597 Timiza Wajibu Wako na Utakuwa Shahidi
1 Bila kujali kinachokupata, lazima uje mbele za Mungu; hili ndilo jambo sahihi la kufanya. Kwa upande mmoja lazima utafakari, na kwa upande mwingine hupaswi kuchelewa kufanya wajibu wako. Usitafakari tu kujihusu na kutofanya wajibu wako. Kuna nyakati nyingi ambazo majaribio ambayo Mungu huwapa watu ni mzigo. Hata mzigo ambao Mungu anakupa ukiwa mzito namna gani, unapaswa kuubeba, kwa sababu Mungu anakuelewa, na Anaelewa kuwa unaweza kuubeba. Mzigo ambao Mungu anakupa hautazidi kimo chako au kukuzidi; hakika unaweza kuubeba.
2 Bila kujali ni aina gani ya mzigo ambao Mungu anakupa, au ni aina gani ya jaribio Analokupa, kumbuka jambo hili: Unapokuwa ukiomba, ikiwa utakuja kuelewa mapenzi ya Mungu au la, ikiwa utapata nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu au la, na ikiwa jaribio ni Mungu akikufundisha adabu au kukupa onyo, haijalishi ikiwa huelewi. Almradi huachi wajibu unaopaswa kufanya, na unaweza kuushikilia kwa uaminifu, kwa njia hii Mungu ataridhika na utakuwa umekuwa shahidi.
Umetoholewa kutoka katika “Ni Kupitia Kutafakari Mara kwa Mara Juu ya Ukweli Tu Ndipo Unaweza Kuwa na Suluhisho” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo