Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I

Leo tunawasiliana kuhusu mada muhimu. Hii ni mada ambayo imezungumziwa tangu kuanza kwa kazi ya Mungu mpaka sasa, na inayo umuhimu mkuu kwa kila mtu. Kwa maneno mengine, hili ni suala ambalo kila mmoja atakutana nalo kwenye mchakato wote wa kusadiki kwake katika Mungu na suala ambalo lazima lizungumziwe. Ni suala muhimu, lisiloepukika ambalo mwanadamu hawezi kujitenganisha nalo. Tukizungumzia umuhimu, ni nini kitu muhimu zaidi kwa kila muumini katika Mungu? Baadhi ya watu wanafikiri kwamba kitu muhimu zaidi ni kuyaelewa mapenzi ya Mungu; baadhi wanasadiki ni muhimu zaidi kula na kunywa maneno ya Mungu; baadhi wanahisi kitu muhimu zaidi ni kujijua wenyewe; wengine wanayo maoni kwamba kitu muhimu zaidi ni kujua namna ya kupata wokovu kupitia kwa Mungu, namna ya kumfuata Mungu, na namna ya kuyatimiza mapenzi ya Mungu. Tutayaweka masuala haya yote pembeni kwa leo. Hivyo basi ni nini tunachozungumzia? Tunazungumzia mada kuhusu Mungu. Je, hii ndiyo mada muhimu zaidi kwa kila mtu? Maudhui ya mada kuhusu Mungu ni yapi? Bila shaka, mada hii haiwezi kamwe kutenganishwa na tabia ya Mungu, kiini cha Mungu na kazi ya Mungu. Hivyo leo, hebu tuzungumzie “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe.”

Tangu wakati binadamu walipoanza kumsadiki Mungu, wamekuwa wakikutana na mada kama vile kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe. Inapokuja kwa kazi ya Mungu, baadhi ya watu watasema: “Sisi ndio tunaofanyiwa kazi ya Mungu; tunaipitia kila siku, na hivyo basi tumezoeana nayo.” Na kuhusiana na tabia ya Mungu, baadhi ya watu watasema: “Tabia ya Mungu ni mada tunayoisoma, kuchunguza, na kuzingatia katika maisha yetu yote, hivyo basi tunafaa kuzoeana nayo.” Na kama ni Mungu Mwenyewe, baadhi ya watu watasema: “Mungu Mwenyewe ndiye tunayemfuata, tuliye na imani Kwake, na ndiye tunayemfuata, hivyo tumejuzwa pia kuhusu Yeye.” Mungu hajawahi kukomesha kazi Yake tangu uumbaji, wakati wote huu Ameendelea kuonyesha tabia Yake na kutumia njia mbalimbali kuonyesha neno Lake. Wakati huohuo, hajawahi kusita kujionyesha Yeye Mwenyewe na kiini Chake kwa mwanadamu, akionyesha mapenzi Yake kwa binadamu na kile Anachohitaji kutoka kwa huyo binadamu. Hivyo kutoka katika mtazamo wa moja kwa moja, mada hizi hazifai kuwa za kigeni kwa yeyote yule. Kwa watu wanaomfuata Mungu leo, hata hivyo, Kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe kwa hakika ni mambo ambayo hayajulikani kwao. Kwa nini hali iko hivi? Kwa kadri binadamu anapopitia kazi ya Mungu, anawasiliana pia na Mungu, na kuwafanya kuhisi ni kana kwamba wanaelewa tabia ya Mungu au wanajua sehemu kidogo kuhusu vile inavyofanana. Hivyo basi, binadamu hafikiri kuwa yeye ni mgeni katika kazi ya Mungu au tabia ya Mungu. Badala yake, binadamu anafikiri ni mwenyeji kabisa na Mungu na anaelewa mengi kuhusu Mungu. Lakini kulingana na hali ya sasa, uelewa wa watu wengi kumhusu Mungu umezuiliwa katika kile walichosoma vitabuni, na upana mfinyu wa kile walichopitia wao binafsi, wakiwa wamezuiliwa na kufikiria kwao, na zaidi ya yote, ukiwa umewekewa mipaka ya ukweli wanaoweza kuona kwa macho yao binafsi. Haya yote yapo mbali sana na Mungu Mwenyewe wa kweli. Sasa huu umbali upo “mbali” vipi? Pengine binadamu mwenyewe hana hakika, au pengine binadamu anayo dhana, ana fununu kiasi—lakini kwake Mungu Mwenyewe, uelewa wa binadamu kumhusu Yeye u mbali sana na kiini cha Mungu Mwenyewe wa kweli. Hii ndiyo maana tunahitajika kutumia mada kama “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe” ili kuwasilisha ujumbe huu hatua kwa hatua na kwa njia mahususi.

Kwa hakika, tabia ya Mungu iko wazi kwa kila mmoja na haijafichwa, kwa sababu Mungu hajawahi kuepuka kimakusudi mtu yeyote na Hajawahi kimakusudi kujaribu kujificha Mwenyewe ili watu wasiweze kumjua Yeye au kumwelewa Yeye. Tabia ya Mungu siku zote imekuwa wazi na siku zote imekuwa ikitazama kila mtu kwa njia ya uwazi. Katika usimamizi wa Mungu, Mungu hufanya kazi Yake akitazama kila mmoja; na kazi Yake ndiyo inafanywa kwa kila mtu. Anapofanya kazi hii, Anafichua bila kusita tabia Yake, huku Akitumia bila kusita kiini Chake na kile Anacho na alicho kuongoza na kukimu kila mmoja. Katika kila enzi na kila awamu, licha ya kama hali ni nzuri au mbaya, tabia ya Mungu siku zote iko wazi kwa kila mtu binafsi, na vile vitu Anavyomiliki na uwepo Wake siku zote viko wazi kwa kila mtu binafsi, kwa njia sawa kwamba maisha Yake yanamtoshelezea mwanadamu kila wakati na bila kusita na kumsaidia mwanadamu. Licha ya haya yote, tabia ya Mungu inabakia fiche kwa baadhi ya watu. Kwa nini iko hivyo? Ni kwa sababu ingawaje watu hawa wanaishi ndani ya kazi ya Mungu na wanamfuata Mungu, hawajawahi kutafuta kuelewa Mungu au kutaka kumjua Mungu, sikwambii hata kumkaribia Mungu. Kwa watu hawa, kuelewa tabia ya Mungu kunamaanisha mwisho wao wawadia; kwa maanisha karibu wanahukumiwa na kushtakiwa na tabia ya Mungu. Hivyo basi, watu hawa hawajawahi kutamani kuelewa Mungu au tabia Yake, na hawatamani uelewa au maarifa ya kina ya mapenzi ya Mungu. Hawanuii kufahamu mapenzi ya Mungu kupitia ushirikiano wa kimakusudi—wanafurahia tu milele na hawachoki kufanya mambo wanayotaka kuyafanya; kusadiki kwa Mungu wanayetaka kusadiki Kwake; kusadiki kwa Mungu aliyepo tu katika fikira zao, Mungu aliyepo tu katika dhana zao; na kusadiki kwa Mungu asiyeweza kutenganishwa na wao katika maisha yao ya kila siku. Na kwake Mungu Mwenyewe wa kweli, wanapuuza kabisa, hawataki kusikia mambo ya Mungu na hawana tamanio la kumwelewa Yeye, kumtilia maanani Yeye, sembuse kuwa na tamanio la kuwa karibu zaidi na Yeye. Wanayatumia tu maneno ambayo Mungu anayaonyesha ili kuweza kujirembesha, kujiandaa upya. Kwa wao, hilo tayari linawafanya kuwa waumini wenye mafanikio na watu walio na imani kwa Mungu ndani ya mioyo yao. Ndani ya mioyo yao, wanaongozwa na kufikiria kwao, dhana zao, na hata ufasili wao binafsi wa Mungu. Mungu Mwenyewe wa kweli, kwa mkono mwingine, hana chochote kuhusiana na wao. Kwa sababu pindi wanapomwelewa Mungu Mwenyewe wa kweli, kuelewa tabia ya Mungu ya kweli, na kuelewa kile Mungu anacho na alicho, hii inamaanisha kwamba vitendo vyao, imani yao, na yale yote wanayoyafuatilia yatashutumiwa. Na ndiyo maana hawako radhi kukielewa kiini cha Mungu, na ndiyo maana wanasitasita na hawako radhi kutafuta kwa bidii au kuomba kumwelewa zaidi Mungu, kupata kujua zaidi kuhusu mapenzi Yake Mungu, na kuelewa kwa njia bora zaidi tabia ya Mungu. Afadhali Mungu kwao awe kitu kilichotungwa, kitu kisicho na chochote na kisicho dhahiri. Afadhali kwao Mungu awe mtu ambaye yupo hasa vile ambavyo wamemfikiria Yeye, Anayeweza kunyenyekea mbele zao, Asiyeishiwa na ujazo na Anayepatikana siku zote. Wanapotaka kufurahia neema ya Mungu, wanamuomba Mungu kuwa hiyo neema. Wanapohitaji baraka za Mungu, wanamuomba Mungu kuwa baraka hizo. Wanapokabiliwa na dhiki, wanamwomba Mungu kuwatia wao moyo, na kuwa usalama wao. Maarifa ya watu hawa kumhusu Mungu imebakia palepale pa mipaka ya neema na baraka. Uelewa wao wa kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na Mungu umezuiliwa pia na kufikiria kwao na vilevile barua na mafundisho ya kidini tu. Lakini wapo baadhi ya watu walio na hamu ya kuielewa tabia ya Mungu, wanaotaka kumwona Mungu Mwenyewe kwa kweli, na kuielewa tabia ya Mungu kwa kweli na kile Anacho na alicho. Watu hawa wanautafuta uhalisia wa ukweli na wokovu wa Mungu na wanatafuta kupokea ushindi, wokovu, na utimilifu wa Mungu. Watu hawa wanaitumia mioyo yao kulisoma neno la Mungu, wanaitumia mioyo yao kuthamini hali na kila mtu, tukio, au kitu ambacho Mungu amewapangia, na kuomba na kutafuta kwa uaminifu. Kile wanachotaka zaidi ni kuyajua mapenzi ya Mungu na kuielewa tabia ya kweli na kiini cha Mungu. Hivi ndivyo ilivyo ili wasiweze tena kumkosea Mungu, na kupitia kwa mambo waliyoyapitia, waweze kuona upendo zaidi wa Mungu na upande Wake wa kweli. Iko hivyo pia ili Mungu halisi na wa kweli ataweza kuwepo ndani ya mioyo yao, na ili Mungu atakuwa na nafasi katika mioyo yao, kiasi cha kwamba hawatakuwa wakiishi tena miongoni mwa kufikiria, dhana, au hali ya kuyaepuka mambo. Kwa watu hawa, sababu inayowafanya kuwa na tamanio kuu la kuielewa tabia ya Mungu na kiini Chake ni kwa sababu tabia ya Mungu na kiini Chake ni mambo ambayo mwanadamu anaweza kuyahitaji wakati wowote katika uzoefu wao, mambo yanayojaza uhai katika maisha yao yote walioishi. Pindi wanapoielewa tabia ya Mungu, wataweza kumheshimu sana kwa njia bora zaidi, kushirikiana kwa njia bora zaidi na kazi ya Mungu, na kuyaweka zaidi katika fikira mapenzi ya Mungu na kutekeleza wajibu wao kwa njia bora zaidi wakitumia uwezo wao. Hawa ndio watu wa aina mbili inapokuja katika mielekeo yao kwa tabia ya Mungu. Watu wa aina ya kwanza hawataki kuielewa tabia ya Mungu. Ingawaje wanasema wanataka kuielewa tabia ya Mungu, kupata kumjua Mungu Mwenyewe, kuona kile Mungu anacho na alicho, na kushukuru kwa dhati mapenzi ya Mungu, ndani yao kabisa wanaona afadhali Mungu asikuwepo. Ni kwa sababu watu wa aina hii wanakosa kumtii Mungu kila wakati na wanampinga; wanapigana na Mungu kwa sababu ya vyeo vilivyo ndani ya mioyo yao na mara nyingi wanashuku na hata kukataa uwepo wa Mungu. Hawataki kuruhusu tabia ya Mungu au kuacha Mungu mwenyewe wa kweli kumiliki mioyo yao. Wanataka tu kutosheleza matamanio, kufikiria, na maono yao binafsi. Hivyo basi, watu hawa wanaweza kumsadiki Mungu, kumfuata Mungu, na hata wanaweza kutupilia mbali familia na kazi zao kwa sababu Yake Yeye, lakini hawasitishi njia zao za maovu. Baadhi yao hata huiba au kubadhiri sadaka au kumlaani Mungu kisirisiri, huku wengine wakiweza kutumia vyeo vyao kushuhudia mara kwa mara kuhusu wao wenyewe, kujiongezea zaidi umaarufu wao, na kushindana na Mungu kwa ajili ya watu na hadhi. Wanatumia mbinu na njia mbalimbali kuwafanya watu kuwaabudu, kujaribu mara kwa mara kuwa na ufuasi mkubwa wa watu na kutaka kuwadhibiti watu hao. Baadhi hata hupotosha kimakusudi watu na kuwafanya kufikiria kwamba wao ni Mungu ili waweze kuchukuliwa kama Mungu. Hawawezi katu kuwaambia watu kwamba wamepotoshwa, kwamba pia wao wamepotoka na wana kiburi, na hivyo basi hawafai kuwaabudu, na kwamba haijalishi watafanya vyema kiasi kipi, haya yote ni kutokana na utukuzaji wa Mungu na kile wanachostahili kufanya kwa kweli. Kwa nini hawasemi mambo haya? Kwa sababu wana hofu kuu ya kupoteza nafasi yao ndani ya mioyo ya watu. Hii ndiyo maana watu kama hao hawamtukuzi Mungu katu na katu hawamshuhudii Mungu, kwani hawajawahi kujaribu kumwelewa Mungu. Wanaweza kumjua Mungu kama hawamwelewi? Haiwezekani! Hivyo, ingawa maneno katika mada “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe” yanaweza kuwa rahisi, maana yao ni tofauti kwa kila mmoja. Kwa mtu anayekosa kumtii Mungu mara kwa mara, na anampinga Mungu na ni mkatili kwa Mungu, maneno hayo yanabashiri shutuma; ilhali mtu anayefuatilia uhalisi wa kweli na mara nyingi anakuja mbele ya Mungu kutafuta mapenzi ya Mungu atayachukulia maneno hayo kama kawaida yake. Hivyo kuwa wale walio miongoni mwenu, wanaposikiza mazungumzo ya tabia ya Mungu na kazi ya Mungu, wanaanza kuumwa na kichwa, mioyo yao inajaa upinzani, na wanakuwa katika hali isiyo na utulivu kabisa. Lakini kuna wengine miongoni mwenu wanaofikiria: Mada hii ndiyo hasa Ninayohitaji, kwa sababu mada hii ni yenye manufaa sana kwangu. Ni sehemu ambayo haiwezi kukosekana katika uzoefu wangu wa maisha; ni swali ambalo halijapata jibu bado, msingi wa imani kwa Mungu, na jambo ambalo mwanadamu hawezi kufikiria kuliacha. Kwenu nyote, mada hii inaweza kuonekana kuwa karibu na mbali, isiyojulikana ilhali inayozoeleka. Lakini haijalishi ni nini, hii ni mada ambayo kila mmoja lazima aisikilize, aijue, na lazima aielewe. Haijalishi ni vipi utakavyoishughulikia, haijalishi ni vipi utakavyoiangalia au utakavyoipokea, lakini umuhimu wa mada hii huwezi kupuuzwa.

Mungu amekuwa akifanya kazi Yake tangu Awaumbe wanadamu. Mwanzoni, ilikuwa kazi rahisi sana, lakini licha ya urahisi wake, ingali ilikuwa na maonyesho ya kiini na tabia ya Mungu. Ingawa kazi ya Mungu sasa imepandishwa daraja, na Yeye akitia kiwango kikubwa mno cha kazi thabiti kwa kila mmoja anayemfuata Yeye, na kuonyesha kiwango kikubwa cha neno Lake, kuanzia mwanzo hadi sasa, nafsi ya Mungu imekuwa ikifichwa kutoka kwa mwanadamu. Ingawaje amekuwa mwili mara mbili, kuanzia wakati wa simulizi za biblia hadi kwa siku za kisasa, nani amewahi kuona nafsi halisi ya Mungu? Kutokana na uelewa wenu, yupo mtu amewahi kuona nafsi halisi ya Mungu? La. Hakuna aliyewahi kuona nafsi halisi ya Mungu, kumaanisha hakuna aliyewahi kuona nafsi ya kweli ya Mungu. Hili ni jambo ambalo kila mmoja anakubaliana nalo. Hivi ni kusema, nafsi halisi ya Mungu, au Roho wa Mungu, amefichwa kutoka kwa binadamu wote, wakiwemo Adamu na hawa, ambao Aliwaumba, na akiwemo Ayubu mwenye haki, ambaye alikuwa Amemkubali. Hata wao hawakuona nafsi halisi ya Mungu. Lakini kwa nini Mungu anaficha kimakusudi nafsi Yake halisi? Baadhi ya watu husema: “Mungu anaogopa kuwaogofya watu.” Wengine husema: “Mungu huficha nafsi Yake halisi kwa sababu binadamu ni mdogo sana na Mungu ni mkubwa sana; wanadamu hawaruhusiwi kumwona Yeye, la sivyo watakufa.” Wapo pia wale wanaosema: “Mungu ameshughulika sana akisimamia kazi Yake kila siku, huenda Asiwe na muda wa kuonekana na kuruhusu watu kumwona Yeye.” Haijalishi ni nini mnachosadiki, Ninayo hitimisho hapa. Hitimisho hilo ni nini? Ni kwamba Mungu hataki hata watu kuona nafsi Yake halisi. Akiwa amefichwa kutoka kwa binadamu ni kitu ambacho Mungu anafanya kimakusudi. Kwa maneno mengine, ni nia ya Mungu kwa watu kutoona nafsi Yake halisi. Hili linafaa kuwa wazi kwa wote sasa. Kama Mungu hajawahi kuonyesha nafsi Yake kwa yeyote, basi mnafikiria nafsi ya Mungu ipo? (Ipo.) Bila shaka ipo. Uwepo wa nafsi ya Mungu haupingiki. Lakini kuhusu nafsi ya Mungu ni kubwa vipi au inafanana vipi, haya ni maswali ambayo mwanadamu anafaa kuchunguza? La. Jibu ni la. Kama nafsi ya Mungu si mada ambayo tunafaa kuchunguza, basi ni swali lipi ambalo tunafaa kuchunguza? (Tabia ya Mungu.) (Kazi ya Mungu.) Kabla hatujaanza kuwasiliana mada hii rasmi, hata hivyo, hebu turudi katika kile tulichokuwa tukikizungumzia muda mfupi uliopita: Kwa nini Mungu hajawahi kuonyesha nafsi Yake kwa mwanadamu? Kwa nini Mungu anaficha kimakusudi nafsi Yake kutoka kwa mwanadamu? Kunayo sababu moja tu, nayo ni: Ingawaje binadamu aliyeumbwa amepitia miaka elfu na elfu ya kazi ya Mungu, hakuna hata mtu mmoja anayejua kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na kiini cha Mungu. Watu kama hao, mbele ya macho ya Mungu, ni upinzani kwake Yeye, na Mungu hatajionyesha kwa watu walio wakatili kwake Yeye. Hii ndiyo sababu ya pekee mbona Mungu hajawahi kumwonyesha binadamu nafsi Yake na ndiyo sababu anaikinga yeye kimakusudi nafsi Yake dhidi yao. Sasa mnaelewa kuhusu umuhimu wa kujua tabia ya Mungu?

Tangu kuwepo kwa usimamizi wa Mungu, siku zote amejitolea kabisa katika kutekeleza kazi Yake. Licha ya kuficha nafsi Yake kutoka kwao, siku zote Amekuwa katika upande wa binadamu, akiwafanyia kazi, akionyesha tabia Yake, akiongoza binadamu wote na kiini Chake, na kufanya kazi Yake kwa kila mmoja kupitia nguvu Zake, hekima Yake, na mamlaka Yake, hivyo akiileta Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na sasa Enzi ya Ufalme katika uwepo. Ingawaje Mungu huificha nafsi Yake kutoka kwa binadamu, tabia Yake, uwepo Wake na miliki Yake, na mapenzi Yake kwa binadamu yanafichuliwa bila wasiwasi wowote kwa binadamu kwa minajili ya kuona na kupitia hali hiyo. Kwa maneno mengine, ingawaje binadamu hawawezi kumwona au kumgusa Mungu, tabia na kiini cha Mungu ambacho binadamu wamekuwa wakigusana nacho ni maonyesho kabisa ya Mungu Mwenyewe. Je, hayo si kweli? Licha ya ni mbinu gani au ni kutoka katika mtazamo gani Mungu hufanya kazi Yake, siku zote Anawatendeakaribisha watu kulingana na utambulisho Wake wa kweli, akifanya kile ambacho Anafaa kufanya na kusema kile Anachofaa kusema. Haijalishi ni nafasi gani Mungu anazungumzia kutoka—Anaweza kuwa amesimama kwenye mbingu ya tatu, au amesimama akiwa mwili Wake, au hata kama mtu wa kawaida—siku zote Anaongea kwa binadamu kwa moyo Wake wote na kwa akili Zake zote, bila uongo na bila ufichaji wowote. Wakati Anapotekeleza kazi Yake, Mungu huonyesha neno Lake na tabia Yake, na huonyesha kile Anacho na alicho, bila kuficha chochote. Anamwongoza mwanadamu na maisha Yake na uwepo Wake na miliki yake. Hivi ndivyo binadamu alivyoishi katika Enzi ya Sheria—enzi asilia ya binadamu—akiongozwa na Mungu asiyeonekana na asiyegusika.

Mungu alipata mwili kwa mara ya kwanza baada ya Enzi ya Sheria, hali ya kupata mwili iliyodumu kwa miaka thelathini na tatu na nusu. Kwa mwanadamu, miaka thelathini na mitatu na nusu ni muda mrefu? (Si mrefu sana.) Kwa sababu urefu wa maisha ya mwanadamu ni mirefu kuliko miaka thelathini na fulani, huu si muda mrefu kwa mwanadamu. Lakini kwa Mungu mwenye mwili, miaka hii thelathini na mitatu na nusu ilikuwa mirefu mno. Aligeuka na kuwa mtu—mtu wa kawaida aliyetekeleza kazi na agizo la Mungu. Hii ilimaanisha kwamba lazima angefanya kazi ambayo mtu wa kawaida asingeweza kufanya, huku akivumilia mateso ambayo binadamu wa kawaida hawezi kuvumilia. Kiwango cha mateso aliyovumilia Bwana Yesu katika Enzi ya Neema, kuanzia mwanzo wa kazi Yake hadi wakati Aliposulubishwa kwenye msalaba, huenda kisiwe ni kitu watu wa leo wangeweza kushuhudia wao binafsi, lakini mnaweza angaa kutambua kiasi kupitia hadithi zilizo kwenye Biblia? Licha ya ni maelezo mangapi yaliyopo kwenye ukweli huu uliorekodiwa, kwa ujumla, kazi ya Mungu katika kipindi hiki kilijaa ugumu na mateso. Kwa mwanadamu aliyepotoka muda wa miaka thelathini na mitatu na nusu si mrefu; mateso kidogo si jambo la kutisha. Lakini kwa Mungu mtakatifu asiye na doa, ambaye lazima avumilie dhambi zote za binadamu, na kula, kulala na kuishi na watenda dhambi, maumivu haya ni mengi mno. Yeye ndiye Muumba, Bwana wa viumbe vyote na Mtawala wa vitu vyote, lakini Alipokuja duniani alilazimika kuvumilia unyanyasaji na ukatili wa wanadamu waliopotoka. Ili kuikamilisha kazi Yake na kuokoa binadamu kutoka kwa taabu, Alilazimika kushutumiwa na binadamu, na kuvumilia dhambi za wanadamu wote. Kiwango cha mateso aliyopitia hakiwezi kwa kweli kueleweka au kutambulika na watu wa kawaida. Mateso haya yanawakilisha nini? Yanawakilisha Mapenzi ya Mungu kwa wanadamu. Yanasimamia udhalilishaji Alioteseka na gharama Aliyolipia kwa sababu ya wokovu wa binadamu, kukomboa dhambi zake, na kukamilisha awamu hii ya kazi Yake. Yanamaanisha binadamu angekombolewa kutoka katika msalaba na Mungu. Hii ndiyo gharama iliyolipwa kwa damu, kwa maisha, gharama ambayo viumbe walioumbwa hawawezi kumudu. Ni kwa sababu Anacho kiini cha Mungu na Amejihami na kile Mungu anacho na alicho, ndiyo maana Anaweza kuvumilia aina hii ya mateso na aina hii ya kazi. Hili ni jambo ambalo hakuna kiumbe aliyeumbwa anaweza kufanya badala Yake. Hii ni kazi ya Mungu katika Enzi ya Neema na ufunuo wa tabia Yake. Je, hii inafichua chochote kuhusu kile Mungu anacho na alicho? Je, wanadamu wanastahili kuijua? Katika enzi hiyo, japokuwa mwanadamu hakuiona nafsi ya Mungu, alipokea sadaka ya Mungu dhidi ya dhambi zake na akakombolewa kutoka kwenye msalaba na Mungu. Huenda mwanadamu awe amezoeana na kazi aliyofanya Mungu katika Enzi ya Neema, lakini yupo yeyote aliyezoeana na tabia na mapenzi yalionyeshwa na Mungu katika kipindi hiki? Binadamu anajua tu kuhusu maudhui ya kazi ya Mungu katika enzi tofauti katika vipindi mbalimbali, au anajua hadithi zinazohusiana na Mungu zilizofanyika kwa wakati mmoja na ule Mungu alikuwa akitekeleza kazi Yake. Maelezo haya na hadithi ni kwa ukweli zaidi taarifa fulani tu au hadithi za kumbukumbu kuhusu Mungu na vyote hivi havina chochote kuhusiana na tabia na kiini cha Mungu. Hivyo haijalishi ni hadithi ngapi watu wanajua kuhusu Mungu, haimaanishi kwamba wanao uelewa wa kina na maarifa kuhusu tabia ya Mungu au kiini Chake. Kama vile katika Enzi ya Sheria, ingawaje watu kutoka Enzi ya Neema walikuwa wamepitia mtagusano wa karibu sana na wa kikweli na Mungu wa mwili, maarifa yao kuhusu Mungu na kiini cha Mungu yalikuwa kweli mambo yasiyokuwepo.

Katika Enzi ya Ufalme, Mungu akawa mwili tena, kwa njia sawa na ile Aliyotumia mara ya kwanza. Katika kipindi hiki cha kazi, Mungu angali anaonyesha bila kusita neno Lake, anafanya kazi anayofaa kufanya na kuonyesha kile Anacho na alicho. Wakati huohuo, Anaendelea kuvumilia na kustahili na kutotii na kutojua kwa binadamu. Je, Mungu hafichui kila wakati tabia Yake na kuonyesha mapenzi yake katika kipindi hiki cha kazi pia? Hivyo basi, kuanzia uumbaji wa binadamu hadi sasa, tabia ya Mungu, nafsi Yake na miliki Zake, na mapenzi Yake, siku zote yamekuwa wazi kwa kila mmoja. Mungu hajawahi kuficha kimakusudi kiini Chake, tabia Yake au mapenzi Yake. Ni vile tu mwanadamu hajali kuhusu kile ambacho Mungu anafanya, mapenzi Yake ni yapi—ndio maana uelewa wa binadamu kumhusu Mungu ni finyu mno. Kwa maneno mengine, wakati Mungu anaficha nafsi Yake, Yeye pia Anasimama kando ya mwanadamu kila wakati, akionyesha waziwazi mapenzi Yake, tabia Yake na kiini chake halisi siku zote. Kimsingi, nafsi ya Mungu pia iko wazi kwa watu lakini kutokana na upofu na kutotii kwa binadamu, siku zote hawawezi kuuona kuonekana kwa Mungu. Hivyo kama hali iko hivyo, basi si kuelewa tabia ya Mungu na Mungu Mwenyewe kunafaa kuwa rahisi mno kwa kila mmoja? Hili ni swali gumu sana kujibu, sivyo? Mnaweza kusema ni rahisi, lakini wakati watu wengine wanatafuta kumjua Mungu, hatimaye hawamjui Yeye au kupata uelewa wa wazi kumhusu Yeye—siku zote ni jambo lililojaa ukungu na lisiloeleweka. Lakini mkisema si rahisi, hilo si sahihi vilevile. Baada ya kuwa mlengwa wa kazi ya Mungu kwa muda mrefu, kila mmoja anafaa, kupitia uzoefu wake, kuwa amepitia kwa kweli mambo mbalimbali na Mungu. Anafaa kuwa amehisi Mungu angalau kwa kiwango fulani katika moyo wake au awe amekuwa na mawasiliano ya kiroho na Mungu, na anafaa angalau kuwa alikuwa na ufahamu kiasi tambuzi kuhusu tabia ya Mungu au kupata uelewa fulani kumhusu Yeye. Kuanzia wakati binadamu alianza kumfuata Mungu hadi sasa, mwanadamu amepokea mengi mno, lakini kutokana na sababu za aina zote—uhodari wa kimasikini ya kibinadamu, kutojua, uasi, na nia mbalimbali—wanadamu wamepoteza mambo mengi mno. Je, Mungu hajampatia mwanadamu mali ya kutosha? Ingawaje Mungu huficha nafsi Yake kutoka kwa wanadamu, Anawatosheleza mahitaji yao kwa kile Anacho na alicho, na hata maisha Yake; maarifa ya binadamu ya Mungu hayafai kuwa vile yalivyo tu sasa. Ndiyo maana Nafikiri inahitajika kuwa na ushirika zaidi na nyinyi kuhusu mada ya kazi ya Mungu, kuhusu tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe. Kusudio ni ili miaka elfu ya utunzaji na fikira ambayo Mungu amemwagia binadamu isije ikaisha bure bilashi, na ili mwanadamu aweze kuelewa kwa dhati na kutambua mapenzi ya Mungu kwake. Ni ili watu waweze kusonga mbele kwenye hatua mpya ya maarifa yao kumhusu Mungu. Itaweza pia kumrudisha Mungu katika nafasi Yake inayofaa kwenye mioyo ya watu yaani kumfanyia Yeye haki.

Ili kuelewa tabia ya Mungu na Mungu Mwenyewe lazima muanzie na jambo dogo sana. Jambo hilo dogo sana mnalopaswa kuanzia ni nini? Kwanza kabisa, Nimezikusanya baadhi ya sura kutoka kwenye Biblia. Taarifa iliyo hapa chini inayo mistari ya Biblia, ambayo yote inahusiana na mada ya tabia ya Mungu, kazi ya Mungu na Mungu Mwenyewe. Nilipata dondoo hizi mahususi kama nyenzo za marejeleo ili kuwasaidia kujua kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe. Hapa Nitayashiriki nanyi ili muweze kuona ni aina gani ya tabia na kiini cha Mungu ambacho kimefichuliwa kupitia kwa kazi Yake ya kitambo lakini watu hawajui kukihusu. Sura hizi zinaweza kuwa nzee, lakini mada tunayowasiliana ni kitu kipya ambacho watu hawana na hawajawahi kusikia. Baadhi yenu huenda mkapata hazieleweki—je, kule kuwataja Adamu na Hawa na kurudi kwa Nuhu si kurudia hatua sawa tena? Haijalishi ni nini mnafikiria, sura hizi ni zenye manufaa kwa mawasiliano ya mada hii na zinaweza kutumika kama maandishi ya mafunzo au nyenzo za matumizi ya kwanza katika ushirika wa leo. Mtaelewa nia Zangu za kuchagua sehemu hizi kufikia wakati Nitakapoumaliza ushirika huu. Wale ambao wamesoma Biblia awali huenda wameona mistari hii michache lakini huenda hawajaelewa. Hebu tuangalie haraka kwanza kabla ya kupitia mistari hii mmoja baada ya mwingine kwa kina zaidi.

Adamu na Hawa ni mababu wa mwanadamu. Kama itabidi tutaje wahusika kutoka kwenye Biblia, basi lazima tuanzie na wawili hawa. Kisha Nuhu, mababu wa pili wa mwanadamu. Mhusika wa tatu ni nani? (Ibrahimu.) Je, nyote mnaijua hadithi ya Ibrahimu? Baadhi yenu mnaweza kuijua, lakini kwa baadhi yenu huenda isiwe wazi sana. Nani ndiye mhusika wa nne? Ni nani anayetajwa kwenye hadithi ya kuangamizwa kwa Sodoma? (Lutu.) Lakini Lutu hajarejelewa hapa. Ni nani anayerejelewa? (Ibrahimu.) Kitu kikuu kilichotajwa kwenye hadithi ya Ibrahimu ni kile Yehova Mungu alikuwa amesema. Je mnaona haya? Nani ndiye mhusika wa tano? (Ayubu.) Je, Mungu hataji mengi kwenye hadithi ya Ayubu wakati wa awamu hii ya kazi Yake? Basi mnajali sana kuhusu hadithi hii? Kama mnajali sana, je mmeisoma hadithi ya Ayubu kwenye Biblia kwa umakinifu? Je, mnajua ni mambo gani Ayubu alisema, ni mambo gani aliyofanya? Wale ambao wameisoma hadithi hiyo sana, ni mara ngapi mmeisoma? Je, mnaisoma mara kwa mara? Akina dada kutoka Hong Kong, tafadhali tuambieni. (Mimi niliisoma mara kadhaa hapo awali tulipokuwa katika Enzi ya Neema.) Hamjawahi soma tena tangu hapo? Kama ni hivyo, basi hiyo ni aibu kubwa. Wacha Niwaambie: Katika awamu hii ya kazi ya Mungu Alimtaja Ayubu mara nyingi, na hilo ni onyesho la nia Zake. Kwamba Alimtaja Ayubu mara nyingi lakini umakini wenu haukuzinduliwa ni thibitisho kwa ukweli kwamba: Hamna haja ya kuwa watu ambao ni wazuri na watu wanaomcha Mungu na kujiepusha na maovu. Hii ni kwa sababu mnatosheka tu na kuwa na wazo la juujuu kuhusu hadithi ya Ayubu iliotajwa na Mungu. Mnatosheka na uelewa wa juujuu wa hadithi yenyewe, lakini hamjali kuhusu na hamtaki kufahamu maelezo ya Ayubu ni nani na kusudio linalomfanya Mungu kumrejelea Ayubu mara kadhaa. Kama hata hamjali mtu kama huyo ambaye Mungu amesifu, basi ni nini hasa mnayotilia maanani? Kama hamjali kuhusu na hamjaribu kuelewa mhusika muhimu sana kama huyu ambaye Mungu amemtaja, basi hiyo inasema nini kuhusu mwelekeo wenu katika neno la Mungu? Hilo si jambo baya? Je, hiyo haithibitishi kwamba wengi wenu hawajihusishi katika mambo ya kimatendo na nyinyi nyote hamfuatilii ukweli? Kama unafuatilia ukweli, utatilia maanani kwa lazima watu ambao Mungu ameidhinisha na hadithi za wahusika ambazo Mungu amezungumzia. Haijalishi kama unaweza kutenda yanavyohitaji au kuona kuwa hadithi zake ni dhahiri shahiri, utaenda haraka na kuisoma, kujaribu kuifahamu, kupata njia za kufuata mfano wake, na kufanya kile unachoweza kwa uwezo wako bora zaidi. Hiyo ndiyo tabia ya mtu anayetamani ukweli. Lakini ukweli ni kwamba wengi wenu mlioketi hapa hamjawahi kuisoma hadithi ya Ayubu. Hii kwa kweli inaniambia kitu.

Hebu turudi katika mada niliyokuwa Nikizungumzia muda mfupi uliopita. Sehemu hii ya maandiko inayoshughulikia Enzi ya Sheria ya Agano la Kale ni haswa hadithi za wahusika Nilizokuwa nimedondoa. Hizi ni hadithi zilizoeleweka kwa watu wengi ambao wamesoma Biblia. Wahusika hawa ni wawakilishi sana. Wale waliosoma hadithi hizi wataweza kuhisi kwamba kazi ambayo Mungu amewafanyia wao na maneno ambayo Mungu amewazungumzia yanashikika na yanafikika kwa watu wa leo. Unaposoma hadithi hizi na rekodi hizi kutoka kwenye Biblia, utaweza kuelewa namna ambavyo Mungu alivyofanya kazi Yake na namna alivyoshughulikia watu wakati huo. Lakini kusudio la Mimi kutafuta sura hizi leo si eti kwamba uweze kujaribu kung’amua hadithi hizi na wahusika ndani zao. Badala yake, ni ili uweze kupitia kwa hadithi za wahusika hawa, kuona vitendo vya Mungu na tabia Yake, na hivyo kurahisisha kujua na kuelewa Mungu, kuuona upande halisi Wake yeye, kusitisha kufikiria kwako, na kukomesha dhana zako kuhusu Yeye, na kusitisha imani yako na kuitoa katika hali ya kutokuwa na hakika. Kujaribu kuifahamu tabia ya Mungu na kuielewa na kupata kujua Mungu mwenyewe bila ya msingi, kunaweza mara nyingi kukufanya kuhisi kama mtu asiyeweza, asiye na nguvu, na asiye na hakika ni wapi wataanzia. Na ndiyo maana Nilifikiria ni wazo zuri kutumia mbinu kama hii na mtazamo ili kukufanya kumwelewa Mungu kwa njia bora zaidi, na kwa uhalisia zaidi kutambua na kushukuru mapenzi ya Mungu na kupata kuijua tabia ya Mungu na Mungu Mwenyewe na kukufanya kuhisi kwa dhati uwepo wa Mungu na kushukuru mapenzi Yake kwa wanadamu. Je, haya si ya manufaa kwenu? Sasa mnahisi vipi ndani ya mioyo yenu mnapoziangalia hadithi hizi na maandiko haya tena? Je, mnafikiria maandiko haya Niliyoyachukua yamezidi kuliko kawaida? Lazima Nitilie mkazo tena kile Nimetoka tu kuwaambia. Nia ya kuwaruhusu kusoma hadithi hizi za wahusika ni kuwasaidia kuelewa namna ambavyo Mungu anafanya kazi Yake kwa watu na mwelekeo Wake kwa wanadamu. Ni kupitia nini ndipo mtaweza kuelewa haya? Kupitia kwa kazi ambayo Mungu amefanya kitambo, na kuunganisha pamoja na kazi ambayo Mungu anafanya sasa hivi kuwasaidia kuelewa mambo mbalimbali kuhusu Yeye. Mambo haya mbalimbali ni ya kweli, na lazima yajulikane na yatambulike na wote wanaotaka kumjua Mungu.

Tutaanza sasa na hadithi ya Adamu na Hawa. Kwanza, hebu tuyasome maandiko.

A. Adamu na Hawa

1. Amri ya Mungu kwa Adamu

Mwa 2:15-17 Naye Yehova Mungu akamchukua mtu huyo, na kumweka ndani ya bustani ya Edeni ili ailime na kuihifadhi. Yehova Mungu akamwamrisha mtu huyo, akisema, Unaweza kula kwa uhuru matunda kutoka miti yote ya bustani: Lakini kutoka mti wa maarifa ya mema na maovu, usiyale: kwa kuwa katika siku ambapo utakula matunda kutoka mti huo bila shaka utakufa.

Je, mlielewa chochote kutoka kwenye mistari hii? Je, ni vipi ambavyo sehemu hii ya maandiko inavyo wafanya kuhisi? Kwa nini “Amri ya Mungu kwa Adamu” ilidondolewa kutoka kwa maandiko? Je, kila mmoja wenu sasa anayo picha ya Mungu na Adamu katika akili yenu? Mnaweza kujaribu kufikiria: Kama ni nyinyi mliokuwa katika tukio hilo, je, Mungu katika moyo wenu angekuwa vipi? Ni hisia gani ambazo picha hii zinafanya mhisi? Hii ni picha ya kusisimua na ya kutuliza moyo. Ingawaje kunaye Mungu tu na binadamu ndani yake, ule ukaribu kati yao unastahili kuonewa wivu: Upendo mwingi wa Mungu amepewa binadamu kwa ukarimu, unamzunguka binadamu; binadamu ni mnyofu na asiye na hatia, aliye huru kabisa na asiyejali chochote, anayeishi kwa furaha kwa uangalizi wa jicho la Mungu; Mungu anaonyesha hali ya kujali binadamu huku naye binadamu anaishi katika ulinzi na baraka za Mungu; kila kitu binadamu anachofanya na kusema kinaunganishwa kwa karibu na Mungu na hakiwezi kutofautishwa.

Mnaweza kusema kwamba hii ndiyo amri ya kwanza ya Mungu aliyoitoa kwa binadamu tangu kumuumba yeye. Je, amri hii ina nini? Amri hii inayo mapenzi ya Mungu, lakini pia inayo wasiwasi Wake kwa wanadamu. Hii ndiyo amri ya kwanza ya Mungu na pia ndio mara ya kwanza Mungu anakuwa na wasiwasi kuhusu binadamu. Hivi ni kusema, Mungu analo jukumu kwa binadamu tangu ule wakati alipomuumba yeye. Jukumu Lake ni lipi? Lazima amlinde binadamu, kumwangalia binadamu. Anatumai kwamba binadamu anaweza kuamini na kutii maneno Yake. Hili pia ndilo tarajio la kwanza la Mungu kwa binadamu. Na ni kwa tarajio hili kwamba Mungu anasema yafuatayo: “Unaweza kula kwa uhuru matunda kutoka miti yote ya bustani: Lakini kutoka mti wa maarifa ya mema na maovu, usiyale: kwa kuwa katika siku ambapo utakula matunda kutoka mti huo bila shaka utakufa.” Maneno haya rahisi yanawakilisha mapenzi ya Mungu. Yanafichua pia kwamba moyo wa Mungu tayari umeanza kuonyesha hali ya kujali binadamu. Miongoni mwa mambo yote, ni Adamu pekee aliyeumbwa kwa taswira ya Mungu; Adamu alikuwa kiumbe wa pekee aliye hai aliye na pumzi ya uhai ya Mungu; angeweza kutembea na Mungu, kuzungumza na Mungu. Na ndiyo maana Mungu alimpa amri kama hiyo. Mungu aliweka wazi katika amri hii kile binadamu anaweza kufanya, na vilevile akaweka wazi kile asichoweza kufanya.

Katika maneno haya machache rahisi, tunauona moyo wa Mungu. Lakini ni aina gani ya moyo tunaouona? Je, kunao upendo katika moyo wa Mungu? Je, upendo huo unao hali yoyote ya kujali ndani yake? Upendo wa Mungu na kujali kwake katika mistari hii hakuwezi kutambulika na kuthaminiwa tu na watu, lakini unaweza pia kuhisiwa vizuri na kwa kweli. Hayo ni kweli? Kwa vile nimesema tayari mambo haya, bado mnafikiria kwamba haya ni maneno machache tu rahisi? Si rahisi hivyo, kweli? Mngeweza kuona hivi awali? Kama Mungu mwenyewe angekuambia maneno hayo machache mngehisi vipi ndani yenu? Kama wewe si mtu mwenye utu, kama moyo wako ni baridi kama barafu, basi usingehisi chochote, usingethamini upendo wa Mungu, na usingejaribu kuuelewa moyo wa Mungu. Lakini kama wewe ni mtu mwenye dhamiri, mwenye ubinadamu, basi utahisi tofauti. Utahisi joto, utahisi kuwa umetunzwa na umependwa, na utahisi furaha. Je, hayo ni kweli? Unapohisi mambo haya, utatenda vipi kwa Mungu? Utahisi ukiwa umeunganishwa kwa Mungu? Utampenda na kumheshimu Mungu kutoka kwenye sakafu ya moyo wako? Moyo wako utakuwa karibu zaidi na Mungu? Unaweza kuona kutoka kwa haya namna ambavyo upendo wa Mungu ulivyo muhimu kwa binadamu. Lakini kile kilicho muhimu zaidi ni kuthamini na kufahamu kwa binadamu upendo huu wa Mungu. Kwa hakika, Mungu hasemi mambo mengi yanayofanana kwenye awamu hii ya kazi Yake? Lakini je, watu wa leo wanauthamini moyo wa Mungu? Je, mnaweza kung’amua mapenzi ya Mungu Niliyoyazungumzia muda mfupi uliopita? Hamwezi hata kutambua mapenzi ya Mungu wakati yanaonekana waziwazi, yanaweza kushikika na ni halisi. Na ndiyo maana Nasema hamna maarifa na uelewa halisi wa Mungu. Je, haya si kweli? Hayo tu ndiyo yote tutakayowasiliana nanyi kwenye sehemu hii.

2. Mungu Amuumba Hawa

Mwa 2:18-20 Yehova Mungu akasema, Si vizuri kuwa mtu huyo akuwe peke yake; nitamuumbia msaidizi anayefanana na yeye. Na kutoka kwa ardhi Yehova Mungu akaumba wanyama wote wa msituni, na ndege wote wa angani; na akawaletea kwa Adamu ndiyo aone majina ambayo angewapa: na chochote ambacho Adamu alikiita kiumbe hai, hilo ndilo likawa jina lake kuanzia hapo. Naye Adamu akawapa wanyama wote wa kufugwa majina, na ndege wa hewani, na wanyama wote wa mwituni; lakini kwa Adamu hakupatikana msaidizi ambaye alifanana na yeye.

Mwa 2:22-23 Nao ubavu, ambao Yehova Mungu aliuchukua kutoka kwa Adamu, Yeye akaufanya uwe mwanamke, na akampeleka kwa Adamu. Naye Adamu akasema, Huyu sasa ni mfupa wa mifupa yangu, na nyama ya nyama zangu: ataitwa Mwanamke, kwa kuwa amechukuliwa kutoka kwa Mwanamume.

Kuna msitari mmoja muhimu kwenye sehemu hii ya Maandiko: “chochote ambacho Adamu alikiita kiumbe hai, hilo ndilo likawa jina lake kuanzia hapo.” Kwa hivyo ni nani aliyepatia viumbe wote haya majina yao? Alikuwa Adamu, si Mungu. Msitari huu unamwambia mwanadamu ukweli: Mungu alimpa binadamu werevu alipomuumba Yeye. Hivi ni kusema kwamba, werevu wa binadamu ulitoka kwa Mungu. Hili ni kweli. Lakini kwa nini? Baada ya Mungu kumuumba Adamu, Adamu alienda shuleni? Je, alijua namna ya kusoma? Baada ya Mungu kuwaumba viumbe hai mbalimbali, je, Adamu aliwatambua viumbe hawa wote? Je, Mungu alimwambia majina ya viumbe hao? Bila shaka, Mungu pia hakumfunza namna ya kutunga yale majina ya viumbe hawa. Huo ndio ukweli! Basi alijua vipi namna ya kupatia viumbe hawa hai majina yao na aina gani ya majina ya kuwapatia? Haya yote yanahusiana na swali kuhusu ni nini ambacho Mungu aliongezea kwa Adamu alipomuumba yeye. Ukweli unathibitisha kwamba wakati Mungu alipomuumba binadamu Alikuwa ameongezea werevu kwake. Huu ni ukweli muhimu sana. Je, nyinyi nyote mmesikiliza kwa makini? Kunao ukweli mwingine muhimu ambao unafaa kuwa wazi kwenu? Baada ya Adamu kuwapatia viumbe hai majina yao, majina haya yalipangwa kwenye msamiati wa Mungu. Kwa nini Ninasema hivyo? Hii pia inahusisha tabia ya Mungu, na lazima Niielezee.

Mungu alimuumba binadamu, Akapumua maisha ndani yake, na pia Akampa baadhi ya werevu Wake, uwezo Wake, na kile Anacho na alicho. Baada ya Mungu kumpa binadamu mambo haya yote, binadamu aliweza kufanya baadhi ya mambo haya kwa uhuru na kufikiria pekee yake. Kama kile binadamu anaunda na kufanya ni kizuri machoni mwa Mungu, basi Mungu anakikubali na haingilii kati. Kama kile binadamu anafanya ni sahihi, basi Mungu atakiacha tu kiwe hivyo milele. Kwa hivyo kauli hii “chochote ambacho Adamu alikiita kiumbe hai, hilo ndilo likawa jina lake kuanzia hapo” inaonyesha nini? Inaopendekeza kwamba Mungu hakufanya marekebisho yoyote kwa majina ya wale viumbe mbalimbali hai. Jina lolote lile ambalo Adamu alimwita, Mungu alisema “Ndiyo” na akasajili jina hilo hivyo. Je, Mungu alionyesha maoni yoyote? La, hilo ni hakika. Kwa hivyo, mnaona nini hapa? Mungu Alimpa binadamu werevu naye binadamu akautumia werevu wake aliopewa na Mungu kufanya mambo. Kama kile binadamu anafanya ni kizuri machoni mwa Mungu, basi kinathibitishwa, kutambulika, na kukubalika na Mungu bila ya utathmini au upinzani wowote. Hili ni jambo ambalo hakuna mtu wala roho wa maovu, wala Shetani, anaweza kufanya. Je, mnauona ufunuo wa tabia ya Mungu hapa. Je, mwanadamu, mwanadamu aliyepotoshwa, au Shetani anaweza kuwakubali wengine kuwawakilisha katika kufanya mambo huku wakitazama? Bila shaka la! Je, wanaweza kupigania cheo na yule mtu mwingine au nguvu nyingine ambayo ni tofauti na wao? Bila shaka wangefanya hivyo! Na kwa muda huo, kama angekuwa ni mtu aliyepotoshwa au Shetani aliyekuwa na Adamu, bila shaka wangekataa kile ambacho Adamu alikuwa akifanya. Ili kuthibitisha kwamba wanao uwezo wa kufikiria kwa uhuru na wanayo maono yao binafsi na ya kipekee, wangekataa kabisa kila kitu alichofanya Adamu: “Unataka kukiita hivyo? Kwa kweli, sitakiita hivyo, nitakiita hivi; ulikiita Tom lakini mimi nitakiita Harry. Lazima nionyeshe ustadi wangu.” Haya ni aina gani ya asili? Hii ni asili ya kiburi kisicho na mipaka? Lakini Mungu anayo tabia kama hii? Je, Mungu alikuwa na upinzani wowote usiokuwa wa kawaida kwa mambo haya ambayo Adamu alifanya? Jibu ni bila shaka la! Kati ya tabia ambayo Mungu anafichua, hakuna hata chembe ya ubishi, ya kiburi, au kujigamba kwa nafsi. Hilo liko wazi kabisa hapa. Hili ni jambo dogo tu, lakini kama huelewi kiini cha Mungu, kama moyo wako hautajaribu kujua namna ambavyo Mungu anatenda na mwelekeo wa Mungu ni ipi, basi hutajua tabia ya Mungu au kuyaona maonyesho na ufunuo wa tabia ya Mungu. Je, hayo si kweli? Je, unakubali kile Nimetoka tu kukuelezea? Kwa kujibu matendo ya Adamu, Mungu hakutangaza kwa sauti kwamba, “Umefanya vyema. Umefanya sahihi Ninakubali.” Katika Moyo Wake, hata hivyo, Mungu aliidhinisha, akathamini, akashangilia kile Adamu alikuwa amefanya. Hili ndilo jambo la kwanza tangu uumbaji ambalo binadamu alikuwa amemfanyia Mungu akifuata maagizo Yake. Ni jambo ambalo binadamu alifanya badala ya Mungu na kwa niaba ya Mungu. Mbele ya macho yake, hili lilitokana na werevu Aliokuwa amempa binadamu. Mungu aliliona kama jambo zuri, kitu kizuri. Kile ambacho Adamu alifanya wakati huo kilikuwa maonyesho ya kwanza ya werevu wa Mungu kwa binadamu. Hili lilikuwa onyesho zuri kutoka kwa maoni ya Mungu. Kile Ninachotaka kuwaambia nyinyi hapa ni kwamba nia ya Mungu katika kuongezea sehemu ya kile Anacho na alicho na werevu wake kwa binadamu ilikuwa ili mwanadamu aweze kuwa kiumbe hai anayemwonyesha Yeye. Kwa kiumbe hai kama huyo kufanya mambo hayo kwa niaba yake, ilikuwa ndicho hasa kile Mungu alikuwa akitamani kuona.

3. Mungu Awatengenezea Adamu na Hawa Nguo za Ngozi

Mwa 3:20-21 Adamu akampa mke wake jina la Hawa; kwa sababu yeye ndiye aliyekuwa mama ya wote wenye uhai. Pia Yehova Mungu akawatengenezea Adamu na mke wake nguo za ngozi; na akawavisha.

Hebu tuangalie kifungu hiki cha tatu, kinachosema kwamba, kunayo maana katika jina Adamu alimpa Hawa, kweli? Hii inaonyesha kwamba baada ya kuumbwa, Adamu alikuwa na fikira zake na alielewa mambo mengi. Lakini kwa sasa, hatutasoma na kuchunguza kile alichoelewa au kwa kiwango kipi alielewa kwa sababu hiyo si hoja kuu Ninayotaka kuzungumzia kwenye kifungu hiki cha tatu. Hivyo hoja kuu katika kifungu cha tatu ni gani? Hebu na tuuangalie mstari huo, “Pia Yehova Mungu akawatengenezea Adamu na mke wake nguo za ngozi; na akawavisha.” Kama hatutakuwa na ushirika kuhusu mstari huu wa maandiko leo, huenda hamtawahi kutambua uzito ulio katika maneno haya. Kwanza, hebu niwape vidokezo fulani. Panua kufikiria kwenu na kuona picha ya bustani ya Edeni, huku Adamu na Hawa wakiishi ndani. Mungu anaenda kuwatembelea lakini wanajificha kwa sababu wako uchi. Mungu hawezi kuwaona, na baada ya kuwaita wao, wanasema, “Hatuwezi kuthubutu kukuona kwa sababu tuko uchi.” Hawathubutu kumwona Mungu kwa sababu wako uchi. Kwa hivyo Yehova Mungu anawafanya nini? Maandishi asilia yanasema: “Pia Yehova Mungu akawatengenezea Adamu na mke wake nguo za ngozi; na akawavisha.” Sasa mnajua kile Mungu alitumia kutengeneza nguo zao? Mungu alitumia ngozi za wanyama kutengeneza nguo zao. Hivyo ni kusema, nguo ambazo Mungu alitengenezea binadamu zilikuwa za koti la manyoya. Hiki ndicho kilichokuwa kipande cha kwanza cha nguo ambacho Mungu alitengenezea binadamu. Koti la manyoya ni mavazi ya soko la vitu vya bei ghali kwa viwango vya leo, kitu ambacho si kila mtu anaweza kumudu kuvaa. Kama mtu atakuuliza: Kipande cha kwanza cha nguo kilichovaliwa na wazee wa wanadamu kilikuwa kipi? Unaweza kujibu: Kilikuwa ni koti la manyoya. Nani aliyetengeneza hilo koti la manyoya? Unaweza kujibu zaidi: Mungu alilitengeneza! Hiyo ndiyo hoja kuu: Nguo hii ilitengenezwa na Mungu. Je, hilo ni jambo la kutilia maanani, sivyo? Kwa vile sasa nimetoka kukifafanua, picha imeibuka katika akili zenu? Kunafaa kuwa angaa na mpangilio wa juu kukihusu. Hoja ya kuwaambia haya leo si kuwafahamisha kuhusu kipande cha kwanza cha nguo cha binadamu kilikuwa nini. Hivyo hoja ni gani? Hoja si lile koti la manyoya, lakini namna ya kujua tabia na uwepo na nafsi zilizofichuliwa na Mungu alipokuwa Akifanya hivi.

“Pia Yehova Mungu akawatengenezea Adamu na mke wake nguo za ngozi; na akawavisha,” Katika tukio hili, ni wajibu gani ambao tunamwona Mungu akiuchukua Anapokuwa na Adamu na Hawa? Na ni katika aina gani ya uajibu ambao Mungu anajitokeza katika ulimwengu akiwa tu na wanadamu wawili? Kutekeleza wajibu wa Mungu? Kaka na dada kutoka Hong Kong, tafadhali jibuni. (Kutekeleza wajibu wa mzazi.) Kaka na dada kutoka Korea Kusini, ni wajibu wa aina gani mnafikiria Mungu anatekeleza hapa? (Kiongozi wa familia.) Kaka na dada kutoka Taiwan, mnafikiria nini? (Wajibu wa mtu katika familia ya Adamu na Hawa, wajibu wa mwanafamilia.) Baadhi yenu mnafikiria kuwa Mungu anajitokeza kama mwanafamilia wa Adamu na Hawa, huku baadhi wakisema kwamba Mungu anajitokeza kama kiongozi wa familia na wengine wanasema kwamba Anajitokeza kama mzazi. Haya yote yanafaa sana. Lakini ni nini hasa Ninachotilia mkazo hapa? Mungu aliwaumba watu hawa wawili na kuwashughulikia kama mtu na mwandani Wake. Akiwa ndiye mwanafamilia pekee wao, Mungu aliangalia kuishi kwao na pia akakidhi mahitaji yao ya kimsingi. Hapa, Mungu anajitokeza kama mzazi wa Adamu na Hawa. Huku Mungu akifanya haya, binadamu haoni namna ambavyo Mungu alivyo mkuu; haoni mamlaka ya juu zaidi ya Mungu, hali Yake ya mafumbo, na hasa haoni hasira au adhama Yake. Kile anachoona tu ni unyenyekevu wa Mungu, upendo Wake, kujali Kwake binadamu na jukumu Lake na utunzaji Wake kwake yeye. Mwelekeo na njia ambayo Mungu alishughulikia Adamu na Hawa ni sawa na namna ambavyo wazazi wa kibinadamu wanavyoonyesha hali ya kuwajali watoto wao binafsi. Ni kama pia namna ambavyo wazazi wa kibinadamu wanavyopenda, kuangalia, na kutunza watoto wao binafsi wa kiume na kike—halisia, namna ya kuonekana, na kushikika. Badala ya kujiweka Yeye Mwenyewe katika cheo cha juu na cha utukufu, Mungu mwenyewe alitumia ngozi kutengeneza nguo za binadamu. Haijalishi kama koti hili la manyoya lilitumika kufunika uchi wao au wao kujikinga dhidi ya baridi. Kwa ufupi, nguo hii iliyotumika kuufunika mwili wa binadamu ilitengenezwa na Mungu mwenyewe kwa mikono Yake mwenyewe. Badala ya kuitengeneza tu kupitia kwa fikira au kwa mbinu za kimiujiza kama watu wanavyofikiria, Mungu alikuwa amefanya kitu cha halali kwa binadamu ambacho binadamu anafikiria Mungu hawezi na hafai kufanya. Kitu hiki kinaweza kuwa rahisi ambacho baadhi huenda hata wasifikirie kwamba kinastahili kutajwa, lakini kinawaruhusu pia wale wote wanaomfuata Mungu lakini awali walikuwa na mawazo yasiyoeleweka kuhusu Yeye kuweza kupata maono kuhusu ukweli na uzuri Wake, na kuuona uaminifu Wake na asili Yake ya unyenyekevu. Kinawafanya watu wenye kiburi kisicho na kifani wanaofikiria kwamba wako juu na wanao utukufu kuinamisha vichwa vyao kwa aibu mbele ya ukweli na unyenyekevu wa Mungu. Hapa, ukweli na unyenyekevu wa Mungu unawezesha zaidi watu kuona namna ambavyo Anapendeka. Kwa kinyume cha mambo, yule Mungu mkubwa sana, Mungu anayependeka na yule Mwenyezi Mungu katika mioyo ya watu ni mdogo sana, asiyevutia, na asiyeweza kuhimiliwa hata mara moja. Unapouona mstari huu na kuisikia hadithi hii, unamkasirikia Mungu kwa sababu Alifanya kitu kama hiki? Baadhi ya watu wanaweza kufanya hivyo, lakini kwa wengine itakuwa ni tofauti kabisa. Watafikiri Mungu ni mkweli na anapendeka, na hasa ni ule ukweli na uzuri wa Mungu ndiyo unaowafurahisha. Kwa kadri wanavyoona ule upande wa kweli wa Mungu, ndipo wanapothamini uwepo wa kweli wa upendo wa Mungu, umuhimu wa Mungu katika mioyo yao, na namna anavyosimama kando yao kila muda.

Kwa wakati huu, tunafaa kuunganisha mazungumzo yetu na sasa. Kama Mungu angeweza kufanya mambo haya madogo mbalimbali kwa binadamu Aliowaumba hapo mwanzo kabisa, hata vitu vingine ambavyo watu hawangethubutu kufikiria ama kutarajia, basi naye Mungu angewafanyia watu leo mambo kama hayo? Baadhi ya watu husema, “Ndiyo!” Kwa nini hivyo? Kwa sababu kiini cha Mungu si bandia, uzuri Wake si bandia. Kwa sababu kiini cha Mungu kwa kweli kipo, na si kitu kilichoongezewa tu na wengine na bila shaka si kitu ambacho kinabadilika na mabadiliko ya muda, mahali, na enzi. Ukweli na uzuri wa Mungu unaweza kwa kweli kuonyeshwa kupitia kufanya jambo ambalo watu wanafikiria si la kipekee na ni dogo, jambo ambalo ni dogo sana kiasi cha kwamba watu hata hawafikirii angeweza kufanya. Mungu si mnafiki. Hakuna kupiga chuku, kufunika ukweli, majivuno au kiburi katika tabia na kiini Chake. Siku zote Hajigambi, lakini badala yake Anapenda, Anaonyesha hali ya kujali, Anaangalia, na kuwaongoza wanadamu Aliowaumba kwa uaminifu na dhati. Haijalishi ni kiwango kipi ambacho watu wanaweza kuthamini, kuhisi, au kuona, Mungu kwa hakika anafanya mambo haya. Je, kujua kwamba Mungu anacho kiini kama hicho kunaweza kuathiri upendo wa watu kwake Yeye? Kutaweza kushawishi namna wanavyomcha Mungu? Ninatumai utakapoelewa upande halisi wa Mungu utaweza kuwa hata karibu zaidi na Yeye na kuweza kuthamini hata zaidi na kwa kweli upendo Wake na utunzaji Wake kwa wanadamu, huku wakati huohuo pia kumpa moyo wako na kutowahi tena kuwa na shaka au wasiwasi wowote kwake Yeye. Mungu anafanya kimyakimya kila kitu kwa ajili ya binadamu, akifanya kimyakimya kupitia ukweli, uaminifu, na upendo Wake. Lakini siku zote Hana hofu au majuto yoyote kwa yale yote Anayofanya, wala hahitaji mtu yeyote kumlipa Yeye kwa njia yoyote au kuwa na nia za kuwahi kupokea kitu kutoka kwa wanadamu. Kusudio tu la kila kitu Alichowahi kufanya ni ili Aweze kupokea imani na upendo wa kweli kutoka kwa wanadamu. Hebu tuhitimishe mada hii ya kwanza hapa.

Je, mazungumzo haya yamewasaidia? Yamewasaidia kwa kiasi kipi? (Uelewa na maarifa zaidi kuhusu upendo wa Mungu.) (Mbinu hii ya mawasiliano inaweza kutusaidia katika siku za mbele ili kuweza kuthamini zaidi neno la Mungu, kufahamu hisia alizokuwa nazo na maana ya mambo Aliyoyasema Alipoyasema, na kuhisi namna Alivyohisi wakati huo.) Je, yupo yeyote kati yenu anayehisi hata zaidi uwepo halisi wa Mungu baada ya kuyasoma maneno haya? Je, mnahisi uwepo wa Mungu si mtupu wala wa kutiliwa mashaka tena? Pindi mnapokuwa na hisia hii, mnahisi kwamba Mungu yupo tu kando yenu? Pengine hisia hiyo si ya dhahiri kwa sasa hivi au hamtaweza kuihisi sasa hivi bado. Lakini siku moja, mtakapokuwa na shukrani ya kina na ya kweli na maarifa halisi kuhusu tabia na kiini cha Mungu ndani ya moyo wako, utahisi kwamba Mungu yupo tu kando yako—ni vile tu kwamba haujawahi kumkubali kwa kweli Mungu ndani ya moyo wako. Haya ni halisi.

Mnafikiria vipi kuhusu mbinu hii ya mawasiliano? Mnaweza kuiendeleza? Mnafikiria aina hii ya ushirika kuhusu mada ya kazi ya Mungu na tabia ya Mungu ni nzito? Mnahisi vipi? (Vizuri sana, kuchangamka.) Ni nini kilichowafanya kuhisi vizuri? Kwa nini mlichangamka? (Ilikuwa sawa na kurudi kwenye Bustani ya Edeni, kurudi kuwa kando ya Mungu.) “Tabia ya Mungu” kwa kweli ni mada ambayo haijazoeleka sana na kila mmoja, kwa sababu kile ambacho unafikiria kwa kawaida, kile unachosoma kwenye vitabu au kusikia kwenye ushirika, siku zote hukufanya kuhisi kama mtu asiyeona akimgusa ndovu—unahisi tu kila pahali kwa kutumia mikono yako, lakini kwa hakika huoni chochote kwa macho yako. “Mguso wa mkono” hauwezi tu kukupa mpangilio wa kimsingi wa maarifa ya Mungu, wacha hata dhana iliyo wazi. Kile ambacho mguso wa mkono unakupatia ni kufikiria zaidi, kiasi kwamba huwezi kufafanua kwa uhakika tabia ya Mungu na kiini halisi. Badala yake, masuala haya ya kutokuwa na uhakika yanayotokana na kufikiria kwako huwa siku zote yanaonekana kujaza moyo wako na shaka. Wakati ambapo huwezi kuwa na uhakika kuhusu kitu na ilhali bado unajaribu kukielewa, ndani ya moyo wako bado siku zote kutaendelea kuwa na mambo yanayopingana na kukinzana, na wakati mwingine huenda hata yakabadilika na kuwa shida, na kukufanya kuhisi ni kana kwamba umepoteza kitu. Je, si jambo la kusikitisha sana unapotaka kumtafuta Mungu, kumjua Mungu, na kumwona Yeye waziwazi, lakini siku zote kutoweza kupata majibu? Bila shaka, maneno haya yanalengwa kwa wale wanaotamani kutafuta uwezo wa kumuheshimu sana Mungu na kuridhisha Mungu. Kwa wale watu ambao hawatilii maanani mambo kama haya, hili kwa hakika si muhimu kwa sababu wanatumaini kwamba ni bora zaidi kuwa uhalisi na uwepo wa Mungu uwe ni ngano ya kale au ndoto, ili waweze kufanya chochote wanachotaka, ili waweze kuwa wale wakubwa zaidi na wenye umuhimu zaidi, na kuweza kutenda vitendo vya maovu bila ya kujali athari zake, na hivyo basi kutoweza kukabiliana na adhabu au kulazimika kuwajibika, ili hata mambo ambayo Mungu anasema kuwahusu watendaji maovu hayataweza kuwahusu wao. Watu hawa hawako radhi kufahamu tabia ya Mungu, wamechoshwa na kujaribu kujua Mungu na kila kitu kuhusu Yeye. Wangependelea kwamba Mungu asiwepo. Watu hawa wanampinga Mungu na wao ndio watakaoondolewa.

Kisha, tutazungumzia hadithi ya Nuhu na namna ambavyo inahusiana na mada ya kazi ya Mungu, tabia ya Mungu na Mungu Mwenyewe.

Mnaona Mungu akimfanya nini Nuhu kwenye sehemu hii ya maandiko? Pengine kila mmoja aliyeketi hapa anajua kitu kuhusu hayo baada ya kusoma maandiko: Mungu alimfanya Nuhu kujenga safina, kisha Mungu akatumia gharika kuangamiza ulimwengu. Mungu alimruhusu Nuhu kujenga safina ili kuokoa familia yake ya wanane, kuwaruhusu kuweza kuishi, ili kuwa babu wa kizazi kifuatacho cha wanadamu. Sasa hebu tuyasome maandiko.

B. Nuhu

1. Mungu Anuia kuangamiza Ulimwengu kwa Gharika, Amwagiza Nuhu Kuijenga Safina

Mwa 6:9-14 Hivi ni vizazi vyake Nuhu: Nuhu alikuwa mtu mwenye haki na mtimilifu katika vizazi vyake, naye Nuhu alitembea na Mungu. Naye Nuhu akapata watoto watatu wa kiume, Shemu, Hamu, na Yafethi. Dunia pia ilikuwa potovu mbele za Mungu, nayo dunia ilijaa vurugu. Naye Mungu akaiangalia dunia, na, tazama, ilikuwa imepotoka; kwa sababu kila aliye na mwili alikuwa amejipotoshea njia yake duniani. Naye Mungu akasema kwake Nuhu, Mwisho wa wote walio na mwili umefika mbele Zangu; kwa kuwa dunia imejawa na vurugu kupitia kwao; na, tazama, nitawaangamiza pamoja na dunia. Ujitengenezee safina ya mbao wa mvinje; utatengeneza vyumba ndani ya safina, na uipake lami ndani na nje.

Mwa 6:18-22 Lakini na wewe nitaliimarisha agano Langu; na utaingia ndani ya safina, wewe, na wana wako, na mke wako, na wake zao wana wako pamoja na wewe. Na kwa kila kilicho na uhai chenye mwili, utawaleta wawili wa kila aina katika safina, kuwaweka hai pamoja nawe; watakuwa wa kiume na wa kike. Kila ndege arukaye kwa aina yake, na mifugo kwa aina yake, kila kinachotambaa duniani kwa aina yake, wawili wa aina yote watakuja kwa wewe, ili uwaweke hai. Na ujichukulie chakula cha kila aina kinacholika, nawe ukikusanye kwako; na kitakuwa kwa ajili ya chakula cha ninyi, na cha wao. Nuhu alifanya hivyo; kulingana na vyote ambavyo Mungu alimwamrisha, alifanya hivyo.

Je sasa mnaelewa kwa jumla Nuhu ni nani baada ya kuzisoma fahamu hizi? Nuhu ni mtu wa aina gani? Maandishi asilia ni: “Nuhu alikuwa mtu mwenye haki na mtimilifu katika vizazi vyake.” Kulingana na uelewa wa watu wa kisasa, mtu mwenye haki wakati huo wa nyuma alikuwa mtu wa aina gani? Mtu mwenye haki anafaa kuwa mtu mtimilifu. Je, mnajua kama mtu huyu mtimilifu ni mtimilifu machoni mwa binadamu au ni mtimilifu machoni mwa Mungu? Bila shaka mtu huyu mtimilifu ni mtu mtimilifu machoni mwa Mungu na wala si machoni mwa binadamu. Haya yote ni kweli! Hii ni kwa sababu binadamu ni kipofu na hawezi kuona, na Mungu tu ndiye anayeiangalia nchi nzima na kila mmoja wetu, Mungu pekee ndiye anayejua Nuhu ni mtu mtimilifu. Hivyo basi, mpango wa Mungu wa kuuangamiza ulimwengu kwa gharika ulianza pindi tu Alipomuita Nuhu.

Katika enzi hiyo, Mungu alinuia kumuita Nuhu ili kufanya kitu muhimu sana. Kwa nini ilikuwa lazima Afanye hivyo? Kwa sababu Mungu alikuwa na mpango kwa moyo Wake wakati huo. Mpango Wake ulikuwa kuangamiza ulimwengu kwa gharika. Kwa nini auangamize ulimwengu? Maandiko yanasema hivi: “Dunia pia ilikuwa potovu mbele za Mungu, nayo dunia ilijaa vurugu.” Mnaona nini kutoka kwenye kauli “dunia ilijaa vurugu”? Ni ajabu duniani wakati ulimwengu na watu wake wanapotoka kwa kupindukia, na ni hivi: “dunia ilijaa vurugu.” Katika lugha ya leo, “ilijaa vurugu” inamaanisha kila kitu kimechanganyika. Kwa binadamu, inamaanisha kwamba katika nyanja zote za maisha hakuna mpangilio, na mambo yamejaa fujo kweli na ni magumu kudhibiti. Katika macho ya Mungu, inamaanisha watu wa ulimwengu wamepotoka sana. Wamepotoka hadi kiwango gani? Wamepotoka hadi kiwango ambacho Mungu hawezi tena kuvumilia kuangalia na hawezi tena kuwa na subira kuhusu hali hiyo. Wamepotoka hadi kiwango ambacho Mungu anaamua kuwaangamiza. Wakati Mungu alipoamua kuuangamiza ulimwengu, Alipanga kupata mtu wa kuijenga safina. Kisha Mungu akamchagua Nuhu kufanya kitu hicho, ambacho ni kumruhusu Nuhu kuijenga safina. Kwa nini Mungu alimchagua Nuhu? Katika macho ya Mungu, Nuhu ni mtu mwenye haki na haijalishi kile ambacho Mungu atamwagiza yeye kufanya, atafanya vivyohivyo. Hii inamaanisha atafanya chochote anachoambiwa kufanya na Mungu. Mungu alitaka kumtafuta mtu kama huyu ili afanye kazi na Yeye, kukamilisha kile alichokuwa amemwaminia kufanya, kuikamilisha kazi Yake hapa duniani. Hapo nyuma, kulikuwa na mtu mwingine kando na Nuhu ambaye angekamilisha kazi hiyo? Bila shaka la! Nuhu ndiye aliyekuwa mtu wa pekee ambaye angeweza kukamilisha kile ambacho Mungu alikuwa amemwaminia kufanya, na hivyo Mungu alimchagua yeye. Lakini je upana na viwango vya Mungu vya kuwaokoa watu hapo nyuma vilikuwa sawa na vile vya sasa? Jibu ni bila shaka kunayo tofauti! Na kwa nini Nauliza hili? Nuhu pekee ndiye aliyekuwa mwanadamu mwenye haki machoni pa Mungu wakati huo, ambalo linadokeza kwamba watoto wake wa kiume, na mke na wakwe wake wote hawakukuwa watu wenye haki, lakini Mungu bado aliwasamehe kwa sababu ya Nuhu. Mungu hakuwawekea matakwa kama Anavyofanya sasa, na badala yake Aliwaweka hai wanachama wote wanane wa familia ya Nuhu. Walipata baraka za Mungu kwa sababu ya Nuhu kuwa mwenye haki. Kama Nuhu asingekuwepo, hakuna yeyote kati yao ambaye angekamilisha kile ambacho Mungu alikuwa amemwaminia kufanya. Hivyo basi Nuhu alikuwa ndiye mtu wa pekee ambaye alitakikana kubakia hai baada ya ulimwengu kuangamizwa wakati huo, na wale wengine walikuwa tu wafadhiliwa wa ziada. Hii inaonyesha kwamba, katika enzi kabla ya Mungu kuanza rasmi kazi Yake ya usimamizi, kanuni na viwango ambavyo Alishughulikia watu na kuwadai mahitaji vilikuwa vimelegezwa kidogo. Kwa watu wa leo, namna ambavyo Mungu alivyoshughulikia familia ya Nuhu ya watu wanane yaonekana kukosa haki. Lakini tukilinganisha na wingi wa kazi ambayo Yeye Anafanya kwa watu na kiwango cha neno Lake Analopitisha, namna Mungu alivyoshughulikia familia ya Nuhu ya watu wanane ilikuwa tu ni kanuni ya kazi Yake aliyoifanyia katika usuli wa kazi Yake wakati huu. Kwa kulinganisha, familia ya Nuhu ya watu wanane ndio ilipokea mengi zaidi kutoka kwa Mungu au ni watu wa Mungu ndio waliopokea?

Kwamba Nuhu aliitwa ni ukweli mdogo, lakini hoja kuu ya kile tunachozungumzia sasa—tabia ya Mungu, mapenzi Yake kiini Chake halisi katika rekodi hii—si rahisi. Ili kuelewa dhana hizi mbalimbali za Mungu lazima kwanza tuelewe ni mtu wa aina gani ambaye Mungu hutamani kuita, nakupitia hii, tuweze kuelewa tabia yake, mapenzi yake na kiini chake halisi. Kufanya hivi ni muhimu. Hivyo katika macho ya Mungu, mtu huyu ni wa aina gani ambaye yeye humwita? Huyu lazima awe ni mtu anayeweza kuyasikiza maneno Yake. Wakati huohuo, lazima mtu huyu awe yule wa kuwajibika, mtu atakayetekeleza neno la Mungu kwa kuliona kuwa jukumu na wajibu ambao anahitajika kukamilisha. Basi mtu huyu anahitajika kuwa mtu anayemjua Mungu? La. Hapo nyuma, Nuhu hakuwa ameyasikia sana mafundisho ya Mungu wala kupitia kazi yoyote ile ya Mungu. Hivyo basi, maarifa ya Nuhu kumhusu Mungu yalikuwa madogo mno. Ingawaje imerekodiwa hapa kwamba Nuhu alitembea na Mungu, aliwahi kuiona nafsi ya Mungu? Jibu ni bila shaka la! Kwa sababu katika siku hizo, wajumbe wa Mungu tu ndio waliowaendea watu. Ingawa waliweza kuwakilisha Mungu katika kusema na kufanya mambo, walikuwa wakipitisha tu mapenzi na nia Zake. Nafsi ya Mungu haikufichuliwa kwa binadamu uso kwa macho. Kwenye sehemu hii ya maandiko, chote tunachoona tu ni kile ambacho mtu huyu Nuhu alilazimika kufanya na maagizo ya Mungu kwake yalikuwa gani. Hivyo basi ni kiini kipi kilichoonyeshwa na Mungu hapa? Kila kitu anachofanya Mungu kimepangiliwa kwa uhakika. Anapoona jambo au hali ikitokea, kutakuwa na kiwango cha kulipima jambo hilo katika macho Yake, na kiwango hiki kitaamua kama Ataanza mpango wa kulishughulikia au namna ya kuchukulia jambo na hali hii. Yeye anajali na ana hisia kwa kila kitu. Kwa hakika ni kinyume kabisa cha mambo. Kunao mstari hapa ambao Mungu alimwambia Nuhu: “Mwisho wa wote walio na mwili umefika mbele Zangu; kwa kuwa dunia imejawa na vurugu kupitia kwao; na, tazama, nitawaangamiza pamoja na dunia.” Katika maneno ya Mungu wakati huu, Alisema kwamba Angeangamiza binadamu tu? La! Mungu Alisema kwamba Angeangamiza viumbe wote hai wenye mwili. Kwa nini Mungu alitaka kuangamiza? Kunao ufunuo mwingine wa tabia ya Mungu hapa: Katika macho ya Mungu, kunayo mipaka ya subira yake kwa kupotoka kwa binadamu, kwa uchafu, vurugu, na kutotii kwa mwili wote. Mipaka Yake ni ipi? Ni kama vile alivyosema Mungu: “Mungu akaiangalia dunia, na, tazama, ilikuwa imepotoka; kwa sababu kila aliye na mwili alikuwa amejipotoshea njia yake duniani.” Kauli hii “kwa sababu kila aliye na mwili alikuwa amejipotoshea njia yake duniani” inamaanisha nini? Inamaanisha kiumbe yeyote hai, wakiwemo wale waliofuata Mungu, wale walioita jina la Mungu, wale waliowahi kutoa sadaka za kuteketezwa kwa Mungu, wale waliomtambua Mungu kwa vinywa vyao na hata kumsifia Mungu—pindi tabia yao ilipojaa upotovu na kufikia macho ya Mungu, basi ingemlazimu kuwaangamiza. Hiyo ndiyo ilikuwa mipaka ya Mungu. Hivyo basi ni hadi kiwango kipi Mungu alibakia kuwa mwenye subira kwa binadamu na upotovu wa mwili wote? Hadi katika kiwango ambacho watu wote, wawe wafuasi wa Mungu au wasioamini, walikuwa hawatembelei njia sahihi. Hadi kiwango ambacho binadamu alikuwa hajapotoshwa tu katika maadili na mwenye wingi wa maovu, lakini pia pale ambapo hakukuwa na mtu aliyesadiki uwepo wa Mungu, tupilia mbali yeyote aliyesadiki kuwa ulimwengu unatawaliwa na Mungu na kwamba Mungu anaweza kuwaletea watu nuru na njia sahihi. Hadi kiwango ambacho binadamu aliudharau uwepo wa Mungu, na hakumruhusu Mungu kuwepo. Pindi upotovu wa mwanadamu ulipofikia kiwango hiki, Mungu asingeweza tena kuwa na subira Ni nini kingechukua nafasi yake? Kuja kwa hasira ya Mungu na adhabu ya Mungu. Huu haukuwa ufunuo kiasi wa tabia ya Mungu? Katika enzi hii ya sasa, yupo bado binadamu mwenye haki katika macho ya Mungu? Yupo bado binadamu mtimilifu katika macho ya Mungu? Enzi hii ndiyo ile ambayo tabia ya miili yote duniani imepotoka mbele ya macho ya Mungu? Katika siku na enzi hii, mbali na wale Mungu anataka kuwafanya kuwa kamili, wale wanaoweza kumfuata Mungu na kuukubali wokovu Wake, huoni kwamba watu wote wa mwili wanapatia changamoto ile mipaka ya subira ya Mungu? Si kila kitu kinachofanyika kando yenu, kila mnachoona kwa macho yenu, na kusikia kwa masikio yenu, na kupitia ninyi binafsi kila siku katika ulimwengu huu kimejaa vurugu? Katika macho ya Mungu, si ulimwengu kama huu, enzi kama hii, inafaa kukomeshwa? Ingawaje usuli wa enzi ya sasa ni tofauti kabisa na usuli wa enzi ya Nuhu, hisia na hasira Alizo nazo Mungu kwa kupotoka kwa binadamu inabakia ileile sawa na ilivyokuwa wakati huo. Mungu anaweza kuwa mwenye subira kwa sababu ya kazi Yake, lakini kulingana na hali na masharti ya aina yote, ulimwengu huu unafaa kuwa uliangamizwa kitambo katika macho ya Mungu. Hali imepita na kupitiliza ile iliyokuwa hapo nyuma wakati ulimwengu uliangamizwa na gharika. Lakini tofauti ni nini? Hili ndilo jambo jingine linalohuzunisha moyo wa Mungu zaidi, na pengine kitu ambacho hakuna yeyote kati yenu anaweza kutambua.

Alipokuwa akiuangamiza ulimwengu kwa gharika, Mungu angemwita Nuhu ili kuijenga safina na kufanya baadhi ya kazi ya matayarisho. Mungu angemwita binadamu mmoja—Nuhu—kumfanyia misururu hii ya mambo. Lakini kwenye enzi ya sasa, Mungu hana mtu yeyote wa kumuita. Kwa nini hivyo? Kila mmoja aliyeketi hapa pengine anaelewa na kujua sababu vizuri sana. Je, mngependa Mimi niweze kuiweka wazi? Kuitaja kwa sauti huenda kukawaaibisha na kufanya kila mmoja kukasirika. Baadhi ya watu wanaweza kusema: “Ingawaje sisi si watu wenye haki na wala sisi si watu watimilifu kwenye macho ya Mungu, kama Mungu atatuelekeza sisi kufanya kitu, bado tutaweza kukifanya. Kabla, Aliposema janga kuu lilikuwa likija, tulianza kutayarisha chakula na vitu ambavyo tungehitaji wakati wa janga hilo. Si haya yote yalifanywa kulingana na mahitaji ya Mungu? Si tulikuwa tukishirikiana kwa hakika na kazi ya Mungu? Mambo haya tuliyofanya hayawezi kulinganishwa na kile Nuhu alifanya? Kwani kufanya kile tulichofanya si utiifu wa kweli? Kwani hatukuwa tunafuata maagizo ya Mungu? Kwani hatukufanya kile Mungu alichosema kwa sababu tunayo imani katika maneno ya Mungu? Basi kwa nini Mungu angali na huzuni? Kwa nini Mungu anasema Hana mtu wa kumwita?” Kunao tofauti wowote kati ya vitendo vyenu na vile vya Nuhu? Tofauti ni nini? (Kutayarisha chakula leo kwa minajili ya janga kulikuwa nia yetu binafsi.) (Matendo yetu hayawezi kufikia yale ya “haki,” ilhali Nuhu ni mtu mwenye haki mbele ya macho ya Mungu.) Kile mlichosema hakiko mbali sana na ukweli. Kile alichofanya Nuhu ni tofauti sana kulingana na kile watu wanafanya sasa. Wakati Nuhu alipofanya kama vile Mungu alivyomwagiza hakujua nia za Mungu zilikuwa nini. Hakujua ni nini ambacho Mungu Alitaka kukamilisha. Mungu alikuwa amempa tu amri, Akamwagiza afanye kitu, lakini bila ya maelezo mengi, na akaendelea mbele na kukifanya. Hakujaribu kuelewa kwa siri nia za Mungu zilikuwa nini, wala hakumpinga Mungu au kuwa na fikira mbili kuhusu jambo hilo. Alienda tu na kuifanya vilivyo kwa moyo safi na rahisi. Chochote ambacho Mungu alimruhusu kufanya alifanya, na kutii na kusikiliza neno la Mungu vyote vilikuwa ni imani yake ya kufanya mambo. Hivyo ndivyo alivyokuwa mnyofu na mwepesi wa kushughulikia kile ambacho Mungu alimwaminia kufanya. Kiini chake—kiini cha vitendo vyake kilikuwa ni utiifu, sio kutarajia kwa kukisia, sio kupinga, na zaidi; kutofikiria kuhusu maslahi yake binafsi na faida zake na hasara zake. Zaidi ya hayo, wakati Mungu aliposema Angeuangamiza ulimwengu kwa mafuriko, Nuhu hakuuliza ni lini au kuuliza kile kitakachovifanyikia vitu, na bila shaka hakumuuliza Mungu namna hasa alivyopanga kuangamiza ulimwengu. Alifanya tu kama Mungu alivyomwagiza. Njia yoyote ile aliyotaka Mungu, safina hiyo iweze kujengwa na hasa kujengwa na nini, alifanya tu vile ambavyo Mungu alimwomba na pia akaanza kazi mara moja. Alitenda kulingana na maagizo ya Mungu kwa mwelekeo wa kutaka kutosheleza Mungu. Je, alikuwa akifanya hivyo kujisaidia yeye kuepuka janga? La. Je, alimwuliza Mungu ni baada ya muda gani zaidi kabla ulimwengu ungeangamizwa? Hakuuliza. Je, alimwuliza Mungu au alijua ingechukua muda gani kuijenga safina? Hakujua hilo pia. Alitii tu, akasikiliza, na kufanya hivyo inavyohitajika. Watu wa sasa si sawa: Pindi tu taarifa fulani inapojitokeza kupitia kwa neno la Mungu, pindi tu watu wanapohisi ishara ya kutatizwa au matatizo, wote watachukua hatua mara moja, haijalishi ni nini, au gharama husika, ili kutayarisha kile ambacho watakula, kunywa, na kutumia athari za baadaye, hata kupanga njia za wao kutoroka wakati janga litakapovamia. Hata ya kuvutia zaidi ni kwamba, wakati huu muhimu, akili za binadamu zinakuwa zenye “manufaa sana.” Katika hali ambazo Mungu hajanipa maagizo yoyote, binadamu anaweza kupanga kila kitu kwa njia inayofaa Mngeweza kutumia neno “sahihi” ili kuielezea. Na kuhusiana na kile Mungu anachosema, nia za Mungu ni nini, au kile Mungu anataka ni nini, hakuna anayejali na hakuna anayejaribu kukitambua. Je, hii siyo tofauti kubwa zaidi kati ya watu wa leo na Nuhu?

Katika rekodi hii ya hadithi ya Nuhu, mnaona sehemu ya tabia ya Mungu? Kunacho mpaka kwa subira ya Mungu kwa upotovu, uchafu, na vurugu la binadamu. Anapofikia ule mpaka, Hatawahi tena kuwa na subira na badala yake Ataanza usimamizi Wake mpya na mpango mpya, kuanza kufanya kile ambacho lazima Afanye, kufichua matendo Yake na upande ule mwingine wa tabia Yake. Kitendo hiki Chake si cha kuonyesha kwamba lazima Asiwahi kukosewa na binadamu au kwamba Yeye amejaa mamlaka na hasira, na wala si kuonyesha kwamba Anaweza kuangamiza binadamu. Ni kwamba tabia Yake na kiini chake takatifu ambacho hakiwezi tena kuruhusu, hakina tena subira kwa aina hii ya binadamu kuishi mbele Yake, kuishi chini ya utawala Wake. Hivyo ni kusema, wakati wanadamu wote wako dhidi Yake, wakati hakuna mtu yeyote Anayeweza kuokoa katika ulimwengu mzima, Hatakuwa tena na subira kwa binadamu kama hawa, na Ataweza, bila ya utundu wowote, kutekeleza mpango Wake—kuangamiza binadamu wa aina hii. Kitendo kama hicho cha Mungu kinaamuliwa na tabia Yake. Hii ni athari inayohitajika, na athari ambayo kila kiumbe aliyeumbwa chini ya utawala wa Mungu lazima ashuhudie. Je, haya hayaonyeshi kwamba katika enzi ya sasa, Mungu hawezi kusubiri kukamilisha mpango Wake na kuokoa watu Anaotaka kuokoa? Katika hali hizi, Mungu anajali kuhusu nini zaidi? Si vile wale wasiomfuata Yeye kabisa au wale wanaompinga Yeye kwa vyovyote vile wanamshughulikia Yeye au kumpinga Yeye, au namna ambavyo mwanadamu anamdanganya Yeye. Anajali tu kuhusu kama wale wanaomfuata Yeye, walengwa wa wokovu Wake katika mpango Wake wa usimamizi, wamewekwa kamili na Yeye, na kama wametimiza utoshelezi Wake. Kuhusiana na watu wale wengine bali na wale wanaomfuata Yeye, Anawatolea tu adhabu kidogo mara kwa mara ili kuonyesha ghadhabu Yake. Kwa mfano tsunami, mitetemeko ya ardhi, kuibuka kwa volkano na kadhalika. Wakati huohuo, Anawalinda kwa dhati na kuwashughulikia wale wanaomfuata Yeye na karibu wanaokolewa na Yeye. Tabia ya Mungu ni hii: Kwa mkono mmoja, Anaweza kuwapatia watu Anaonuia kutekeleza subira na ustahimilivu kamili wa kupindukia na kuwasubiria wao kwa muda mrefu Anavyoweza; kwa mkono mwingine, Mungu anachukia na kuchukizwa kwa dhati na watu wa aina ya Shetani wasiomfuata Yeye na wanaompinga Yeye. Ingawaje Hajali kama hawa watu wa aina ya Shetani wanamfuata au wanamwabudu Yeye, bado Anawachukia wao huku akiwa na subira na wao katika moyo Wake, na Anapoamua mwisho wa hawa watu wa aina ya Shetani, Yeye pia anasubiria kufika kwa hatua za mpango Wake wa usimamizi.

Hebu tuangalie kifungu kinachofuata.

2. Baraka za Mungu kwa Nuhu Baada ya Gharika

Mwa 9:1-6 Naye Mungu akawabariki Nuhu na wana wake, na akasema kwao, Ninyi Zaeni, na muongezeke, na muijaze tena dunia. Na wanyama wote wa dunia watawaogopa na kuwa na hofu nanyi, na ndege wote wa angani, na vyote vitembeavyo duniani, na kila samaki wa baharini; wamewekwa katika mikono yenu. Kila kisongacho kilicho na uhai kitakuwa chakula chenu, jinsi ambavyo nimewapa mboga ndivyo ninavyowapa vitu vyote. Lakini nyama iliyo na uhai, ambayo ni damu yake, ninyi msiile. Na bila shaka nitahitaji damu yenu ya uhai wenu, nitaihitaji kwa mkono wa kila mnyama, na kwa mkono wa mwanadamu, nitahitaji uhai wa mwanadamu kwa mkono wa ndugu wa kila mwanadamu. Yeyote ambaye atamwaga damu ya mwanadamu, damu yake itamwagika na mwanadamu: kwa kuwa Mungu alimfanya mwanadamu kwa mfano Wake.

Ni nini mnachoona katika kifungu hiki? Kwa nini Nikachagua mistari hii? Kwa nini Sikuchukua dondoo la Nuhu na maisha ya familia yake kwenye safina? Kwa sababu maelezo haya hayana muunganisho mwingi na mada ambayo tunawasiliana leo. Kile tunachotilia maanani ni tabia ya Mungu. Kama mnataka kujua kuhusu maelezo hayo, basi mnaweza kuchukua Biblia ili muweze kujisomea mwenyewe. Hatutaizungumzia hiyo hapa. Kitu kikuu tunachozungumzia leo ni kuhusu namna ya kujua matendo ya Mungu.

Baada ya Nuhu kukubali maagizo ya Mungu na kujenga safina na kuishi katika siku zile husika Mungu alitumia gharika ili kuangamiza ulimwengu, familia yake nzima ya wanane ilinusurika. Mbali na familia ya Nuhu ya wanane, wanadamu wote waliangamizwa, na viumbe wote nchini wakaangamizwa. Kwa Nuhu, Mungu alimpa baraka, na akasema baadhi ya mambo kwake na watoto wake wa kiume. Mambo haya yalikuwa yale ambayo Mungu alikuwa akimpa yeye na pia baraka zake kwake yeye. Hizi ndizo baraka na ahadi Mungu humpa yule ambaye anaweza kumsikiliza Yeye na kuyakubali maagizo Yake, na pia namna anavyotuza watu. Hivi ni kusema, haijalishi kama Nuhu alikuwa binadamu mtimilifu au alikuwa binadamu mwenye haki mbele ya macho ya Mungu, na haijalishi ni kiwango kipi alichomjua Mungu, kwa ufupi, Nuhu na watoto wake wa kiume watatu wote waliyasikiliza maneno ya Mungu, wakaratibu na kazi ya Mungu, na kufanya kile walichofaa kufanya kulingana na maagizo ya Mungu. Kutokana na hayo, walimsaidia Mungu kuweza kubakiza binadamu na aina mbalimbali za viumbe walio na uhai baada ya kuangamizwa kwa ulimwengu na gharika, na hivyo wakawa wamefanya mchango mkubwa kwa hatua iliyofuata ya mpango wa usimamizi wa Mungu. Kwa sababu ya kila kitu alichokuwa amefanya, Mungu alimbariki. Pengine kwa watu wa leo, kile alichofanya Nuhu hakikuwa sana na thamani ya kutajwa. Baadhi wanaweza hata kufikiria: Nuhu hakufanya chochote; Mungu alikuwa ameamua akilini Mwake kumhifadhi, hivyo kwa hakika angehifadhiwa. Kuwepo kwake si kwa sababu yake. Hili ndilo jambo ambalo Mungu alitaka lifanyike, kwa sababu binadamu ni mtulivu. Lakini hicho sicho Mungu alikuwa anafikiria. Kwa Mungu, haijalishi kama mtu ni mkubwa au asiye wa maana, mradi tu aweze kumsikiliza Yeye, kutii maagizo Yake na kile anachomwaminia na aweze kushirikiana na kazi Yake, mapenzi Yake, na mpango Wake, ili mapenzi Yake na Mpango Wake iweze kukamilika vizuri, basi mwenendo wake unastahili kukumbukwa na Yeye na kustahili kupokea baraka Zake. Mungu huthamini sana watu kama hao, na Yeye Hupenda sana vitendo vyao na upendo wao na huba yao Kwake. Huu ndio mwelekeo wa Mungu. Hivyo kwa nini Mungu alimbariki Nuhu? Kwa sababu hivi ndivyo Mungu anavyoshughulikia vitendo kama hivyo na utiifu wa mwanadamu.

Kuhusiana na baraka za Mungu kwa Nuhu, baadhi ya watu watasema: “Kama binadamu atamsikiliza Mungu na kumtosheleza Mungu, basi Mungu anafaa kumbariki binadamu. Je, hilo halifanyiki hivyo bila kusema?” Tunaweza kusema hivyo? Baadhi ya watu husema: “La.” Kwa nini hatuwezi kusema hivyo? Baadhi ya watu husema: “Binadamu hastahili kufurahia baraka za Mungu.” Hilo si sahihi kabisa. Kwa sababu wakati mtu anapokubali kile Mungu amemwaminia, Mungu anacho kiwango cha kuhukumu kama vitendo vya mtu huyu ni vizuri au vibaya na kama mtu huyu amemtii, na kama mtu huyu ametosheleza mapenzi ya Mungu na kama kile anachofanya kimeruhusiwa. Kile anachojali Mungu ni kuhusu moyo wa mtu huyu, si vitendo vyake vya juujuu. Si jambo kwamba Mungu anafaa kubariki mtu mradi tu afanye hivyo, licha ya namna anavyofanya hivyo. Huku ni kutoelewa kwa watu kumhusu Mungu. Mungu huangalia tu mwisho wa matokeo ya mambo, lakini Anatilia mkazo zaidi kuhusu namna moyo wa mtu ulivyo na namna mwelekeo wa mtu ulivyo wakati wa maendeleo ya mambo, na Anaangalia kama kunao utiifu, utiliaji maanani, na tamanio ya kumtosheleza Mungu ndani ya moyo wake. Nuhu alijua kiasi kipi kumhusu Mungu wakati huo? Kiasi hicho kilikuwa kingi kama mafundisho ya dini mnayojua sasa? Kuhusu dhana za ukweli kama vile dhana na maarifa ya Mungu, alipokea kunyunyizia na uchungaji kama ninyi? La, hakupokea! Lakini kunao ukweli mmoja ambao haupingiki: Katika fahamu, akili, na hata kina cha mioyo ya watu wa leo, dhana zao na mwelekeo wao kwa Mungu umejaa ukungu na haueleweki. Mnaweza hata kusema kwamba sehemu fulani ya watu inashikilia mwelekeo mbaya kwa uwepo wa Mungu. Lakini katika moyo wa Nuhu na fahamu yake, uwepo wa Mungu ulikuwepo na bila shaka, na hivyo basi utiifu wake kwa Mungu ulikuwa haujatiwa doa wala toa na ungeweza kustahimili majaribio. Moyo wake ulikuwa safi na wazi kwa Mungu. Hakuhitaji maarifa ya mafundisho ya dini mengi mno ili kujishawishi kufuata kila neno la Mungu, wala hakuhitaji ukweli mwingi kuthibitisha uwepo wa Mungu, ili akubali kile Mungu alimwaminia na kuweza kufanya chochote kile ambacho Mungu angemruhusu kufanya. Hii ni tofauti muhimu kati ya Nuhu na watu wa leo, na pia ndio ufasili wa kweli hasa kuhusu binadamu mtimilifu alivyo machoni mwa Mungu. Kile anachotaka Mungu ni watu kama Nuhu. Yeye ni aina ya mtu anayesifiwa na Mungu, na pia hasa mtu wa aina ile ambaye Mungu hubariki. Mmepokea nuru yoyote kutoka haya? Watu huangalia watu kutoka nje, huku naye Mungu anaangalia mioyo ya watu na kiini chao. Mungu hamruhusu yeyote kuwa na moyo wowote wa kukosa ari au shaka kwake Yeye, wala Hawaruhusu watu kushuku au kumjaribu Yeye kwa njia yoyote ile. Hivyo, ingawaje watu wa leo wako uso kwa uso na neno la Mungu, au mnaweza hata sema kwamba wako uso kwa uso na Mungu, kutokana na kitu kilicho ndani ya mioyo yao, uwepo wa kiini chao potovu, na mwelekeo wao wenye ukatili kwake Yeye, wamezuiliwa kutoka kwa imani yao ya kweli kwa Mungu na kuzibwa kutoka kwa utiifu wao kwake Yeye. Kwa sababu ya haya, ni vigumu sana kwao kutimiza baraka sawa ambazo Mungu alikabidhi Nuhu.

Kisha, hebu tuangalie sehemu hii ya maandiko kuhusu namna Mungu alivyounda upinde wa mvua kama ishara ya Agano lake na binadamu.

3. Mungu Atumia Upinde wa Mvua Kama Ishara ya Agano Lake na mwanadamu

Mwa 9:11-13 Na nitaweka agano Langu na ninyi, wala miili yote haitaondolewa tena na maji ya gharika; wala hakutakuwa na gharika tena kuiharibu dunia. Naye Mungu akasema, Hii ni alama ya agano ambayo naifanya kati ya Mimi na ninyi na viumbe vyote vyenye uhai vilivyo nanyi, kwa vizazi vya kudumu: naweka upinde Wangu mawinguni, na utakuwa alama ya agano kati ya Mimi na dunia.

Watu wengi zaidi wanajua upinde wa mvua ni nini na wamesikia baadhi ya hadithi zinazohusiana na pinde za mvua. Kuhusiana na hadithi ile ya upinde wa mvua kwenye biblia, baadhi wa watu wanaisadiki, baadhi wanaichukulia tu kama hadithi ya kale, huku wengine hawaisadiki kamwe. Haijalishi ni nini, kila kitu kilichofanyika kuhusiana na upinde wa mvua ndicho kila kitu ambacho Mungu Alifanya hapo awali, na mambo yaliyofanyika katika mchakato huu wa usimamizi wa Mungu wa binadamu. Mambo haya yamerekodiwa vivyo hivyo kwenye Biblia. Rekodi hizi hazituambii chochote kuhusu hali ya Mungu ilivyokuwa wakati huo au nia zake nyuma ya maneno haya ambayo Mungu alisema. Zaidi, hakuna anayeweza kutambua ni nini Mungu alikuwa akihisi Aliposema maneno hayo. Hata hivyo, hali ya akili ya Mungu kuhusiana na hiki kitu chote inafichuliwa katikati ya mistari ya maandishi. Ni kana kwamba fikira zake wakati huo zinatoka kwenye ukurasa kupitia kila neno na kauli ya neno la Mungu.

Fikira za Mungu ni kile ambacho watu wanafaa kujali kuhusu na kile wanafaa kujaribu kujua zaidi. Hii ni kwa sababu fikira za Mungu zinahusiana kwa karibu na uelewa wa binadamu wa Mungu na uelewa wa binadamu wa Mungu ni kiungo muhimu sana kwa kuingia kwa binadamu katika maisha. Hivyo ni nini alichokuwa akifikiria Mungu wakati huo mambo haya yalipofanyika?

Hapo mwanzo, Mungu aliumba binadamu ambao katika macho Yake walikuwa wazuri sana na karibu na Yeye, lakini waliangamizwa na gharika baada ya kuasi dhidi Yake. Je, ilimwumiza Mungu kwamba binadamu kama hao walitoweka tu papo hapo hivyo? Bila shaka Aliumizwa! Kwa hivyo Maonyesho Yake ya maumivu haya yalikuwa nini? Ilirekodiwa vipi kwenye Biblia? Ilirekodiwa kwenye Biblia kama: “Na nitaweka agano langu na ninyi, wala miili yote haitaondolewa tena na maji ya gharika; wala hakutakuwa na gharika tena kuiharibu dunia.” Sentensi hii rahisi inafichua fikira za Mungu. Kuangamizwa huku kwa ulimwengu kulimpa Yeye maumivu sana. Kwa maneno ya binadamu, Alikuwa na huzuni sana. Tunaweza kufikiria: Ni vipi ambavyo dunia iliyokuwa imejaa maisha inavyofanana baada ya kuangamizwa na gharika? Ni vipi ambavyo dunia iliyokuwa imejaa binadamu inavyofanana hivi sasa? Hakuna makazi ya binadamu, hakuna viumbe walio hai, maji kila mahali na machafuko kabisa juu ya maji. Hilo ndilo lililokuwa onyesho la kusudio la asili ya Mungu wakati alipoumba ulimwengu? Bila shaka la! Nia asilia ya Mungu ilikuwa ni kuyaona maisha katika maeneo yote, kuwaona wanadamu Aliowaumba wakimwabudu Yeye, si tu kwa Nuhu kuwa mtu pekee anayemwabudu, au kuwa wa pekee ambaye angejibu mwito Wake ili kukamilisha kile alichoaminiwa kufanya. Wakati binadamu walitoweka, Mungu hakuona kile alichonuia awali lakini kinyume cha mambo. Ni vipi ambavyo moyo Wake usingekuwa katika maumivu? Hivyo Alipokuwa akifichua tabia Yake na kuelezea hisia Zake, Mungu alifanya uamuzi. Ni aina gani ya uamuzi Alifanya? Kuunda uta mawinguni (upinde wa mvua tunaouona) kama agano na binadamu, ahadi kwamba Mungu hangemwangamiza mwanadamu kwa gharika tena. Wakati huohuo, ulikuwa pia ni kuwaambia watu kwamba Mungu aliwahi kuangamiza ulimwengu kwa gharika, kumfanya mwanadamu kukumbuka milele ni kwa nini Mungu alifanya kitu kama hicho.

Je, kuangamizwa kwa ulimwengu wakati huu kulikuwa ni jambo alilotaka Mungu? Bila shaka lilikuwa ni jambo asilotaka Mungu Huenda tukaweza kufikiria sehemu ndogo ya picha ile ya kusikitikia ya ulimwengu baada ya kuangamizwa kwa ulimwengu lakini hatuwezi kukaribia kufikiria namna hali ilivyokuwa wakati huo mbele ya macho ya Mungu. Tunaweza kusema kwamba, haijalishi kama ni watu wa sasa au wa wakati huo, hakuna yeyote anayeweza kufikiria au kutambua ni vipi Mungu alikuwa akihisi Aliposhuhudia tukio hilo, picha hiyo ya ulimwengu baada ya kuangamizwa kwake kwa gharika. Mungu alilazimishwa kufanya haya kutokana na kutotii kwa binadamu, lakini maumivu ambayo moyo wa Mungu ulipitia kutokana na maangamizo haya ya ulimwengu kwa gharika ni uhalisia ambao hakuna anayeweza kuufikiria au kuutambua. Ndiyo maana Mungu aliweka agano na mwanadamu, ambalo lilikuwa ni kuambia watu kukumbuka kwamba Mungu aliwahi kufanya kitu kama hiki, na kuapa kwamba Mungu asingewahi kuangamiza ulimwengu kwa njia hii tena. Katika agano hili, tunauona moyo wa Mungu—tunaona kwamba moyo wa Mungu ulikuwa katika maumivu Alipoangamiza binadamu hawa. Katika lugha ya binadamu, wakati Mungu aliangamiza mwanadamu na Akaona mwanadamu akitoweka, moyo Wake ulikuwa ukiomboleza na kuvuja damu. Je, hivyo sivyo tunavyoweza kuifafanua kwa njia bora zaidi? Maneno haya yanatumika na binadamu kuonyesha hisia za binadamu, lakini kwa sababu lugha ya binadamu inao ukosefu mwingi, kuitumia kufafanua hisia za Mungu hakuonekani kuwa mbaya sana kwangu Mimi, na wala si kubwa mno. Angaa inawapa uelewa sahihi kabisa, wa kufaa zaidi, wa hali ya Mungu ilivyokuwa wakati huo. Sasa mtafikiria nini mtakapouona upinde wa mvua tena? Angaa mtakumbuka namna ambavyo Mungu aliwahi kuwa katika huzuni kwa sababu ya kuangamiza ulimwengu kwa gharika. Mtakumbuka namna, hata kama Mungu aliuchukia ulimwengu huu na kudhalilisha binadamu hawa, Alipowaangamiza wanadamu Alioumba kwa mikono Yake mwenyewe, moyo Wake ulikuwa ukisononeka, ukipambana kuachilia, ukihisi kusita, na kuhisi vigumu kuvumilia mambo. Tulizo lake pekee lilikuwa katika familia ya wanane ya Nuhu. Ulikuwa ni ushirikiano wa Nuhu uliofanya jitihada Zake za kipekee za kuumba viumbe wote kuwa cha thamani. Kwa wakati ambao Mungu alikuwa akiteseka, hili ndilo jambo tu ambalo lingeweza kusawazisha maumivu Yake. Kuanzia hapo, Mungu aliweka matarajio Yake yote ya binadamu kwa familia ya Nuhu, akitumai kwamba wangeishi chini ya baraka Zake na si laana Yake, akitumai kwamba wasingewahi kumwona Mungu akiuangamiza ulimwengu kwa gharika na pia akitumai kwamba wasingeangamizwa.

Ni sehemu gani ya tabia ya Mungu tunayofaa kuelewa kutoka hapa? Mungu alikuwa amemdharau binadamu kwa sababu binadamu alikuwa na uadui na Yeye, lakini ndani ya moyo Wake, utunzaji Wake, kujali Kwake, na huruma Yake kwa binadamu vilibakia vilevile. Hata wakati alipowaangamiza wanadamu, moyo Wake hukubadilika. Wakati binadamu walikuwa wamejaa upotovu na kutotii Mungu hadi katika kiwango fulani, Mungu alilazimika, kwa sababu ya tabia Yake na kiini Chake, na kulingana na kanuni Zake, kuangamiza binadamu hao. Lakini kwa sababu ya kiini cha Mungu, bado Alisikitikia binadamu, hata Akataka kutumia njia mbalimbali za kuwakomboa wanadamu ili waweze kuendelea kuishi. Badala yake, binadamu alimpinga Mungu, akaendelea kutomtii Mungu, na kukataa kukubali wokovu wa Mungu, yaani, alikataa kukubali nia Zake nzuri. Haijalishi ni vipi Mungu aliwaita wao, aliwakumbusha, akawatosheleza haja zao, akawasaidia wao, au akawavumilia wao, binadamu hakutambua haya, wala hakutilia maanani. Katika maumivu Yake, Mungu bado hakusahau kumpa binadamu uvumilivu Wake wa kiwango cha juu zaidi, akisubiri binadamu kugeuka na kubadilika. Baada ya Yeye kufikia kikomo Chake, Alifanya kile Alicholazimika kufanya bila ya kusita. Kwa maneno mengine, kulikuwa na kipindi cha muda mahususi na mchakato kutoka pale ambapo Mungu alipanga kuangamiza wanadamu hadi katika mwanzo rasmi wa kazi Yake ya kuwaangamiza wanadamu. Mchakato huu ulikuwepo kwa kusudio la kumwezesha binadamu kugeuka, na ndio uliokuwa fursa ya mwisho ya Mungu kumpa binadamu. Hivyo ni nini ambacho Mungu alifanya kwenye kipindi hiki kabla ya kuangamiza wanadamu? Mungu alifanya kiwango kikubwa cha kazi ya kukumbusha na kazi ya kusihi. Haijalishi ni maumivu kiasi kipi na huzuni ambayo ilikuwa ndani ya moyo wa Mungu, Aliendelea kufanyisha zoezi utunzaji Wake, wasiwasi, na huruma nyingi juu ya binadamu. Tunaona nini kutoka kwa haya? Bila shaka, tunaona kwamba upendo wa Mungu kwa wanadamu ni wa kweli na si tu jambo ambalo Analizungumzia tu bila matendo. Ni jambo hakika, linaloweza kushikika na kutambulika, si bandia, halijatiwa najisi, halidanganyi wala halisingizii. Mungu kamwe hatumii uongo au kuunda taswira za bandia ili kufanya watu kuona kwamba Yeye anapendeka. Kamwe hatumii ushuhuda wa uongo ili kuwafanya kuona uzuri Wake, au kuringia uzuri wake na utakatifu Wake. Je, dhana hizi za tabia ya Mungu zinastahili upendo wa binadamu? Kwani nazo hazistahili kuabudiwa? Kwani nazo hazistahili kupendwa sana? Kwa sasa, Ningependa kuwauliza: Baada ya kuyasikia maneno haya, mnafikiri kwamba ukubwa wa Mungu ni maneno matupu tu kwenye kipande cha karatasi? Je, uzuri wake Mungu ni maneno matupu tu? La! Bila shaka la! Mamlaka ya juu, ukubwa, utakatifu, uvumilivu, upendo, wa Mungu na kadhalika—kila utondoti wa kila mojawapo ya vipengele vya tabia ya Mungu na kiini Chake unapata maonyesho ya vitendo kila wakati Anapoanza kazi Yake, zikiwa katika mapenzi Yake kwa binadamu, na pia zikitimizwa na kuonyeshwa kwa kila mtu. Licha ya kama umewahi kuzihisi awali, Mungu anamtunza kila mtu katika kila njia inayowezekana, kwa kutumia moyo Wake wa dhati, hekima, na mbinu mbalimbali ili kupashana mioyo ya kila mtu, na kuzindua roho ya kila mmoja. Huu ni ukweli usiopingika. Haijalishi ni watu wangapi wameketi hapa, kila mtu amekuwa na uzoefu tofauti na hisia tofauti kwa ustahimilivu, uvumilivu, na uzuri wake Mungu. Uzoefu huu wote wa Mungu na hisia hizi au utambuzi wa Yeye—kwa ufupi, mambo haya yote mazuri yanatoka kwa Mungu. Hivyo kwa kutangamanisha uzoefu wa kila mmoja na maarifa ya Mungu na kuziweka kwa pamoja na masomo yetu ya vifungu hivi vya Biblia leo, je sasa unao uelewa halisi na bora zaidi kumhusu Mungu?

Baada ya kuisoma hadithi hii na kuelewa baadhi ya tabia za Mungu zilizofichuliwa kupitia kwa hafla hii, ni aina gani mpya kabisa ya shukrani mliyo nayo kwa Mungu? Je, imewapa uelewa wa kina zaidi wa Mungu na moyo Wake? Mnahisi tofauti sasa mnapoiangalia hadithi ya Nuhu tena? Kulingana na maoni yenu, ingehitajika kufanya mawasiliano ya mistari hii ya Biblia? Kwa vile tumewasiliana kuihusu, mnafikiria kwamba ilihitajika? Ilihitajika, siyo? Ingawaje kile tulichosoma ni hadithi, ni rekodi ya kweli ya kazi ya Mungu ambayo aliwahi kuifanya. Nia yangu haikuwa kuwawezesha kufahamu maelezo ya hadithi hizi au mhusika huyu, wala haikuwa kwamba mweze kuenda kusomea kuhusu mhusika huyu, na bila shaka si eti mweze kurudi katika uchambuzi wa Biblia tena. Mnaelewa? Hivyo, hadithi hizi zimesaidia maarifa yenu ya Mungu? Hadithi hii imeongezea nini uelewa wenu wa Mungu? Twambie, kina kaka na kina dada kutoka Hong Kong. (Tuliona kwamba upendo wa Mungu ni kitu ambacho hakuna yeyote kati yetu binadamu potovu anamiliki.) Twambie, akina kaka na akina dada kutoka Korea Kusini. (Upendo wa Mungu kwa binadamu ni wa kweli. Upendo wa Mungu kwa binadamu unao tabia Yake na unabeba ukuu Wake, utakatifu, uongozi, na ustahimilivu Wake. Inafaa sisi tujaribu kupata uelewa wa kina zaidi.) (Kupitia kwa mawasiliano ambayo tumetoka kuwa nayo, kwa upande mmoja Ninaweza kuona haki ya Mungu na tabia ya kitakatifu, na Ninaweza pia kuona wasiwasi alionao Mungu kwa mwanadamu, rehema za Mungu kwa mwanadamu, na kwamba kila kitu anachofanya Mungu na kila fikira na wazo Alilonalo linafichua upendo na kujali Kwake kwa binadamu.) (Uelewa wangu katika siku zilizopita ulikuwa kwamba Mungu alitumia gharika kuangamiza ulimwengu kwa sababu mwanadamu alikuwa amegeuka na kuwa mwovu kwa kiwango fulani, na ilikuwa ni kana kwamba Mungu aliangamiza binadamu hawa kwa sababu Aliuchukia. Ilikuwa tu baada ya Mungu kuzungumza kuhusu hadithi ya Nuhu leo na Akasema ya kwamba moyo wa Mungu ulikuwa unavuja ndipo Ninatambua kwamba Mungu alikuwa kwa hakika shingo upande kuachilia binadamu hawa. Ilikuwa tu ni kwa sababu mwanadamu alikuwa mtovu wa kusikia sana kiasi cha kwamba Mungu alikuwa hana chaguo lakini kumwangamiza. Kwa hakika, moyo wa Mungu wakati huo ulikuwa umesikitika sana. Kutokana na haya Ninaweza kuona katika tabia ya Mungu utunzaji na kujali Kwake kwa mwanadamu. Hili ni jambo ambalo Sikulijua awali.) Vizuri sana! Mnaweza kwenda kwa kifuatacho. (Niliathiriwa sana baada ya kusikiliza. Nimeisoma Biblia kitambo, lakini sijawahi kuwa na uzoefu kama leo pale ambapo Mungu anachambua kwa njia ya moja kwa moja mambo haya ili tuweze kumjua Yeye. Kwa Mungu kutushika mkono kuweza kuona Biblia inanifanya nijue kwamba kiini cha Mungu kabla ya kupotoshwa kwa binadamu kilikuwa ni upendo na utunzaji kwa mwanadamu. Tangu wakati ule binadamu alipopotoka hadi katika siku za mwisho za sasa, ingawaje Mungu anayo tabia ya haki, upendo na utunzaji Wake unabakia vilevile, haubadiliki. Hii inaonyesha kwamba kiini cha upendo wa Mungu, kuanzia uumbaji hadi sasa, licha ya kama binadamu amepotoka, haubadiliki.) (Leo niliona kwamba kiini cha Mungu hakitabadilika kutokana na mabadiliko ya muda au mahali pa kazi Yake. Niliona pia kwamba, haijalishi kama Mungu anauumba ulimwengu au anauangamiza baada ya binadamu kupotoka, kila kitu Anachofanya kina maana na kinayo tabia Yake. Hivyo basi niliona kwamba upendo wa Mungu hauna kikomo na haupimiki, niliona pia, kama vile ambavyo wale kaka na dada wengine, utunzaji na rehema ya Mungu kwa mwanadamu wakati Alipouangamiza ulimwengu.) (Haya ni mambo kwa hakika sikuyajua kuhusu hapo awali. Baada ya kusikiliza leo, nahisi kwamba Mungu ni wa ajabu kwa kweli, wa kuaminika kwa kweli, anayestahili kusadikiwa, na kwamba kwa kweli Yupo. Ninaweza kutambua kwa dhati ndani ya moyo wangu kwamba tabia ya Mungu na upendo wa Mungu kwa kweli ni vitu vinavyoshikika. Hii ndiyo hisia niliyo nayo baada ya kusikiliza leo.) Safi kabisa! Yaonekana nyote mmechukua kile mlichosikia na kukitia moyoni.

Je, mmetambua ukweli fulani kutoka mistari yote ya Biblia, zikiwemo hadithi zote za Biblia tulizowasiliana leo? Je, Mungu amewahi kutumia lugha Yake mwenyewe ili kuelezea fikira Zake binafsi au kuelezea upendo na utunzaji Wake kwa binadamu? Kunayo rekodi ya Yeye kutumia lugha ya kawaida kutaja ni kiasi kipi ambacho Anajali na Anapenda mwanadamu? La! Je, si hayo ni kweli? Kunao wengi sana miongoni mwenu ambao wamesoma Biblia au vitabu vingine mbali na Biblia. Je, yupo yeyote kati yenu aliyeyaona maneno kama hayo? Jibu bila shaka ni la! Yaani, kwenye rekodi za Biblia, yakiwemo maneno ya Mungu au urekodi wa kazi Yake, Mungu hajawahi katika enzi yoyote au kipindi chochote kile kutumia mbinu Zake mwenyewe kufafanua hisia Zake au kuelezea upendo na utunzaji Wake kwa mwanadamu wala Mungu hajawahi kutumia matamshi au vitendo kufikisha hisia na mawazo Yake—Je, si hiyo ni ukweli? Kwa nini Ninasema hivyo? Kwa nini lazima Nitaje hii? Ni kwa sababu hii pia inayo uzuri wa Mungu na tabia Yake.

Mungu aliwaumba wanadamu; licha ya kama wamepotoka au kama wanamfuata Yeye, Mungu hushughulikia binadamu kama wapendwa Wake wanaothaminiwa zaidi—au kama vile binadamu wangesema, watu walio wapenzi Wake sana—na wala si kama vikaragosi Wake. Ingawaje Mungu anasema Yeye ndiye muumba na kwamba binadamu ni uumbaji Wake, hali ambayo inaweza kuonekana ni kana kwamba kuna tofauti kiasi katika mpangilio wa cheo, uhalisia ni kwamba kila kitu ambacho Mungu amefanya kwa mwanadamu kinazidi kabisa uhusiano wa asili hii. Mungu anampenda mwanadamu, anamtunza mwanadamu, na anaonyesha kwamba anamjali mwanadamu, pamoja na kumkimu mwanadamu bila kuacha na bila ya kusita. Kamwe hahisi katika moyo Wake kwamba hii ni kazi ya ziada au ni kitu kinachostahili sifa nyingi. Wala Hahisi kwamba kuokoa binadamu, kuwatosheleza, na kuwapatia kila kitu, ni kutoa mchango mkuu kwa binadamu. Anamkimu tu mwanadamu kimyakimya na kwa unyamavu, kwa njia Yake mwenyewe na kupitia kwa kiini Chake na kile Anacho na alicho. Haijalishi ni toleo kiasi kipi na ni msaada kiasi kipi ambao wanadamu wanapokea kutoka kwa Yeye, Mungu siku zote hajawahi kufikiri kuhusu au kujaribu kutaka sifa yoyote. Hii inaamuliwa na kiini cha Mungu, na pia hasa ni maonyesho ya kweli pia ya tabia ya Mungu. Na ndio maana, haijalishi kama iko kwa Biblia au kitabu chochote kingine, hatujawahi kumpata Mungu akionyesha fikira Zake, na hatujawahi kumpata Mungu akifafanua au akitangazia wanadamu ni kwa nini Anafanya mambo haya, au ni kwa nini Anamjali sana mwanadamu, ili kumfanya mwanadamu kumshukuru Yeye au kumsifu Yeye. Hata wakati Amejeruhiwa, wakati moyo Wake umo katika maumivu makali, Hajawahi kusahau jukumu Lake kwa mwanadamu au wasiwasi Wake kwa mwanadamu, huku haya yote yakiendelea, Anavumilia madhara na maumivu akiwa pekee katika ukimya. Kinyume cha mambo ni kwamba, Mungu anaendelea kumkimu mwanadamu kama Anavyofanya siku zote. Ingawaje mwanadamu mara nyingi humsifia Mungu au huwa na ushuhuda Kwake, hakuna kati ya tabia hii ambayo imedaiwa na Mungu. Hii ni kwa sababu Mungu hajawahi kunuia mambo yoyote mazuri Anayomfanyia binadamu yeye pia naye kumfanyia vivyo hivyo kama ishara ya shukrani au ili iweze kuonekana kwamba anafanyiwa mazuri aliyofanya. Kwa mkono mwingine, wale wanaomcha Mungu na kujiepusha na maovu, wale wanaomfuata Mungu kwa kweli, wanaomsikiliza Yeye, na walio waaminifu Kwake yeye, na wale wanaomtii Yeye—hawa ndio watu ambao mara nyingi watapokea baraka za Mungu, na Mungu atawakabidhi baraka hizo bila kusita. Isitoshe, baraka ambazo watu hupokea kutoka kwa Mungu mara nyingi zinazidi kufikiria kwao na pia zinazidi kitu chochote ambacho binadamu wanaweza kubadilishana na yale waliyofanya au gharama waliyolipia. Wakati mwanadamu anafurahia baraka za Mungu, Je, yupo yeyote anayejali ni nini Mungu anafanya? Je, yupo yeyote anayeonyesha wasiwasi wowote kuhusu vile ambavyo Mungu anahisi? Je, yupo yeyote anayethamini maumivu ya Mungu? Jibu la uhakika la maswali haya ni: La! Je, mwanadamu yeyote, akiwemo Nuhu, anaweza kuthamini yale maumivu ambayo Mungu alikuwa akihisi wakati huo? Je, mtu yeyote anaweza kufahamu ni kwa nini Mungu alianzisha agano kama hilo? Hakuna anayeweza! Mwanadamu hathamini maumivu ya Mungu si kwa sababu hawezi kuelewa maumivu ya Mungu, na si kwa sababu ya nafasi iliyopo kati ya Mungu na mwanadamu au tofauti kati ya hadhi yao; badala yake, ni kwa sababu mwanadamu hata hajali kuhusu hisia zozote za Mungu. Mwanadamu anafikiria Mungu yuko huru—Mungu hahitaji watu wa kujali kuhusu Yeye, kumwelewa au kumwonyesha namna anavyomfikiria. Mungu ni Mungu, hivyo Hana maumivu, hana hisia; Hatakasirika, Hahisi huzuni, hata Halii. Mungu ni Mungu, hivyo Hahitaji maonyesho yoyote ya kihisia na Hahitaji faraja yoyote ya kihisia. Kama Hahitaji mambo haya katika hali fulani, basi Atatatua mwenyewe na Hatahitaji usaidizi wowote kutoka kwa mwanadamu. Lakini kinyume chake ni kuwa, ni wale binadamu wanyonge, wanaohitaji tulizo, toshelezo, himizo la Mungu na hata pia kwake Yeye kuweza kutuliza hisia zao wakati wowote mahali popote. Fikira kama hiyo inajificha ndani kabisa ya mioyo ya mwanadamu: Binadamu ndiye mnyonge; wanahitaji Mungu ili awatunze kwa kila njia, wanastahili utunzaji wote wanaopokea kutoka kwa Mungu, na wanafaa kudai kutoka kwa Mungu chochote kile wanachohisi kinafaa kuwa ni chao. Mungu ndiye mwenye Nguvu; Anacho kila kitu, na Anahitaji kuwa mlezi wa mwanadamu na Anayetoa baraka. Kwa sababu Yeye tayari ni Mungu, Yeye Mwenyezi na Hahitaji katu chochote kutoka kwa mwanadamu.

Kwa vile binadamu hatilii maanani ufunuo wowote wa Mungu, hajawahi kuhisi huzuni, maumivu au furaha ya Mungu. Lakini kinyume chake ni kwamba, Mungu anajua maonyesho yote ya binadamu kama vile anavyojua sehemu ya kiganja cha mkono Wake. Mungu hutosheleza mahitaji ya kila mtu siku zote na pahali pote, akiangalia fikira zinazobadilika za kila mmoja na hivyo basi kuwatuliza na kuwahimiza, na kuwaongoza na kuwaangazia. Kuhusu mambo yote ambayo Mungu amemfanyia mwanadamu, na gharama zote Alizolipia kwa sababu yao, watu wanaweza kupata kifungu kutoka kwa Biblia au kutoka kwa chochote ambacho Mungu amesema mpaka sasa kinachoelezea waziwazi kwamba Mungu atadai kitu kutoka kwa binadamu? La! Kinyume cha mambo, haijalishi ni vipi watu wanapuuza kufikiria kwa Mungu, Bado Anawaongoza kwa marudio wanadamu, Anamkimu kwa kurudia mwanadamu na kumsaidia, kuwaruhusu kufuata njia za Mungu ili waweze kupokea hatima nzuri ambayo Amewatayarishia. Inapokuja kwa Mungu, kile Anacho na alicho, neema Yake, rehema Yake, na tuzo Zake zote, zitakabidhiwa bila ya kusita kwa wale wanaompenda na kumfuata Yeye. Lakini hajawahi kufichua kwa mtu yeyote maumivu aliyopitia Yeye au hali ya akili Yake, na katu halalamiki kuhusu yeyote ambaye hamtilii Yeye maanani au hajui mapenzi Yake. Anavumilia tu haya yote kimyakimya, akisubiria siku ambayo mwanadamu ataweza kuelewa.

Kwa nini Nasema mambo haya hapa? Ni nini mnachoona kutoka kwa mambo haya Niliyosema? Kuna kitu katika kiini na tabia ya Mungu ambacho ndicho rahisi zaidi kupuuza, kitu ambacho kinamilikiwa tu na Mungu na wala si mtu yeyote, wakiwemo wale wengine wanafikiria kwamba ni watu wakubwa, watu wazuri, au Mungu wa kufikiria kwao. Kitu hiki ni nini? Ni kule kutokuwa na nafsi kwa Mungu. Tunapozungumzia kutokuwa na nafsi, unaweza kufikiria kwamba pia wewe huna nafsi, kwa sababu inapokuja kwa watoto wako, haujadiliani juu ya bei na wao na wewe ni mkarimu sana kwao, au unafikiria kwamba wewe huna nafsi sana inapokuja kwa wazazi wako. Haijalishi ni nini unafikiria, angaa unayo dhana ya neno “kutokuwa na nafsi” na unalifikiria kama neno zuri, na kwamba kuwa mtu asiye na nafsi ni jambo la kipekee. Wakati huna nafsi, unafikiri kuwa wewe ni mkubwa. Lakini hakuna mtu anayeweza kuona kutokuwa na nafsi kwa Mungu miongoni mwa viumbe wote, miongoni mwa watu, hafla, na vitu, na kupitia kazi ya Mungu. Kwa nini hali iko hivi? Kwa sababu binadamu ni mchoyo sana! Kwa nini Ninasema hivyo? Mwanadamu anaishi katika ulimwengu wa uyakinifu. Unaweza kumfuata Mungu, lakini huoni wala kushukuru namna ambavyo Mungu anakukimu, anavyokupenda na anavyoonyesha kwamba anakujali. Kwa hivyo unaona nini? Unaona watu wako wa ukoo wanaokupenda au kukupenda sana. Unayaona mambo ambayo ni ya manufaa kwa mwili wako, unajali kuhusu watu na vitu unavyopenda. Huku ndiko kutokuwa na nafsi kwa binadamu kunakodaiwa. Watu kama hao “wasiokuwa na nafsi” hata hivyo, huwa hawajali katu kuhusu Mungu anayewapa maisha. Kinyume na Mungu, kutokuwa na nafsi kwa binadamu kunakuwa cha nafsi na yenye uchoyo. Kutokuwa na nafsi ambako binadamu anasadiki katika ni ulio mtupu na usio halisi, uliotiwa madoa, usiolingana na Mungu, na usiohusika na Mungu. Kutokuwa na nafsi kwa binadamu ni kwa ajili yake, huku kutokuwa na nafsi kwa Mungu ni ufunuo wa kweli wa kiini Chake. Ndipo hasa kutokana na kujitolea nafsi kwa Mungu ndipo binadamu anapokea mfululizo usiosita wa ujazo kutoka kwake. Huenda msiathirike sana na mada hii Ninayozungumza kuhusu leo na unaweza kuwa tu unatikisa kichwa chako kwa kukubaliana nami, lakini wakati unapojaribu kufurahia moyo wa Mungu katika moyo wako, utaweza kwa kutojua kugundua: Miongoni mwa watu wote, masuala, na mambo unaweza kuhisi katika ulimwengu huu ni kutokuwa na nafsi tu kwa Mungu ambako ni kweli na dhabiti, kwa sababu ni upendo wa Mungu tu kwako ndio ambao hauna masharti na hauna madoa. Mbali na Mungu, kutokuwa na kile kinachodaiwa kutokuwa na nafsi wa mtu mwingine ni bandia, cha juujuu, kisicho na msingi; kina kusudio, nia fulani, kinatekeleza shughuli ya masikilizano, na hakiwezi kupimwa kamwe. Mnaweza hata kusema kwamba ni ki chafu, na cha kudharauliwa. Je, mnakubali?

Ninajua hamjazoeana na mada hizi na mnahitaji muda kidogo ili ziweze kuingia ndani yenu kabla muweze kuelewa kwa kweli. Kwa kadri mnavyokuwa kwamba hamjazoeana na masuala na mada hizi, ndipo inapothibitisha zaidi kwamba mada hizi zinakosekana katika mioyo yenu. Kama Singetaja mada hizi, yupo yeyote kati yenu ambaye angeweza kujua kidogo kuzihusu? Nasadiki hamngewahi pata kuyajua. Hii ni ya hakika. Haijalishi ni kiasi kipi mnachoweza kufahamu au kuelewa, kwa ufupi, mada hizi Ninazozungumzia ndizo ambazo watu wanakosa sanasana na wanazofaa kujua kuhusu zaidi. Mada hizi ni muhimu kwa kila mmoja—ni zenye thamani na ndiyo maisha, na ni mambo ambayo lazima mmiliki vizuri kwa safari ijayo. Bila ya maneno haya kama mwongozo, bila ya uelewa wako wa tabia ya Mungu na kiini, siku zote utabakia na alama ya kiulizo inapokuja kwa Mungu. Unawezaje kusadiki kwa Mungu kwa njia bora kama hata humwelewi Yeye? Hujui chochote kuhusu hisia Zake, mapenzi Yake, hali ya akili Yake, kile Anachofikiria, nini kinachomfanya Yeye kuwa na huzuni, na nini kinachomfanya Yeye kuwa na furaha, hivyo unawezaje kuweka moyo wa Mungu katika fikira?

Kila wakati Mungu anapokuwa amekasirika, Anakumbana na mwanadamu ambaye hamtilii maanani kamwe, mwanadamu anayemfuata Yeye na anayedai kumpenda Yeye lakini anapuuza kabisa hisia Zake. Moyo Wake utakosaje kuumia? Katika kazi ya usimamizi ya Mungu, Anaitekeleza kwa dhati kazi Yake na Anaongea na kila mmoja Anawatazama bila kizuizi chochote au kujificha, lakini kinyume chake ni kuwa, kila mtu anayemfuata Yeye anatenganishwa na Yeye, na hakuna aliye radhi kujishughulisha na kuwa karibu na Yeye, kuelewa moyo Wake, au kutilia maanani hisia Zake. Hata wale wanaotaka kuwa wandani wa Mungu hawataki kuwa karibu na Yeye, kutilia maanani moyo Wake, au kujaribu kumwelewa Yeye. Wakati Mungu anashangilia na ana furaha, hakuna yeyote yule wa kushiriki katika furaha hiyo na Yeye. Wakati Mungu anakosa kueleweka na watu, hakuna mtu wa kutuliza moyo Wake ulio na majeraha. Wakati moyo Wake unaumia, hakuna hata mtu mmoja aliye radhi kumsikiliza Yeye na kuwa mwandani Wake. Katika hii maelfu ya miaka ya usimamizi wa kazi ya Mungu, hakuna mtu anayeelewa hisia za Mungu, hakuna hata mtu anayefahamu au kutambua hisia Zake, tupilia mbali hata yeyote ambaye angesimama kando ya Mungu ili kushiriki katika furaha na huzuni Zake. Mungu ni mpweke. Yeye ni pweke! Mungu ni mpweke si tu kwa sababu wanadamu waliopotoka wanampinga Yeye, lakini zaidi kwa sababu wale wanaofuatilia kuwa wa kiroho, wale wanaotafuta kumjua Mungu na kumwelewa Yeye, na hata wale walio radhi kujitolea maisha yao yote kwake Yeye, pia hawajui fikira Zake, na hawaielewi tabia Yake na hisia Zake.

Mwishoni mwa hadithi ya Nuhu, tunaona kwamba Mungu alitumia mbinu isiyo ya kawaida kuelezea hisia Zake wakati huo. Mbinu hii ni maalumu sana, na ni kuweka agano na binadamu. Ni mbinu inayotangaza mwisho wa matumizi ya gharika na Mungu katika kuangamiza ulimwengu. Kutoka nje, kuweka agano kunaonekana kuwa jambo lililo la kawaida sana. Si jambo lolote zaidi ya kutumia maneno kufunga wahusika ili wasitende vitendo vitakavyokiuka agano, ili kusaidia kutimiza kusudio la kulinda maslahi ya pande zote mbili. Kwa umbo, ni jambo la kawaida sana, lakini kutoka kwa motisha zilizopo na maana ya Mungu kufanya kitu hiki, ni ufunuo wa kweli wa tabia ya Mungu na hali Yake ya akili. Endapo utayaweka maneno haya kando na kuyapuuza, kama Sitawahi kukuambia ukweli wa mambo, basi binadamu hawatawahi kwa hakika kujua kufikiria kwa Mungu. Pengine katika kufikiria kwako Mungu alikuwa akitabasamu wakati alipofanya agano hili, au pengine maonyesho Yake yalikuwa mazito, lakini haijalishi ni watu wanavyofikiria Mungu alikuwa na maonyesho gani ya kawaida kabisa, hakuna ambaye angeweza kuuona moyo wa Mungu au maumivu Yake, na hata upweke Wake. Hakuna mtu anayeweza kumfanya Mungu kumwamini au anayestahili kuaminiwa na Mungu, au kuwa mtu Anayeweza kueleza fikira Zake au kuwa mwandani Wake wa kuambia maumivu Yake. Ndiyo maana Mungu hakuwa na chaguo ila kufanya kitu kama hicho. Kwa juujuu, Mungu alifanya jambo rahisi la kuwaaga binadamu wale wa awali, kuhitimisha hali ya kale ilivyokuwa na kufikia hitimisho halisi katika kuangamiza Kwake kwa ulimwengu akitumia gharika. Hata hivyo, Mungu alikuwa ameyazika maumivu kutoka muda huu ndani kabisa ya moyo Wake. Kwa wakati ambao Mungu hakuwa na yeyote wa kuita mwandani, aliunda agano na wanadamu, akiwaambia kwamba asingeuangamiza ulimwengu kwa gharika tena. Wakati upinde wa mvua unapojitokeza ni kukumbusha watu kwamba, kitu kama hicho kiliwahi kufanyika, kuwapa onyo watu dhidi ya kufanya maovu. Hata katika hali hiyo ya maumivu, Mungu hakusahau kuwahusu wanadamu na bado akaonyesha kujali kwingi sana kwao. Je, huu si upendo na kutokuwa na nafsi kwa Mungu? Lakini nao watu wanafikiria nini wakati wanapoteseka? Kwani huu si wakati ambao wanamhitaji Mungu zaidi? Katika nyakati kama hizi, siku zote watu humkokota Mungu katika mambo yao ili Mungu aweze kuwapa tulizo. Haijalishi ni lini, Mungu hatawahi kuwavunja moyo watu wake, na siku zote Atawaruhusu watu kutoka katika changamoto zao na kuishi katika mwangaza. Ingawaje Mungu anawakimu wanadamu, ndani wa moyo wa binadamu, Mungu si chochote wala lolote ila tembe ya kumhakikishia tu mambo, dawa ya tulizo. Wakati Mungu anateseka, wakati moyo Wake una majeraha, kuwa na kiumbe aliyeumba au mtu yeyote wa kuwa mwandani wake au wa kumtuliza Yeye kwa kweli kwake Mungu ni tamanio tu la kibadhirifu asiloweza kutegemea. Siku zote binadamu hatilii maanani hisia za Mungu, hivyo Mungu siku zote haulizii wala hatarajii kuwa kuna mtu anayeweza kumtuliza Yeye. Anatumia mbinu Zake mwenyewe kueleza hali Yake. Watu hawafikirii kwamba ni jambo kubwa kwa Mungu kupitia mateso fulani, lakini unapojaribu tu kuelewa Mungu kwa kweli, unapoweza kushukuru kwa dhati, nia nzuri za Mungu katika kila kitu anachofanya, ndipo unapoweza kuhisi ukubwa wa Mungu na kutokuwa na nafsi kwake. Ingawaje Mungu aliunda agano na wanadamu kutumia upinde wa mvua, hakuwahi kuambia yeyote kwa nini alifanya hivi, kwa nini alianzisha agano hili, kumaanisha hakuwahi kuambia mtu fikira Zake halisi. Hii ni kwa sababu hakuna mtu anayeweza kufahamu kina cha upendo ambao Mungu anao kwa wanadamu Aliowaumba kwa mikono Yake mwenyewe, na hakuna pia mtu anayeweza kutambua ni kiasi kipi cha maumivu moyo Wake uliteseka wakati Alipoangamiza binadamu. Hivyo basi, hata kama Angeambia watu namna Anavyohisi, hawawezi kumwamini. Licha ya kuwa katika maumivu, angali Anaendelea na hatua inayofuata ya kazi Yake. Siku zote Mungu Anautoa upande wake bora zaidi na mambo bora zaidi kwa wanadamu huku yeye Mwenyewe Akistahimili kimyakimya mateso yote. Mungu kamwe hafichui mateso haya. Badala yake, Anayavumilia na kusubiri kwa kimya. Ustahimilivu wa Mungu si wa kimya tu, usio na hisia, au usio na suluhu, wala si ishara ya unyonge. Ni kwamba upendo na kiini cha Mungu siku zote yamekuwa bila nafsi. Huu ni ufunuo wa kiasili wa kiini na tabia Yake na maonyesho halisi wa utambulisho wa Mungu kama Muumba wa kweli.

Baada ya kusema hayo, wengine wanaweza kufasili vibaya kile Ninachomaanisha. “Je kufafanua hisia za Mungu kwa maelezo kama hayo, kwa hali ya hisia nyingi sana, inanuia kuwafanya watu kuhisi masikitiko kwa Mungu?” Je, hayo ndiyo madhumuni hapa? (La.) Kusudio la pekee la Mimi kusema maneno haya ni kuwafanya kujua Mungu kwa njia bora zaidi, kuelewa kila sehemu Yake, kuelewa hisia Zake, kutambua kiini na tabia ya Mungu, kwa uthabiti na kwa kidogo kidogo, iliyoelezewa kupitia kwa kazi Yake, kinyume na vile inavyotumiwa kupitia kwa maneno matupu ya binadamu, barua na mafundisho yao ya kidini, au kufikiria kwao. Hivi ni kusema, Mungu na kiini cha Mungu kwa kweli vipo—si tu uchoraji, havijafikiriwa, havijajengwa na binadamu, na bila shaka havijabuniwa na wao. Je, mnatambua hii sasa? Kama mnaitambua, basi maneno Yangu leo yametimiza shabaha yao.

Tulijadili mada tatu leo. Nina imani kwamba kila mmoja amepata pakubwa kutoka katika ushirika wetu juu ya mada hizi tatu. Ninaweza kusema kwa hakika kwamba, kupitia kwa mada hizi tatu, fikira za Mungu Nilizofafanua au kiini cha Mungu na tabia Nilizotaja vyote vimebadili mawazona ufahamu wa watu kuhusu Mungu, hata kubadili imani za kila mmoja kwa Mungu, na zaidi, kubadili picha ya Mungu inayopendwa na kila mmoja katika mioyo yao. Haijalishi chochote, Natumai kwamba kile ambacho mmejifunza kuhusu tabia ya Mungu katika sehemu hizi mbili za Biblia ni cha manufaa kwenu, na Natumai kwamba baada ya nyinyi kurudi mtajaribu kukitafakari zaidi. Kikao cha leo kinahitimishwa hapa. Kwaheri!

Novemba 4, 2013

Iliyotangulia: Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo Ambayo Kazi Yake Itafanikisha

Inayofuata: Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp