Wake. Ndani ya Mwana wa Adamu, watu waliweza kuona namna ambavyo Mungu katika mwili alivyoishi kwa kudhihirisha ubinadamu Wake, na wakaona uungu wa Mungu ulioonyeshwa kupitia kwa mwili. Aina hizi mbili za maonyesho ziliwaruhusu watu kuweza kumwona Mungu aliye halisi sana, na kuwaruhusu kuwa na dhana tofauti ya Mungu. Hata hivyo, katika kipindi cha muda kati ya uumbaji wa ulimwengu na mwisho wa Enzi ya Sheria, yaani, kabla ya Enzi ya Neema, kile kilichoonekana, kilichosikizwa, na kupitiwa na watu kilikuwa tu kipengele kitakatifu cha Mungu. Kilikuwa kile ambacho Mungu alifanya na kusema katika himaya ile isiyoshikika, na mambo ambayo Aliyaonyesha kutoka katika nafsi Yake halisi ambayo yasingeweza kuonekana au kuguswa. Mara nyingi, mambo haya yaliwafanya watu kuhisi kwamba Mungu alikuwa mkubwa sana, na kwamba wasingeweza kusonga karibu na Yeye. Picha ambayo Mungu kwa kawaida aliwapa watu ilikuwa kwamba Alionekana akipotea, na watu walihisi hata kwamba kila mojawapo ya fikira na mawazo Yake yalikuwa yenye mafumbo mno na yasiyoeleweka mno kiasi kwamba hakukuwa na njia ya kuyafikia, isitoshe hata kujaribu kuelewa na kuyashukuru. Kwa watu, kila kitu kuhusu Mungu kilikuwa cha mbali—mbali mno kiasi kwamba watu wasingeweza kukiona, wasingeweza kukigusa. Ilionekana Alikuwa juu katika mbingu, na ilionekana kwamba Hakukuwepo kamwe. Hivyo basi kwa watu, kuelewa moyo na akili ya Mungu au kufikiria Kwake kokote kusingeweza kutimizika, na hata kufikika. Ingawa Mungu alitenda kazi fulani thabiti katika Enzi ya Sheria, na Akaweza kutoa pia maneno fulani na kuonyesha tabia fulani mahususi ili kuwaruhusu watu kushukuru na kuona maarifa halisi fulani kumhusu, bado hatimaye, hilo lilikuwa ni maonyesho ya Mungu kuhusu Alicho nacho na kile Alicho katika ulimwengu usioshikika, na kile watu walielewa, kile walichojua kilikuwa bado kile cha kipengele takatifu kuhusu kile Alicho nacho na kile Alicho. Mwanadamu asingeweza kupata dhana thabiti kutoka kwa kile Alicho nacho na kile Alicho, na ile picha waliyokuwa nayo kuhusu Mungu ilikuwa bado ndani ya mawanda ya “mwili wa kiroho ulio mgumu kukaribia, unaoonekana na kupotea ndani na nje ya mtazamo.” Kwa sababu Mungu hakutumia kifaa mahususi au taswira katika ulimwengu wa kimwili kuonekana kwa watu, bado wasingeweza kumfafanua Yeye kwa kutumia lugha ya kibinadamu. Katika mioyo na akili za watu, siku zote walitaka kutumia lugha yao binafsi ili kuanzisha kiwango kwa ajili ya Mungu, kumfanya Agusike na kumfanya Awe binadamu, kama vile Alikuwa mrefu kiasi gani, Alikuwa mkubwa kiasi gani, Alifanana vipi, Anapenda nini hasa na hulka Yake mahususi ni gani. Kwa kweli, moyoni Mwake Mungu alijua kwamba watu walifikiria hivyo. Alikuwa wazi sana kuhusu mahitaji ya watu, na bila shaka Alijua pia kile Alichofaa kufanya, hivyo basi Alitenda kazi Yake kwa njia tofauti na Enzi ya Neema. Njia hii ilikuwa takatifu na vilevile iliyostaarabishwa. Katika kipindi cha Muda ambacho Bwana Yesu alikuwa akifanya kazi, watu wangeweza kuona kwamba Mungu alikuwa na maonyesho mengi ya kibinadamu. Kwa mfano, Aliweza kucheza, Aliweza kuhudhuria harusi, Aliweza kuwasiliana kwa karibu na watu, kuongea na wao, na kujadili mambo pamoja nao. Aidha, Bwana Yesu aliweza pia kukamilisha kazi nyingi zilizowakilisha uungu Wake, na bila shaka kazi Yake yote ilikuwa ni maonyesho na ufichuzi wa tabia ya Mungu. Katika kipindi hiki, wakati uungu wa Mungu ulitambuliwa kupitia kwa mwili wa kawaida ambao watu wangeweza kuona na kugusa, hawakuhisi tena kwamba Alikuwa akionekana na kutoweka, na kwamba wangeweza kumkaribia. Kinyume cha mambo ni kwamba, wangejaribu kuelewa mapenzi ya Mungu au kuuelewa uungu Wake kupitia kila hatua, maneno, na kazi ya Mwana wa Adamu. Mwana wa Adamu mwenye mwili alionyesha uungu wa Mungu kupitia kwa ubinadamu Wake na kuwasilisha mapenzi ya Mungu kwa binadamu. Na kupitia maonyesho ya mapenzi na tabia ya Mungu, Aliwafichulia watu yule Mungu asiyeweza kuonekana au kuguswa katika ulimwengu wa kiroho. Kile watu walichoona kilikuwa Mungu Mwenyewe, anayeshikika na aliye na mwili na mifupa. Hivyo basi Mwana wa Adamu mwenye mwili Alifanya mambo kama vile utambulisho binafsi wa Mungu, hadhi, taswira, tabia, na kile Alicho nacho na kile Alicho kuwa thabiti na kupewa picha ya binadamu. Ingawa sura ya nje ya Mwana wa Adamu ilikuwa na upungufu fulani kuhusiana na taswira ya Mungu, kiini Chake na kile Alicho nacho na kile Alicho yote hayo yaliweza kwa kikamilifu kuwakilisha utambulisho na hadhi binafsi ya Mungu—kulikuwa tu na tofauti fulani katika jinsi ya maonyesho. Bila kujali kama ni ubinadamu wa Mwana wa Mungu au uungu Wake, hatuwezi kukana kwamba Aliwakilisha utambulisho na hadhi binafsi ya Mungu mwenyewe. Katika kipindi hiki cha muda, hata hivyo, Mungu alifanya kazi kupitia mwili, Akaongea kutoka kwa mtazamo wa mwili, na kusimama mbele ya mwanadamu kwa utambulisho na hadhi ya Mwana wa Adamu, na hili liliwapa watu fursa ya kukumbana na kupitia maneno na kazi ya kweli ya Mungu miongoni mwa binadamu. Iliweza pia kuwaruhusu watu kuwa na utambuzi wa uungu Wake na ukubwa Wake katikati ya unyenyekevu, vilevile na kupata ufahamu wa mwanzo na ufafanuzi wa mwanzo wa uhalali na uhalisi wa Mungu. Hata ingawa kazi iliyokamilishwa na Bwana Yesu, njia Zake za kufanya kazi, na mitazamo ambayo kutoka kwayo Aliongea ilitofautiana na ile ya nafsi halisi ya Mungu katika ulimwengu wa kiroho, kila kitu kumhusu kilimwakilisha kwa kweli Mungu Mwenyewe ambaye binadamu walikuwa hawajawahi kumwona awali—hili haliwezi kukataliwa! Hivi ni kusema, haijalishi ni kwa umbo gani ambalo Mungu huonekana, haijalishi huongea kutoka katika mtazamo upi, au Yeye hukabiliana na binadamu kupitia kwa taswira gani, Mungu hawakilishi chochote isipokuwa Yeye Mwenyewe. Hawezi kumwakilisha binadamu yeyote—Hawezi kumwakilisha binadamu yeyote aliyepotoka. Mungu ni Mungu Mwenyewe, na hili haliwezi kukataliwa.

Kifuatacho tutaangalia mfano uliozungumziwa na Bwana Yesu katika Enzi ya Neema.

3. Mfano wa Kondoo Aliyepotea

Mat 18:12-14 Mnafikiri vipi? Iwapo mtu ana kondoo mia moja, na mmoja wao apotee, je, hawaachi hao tisini na tisa, na kuenda milimani, na amtafute huyo ambaye amepotea? Na iwapo atampata, kweli nawaambia, anafurahi zaidi kwa sababu ya huyo kondoo, kuliko wao tisini na tisa ambao hawakupotea. Kwa namna hiyo siyo mapenzi ya Baba yenu ambaye yuko mbinguni, kuwa mmoja wa hawa wadogo aangamie.

Kifungu hiki ni fumbo—ni hisia gani watu wanapata kutokana fumbo hili? Namna ya kujieleza—fumbo—lilitumika hapa ni mbinu za lugha katika lugha ya binadamu, na kwa hivi ni kitu kilicho ndani ya mawanda ya maarifa ya binadamu. Kama Mungu angekuwa amesema kitu kinachofanana katika Enzi ya Sheria, watu wangehisi kwamba hakikuambatana na Alichokuwa Mungu, lakini Mwana wa Adamu alipoonyesha kifungu hiki katika Enzi ya Neema, kilionekana cha kufariji, chenye uzuri, na kilicho karibu kwa watu. Mungu alipokuwa mwili, Alipoonekana katika umbo la binadamu, Alitumia sitiari inayofaa sana kuonyesha sauti ya roho Yake katika ubinadamu. Sauti hii iliwakilisha sauti binafsi ya Mungu na kazi Aliyotaka kufanya katika enzi hiyo. Pia iliwakilisha mtazamo ambao Mungu alikuwa nao kwa watu katika Enzi ya Neema. Tukiangalia kutoka kwa mtazamo wa mwelekeo wa Mungu kwa watu, Alimfananisha kila mtu na kondoo. Kama kondoo amepotea, Atafanya kila awezalo ili kumpata. Hii inawakilisha kanuni ya kazi ya Mungu miongoni mwa binadamu wakati huu katika mwili. Mungu aliutumia mfano huu kufafanua uamuzi na mwelekeo Wake katika kazi hiyo. Haya ndiyo yaliyokuwa manufaa ya Mungu kuwa mwili: Angeweza kutumia vizuri maarifa ya binadamu na kutumia lugha ya binadamu kuongea na watu, kuonyesha mapenzi Yake. Aliwaelezea au “kuwatafsiria” binadamu lugha Yake ya maana sana, ya kiungu ambayo watu walipata ugumu kuelewa kupitia lugha ya binadamu, kwa njia ya kibinadamu. Hii iliwasaidia watu kuelewa mapenzi Yake na kujua kile Alichotaka kufanya. Angeweza pia kuwa na mazungumzo na watu kutoka katika mtazamo wa kibinadamu, kwa kutumia lugha ya kibinadamu, na kuwasiliana na watu kwa njia waliyoelewa. Aliweza pia kuongea na kufanya kazi kwa kutumia lugha na maarifa ya kibinadamu ili watu waweze kuhisi wema na ukaribu wa Mungu, ili wangeweza kuuona moyo Wake. Mnaona nini katika hili? Kwamba hakuna kuzuiliwa katika maneno na vitendo vya Mungu? Namna watu wanavyoona, hakuna njia ambayo Mungu angetumia maarifa ya kibinadamu, lugha, au njia za kuongea ili kuzungumza kuhusu kile ambacho Mungu Mwenyewe alitaka kusema, kazi Aliyotaka kufanya, au kuonyesha mapenzi Yake mwenyewe; huku ni kufikiria ambako si sahihi. Mungu alitumia aina hii ya sitiari ili watu waweze kuhisi ule uhalisi na uaminifu wa Mungu, na kuona mwelekeo Wake kwa watu katika kipindi hicho cha muda. Mfano huu uliwazindua watu waliokuwa wakiishi chini ya sheria kwa muda mrefu kutoka katika ndoto, na vilevile uliweza kuhemsha kizazi baada ya kizazi cha watu walioishi katika Enzi ya Neema. Kwa kukisoma kifungu cha mfano huu, watu wanajua uaminifu wa Mungu katika kuwaokoa binadamu na wanaelewa uzito wa mwanadamu katika moyo Wake.

Hebu tuangalie kwa mara nyingine sentensi ya mwisho katika dondoo hii: “Kwa namna hiyo siyo mapenzi ya Baba yenu ambaye yuko mbinguni, kuwa mmoja wa hawa wadogo aangamie.” Haya yalikuwa maneno binafsi ya Bwana Yesu, au yalikuwa maneno ya Baba Yake aliye mbinguni? Kwa juujuu, yaonekana alikuwa Bwana Yesu akiongea, lakini mapenzi Yake yanawakilisha mapenzi ya Mungu Mwenyewe, na ndiyo maana Akasema: “Kwa namna hiyo siyo mapenzi ya Baba yenu ambaye yuko mbinguni, kuwa mmoja wa hawa wadogo aangamie.” Watu wakati huo walimtambua tu Baba aliye mbinguni kama Mungu, na mtu huyu waliyeona mbele ya macho yao alikuwa ametumwa tu na Yeye, na hakuweza kuwakilisha Baba aliye mbinguni. Ndiyo maana Bwana Yesu alilazimika kusema hivyo vilevile, ili waweze kuhisi kwa kweli mapenzi ya Mungu kwa mwanadamu, na kuhisi ule uhalali na usahihi wa kile Alichosema. Hata ingawa jambo hili lilikuwa jepesi kusema, lilikuwa lenye utunzaji mwingi na lilifichua unyenyekevu na ufiche wa Bwana Yesu. Bila kujali kama Mungu alikuwa mwili au Alifanya kazi katika ulimwengu wa kiroho, Aliujua moyo wa binadamu kwa njia bora zaidi, na Alielewa kwa njia bora zaidi kile watu walichohitaji, Alijua ni nini watu walikuwa na wasiwasi kuhusu, na kile kilichowakanganya, hivyo Akaongeza mstari huu. Mstari huu uliangazia tatizo lililofichika ndani ya mwanadamu: Watu hawakuamini kile ambacho Mwana wa Adamu alisema, hivi ni kusema kwamba, Bwana Yesu alipokuwa akiongea Alilazimika kuongeza: “Kwa namna hiyo siyo mapenzi ya Baba yenu ambaye yuko mbinguni, kuwa mmoja wa hawa wadogo aangamie.” Ni katika kauli hii tu ndiyo maneno Yake yangezaa matunda, kuwafanya watu kuamini usahihi wao na kuboresha kiwango cha kuaminika kwa maneno hayo. Hii inaonyesha kwamba Mungu alipokuwa Mwana wa Adamu wa kawaida, Mungu na mwanadamu walikuwa na uhusiano mgumu sana, na kwamba hali ya Mwana wa Adamu ilikuwa ya kuaibisha mno. Inaonyesha pia namna ambavyo hadhi ya Bwana Yesu ilivyokuwa isiyo na maana miongoni mwa binadamu wakati huo. Aliposema haya, kwa hakika ilikuwa ni kuwaambia watu: Mnaweza kuwa na uhakika kwamba—haya hayawakilishi yale yaliyo moyoni Mwangu mwenyewe, lakini ni mapenzi ya Mungu aliye mioyoni mwenu. Kwa mwanadamu, jambo hili halikuwa la kejeli? Ingawa Mungu kufanya kazi katika mwili kulikuwa na manufaa mengi ambayo Hakuwa nayo katika nafsi Yake, Alilazimika kustahimili shaka na kukataliwa na wao pamoja na kutojali na kutochangamka kwao. Yaweza kusemekana kwamba mchakato wa kazi ya Mwana wa Adamu ulikuwa mchakato wa kupitia kukataliwa na mwanadamu, na kuhisi mashindano yao akishindana dhidi Yake. Zaidi ya hayo, ulikuwa ni mchakato wa kufanya kazi ili kuendelea kushinda imani ya mwanadamu na kumshinda mwanadamu kupitia kile Alicho nacho na kile Alicho, kupitia kiini Chake binafsi halisi. Haikuwa sana kwamba Mungu mwenye mwili Alikuwa akipigana vita vikali dhidi ya Shetani; ilikuwa zaidi kwamba Mungu aligeuka na kuwa binadamu wa kawaida na kuanzisha mapambano pamoja na wale wanaomfuata Yeye, na katika mapambano haya Mwana wa Adamu alikamilisha kazi Yake kwa unyenyekevu Wake, pamoja na kile Alicho nacho na kile Alicho, na upendo na hekima Yake. Aliwapata watu Aliowataka, kushinda utambulisho na hadhi Aliyostahili, na “kurudi” kwa kiti Chake cha enzi.

Kifuatacho, hebu basi tuangalie dondoo mbili zifuatazo katika maandiko.

4. Samehe Sabini Mara Saba

Mat 18:21-22 Kisha Petro akakuja kwake, na kusema, Bwana, ni mara ngapi ndugu yangu atanikosea, nami nimsamehe? Hadi mara saba? Yesu akasema kwake, sikuambii, hadi mara saba: ila, hadi sabini mara saba.

5. Upendo wa Bwana

Mat 22:37-39 Yesu akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako mzima, na roho yako nzima, na akili yako nzima. Hii ni amri ya kwanza na kubwa. Na ya pili ni kama hiyo, Mpende jirani yako kama unavyojipenda.

Kati ya dondoo hizi mbili, moja yazungumzia msamaha na nyingine inazungumzia upendo. Mada hizi mbili zinaangazia kwa kweli kazi ambayo Bwana Yesu alitaka kutekeleza katika Enzi ya Neema.

Wakati Mungu alipokuwa mwili, Alileta pamoja naye hatua ya kazi Yake—Alileta pamoja naye kazi mahususi na tabia Aliyotaka kuonyesha katika enzi hii. Katika kipindi hicho, kila kitu ambacho Mwana wa Adamu alifanya kilizungukia kazi ambayo Mungu alitaka kutekeleza katika enzi hii. Asingeweza kufanya zaidi au kufanya kidogo zaidi. Kila kitu Alichosema na kila aina ya kazi Aliyotekeleza ilihusiana yote na enzi hii. Haijalishi kama Alionyesha kwa njia ya kibinadamu Akitumia lugha ya kibinadamu au kupitia kwa lugha ya kiungu—haijalishi ni njia gani, au kutoka kwa mtazamo gani—lengo Lake lilikuwa ni kuwasaidia watu kuelewa kile Alichotaka kufanya, mapenzi Yake yalikuwa nini, na mahitaji Yake yalikuwa yapi kutoka kwa watu. Anaweza kutumia mbinu mbalimbali kutoka mitazamo mbalimbali ili kuwasaidia watu kuelewa na kujua mapenzi Yake, kuelewa kazi Yake ya kuwaokoa binadamu. Hivyo basi katika Enzi ya Neema tunamwona Bwana Yesu akitumia lugha ya kibinadamu wakati mwingi kuonyesha kile Alichotaka kuwasilisha kwa mwanadamu. Hata zaidi, tunamwona kutoka katika mtazamo wa mwelekezi wa kawaida Akiongea na watu, Akishughulikia mahitaji yao, na Akiwasaidia na kile walichoomba. Njia hii ya kufanya kazi haikuonekana katika Enzi ya Sheria iliyokuja kabla ya Enzi ya Neema. Aligeuka na kuwa karibu zaidi na mwenye huruma zaidi kwa binadamu, pamoja na kuweza kutimiza zaidi matokeo ya kimatendo katika umbo Lake na tabia Yake. Istiara kuhusu kusamehe watu sabini mara saba unafafanua zaidi hoja hii. Kusudio lililotimizwa kupitia kwa nambari katika Istiara hii ni kuwaruhusu watu kuelewa nia ya Bwana Yesu wakati huo aliposema hayo. Nia Yake ilikuwa kwamba watu wanafaa kuwasamehe wengine—si mara moja wala mara mbili na wala si hata mara saba, lakini sabini mara saba. Hili wazo la “sabini mara saba” ni la aina gani? Ni la kuwafanya watu kufanya msamaha kuwa wajibu wao wa kibinafsi, kitu ambacho lazima wajifunze, na “njia” ambayo kwayo ni lazima waishi. Hata ingawa hii ilikuwa Istiara tu, iliwasaidia watu kufahamu kwa kina. Ilisaidia pwatu kutafuta njia bora za kufanyia mazoezi na kanuni na viwango vya utendaji. Istiara hii iliwasaidia watu kuweza kuelewa waziwazi na ikawapa wazo sahihi—kwamba wanafaa kujifunza kusamehe na wasamehe nambari yote bila ya masharti na bila ya upungufu wowote, lakini kwa mtazamo wa uvumilivu na ufahamu kwa wengine. Bwana Yesu aliposema haya, ni nini kilichokuwa moyoni Mwake? Alikuwa akifikiria kwa kweli kuhusu sabini mara saba? Hakuwa akifikiri kuhusu hilo. Ipo idadi ya mara ambazo Mungu atawasamehe binadamu? Kunao watu wengi walio na shauku katika “idadi” iliyotajwa, wanaotaka kwa kweli kuelewa asili na maana ya nambari hii. Wanataka kuelewa kwa nini nambari hii ilitoka kinywani mwa Bwana Yesu; wanaamini kwamba kuna uhusisho wa kina zaidi katika nambari hii. Kwa hakika, huu ulikuwa ni usemi tu wa Mungu katika ubinadamu. Uhusisho au maana yoyote lazima ichukuliwe pamoja na mahitaji ya Bwana Yesu kwa mwanadamu. Wakati Mungu alikuwa bado hajawa mwili, watu hawakuelewa mengi ya Alichosema kwa sababu kilitoka katika uungu kamilifu. Mtazamo na muktadha wa kile Alichosema ulikuwa hauonekani na haufikiwi na mwanadamu; ulionyeshwa kutoka katika ulimwengu wa kiroho ambayo watu wasingeweza kuiona. Kwa watu walioishi katika mwili, wasingeweza kupita katika ulimwengu wa kiroho. Lakini baada ya Mungu kuwa mwili, Aliongea na mwanadamu kutoka katika mtazamo wa ubinadamu, na Alitoka kwa na, na akazidi mawanda ya ulimwengu wa kiroho. Angeweza kuonyesha tabia Yake ya uungu, mapenzi, na mtazamo, kupitia mambo yale ambayo binadamu wangeweza kufikiria na mambo yale wangeweza kuona na kukumbana nayo katika maisha yao, kwa kutumia mbinu ambazo binadamu wangeweza kukubali, kwa lugha ambayo wangeweza kuelewa, na maarifa ambayo wangeweza kuelewa, ili kuruhusu mwanadamu kumwelewa na kumjua Mungu, kufahamu nia Yake na viwango Vyake hitajika ndani ya mawanda ya uwezo wao; hadi kufikia kiwango ambacho wangeweza. Hii ndiyo iliyokuwa mbinu na kanuni ya kazi ya Mungu kwa ubinadamu. Ingawa njia za Mungu na kanuni Zake za kufanya kazi katika mwili ziliweza kutimizwa sana kwa, au kupitia kwa ubinadamu, ziliweza kwa kweli kutimiza matokeo ambayo yasingeweza kutimizwa kwa kufanya kazi moja kwa moja katika uungu. Kazi ya Mungu katika ubinadamu ilikuwa thabiti zaidi, halisi, na yenye malengo, mbinu zilikuwa zaweza kubadilika kwa urahisi zaidi, na kwa umbo iliweza kupita Enzi ya Sheria.

Hapa chini, hebu tuzungumzie kumpenda Bwana na kumpenda jirani yako kama unavyojipenda. Je, hili ni jambo linaloelezewa moja kwa moja kupitia uungu? Bila shaka silo! Haya yalikuwa mambo yote ambayo Mwana wa Adamu alisema kwa ubinadamu; watu tu ndio wangeweza kusema kauli kama “Mpende jirani yako kama unavyojipenda. Kuwapenda wengine ni sawa na kuyatunza maisha yako binafsi,” na watu tu ndio wangeweza kuongea kwa njia hii. Mungu hajawahi kuongea kwa njia hiyo. Kwa kiwango cha chini zaidi, Mungu hana aina hii ya lugha katika uungu Wake kwa sababu Hahitaji aina hii ya imani, “Mpende jirani yako kama unavyojipenda” ili kudhibiti upendo Wake kwa mwanadamu, kwa sababu upendo wa Mungu kwa mwanadamu ni ufichuzi wa kiasili wa kile Alicho nacho na kile Alicho. Ni lini mmewahi kusikia kwamba Mungu alisema kitu kama “Nampenda binadamu kama Ninavyojipenda”? Kwa sababu upendo umo katika kiini cha Mungu, na ndani ya kile Alicho nacho na kile Alicho. Upendo wa Mungu kwa binadamu na jinsi Anavyowashughulikia watu na mtazamo Wake ni maonyesho ya kiasili na ufichuzi wa tabia Yake. Hahitaji kufanya hili kwa njia fulani kimakusudi, au kufuata mbinu fulani au mfumo wa maadili kimakusudi ili kutimiza kumpenda jirani Yake kama Anavyojipenda—tayari Anamiliki aina hii ya kiini. Unaona nini katika haya? Wakati Mungu alipofanya kazi katika ubinadamu, mbinu, maneno, na ukweli Wake mwingi vyote vilionyeshwa kwa njia ya kibinadamu. Lakini wakati uo huo tabia ya Mungu, kile Alicho nacho na kile Alicho, na mapenzi Yake vyote vilionyeshwa kwa watu kuweza kujua na kuvielewa. Kile walichojua na kuelewa kilikuwa hasa kiini Chake na Alicho nacho na kile Alicho, vyote ambavyo vinawakilisha utambulisho na hadhi ya asili ya Mungu Mwenyewe. Hivyo ni kusema kwamba, Mwana wa Adamu kwa mwili Alionyesha tabia ya asili na kiini cha Mungu Mwenyewe kwa kiwango kikubwa zaidi kinachowezekana na kwa usahihi zaidi unaowezekana. Ubinadamu wa Mwana wa Adamu haukuwa pingamizi au kizuizi cha mawasiliano na kuingiliana kwa binadamu na Mungu mbinguni tu, bali kwa hakika ilikuwa ndio njia ya pekee na daraja la pekee la mwanadamu kuungana na Bwana wa uumbaji. Wakati huu, je, hamhisi kwamba kunayo mifanano mingi kati ya asili na mbinu za kazi iliyofanywa na Bwana Yesu katika Enzi ya Neema na awamu ya sasa ya kazi? Hatua ya sasa ya kazi inatumia pia lugha nyingi za kibinadamu kueleza tabia ya Mungu, na inatumia lugha na mbinu nyingi kutoka katika maisha ya kila siku ya binadamu na maarifa ya kibinadamu ili kuonyesha mapenzi binafsi ya Mungu. Punde Mungu anapokuwa mwili, haijalishi kama Anaongea kutoka kwa mtazamo wa kibinadamu au mtazamo wa kiungu, wingi wa lugha na mbinu Zake za maonyesho yote ni kupitia katika njia ya lugha na mbinu za kibinadamu. Yaani, wakati Mungu anapokuwa mwili, ndiyo fursa bora zaidi ya wewe kuweza kuona kudura ya Mungu na hekima Yake, na kujua kila kipengele halisi cha Mungu. Mungu alipogeuka na kuwa mwili, wakati Alikuwa Akikua, Alipata kuelewa, kujifunza, na kuelewa baadhi ya maarifa ya binadamu, maarifa ya kawaida, lugha, na mbinu za maonyesho katika ubinadamu. Mungu mwenye mwili alimiliki mambo haya yaliyotokana na binadamu Aliyekuwa ameumba. Waligeuka na kuwa zana za Mungu katika mwili za kueleza tabia Yake na uungu Wake, na wakamruhusu kuifanya kazi Yake ya kufaa zaidi, halisi zaidi, na sahihi zaidi Alipokuwa akifanya kazi katikati ya mwanadamu, kutoka katika mtazamo wa kibinadamu na kwa kutumia lugha ya kibinadamu. Iliiwezesha kufikiwa zaidi na kueleweka kwa urahisi zaidi na watu, hivyo basi kutimiza matokeo ya kile Mungu Alichotaka. Je, si jambo la busara zaidi kwa Mungu kufanya kazi kupitia kwa mwili kwa njia hii? Je, hii sio hekima ya Mungu? Wakati Mungu alipogeuka na kuwa mwili, wakati mwili wa Mungu uliweza kuchukua kazi Aliyotaka kutekeleza, ndipo Angeonyesha tabia Yake na kazi Yake kwa utendaji, na huu ndio wakati pia ambao Angeanza rasmi huduma Yake kama Mwana wa Adamu. Hii ilimaanisha kwamba hakukuwepo tena pengo la kizazi kati ya Mungu na binadamu, kwamba Mungu angesitisha karibuni kazi Yake ya kuwasiliana kupitia kwa wajumbe, na kwamba Mungu Mwenyewe binafsi angeweza kuonyesha maneno na kazi zote Alizotaka kufanya katika mwili. Hii ilimaanisha pia kwamba watu ambao Mungu huokoa walikuwa karibu na Yeye, na kwamba kazi Yake ya usimamizi ilikuwa imeingia eneo jipya, na kwamba binadamu wote walikuwa karibu kukumbwa na enzi mpya.

Kila mtu ambaye amesoma Biblia anajua kwamba mambo mengi yalifanyika Bwana Yesu alipozaliwa. Kubwa zaidi miongoni mwa hayo lilikuwa kutafutwa na mfalme wa ibilisi, hadi kufikia kiwango cha watoto wote wenye umri wa miaka miwili na chini katika eneo hilo kuchinjwa. Ni dhahiri kwamba Mungu alichukua hatari kubwa kwa kuwa mwili miongoni mwa binadamu; gharama kubwa Aliyolipia kwa ajili ya kukamilisha usimamizi Wake wa kumwokoa mwanadamu pia ni wazi. Matumaini makubwa ambayo Mungu alishikilia kwa ajili ya kazi Yake miongoni mwa wanadamu katika mwili pia ni wazi. Wakati mwili wa Mungu uliweza kuchukua kazi miongoni mwa wanadamu, Alikuwa anahisi vipi? Watu wanafaa kuweza kuelewa hilo kidogo, sivyo? Kwa kiwango cha chini zaidi, Mungu alifurahia kwa sababu Angeanza kuendeleza kazi Yake mpya miongoni mwa wanadamu. Bwana Yesu alipobatizwa na kuanza rasmi kazi Yake kukamilisha huduma Yake, moyo wa Mungu ulijawa na furaha kwa sababu baada ya miaka mingi sana ya kusubiri na matayarisho, hatimaye Angeweza kuuvaa mwili wa binadamu wa kawaida na kuanza kazi Yake mpya katika umbo la binadamu aliye na mwili na damu ambao watu wangeweza kuona na kugusa. Angeweza kuzungumza ana kwa ana na moyo kwa moyo na watu kupitia utambulisho wa binadamu. Mungu hatimaye angeweza kuwa ana kwa ana na mwanadamu katika lugha ya kibinadamu, kwa njia ya kibinadamu; Angeweza kumruzuku mwanadamu, kumwelimisha binadamu, na kumsaidia binadamu kwa kutumia lugha ya kibinadamu; angeweza kula kwenye meza moja na kuishi katika nafasi sawa na binadamu. Angeweza pia kuwaona binadamu, kuona vitu, na kuona kila kitu kwa njia ambayo binadamu walifanya hivyo na hata kupitia kwa macho yao. Kwake Mungu, huu ulikuwa tayari ushindi Wake wa kwanza wa kazi Yake katika mwili. Yaweza pia kusemekana kwamba yalikuwa ni ufanikishaji wa kazi kubwa—hili bila shaka ndilo ambalo Mungu alilifurahia zaidi. Kuanzia hapo ndiyo mara ya kwanza ambayo Mungu alihisi tulizo fulani katika kazi Yake miongoni mwa wanadamu. Matukio haya yote yalikuwa ya kimatendo sana na ya asili sana, na tulizo ambalo Mungu alihisi lilikuwa halisi. Kwa mwanadamu, kila mara hatua mpya ya kazi ya Mungu inapokamilishwa, na kila mara Mungu anapohisi kuridhika, ndipo mwanadamu anapoweza kusogea karibu zaidi na Mungu, na ndipo watu wanapoweza kusonga karibu zaidi na wokovu. Kwa Mungu, huu pia ni uzinduzi wa kazi Yake mpya, wakati mpango Wake wa usimamizi unapoendelea hatua moja zaidi, na, aidha, wakati mapenzi Yake yanapokaribia mafanikio kamili. Kwa mwanadamu, kuwasili kwa fursa kama hiyo ni bahati, na nzuri sana; kwa wale wote wanaosubiria wokovu wa Mungu, ni kubwa na habari za furaha. Mungu anapotekeleza hatua mpya ya kazi, basi Anao mwanzo mpya na wakati ambapo kazi hii mpya na mwanzo mpya vinazinduliwa na kufahamishwa miongoni mwa binadamu, ni wakati ambao matokeo ya hatua hii ya kazi tayari yameamuliwa, na kufanikishwa, naye Mungu tayari ameona athari yake ya mwisho na tunda. Huu pia ndio wakati ambapo athari hizi zinamfanya Mungu aridhike, na moyo Wake, bila shaka una furaha. Kwa sababu katika macho ya Mungu, tayari ameona na kuamua watu anaowatafuta, na tayari Amelipata kundi hili, kundi ambalo linaweza kufanya kazi Yake kufanikiwa na kumpa utoshelevu, Mungu anahisi Akiwa ameondolewa shaka, Anaweka pembeni wasiwasi Wake, na Anahisi mwenye furaha. Kwa maneno mengine, wakati mwili wa Mungu unaweza kuanza kazi mpya miongoni mwa binadamu, na Anaanza kufanya kazi ambayo lazima Afanye bila ya kizuizi, na wakati Anapohisi kwamba yote yamefanikishwa, tayari Ameuona mwisho. Na kwa sababu ya mwisho huu Anatosheka, na kuwa mwenye moyo wa furaha. Furaha ya Mungu inaonyeshwa vipi? Unaweza kufikiria jawabu litakuwa lipi? Je, Mungu anaweza kulia? Mungu Anaweza kulia? Mungu Anaweza kupiga makofi? Mungu Anaweza kucheza? Mungu Anaweza kuimba? Na wimbo huo ungekuwa upi? Bila shaka Mungu Angeweza kuimba wimbo mzuri, wa kusisimua, wimbo ambao unaweza kuonyesha shangwe na furaha katika moyo Wake. Angeweza kuwaimbia binadamu, kujiimbia Mwenyewe, na kuuimba kwa viumbe vyote. Furaha ya Mungu inaweza kuonyeshwa kwa njia yoyote—yote haya ni kawaida kwa sababu Mungu ana shangwe na huzuni, na hisia Zake mbalimbali zinaweza kuonyeshwa kwa njia mbalimbali. Hii ndiyo haki Yake na hakuna kitu kingekuwa cha kawaida zaidi na sahihi. Watu hawafai kufikiria chochote kingine kuhusu hili. Hufai kujaribu kutumia “laana ya kukzana mshipi”[a] kwa Mungu, ukimwambia kwamba Yeye hafai kufanya hiki au kile, Hafai kutenda kwa njia hii au ile, kuwekea mipaka shangwe Yake au hisia yoyote ile Aliyo nayo. Katika mioyo ya watu Mungu hawezi kuwa na furaha, Hawezi kutokwa na machozi, Hawezi kulia—Hawezi kuonyesha hisia zozote. Kupitia yale tuliyowasiliana katika nyakati hizi mbili, Naamini hamtamwona tena Mungu kwa njia hii, lakini mtamruhusu Mungu kuwa na uhuru na uachiliaji fulani. Hiki ni kitu kizuri. Katika siku za usoni kama mtaweza kuhisi kwa kweli huzuni ya Mungu mnaposikia kwamba Yeye ana huzuni, na mnaweza kuhisi kwa kweli shangwe Yake mnaposikia kuhusu Yeye kuwa na furaha—angalau, mnaweza kujua na kuelewa waziwazi kile kinachomfanya Mungu kuwa na furaha na kile kinachomfanya Yeye kuwa na huzuni—unapoweza kuhisi huzuni kwa sababu Mungu ana huzuni na kuhisi furaha kwa sababu Mungu ana furaha, Atakuwa ameupata moyo wako na hakutakuwa tena na kizuizi chochote na Yeye. Hamtajaribu tena kumzuilia Mungu na fikira na maarifa ya binadamu. Wakati huo, Mungu atakuwa hai na dhahiri moyoni mwako. Atakuwa Mungu wa maisha yako na Bwana wa kila kitu chako. Je, mnalo tamanio kama hili? Je, mnayo imani kuwa mnaweza kutimiza haya?

Halafu hebu tusome fahamu zifuatazo.

6. Ibada Mlimani

Sifa na Heri (Mat 5:3-12)

Chumvi na Nuru (Mat 5:13-16)

Sheria (Mat 5:17-20)

Kuhusu Hasira (Mat 5:21-26)

Kuhusu Uzinzi (Mat 5:27-30)

Kuhusu Talaka (Mat 5:31-32)

Kuhusu Viapo (Mat 5:33-37)

Kuhusu Kulipiza Kisasi (Mat 5:38-42)

Upendo kwa Adui (Mat 5:43-48)

Kuhusu Utoaji Sadaka (Mat 6:1-4)

Kuhusu Maombi (Mat 6:5-8)

7. Mifano ya Bwana Yesu

Mfano wa Mpanzi (Mat 13:1-9)

Mfano wa Magugu katikati ya Ngano (Mat 13:24-30)

Mfano wa Punje ya Haradali (Mat 13:31-32)

Mfano wa Chachu (Mat 13:33)

Mfano wa Magugu Umeelezwa (Mat 13:36-43)

Mfano wa Hazina (Mat 13:44)

Mfano wa Lulu (Mat 13:45-46)

Mfano wa Wavu (Mat 13:47-50)

8. Amri

Mat 22:37-39 Yesu akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako mzima, na roho yako nzima, na akili yako nzima. Hii ni amri ya kwanza na kubwa. Na ya pili ni kama hiyo, Mpende jirani yako kama unavyojipenda.

Hebu kwanza tuangalie katika kila sehemu ya “Ibada Mlimani.” Haya yote yanahusiana na nini? Yaweza kusemekana kwa uhakika kwamba haya yote yameinuliwa zaidi, yana uthabiti zaidi na karibu zaidi katika maisha ya watu kuliko taratibu zile za Enzi ya Sheria. Kuzungumza katika muktadha wa kisasa, yanahusiana zaidi na matendo halisi ya watu.

Hebu tusome maudhui mahususi ya yafuatayo: Mnafaa kuzielewa vipi hali hizi za heri? Ni nini mnachofaa kujua kuhusu sheria? Ghadhabu inafaa kufasiliwa vipi? Wazinzi wanafaa kushughulikiwa vipi? Ni nini kinachosemwa, na ni sheria aina gani zipo kuhusu talaka, na ni nani anayeweza kutalikiwa na ni nani asiyeweza kutalikiwa? Na je, viapo, jicho kwa jicho, kuwapenda adui zako, maagizo kuhusu sadaka? Na kadhalika Mambo haya yote yanahusu kila kipengele cha matendo ya imani ya mwanadamu kwa Mungu, na ufuataji wao wa Mungu. Baadhi ya desturi hizi zinatumika leo, lakini bado yapo katika hali ya kimsingi kuliko mahitaji ya sasa ya watu. Kwa kiasi kikubwa uko katika hali ya kimsingi ambao watu wanakumbana nao katika kuamini kwao katika Mungu. Tangu wakati Bwana Yesu alianza kufanya kazi, Alikuwa tayari anaanza kufanya kazi kwa tabia ya maisha ya binadamu, lakini yalitokana na msingi wa sheria. Je, sheria na misemo kuhusu mada hizi ilikuwa na uhusiano wowote na ukweli? Bila shaka zilikuwa nao! Taratibu, kanuni na ibada zote zingine za awali katika Enzi ya Neema zilikuwa na uhusiano, na tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho na bila shaka kwa ukweli. Haijalishi ni nini ambacho Mungu anaonyesha, kwa njia gani Anaonyesha, au Akitumia lugha gani, asili yake, na mwanzo wake, vyote vinatokana na kanuni za tabia Yake na kile Alicho nacho na kile Alicho. Hili halina kosa. Kwa hivyo ingawa haya mambo Aliyoyasema yanaonekana kuwa ya juujuu, bado hamwezi kusema kwamba mambo haya si ukweli, kwa sababu yalikuwa mambo ambayo yalikuwa ya lazima kwa watu katika Enzi ya Neema ili kuridhisha mapenzi ya Mungu na kutimiza mabadiliko katika tabia yao ya maisha. Unaweza kusema kwamba mambo yoyote yale katika ibada hayaambatani na ukweli? Huwezi! Kila mojawapo ya mambo haya ni ukweli kwa sababu yote yalikuwa mahitaji ya Mungu kwa mwanadamu; yote yalikuwa kanuni na mawanda yaliyotolewa na Mungu kuhusu namna ambavyo unaweza kuwa na mwenendo, na yanawakilisha tabia ya Mungu. Hata hivyo, kutokana na kiwango cha ukuaji wao katika maisha wakati huo, waliweza tu kukubali na kuyafahamu mambo haya. Kwa sababu dhambi ya mwanadamu ilikuwa bado haijatatuliwa, Bwana Yesu angeweza tu kuyatoa maneno haya, na Angeweza kutumia mafundisho mepesi kama hayo miongoni mwa aina hii ya upana ili kuwaambia watu wa wakati huo namna ambavyo walifaa kutenda, kile walichofaa kufanya, ndani ya kanuni na upana gani walifaa kufanya mambo, na vipi walivyofaa kuamini katika Mungu na kutimiza mahitaji Yake. Haya yote yaliamuliwa kulingana na kimo cha mwanadamu wakati huo. Haikuwa rahisi kwa watu wanaoishi katika sheria kuyakubali mafundisho haya, hivyo basi kile Alichofunza Bwana Yesu lazima kingebaki ndani ya mawanda haya.

Halafu, hebu tuangalie ni nini kilicho katika “Mifano ya Bwana Yesu.”

Mfano wa kwanza ni mfano wa mpanzi. Huu ni mfano wa kusisimua kweli; upanzi wa mbegu ni tukio maarufu sana katika maisha ya watu. Mfano wa pili ni mfano wa magugu. Kulingana na jinsi magugu yalivyo, yeyote ambaye amewahi kupanda mimea na watu wazima watajua. Wa tatu ni mfano wa punje ya haradali. Nyinyi nyote mnajua haradali ni nini, sivyo? Kama hujui, unaweza kupekuapekua katika Biblia. Nao mfano wa nne ni mfano wa chachu, watu wengi wanajua kwamba chachu inatumiwa katika kutia chachu; ni kitu ambacho watu wanatumia katika maisha yao ya kila siku. Mifano yote iliyotajwa hapa chini ukiwemo mfano wa sita, mfano wa hazina, mfano wa saba, mfano wa lulu, na wa nane mfano wa wavu; ni mifano iliyotolewa katika maisha ya watu; inatoka katika maisha ya watu halisi. Ni picha ya aina gani inayoonyeshwa na mifano hii? Hii ni picha ya Mungu akigeuka kuwa mtu wa kawaida na kuishi pamoja na mwanadamu, Akitumia lugha ya maisha ya kila siku, Akitumia lugha ya mwanadamu ili kuwasiliana na binadamu na kuwapa kile wanachohitaji. Wakati Mungu alikuwa mwili na kuishi miongoni mwa wanadamu kwa muda mrefu, baada ya kupitia na kushuhudia hali ya maisha mbalimbali ya watu, hali hii Aliyopitia kilikuwa kitabu Chake cha kiada cha kubadilisha lugha Yake ya kiungu kuwa lugha ya binadamu. Bila shaka, mambo haya Aliyoyaona na kuyasikia katika maisha yaliweza pia kumwimarisha Mwana wa Adamu kupitia yale Aliyopitia akiwa binadamu. Alipowataka watu waelewe ukweli fulani, ili kuwaelewesha mapenzi fulani ya Mungu, Angetumia mifano inayofanana na ile iliyotajwa hapo juu ili kuwaeleza watu kuhusu mapenzi ya Mungu na mahitaji Yake kwa binadamu. Mifano hii yote ilihusiana na maisha ya watu; hakukuwa na hata mmoja ambao haukuwa na mguso wa maisha ya binadamu. Bwana Yesu alipoishi na binadamu, Aliwaona wakulima wakilima mashamba yao; Alijua magugu yalikuwa nini na kutia chachu kulikuwa nini; Alielewa kwamba binadamu wanapenda hazina na hivyo basi Alitumia sitiari za hazina na hata lulu. Kwa mjibu wa Maisha mara kwa mara Aliwaona wavuvi wakizirusha nyavu zao na kadhalika; Bwana Yesu aliziona hizi na shughuli zingine zilizo na uhusiano na maisha ya wanadamu, Akipitia milo mitatu kwa siku ya binadana pia alipitia shughuli za kawaida za kila siku na kula mara tatu kwa siku. Aliweza kupitia kibinafsi maisha ya mtu wa kawaida na akashuhudia maisha ya wengine. Aliposhuhudia na kupitia haya yote binafsi, kile Alichofikiria kilikuwa si namna ya kuwa na maisha mazuri au namna ambavyo Angeishi kwa uhuru zaidi au kwa utulivu zaidi. Alipokuwa akipitia maisha halisi ya binadamu, Bwana Yesu aliuona ugumu katika maisha ya watu, Aliuona ugumu, ule ufukara, huzuni ya watu waliopotoshwa na Shetani, wakiishi katika utawala wa Shetani na walioishi katika dhambi. Huku akiyapitia maisha ya binadamu, Yeye binafsi aliweza pia kushuhudia namna ambavyo watu waliokuwa wakiishi ndani ya upotovu walivyokuwa wasioweza kujisaidia, na Akawaona kupitia ile hali duni ya wale walioishi katika dhambi, wale waliopotea katika mateso ya Shetani, ya mwovu. Bwana Yesu alipoyaona mambo haya, Aliyaona kwa macho Yake ya uungu au macho Yake ya ubinadamu? Ubinadamu Wake ulikuwepo kwa kweli—ulikuwepo waziwazi—Angeweza kuyapitia na kuyaona haya yote na bila shaka Aliyaona katika kiini Chake halisi, katika uungu Wake. Yaani, Kristo Mwenyewe, Bwana Yesu, binadamu Aliyaona haya na kila kitu Alichokiona kilimfanya kuhisi umuhimu na haja ya kazi Aliyokuwa Ameamua kuifanya wakati huu akiwa mwili. Hata ingawa Yeye Mwenyewe Alijua kwamba jukumu Alilohitaji kushughulikia Akiwa mwili lilikuwa kubwa mno, na namna ambavyo Angepitia maumivu ya kikatili, Alipomwona mwanadamu asiyejiweza ndani ya dhambi, Alipoona umaskini wa maisha yao na mapambano hafifu chini ya sheria, Alihuzunika zaidi na zaidi, na Akawa na hamu kubwa zaidi na zaidi ya kumwokoa binadamu kutoka dhambini. Haijalishi ni ugumu wa aina gani ambao Angepitia au ni aina gani ya maumivu Angehisi, Alikuja akawa na ushupavu zaidi na zaidi katika kuwakomboa wanadamu, ambaye alikuwa akiishi katika dhambi. Wakati wa mchakato huu, unaweza kusema kwamba Bwana Yesu alianza kuelewa waziwazi kazi Aliyohitajika kufanya na kile Alichokuwa Ameaminiwa kutekeleza. Alikuwa pia mwenye hamu kubwa zaidi ya kukamilisha kazi ambayo Alikuwa Aichukue—kushughulikia dhambi zote za mwanadamu, upatanisho wa Mungu na binadamu ili wasiishi tena katika dhambi naye Mungu Angeweza kusahau dhambi za binadamu kwa sababu ya sadaka ya dhambi, na hivyo basi kumruhusu kuendeleza kazi Yake ya kuwaokoa wanadamu. Yaweza kusemwa kwamba katika moyo wa Bwana Yesu, Alikuwa radhi kujitoa kwa ajili ya mwanadamu, kujitoa Mwenyewe. Alikuwa radhi pia kuchukua nafasi ya sadaka ya dhambi, kusulubishwa msalabani, na Alikuwa na hamu ya kukamilisha kazi hii. Alipoona hali za kusikitisha za maisha ya binadamu, Alitaka hata zaidi kukamilisha misheni Yake haraka iwezekanavyo, bila ya kuchelewa hata dakika au sekunde moja. Alipokuwa na hisia hii ya dharura, Alikuwa hafikirii namna ambavyo maumivu Yake binafsi yangekuwa wala hakufikiria kwa muda wowote zaidi kuhusu ni kiwango kipi cha udhalilishaji ambacho Angevumilia—Alishikilia azimio moja tu moyoni Mwake: Mradi tu Alijitoa Mwenyewe, mradi tu Angesulubishwa msalabani kama sadaka ya dhambi, mapenzi ya Mungu yangetendeka na Angeweza kuanza kazi mpya. Maisha ya wanadamu katika dhambi, hali yao ya kuwepo katika dhambi ingebadilika kabisa. Imani yake na kile Alichoamua kufanya vyote vilihusiana na kumwokoa binadamu, na Alikuwa na lengo moja tu: kufanya mapenzi ya Mungu ili Aweze kuanza kwa ufanisi hatua ambayo ingefuata katika kazi Yake. Haya ndiyo yaliyokuwa katika akili ya Bwana Yesu wakati huo.

Akiishi katika mwili, Mungu mwenye mwili Alimiliki ubinadamu wa kawaida; Alikuwa na hisia na kule kuwaza kwa mtu wa kawaida. Alijua furaha ilikuwa nini, maumivu yalikuwa nini na Alipowaona wanadamu katika hali hii ya maisha, Alihisi kwa kina kwamba kuwapatia watu kiasi cha mafunzo tu, kuwapatia kitu au kuwafunza kitu kusingewaongoza kutoka katika dhambi. Wala kuwafanya kutii amri pia kusingewakomboa kutoka katika dhambi—pale tu Alipozichukua dhambi za binadamu na kuwa mfano wa mwili wenye dhambi ndipo Alipoweza kuibadilisha na uhuru wa mwanadamu na kuibadilisha na msamaha wa Mungu kwa binadamu. Kwa hivyo baada ya Bwana Yesu kupitia na kushuhudia maisha ya binadamu katika dhambi, kulikuwa na tamanio kuu lililojionyesha katika moyo Wake—kuwaruhusu wanadamu kujiondoa kutoka katika maisha yao ya kupambana na dhambi. Tamanio hili lilimfanya kuhisi zaidi na zaidi kwamba lazima Aende katika msalaba na kuzichukua dhambi za binadamu haraka iwezekanavyo, kwa dharura. Hizi ndizo zilizokuwa fikira za Bwana Yesu wakati huo, baada ya Yeye kuishi na watu na kuwaona, kuwasikia, na kuhisi umaskini wa maisha yao ndani ya dhambi. Kwamba Mungu mwenye mwili Angekuwa na nia ya aina hii kwa mwanadamu, kwamba Angeweza kueleza na kufichua tabia ya aina hii—je, hili ni jambo ambalo mtu wa kawaida angekuwa nalo? Mtu wa kawaida angeona nini akiishi katika mazingira ya aina hii? Angefikiria nini? Kama mtu wa kawaida angekumbwa na haya yote, angeangalia matatizo haya kwa mtazamo wa juu? Bila shaka hapana! Ingawa kuonekana kwa Mungu mwenye mwili ni kama mwanadamu, Anajifunza maarifa ya mwanadamu na kuongea lugha ya mwanadamu, na wakati mwingine Anaonyesha hata mawazo Yake kwa jinsi na hisia za mwanadamu, namna Anavyowaona wanadamu, kiini cha vitu, na namna ambavyo watu waliopotoka wanavyomwona mwanadamu na kiini cha vitu kwa hakika si sawa kabisa. Mtazamo Wake na kimo Anachosimamia ni jambo ambalo halifikiwi na mtu aliyepotoka. Hii ni kwa sababu Mungu ni ukweli, mwili Anaouvalia unamiliki pia kiini cha Mungu, na fikira Zake na kile ambacho kinadhihirishwa na ubinadamu Wake pia ni ukweli. Kwa watu waliopotoka, kile Anachoeleza katika mwili ni matoleo ya ukweli na maisha. Matoleo haya si ya mtu mmoja tu lakini kwa wanadamu wote. Kwa mtu yeyote aliyepotoka, katika moyo wake kunao tu wale watu wachache ambao wanahusiana na yeye. Kunao tu hao watu kadhaa ambao anawatunza ambao anajali kuwahusu. Wakati janga linakaribia, anafikiria kwanza kuhusu watoto wake binafsi, mume au mke au wazazi, na mtu mwenye moyo wa kujitoa zaidi kuhusu mwanadamu angefikiria zaidi kuhusu baadhi ya watu wa ukoo au rafiki mzuri; je yeye huwafikiria wengine? La hasha! Kwa sababu binadamu ni, kwa hakika, binadamu, na wanaweza tu kuangalia kila kitu kutoka kwa mtazamo na kutoka katika kimo cha mtu. Hata hivyo, Mungu mwenye mwili ni tofauti kabisa na mtu aliyepotoka. Bila kujali ni vipi ambavyo mwili wa Mungu mwenye mwili ulivyo wa kawaida, ulivyo kama wengine, ulivyo wa chini, au hata namna ambavyo watu wanamdharau Yeye, fikira Zake na mwelekeo Wake kwa wanadamu ni mambo ambayo hakuna binadamu angeweza kufuatisha na wala hakuna binadamu angeweza kuiga. Siku zote Atawaangalia wanadamu kutoka kwa mtazamo wa uungu, kutoka katika kimo cha madaraka Yake kama Muumba. Siku zote Atawaona wanadamu kupitia katika kiini na akili ya Mungu. Hawezi kabisa kuwaona wanadamu kutoka katika kimo cha mtu wa kawaida na kutoka kwa mtazamo wa mtu aliyepotoka. Watu wanapowaangalia wanadamu, wanawaangalia kwa mtazamo wa binadamu, na wanatumia mambo kama vile maarifa ya binadamu na masharti na nadharia za binadamu kama kipimo. Hali hii imo ndani ya mawanda ya kile ambacho watu wanaweza kuona kwa macho yao; ni ndani ya upana ambao watu waliopotoka wanaweza kutimiza. Mungu anapowatazama wanadamu, Anawatazama kwa macho ya kiungu, na Anatumia kiini Chake na kile Alicho nacho na kile Alicho kama kipimo. Mawanda haya yanajumuisha mambo ambayo watu hawawezi kuona, na hapo ndipo Mungu mwenye mwili na wanadamu waliopotoka walivyo tofauti kabisa. Tofauti hii inaamuliwa na viini tofauti vya wanadamu na vya Mungu na ndivyo vinavyoamua utambulisho na nafasi zao pamoja na mtazamo na kimo ambacho wanaona mambo. Je, unaona udhihirisho na ufichuzi wa Mungu Mwenyewe ndani ya Bwana Yesu? Unaweza kusema kwamba kile ambacho Bwana Yesu alifanya na kusema kilihusiana na huduma Yake na kazi ya usimamizi ya Mungu binafsi, kwamba yote hayo yalikuwa ni udhihirisho na ufichuzi wa kiini cha Mungu. Ingawa Alikuwa na udhihirisho wa binadamu, kiini Chake cha kiungu na ufichuzi Wake wa kiungu hauwezi kukataliwa. Je, udhihirisho huu wa wanadamu ulikuwa udhihirisho wa kweli wa ubinadamu? Udhihirisho Wake wa ubinadamu ulikuwa, kwa kiini chake, tofauti kabisa na udhihirishaji wa ubinadamu wa watu waliopotoka. Bwana Yesu alikuwa Mungu mwenye mwili, na kama Angekuwa kweli mmojawapo wa wale wa kawaida, watu waliopotoka, Angeweza kuyaona maisha ya wanadamu ndani ya dhambi kutoka katika mtazamo wa kiungu? La hasha! Hii ndiyo tofauti kati ya Mwana wa Adamu na watu wa kawaida. Watu wote waliopotoka wanaishi ndani ya dhambi na wakati mtu yeyote anaiona dhambi, hana hisia zozote kuihusu hiyo dhambi; wako sawa tu, kama vile nguruwe anayeishi kwenye matope na hahisi chochote kamwe kuhusu kutokuwa na utulivu, au uchafu—anakula vizuri na kulala vizuri. Kama mtu anasafisha nyumba ya nguruwe, nguruwe kwa hakika hatahisi utulivu, na hatabakia akiwa msafi. Baada ya muda mfupi tu atakuwa tena akijigaragaza katika matope akiwa mtulivu kabisa, kwa sababu yeye ni kiumbe mchafu. Wakati binadamu wanapomwona nguruwe wanahisi kwamba anao uchafu na ukimsafisha yule nguruwe hahisi vyema zaidi—ndio maana hakuna anayemfuga nguruwe ndani ya nyumba yake. Namna ambavyo wanadamu wanavyomwona nguruwe itakuwa tofauti siku zote na namna ambavyo nguruwe wenyewe wanavyojihisi, kwa sababu wanadamu na nguruwe si wa aina moja. Na kwa sababu Mwana wa Adamu kwa mwili si wa aina moja na wanadamu waliopotoka, Mungu mwenye mwili tu ndiye Anayeweza kusimama kutoka kwa mtazamo wa kiungu, na kusimama kutoka katika kimo cha Mungu ili kuwaona wanadamu, ili kuona kila kitu.

Mungu anapokuwa mwili na kuishi miongoni mwa wanadamu, ni mateso yapi Anayopitia katika mwili? Yupo yeyote anayeelewa kwa kweli? Baadhi ya watu husema kwamba Mungu huteseka pakubwa, na ingawa Yeye ni Mungu Mwenyewe, watu hawaelewi kiini Chake na siku zote wanamchukulia Yeye kama mtu, hali ambayo humfanya Yeye kuhisi vibaya na kuona kwamba Amekosewa—wanasema kwamba mateso ya Mungu kwa kweli ni makubwa. Baadhi ya watu husema kwamba Mungu hana hatia na hana dhambi, lakini Yeye huteseka sawa na wanavyoteseka wanadamu, na Yeye hupitia mateso, matusi, na kuvunjiwa heshima pamoja na wanadamu; wanasema Yeye pia huvumilia kutoelewana na kutotiiwa na wafuasi Wake—kuteseka kwa Mungu kwa kweli hakuwezi kupimwa. Yamkini humwelewi Mungu kwa kweli. Kwa hakika, mateso haya unayoyaongelea hayaonekani kuwa mateso ya kweli kwake Mungu, kwa sababu kunayo mateso makubwa zaidi ya haya. Basi mateso ya kweli kwa Mungu Mwenyewe ni yapi? Mateso ya kweli ya mwili wa Mungu ni yapi? Kwa Mungu, wanadamu kutomwelewa Yeye haihesabiki kuwa ni mateso, na kwa watu kuwa kutokuwa na uelewano fulani wa Mungu na kwa kutomwona Yeye kama Mungu hakuhesabiki kuwa mateso. Hata hivyo, mara nyingi watu huhisi kwamba Mungu lazima alipitia dhuluma kubwa sana, kwamba wakati Mungu yumo katika mwili Hawezi kuionyesha nafsi Yake kwa wanadamu na kuwaruhusu kuuona ukubwa Wake, na Mungu anajificha kwa unyenyekevu katika mwili duni na hivyo basi hali hii lazima ilikuwa ya kumpa Yeye maumivu makali. Watu hushikilia moyoni kile wanachoweza kuelewa na kile wanachoweza kuona kuhusu mateso ya Mungu, na kuweka aina zote za huruma kwake Mungu na mara nyingi hata wataisifia kidogo hali hiyo. Kwa uhakika, kunayo tofauti, kuna pengo kati ya kile watu wanachoelewa, kile watu wanachoelewa kuhusu mateso ya Mungu na kile Anachohisi kwa kweli. Nakwambia ukweli—kwa Mungu haijalishi kama ni Roho wa Mungu au mwili wa Mungu, mateso hayo si mateso ya kweli. Basi ni nini hasa ambacho kwa kweli Mungu huteseka? Hebu tuzungumze kuhusu mateso ya Mungu kutoka katika mtazamo wa Mungu mwenye mwili pekee.

Wakati Mungu anapokuwa mwili, kugeuka ndani wa wastani, mtu wa kawaida akiishi miongoni mwa wanadamu, miongoni mwa watu, je, Hawezi kuona na kuhisi mbinu za watu, sheria na falsafa zao za kuishi? Ni vipi ambavyo mbinu na sheria hizi zinamfanya Yeye kuhisi? Je, Anahisi kuwa na chuki katika moyo Wake? Kwa nini Ahisi chuki? Mbinu na sheria za kuishi za wanadamu ni gani? Zimekita mizizi katika kanuni gani? Ziko katika msingi upi? Mbinu, sheria, n.k za kuishi kwa wanadamu, —zote hizi zimeundwa kwa misingi ya mantiki, maarifa na falsafa ya Shetani. Wanadamu wanaoishi chini ya aina hizi za sheria hawana ubinadamu, hawana ukweli—wote wanaukataa ukweli, na ni wakatili kwa Mungu. Tunapoangalia kiini cha Mungu, tunaona kwamba kiini Chake ni kinyume kabisa na mantiki, maarifa na falsafa ya Shetani. Kiini Chake kimejaa haki, ukweli, na utakatifu na uhalisi mwingine wa mambo yote mazuri. Mungu, akimiliki kiini hiki na Akiishi miongoni mwa wanadamu—Anahisi vipi katika moyo Wake? Je, haujajaa maumivu? Moyo Wake umo katika maumivu, na maumivu haya ni kitu ambacho hakuna mtu anayeweza kuelewa wala kutambua. Kwa sababu kila kitu Anachokumbana nacho, kukabiliana nacho, kusikia, kuona na kupitia vyote ni upotovu wa wanadamu, uovu, na uasi wao dhidi ya, na upinzani wa ukweli. Kila kitu kinachotoka kwa wanadamu ndicho chanzo cha mateso Yake. Hivi ni kusema kwa sababu kiini Chake halisi si sawa na wanadamu waliopotoka, kupotoka kwa wanadamu kunakuwa ndiko chanzo cha mateso Yake makuu. Wakati Mungu anapokuwa mwili, Anaweza kupata mtu anayetumia lugha moja na Yeye? Hili haliwezi kupatikana miongoni mwa wanadamu. Hakuna anayeweza kupatikana anayeweza kuwasiliana, anayeweza kuwa na mabadilishano haya na Mungu—unaweza kusema Mungu anayo hisia aina gani? Yale mambo ambayo watu huzungumza ambayo wanapenda, ambayo wanafuatilia na kutamani yote yanahusu dhambi, na yana mielekeo ya uovu. Wakati Mungu anapokabiliana na haya, haya si kama kisu katika moyo Wake? Akiwa Amekabiliwa na mambo haya, Anaweza kuwa na furaha katika moyo Wake? Anaweza kupata kitulizo? Wale wanaoishi na Yeye ni wanadamu waliojaa uasi na uovu—je, moyo Wake utakosaje kuteseka? Mateso haya kwa kweli ni makubwa vipi, na ni nani anayeyajali? Ni nani anayeyasikiliza? Na ni nani anayeweza kuyatambua? Watu hawana njia yoyote ya kuuelewa moyo wa Mungu. Mateso Yake ni kitu ambacho watu hawawezi hasa kutambua, na ubaridi, na kutojua kwa binadamu kunayafanya mateso ya Mungu kuwa yenye kina zaidi.

Kunao baadhi ya watu ambao huonea huruma hali ya Kristo kwa sababu kunao mstari katika Biblia unaosema: “Mbweha wana mashimo, na ndege wanavyo viota; lakini Mwana wa Adamu hana pahali pa kupumzisha kichwa chake.” Wakati watu wanaposikia haya, wanayatia moyoni na kuamini kwamba haya ndiyo mateso makubwa zaidi ambayo Mungu huvumilia, na mateso makubwa zaidi ambayo Kristo huvumilia. Sasa, tukiangalia katika mtazamo wa ukweli, hivyo ndivyo ilivyo? Mungu haamini kwamba ugumu huu ni mateso. Hajawahi kulia dhidi ya dhuluma hizi kwa ajili ya ugumu wa mwili, na hajawahi kuwalipizia kisasi wanadamu au Kujitoza na chochote. Hata hivyo, Anaposhuhudia kila kitu cha wanadamu, maisha yaliyopotoka na uovu wa wanadamu waliopotoka, Anaposhuhudia kwamba wanadamu wamo katika ung’amuzi wa Shetani na wamefungwa na Shetani na hawawezi kukwepa, kwamba wanaoishi ndani ya dhambi hawajui ukweli ni nini—Hawezi kuvumilia dhambi hizi zote. Chuki Yake kwa binadamu huongezeka siku baada ya siku, lakini lazima Avumilie yote haya. Haya ni mateso makuu ya Mungu. Mungu hawezi kujieleza kikamilifu hata sauti ya moyo Wake au hisia Zake miongoni mwa wafuasi Wake, na hakuna yeyote miongoni mwa wafuasi Wake anayeweza kuelewa kwa kweli mateso Yake. Hakuna yule ambaye hujaribu kuyaelewa au kuutuliza moyo Wake—moyo Wake huvumilia mateso haya siku baada ya siku, mwaka baada ya mwaka, mara kwa mara. Unaona nini katika yote haya? Mungu hahitaji chochote kutoka kwa wanadamu kama malipo kwa kile Alichokitoa, lakini kwa sababu ya kiini cha Mungu, Hawezi kuvumilia kamwe uovu, upotovu na dhambi ya wanadamu, lakini Anahisi chukizo na chuki kupindukia, hali ambayo husababisha moyo wa Mungu na mwili Wake kuvumilia mateso yasiyoisha. Je, ungeyaona yote haya? Kuna uwezekano, hakuna yeyote kati yenu ambaye angeyaona kwa sababu hakuna yeyote kati yenu anayeweza kumwelewa Mungu kwa kweli. Baada ya muda mnaweza kuyapitia haya wenyewe kwa utaratibu.

Halafu, hebu tuangalie vifungu vifuatavyo katika maandiko.

9. Yesu Atenda Miujiza

a. Yesu Awalisha Watu Elfu Tano

Yohana 6:8-13 Mmoja wa wanafunzi wake, Andrea, ndugu yake Simoni Petro, akasema kwake, Kuna mvulana hapa, aliye na mikate mitano ya shayiri nao samaki wawili wadogo: lakini ni yapi miongoni mwa watu wengi? Naye Yesu akasema, Wafanye watu waketi chini. Na kulikuwa na nyasi nyingi pahali hapo. Kwa hivyo wanaume wakaketi chini, wakiwa idadi ya takribani elfu tano. Naye Yesu akaichukua ile mikate, na baada ya kutoa shukrani, akagawanya kwa wanafunzi, na wanafunzi wakawapa wale waliokuwa wameketi chini; na vivyo hivyo wale samaki kadiri kiasi walichotaka. Baada ya kushiba, alisema kwa wanafunzi wake, Ninyi kusanyeni vipande ambavyo vimebaki, ndiyo chochote kisipotezwe. Kwa hivyo walivikusanya pamoja, na wakavijaza vikapu kumi na mbili na vipande vya mikate mitano ya shayiri vilivyobaki baada ya wale watu kula.

b. Kufufuka kwa Lazaro Kwampa Mungu Utukufu

Yohana 11:43-44 Na baada ya yeye kuzungumza, akasema kwa sauti kuu, Lazaro, kuja nje. Na yeye ambaye alikuwa amefariki akatoka nje, akiwa amefungwa mkono na mguu na sanda: na uso wake ulikuwa umefungwa kwa kitambaa. Yesu akasema kwao, Mfungueni yeye, na mwache aondoke.

Kati ya miujiza iliyotendwa na Bwana Yesu, tumechagua tu hii miwili kwa sababu inatosha kuwaonyesha kile ambacho Ningependa kuzungumzia hapa. Miujiza hii miwili inashangaza ajabu, na inawakilisha hasa miujiza ya Bwana Yesu katika Enzi ya Neema.

Kwanza, hebu tuangalie ufahamu wa kwanza: Yesu Awalisha Watu Elfu Tano.

Dhana ya “mikate mitano na samaki wawili” ni ya aina gani? Ni watu wangapi ambao mikate mitano na samaki wawili hulisha kwa kawaida? Mkipima kulingana na hamu ya kula ya mtu wa kawaida, inaweza kutosha tu watu wawili. Hii ndiyo dhana ya kimsingi kabisa ya mikate mitano na samaki wawili. Hata hivyo, imeandikwa katika dondoo hii kwamba mikate mitano na samaki wawili viliwalisha watu wangapi? Imerekodiwa katika Maandiko hivi: “Na kulikuwa na nyasi nyingi pahali hapo. Kwa hivyo wanaume wakaketi chini, wakiwa idadi ya takribani elfu tano.” Tukilinganisha na mikate mitano na samaki wawili, elfu tano ni idadi kubwa? Ni nini maana ya idadi hii kuwa kubwa sana? Kutoka kwa mtazamo wa binadamu, kugawanya mikate mitano na samaki wawili kati ya watu elfu tano haitawezekana, kwa sababu tofauti kati ya idadi hizi ni kubwa mno. Hata kama kila mtu angepata tu kipande kidogo cha kutafuna, bado mikate hiyo isingetosha watu hao elfu tano. Lakini hapa Bwana Yesu alitenda muujiza—Hakuruhusu watu elfu tano kula hadi wakashiba tu, ila kulikuwa na vyakula vilivyobaki. Maandiko yanasema: “Baada ya kushiba, alisema kwa wanafunzi wake, Ninyi kusanyeni vipande ambavyo vimebaki, ndiyo chochote kisipotezwe. Kwa hivyo walivikusanya pamoja, na wakavijaza vikapu kumi na mbili na vipande vya mikate mitano ya shayiri vilivyobaki baada ya wale watu kula.” Muujiza huu uliwaruhusu watu kutambua utambulisho na hadhi ya Bwana Yesu, na uliwaruhusu pia kuona kwamba hakuna kisichowezekana kwa Mungu—waliuona ukweli wa kudura ya Mungu. Mikate mitano na samaki wawili viliweza kutosha kuwalisha watu elfu tano lakini kama kusingekuwa na chakula chochote, Mungu angeweza kuwalisha watu hao elfu tano? Bila shaka Angeweza! Huu ulikuwa muujiza, hivyo basi bila shaka watu walihisi hali hii kutoeleweka na wakahisi kwamba haikuaminika na iliwashangaza lakini kwa Mungu kufanya kitu kama hicho halikuwa kitu. Kwa sababu hili lilikuwa jambo la kawaida kwa Mungu, kwa nini litengwe ili liweze kufasiriwa? Kwa sababu kile kilichomo nyuma ya muujiza huu kimebeba mapenzi ya Bwana Yesu, ambayo hayajawahi kugunduliwa na wanadamu.

Kwanza, hebu tujaribu kuelewa watu hawa elfu tano walikuwa wa aina gani. Walikuwa wafuasi wa Bwana Yesu? Kutoka kwa Maandiko, tunajua kwamba hawakuwa wafuasi Wake. Walijua Bwana Yesu alikuwa nani? Bila shaka hawakujua! Kwa kiwango cha chini sana, hawakujua yule mtu aliyekuwa amesimama mbele yao alikuwa Kristo, au pengine baadhi ya watu walijua tu jina Lake lilikuwa nani, na kujua kitu kumhusu Yeye au walikuwa wamesikia kitu kuhusu mambo aliyokuwa Amefanya. Walikuwa na mshawasha tu kuhusu Bwana Yesu kutoka katika hadithi, lakini bila shaka hamwezi kusema kwamba wao walimfuata Yeye, wala hata Kumwelewa. Bwana Yesu alipowaona watu hawa elfu tano, walikuwa na njaa na Angefikiria tu kuwalisha hadi washibe, na hivyo basi ilikuwa katika muktadha huu ndipo Bwana Yesu aliporidhisha matamanio yao. Baada ya kuyaridhisha matamanio yao, ni nini kilichokuwa moyoni Mwake? Mwelekeo Wake kwa watu hawa waliotaka tu kula hadi kushiba ulikuwa upi? Wakati huu, fikira na mwelekeo Wake Bwana Yesu lazima ungehusu tabia ya Mungu na hali Yake halisi. Kuwa mbele ya watu hawa elfu tano waliokuwa na njaa na ambao walitaka tu kula chakula hadi kushiba, kuwa mbele ya watu hawa waliojaa mshawasha na matumaini kumhusu, Bwana Yesu alifikiria tu kutumia muujiza huu ili kuwatolea neema. Hata hivyo, Hakujipa tumaini sana kwamba watakuwa wafuasi Wake, kwani Alijua walitaka kujiunga na furaha hiyo na kuweza kula hadi kushiba, hivyo basi Aliweza kutumia kwa njia bora zaidi kile Alichokuwa nacho hapo, na Akatumia mikate mitano na samaki wawili kuwalisha watu elfu tano. Aliwafumbua macho watu hawa waliofurahia burudani hiyo, waliotaka kuiona miujiza, na wakaona kwa macho yao mambo yale ambayo Mungu mwenye mwili Angeweza kukamilisha. Ingawa Bwana Yesu alitumia kitu kinachoweza kushikika ili kuridhisha mshawasha wao, tayari Alijua katika moyo Wake kwamba watu hawa elfu tano walitaka tu kuwa na mlo mzuri, hivyo basi Hakusema chochote kamwe au kuwahubiria kamwe—Aliwaacha tu kuuona muujiza ukifanyika. Bila shaka Asingeweza kuwashughulikia watu hawa kwa njia sawa ambayo aliwashughulikia wanafunzi Wake ambao walimfuata Yeye kwa kweli, lakini katika moyo wa Mungu, viumbe vyote vilikuwa katika utawala Wake, na Angeviruhusu viumbe vyote katika macho Yake kufurahia neema ya Mungu kila ilipohitajika. Hata ingawa watu hawa hawakujua Yeye alikuwa nani au kumwelewa, au kuwa na picha yoyote fulani kumhusu au kutoa shukrani Kwake hata baada ya kula mikate na samaki, hili halikuwa jambo ambalo Mungu Alijali kuhusu—Aliwapa watu hawa fursa nzuri ya kufurahia neema ya Mungu. Baadhi ya watu husema kwamba Mungu ana kanuni katika kile Anachofanya, na kwamba Hawaangalii wala kuwalinda wale wasioamini, na Yeye hasa hawaruhusu kufurahia neema Yake. Je, hivyo ndivyo ilivyo kwa hakika? Machoni mwa Mungu, mradi tu viwe ni viumbe vyenye uhai ambavyo Yeye Mwenyewe aliviumba, Ataweza kuvisimamia na kuvitunza; Atavitunza, Atavipangia, na Atavitawala katika njia tofauti. Hizi ndizo fikira na mtazamo wa Mungu kwa mambo yote.

Ingawa watu hawa elfu tano walioila mikate hiyo na samaki hawakupanga kumfuata Bwana Yesu, Hakuwa mkali kwao; baada ya wao kula hadi kushiba, je, mwajua kile Alichofanya Bwana Yesu? Je, Aliwahubiria chochote? Alienda wapi baada ya haya? Maandiko hayarekodi kwamba Bwana Yesu alisema chochote kwao; Alipokamilisha kutenda muujiza Wake Aliondoka kimya kimya. Hivyo basi Aliwawekea mahitaji yoyote watu hawa? Kulikuwa na chuki yoyote? Hakukuwepo na chochote kati ya hizi—Yeye hakutaka tu kutilia maanani akili yoyote kwa watu hawa ambao wasingeweza kumfuata, na kwa wakati huu moyo Wake ulikuwa katika maumivu. Kwa sababu alikuwa Ameuona upungufu wa wanadamu na Alikuwa amehisi namna ambavyo wanadamu walivyomkataa, na Alipowaona watu hawa au Alipokuwa na wao, upumbavu wa binadamu na kutojua kwao kulimfanya awe na huzuni sana na kukamwacha na maumivu katika moyo Wake, hivyo basi Alitaka tu kuwaacha watu hawa haraka iwezekanavyo. Bwana hakuwa na mahitaji yoyote kwao katika moyo Wake, Hakutaka kuwatilia maanani, Yeye hasa hakutaka kutumia nguvu Zake zozote kwao, na Alijua kwamba wasingeweza kumfuata—licha ya haya yote, mtazamo Wake kwao ulikuwa bado wazi kabisa. Alitaka tu kuwashughulikia kwa huruma, kuwarudishia neema—huu ndio uliokuwa mtazamo wa Mungu kwa kila kiumbe kilicho katika utawala Wake: kwa kila kiumbe, kishughulikie kwa huruma, watoshelezee mahitaji yao, wawaruzuku wao. Kwa sababu hasa ambayo Bwana Yesu alikuwa Mungu mwenye mwili, Aliweza kwa hali ya kimaumbile sana kufichua kiini cha Mungu binafsi na kuwashughulikia watu hawa kwa huruma. Aliwatendea kwa ukarimu na moyo wa rehema na uvumilivu. Haijalishi ni vipi watu hawa walimwona Bwana Yesu, na haikujalisha ni aina gani ya matokeo ambayo yangekuwepo, Alikitendea tu kila kiumbe kutokana na nafasi Yake kama Bwana wa uumbaji wote. Kile Alichofichua kilikuwa, bila kuachwa, tabia ya Mungu, na kile Alicho nacho na kile Alicho. Kwa hivyo Bwana Yesu alifanya kitu kimya kimya, kisha Akaondoka kimya kimya—hii ni sura gani ya tabia ya Mungu? Unaweza kusema kwamba hii ni rehema ya upendo wa Mungu? Unaweza kusema kwamba Mungu ni Mwenye kujitolea? Mtu wa kawaida anaweza kufanya hivi? Bila shaka hawezi! Katika kiini, wale watu elfu tano ambao Bwana Yesu aliwalisha kwa mikate mitano na samaki wawili walikuwa kina nani? Tunaweza kusema kwamba walikuwa watu waliolingana na Yeye? Unaweza kusema kwamba wote walikuwa wakatili kwa Mungu? Inaweza kusemekana kwa uhakika kwamba hawakuwa kabisa wanaolingana na Bwana, na kiini chao halisi kilikuwa kikatili kabisa kwa Mungu. Lakini Mungu aliwashughulikia vipi? Alitumia mbinu ya kuutuliza ukatili wa watu kwa Mungu—mbinu hii inaitwa “huruma.” Yaani, ingawa Bwana Yesu aliwaona kama watendaji dhambi, machoni mwa Mungu walikuwa hata hivyo uumbaji Wake hivyo basi bado aliwashughulikia watendaji dhambi hawa kwa huruma. Huu ndio uvumilivu wa Mungu, na uvumilivu huu unaamuliwa na utambulisho na kiini cha Mungu binafsi. Hivyo basi, hili ni jambo ambalo hakuna mwanadamu aliyeumbwa na Mungu anaweza kufanya—Mungu pekee ndiye anayeweza kufanya hivi.

Unapoweza kutambua kwa kweli fikira na mtazamo wa Mungu kwa wanadamu, wakati unapoweza kuelewa kwa kweli hisia na kujali kwa Mungu kwa kila kiumbe, utaweza kuelewa kule kujitolea na upendo unaotumika kwa kila mmoja wa watu walioumbwa na Muumba. Haya yanapofanyika, utatumia maneno mawili kufafanua upendo wa Mungu—maneno hayo mawili ni yapi? Baadhi ya watu husema “mwenye kujitolea” na baadhi ya watu wakasema “kuwa na huruma nyingi ya kutoa msaada.” Kati ya kauli hizi mbili, “kuwa na huruma nyingi ya kutoa msaada” ndiyo kauli ambayo inafaa kwa kiasi kidogo zaidi kuufafanua upendo wa Mungu. Hii ni kauli ambayo watu hutumia kufafanua fikira na hisia za mtu kwa upana wa akili zake. Naichukia kweli kauli hii kwa sababu inarejelea ule utoaji wa msaada bila mpango na bila ubaguzi, bila kujali kanuni zozote. Ni maelezo ya kihisia za ziada za watu wajinga na waliochanganyikiwa. Wakati neno hili linatumika kufafanua upendo wa Mungu, bila shaka kuna nia ya kumaanisha kukufuru. Nina maneno mawili ambayo yanafafanua kwa usahihi zaidi upendo wa Mungu—maneno hayo mawili ni yapi? Neno la kwanza ni “kubwa.” Je, si neno hili huamsha na kuleta hisia? Neno la pili ni “pana.” Kunayo maana halisi katika maneno haya mawili mbili Ninazotumia katika kufafanua upendo wa Mungu. Kama yatachukuliwa kwa njia ya moja kwa moja, “kubwa” linafafanua ukubwa au wingi wa kitu, lakini haijalishi kitu hicho kina ukubwa gani—ni kitu ambacho watu wanaweza kugusa na kuona. Hii ni kwa sababu kipo, si kifaa cha kidhahania na kinapatia watu hisia kwamba kwa kiasi fulani kina usahihi na hali ya kimatendo. Haijalishi kama unakiangalia kutoka katika mtazamo bapa au wa pande zote tatu; huhitajiki kufikiria uwepo wake, kwa sababu ni kitu ambacho kwa kweli kipo. Hata ingawa kwa kutumia “kubwa sana” kufafanua upendo wa Mungu kunaweza kuhisiwa kana kwamba tunataka kupima wingi wa upendo Wake, lakini hata hivyo linatoa hisia kwamba hauwezi kupimwa. Nasema kwamba upendo wa Mungu unaweza kupimwa kwa sababu upendo Wake si aina fulani ya kitu kisichojulikana, wala hauchipuki tu kutoka kwa ngano yoyote. Badala yake, ni kitu cha kutumiwa kwa pamoja na vitu vyote katika utawala wa Mungu, na ni kitu cha kufurahiwa na viumbe vyote hadi kwa viwango tofauti na kutoka katika mitazamo tofauti. Ingawa watu hawawezi kukiona au kukigusa, upendo huu huleta maendelezo na maisha katika vitu vyote kwani kinafichuliwa hatua kwa hatua katika maisha yao, na wanahesabu na kushuhudia upendo wa Mungu wanaofurahia kila wakati. Nasema kwamba upendo wa Mungu hauwezi kuhesabiwa kwa sababu fumbo la Mungu la Yeye kukidhi na kuimarisha vitu vyote ni kitu ambacho ni kigumu kwa wanadamu kuelewa, kama vile tu zilivyo fikira za Mungu katika vitu vyote na hasa vile vya mwanadamu. Hivyo ni kusema hakuna anayejua damu na machozi ambayo Muumba ametoa kwa sababu ya wanadamu. Hakuna anayeweza kufahamu, hakuna anayeweza kuelewa kina au uzito wa upendo ambao Muumba anao kwa ajili ya wanadamu, aliowaumba kwa mikono Yake binafsi. Kufafanua upendo wa Mungu kama mkubwa sana ni kuwasaidia watu kutambua na kuelewa upana wake na ukweli wa uwepo wake. Iko hivyo ili watu waweze kufahamu kwa kina zaidi maana halisi ya neno “Muumba,” na ili watu waweze kupata ufahamu wa kina zaidi wa maana ya “uumbaji.” Neno “pana” kwa kawaida huwa linafafanua nini? Linatumika kwa ujumla kumaanisha bahari au ulimwengu kama vile ulimwengu mpana au bahari pana. Ule mtanuko na kina kitulivu cha ulimwengu unazidi ufahamu wa binadamu na ni kitu ambacho kinanata fikra za binadamu, ambacho kwacho wamejawa na upendezwaji. Fumbo lake na umuhimu wake vyote vimo katika uwezo wa kuonekana lakini haviwezi kufikika. Unapofikiria kuhusu bahari, unafikiria kuhusu upana wake—yaonekana isiyo na mipaka, na unaweza kuhisi ile hali ya bahari hiyo kuwa fumbo na ujumuishwaji wake pia. Ndiyo maana Nimetumia neno “pana” kufafanua upendo wa Mungu. Ni kuwasaidia watu wahisi namna neno hilo lilivyo na thamani, na ili wahisi ule urembo wa kipekee wa upendo Wake, na kwamba nguvu za upendo wa Mungu haziishi na zimeenea. Ni kwa minajili ya kuwasaidia kuhisi utakatifu wa upendo Wake, na heshima pamoja na hali ya kutoweza kukosewa ya Mungu ambayo inafichuliwa kupitia upendo Wake. Sasa unafikiri kwamba “pana” ni neno linalofaa kufafanua upendo wa Mungu? Je, upendo wa Mungu unaweza kufikia maana ya maneno haya mawili, “kubwa sana” na “pana”? Bila shaka! Katika lugha ya binadamu, maneno haya mawili tu ndiyo ambayo yanafaa kwa kiasi fulani, na kwa kiasi fulani yanakaribia kuufafanua upendo wa Mungu. Je, huoni hivyo? Kama Ningewaulizeni kuufafanua upendo wa Mungu, je, mngetumia kauli hizi mbili? Kuna uwezekano mkubwa zaidi, msingeyatumia kwa sababu ufahamu na utambuzi wenu wa upendo wa Mungu ni finyu na unafikia tu mtazamo bapa, na bado haujakwea ngazi hadi katika ule urefu wa nafasi ya pande zote tatu. Hivyo basi kama Ningetaka mfafanue upendo wa Mungu, mngehisi kwamba mnakosa maneno; huenda pengine hata mtakosa kuongea kabisa. Maneno haya mawili ambayo Nimeyazungumzia leo yanaweza kuwa magumu kwako kuelewa, au pengine kwa ufupi tu hukubali. Hali hii inaweza kuongelea tu hoja kwamba utambuzi na ufahamu wako wa upendo wa Mungu ni wa juujuu na ndani ya upana mwembamba. Nimesema awali kwamba Mungu ni mwenye kujitolea—unakumbuka neno kujitolea? Inaweza kusemekana kwamba upendo wa Mungu unaweza kufafanuliwa tu kuwa wa kujitolea? Je, si haya si mawanda membamba mno? Mnafaa kutafakari suala hili zaidi ili kuweza kufaidika kutoka kwalo.

Yale yaliyotajwa hapo juu ndiyo yale tuliyoyaona ya tabia ya Mungu na kiini Chake kutoka katika muujiza wa kwanza. Hata ingawa ni hadithi ambayo watu wameisoma kwa maelfu kadhaa ya miaka, inao mtiririko mwepesi, na inaruhusu watu kuweza kuona suala la pekee, ilhali katika mtiririko huu mwepesi tunaweza kuona kitu chenye thamani zaidi, hali ambayo ni tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho. Mambo haya kuwa Alicho nacho na kile Alicho yanamwakilisha Mungu Mwenyewe, na ni maelezo ya fikira za Mungu binafsi. Wakati Mungu anapoonyesha fikira Zake, ni udhihirisho wa sauti ya moyo Wake. Anatumai kwamba kutakuwa na watu wanaoweza kumwelewa Yeye, kumjua Yeye na wanafahamu mapenzi Yake, na Anatumai kutakuwa na watu wanaoweza kuisikia sauti ya moyo Wake na wataweza kushirikiana kwa bidii ili kuridhisha mapenzi Yake. Na vitu hivi ambavyo Bwana Yesu alifanya vilikuwa ni maelezo ya kimya ya Mungu.

Halafu, hebu tuuangalie dondoo hii: Kufufuka kwa Lazaro Kwatukuza Mungu.

Mnayo picha gani baada ya kusoma dondoo hii? Umuhimu wa muujiza huu ambao Bwana Yesu alitenda ulikuwa mkubwa zaidi kuliko ule wa awali kwa sababu hakuna muujiza ambao unajitokeza zaidi kuliko ule wa kufufua binadamu aliyekufa na kutoka katika kaburi. Bwana Yesu kufanya kitu kama hiki kulikuwa na umuhimu mkubwa mno katika enzi hiyo. Kwa sababu Mungu alikuwa mwili, watu waliweza kuona tu kuonekana Kwake kwa kimwili, upande Wake wa kimatendo, na upande Wake usio na umuhimu. Hata kama baadhi ya watu waliona na kuelewa hulka Yake fulani au nguvu Zake ambazo alionekana kuwa nazo, hakuna aliyejua pale ambapo Bwana Yesu alipotokea, ambaye kiini Chake cha kweli kilikuwa, na nini kingine zaidi ambacho Angeweza kufanya. Haya yote hayakujulikana kwa mwanadamu. Watu wengi mno walitaka ithibati ya kitu hiki, na kuujua ukweli. Je, Mungu angeweza kufanya kitu ili kuthibitisha utambulisho Wake Mwenyewe? Kwa Mungu, huu ulikuwa upepo mwanana—lilikuwa jambo rahisi sana. Angefanya kitu popote, wakati wowote ili kuthibitisha utambulisho na kiini Chake, lakini Mungu alikuwa na njia Yake ya kufanya mambo—kwa mpango, na kwa hatua. Hakufanya vitu bila mpangilio; Alitafuta muda unaofaa, na fursa inayofaa kufanya kitu chenye maana zaidi kwa wanadamu kuweza kuona. Hili lilithibitisha mamlaka Yake na utambulisho Wake. Hivyo basi, kufufuka kwa Lazaro kungeweza kuthibitisha utambulisho wa Bwana Yesu? Hebu tuangalie kifungu hiki cha maandiko: “Na baada ya yeye kuzungumza, akasema kwa sauti kuu, Lazaro, kuja nje. Na yeye ambaye alikuwa amefariki akatoka nje….” Wakati Bwana Yesu alipofanya haya, Alisema tu jambo moja: “Lazaro, kuja nje.” Kisha Lazaro akatoka nje ya kaburi—hii ilikamilika kwa sababu ya mstari mmoja uliotamkwa na Bwana. Katika wakati huu, Bwana Yesu hakuweza kuandaa madhabahu, na Hakutekeleza hatua zote nyingine. Alisema tu jambo moja. Hili linaweza kutaitwa muujiza au amri? Au lilikuwa aina fulani wa uchawi? Kwa juujuu, yaonekana ingeweza kuitwa muujiza, na ukiangalia hali hiyo kutoka mtazamo wa kisasa, bila shaka mnaweza bado kuliita muujiza. Hata hivyo, bila shaka hali hiyo isingeweza kuitwa apizo la kuiita nafsi kurudi kutoka kwa wafu, na bila shaka si uchawi. Ni sahihi kusema kwamba muujiza huu ulikuwa ni onyesho la kawaida zaidi, dogo ajabu la mamlaka ya Muumba. Haya ndiyo mamlaka, na uwezo wa Mungu. Mungu ana mamlaka ya kumwacha mtu afe, kuruhusu nafsi yake iondoke mwilini mwake na kurudi kuzimu au popote pale itakapoenda. Mtu anapokufa, na anakokwenda baada ya kifo—haya yanaamuliwa na Mungu. Yeye anaweza kufanya haya wakati wowote na mahali popote. Yeye hazuiliwi na binadamu, matukio, vifaa, nafasi au mahali. Akitaka kulifanya Anaweza kulifanya, kwa sababu vitu vyote na viumbe vyenye uhai vinatawaliwa na Yeye, na vitu vyote vinaongezeka, vinaishi na kuangamia kwa neno Lake na mamlaka Yake. Anaweza kumfufua binadamu aliyekufa, na pia hiki ni kitu Anachoweza kufanya wakati wowote mahali popote. Haya ndiyo mamlaka ambayo Muumbaji pekee humiliki.

Bwana Yesu alipofanya kitu kama vile kumleta Lazaro kutoka kwa wafu, lengo Lake lilikuwa ni kutoa ithibati kwa wanadamu na Shetani aweze kuona, na kuacha wanadamu na Shetani kujua kwamba kila kitu cha wanadamu, maisha na kifo cha wanadamu vyote vinaamuliwa na Mungu, na kwamba ingawa Alikuwa amekuwa mwili ilivyo kama siku zote, Alibaki katika mamlaka juu ya ulimwengu wa kimwili unaoweza kuonekana pamoja na ulimwengu wa kiroho ambao wanadamu hawawezi kuuona. Huku kulikuwa kuwaruhusu wanadamu na Shetani kujua kwamba kila kitu cha wanadamu hakiko katika amri ya Shetani. Huu ulikuwa ni ufunuo na onyesho la mamlaka ya Mungu, na ilikuwa pia njia ya Mungu kuutuma ujumbe wake kwa viumbe vyote kwamba maisha na kifo cha wanadamu kimo mikononi mwa Mungu. Bwana Yesu kumfufua Lazaro—kutenda kwa aina hii ni mojawapo ya njia za Muumba za kumfunza na kumwelekeza wanadamu. Ilikuwa ni hatua thabiti ambapo Aliutumia uwezo Wake na mamlaka Yake kuwaelekeza wanadamu, na kuwatolea wanadamu. Ilikuwa njia bila matumizi ya maneno kwa Muumba ya kuwaruhusu wanadamu kuweza kuuona ukweli wa Yeye kuwa na mamlaka juu ya viumbe vyote. Ilikuwa njia Yake ya kuwaambia binadamu kupitia kwa hatua za kimatendo kwamba hamna wokovu mbali na kupitia Yeye. Mbinu za aina hii za kimya za Yeye kuwaelekeza wanadamu zinadumu milele—hazifutiki, na iliweza kuleta katika mioyo ya wanadamu mshtuko na kupatikana kwa nuru ambayo haiwezi kufifia. Kufufuliwa kwa Lazaro kulimtukuza Mungu—hali hii inayo athari ya kina katika kila mojawapo wa wafuasi wa Mungu. Inakita mizizi kwa kila mmoja anayeelewa kwa kina tukio hili, ufahamu, maono kwamba ni Mungu tu anayeweza kuamuru maisha na kifo cha wanadamu. Ingawa Mungu ana aina hii ya mamlaka, na ingawa Aliutuma ujumbe kuhusu uhuru Wake dhidi ya maisha na kifo cha wanadamu kupitia kwa kufufuka kwa Lazaro, hii haikuwa kazi Yake ya msingi. Mungu katu hafanyi kitu bila maana. Kila kitu Anachofanya kina thamani kuu na kito kupita ndani ya ghala la hazina. Bila shaka Yeye hangefanya “kuwa na mtu kutoka katika kaburi lake” kuwa sababu ya kimsingi au lengo au sababu kuu katika kazi Yake. Mungu hafanyi chochote ambacho hakina maana. Kufufuka kumoja kwa Lazaro kunatosha kuonyesha mamlaka ya Mungu. Kunatosha kuthibitisha utambulisho wa Bwana Yesu. Hii ndiyo sababu Bwana Yesu hakurudia aina hii ya muujiza. Mungu hufanya mambo kulingana na kanuni Zake binafsi. Katika lugha ya binadamu, ingekuwa kwamba Mungu anajali kazi muhimu. Yaani, wakati Mungu anapofanya mambo Hapotoki kutoka kwenye kusudio Lake la kazi. Anajua ni kazi gani Anayotaka kutekeleza katika awamu hii, kile Anachotaka kukamilisha, na Atafanya kazi mahususi kulingana na mpango Wake. Kama mtu aliyepotoka angekuwa na aina hiyo ya uwezo, angekuwa akifikiria tu kuhusu njia za kufichua uwezo wake ili wengine wajue namna alivyokuwa thabiti, hivyo basi kumwinamia, ili aweze kuwadhibiti na kuwameza. Huu ndio uovu unaotoka kwa Shetani—huu unaitwa upotovu. Mungu hana tabia kama hiyo, na Hana kiini kama hicho. Kusudio Lake katika kufanya mambo si kujionyesha Mwenyewe, lakini kuwapa wanadamu ufunuo na mwongozo zaidi, ili watu waweze kuiona mifano michache katika Biblia kuhusu aina hii ya jambo. Hii haimaanishi kwamba uwezo wa Bwana Yesu ulikuwa finyu, au kwamba asingeweza kufanya jambo la aina hiyo. Ni kwamba Mungu hakutaka tu kulifanya jambo hilo, kwa sababu Bwana Yesu kumfufua Lazaro kulikuwa na umuhimu wa kimatendo kabisa, na pia kwa sababu kazi kuu ya Mungu kuwa mwili haikuwa ni kutenda miujiza, haikuwa ni kuwaleta watu kutoka katika kifo, lakini ilikuwa ni kazi ya ukombozi wa wanadamu. Hivyo basi, wingi wa kazi ambayo Bwana Yesu alikamilisha ilikuwa ni kuwafunza watu, kuwatoshelezea haja zao, na kuwasaidia, na mambo kama vile kumfufua Lazaro yalikuwa tu mambo madogo ya huduma ambayo Bwana Yesu alitekeleza. Hata zaidi, mnaweza kusema kwamba “kujionyesha” si sehemu ya kiini cha Mungu, hivyo basi kutoonyesha miujiza zaidi hakukuwa kujizuia kimakusudi, wala hakukuwa kwa sababu ya vizuizi vya kimazingira, na bila shaka hakukuwa kwa sababu ya ukosefu wa uwezo.

Bwana Yesu alipomleta Lazaro kutoka kwa wafu, Alitumia mstari mmoja: “Lazaro, kuja nje.” Hakusema kitu kingine mbali na hiki—maneno haya yanawakilisha nini? Yanawakilisha hoja kwamba Mungu anaweza kukamilisha chochote kupitia maongezi, kukiwemo kumfufua mtu aliyekufa. Mungu alipoumba viumbe vyote, Alipouumba ulimwengu, Alifanya hivyo kwa maneno—amri za kutamkwa, maneno yaliyotamkwa kwa mamlaka, na hivyo tu viumbe vyote viliumbwa. Yalikamilishwa hivyo. Mstari huu mmoja uliozungumzwa na Bwana Yesu ulikuwa sawa na maneno yaliyotamkwa na Mungu alipoziumba mbingu na dunia na viumbe vyote; mstari huo pia uliweza kushikilia mamlaka ya Mungu, uwezo wa Muumba. Viumbe vyote viliumbwa na vikasimama kwa sababu ya matamshi kutoka kwa kinywa cha Mungu, na vivyo hivyo, Lazaro alitembea kutoka katika kaburi lake kwa sababu ya matamshi kutoka katika kinywa cha Bwana Yesu. Haya ndiyo yaliyokuwa mamlaka ya Mungu, yaliyoonyeshwa na kutambuliwa katika mwili Wake. Aina hii ya mamlaka na uwezo vilimilikiwa na Muumba, na kwa Mwana wa Adamu ambaye kwake Muumba alitambuliwa. Huu ndio ufahamu uliofunzwa kwa mwanadamu kwa Mungu kumleta Lazaro kutoka kwa wafu. Hayo ndiyo yote katika mada hii. Halafu, hebu tuyasome maandiko.

10. Hukumu ya Mafarisayo kwa Yesu

Marko 3:21-22 Na wakati marafiki zake walisikia kuhusu hilo, walitoka kumshika: kwani walisema, Yeye si wa akili sawa. Nao waandishi waliokuja kutoka Yerusalemu walisema, Ana Beelzebubi, na kupitia mwana wa mfalme wa mapepo huwaondoa mapepo.

11. Mafarisayo Kukemewa na Yesu

Mat 12:31-32 Ndiyo sababu nawaambieni, Wanadamu watasamehewa kila namna ya dhambi na kukufuru: lakini wanadamu hawatasamehewa kukufuru dhidi ya Roho Mtakatifu. Na yeyote ambaye atasema neno dhidi ya Mwana wa Adamu atasamehewa: ila yeyote ambaye atasema dhidi ya Roho Mtakatifu, hatasamehewa, wala katika dunia hii, wala katika dunia itakayokuja.

Mat 23:13-15 Lakini ole wenu nyinyi, waandishi na Mafarisayo, mlio wanafiki! Kwa maana mnafunga ufalme wa mbinguni wasiingie wanadamu: kwani ninyi hamwingii wenyewe, wala hamkubali wanaoingia ndani waingie. Ole wenu nyinyi, waandishi na Mafarisayo, mlio wanafiki! Kwani mnazila nyumba za wanawake wajane, na mnatoa sala ndefu kwa kujifanya: kwa hivyo mtapokea laana kubwa zaidi. Ole wenu nyinyi, waandishi na Mafarisayo, mlio wanafiki! Kwa maana mnazingira bahari na ardhi kwa ajili ya kumfanya mtu kubadili imani, na anapobadili, mnamfanya awe mwana wa kuzimu mara dufu zaidi kuwaliko.

Kunazo dondoo mbili tofauti hapo juu—hebu kwanza tuangalie dondoo ya kwanza: Hukumu ya Mafarisayo kwa Yesu.

Katika Biblia, tathmini ya Mafarisayo kwa Yesu Mwenyewe na mambo alioyafanya ilikuwa: “walisema, Yeye si wa akili sawa. … Ana Beelzebubi, na kupitia mwana wa mfalme wa mapepo huwaondoa mapepo” (Marko 3:21-22). Hukumu ya waandishi na Mafarisayo kwa Bwana Yesu haikuwa ikiiga mambo au ikifikiria tu kutoka popote—ilikuwa hitimisho yao kuhusu Bwana Yesu kutokana na yale walioyaona na kuyasikia kuhusu vitendo Vyake. Ingawa hitimisho yao ilitolewa kwa njia isiyo ya kweli au ya uongo kwa jina la haki, na kuonekana mbele ya watu ni kana kwamba ilikuwa imeshughulikiwa vyema, kiburi ambacho walitumia kumhukumu Bwana Yesu kilikuwa kigumu hata kwa wao wenyewe kuvumilia. Nguvu zao mchafukoge za chuki yao kwa Bwana Yesu ziliweza kufichua maono yao binafsi yasiyo na mipaka na sura zao za kishetani na uovu, pamoja na maumbile yao yenye nia mbaya ya kumpinga Mungu. Mambo haya waliyoyasema katika hukumu yao kwa Bwana Yesu yaliendeshwa na maono yao yasiyo na misingi, ya wivu, na hali ya ubovu na ubaya na ukatili wao dhidi ya Mungu na ukweli. Hawakuchunguza chanzo cha hatua za Bwana Yesu wala kuchunguza kiini cha kile Alichosema au kufanya. Badala yake, walimshambulia bila mpango, bila subira, kwa njia za kishenzi, na kwa makusudi ya kijicho pamoja na kutupilia mbali kile Alichokuwa Amefanya. Hii ilikuwa hadi kufikia kiwango cha kutupilia mbali Roho Wake bila kubagua, Yaani, Roho Mtakatifu, Roho wa Mungu. Hivi ndivyo waliyomaanisha waliposema “Amerukwa na akili,” “Beelzebuli,” na “mkuu wa pepo.” Hii ni kusema kwamba walisema Roho wa Mungu alikuwa Beelzebuli na pia mkuu wa pepo. Waliweza kupatia sifa ya kazi ambayo Roho wa Mungu mwenye mwili alikuwa amevalia kama kurukwa akili. Hawakukufuru tu Roho wa Mungu kama Beelzebuli na mkuu wa pepo, lakini waliishutumu kazi ya Mungu. Walimshutumu na kumkufuru Bwana Yesu Kristo. Kiini cha upingaji wao na kukufuru Mungu kilikuwa sawa kabisa na kiini cha Shetani na upingaji wa Shetani na kumkufuru Mungu. Wao hawakuwakilisha wanadamu waliopotoka tu, lakini hata zaidi walikuwa mfano halisi wa Shetani. Walikuwa ni njia ya Shetani kutumia miongoni mwa wanadamu, na walikuwa washiriki na watumishi wa Shetani. Kiini cha kukufuru kwao na utovu wao wa nidhamu kwa Bwana Yesu Kristo ndicho kilichokuwa mapambano yao na Mungu kwa ajili ya hadhi, mashindano yao na Mungu, na mapambano yao na Mungu yasiyoisha. Kiini cha upingaji wao kwa Mungu na mwelekeo wao wa ukatili kwake Yeye, pamoja na maneno yao na fikira zao moja kwa moja vilimkufuru na kumghadhabisha Roho wa Mungu. Hivyo basi, Mungu aliamua hukumu inayofaa ya na yale waliyoyasema na kufanya, na akaamua matendo yao kuwa dhambi ya kukufuru dhidi ya Roho Mtakatifu. Dhambi hii haiwezi kusameheka ulimwenguni humu na hata ulimwengu unaokuja, kama vile tu maandiko yafuatayo yanasema: “Wanadamu hawatasamehewa kukufuru dhidi ya Roho Mtakatifu” na “Yeyote ambaye atasema dhidi ya Roho Mtakatifu, hatasamehewa, wala katika dunia hii, wala katika dunia itakayokuja.” Leo, hebu tuzungumzie maana halisi ya maneno haya kutoka kwa Mungu “hatasamehewa, wala katika dunia hii, wala katika dunia itakayokuja.” Hii ni, acha tuweke wazi namna ambavyo Mungu hukamilisha matamshi yake: “haitasamehewa, wala katika dunia hii, wala katika dunia itakayokuja.”

Kila kitu ambacho tumezungumzia kuhusu yote haya kinahusiana na tabia ya Mungu, na mweleko Wake kwa watu, masuala na mambo, na mambo. Kikawaida, dondoo hizo mbili hapo juu haziwezi kuachwa. Je, mlitambua chochote katika dondoo hizi mbili za maandiko? Baadhi ya watu husema wanaiona ghadhabu ya Mungu. Baadhi ya watu husema wanauona upande wa tabia ya Mungu ambao hauvumilii kosa la wanadamu, na kwamba watu wakifanya kitu ambacho kinamkufuru Mungu, hawatapata msamaha Wake. Licha ya ukweli kwamba watu wanaona na kutambua ghadhabu na kutovumilia makosa ya wanadamu kwa Mungu katika vifungu hivi viwili, bado hawaelewi kwa kweli mtazamo Wake. Dondoo hizi mbili zinao ufafanuzi wa mwelekeo na mtazamo wa kweli wa Mungu kwa wale wanaomkufuru na kumghadhabisha Yeye. Dondoo hii katika maandiko inashikilia maana halisi ya mwelekeo na mtazamo Wake: “Yeyote ambaye atasema dhidi ya Roho Mtakatifu, hatasamehewa, wala katika dunia hii, wala katika dunia itakayokuja.” Watu wanapomkufuru Mungu, wakati wanapomghadhabisha Yeye, Yeye hutoa hukumu, na hukumu hii ndiyo matokeo yaliyotolewa na Yeye. Hali hii inafafanuliwa hivi katika Biblia: “Ndiyo sababu nawaambieni, Wanadamu watasamehewa kila namna ya dhambi na kukufuru: lakini wanadamu hawatasamehewa kukufuru dhidi ya Roho Mtakatifu” (Mat 12:31), na “Lakini ole wenu nyinyi, waandishi na Mafarisayo, mlio wanafiki!” (Mat 23:13). Hata hivyo, imerekodiwa katika Biblia matokeo yapi yalikuwepo kwa wale waandishi na Mafarisayo, pamoja na wale watu waliosema Alikuwa amerukwa na akili baada ya Bwana Yesu kuyasema mambo hayo? Je, imerekodiwa kama walipata adhabu yoyote? Kuna uhakika kwamba hakukuwa na adhabu: Kusema hapa kwamba “hakukuwa” si kwamba haikurekodiwa, lakini kwa hakika hakukuwa na matokeo yoyote ambayo yangeonekana kwa macho ya binadamu. Neno hili “hakukuwa” linaelezea suala, yaani, mwelekeo na kanuni za Mungu katika kushughulikia mambo fulani. Namna ambavyo Mungu anawatendea watu wanaomkufuru au hata wanaompinga, au hata wale wanaomkashifu—watu wanaomshambulia kimakusudi, kumkashifu, na kumlaani—hajifanyi kwamba kila kitu kiko sawa. Anao mwelekeo wazi kwa hawa. Anawadharau watu hawa, na moyoni Mwake anawashutumu. Anatangaza waziwazi hata matokeo kwa ajili yao, ili watu waweze kujua kwamba Anao mwelekeo wazi kwao wanaomkufuru Yeye, na ili wajue namna atakavyoamua matokeo yao. Hata hivyo, baada ya Mungu kusema mambo haya, watu bado wangeona kwa nadra ukweli wa namna ambavyo Mungu angeshughulikia watu hao, na wasingeelewa kanuni zinazotawala matokeo ya Mungu, hukumu Yake kwao. Hiyo ni kusema, wanadamu hawawezi kuuona mwelekeo na mbinu fulani za Mungu katika kuwashughulikia. Hali hii inahusu kanuni za Mungu za kufanya mambo. Mungu hutumia ujio wa hoja katika kushughulikia tabia yenye uovu ya baadhi ya watu. Yaani, Hatangazi dhambi yao na haamui matokeo yao, lakini Anatumia moja kwa moja ujio wa hoja ili kuwaruhusu kuadhibiwa, wao kupata adhabu wanayostahili. Wakati hoja hizi zinapofanyika, ni miili ya watu inayoteseka kwa adhabu; hili ni jambo ambalo linaweza kuonekana kwa macho ya binadamu. Wakati wa kushughulikia tabia ya uovu kwa baadhi ya watu, Mungu huwalaani tu kwa matamshi, lakini wakati uo huo, ghadhabu ya Mungu huwapata, na adhabu wanayopokea inaweza kuwa jambo ambalo watu hawalioni, lakini aina hii ya matokeo inaweza kuwa hata mbaya zaidi kuliko matokeo ambayo watu wanaweza kuona ya kuadhibiwa au kuuawa. Hii ni kwa sababu katika hali zile ambazo Mungu ameamua kutomwokoa mtu wa aina hii, kutoonyesha tena rehema au uvumilivu kwao, kutowapa fursa zaidi, mwelekeo Anaouchukua kwao ni kuwaweka pembeni. Ni nini maana ya “kuweka pembeni”? Maana ya kauli hii kibinafsi ni kuweka kitu kwa upande mmoja, kutokizingatia tena. Lakini hapa, wakati Mungu “anapomweka mtu pembeni,” kuna fafanuzi mbili tofauti kuhusu kile Alicho: Ufafanuzi wa kwanza ni kwamba Amempa Shetani kuyashughulikia maisha ya mtu huyo, na kila kitu cha mtu huyo. Mungu hatamwajibikia tena na Hataweza kumsimamia tena. Kama mtu huyo amerukwa na akili, au ni mpumbavu, na kama katika maisha au kifo, au kama angeshushwa jahanamu ili kupata adhabu yake, hayo yote yasingemhusu Mungu. Hiyo ingemaanisha kwamba kiumbe hicho hakitakuwa na uhusiano wowote na Muumba. Ufafanuzi wa pili ni kwamba Mungu ameamua kwamba Yeye Mwenyewe anataka kufanya kitu na mtu huyu, kwa mikono Yake mwenyewe. Inawezekana kwamba Ataweza kutumia huduma ya mtu wa aina hii, au kwamba atatumia mtu wa aina hii kama foili[b]. Inawezekana kwamba Atakuwa na njia maalum ya kushughulikia mtu wa aina hii, njia maalum ya kumshughulikia—kama tu Paulo. Hii ndio kanuni na mwelekeo katika moyo wa Mungu kuhusu namna Alivyoamua kumshughulikia mtu wa aina hii. Hivyo basi wakati watu wanapompinga Mungu, na kumkashifu na kumkufuru Yeye, kama wataendelea kusema ubaya kuhusu tabia Yake, au kama watafikia ile hali ya kimsingi ya Mungu, athari zake hazifikiriki. Athari zile mbaya zaidi ni kwamba Mungu anayakabidhi maisha yao na kila kitu chao kwa Shetani, mara moja na kabisa. Hawatasamehewa daima dawamu. Hii inamaanisha kwamba mtu huyu amekuwa chakula katika kinywa cha Shetani, mwanasesere katika mikono yake, na kuanzia hapo, Mungu hahusiki naye. Mnaweza kufikiria ni aina gani ya masikitiko iliyokuweko wakati Shetani alipomjaribu Ayubu? Katika hali kwamba Shetani hakuruhusiwa kuyadhuru maisha ya Ayubu, Ayubu aliteseka pakubwa. Na huoni kwamba ni ngumu hata zaidi kufikiria kupitia kwa mateso ya Shetani namna ambavyo mtu atakavyopitia ambaye amekabidhiwa Shetani kabisa, ambaye yumo katika mashiko ya Shetani kabisa, ambaye amepoteza kabisa utunzaji na rehema ya Mungu, ambaye hayuko tena katika utawala wa Muumba, ambaye amenyang’anywa haki ya kumwabudu Yeye, na haki ya kuwa kiumbe katika utawala wa Mungu, ambaye uhusiano wake na Bwana wa uumbaji umekatizwa kabisa? Kuteswa kwa Ayubu na Shetani kulikwa jambo ambalo lingeonekana kwa macho ya binadamu, lakini Mungu anapomkabidhi Shetani maisha ya mtu, athari zake zitakuwa jambo ambalo mtu hawezi kufikiria. Ni sawa tu na baadhi ya watu kuweza kuzaliwa tena wakiwa ng’ombe, au punda, au baadhi ya watu wakichukuliwa kabisa, na kupagawa na roho chafu, za uovu, na kadhalika. Haya ndiyo matokeo, mwisho wa baadhi ya watu ambao Mungu anawakabidhi kwa Shetani. Kwa nje, yaonekana kwamba watu hao waliomdhihaki, waliomkashifu, kumshutumu, na kumkufuru Bwana Yesu hawakupata athari zozote. Hata hivyo, ukweli ni kwamba Mungu Anao mwelekeo wa kushughulikia kila kitu. Huenda Asitumie lugha wazi kuwaambia watu matokeo ya namna Anavyowashughulikia kila aina ya watu. Wakati mwingine Haongei kwa njia ya moja kwa moja, lakini Anafanya mambo kwa njia ya moja kwa moja. Kwamba haongelei jambo haimaanishi kwamba hakuna matokeo—yawezekana kwamba matokeo ni mabaya zaidi. Inavyoonekana, yaelekea Mungu haongei na watu fulani ili kufichua mwelekeo Wake; kwa uhakika, Mungu hajataka kuwaza juu yao kwa muda mrefu. Hataki kuwaona tena. Kwa sababu ya mambo ambayo wamefanya, tabia yao, kwa sababu ya asili yao na kiini chao, Mungu anawataka tu watoweke machoni Mwake, Anataka kuwakabidhi moja kwa moja kwa Shetani, kumpa Shetani roho yao, nafsi yao na mwili wao, kumruhusu Shetani kufanya atakacho. Ni wazi ni hadi kiwango gani Mungu anawachukia, ni hadi kiwango gani Ameudhika nao. Kama mtu atamghadhabisha Mungu kufikia kiwango ambacho Mungu hataki kumwona tena, kwamba Atakata tamaa kabisa naye, hadi katika kiwango ambacho Mungu hataki tena kushughulika naye Yeye mwenyewe—kama itafikia kiwango hiki ambapo Atawakabidhi kwa Shetani ili aweze kufanya apendavyo, kumruhusu Shetani kumdhibiti, kumtumia, na kumtendea kwa njia yoyote—mtu huyu kwa kweli amemalizika. Haki yake ya kuwa binadamu imebatilishwa kabisa, na haki yake ya kuwa kiumbe imefikia mwisho. Je, huoni kwamba hii ndiyo adhabu mbaya zaidi?

Yote haya yaliyo hapo juu ni maelezo kamilifu ya maneno: “hatasamehewa, wala katika dunia hii, wala katika dunia itakayokuja,” na pia ni utoaji maoni mwepesi kuhusu dondoo za maandiko haya. Nafikiri kwamba mnao ufahamu wake sasa!

Sasa hebu tusome dondoo za maandiko zilizo hapa chini.

12. Maneno ya Yesu kwa Wanafunzi Wake Baada ya Kufufuka Kwake

Yohana 20:26-29 Na kufuatia siku nane tena wanafunzi wake walikuwa ndani, naye Tomaso alikuwa nao: kisha Yesu akaja, milango ikiwa imefungwa, na kusimama katikati, na kusema, Amani iwe nanyi. Kisha akasema kwa Tomaso, nyoosha kidole chako hapa, na uitazame mikono yangu, nyoosha mkono wako hapa, na uusongeshe mbavuni mwangu: na usiwe bila imani, ila mwenye imani. Naye Tomaso akajibu na kumwambia, BWANA Wangu na Mungu wangu. Yesu akasema kwake, Tomaso, kwa sababu umeniona, umeamini, wamebarikiwa wale ambao hawajaona, lakini wameamini.

Yohana 21:16-17 Akasema kwake tena mara ya pili, Simioni, mwana wa Yohana, unanipenda mimi? Akasema kwake, Ndiyo, Bwana, unajua kwamba mimi nakupenda. Akasema kwake, Walishe kondoo wangu. Akasema kwake mara ya tatu, Simioni, mwana wa Yohana, Unanipenda Mimi? Petro alisikitika kwa sababu alimwambia mara ya tatu, Unanipenda Mimi? Na akamwambia, Bwana, wewe unajua vitu vyote, unajua kwamba mimi nakupenda. Yesu akamwambia, Walishe kondoo wangu.

Kile ambacho dondoo hizi zinasimulia ni baadhi ya mambo ambayo Bwana Yesu alifanya na kusema kwa wanafunzi wake baada ya kufufuka Kwake. Kwanza, hebu tuangalie tofauti zozote kati ya Bwana Yesu kabla na baada ya kufufuka Kwake. Alikuwa bado ni yule yule Bwana Yesu wa siku za kale? Maandiko yanao mstari ufuatao unaomfafanua Bwana Yesu baada ya kufufuka kwake: “Kisha Yesu akaja, milango ikiwa imefungwa, na kusimama katikati, na kusema, Amani iwe nanyi.” Ni wazi sana kwamba Bwana Yesu wakati huo hakuwa tena mwili, lakini alikuwa katika umbo la kiroho. Hii ni kwa sababu Alikuwa amepita ile mipaka ya mwili, na wakati ambapo mlango ulifungwa Aliweza bado kuja katikati ya watu na kuwaruhusu wao kumwona Yeye. Hii ndiyo tofauti kubwa zaidi kati ya Bwana Yesu baada ya kufufuka na Bwana Yesu aliyeishi kwa mwili kabla ya kufufuka. Hata ingawa hakukuwa na tofauti yoyote kati ya kutokea kwa ule mwili wa kiroho wa wakati huo na dhihirisho la Bwana Yesu kutoka awali, Yesu katika muda huo alikuwa amekuwa Yesu aliyehisi na kujioa mgeni kwa watu, kwa sababu Alikuwa amekuwa mwili wa kiroho baada ya kufufuka kutoka kwa wafu, na Akilinganishwa na mwili Wake wa awali, mwili huu wa kiroho ulikuwa wa kushangaza na kuchanganya kwa watu zaidi. Hali hii iliunda nafasi kubwa zaidi kati ya Bwana Yesu na watu, nao watu wakahisi katika mioyo yao kwamba Bwana Yesu wa wakati huo alikuwa haeleweki kabisa. Ufahamu na hisia hizi kwa upande wa watu ghafla uliwarudisha katika enzi ya kuamini kwa Mungu ambaye hakuweza kuonekana wala kugusika. Hivyo basi, kitu cha kwanza ambacho Bwana Yesu alifanya baada ya kufufuka Kwake kilikuwa kuruhusu kila mmoja kuweza kumwona, kuthibitisha kuwa yupo, kuthibitisha hoja ya kufufuka Kwake. Kuongezea hayo, hali hiyo ilirejesha uhusiano Wake na watu hadi ule uhusiano Aliokuwa nao Alipokuwa akifanya kazi kupitia kwa mwili, na Alikuwa Kristo ambaye wangeweza kuona na kugusa. Kwa njia hii, mojawapo ya matokeo ni kwamba watu hawakuwa na shaka kwamba Bwana Yesu alikuwa amefufuka kutoka kwa kifo baada ya kusulubishwa msalabani, na hakukuwa na shaka katika kazi ya Bwana Yesu ya kuwakomboa wanadamu. Na matokeo mengine ni kwamba hoja ya Bwana Yesu kujitokeza kwa watu baada ya kufufuka Kwake na kuwaruhusu watu kuweza kumwona na kumgusa Yeye kwa udhabiti kuliweza kuwasalimisha wanadamu katika Enzi ya Neema. Kuanzia wakati huu, watu hawakuweza kurudi katika enzi ya awali, Enzi ya Sheria, kwa sababu ya “kutoweka” au “kuacha na kuondoka” kwa Bwana Yesu lakini wangeendelea mbele, kufuata mafundisho ya Bwana Yesu na kazi Aliyokuwa amefanya. Hivyo basi, awamu mpya katika kazi ya Enzi ya Neema iliweza kufunguliwa rasmi na watu waliokuwa katika sheria walikuja rasmi kutoka katika sheria kuanzia hapo kuenda mbele, na kuingia katika enzi mpya, katika mwanzo mpya. Hizi ndizo maana nyingi za kujitokeza kwa Bwana Yesu kwa wanadamu baada ya kufufuka Kwake.

Kwa sababu Alikuwa mwili wa kiroho, watu waliwezaje kumgusa Yeye na kumwona Yeye? Hii inahusu umuhimu wa kujitokeza kwa Bwana Yesu kwa wanadamu. Je, mlitambua chochote katika dondoo hizi za maandiko? Kwa ujumla miili ya kiroho haiwezi kuonekana wala kuguswa, na baada ya kufufuka, kazi ambayo Bwana Yesu alikuwa amechukua tayari ilikuwa imekamilika. Hivyo basi, kinadharia Hakuwa na haja kabisa ya kurudi katikati ya watu akiwa katika taswira Yake ya asili ili kukutana na wao, lakini kujitokeza kwa mwili wa kiroho wa Bwana Yesu kwa watu kama vile Tomaso kulifanya umuhimu wake kuwa thabiti zaidi, na hali hii iliweza kupenyeza zaidi kwa kina katika mioyo ya watu. Alipomjia Tomaso, alimwacha Tomaso aliyekuwa akishuku kumgusa mkono Wake na kumwambia maneno haya: “Nyoosha mkono wako hapa, na uusongeshe mbavuni mwangu: na usiwe bila imani, ila mwenye imani.” Maneno haya, vitendo hivi vyote havikuwa vitu ambavyo Bwana Yesu alitaka kusema na kufanya tu baada ya Yeye kufufuka, lakini yalikuwa mambo Aliyotaka kuyafanya kabla ya kusulubishwa msalabani. Ni wazi kwamba Bwana Yesu ambaye alikuwa hajasulubishwa katika msalaba tayari alikuwa na ufahamu wa watu kama Tomaso. Hivyo basi, tunaweza kuona nini kutokana na haya? Alikuwa angali Bwana Yesu yule yule hata baada ya kufufuka Kwake. Kiini chake kilikuwa hakijabadilika. Kushuku kwa Tomaso hakukuwa kumeanza tu lakini kulikuwa ndani yake muda wote aliokuwa akimfuata Bwana Yesu, lakini Alikuwa Bwana Yesu aliyekuwa amefufuka kutoka kwa kifo na alikuwa amerudi kutoka katika ulimwengu wa kiroho akiwa na taswira Yake asilia, na tabia Yake binafsi, na kwa ufahamu huu wa wanadamu kutoka kwa wakati Wake akiwa mwili, kwa hivyo basi Alienda kumfuta Tomaso kwanza, ili kumfanya Tomaso kugusa mbavu Zake, kumfanya kutoona tu mwili Wake wa kiroho baada ya kufufuka, lakini pia kumruhusu auguse na kuuhisi uwepo wa mwili Wake wa kiroho, na kutupilia mbali kabisa shaka zake. Kabla ya Bwana Yesu kusulubishwa msalabani, Tomaso siku zote alishuku kwamba Yeye ni Kristo, na hakuweza kuamini. Imani yake katika Mungu ilianzishwa tu kwa msingi wa kile ambacho angeweza kuona kwa macho yake, kile ambacho angeweza kugusa kwa mikono yake. Bwana Yesu alikuwa na ufahamu mzuri wa imani ya mtu wa aina hii. Waliamini tu katika Mungu wa mbinguni, na hawakuamini kamwe, na wasingekubali Yule Aliyetumwa na Mungu, au Kristo katika mwili. Ili kufanya yeye kuweza kutambuliwa na kuaminiwa katika uwepo wa Bwana Yesu na kwamba kweli Alikuwa Mungu mwenye mwili, Alimruhusu Tomaso kuunyosha mkono wake na kugusa ubavu Wake. Je, Tomaso alikuwa akishuku kwa njia tofauti kabla na baada ya kufufuka kwa Bwana Yesu? Alikuwa daima akishuku, na mbali na mwili wa kiroho wa Bwana Yesu kujitokeza binafsi kwake na kumruhusu Tomaso kugusa alama za misumari katika mwili Wake, hakuna aliyeweza kutatua shaka zake, na hakuna mtu ambaye angemfanya kuziachilia. Hivyo basi, kuanzia muda ambao Bwana Yesu alimruhusu kuugusa ubavu Wake na kumwacha akihisi uwepo wa alama za misumari, shaka ya Tomaso ikatoweka na akajua kwa kweli kwamba Bwana Yesu alikuwa amefufuka na akatambua na kuamini kwamba Bwana Yesu ndiye aliyekuwa Kristo wa kweli, na kuamini kwamba alikuwa Mungu mwenye mwili. Ingawa wakati huu Tomaso hakushuku tena, alikuwa amepoteza milele fursa ya kukutana na Kristo. Alikuwa amepoteza milele fursa ya kuwa pamoja na Yeye, kumfuata Yeye, na kumjua Yeye. Alikuwa amepoteza fursa ya Kristo kumfanya yeye kuwa mtimilifu. Kuonekana kwa Bwana Yesu na maneno Yake yalitoa hitimisho, na hukumu kuhusiana na imani ya wale ambao walijawa na kutoamini kwingi. Alitumia maneno na vitendo Vyake halisi kuwaambia wale waliokuwa wakishuku, kuwaambia wale ambao waliamini tu katika Mungu aliye juu mbinguni lakini amini hawakumwamini Kristo: Mungu hakuitukuza imani yao, wala Hakuupongeza ufuasi wao uliojawa na shaka. Ile siku waliamini kikamilifu Mungu naye Kristo angeweza tu kufanya hivyo siku ile ambayo Mungu alikuwa akamilishe kazi Yake kuu. Bila shaka, siku hiyo ndiyo iliyokuwa siku ambayo kushuku kwao kulipokea uamuzi. Mwelekeo wao katika Kristo uliamua majaliwa yao, na kushuku kwao katika usumbufu kulimaanisha imani yao haikuwapatia matokeo yoyote, na ugumu wao kulimaanisha matumaini yao yaliambukia patupu. Kwa sababu imani yao katika Mungu aliye mbinguni ilisababishwa na njozi, na kushuku kwao katika Kristo kulikuwa kwa kweli mwelekeo wao wa kweli kwa Mungu, hata ingawa walizigusa alama za msumari kwenye mwili wa Bwana Yesu, imani yao ilikuwa bado bure bilashi na matokeo yao yangeweza tu kufafanuliwa kama kuchota maji na kikapu cha mianzi—yote ni bure bilashi. Kile Bwana Yesu Alichomwambia Tomaso kilikuwa kikisema hivyo waziwazi kwa kila mtu: Yule Bwana Yesu aliyefufuka ndiye Bwana Yesu ambaye mwanzo alikuwa ametumia miaka thelathini na mitatu na nusu akifanya kazi miongoni mwa wanadamu. Ingawa alikuwa amesulubishwa msalabani na kupitia bonde la kivuli cha mauti, alikuwa amepitia kitendo cha kufufuka, kila dhana Yake haikuwa imepitia mabadiliko. Ingawa kwa sasa alikuwa na alama za misumari kwenye mwili Wake, na ingawa Alikuwa amefufuka na kutoka kaburini akitembea, tabia Yake, ufahamu Wake wa wanadamu na nia Zake kwa wanadamu bado zilikuwa hazijabadilika hata kidogo. Pia, Alikuwa akiwaambia watu kwamba Alikuwa ameshuka kutoka kwenye msalaba, ameshinda dhambi, amepata ushindi juu ya ugumu, na akupata ushindi dhidi ya kifo. Alama zile za misumari zilikuwa tu ithibati ya ushindi Wake dhidi ya Shetani, ithibati ya kuwa sadaka ya dhambi ili kuweza kuwakomboa kwa ufanisi wanadamu wote. Alikuwa akiwaambia watu kwamba tayari Alikuwa ameanza kushughulikia dhambi za wanadamu na Alikuwa amekamilisha kazi Yake ya ukombozi. Aliporudi ili kuwaona wanafunzi Wake, Aliwaambia kwa kuonekana Kwake: “Mimi niko hai, bado Nipo; leo kwa kweli nasimama mbele yenu ili mweze kuniona na kunigusa Mimi. Siku zote nitakuwa na wewe.” Bwana Yesu alitaka pia kutumia mfano huo wa Tomaso kama onyo kwa watu wa siku za usoni: Ingawa unaamini Bwana Yesu, huwezi kumwona wala kumgusa Yeye, na bado, unaweza kubarikiwa kutokana na imani yako ya kweli, na unaweza kumwona Bwana Yesu kupitia kwa imani yako ya kweli; mtu aina hii amebarikiwa.

Maneno haya yaliyorekodiwa katika Biblia ambayo Bwana Yesu aliongea Alipojitokeza kwa Tomaso ni msaada mkubwa kwa watu wote katika Enzi ya Neema. Kuonekana Kwake na maneno Yake kwa Tomaso yamekuwa na athari kubwa kwa vizazi vijavyo, na yatakuwa na umuhimu wa kudumu daima dawamu. Tomaso anawakilisha mtu wa aina ya kuamini Mungu ilhali anamshuku Mungu. Wao wanayo maumbile ya kushuku, wana mioyo isiyoeleweka, wao wenyewe ni wadanganyifu, na hawaamini mambo ambayo Mungu anaweza kukamilisha. Hawaamini katika kudura ya Mungu na utawala Wake, na hawaamini katika Mungu kuwa mwili. Hata hivyo, kufufuka kwa Bwana Yesu kulikuwa ni sawa na kuzabwa kofi katika nyuso zao, na pia kuliwapa fursa ya kugundua ni shaka yao wenyewe, kutambua kushuku kwao binafsi, na kuukubali udanganyifu wao binafsi na hivyo basi kuamini katika kuwepo na kufufuka kwa Bwana Yesu. Kile kilichomfanyikia Tomaso kilikuwa onyo na tahadhari kwa vizazi vijavyo ili watu wengi zaidi waweze kujitahadharisha na ili wasiwe wa kushuku kama Tomaso, na kama wangekuwa hivyo, wangezama katika giza. Ukimfuata Mungu, lakini kama Tomaso, siku zote unataka kuugusa ubavu wa Bwana na kuhisi alama Zake za msumari ili kuthibitisha, ili kuhakikisha, ili kuchambua kama Mungu yupo, basi Mungu atakuacha. Hivyo basi, Bwana Yesu anawahitaji watu wasiwe kama Tomaso, kuamini tu kile wanachoweza kuona kwa macho yao, lakini kuwa bila kasoro, mtu mwaminifu, kutouwa na shaka yoyote dhidi ya Mungu, lakini kumwamini tu na kumfuata Yeye. Mtu wa aina hii amebarikiwa. Hili ni hitaji dogo sana la Bwana Yesu kwa watu, na onyo kwa wafuasi Wake.

Huu ndio mwelekeo wa Bwana Yesu kwa wale waliojaa shaka. Hivyo basi ni nini ambacho Bwana Yesu alimwambia, na ni nini Alichofanya kwa wale ambao wanaweza kuamini kwa uaminifu na kumfuata Yeye? Maswali hayo ndiyo tutakayoyaangalia katika kipindi kifuatacho, kuhusiana na kitu ambacho Bwana Yesu alimwambia Petro.

Katika mazungumzo haya, Bwana Yesu alimwuliza Petro mara kadhaa kuhusu jambo moja: “Simoni, mwana wa Yohana, je, unanipenda?” Hiki ndicho kiwango cha juu zaidi ambacho Bwana Yesu alihitaji kutoka kwa watu kama vile Petro baada ya kufufuka Kwake, wanaoamini Kristo kwa kweli na kulenga kumpenda Bwana. Swali hili lilikuwa aina fulani ya uchunguzi, na aina fulani ya kuhoji, lakini hata zaidi lilikuwa hitaji na tarajio la watu kama Petro. Aliitumia mbinu hii ya kuuliza maswali ili watu waweze kuwaza na kuwazua kujihusu na kuangalia katika maisha yao wenyewe: Mahitaji ya Bwana Yesu kwa watu ni yapi? Je, nampenda Bwana? Mimi ni mtu anayempenda Mungu? Nafaa vipi kumpenda Mungu? Hata ingawa Bwana Yesu aliuliza tu swali hili kwa Petro, ukweli ni kwamba katika moyo Wake, Alitaka kutumia fursa hii ya kumwuliza Petro ili kuuliza swali la aina hii kwa watu wengi zaidi wanaoutafuta kumpenda Mungu. Ni kwa sababu tu kuwa Petro alibarikiwa kuwa mwakilishi wa mtu wa aina hii, ili kupokea swali hilo kutoka kwa kinywa cha Bwana Yesu mwenyewe.

Likilinganishwa na “nyoosha mkono wako hapa, na uusongeshe mbavuni mwangu: na usiwe bila imani, ila mwenye imani,” ambalo Bwana Yesu alimwambia Tomaso baada ya kufufuka Kwake, Yeye kumwuliza Petro swali mara tatu: “Simioni, mwana wa Yohana, unanipenda mimi?” waruhusu watu kuweza kuhisi kwa njia bora zaidi ule ukali wa mwelekeo wa Bwana Yesu na umuhimu Aliouhisi wakati huu wa kuuliza maswali hayo. Kuhusiana naye Tomaso wa kushuku pamoja na asili yake ya udanganyifu, Bwana Yesu alimruhusu yeye kufikisha mkono wake na kuzigusa zile alama Zake za msumari, jambo ambalo lilimfanya yeye kuamini kwamba Bwana Yesu ndiye aliyekuwa Mwana wa Adamu aliyefufuka na akatambua utambulisho wa Bwana Yesu kama Kristo. Na ingawa Bwana Yesu hakumkemea kwa ukali Tomaso, wala hakuonyesha kwa matamshi hukumu yoyote ilio wazi kwake, Alimjuza kwamba Alimwelewa kupitia kwa hatua za kimatendo, huku pia akionyesha mtazamo Wake na uamuzi wa aina hiyo ya mtu. Mahitaji na matarajio ya Bwana Yesu ya mtu wa aina hiyo hayawezi kuonekana kutokana na kile Alichosema. Kwa sababu watu kama Tomaso hawana katu imani ya ukweli. Mahitaji ya Bwana Yesu kwao yanapatikana tu katika, lakini mwelekeo Alioufichua kwa watu kama Petro ni tofauti kabisa. Hakuhitaji kwamba Petro aunyoshe mkono wake na kuzigusa hizo alama Zake za misumari, wala hakumwambia Petro: “usiwe bila imani, ila mwenye imani.” Badala yake, Alimwuliza Petro kwa kurudia swali lilo hilo. Hili lilikuwa swali la kuchokonoa fikira, na lenye maana ambalo halina budi kumfanya kila mfuasi wa Kristo kuhisi majuto, na woga, lakini pia kuhisi ile hali ya moyo wa wasiwasi, na huzuni ya Bwana Yesu. Na wakati wakiwa katika maumivu na mateso makali, wanaweza kuelewa zaidi wasiwasi wa Bwana Yesu Kristo na utunzaji Wake; wanatambua mafundisho Yake ya dhati na mahitaji makali kuhusu watu wasio na kasoro, waaminifu. Swali la Bwana Yesu linawaruhusu watu kuhisi kwamba matarajio ya Bwana kwa watu yaliofichuliwa kupitia kwa maneno haya mepesi si ya kuamini tu na kumfuata Yeye, lakini kutimiza yote kwa kuwa na upendo, kumpenda Bwana wako, kumpenda Mungu wako. Upendo wa aina hii ni wa utunzaji na utiifu. Ni wanadamu kuishi kwa ajili ya Mungu, kufa kwa ajili ya Mungu, kujitolea kila kitu chao kwa ajili ya Mungu, na kutumia na kutoa kila kitu chao kwa ajili ya Mungu. Upendo wa aina hii pia ni kumpa Mungu tulizo, kumruhusu Yeye kufurahia ushuhuda, na kumruhusu Yeye kupumzika. Ni fidia ya wanadamu kwa Mungu, uwajibikaji wao, na wajibu wao, na ni njia ambayo wanadamu lazima wafuate kwa maisha yao yote. Haya maswali matatu yalikuwa mahitaji na ushawishi ambao Bwana Yesu alitoa kwa Petro na watu wote ambao wangefanywa kuwa watimilifu. Ni maswali haya matatu ndiyo yaliyomwongoza na kumpa motisha Petro kukamilisha njia yake ya maisha, na yalikuwa maswali haya wakati ule wa Bwana Yesu kuondoka ambayo yalimfanya Petro kuanza njia yake ya kufanywa mtimilifu, na yaliyomwongoza, kwa sababu ya upendo wake kwa Bwana, kuutunza moyo wa Bwana, kumtii Bwana, kumpa tulizo Bwana, na kuyatoa maisha yake yote na kila kitu chake chote kwa sababu ya upendo wake.

Katika Enzi ya Neema, kazi ya Mungu ilikuwa kimsingi ya aina mbili ya watu. Wa kwanza alikuwa aina ya aliyeamini Kwake na kumfuata, ambaye angetii amri Zake, ambaye angeweza kuuvumilia msalaba na kuushikilia hadi katika njia ya Enzi ya Neema. Mtu wa aina hii angepata baraka za Mungu na kufurahia neema ya Mungu. Aina ya pili ya mtu alikuwa kama Petro, mtu ambaye angeweza kufanywa kuwa mtimilifu. Hivyo basi, baada ya Bwana Yesu kufufuka, Alifanya kwanza mambo haya mawili yenye umuhimu sana. Kwanza lilikuwa ni kwa Tomaso, na jingine lilikuwa kwa Petro. Mambo haya mawili yanawakilisha nini? Yanawakilisha nia za kweli za Mungu katika kuwaokoa binadamu? Yanawakilisha uaminifu wa Mungu kwa binadamu? Kazi Aliyoifanya na Tomaso ilikuwa ni kuwapa onyo watu wasiwe wanashuku, lakini kuamini tu. Kazi Aliyofanya na Petro ilikuwa ni kuipatia nguvu imani ya watu kama vile Petro, na kuweka wazi mahitaji ya aina hii ya watu, ili kuonyesha ni shabaha zipi wanafaa kuwa wakifuatilia.

Baada ya Bwana Yesu kufufuka, Alijitokeza kwa watu aliofikiria walifaa, Akaongea na wao, na kuwapa wao mahitaji, huku akiacha nyuma nia Zake, na matarajio Yake kwa watu. Hivi ni kusema, kama Mungu mwenye mwili, haijalishi kama ulikuwa katika wakati Wake akiwa mwili, au katika mwili wa kiroho baada ya kusulubishwa msalabani na kufufuliwa—haja Yake kwa wanadamu na mahitaji kwa wanadamu hayakubadilika. Alijali kuwahusu wanafunzi hawa kabla ya kufika msalabani; ndani ya moyo Wake, Alikuwa wazi katika hali ya kila mmoja, Alielewa upungufu wa kila mmoja, na bila shaka ufahamu Wake wa kila mtu ulikuwa namna ile ile baada ya Yeye kuaga dunia, kufufuka, na kuwa mwili wa kiroho kama hali ilivyokuwa Alipokuwa katika mwili. Alijua kwamba watu hawakuwa kwa kikamilifu na uhakika kuuhusu utambulisho Wake kama Kristo, lakini katika kipindi Chake akiwa mwili Hakuwa anatoa amri kali kuhusu watu. Lakini baada ya kufufuliwa Alijitokeza kwao, na Akawafanya wawe na hakika kabisa kwamba Bwana Yesu alikuwa amekuja kutoka kwa Mungu, kwamba Alikuwa Mungu mwenye mwili, na Alitumia hoja hiyo ya uwepo Wake na kufufuka Kwake kama maono na motisha kubwa zaidi kwa muda mrefu katika ufuatiliaji wa wanadamu. Kufufuka kwake kutoka kifo hakukuwapa nguvu tu wale wote Waliomfuata, lakini pia kuliweka katika taathira kazi Yake ya Enzi ya Neema miongoni mwa wanadamu, na hivyo basi wokovu wa injili ya Bwana Yesu katika Enzi ya Neema kwa utaratibu ukaenea katika kila pembe ya binadamu. Unaweza kusema kwamba kutokea kwa Bwana Yesu baada ya kufufuka Kwake kulikuwa na umuhimu wowote? Kama ungekuwa Tomaso au Petro wakati huo, na ukumbane na kitu hiki kimoja katika maisha yako ambacho kilikuwa na maana sana, ni athari ya aina gani ambayo kitu hicho kingekuwa nayo kwako? Je, ungeona huu kama msukumo wako katika kumfuata Mungu? Ungeona hali hii kama nguvu endeshi zako wewe kumfuata Mungu, kujaribu kumridhisha Yeye, na kufuatilia upendo wa Mungu katika maisha yako? Ungeweza kutumia jitihada za maisha yako yote ili kueneza maono haya makubwa zaidi? Ungefanya kueneza wokovu wa Bwana Yesu kuwa kazi unayokubali kutoka kwa Mungu? Hata ingawa hamjapitia haya, zile hali mbili za Tomaso na Petro tayari zinatosha kwa watu wa kisasa kuwa na ufahamu wazi kuhusu mapenzi ya Mungu na kumhusu Mungu. Inaweza kusemekana kwamba baada ya Mungu kuwa mwili, baada ya Yeye binafsi kupitia maisha miongoni mwa wanadamu na kuwa na maisha ya binadamu, na baada ya Yeye kuona uharibifu wa tabia wa wanadamu na hali ya maisha ya binadamu, Mungu katika mwili alihisi kwa kina zaidi jinsi mwanadamu alikuwa asiyejiweza, mwenye masikitiko na wa kuonewa huruma. Mungu alipata huruma zaidi kwa hali ya binadamu kwa sababu ya ubinadamu Wake wakati akiishi katika mwili, kwa sababu ya silika Zake katika mwili. Hili lilimsababisha kuwa na wasiwasi mkubwa zaidi juu ya wafuasi Wake. Haya pengine ni mambo ambayo huwezi kuelewa, lakini Naweza kufafanua wasiwasi na utunzaji wa Mungu katika damu kwa kila mmojawapo wa wafuasi Wake kwa kauli hii: kujali kwingi. Hata ingawa kauli hii inatokana na lugha ya binadamu, na hata ingawa ni kauli yenye ubinadamu sana, inaonyesha kwa kweli na kufafanua hisia za Mungu kwa wafuasi Wake. Na kwa kujali kwingi kwa Mungu kwa ajili ya binadamu, kwa mkondo wa yale yote ambayo wewe umeyapitia utaanza kuhisi kwa utaratibu yote haya na kuyaonja. Hata hivyo, hali hii inaweza kutimizwa tu kwa kuelewa kwa utaratibu tabia ya Mungu kwa msingi wa kufuatilia mabadiliko katika tabia yako wewe binafsi. Kuonekana kwa Bwana Yesu kulifanikisha kujali Kwake kwingi kwa minajili ya wafuasi Wake katika ubinadamu na akakupokeza kwa mwili Wake wa kiroho, au unaweza kusema uungu Wake. Kuonekana Kwake kuliwaruhusu watu kuwa na hali nyingine waliyopitia na hisia walizopitia zinazohusu kujali na utunzaji wa Mungu huku kukithibitisha kwa uthabiti kwamba Mungu Ndiye anayefungua enzi, anayeiendeleza enzi, na Yeye ndiye anayetamatisha enzi. Kupitia kwa Kuonekana Kwake Aliipatia nguvu imani ya watu wote, na kupitia kwa Kuonekana Kwake alithibitishia ulimwengu hoja kwamba Yeye ni Mungu Mwenyewe. Hali hii iliwapa wafuasi Wake uthibitisho wa milele, na kupitia kwa Kuonekana Kwake pia Aliweza kufungua awamu ya kazi Yake katika enzi mpya.

13. Yesu Ala Mkate na Kuonyesha Maandiko Baada ya Kufufuka Kwake

Luka 24:30-32 Na ikatimia, alipokuwa akikaa na wao ili wale, aliuchukua mkate, na kuubariki, na akaupasua, na kuwapa. Na macho yao yakafunguka, na wakamjua, na akatoweka wasimwone. Na wakaambiana, je, Mioyo yetu haikuwaka ndani yetu sisi, wakati alipokuwa akituzungumzia njiani, na wakati alipotufungulia maandiko?

14. Wanafunzi Wampa Yesu Kipande cha Samaki wa Kuokwa Ale

Luka 24:36-43 Na wakati walipokuwa wakinena hayo, Yesu mwenyewe alisimama katikati yao, na akasema kwao, Amani iwe kwenu ninyi. Lakini walikuwa na woga na hofu sana, na wakafikiri kwamba walikuwa wameona roho. Naye akawaambia, Mbona mnasumbuka? na mbona mashaka yanaibuka mioyoni mwenu? Tazameni mikono yangu na miguu yangu, ya kwamba ni mimi mwenyewe: Niguseni, na kuona; kwa sababu roho haina mwili na mifupa, jinsi mnavyoniona mimi nikiwa nayo. Na baada ya yeye kunena hayo, akawaonyesha mikono yake na miguu yake. Na wakati walikuwa bado hawajaamini kwa furaha, na wakishangaa, akawaambia, Mnacho chakula chochote huku? Na wakampa kipande cha samaki wa kuokwa kwa asali. Na akakichukua, na kukila mbele yao.

Halafu tutaangalia dondoo zilizo hapo juu. Dondoo ya kwanza inamulika upya ulaji wa mkate na Bwana Yesu na unaeleza maandiko baada ya kufufuka Kwake na dondoo ya pili inaonyesha upya Bwana Yesu akila kipande cha samaki aliyekaushwa. Ni aina gani ya msaada ambao dondoo hii mara mbili inatupa kwa kuijua tabia ya Mungu? Unaweza kuwaza ni picha ya aina gani unayopata kutoka katika ufafanuzi huu wa Bwana Yesu akila mkate na kisha kipande cha samaki aliyekaushwa? Unaweza kufikiria, kama Bwana Yesu alikuwa Amesimama mbele yako wewe ukila mkate, unaweza kuhisi vipi? Au kama Angekuwa Akila pamoja nawe kwenye meza moja, huku Akila samaki kwa mkate na watu, ni hisia aina gani ambayo ungekuwa nayo wakati huo? Kama unahisi ungekuwa karibu sana na Bwana, kwamba yuko karibu sana na wewe, basi hisia yako i sahihi. Hivi ndivyo hasa tokeo ambalo Bwana Yesu alitaka kulileta kutokana na kula Kwa mkate na samaki mbele ya umati wa watu uliokusanyika baada ya kusulubishwa Kwake. Kama Bwana Yesu angekuwa ameongea tu na watu baada ya kufufuka Kwake, kama wasingeweza kuhisi mwili na mifupa Yake, lakini walihisi Alikuwa roho isiyoweza kufikika, wangehisi vipi? Hawangesikitishwa? Wakati watu wangesikitishwa, hawangehisi kwamba wameachwa? Hawangehisi ule umbali wa Bwana Yesu Kristo? Ni athari hasi ya aina gani ambayo umbali huu ungeweza kujenga katika uhusiano wa watu na Mungu? Watu wangehisi woga bila shaka, kwamba wasingethubutu kusonga karibu na Yeye, na wangekuwa na mwelekeo wa kumweka kwa mbali kiasi. Kuanzia hapo mpaka leo, wangekatiza uhusiano wao wa karibu na Bwana Yesu Kristo, na kurudi katika uhusiano kati ya wanadamu na Mungu aliye juu mbinguni, kama ilivyokuwa kabla ya Enzi ya Neema. Mwili wa kiroho ambao watu wasingeweza kuugusa au kuuhisi ungesababisha ukomeshaji wa ukaribu wao na Mungu, na ungefanya ule uhusiano wa karibu—ulioanzishwa wakati Bwana Yesu Kristo akiwa mwili bila ya umbali wowote kati Yake yeye na binadamu—ukose kuwepo. Hisia za watu kwa mwili wa kiroho ni za woga tu, kuepuka, na mtazamo usioeleweka. Hawathubutu kukaribia zaidi au kuwa na mazungumzo na Yeye, sikuambii hata kufuata, kuwa na imani, au kuwa na matumaini Kwake. Mungu hakupenda kuiona hisia ya aina hii ambayo wanadamu walikuwa nayo kwake Yeye. Hakutaka kuwaona watu wakimwepuka Yeye au wakijiondoa Kwake yeye; Aliwataka tu watu kumwelewa Yeye, kumkaribia na kuwa familia Yake. Kama familia yako binafsi, watoto wako wangekuona lakini wasingekutambua wewe, na hawakuthubutu kukukaribia lakini siku zote walikuepuka wewe, kama usingeweza kupata ufahamu wao kwa kila kitu ulichokuwa umewafanyia, ungehisi vipi? Halingekuwa jambo la uchungu? Je, hungevunjika moyo? Hivyo hasa ndivyo Mungu anavyohisi wakati watu wanamwepuka. Hivyo basi, baada ya kufufuka Kwake, Bwana Yesu bado alijitokeza kwa watu katika umbo Lake la mwili na damu, na kula na kunywa pamoja nao. Mungu huwaona watu kama familia na pia anataka wanadamu kumwona Yeye kwa njia hiyo; ni kwa njia hii tu ndivyo Mungu anavyoweza kuwapata watu kwa kweli, na ndio watu wanavyoweza kumpenda na kumwabudu Mungu kwa kweli. Sasa mnaweza kuelewa nia Yangu katika kudondoa dondoo hizi mbili kutoka katika maandiko pale ambapo Bwana Yesu anaula mkate na kuonyesha maandiko baada ya kufufuka Kwake, na wanafunzi wanampa kipande cha samaki aliyechomwa ale?

Inaweza kusemekana kwamba misururu ya mambo ambayo Bwana Yesu alisema na kufanya baada ya kufufuka Kwake yalikuwa ya fikira njema, na kufanywa kwa nia njema. Walijaa huruma na huba ambayo Mungu alishikilia kwa binadamu, na akiwa amejaa pia na mapenzi na utunzaji wa makini Aliokuwa nao kwa minajili ya uhusiano wa karibu aliokuwa Ameanzisha na wanadamu wakati Akiwa katika mwili. Hata zaidi walijaa kumbukumbu za kitambo na tamaa Alilokuwa nayo kutokana na maisha Yake ya kula na kuishi miongoni mwa wafuasi Wake wakati akiwa katika mwili. Hivyo basi, Mungu hakuwataka watu kuhisi umbali kati ya Mungu na binadamu, wala Hakutaka wanadamu kuwa mbali na Mungu. Hata zaidi, Hakutaka wanadamu wahisi kwamba Bwana Yesu baada ya kufufuka Kwake hakuwa tena Bwana ambaye alikuwa wa karibu na watu, kwamba Hakuwa pamoja tena na wanadamu kwa sababu Alirudi katika ulimwengu wa kiroho, alirudi kwa Baba ambaye watu wengi wasingeweza kumwona wala kumsikia. Hakutaka watu kuhisi kwamba kulikuwa na tofauti yoyote katika cheo kati Yake na wanadamu. Mungu anapowaona watu wanaotaka kumfuata lakini wanamweka katika umbali fulani, moyo Wake unapata maumivu kwa sababu hiyo inamaanisha kwamba mioyo yao iko mbali sana na Yeye, inamaanisha kwamba itakuwa vigumu sana Kwake yeye kuweza kuipata mioyo yao. Hivyo basi kama angekuwa amejitokeza kwa watu kupitia kwa mwili wa kiroho ambao wasingeweza kuuona ama kuugusa, hali hii kwa mara nyingine tena ingeweza kumweka binadamu mbali na Mungu, na ingewasababisha wanadamu kumwona Kristo kimakosa baada ya kufufuka Kwake kuonekana kuwa Amegeuka kuwa na majivuno, wa aina tofauti na wanadamu, na mtu ambaye asingeweza tena kushiriki meza na kula pamoja na binadamu kwa sababu wanadamu ni wenye dhambi, wananuka, na hawawezi kumkaribia Mungu hata kidogo. Ili kuondoa kutoelewana huku kwa wanadamu, Bwana Yesu alifanya mambo kadha wa kadha ambayo mara kwa mara Alifanya katika mwili, kama ilivyorekodiwa katika Biblia, “aliuchukua mkate, na kuubariki, na akaupasua, na kuwapa.” Pia Aliwachambulia maandiko, kama Alivyokuwa amezoea kufanya. Yote haya ambayo Bwana Yesu alifanya yalimfanya kila mmoja aliyemwona Yeye kuhisi kwamba Bwana hakuwa amebadililika, kwamba alikuwa bado Bwana Yesu. Hata ingawa Alikuwa amesulubishwa msalabani na kupitia kifo, Alikuwa amefufuliwa, na hakuwa amemwacha binadamu. Alikuwa amerudi kuwa miongoni mwa wanadamu, na kila kitu Chake hakikuwa kimebadilika. Mwana wa Adamu akiwa amesimama mbele ya watu alikuwa bado Bwana Yesu. Mwenendo Wake na mazungumzo Yake na watu yalikuwa ya kawaida sana. Alikuwa angali bado na huruma na upendo, neema, na uvumilivu—Alikuwa bado Bwana Yesu aliyewapenda wengine kama Alivyojipenda Mwenyewe, ambaye angeweza kuwasamehe wanadamu mara sabini mara saba. Kama kawaida, Alikula na watu, kuzungumza maandiko na wao, na hata muhimu zaidi, sawa tu na kama alivyofanya awali, Alifanywa kuwa mwili na damu na aliweza kuguswa na kuonekana. Mwana wa Adamu katika njia hii aliwaruhusu watu kuhisi upendo huo, kuhisi kuwa watulivu, na kuhisi furaha ya kupata tena kitu ambacho kilikuwa kimepotea, na wao pia walihisi watulivu kwa njia tosha ya kuanza kumtegemea na kumtumainia Mwana huyu wa Adamu kwa ujasiri na kwa imani ambaye angeweza kuwasamehe wanadamu dhambi zao. Walianza pia kuomba katika jina la Bwana Yesu bila ya kusita, kuomba ili kupokea neema Yake, baraka Zake, na kupokea amani na furaha kutoka Kwake, kupata utunzaji na ulinzi kutoka Kwake na kuanza kutenda uponyaji na kupunga mapepo kwa jina la Bwana Yesu.

Katika muda huu ambao Bwana Yesu alifanya kazi katika mwili, wengi wa wafuasi Wake wasingeweza kuthibitisha kikamilifu utambulisho Wake na mambo Aliyoyasema. Wakati aliposulubishwa msalabani, mwelekeo wa wafuasi Wake ulikuwa ule wa matarajio; aliposulubiwa msalabani na kupitishiwa yale yote aliyopitishiwa hadi alipowekwa katika kaburi, mwelekeo wa watu Kwake yeye ulikuwa wa kutoridhika. Wakati huu, watu walikuwa tayari wameanza kusonga katika mioyo yao kutoka katika kushuku hadi kukataa mambo ambayo Bwana Yesu alikuwa amesema wakati Akiwa mwili. Na Alipotembea nje ya kaburi na kujitokeza kwa watu mmoja baada ya mwingine, wengi wa watu ambao walikuwa wamemwona Yeye kwa macho yao au kusikia habari za kufufuka Kwake, walibadilika kwa utaratibu kutoka katika hali ya kumkataa hadi ile ya nadharia ya kushuku. Kufikia muda ule ambao Bwana Yesu alimfanya Tomaso kuuweka mkono wake katika upande Wake, kufikia wakati ambao Bwana Yesu aliuvunja mkate na kuula mbele ya umati wa watu baada ya kufufuka Kwake na baada yake kula kipande cha samaki aliyechemshwa mbele yao, hapo tu ndipo walipokubali kwa kweli Bwana Yesu ni Kristo katika mwili. Mnaweza kusema kwamba ni kana kwamba mwili huu wa kiroho ulio na nyama na damu uliosimama mbele ya hao watu ulikuwa ukizindua kila mmoja wao kutoka katika ndoto. Mwana wa Adamu akiwa amesimama mbele yao Ndiye aliyekuwepo tangu miaka hiyo ya nyuma. Alikuwa na umbo, na mwili, na mifupa, na Alikuwa tayari ameishi na kula na wanadamu kwa muda mrefu…. Wakati huu, watu walihisi kwamba uwepo Wake ulikuwa halisi, wa ajabu sana; wote walichangamka na kufurahi mno, na wakati uo huo walijawa na hisia. Na kuonekana Kwake tena kuliwaruhusu watu waweze kuona kwa kweli unyenyekevu Wake, kuhisi ukaribu Wake na tamanio Lake, uhusiano Wake wa karibu na wanadamu. Kupatana huku kwa kufupi kuliwafanya watu waliomwona Bwana Yesu kuhisi kana kwamba muda mrefu umepita. Mioyo yao iliyopotea, kuchanganyikiwa, yenye woga, yenye wasiwasi, inayotarajia na isiyosikia hisia zozote vyote vilipata utulivu. Hawakuwa na shaka tena au kutoridhika tena kwa sababu walihisi kwamba sasa kulikuwa na tumaini na kitu cha kutegemea. Mwana wa Adamu akiwa amesimama mbele yao Angekuwa nao milele, Angekuwa mnara wao dhabiti, kimbilio lao la kila wakati.

Ingawa Bwana Yesu alifufuliwa, moyo Wake na kazi Yake vyote havikuwa vimeondoka kwa wanadamu. Aliwaambia watu Alipoonekana ya kwamba haijalishi ni umbo gani Alilokuwemo ndani, Angeandamana na watu, kutembea na wao, na kuwa na wao siku zote na katika sehemu zote. Na nyakati zote na mahali popote, Angewatosheleza wanadamu na kuwachunga, kuwaruhusu kumgusa na kumwona Yeye, na kuhakikisha kwamba hawatawahi kuhisi tena kama wasio na msaada. Bwana Yesu alitaka pia watu wajue yafuatayo: Maisha yao ulimwenguni hawapo pekee. Mwanadamu ana utunzaji wa Mungu, Mungu yuko pamoja nao; watu siku zote wanaweza kumwegemea Mungu; Yeye ndiye familia ya kila mmoja wa wafuasi Wake. Akiwa na Mungu wa kumwegemea, mwanadamu hatawahi tena kuwa mpweke au bila usaidizi, na wale wanaomkubali kama sadaka yao ya dhambi hawataishia katika dhambi tena. Katika macho ya binadamu, sehemu hizi za kazi Zake ambazo Bwana Yesu alitekeleza baada ya kufufuka Kwake zilikuwa chache mno lakini Ninavyoona Mimi, kila kitu kilikuwa na maana yenye thamani sana na zote zilikuwa zenye umuhimu na uzito.

Ingawa muda wa Bwana Yesu kufanya kazi katika mwili ulijaa ugumu na mateso, kupitia katika kuonekana Kwake katika mwili Wake wa kiroho wa mwili na damu, Alikamilisha vyema na kwa njia timilifu kazi Yake ya wakati huo akiwa kwa mwili ili kuwakomboa wanadamu. Aliianza huduma Yake kwa kugeuka mwili na Alihitimisha huduma Yake kwa kujitokeza kwa wanadamu Akiwa katika umbo Lake la mwili. Alikuwa mjumbe wa Enzi ya Neema, Aliianzisha Enzi ya Neema kupitia kwa utambulisho Wake kama Kristo. Kupitia utambulisho Wake kama Kristo, Alitekeleza kazi katika Enzi ya Neema na Akaipatia nguvu na kuwaongoza wafuasi katika Enzi ya Neema. Inaweza kusemwa kuhusu kazi ya Mungu kwamba kwa kweli Yeye humaliza kazi Anayoianza. Kunazo hatua na mpango, na umejaa hekima ya Mungu, kudura Yake, na matendo Yake ya ajabu. Umejaa pia upendo na rehema za Mungu. Bila shaka, uzi mkuu unaotiririka katika kazi yote ya Mungu ni utunzaji Wake kwa binadamu; umejawa na hisia Zake za kujali ambazo Hawezi kuweka pembeni. Katika aya hizi za Biblia, katika kila kitu ambacho Bwana Yesu alifanya baada ya kufufuka Kwake, kile kilichofichuliwa kilikuwa ni matumaini yasiyobadilika ya Mungu na kujali Kwake kwa wanadamu, pamoja na utunzaji wa Mungu wenye umakinifu na kuwathamini wanadamu. Mpaka sasa hakuna chochote kati ya hivi vyote ambacho kimebadilika—unaweza kukiona? Unapoviona hivi, moyo wako haugeuki bila kusukumwa na kuwa karibu na Mungu? Kama uliishi katika enzi hiyo na Bwana Yesu Akakuonekania baada ya kufufuka Kwake, kwa njia ya kushikika ili wewe uweze kuona, na kama Aliketi mbele yako, Akala mkate na samaki na kukuchambulia wewe maandiko, Akaongea na wewe, basi ungehisi vipi? Ungehisi furaha? Je, ungehisi kuwa mwenye hatia? Kutoelewana kwa awali na kuepuka Mungu kwa awali, migogoro na shaka dhidi ya Mungu—hivi vyote havingetoweka tu? Je, unadhani kwamba uhusiano kati ya binadamu na Mungu ungekuwa bora zaidi?

Kupitia kwa ufasiri wa sura hizi finyu za Biblia, uligundua makosa yoyote katika tabia ya Mungu? Uligundua uchafuzi wowote katika upendo wa Mungu? Uliuona udanganyifu au uovu wowote katika kudura ya Mungu au hekima? Bila shaka la! Sasa unaweza kusema kwa uhakika kwamba Mungu ni mtakatifu? Unaweza kusema kwa uhakika kwamba hisia za Mungu zinafichua kiini Chake na tabia kwa ujumla? Natumai kwamba baada ya kuyasoma maneno haya, kile ambacho umeelewa kutoka katika maneno haya kitakusaidia na kukufaidi katika ufuatiliaji wako wa mabadiliko katika tabia na hali ya kumcha Mungu. Natumai pia kwamba maneno haya yataweza kukuzalia matunda ambayo yatakua kila siku, hivyo basi katika mchakato wa ufuatiliaji huu kukuleta karibu na Mungu zaidi na zaidi, wa kukuleta karibu na karibu zaidi na kiwango ambacho Mungu anahitaji, ili usichoke tena na ufuatiliaji wa ukweli na usihisi tena kwamba ufuataji wa ukweli na ule wa mabadiliko katika tabia ni usumbufu au jambo duni. Ni, kwa kweli, udhihirisho wa tabia ya kweli ya Mungu na kiini kitakatifu cha Mungu ambayo yanakupa motisha kutamani mwangaza, kutamani haki, na kuazimia kufuatilia ukweli, kufuatilia ridhaa ya mapenzi ya Mungu, na kuwa binadamu anayepatwa na Mungu, na kuwa mtu halisi.

Leo tumezungumzia baadhi ya mambo ambayo Mungu alifanya katika Enzi ya Neema wakati ambapo Alikuwa mwili kwa mara ya kwanza. Kutoka kwa mambo haya, tumeona tabia ambayo Alionyesha na kuifichua katika mwili, pamoja na kila kipengele cha kile Alicho nacho na kile Alicho. Vipengele hivi vyote vya kile Alicho nacho na kile Alicho vinaonekana kuhisishwa mno, lakini uhalisi ni kwamba kiini cha kila Alichofichua na kuonyesha hakiwezi kutenganishwa na tabia Yake mwenyewe. Kila mbinu na kila dhana ya Mungu mwenye mwili inaonyesha tabia Yake katika ubinadamu na imeunganishwa bila kutenganishwa katika kiini Chake Mwenyewe. Hivyo, ni muhimu sana kwamba Mungu alikuja kwa wanadamu kwa njia ya kuwa mwili na kazi aliyofanya katika mwili ni muhimu sana pia. Na, tabia Aliyoifichua na mapenzi Alionyesha ni muhimu hata sana kwa kila mtu anayeishi katika mwili, kwa kila mtu anayeishi katika upotovu. Je, hili ni jambo ambalo unaweza kuelewa? Baada ya kuelewa tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho, umefanya hitimisho lolote kuhusiana na namna unavyofaa kumtunza Mungu? Katika kulijibu swali hili, kwa hitimisho Ningependa kukupa onyo tatu: Kwanza, usimjaribu Mungu. Haijalishi ni kiasi kipi unachoelewa kuhusu Mungu, haijalishi ni kiwango kipi unachojua kuhusu tabia Yake, kwa vyovyote vile usimjaribu Yeye. Pili, usishindane na Mungu kuhusiana na hadhi. Haijalishi ni aina gani ya hadhi ambayo Mungu anakupa au ni kazi ya aina gani Anayokuaminia kuifanya, haijalishi ni wajibu wa aina gani ambao Atakuinua ili utende, na haijalishi ni kiasi kipi ambacho umegharimika au kujitolea kwa ajili Mungu, kwa vyovyote vile usishindane na Mungu kwa hadhi. Tatu, usishindane na Mungu. Haijalishi kama unaelewa au kama unaweza kutii kile ambacho Mungu anafanya na wewe, kile Anachopanga na wewe, na mambo Anayokuletea wewe, kwa vyovyote vile usishindane na Mungu. Kama unaweza kutekeleza onyo hizi tatu, basi utakuwa salama kwa kiasi fulani, na hutamghadhabisha Mungu kwa urahisi. Hayo ndiyo yote ya kushiriki kwa siku ya leo.

Novemba 23, 2013

Tanbihi:

a. “Laana ya kukaza na mshipi” ni laana inayotumiwa na mtawa Tang Sanzang katika riwaya ya Kichina iitwayo Safari kwenda Magharibi. Anatumia laana hii kumdhibiti Sun Wukong kwa kukaza mshipi wa chuma kwenye kichwa chake, ukimpa maumivu makali ya kichwa, na hivyo kumdhibiti. Imekuwa istiara ya kuelezea kitu kinachomfunga mtu.

b. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.

Iliyotangulia: Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II

Inayofuata: Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp