225 Nampa Mungu Upendo Wangu

1 Mungu alipoonekana kufanya kazi katika mwili, Alipitia aibu kubwa. Mnyenyekevu na aliyejificha, Alionyesha ukweli kumwokoa tu mwanadamu. Lakini niliposikia sauti ya Mungu, sikumtambua, na nikawafuata wazee na wachungaji katika kumkana na kuihukumu kazi Yake. Mungu hakuniadibu kwa makosa yangu, lakini alivumilia kutotii kwangu, na akabisha mlangoni kwangu. Nilipoona huruma ya Mungu kwangu, nilihisi aibu isiyovumilika; kwa kweli sikustahili kuupokea upendo wa Mungu.

2 Maneno ya Mungu huuchoma moyo wangu kama upanga mkali. Naona kuwa kiburi changu kimenipokonya akili na ubinadamu wote, kwamba natumia dhana na fikira kukemea kuonekana na kazi ya Mungu, nikizuia nafasi ya wokovu wa waumini wengi sana. Nina dhambi namna gani, kumpinga na kumhukumu Mungu. Kwa kweli sistahili upendo wa Mungu, sistahili kuishi mbele Yake. Kupitia hukumu Yake kumeniamsha, na moyo wangu umejaa mahangaiko. Naamua kuanza upya, kufuatilia ukweli na kumridhisha Mungu. Mungu ni mkarimu sana, unauyeyusha moyo wangu mgumu. Nampa Mungu upendo wangu, na naomba tu kwamba moyo Wake ufarijike. Haijalishi mateso na shida ilivyo kubwa, nitakuwa mwaminifu hadi mwisho. Naazimia kutoa ushuhuda mkuu kwa Mungu na kumletea utukufu.

Iliyotangulia: 224 Nimekusudia Kumridhisha Mungu kwa Uaminifu

Inayofuata: 226 Kile Ambacho Waumini Katika Mungu Wanapaswa Kutafuta

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp