252 Nampa Mungu Moyo Wangu Mwaminifu

1

Kubarikiwa na kuingia katika ufalme wa mbinguni, nilikaa ndani ya nyumba ya Mungu.

Ingawa nilikuwa nikitekeleza wajibu wangu, ulinajisiwa na mtazamo wangu wa kubadilishana.

Ni kupitia tu hukumu na ufunuo wa maneno ya Mungu ndiyo niliona wazi ukweli wa upotovu wangu.

Nina ubinafsi na udanganyifu, nilipoteza dhamiri na mantiki yoyote kitambo.

Mungu ananifundisha kwa maneno Yake bila kuchoka, akitumaini kwamba tabia yangu potovu inaweza kubadilika hivi karibuni.

Mungu anasubiri, Mungu anatarajia, kama mama anayesubiri kurudi kwa mwanawe karibuni.

Nikikumbuka neema ya Mungu, moyo wangu unajaa majuto, kwa kweli sipaswi kuwa mwasi na mdanganyifu sana kwa Mungu.

Ninachukia sana upotovu wangu wa kina; bila kufuatilia ukweli, nimeuumiza sana moyo wa Mungu.

Nimekosa nafasi nyingi za kukamilishwa; muda mwingi mzuri umepotea.

Ningeendeleaje kumwasi na kumjeruhi Mungu? Niko tayari kufuatilia ukweli na kuishi kwa kudhihirisha mfano wa mwanadamu.

2

Najitahidi kutenda maneno ya Mungu ili nipate ukweli.

Upotovu wangu mara nyingi hujitokeza, kisha nahukumiwa na kuadibiwa na maneno ya Mungu.

Ingawa kuna mateso na dhiki, maneno ya Mungu daima huwa nami.

Nimepata maarifa kiasi juu ya utakatifu na haki ya Mungu, uchaji Kwake umekua moyoni mwangu.

Najichukia kwa kutamani raha, nimeazimia kujali hisia za Mungu na kutenda ukweli.

Nikifikiria zamani, nikikumbuka neema ya Mungu, naona kuwa Mungu tu ndiye upendo.

Nimebadilika tu kwa sababu ya kupogolewa, kushughulikiwa, majaribio na usafishaji wa mara kwa mara ambao umekuwa nami wakati huu wote.

Sijarudisha neema kubwa ya Mungu, nimejawa na hatia na sistahili kuuona uso Wake.

Kwa kupata neema ya Mungu, nashukuru moyoni mwangu. Nitathamini siku zangu zilizobaki zaidi.

Natamani kumuishia Mungu mara hii, kuwa mtu mwaminifu anayemtukuza na kumshuhudia Mungu.

Nampa Mungu moyo wangu mwaminifu, nitatimiza wajibu wangu kulipiza upendo wa Mungu.

Iliyotangulia: 251 Thamini Fursa ya Kumpenda Mungu

Inayofuata: 253 Ninaomba tu Kwamba Mungu Aridhike

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp